Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, August 24, 2012

Mbio za sakafuni huishia ukingoni-7Niliondoka pale  nyumbani nikiwa sina raha, kumuacha mke wangu katika ile hali kulitia simanzi, lakini sikuwa na jinsi maana hiki ninachokihangaikia ni kwa ajili ya maslahi yetu ya baadaye. Mke wangu alikuwa msitari wa mbele kunisaidia, na kila mara alikuwa akijaribu kunipa mawazo, lakini ilifika mahali akakata tamaa, alipoona mali nyingi inatumka ovyo, ...

'Hivi mume wangu tuishindwa hapa itakuwaje, maana umeuza karibu kila kitu, mwishowe tutabakia masikini?' akaniuliza.
'Hayo unayaona sasa hivi, mbona mwanzoni ulikuwa ukitia shinikizo, uza, ....fanya, sasa umeanza kuingiwa na wasiwasi, ....maji tumeshayafulia nguo hatuna budi tuyanywe mke wangu, hivi ni vita vya kimaisha, usipopambana utaachwa njia panda....'nikamwambia.

'Haya yangu ..yangu macho, ...'akasema na kuonyesha kukata tamaa, na hasa pale wajumbe wengi walipokuwa hawamshirikishi kwenye baadhi ya maamuzi.

****

Tulifika kwenye kikao, na hapo kikaoni, kulikuwa na wajumbe sita tu ,watu wangu wawili na waafdhili wane ambao wanatoka huko kijijini, lakini wamewekeza hapa mjini, na kila mmoja alikuwa na nia ya kuendeleza huko kwao, ndio maana wakajiolea mali zao .

‘Sasa tuambieni mumejiandaaje, maana sisi ni wafadhili wenu, lakini hatutaweza kujitolea kila kitu moja kwa moja, tunataka kuwasikiliza nyie, ….’akasema mmojawapo.

‘Tumejitahidi vya kutosha, …hapa tuna milioni thelathibi za kuanzia, na tutrajia kupata nyingine baada ya kuuza baadhi ya vitu, ..imebidi tuuze vitu ili tuweze kuwekeza katika uhidani huu, nia na lengi ni kuhakikihsa tunashida, …..’akasema mmoja wa watu wangu.

‘Ni pesa ndogo ana hiyo, ….lakini sisi tutajitahidi kadri ya uwezo wetu, na tutahamasishana weneywe hasa wale wanaotokea maeeno ya huko, cha muhimu ni kuhakikihs hamtatuangausha, tunatarajai ukishidna unawea ukawa waziri, sasa vitega uchumi vyetu, unatakwia uvipe kipa umbele…’akasema moja wa wafadhili.

‘Hlo usitie neno kabisa,….nyie mtaangaliwa kwa jich la pejee kabisa, chamuhimu ni kuhakikihsa tunashinda,…viongzi wote wakubwa wanakutegemea wewe, ….najua upo upinzani wa nguvu, na maadui wapo kila kona, na cha ajabu hata yule rafiki yako mkuu, anampigia debe mpinzani wako, ….’akasema mmoja wa watu wangu.

‘Nilitarajia hilo, maana upinzani wangu nay eye umeanzia mbali, sikujua kuwa tutafik hapo, na nasiki kaahidi kuwa atahakikihs nashindwa vibaya sana,,,,,,’nikasema.

‘Hilo usijali, hata kama anamwanga pesa kwa watu, bado sis tuna nafasi kubwa, kwani wananchi wanatujua, cha muhimu ni kwenda huko, na kuanza kampeni ya nguvu, ndio maana tunahitaji pesa, tunahitaji usafiri, tunahitaji vifaa, ili tuweze kuifanya hiyo kazi….’akasema mtu wangu.

‘Hilo tuachieni sisi, cha muhimu na nyie mjitahisi sana,…’akasema mfadhili.

‘Kwani huyo rafiki yako hatuwezi lumshawishi , maana ni tishio kubwa sana, kama tutacheza vibaya, anaweza akamsaidia sana mpinzani wako kushinda, hayo jamaa kwanini anakufuafuata sana, nasikia ndiye anayeeneza uvumi na hata kudhamini magazeti, ili kukuhaharibia.?’ Akauliza mmoja wa wafadhili.
Ikabidii nianze kuwasimulia kisa changu na huyo rafiki yangu tukianzia pale tulipoweza kumchukua yule binti akiwa tayari kufungishwa ndoa….

******
Walipoingia wale watu wawili, walikuwa mama mmoja na binti, na sauti toka nje ikasema;

 ‘Fanyeni haraka, nimesikia msafara wa bwana harusi upo njiani, kama hataki mbebeni kwa nguvu…’, nilishikwa na butwa, na kujiuliza hawa ni akina nani tena ….

Mara huko nje, nikasikia kelele nyingi, na mlio wa ngomakama ile ya mdunduiko, mimi nikajua bwana harusi keshaingia,….nikachanganyikiwa,  na kweli nikasikia watu wakishangilia kwa nguvu, na jinsi watu walivyo, wengi walikimbilia kwenda huko ngoma inapotokea. Na jinsimuda ulivyokuwa ukisogea, ndivyowatu walivyokuwa wakipungua hapo nje.

Ilionekana kinachotokea huko sio ngoma tu, maana kila mmoja aliataka kwenda na nilipochungulia kwenye upenyo wa mlango, niligundua kuwa watu  wote wamekimbilia huko, nani kimpite, na makelele mengi, yaliongezeka. Hakukubakia hata mtu mmoja, …na hata wale watu walioingia walionyesha wasiwasi kidogo, kwani ilionekana walikuwa wakisubiri amri, au kusubiri jambo fulani. Na kweli  mara ikasikia sauti toka nje ikisema tena,…

‘Mambo yamekwenda safi, fanyeni haraka,…. msiwe na wasiwasi, …’na hapo mlango ukafunguka tena na wakaingia watu wengine .Nikiwa pale kando ya mlango, niliamua kujisogeza, ….ili nione ni kitu gani kinaendelea na hawo watu walioingia sasa hivi, walinitia wasiwasi, nikajua kuna jambo baya linataka kutokea, walikuwa vijana watatu wenye nguvu  kama wale wainua vyuma.

Nikawa nawaangalia kwa kujificha, nikiogopa kujitokeza, maana siwajui ni akina nani,  na lengo lao ni nini, nilishindwa nifanyeje maana wenzangu walikuwa sehemu  wakisubiri niwape ishara ili waingie tufanye yale tuliyokuwa tumepanga,….

Tulikuwa tumepanga kuwa kufanyike jambo ambalo litawavuta watu waondoke eneo la hapo, halafu tunamtoa huyo binti kinamna,hata kwa kumvalisha nguo za kiume, asigundulikane, na humo kuna msichana mmoja tulipanga naye, kuwa atabakia humo,ajifanye yeye kama bibi harusi, na wakati huo sisi tutakuwa tumeshaondoka na kwenda kujificha kusikojulikana…..yale tuliyopanga sasa nayaona yanafanywa na watu wengine tusiowajua…

Sasa tumeingiliwa, nahapo nilipo nilikuwa kama mtu aliyepigwa na ganzi hasa nikiwaangalia wale vijana waliojazia vifua kama wainua vyuma, …mwanzoni nilijua kuwa ni watu wa huyo mume mtarajiwa kafanya hivyo ili kuzuia mtu yoyote asifanye lolote kwa mchumba wake, lakini niliyoyaona hapo yalionyesa wazi kuwa kuna jambo jingine.

Walipoingia,walimuamrisha yule binti avue lile gauni la harusi, na aliposita kufanya hivyo, yule mwanamama ambaye alikuwa kavaa mawani makubwa na nywele za bandia, alimvua yule binti kwa nguvu, na lile gauni wakamvalisha yule msichana waliyekuja naye, akafanya kazi ya kumremba, ili aonekane sawa na huyo binti, bibi harusi mtarajiwa, …

‘Nyie ni nani na manataka kufanya nini….’akawa analalamika yule binti, akawa kazibwa mdomo…

Yule mwanamama, akamvalisha yule binti haya magauni mapana,na kumvisha nywele za bandia kama yeye, akamvalisha miwani, aliyokuwa kaiweka kwenye mfuko wake,na alipomaliza, akamshika mkono, na kumkabidhi mmoja wa wale vijana atoke naye, yeye akabakiwa kwa muda,  na baadaye naye akatoke na wale wengine,…huko nje bado kulikuwa na vurumai ya aina yake…

Nilipoona kupo kimiya, nikajitokeza pale mlangoni, na yule binti alikuwa kajifunua usoni, akijiandaa kukaa vyema alikuwa kajisahau kwani alijua kuwa hakuna mtu, na akageuka na kuniona, akakunja uso,  akionyesha wasiwasi,  akauliza;

‘Wewe ni nani….?’

‘Kama ungelikuwa wewe ndiye muhusika usingeliniuliza hilo swali, niambie wewe ni nani kabla sijakuumbua…’nikasema kwa hasira.

‘Waulize hawo walionileta hapa, mimi sijui, na ukiniumbua hutapata faida yoyote, maana kila kitu kimeshakamiika, wewe unatakaje, fanya ufanyalo, ….lakini na mimi nitakuwa nimelipikiza kisasi, hawezi kuniacha na kuja kumuua huyu kinyangarika….’akasema akionyesha kutokujali.

‘Hebu niambie kuna nini kimepangwa, maana sizani kuwa hayo yana lengo jema kwa muoaji, kwanini mumefanya hivyo…?’ nikauliza.

‘Liwe lengo jema au baya, mimi sijui, mwisho wa siku na mimi nitakuwa nimetimiza lengo lang, na pia nitakuwa nimeshika mkwanja wanguvu, yeye si anajifanya ana pesa, na anaweza kubadili wanawake kamanguo, tutaona leo,…mengine tutajua mbele kwa mbele , na wakizubaa nakuwa mimi bibi harausi….hehehehe…mjini hapa, alifikiri mimi ni wakuja,…atakoma ubishi…’akasema huyo binti, na kujifunik vyema.

Mara nikasikia kama watu wanakuja, …wengi wakisema `bwana harusi anakuja….’ Na yule binti akajifunika usoni na mavazi yake ya bibi harusi, asionekane usoni, na mimi haraka nikafungua mlango, huku nimevaa kofia langu pana, lillofunika uso wote, nikatoka haraka na kukutana na shangazi mtu,pale mlangoni, aliponiona akanitilia shaka,akaniuliza;

‘Wewe ni nani…?’

NB: Naona muda umekwisha, wewe ni nani jibu tutalipata sehemu ijayo, tukijaliwa.

WAZO LA LEO: Dunia ilivyo, na wanadamu tulivyo,  hata kuwe na sheria kali kiasi gani,bado kutakuwa na wavunja sheria. Hii ni kutokana na kukosekana kwa haki, ukosefu wa maadili mema, kulikotokana na ukosefu wa malezi bora. Tukumbuke, malezi bora , na maadili mema yanajengwa toka utotoni, toka kwa wazazi na walezi.


Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Hongera, kazi nzuri, tunasubiri vitabu vya visa vilivyopita, swali langu hujanijibu, kwanini ww hupendi kuweka picha yako tukujue?

emu-three said...

Nashukuru Anony hapo juu,kuwa nami,na sifa zako kwangu.Na ni kweli najitahidi kuzipitia hizi kazi, ili ziwe katika mfumo mzuri wa kitabu. Ni kazi ndefu, na inahitaji muda, ndio maana hata kisa chetu kipya nakiandika kwa ufupi zaidi, ili niweze kupata muda kidogo wa kupitia kazi zilizopita. Na wewe kama unajinsi yoyote ya kusaidia tunakukaribisha.

Ama kuhusu kutokakutaja jina langu kamili, au kuweka picha yangu kwenye blog, mimi sio lengo langu kubwa,lengo langu kubwa ni kutoa kile nilichokuwa nacho ambacho siku nyini nilikuwa nikitafuta jinsi gani ya kukitoa kwa wenzangu ili wapate kukiona. Na kama haya ninayoandika yanakubalika, basi hilondilo lengo langu kubwa, sura yangu sio muhimu sana, kuliko hilo lengo langu,na kama ni lazima ipo siku nitaweka picha yangu!

Nashukuru sana kwa wazo lako, na tupo pamoja

Anonymous said...

Thank you, I've just been searching for information approximately this subject for a long time and yours is the best I have came upon till now. But, what concerning the bottom line? Are you positive in regards to the supply?
Take a look at my page ... Bielizna

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Mbona Annony hajataja jina lake, mahali alipo na kuweka sura yake? Hoja na maswali mengine bana!
Anyway, ukipata nauli M3 wawekee sura yako na majina yako yote ambayo yako kwenye rejista ya mjomba ha ha ha ha haaaaa!

Yasinta Ngonyani said...

Nasubiri sana kujua "wewe ni nani? kazi nzuri ndugu wangu.. nimecheka kidogo na nimejikuta najiuliza kwa sauti. Usiye na jina hapo juu wewe umeuliza kwa nini asiweke picha yake na jina lake kamili? Nimeona kama umejiuliza mwenyewe mbona wewe hujaandika jina lako?...samahani kwa kutoka nje ya mada lakini..