Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, August 29, 2012

Mbio sa sakafuni huishia ukingoni-9






‘Mume wangu nimechoka na kazi za hapa nyumbani, zimeniwia ngumu sana, kama tusipopata mfanyakazi wa nyumbani, nahisi nitapatwa na wazimu, na nitazeeka kabla ya muda wangu….’akalalamika mke wangu alipofungua mlango.

Nilimwangalia kwa macho ya huruma, maana alikuwa kachafuka, na jasho linamtoka, kwani alikuwa akitokea jikoni, alipokuwa akifanay usafi, na aliposikia nimekuja akaja kunipokea,….

‘Samhani mume wangu nimechafuka sana hata kukushika mkono siwezi, ingia na mizigo yako uweke ndani, ..’akaniambia nami niliingia na kuweka mizigo yangu,halafu nikarudi varandani, na baadaye alikuja na kusimama mbele yangu.

‘Pole sana mke wangu na kazi za nyumbani….’nikasema.

`Pole na wewe na kazi za jukwaani, kazi za kupepeta mdomo,…’akaseama na kucheka kwa zihaka.

‘Sasa mke wangu, nipe muda kidogo tuongee, maana najua ukiingia huko jikoni hatutaongea ahdi jioni, na mimi ninaweza nikaitwa wakato wowote, naomba tuongee kidogo’ nikasema.

‘Haya siasa zako zimeanza, ….ninakusikiliza, unataka kusema nini tena, tukauze nini tena, maana sasa ndio zako unataka kuuza kila hata, hata mimi unaweza ukaniuza…’akasema huku akijisogeza kwenye sofa,lakini hakukaa, akasimama na kuniangalia kwa mashaka.

‘Nikuhusu hizikazi nyumbani na matatizo haya ya wafanyakazi wandani…’nikasema.

 ‘Kwanini tusiwe na wazo la kudumu, kwanini tutafute mfanyakazi ambaye mkataba wake haueleweki,….?’ nikauliza.

‘Kwahiyo unasemaje…?’ akaniuliza,nakabla sijasema hilo nililopanga, akaanzakuzungumzia mambo ya siasa.

‘Kwanza alikuja yule rafiki yako wa zamani, adui yako, akanionya kuwa nikuambai kuwa uachane na mambo hayo ya kisiasa maana yatakuweka pabaya, nilimsikiliza kwa makini, ingawaje sikumwamini sana, maana huyu mtu hana heri kwetu’akasema.

‘Achana naye huyo….kwanza alikuja hapa kufanya nini, ..sinilimpiga marufuku kuja hapa nyumbani…au mna yenu ya siri nini…?’ nikasema kwa hamaki.

‘Mimi siwezi kumfukuza mgeni, alipita na gari lake la kifahari, akaniona nipo hapo nje, akaniongelesha, na wala hakushuka kwenye gari lake, akawa anabwabwaja maneno yake, yaliyokuwa yakiingia huku na kutoka huku..’akasema.

‘Huyo achana naye, tuongee maswala yetu muhimu…’nikasema.

‘Haya ongea na kusikiliza…ila kama ni hayo ya kisiasa sitayaunga mkono tena, kama hujakoma ubishi, endelea nayo, sasa hivi pesa hatuna, mali zote tuliuza, na tuna madeni ya kufa mtu, bado hujakata tamaa, mimi sasa sihusiki tena, maana ulishaanza kunitupia lawama mimi, safari hii utafanya utakavyo, mimi simo….hebu niambie, utafanyaje na wewe huna pesa, kumbuka nyumba hii ipo chini ya dhamana ya deni la watu…’ akasema akionyesha kukata tamaa.

‘Sikiliza mke wangu nikupe wazo moja, nahisi hilo ukilifikiria kwa makini  tunaweza tukayatatua haya yote yanayotukabili. Mimi kuna wazo nimelipata, na wewe ukiliwaza kwa makini tunaweza kupata ufumbuzi…’nikasema.

‘Wazo gani, kuhusu nini…?’ akaniuliza.

‘Kuhusu unavyolalamika hapa nyumbani ,najua kazi ni nyingi, najua jinsi gani unavyotaabika, sasa tulitafutie ufumbuzi wa kudumu….’nikasema.

‘Haya ufumbuzi gani wa kudumu….?’akaniuliza.
 Mke wangu akatulia akiniangalia kwa makini, akijaribu kutafakari, nini ninachotaka kumwambia, akasema kwa haraka
.
‘Unajua mke wangu, wewe una akili sana, una hekima sana, mimi nimeliwaza hili, naomba utumie hekima na akili ya kulitafakari kwa makini, kwasababu, ….kwanini tutafute mfanyakazi ambaye mkataba wake haueleweki, siku mbili tatu kakimbia,….sasa tuna mambo mengi sana ya kufikiria, ukiangalai haya mambo ya kisasa, mimi natakiwa nitulize kichwa kwenye mambo hayo, mwaka jana tulikosa ubunge kwa kutokuwa makini,lakini bahati nzuri, nafasi hiyo ipo wazi tena, tusifanye makosa hayo tena, …’nikasema.’

‘Kwahiyo unataka kusema nini, kuwa muwazi, usilete siasa zako hapo ndani, hapo sio kwenye jukwaa la siasa, maneno mengi, hayatanisaidia mimi,napoteza muda wangu….jikono kunanihitaji, sasa hivi utaanza kulia njaa,..?’ akaniuliza mke wangu.

‘Mimi nimeonelea tutafute mtu wa kudumu, ..badala ya hawa watu wa kupita, tukipata mtu wa kudumu ambaye atabeba majukumu kama mwanafamilia hakutakuwa na shida tena, ….yeye atakuwa na uchungu wa mambo yote ya hapandani, hata tukitoka hatuna wasiwasi,….angalia hapa ilivyo, wewe unakwenda kazini, huku nyuma tunamuaha mtu ambaye hatuna imani naye sana, na mimi nadumkia kazini, lakini huyo tutakaye mtafuta anakuwa kweli ni mwenye uchungu na familia, maana kutakuwa kwake…’nikasema.

‘Mimi bado unanichanganya, ina maana tuchukue ndugu,…au unasemaje…i?’ akaniuliza huku kashika kiuno na usoni kulijaa kulionyesha kuwaza.

‘Nina maana kuwa badala ya mfanyakazi wa nyumbani , ni bora, tukamtafuta mtu wa kudumu, kwa mfano tukitafuta mama wa nyumbani….ambaye atakuwa msaididzi wako huoni itakuwa ni vyema kabisa…?’ nikawa kama namuuliza.

‘Mimi bado sijakuelewa, mama wa nyumbani…..!?’ akashikakichwa, akitafakari,halafu akasema;

‘Una maana gani,…maana sikuelewi, sisi hapa tunazungumzia swala la mfanyakazi wa ndani, kwanini hawatulii, kila mfanyakazi akija hapa anakaa wiki mbili anaondoka,  huyo ambaye nilijua kabisa atakaa kwa muda mrefu kwani tulimuahidi kumpa mshahara mkubwa naye kaondoka, kadanganywa na hawa wanaume wanaorubuni watoto wa watu, mwisho wa siku wanawatelekeza, ….nyie wanaume mna dhambi kweli....’akasema mke wangu

‘Mke wangu nataka unielewe, sina nia mbaya, na wala sisemi haya kwa kuwa nimeamua iwe hivyo, nalitoa hili kama wazo ili tulijadili, wapo wamefanya hivyo na wametulia, hawana shida, kinachotakiwa ni wewe urizike, uwe na amani, ….na kuwa mke mwanza sio kitu kibaya….’nikainuka nakumsogelea.

Mke wangu alishituka nilipotamka hilo neno mke mwenza, kwani muda wote huo alikuwa bado hajanielewa, aliniangalai kwa macho yaliyotoka kama vile kasikia jambo laktisha, na ghafla nikashitukia kofi la nguvu likiingia shavuni mwangu.

‘Yaani kumbe ndio maana yako hiyo,….kumbe ndio maana umebadilika kiasi hicho, kumbe…ooh,mungu wangu, ….siamini hayo maneno yako, na kofi hilo likufundishe adabu, maana naona sasa kumbe umeshanichoka …’akasema huku macho yakianza kulowana machozi.

‘Mke wangu sikuwa na nia mbaya, ni wazo tu….’nikasema nikijarubu kumsogelea, yeye akanyosha mikono mbele yangu kunizuia nisimsogelee.

‘Nisikilize kwa makini,  kama umenichoka, nipe talaka yangu, mimi nipo tayari kurudi kwetu,…sio lazimaniishi na wewe, na hata hivyo mimi sasa ni mtu mzima ninaweza kuishi maisha yangu, nikajitegemea, ….najua unajiamini kuwa sitaweza kurudi kwetu, kwasababu niliondoka bila wao kurizika, kwahiyo hawataweza kunipokea, hata kama mama atanisimanga, mimi naweza kujitegemea mwenyewe, sishindwi kuishi kivyangu,…..’akasema na kuniangalia kwa hasira, na nilipojaribu kufunua mdomo, akageuka na kukimbilia ndani…nakajua sasa nimelikoroga.

Nilibakia nikiwa nimeshika shavu, ….nikiwaza hilo kofi, kwani hilo kofi lilikuwa ni la pili, maana huko nilipotoka nilisha zabwa kofi jingine la aina yake. Lilikuwa sio kofi la mkono, bali ni kofi la moyoni, kwani pale nilipogundua kuwa jina langu halikupita kwenye wabunge waliopitishwa ili wakapigiwe kura, lilikuwa ni kofi ambalo sikulitegemea. Sikuamini maana nilipoteza pesa nyingi sana, kuhakikisha nipo kwenye uchaguzi huo,…na hata wale wahusika wakuu walishaniambia kuwa jina langu litapita tu kwenye mchakato huo, maana nilishapitishwa mwanzonu, na mimi ndiye ninayestahili kutetea nafasi hiyo tena.

*******

Nilijuta kwanini nilitoa wazo hilo ambalo alinishauri rafiki yangu mmoja, aliniambia kuwa kazi hii ya siasa inahitaji matulizo ya moyo, sitaweza kuimudu, kama nitakuwa na matatizo ya kifamilia, akanishauri kuwa yeye alikuwa na tatizo kama hilo, akashauriana na mkewe wakakubaliana watafute msaidizi, na mkewe akasema yeye atamtafuta mke mwenza ili wasaidiane kazi.

‘Haiwezekani, yaani mke wako atoe ushauri kama huo, ulimwamini kweli, isije akawa na yeye kakuchoka anatafuta mbinu za kukutema…..’nikamwambia huyo rafiki yangu nikionyesha mshangao.

‘Inawezekana, kwanini isiwezekane, hutaamini, maana hata mimi alipotoa ushauri huo nilijua ananitania kunitega, …yeye mwenyewe akamtafuta mke mwenza, na alimtafute mke kweli, sio kwasababu anatafuta mke mwenza, labda angelitafuta mtu ambaye hatamuonea wivu, …hapana, yeye alitafuta kimwana wa nguvu, …mrembo,….nikamuoa’akasema rafiki yangu.

‘Ina maana yule mke ulitafutiwa na mkeo?’ nikamuuliza.

‘Ndio watu hawaamini, lakini ndivyo ilivyokuwa, na wanaishi kama mtu na mdogo wake, wanapendana isivyo maelezo, ukiwaona utafikiri ni ndugu, na wanavyofanana, watu wanasema labda ni mtu na mdogo wake, ….’akasema rafiki yangu akiwa kashika kitambi chake,ambacho kiliiuka ghfala abada ya kuoa.

‘Mhh, mimi siamini, ….niende nikamwambia mke wangu kuwa tutafute msaidizi, na msaidizi huyo awe mke  mwenza, sijui, kama kutakalika’nikasema.

‘Unajua kuna kitu ambacho tunashindwa kujua, …kila jambo linahitaji hekima yake, na jinsi gani ya kuliongelea, cha mhumi ni kuongea, kaeni muongee, sio kwamba nawashauri kuwa iwe hivyo, hapana, ila inawezekana, kwasababu ….’akatulia kwa muda kama anawaza jambo.

‘Kwasababu kama unaweza kumchukua mafanyakazi wa ndani, na mtu mwingine na familia  yako mkaweza kuishi bila matatizo, kwanini ishindikane kumchukua mke msaidizi, mkashirikiana, ilimradi kuwe na maelewano, inawezekana rafiki yangu kajaribu kuongea na mkeo, wewe ni mtaalamu wakuongea, kama unajimudu….nina maana uwe  kweli unaweza, inawezekana’akaniambia na mimi nikajikuta naingiwa na wazo hilo ambalo sikuwa nalo akilini kabisa.

‘Nitajaribi kumshauri mke wangu, ….kama akikubali, basi najua tutakuwa na nguvu mpya kwenye familia, na kama ….nitamchukua yule yule wa kule maeneo…’kabla sijamaliza kuongea  wakaja marafiki zangu wengine na tukaanza kujadili mambo ya kisiasa.

********

Nilibakia nikiwa nimeshika shavu, ….hili kofi lilikuwa la pili maana huko nilipotoka kwenye kikao cha kisiasa, nilisha zabwa kofi jingine lililopenya hadi akilini, lakini ofi hilo halikutoka mkononi mwa tu, lilikuwa kofi lisiloonekana, lenye maumivu yakipekee kabisa ambayo yalikuwa makubwa zaidi.

Katika uchaguzi huu baada ya matokea kutenguliwa, nilitarajia kuwa jina langu lingelipitishwa tena, lakini haikuwa hivyo, kwani jina langu lilienguliwa kimizengwe, sikutakiwa nikagombee nafasi hiyo ya ubunge tena. 

Sikutarajia iwe hivyo,  maana nilishapoteza pesa nyingi sana , isitoshe hata wale wahusika wakuu walishaniambia kuwa jina langu litapita kwenye mchakato huo, nisiwe na wasiwasi. Niliposikia kuwa jina langu limeenguliwa, niliishiwa nguvu, na nilianza kuhisi yale maumimvu ambayo hutokea mara kwa mara ninapokwazika.

Nilimuangalia yule mzee ambaye ni mmoja wa viongozi wakubwa wa chama na ndiye aliyekuwa mtu wangu muhimu huko kweye ngazi kubwa, na nilijua akiongea yeye unasikilizwa, nikajau kuwa yeye ndiye nafasi yangu ya mwisho, akishindwa yeye tena , basi, nikamwangalia kwa macho ya huzuni, naye akasema;

‘Sikiliza kiongozi, wewe tafuta pesa, haya matokeo ni ya awali, walikaa wakubwa wakapitisha hawo watu wao, lakini wewe una haki ya kuendelea kutetea nafasi yako, sisi tutakaa na hawo watu tuone jinsi gani ya kuweka mambo sawa,.. tutayabatilisha hayo maamuzi yao, maana naona kuna watu wanataka kutuingilia, ila….’akatulia kama anawaza jambo.

‘Tunahitaji nguvu,… maana huku kwenye kikao kikubwa ndipo tunaamua ni nani anatufaa, mimi nitajenga hoja kuwa wewe ndiye unayestahili kuutetea nafasi yako na hata kura ulizopata zilikuwa karibu sawa na huyo aliyekuwa kashinda kinamna,sioni kwanini wakutoe, nitakupigania kwa guvu zote, wewe ni kiongozi wetu mtarajiwa bwana, unastahili kuwa kwenye nafasi hiyo.….’akaniambia huyo mzee.

‘Lakini kunahitajika pesa, pesa nyingi…hili sio swala la mchezo, na ujue hapo unatafuta maisha yako ya baadaye, najua jinsi gani ulivyopigika kweney huo uchaguzi, una madeni una mambo mengi ya kujiweka sawa tena, nafasi hiyo ukiikosa tena , utaathirika sana, na hata hivyo wewe unafaa sana kuwa kiongozi cha muhimu hakikisha huwi na kashifa yoyote, mimi nilishakuoan siku nyingi wewe ni kiongozi mtarajiwa, nyota yako ni ya uongozi inang’ara,,…na ukipita hapi najua kabisa utakuwa mbali, wewe unastahili kuwa waziri…’akaniambai mzee huyo.

‘Pesa….pesa, mzee ninakuelewa sana, lakini ukitaja pesa kwa sasa, sijui nifanyeje, maana kuwafuata hawo watu wangu tena, naona aibu, na sijui kama watanielewa tena. Kwahiyo tusema huko kwenye kikao zinahitaji kama Shilingi ngap..i?’ nikauliza huku nikiwawaza wafadhili wangu.

‘Milioni kumi, kwa yule bwana, kumi kwa watu moja mbili tatu, wale wengine tano tano zinawatisha,…mmh, tusema kwa sasa ukipata milioni arubaini hivi, tutaweza kuweka mambo sawa, ….’akasema kama vile anataka pesa ndogo sana.

‘Ukinipatia hizo pesa, nitaweza kuzigawa kwa watu wangu, ….hiyo sio rushwa, elewa kijana hiyo ni pesa itakayowasaidia wao kupoteza muda wako kukusaidia wewe,….halafu baadaye tutatafuta milioni thelathini nyingine kwa ajili ya watu maalumu wa kampeni,….’akasema kama vile kwake pesa kama hizo ni ndogo sana, sijui alikuwa akinielewa vipi, kuwa labda mimi nina ushirika na freemason, au nina kisima cha mafuta, nilimwangalia kwa macho ya wasiwasi.

Mzee sijui, ngoja nikahangaike, maana siunajau tena, yote hayo nategema wafadhili, wao wakikubali,basio tutaangalia,,lakini mzee nakuomba usiniangushe, maana hizo pesani dhamana ya watu, ni deni kwangu…’nikasema.

‘Usiwe na shaka,sisi ndio wenyewe,….jina nitahakikisha linapita, ila nakuomba tena, hakikisha kuwa huwi na kashifa nyingine yoyote…haya mambo ya pesa, ni mambo ya kawaida ni gharama za uendeshaji na mambo ya kawaida, tunajau jinsi ya kuyaweka sawa, lakini kashifa mbaya zitakazo igusa jamii, mimi sitaweza kuzizuia….uwe makini sana…’akasema na tukaagana.

*******

Nilipotoka kwenye kikao na yule mzee ikabidi nichakarike, nianze kiguu na njia kuwatafuta wafadhili, nikawa sikai nyumbani, nikauza gari la bei mbaya, nikawa natumia gari la kawaida, na nyumba ya mke wangu nikaiuza pia, nyumba ambayo aliijenga kwa mkopo wa benki, nikijua hayo yataisha na pesa itarudi tu,…tulikuwa na biashara nyingine za masafaambazo alikuwa akizisimamia mke wangu, nikajua hizo zinaweza kutusukuma.

Baada ya kuhangaika nikafanikiwa na pesa hizo nikamkabidhi huyo kiongozi na nikajua mambo sasa yapo kweupe, huko mbeleni kwenye kampeni, mambo yatasimamiwa na chama, nilihitajika kuwa na pesa za kawaida tu, sio kama ule uchaguzi wa mwanzo. Nilipofanikisha hilo kwa siku hiyo nikarudi nyumbani nikiwa na furaha zawadi tele mkononi, na nikiwa na wazo hilo la kupata msaidizi, na masaidizi mwenyewe ni mke mwenza, …

Msaidizi na msaidizi mwenyewe ni mke mwenza, ….nikawaza huku nikiangalia juu, nikaziangalia zile zawadi nilizokuwa nimeziweka juu ya meza,nikaziona hazina maana tena,….

Nikashika shavu langu nikiumia kimoyomoyo, nikiwaza nini kinachoendelea huko kwenye kikao maalumu,kikao cha kupitisha majina ya mbunge atakaye pamabana kweye uchaguzi wa pili. Moyoni sikuwa na wasiwasi,…nikatulia na mara simu ikalia,…..

Niliogopa kuipokea, sijui kwanini,ingawaje muda mfupi uliopita nilikuwa nikipokea simu kwa haraka, nikiwa na hamasa kuwa nitasikia kuwa jina langu limepita,…lakini kila aliponipiga rafiki yangu huyo, ikawa naambiwa mambo bado,nisiwe na shaka…sasa simu hiyo, huenda ndio yeye, huenda mambo yameshakamilika,…naikaichukua ile simu,  nilipotizama nikaona aliyepiga ni yule rafiki yangu wa zamani ambaye sasa namuita adui yangu.

Nikataka nisiipokee, niikate, lakini baadaye nikaipokea, nikamsikia rafiki yangu huyo,akihema kama kawaida yake, maana sio yule jamaa niliyemjua, sasa hivi ni bonge,kashiba mwili mzima, na kilo zake ni mia kwenda juu, akasema kwa kwa lugha, lafudhi ya kiingereza. Sasa hivi ni mkurugenzi wa kampuni kubwa sana ya kimataifa….

‘Nasikia weye, unataka kuingi-ya kwenye kinyang’anyiro tena,…hujakata-tamaa, hujasalimu amri,sio, nakushawu-uri weye-kama rafiki yangu wa zamani, acha-ana na hiyo nafasi maana utaumbuka ….very bad…’akasema.

‘Umeanza vitisho vyako tena, niumbuke kwa lipi, mbona wewe hujaumbuka licha ya kugundulikana kuwa wewe ndiye uliyerubuni hadi huyo mtu wako akapita…’nikasema.

‘Sikiliza mimi sio mtu wa mchezo, nikikuambia hivyo nina maana yangu,…kama hutafanya hivyo safari hii nahakikisha unakwenda chini,…na mke nachukua, siunajua zile zangu za zamani,….nitahakikisha utakuwa omba omba, ….’akatulia na kucheka kicheko cha kebehi.

‘Usinitishe wewe….’nikajipamoyo na kusema.

‘Sikutishi, ila ndivyo itakuwa,….kumbuka madeni uliyo nayo, kumbuka mapesa uliyoyamwaga,ulipojiingiza kwenye mambo ya siasa kichwa kichwa, wewe unauza nyumba,magari,…toka lini ukafanya hayo kwa mali yako, vitu kama hivyo unatafuta matajiri kama sisi, wenye pesa, tunaotaajia kukutumia baadaye,lakini weye, ukatoswa….sasa angalia maana hayo, yote tunayo kwenye kumbukumbu zatu, kama ushahidi ikibid kwenda mhakamani, lakini hiyo haitoshi, ….’akatulia, na mimi pale moyo ukaanza kwenda mbio, nikashika ubavuni, sijui kwanini hali ile ilikuwa ikinitokea.

‘Wewe ni mume na una mke mwema mstaarabu, na tulitaraia ungelikwua mfano mwema ,…kiongozi mwema ni yule anayejali familia yake, ..wewe una mke, lakini hujatosheka na mkeo,  …unakumbuka kile kikao mlichofanya kule makao makuu, mkanywa na kupitiliza, ukifurahia ushindi ambao haukuwepo, kumbuka yule mwanamke uliyekuwa naye, ambaye sasa unamtaka awe mke msaidizi…mlifanay nini naye siku ile…..’akasema na mara mlango wa chumbani ukafungulia. Mke wangu akawa kasimama mlangoni huku akiniangalia kwa macho yaliyojaa hasira.

Nilitamani niizime ile simu, lakini nguvu za mkono zilikuwa zimekwisha, maana nilikuwa nimeishika kwa mkono wa kushoto, na mkono huo ukawa hauna nguvu tena, ulikuwa kama sio wangu….nikawa kama mtu aliyeganda, na maneno yaliyofuata hapo, kutoka kwa huyo rafiki yangu, yailikuwa kama mtu ananichoma kisu moyoni,pigo moja baada ya jingine …..maumivu makali yakatanda ubavuni mwa kushoto,….nikahsi kichwa kikuma maumivu makali yasiyo ya kawaida, nilichosikia kwa mara ya mwisho ni  yale maneno ya huyo rafiki-adui yangu,yakisema;

‘Ikipita saa moja, kabla hatujasikia kauli yako ya kujitoa, kwanza kabisa namtumia hizo picha mke wako,na ukumbuke ana shinikizo la damu ya kushuka, akiziona tu, sizani kama atahimili mapigo, unakumbuka mliyoyafanya na yule mwanamke, ambaye kakubuhu ufusuka,….sasa jiulize kweli unampenda mkeo, au ulimuoa tu, ili kuninyima mimi mwenye haki naye…’akatulia na kukohoa.

‘Wewe una haki naye kwa vipi..?’ nikamuuliza kwa sauti ya kukwaruza, kuonyesha kuwa nguvu za mwili sio zangu tena.

‘Huyu mrembo anahitaji watu wenye pesa kama sisi, anahitaji kukaa kwenye raha, sio hapo anaishi kama mfanyakazi wa nyumbani, huoni kuwa ilikuwa na haki yangu, …’akasema na kutilia.

‘Sasa tusipotezeane muda, unaamua lipi, nianze kwa kumtumia mke wako hizp picha, au nianze huko kwenye kikao, au nianze huko ukweni, au kwa wazazi wako,….amua moja haraka…’akasema kwa hasira.

‘Sikiliza,hilo unalotaka kulifanya ni uwoga,inaonyesha jinsi gani mlivyo wazaifi kisiasa, acheni tupambeane kwenye majukwaa, sio kinafiki namna hiyo, na njia hiyo haionyeshi kukomaa kisiasa’nikajitahiki kusema.

‘Kumbuka yale uliyokuwa ukifanya, je hayo matendo yanaonyesha kukoamaa kisiasa, je ndio mtawala bora huyo tunayemtegemea katika nchi yetu hiii takatifu, mtawala fusuka,..kweli kwa tabia kama hiyo,utaiweza nchi kama hii, kama sio kubadili wake kama nguo, na kuzaa watoto wengi wa nje… je huko ndio kukomaa kisiasa…,nakuulizawewe….au utaoa kama watawala wa mababu zetu, waliokuwa na wake kumi kidogo, na ni heri ungelioa, lakini hayo uliyokuwa ukifanya ni umalaya…au tutauitaje?’ akatulia.

‘Fanya unalotaka kufanya bwana, maana hata kama nikitoa kauli yangu,nitahakikishaje kuwa hamtufanya hayo mliyoyakusudia,..’nikasema kwa kujipa moyo.

‘Sawa kama umejiamini hivyo, ..kwanza naanza kukutumia wewe mwenyewe, hebu fungua huo ujumbe kwenye simu yako..’akakata simu na kweli baadaye uliingia ujumbe. Kwa hali nilyokuwa nayo, nilishindwa hata kuinua mkono wangu wa kushoto, sikujua ni kitu gani kimenipata. Jasho, woga, na wasiwasi vikaniandama na hali hiyo ikazidisha shinikizo la damu.

‘Hivi wewe una nini….?’ Akaniuliza mke wangu akiwa na wasiwasi.

‘Hakuna kitu, ni huyu mshenzi ananitishia,…’nikasema na kwa haraka nikatumia mkono wangu wa kulia ambao ulikuwa na nguvu, na kufungua ule ujumbe ulioingia kwenye simu,picha ilionekana wazi kabisa…ilikuwa haifai kutizimwa,…. nikahisi mwili ukiisha nguvu, nikamwangalia mke wangu ambaye alikuwa akinisogelea kwa taraibu,  kwa haraka nikajaribu kuufuta ule ujumbe, lakini simu ikawa haikubali, jasho likawa linanitoka kama mtu aliyemwagiwa maji ….

‘Mbona unahangaika hivyo, kakutumia nini huyo mtu ….?’ Akaniuliza mke wangu huku akiwa tayari keshanikaribia, na nikajaribu kuiweka ile simu mbali na macho yake na muda huo huo simu ikaita tena, na bila kujijua nikawa nimeipokea, na kujitutumua hadi nikawa nimekaa mbali kidogo na alipokuwa kasimama mke wangu, nikaanza kusikia huyu jamaa akinimaliza kwa maneno yake …

‘Umeiona hiyo, sasa hiyo ni ndogo yake, sasa hivi ninamtumia mkeo picha ile mbaya yake, ili aone nini ulichokuwa ukikifanya….’akasema .

‘Sikiliza wewe maaluni….nita….nita….’kichwa kikawa kinagonga, mwili nikaanza kuhisi vibaya.,yeye huko akawa aanongea, na nilishindwa kabisa kuizima ile simu….mke wangu akawa ananiangalai ninavyohangaika, lakini hakufanay kitu, akawa katulia akiniangalia .

‘Mkeo, mkweo na wajumbe kwenye huo mkutano wataziona hizo picha, na kesho magazeti yote yatapamba picha zako,….yote  uliyokuwa ukiyafanya na huyo hawara wako,  yatajulikana kwa watu wote hasa wa huko kwenye jimbo lako, nakupa nusu saa ya kuamua…. ‘akatulia.

‘Unachotakiwa kufanya ni kutoa kauli yako ….kuwa umejitoa, ….kuwa kwasababu za kiafya umeona hutaweza kugombea tena huo uchaguzi, utajiokoa wewe na mkeo, na ….’nikawa sisisikii kabisa anachoongea,…giza nene likatanda kichwani, na kilichofuata ni zile kumbukumbu za siku ile, siku ile ambayo nilifanay jambo ambalo nililijutia maishani, na kumbe lilikuwa limepangwa, ….

‘Mume wangu jamani vipi, nisaidieni jamani huku….’ilikuwa sauti ya mke wangu, lakini sikuweza kusikia zaidi ya hapo, nikapoteza fahamu.

NB Je ilikuwaje tuwepo kwenye sehemu ijayo, ili tuone nini kilitokea…

WAZO LA LEO: Usizani kila anayekuchekea ni rafiki yako,…


Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

8 comments :

Anonymous said...

Ungemuongeza kofi jingine.Safi kama ingelikuwa mimi kusingelikalika.
Maana najiuliza kwanini msaidizi mpaka awe mwanamke, kwanini hakusema, atafute mwanaume wa kusaidia kazi, kwani haiwezekani. Kama hakutaki akuache tu, kwanza mtu mwenyewe keshazini nje, ndoa ipo kweli hapo?

M3 endeleza basi kidogo, umeachia patamu!

Anonymous said...

Mimi nauliza swali, hivi mtu akizini nje ya ndoa , ndoa bado ipo?
Watu wa dini zote hebu nisaidieni hili swali au tatizo, maana watu wanatoka sana nje ya ndoa, na kama ndoa hazipo basi ina maana ndoa nyingi zimeshavunjika au nimekosea
Na wewe , M3 unaweza kuchangia.
Mimi mama N.

Yasinta Ngonyani said...

Duh Kaazi kwelikweli hapa..na kweli wote wakuchekeao si marafiki..Pamoja daima.

Anonymous said...

Weweeeeeeeeeee, napenda weye!

Unknown said...

Duuuh, patamu hapooo!

Subira said...

Kwanza hakuna kitu kinachoitwa kuzini nje ya ndoa, kuzini au uzinifu maana yake ni kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa. Kwa waislamu ni hivi mtu akizini yaani hana ndoa na adhabu yake ni kupigwa mawe mpaka afe, awe mwanaume au mwanamke.

Tukirudi kwenye uwepo au kutokuwepo kwa ndoa baada ya tendo la uzinifu, mimi ninavyoona hakuna ndoa kati ya maiti na mtu mzima. Maana mtu anapoamua kuzini anajiweka kwenye kundi la wafu. Sasa sijui hao masheikh wanasemaje, jaribu kuwauliza je kuna ndoa ikiwa mmoja wa wanandoa amezini? Nadhani watakachokifanya ni kuzunguka zunguka kutafuta justification lakini ndoa hapo hakuna.

Precious said...

Wazo la leo ni zuri sana kutokana mazingira tunayoishi makazini, majumbani, na kwenye jamii kwa ujumla...Tuko pamoja sana M3

Ammy K said...

kwa kweli kama mwenyezi mungu angekuwa anaumbua watu wanaotoka nje ya ndoa, kwa kweli wangeumbuka wengi. mana ndoa za sasa ni kizaazaa mpka sisi ambao bdo kuolewa tunaogopa kuolewa.Rafiki mkia wa fisi ukimshiriki atakufilisi. wazo la leo nimelipenda sana. naweza sema swadakta..