Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, August 9, 2012

Hujafa Hujaumbika-80 hitimisho-38(mwisho)



         
             %%%%%%%%%                         HITIMISHO             %%%%%%%%%%%%%%
Wakili mwanadada na yule binti walipotoka pale hospitalini baada ya nesi kuchukuliwa na polisi, waliwapitia Msomali na Tausi ambao walikuwa wakimsubiri kwa hamu, na wakati wapo hapo, alikuja naye mke wa wakili mkuu, akionekana mnyonge kupita kiasi, alimsogelea yule binti yake wa kufikia wakakumbatiana, na kilio kikitanda kwa muda baadaye wakatulia.


‘Pole sana binti yangu, naamini sasa haya yamekwisha, na uwongo uliozuliwa na watu wasio wema, mwisho wake umewaumbua wao wenyewe, ….’akasema mama mtu.

‘Ahsante mama yangu, pole sana na wewe pia, mpaka sasa siamini kuwa haya yote yametokea, na kweli sina hata la kusema…..’akasema huyo binti na kabla hajamaliza akaingilia wakili mwanadada,nakusema;

‘Jamani samahanini sana, najua mna maswali mengi ya kuniuliza, mna mengi ya kuongea, na muda hautoshi, ninachoweza kuwaambia kwa sasa ni kuwa,nyie wote, bado mnahitajika mahakamani, kuna taratibu za kwaida tunahitajika tukazifuate, maana nyie mumehusika bila kujua kwenye hili kundi haramu..na katika …..lakini nitakwenda kuyamaliza hayo….’akasema huku akiwaangalia mmoja mmoja.

‘Hilo kundi haramu ni kundi gani  hilo , …?’akauliza yule binti.

‘Kundi hilo haramu mwanzoni lilianzishwa nchi ya jirani, kabla halijashutukiwa na kusambaratishwa, …baadaye wahusika wale wakatawanyika, na wengi waliingiahuku kwetu kwa mbinu zao, na bila hata kujulikana kuwa huko walipokuwa walikuwa na makosa. Wengine walikuja huku kwetu, na kwa vile walikuwa na taaluma zao, waliomba kazi, na sisi tulichojali zaidi ni zile taaluma zao, wakaajiriwa humu nchini.

Na wengi zaidi ya walioingia huku ni Watanzania wenzetu, ambao huko pia waliishi kama raia, hakuna aliyewashutukia kwa hilo. Wazo la kuendeleza hayo waliyokuwa wameyaanzisha huko walipokuwa bado walikuwa nayo kichwani mwao, kwani walishaonja asali na kungundua kuwa kazi hiyo inaweza kuwaingizia pesa nyingi.Wakaanza kuwasiliana, na baadaye wakakubaliana kuwa hapa nchii wanaweza kufanya mambo yao bila kujulikana.

Huku alikuwepo Sokoti, na wataalamu wengine, ambao mtawaona mahakamani, hutaamini kabisa ukiwaona kuwa kumbe walikuwa ni watu waliovaa ngozi ya kondoo kumbe ni chui. Ni wataalamu kweli  kwenye fani zao, lakini walizitumia hizo fani kama sehemu ya kufichia makucha yao, na kiukweli huko walipotoka walifukuzwa makazini kwasababau mbali mbali za ukiukaji wa sheria, wapo madakitari, wanasheria, wanajeshi, na watu wa kila fani hata waheshimiwa.

Kitu walichofanya ni kuchunguza udhaifu wa watu, kama binadamu kila mtu anaudhaifu wake, ambao kama aspojitahidi zaidi unakuwa ni ulevi. Wapo watu wana wake zao lakini ile tabia ya uzinzi imewatawala, wapo walevi kupindikia, wapo wala rushwa, wapo wenye tamaa za kupata zaidi, zote hizo ukichunguza ni makosa makubwa. Wao wakazifanyia kazi , na kugundua kuwa hapa nchini, wengi,hasa viongozi wana tabia hizo.

  Kwahiyo wao wakaanza kama kundi maalumu la kurekebisha tabia, kila mmoja akianzia sehemu yake ya kazi, na baadaye hukutana wenyewe na kupeana taarifa ni nani katii viongozi, au matajiri anaweza akafanyiwa hayo waliyoyapanga. Waligundua kuwa ndanii ya ndoa watu wanamatatizo makubwa, huwezi amini hilo, watu wanafika makazini, wanaonekana wapo shwari, lakini ndani ya ndoa zao kuna sintofahamu. Hiliwaliliona na wakaona kumbe huko kungekuwa ni sehemu ya kuanzia.

Kuna sehemu nyingine ambazo pia waliziona kama vile makazini,waliguduakuwa viongozi wengi ni wadhaifu,…wana madhambi mengi, kama kula rushwa kupitisha miradi kinamna , wakaona na huko wanaweza kuchomkea mambo yao kwa mtindo ule ule, ambao wenzetu wanauita blackmail, au mlungula…wakachomeka mambo yao, kinamna.’akatulia na kuwaangalia watu wake kama wamemuelewa.

‘Mambo yao ni kama yapi,…wao walibuni njia moja rahisi , kwanza ni kuwa na watu wao ambao wanajiingiza kwenye hiyo mipango, mtu anaingia kwenye makubalianoyakupitisha miradi mbali mbali, zabuni nk.Wanachofanya wao, ni kuchukua picha ya video wakati mambo hayo yanafanyika  …liwe tendo la kugushi nyaraka, kupitisha miradi ya uwongo, kukubali zabuni za uwongo, kufumaniwa, na mengine ambayo ni dhuluma kwa jamii.. wanahifadhi zile kanda.

Wakihitaji pesa kutokana na mpangilio wao, ambao kwanza wanaangali huyomtu ana kiasi gani kwenye accounti yake ya benki, hawakurupuki tu. 

Wao kwa mtizamo wao, kama watakuja kugundulikana watajikosha kwa kusema walikuwa wakipigana na hawo watu wabaya ndani ya jamii, kama uliwahi kumsikia nesi akisema `wengi hawatamuelewa kwa sasa, wao walikuwa kwenye vita ya kupambana na wahujumu, wazinzi nk…’. 

Lakini kwa vipi muwadai hawo watu pesa nyingi, maana hawa watu ni matajiri wa kutupwa, wana majumba makubwa na miradi mingi, imekuwaje wakachuma huo utajiri kwa muda mfupi, hapo ndipo tunapogundua kuwa lengo lao halikuwa jema, lengo lao lilikuw akuchuma kwa kutumia mgongoo wa udhaifu wa watu katika jamii….’akasema wakili mwanadada.

‘Kumbe….’akasema mke wawakili mkuu.

‘Ndio hivyo, jitahidini wanandoa, jitahidi sana msifarakane, maana mambo kama haya yanakuja kwa kasi, huku kwetu hayakuwa wazi kiasi hicho, sasa watu wajanja wameshagundua kuwa kumbe watu hasa watu wakubwa, wanaweza kutumiwakutokana na udhaifu wao, hasa katika ndoa na mambo yao mbaya yakitumiwa kama vitisho yanaweza yakawa mradi mkubwa.

Kitu nilichokigundua ni kuwa , waume wengi, hasa wale walioshikilia madaraka, matajiri , na wafanaybiashara wakubwa, wana matatizo mengi ndani ya ndoa zao, na kwa hivyo wamekuwa wakitoka sana nje ya ndoa kisiri, na matokeo yake, wakajikuta wakinaswa na mtego huu,…na kwa kuogopa kashfa, na kwa vile,... kashifa kwao itawaharibia kila kitu, na ili wasiingie kwenye hiyo kashifa inabidi wahonge, ….watoe chochote ili wasianikwe madhambi yao, ….sasa jitahidini jamani

‘Umesema hutaki swali lakini mimi bado sijaelewa kwanini walimuua Kimwana nay eye alikuwa ni mtu wao?’ akaulizwa swali.

‘Kimwana alikuwa mtu wao na ni mmoja wa viongozi, yeye alikuwa upande wa ndoa za watu, yeye kazi yake ilikuwa kuwanasa wanaume wasiotulia ndani ya ndoa, na kuhakikisha kuwa kuna vielelezo muhimu ambavyo vitamfanya yule mtu aogope, na afuate hayo wanayoyataka. Wao walipewa kazi hiyo mapema, kama majaribio, bila wao kujijua, wakapata mbinu za kuibia watu kwa kuwabambikia kesi….

Hata nesi alipokuja hapa nchini toka nchi ya jirani, Kimwana hakuwa anajua kuwa huyo nesi ndiye aliyekuwa akiwafundisha mbinu za kupata pesa  kwa njia hiyo ya kubambikia wanaume waliomtaka kimapenzi, aliyekuwa akijua hilo ni Sokoti na dereva wake, na baadhi ya viongozi wengine ambao walikuwa wanachama,lakini hawakutaka kabisa kujulikana.

Hata siku ile Kimwana alipoitwa kuwa anatakiwa kujiunga, hakujua kuwa wenzake walikuwa wamemjua siku nyingi, na walishaona kuwa anafaa katika kundi lao. Na alipokaa kwenye kundi kwa muda wakamuamini na kuanza kumpa siri za kundi, na hata kupata cheo cha juu kwenye kundi. Yeye akajiamini na kujua sasa yeye ni mmoja wa watu muhimu na anaweza kuwa na maamuzi ya juu, kitu ambacho wenzake hawakukubaliana nacho.

Mgogoro ukaanzia hapo, na kundi likakutana kwa siri bila Kimwana kujua, na wenzake wakakubalia kuwa aondolewe kweney ngazi za juu , na kama ataonaekana hawezi kutunza siri za kundi, ni bora wamzibe mdomo. Mbinu yao ni ile ile, ukitama kumuua mbwa muite majina mabaya, wakaanza kumpikia majungu na kumuonyesha kuwa ni mtu mbaya kwenye jamii, ili mwisho wa siku ikizwezekana jamii ndiyo imfanyie hilo walilolitaka, la kumziba mdomo.

Kama nilivyosema awali kwenye  kundi hilo kulikuwa na wataalamu wa kila namna, kati yao kulikuwa na watu wanajua kuigiza watu wengine, kilichohitajika ni mabadiliko kidogo kwenye mwili, na hata ikibidi mtu aliweza kuvikwa ngozi inayofanana na mtu wanayemuhitaji, na kuigiza kila kitu kama huyo huyo wanayemuhitaji.

‘Kama unakumbuka vyema, watu walioigizwa na mke wa wakili mkuu, na rafiki yake, hawo walionekana ni watu muhimu katika kutimiza malengo yao, kwa vile walikuwa na vigezo walivyovihitaji.Na rafiki wa mke wa wakili mkuu, kwa jina Tauzi, aliigizwa kwa vile alikuwa na kisasi na mtu aliyempenda,….na mtu huyo waliona wamuingize kwenye baadhi ya mambo yao kwa vile alikuwa na umbo la mvuto, la kuwapata wake wa wakubwa, walimtumia kwa minaji ya kutengeneza kashfa,….

 ‘Kimwana hakuwa legelege alianza kujihami mwenyewe,akiwa anamtumia dereva kama mlinzi wake bila kujua kuwa huyo dereva yake ni miongoni wa wahusika wakuu, licha ya kuwa walikuwa wapenzi wa mudamrefu. Utaona jinsi gani watu hawo walivyokuwa wasiri wakubwa.

Ili kumshinda Kimwana walichofanya kwa hatua ya kwanza ni ilembinu ya kumchonganisha na watu ambao walishaumizwa kwenye mambo yao. Wale ambao alifnya nao uchafu halafu ukatolewa mikanda, watu hawo hawo wengine walianza kumshuku Kimwana kuwa hunda anahusika, licha yeye kukana kuwa hata yeye hajui nini kinachoendelea. Jamii ikashituka, na wanajamii bila kujua, wakavutika na mtego huo, kuwa Kimwana ni mtu mbaya,….hawajua kuwa  avumae papa baharini, kumbe samaki wengine wapo.

Wakati wanamuwinda Kimwana,na huku wanaendelea na mambo yao,…walianza kumtema kwenye mipango yao, akaonekane kama mtu baki, wakamwingiza katika yale mabaya aonekane kama yupo kivyake, kama tulivyomuona, na walichofanya ni kupandikiza fitina pia kwa wake za hwo waume,kwa kusambazo zile kanda za mabaya aliyoyafanya

‘Kila mtu akawa anamnyoshea kidole Kimwana kuwa ni mtu mbaya, ndiye anayeongoza kundi la wahuni,….ndiye anatengeneza kanda mbaya,…..ndiye anayeiba waume za watu…na wake zao, wakaanza kujenga kisasi juu yake, chuki juu yake ikazidi. Na watu kama mke wa wakili mkuu, na rafiki yake wakaanza kumsaka kama tulivyoona.

‘Na ndio hapo mkajikuta nyie mkiingizwa bila kujijua, kwanza kutokana na mifarakano yenu ya ndoa, na historia zenu za kimapenzi ambazo walishazingundua mapema na pia kwa kupitia hizo shule walizozibuni kinamna, waliweza kuwajua undani wenu, na wale waliowahitaji, wao waliiga shule ile iliyoanzishwa na mama docta.Mama docta yeye alikuwa na lengo jema kabisa, wao wakatumia lile lengo jema la yule mama na kuligeuza kama sehemu ya kufichia mambo yao.

Walianza kufanikiwa na kukusanya pesa nyingi kwa wale waliojikuta kwenye mitego yao, ….wakanza kujiimarisha,..lakini dhuluma haidumu, na tamaa ya mzandiki, haikomi,…wakaanza kugeukana.

Kama mtakumbuka vyema kulikuwa na mwanadada mmoja ambaye alipigwa risasi. Huyu ni miongoni mwa wanadada watatu ambao waliaminika sana katika kuigiza sura na matendo ya watu wengine, hawa walikuwa karibu sana na Kimwana. Kimwana alipouliwa, wakaanza kuogopa, na kwa vile walimpenda sana Kimwana, wakaanza kutafuta mbinu za kujitia, kwani walijua kuwa huenda na wao wapo mbionikuuliwa.

Hawa walijua kuwa waliomuua Kimwana na hawo wanajamii waliumizwa, na mtendo wanayoyafanya, hawakujua zaidi kuna nini ndani ya kundi. Yule mwanadada akawa anataka kujitoa, kwani pia alishahidi kuwa watu kama Sokoti ambao ndiye aliyejulikana kama mkuu wa kundi keshaanza kumuonyesha chuki za waziwazi, na alishawahikuitwa kuwa anaonekana kuwa anataka kusaliti kundi.

Alipoona hivyo, akatafuta ushahidi na kuuweka kwenye kiboksi, humo aliweka mambo ambayo yangelisaidia kufichua baaadhi ya matendo kwenye hilo kundi, na picha alizopewa kwa ajili ya kuigiza kuwa yeye ni Tausi, na alishaambiwa kuwa Tauzi wakati mwingine anachanagnyikiwa, nay eye akaelekezwa jinsi gani ya kuigiza.

Na pale walipogundua kuwa Msomali anamfuatilia na huenda akaweza kupatikana, akaambiwa kuwa Tausi alikuwa kama anachanganyikiwa, kwahiyo Msomali akimkaribia anachotakiwa kufanya ni kumkimbia kinamna, kama vile anamuogopa, kamamlivyoona…Sasa huyu binti alipoona maisha yake yapo hatarini, ndio akaona ajitoe .

Je atajitoaje kwenye kundi hatari kama hilo,na usalama wake utakuwaje, akaona hana jinsi kwani ajitoe asijitoe, bado anajiona yupo hatarini, Alichofanya ni kutafuta jinsi ya kuonana na Msomali, ambaye alijua kwa sasa yupo peke yake hana mke, mke wake Kimwana keshauwawa, kwanza pia alisampenda, kwahiyo anaweza kuua ndeeg wawili kwa jiwe moja, akatayarisha vitu vya kuweza kumsaidia na kuviweka kwenye boksi, kumbe wenzake walishamgundua. Wakampiga risasi....!

Ukiangalia kwa makini, upigwa risasi wa risasi wa hawa wanawake wawili…. Upigwaji wa risasi hauna tofauti na ule wa Kimwana, ukiuchunguza kwa makini, wakawa wanajichora wenyewe, ina maana mlengaji huyo alikuwa mbali sana,lakini kwa vile ana shabaha kali aliweza kumlenga kwa kupitia kwenye upenyo mdogo tu. Hili tuliliweka kwenye kumbukumbu zetu za upelelezi, kuwa muuaji lazima awe na shabaha sana….

Huyu mwanadada alikuwa mahututi sana,na kwa vile tulishagundua kuwa anaweza kutusaidia kupata undai wa hilo kundi, tukatumia njia za kiuslama, kwakweli kutikana na hali hatukutegemea kuwa nangelipona,…aliponnea tundu la sindani,ila tulichofanya ni kumuondoa kabisa hapo hospitalini na kumpeleka nje ya mkoa huu, ambapo ndipo aliendelea na matibabu, baada ya kutubainisha wazo kuwa hata huko mahospitalini kuna watu wao, lakini yeye hawajui.

Tulichofanya ni kumweka mtu wetu wa upelelezi, akawa kama ndiye mgonjwa, …

Wakili mkuu aliwahi kuwa na mahusiano na huyo dada, na alijua kuwa huyo anaweza kuwa ni miongoni mwa hawo watu, na alishabonyezwa na watu wa hilo kundi kuwa huyo anataka kumfitini huko kazini kwake, na yeye bila kutambua akajitosa kummaliza akiwa kule hospitalini, kwani yeye alihsumizwa sana na hilo kundi, na alishafikia hatu ya kulimaliza hilo kundi kivyake, akaona njia bora ni kumuondoa mmoja mmjoa, katika hawo watu aliogundua kuwa wanahusika, katika orodha hiyo, walikuwep hawo dada watu,…akiwemo Kimwana.

Munakumbuka huyo mwanadada alilazwa muda mrefu hospitalini ,yule aliyekuwa pale muda wote hakuwa yeye huyo mwanadada, yule alikuwa mtu wa usalama aliyewekwa hapo ili kuwanasa hawo watu. Yule mwanadada aliyejeruhiwa na risasi alikuwa kafichwa nje ya mkoa, hili ilikuwa siri kubwa ndani ya usalama, waliojua ni mkuu , mimi na mtu mwingine, ambaye siwezi kumtaja hapa, kiusalama.

Huyo mwanadada, ingawaje alikuwa mtu muhimu kwao kwa kuigiza watu wengine, lakini hakuwa ana jua mengi kwenye kundi, ila alihisi kuwa Kimwana ni mtu muhimu kwenye kundi, lakini viongozi wengine walikuwa hawajui vyema. Kabla ha huyu dada, kutokana na jamii kuelewa kuwa Kimwana ni mtu mbaya, hata mimi kwa kipndi kile nilielewa hivyo, kwahiyo ili nimjue vyema Kimwana,  nikawa namtafuta Kimwana ili niweze kuongea naye, na ikibidi nimshawishi achane na hayo mambo anayonyoshewa anyo kidole.

Na kumbe kipindi hicho wakati namtafuta Kimwana na yeye alikuwa katika mipango ya kunitafuta, ili aniamie kile alichokusudia kuniambia,…wao wakalijua hilo mapema, wakatafuta njia zakumuwahi kabla hajaniambia chochote. Kimwana aliuliwa mikononi mwangu mwenyewe, kipindi ambacho, alishaamua kunisimulia kila kitu kuhusu hilo kundi….’akasema wakili mwanadada kwa sauti ya huzuni.

‘Ilikuwa kama anafahamu kuwa mwisho wake upo karibu,kwani kwa muda ule licha ya kujijua kuwa yeye ni kiongozi muhimu, lakini aliona jinsi gani walivyokuwa wakimtenga, …, nakumbuka kauli yake aliyosema kwa mara ya mwisho kuwa;

‘Najua nipo hatarani, lakini kabla sijakumbwa na lolote, nataka kukuambia jambo moja kubwa sana kuhusu kundi moja haramu,….ambalo nipo…na rafiki yangu mkubwa na asimu yangu ni mmoja wa kiongozi…’akasema na kukatishwa na hiyo risasi iliyomfanya apige yowe… Kwahiyo tangu siku ile mimi nikawa na kazi kubwa ya kumtafuta huyo rafiki yake mkubwa, na asimu yake ni nani…kumgundua ilikuwa jambo jingine, lakini kuwa na ushahidi wa kutosha ilikuwa jambo jingine la muhimu, lakini lilikuwa ni gumu sana,…’ akatulia huku akionyesha uso wa furaha.

‘Kwa ujumla haikuwa kazi rahisi, ukijua kuwa hawo wenzetu walishajiandaa, na walikuwa na watu wamewapandikiza kila sehemu nyeti, na walikuwa wasiri wakubwa, wakitumia kila upenyo kupenyeza mambo yao,kiasi kwamba ilikuwa vigumu kuwagundua,…na ndipo nikaja na mbinu ya kuwaita wale wote niliowahisi wanahusika kwa namna moja au nyingine, ili waje wajielezee wenyewe. Kwetu sisi mawakili inatusaidia sana, pale unaposikia mtu akiongea, akijieleza…na ukimhoji, unafichua mambo mengi…..’akatulia na kushika kichwa kama vile anakuna nywele zakke , halafu akasema;

‘Kwangu mimi kuuwawa kwa KImwana, ilikuwa ni sehemu moja muhimu iliyonifanya nizame ndani ya maficha ya amadui, ilikuwa ni kosa kubwa kwao , kwani kulinifanya nitafute kwanini, na kuna nini Kimwana alitaka kuniambia.

Wengi wangelichukulia kuwa ni migangano yao ya kikazi ,ni mambo ya wivu, lakini hata kama hilo, ….nilihisi kuna kitu kimejificha ndani yake,…. Kwao wao, waliona hio ndio njia njema ni kuwaziba mdomo wale waliotaka kuwasaliti. Na hata walipomuondoa Kimwana waliona wameondoa fitina, na ubaya wa damu, ukishaimwaga, inachochea mengi, wakatokea akina Kimwana wengine kama yule mwanadada, ambaye naye waliona njia njema ni hiyo hiyo kumziba mdomo..

Lakini kumbe akina KImwana waliibuka kila siku na walikuwa wameshahisi wapo hatarini, na wengine, walishachoka na mambo yao ndani ya kundi, ambapo walisema waziwazi kuwa wao waliokuwa wakitumika sana lakini wanaofaidi ni wachache…’akasema wakili mwanadada, na kutulia kwa muda kama vile anawaza jambo fulani kwa makini.

‘Kosa kubwa katika jamii yetu ni kule kuwaajiri watu bila kujua historia zao za nyuma, watu wanakuja kutoka huko nje, hawaeleweki kuwa huko walikotoka wametokaje, walifanya nini, sisi kwa ukarimu wetu, au kwa maslahi yetu, tunawakaribisha, ….tena hadi chumbani, tunawaajiri, tena katika sehemu nyeti, ..hilo ni kosa katika jamii yetu tuweni makini, maana mwisho wa siku inakula kwetu, inaumiza uchumi wetu, na kudidimiza maisha yetu, kwani uchumi mwingi unakimbilia nje, wenzetu wananeemeka, sisi tunazidi kubakia masikini.

`Angalieni miradi mingi, angalieni makampuni mengi yaliyokuwa makubwa, ni ajabu kuona ymefirisika, yanaendeshwa kihasara, na baadaye yanakuja kuuzwa,…, ina maana sisi hatuna akili ya kuyaendesha, hatuna wataalamu waliohitimu.?’ Akatulia kama vile anawaza jambohalafu akasema;

Sio kweli kwamba hatuna wataalmu, Wataalamu wapo, lakini kuna watu wameshachomekwa ndani ya jamii na mitizamo yao, wameshachomekwa ndani ya makampuni, ndani ya siasa, kila mahali sasa wapo, kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanafanikiwa malengo yao, na huenda malengo yao yakawa ni ya muda mrefu, mkija kugundua wapo mbali na wamesha jizatiti zaidi, kwa hatua nyingine, na sisi kwa kutokujua,tunaishia kulalamika, tunabakia masikini…..tunanyosheana vidole….’akasema wakili mwanadada.

‘Naona kuna mengi mnataka kuyajua, lakini mpaka hapo mumeshaona ni nini kilikuwepo,….mengine mtayasikia mahakamani ila kwasasa hawa watu hawana ujanja tena, maana wengi wameshaamua kusema kila kitu, kwa ajili ya usalama wao,…’akatulia kidogo na kujaribu kuwaangali watu kila mmoja kwa wakati wake, halafu alipoona watu wapo kimiya wakimngojee aendelee kuongea akasema;

‘Watu wameshaanza kuamuka, ndio maana unaona kila kona ya dunia kuna miamuko, maandamano, demokrasia inakua, vijana na nyanja mbalimbali zinakuja juu kudai haki na maslahi yao yanayopotea kiujanja, ….hizi nyakati na nyakati zijazo ni nyakati nyingine, na mwenye akili ya kutafakari anatakiwa kuchukua hatu mapema, na viongozi wajue sasa sio zile zama za kulindana tena, kila mmoja kakalia kuti kavu,…nawaasa viongozi, kuwa uongozi ni dhamana ya watu, sio sehemu ya kuchumia utajiri….

‘Wengi wa kundi hili wameliona hilo, wameona  ili wawe salama ni kuhakikisha wanasema ukweli,uliojificha, kwenye hilo kundi, na kutoboa madhambi yote ili wasifuge nyoka, nyoka mwenyewe ni nyoka mwenye sumu, ambaye mwisho wa siku atakuja kuwagonga wao wenyewe. Hilo wameliona na njia njema ni kulisambaratisha hilo kundi, ni kuwafichua viongozi wabovu,….na ikibidi kwa njia ya amani, ili sheria ichukue mkondoo wake. Lakini wakikaidi, sijui,….mtaona wenyewe ….’akatulia na kuangalia saa yake halafu akasema;

`Kwa sasa hatuna muda wa maongezi zaidi, naona ….muda umekwisha,..labda kwasasa kwa haraka ningelipenda kujua hatima ya ndoa zenu,….’akamgeukiwa mke wa wakili mkuu, na kumwangalia machoni,akasema ;

‘Hebu niambie, dada yangu mpendwa…ehe,  mumefika wapi?’ Mke wa wakili mkuu akajitahidi kutabsamu, na kwa sauti ya huzuni akasema;.

‘Hayo yapo ndani ya familia zetu, bado kuna mvutano, hatima ya yote itaamuliwa na familia zetu, ila msimamo wangu bado upo palepale…hadi hapo mambo yatakapowekwa sawa,….maana usije ukaishi na mtu kumbe hana upendo wowote na wewe,….’akatulia kwa muda, halafu kama vile kakumbuka kitu akasema;
‘Lakini kwa vile tumeshajua ni nini kilitokea, basi mimi nitakuwa tayari kwa lolote litakaloamuliwa na familia zetu….’akasema mke wa wakili mkuu.

‘Kwahiyo utakubali tu kwa maslahi ya familia na sio kwa ajili ya upendo wa moyoni?’ akauliza wakili mwanadada.

‘Mimi sio siri,nampenda sana mume wangu,lakini  je yeye ananipenda, hilo ni yeye aliweke hadharani, najua kwa sasa hana jinsi maana keshagundua kuwa mtu aliyekuwa akijifanya anampenda, na kweli alikuwa kwa namna moja au nyingine wanapendana, lakini pedno lao limeshaingia doa, na sijui kama lipo tena…’akasema mke wa wakili mkuu.

‘Haya…huko sitaki kudodosa tena,… hilo sasa tunawaachia wenyewe na familia zenu, je nyie….’akanigeukia mimi na Tausi,akatuangalai kwa muda kila mtu kwa zamu yake, akasema;
‘Hebu niambieni, ni nini hatima y a pendo lenu la kihistoria la toka utotoni hadi sasa hivi, niambieni Msomali na Tauzi, mna matarajio gani..?’ Tukabakia kucheka kwa muda huku tukiangaliana ni nani aanze kuongea, na mimi nikasema;

`Ama kuhusu sisi wawili tumeshakubaliana, ila mwenzangu anakwenda kusoma nje kwa miezi kadhaa, tumeona kuwa huo sio muda mwingi sana, tunaweza kuvumilia, na tumeona kuwa tusiharakishe hii ndoa, akirudi tutafunga ndoa yetu rasmi huko kijijini tukipata Baraka za wazazi wetu….’nikasema na Tausi naye akaendelezea kwa kusema;

‘Pia tumekubalina kuwa na yeye aendelee na masomo yake, ambayo ulishamuanzishia..licha ya kuwa hana kazi bado, ila wewe ulishamuahidi kuwa utmachukua kwenye ofisi yako mpya, kwani elimu ni muhimu sana,,…. Yeye ataishi kishida shida hivyo hivyo kwa kubangaiza hapa na pale, hadi amalize masomo yautafunga ndoa na kuunganisha nguvu za pamoja za mke na mume.’akasema Tausi, huku akiwa kamuangalia wakili mwanadada.

Wakili mwanadada akatabasamu na kusema;

`Nashukuru sana kusikia hilo, nami moyo wangu umefarijika kupita kiasi kwani lengo langu limetimia, ila kuna jambo moja nataka kukuomba dada yangu mpendwa,…’akageuka kumwangalia mke wa wakili mkuu;

‘Ni kuhusu huyu binti…najua ni binti yako naunamuhitaji sana kuwa naye, kwani ulimlea kama binti yako,..hata hivyo nahisi kuwa hata mimi nataka nitoe mchango wangu kwake….’akasema na kumwaangalia yule binti akiwa kashikana na mama yake wakufikia.

‘Aaah, mimi sikatai mchango wowote, ingawaje sijajua ni mchango gani,…na hilo halihitaji kukaa na mwenzangu maana kama ulivyoona,…siwezi kumwamini moja kwa moja tena…lakini hilo nitaliangalai mwenyewe kwa makini…’akasema huku akikunja uso wa huzuni.

 `Mimi sio kwamba nataak kutoa mchango wa pesa, ….nataka nimchukue huyu binti, nikae naye, mimi nataka nimsomeshe mwenyewe, lakini akiwa kwangu, nataka awe wakili kama mimi…’akasema huku akitabasamu, lile tabasamu la furaha.

Yule binti aliposikia hivyo akamgeukia mama yake, na mama yake wa kufikia akatabasamu, akawa kama anamuuliza je upo tayari kwa hilo, kwa ishara ya uso na mdomo…Yule binti akamkimbilia wakili mwanadada, na kumkumbatia na kusema `nashukuru saa…ama kweli wewe ni dada mwema, mimi nipo tayari, lakini tu kama mama atakubali’

Mke wa wakili mkuu akasema;


‘Mimi sina shida,siwezi kukataa maana watoto ni Wetu sote, na kila mtu ana jukumu la kusaidia watoto hawa, ili waondokane na huo unyonge wa kujiona, masikini, au mayatima,…nimekubali na utakuwa umenisaidia sana, kwani bado sitakuwa na imani akiwemo hapo na mume wangi, ingawaje sijajua majaliwa na hiyo ndoa, ila kwa vyovyote itakavyokuwa,tutashirikiana na mwenzangu huyo kuhakikisha kuwa unafanikiwa katika hayo masomo , uwe wakili mwema ili uje uwatete wanawake, …’ akapiga makofi na wengine wakamfuatia, na kupiga makofi ,halafu akaendela kusema;

‘Unajua sio siri, wanawake wengi wamejikuta kwenye mitihani migumu, ….kuna mitihani ya kimaisha, kuna mitihani ndoa, kuna mitihani ya malezi, na mengine mengi ambayo kwa mwanamke imekuwa ni mzigo, na hata wengine kujikuta wakidhukumiwa haki zao bila kujua …basi nyie mkiwa wasomi wengi, mtaweza kuzitetea hizo haki zao,  ….nakutakia kila la heri

Mimi nikamgeukai Tausi na kusema ; ‘Nakupenda sana Tausi naomba uwe mke wangu…,’

Tausi akacheka kwanza na kusema ‘Mimi hata bia kusema neno, nilishakubali kwa matendo,na mungu ni shahidi yangu, ..nakupenda sana Msomali wangu….na nimekubali niwe mke wako…..’
Watu wakashangilia na wakili mwanadada akasema,`sio mbaya mkIkumbatiana kidogo, ..kidogo tu, kuonyesha sasa kuwa nyie ni wachumba…’

 Tausi kwanza aliniangalia kwa aibu, akasita kunikaribia, mimi nikatabsamu, aibu kwangu haikuwepo tena, soni kwangu kulitanda ni ile taswira yautotoni, wakati tupo kwenye ile michezo ya baba na mama, na hapo hapo, nilimuona Tausi kama ua waridi lilifunguka , au kama yule ndege Tausi akitawanya mkia wake na rangi mbalimbali za  kupendeza zikatawala ubongo wangu, nikajikuta nikinyosha mikono ya kumkaribisha Tausi kifuani kwangu, akanisogelea tukakumbatiana kwa furaha….vigelegele vikanda hewani.

*******

Rafiki yangu hayo ndio maisha yangu, na sasa nipo kwenye harakati za kusoma, ndio maana unanikuta nipo hohehahe, lakini nikijua kuwa mchumia juani hulia kivulini, na nimejifunza mengi kuwa katika maisha haya, usikate tamaa, kwani yapo membo ya kujifunza, na yapo mengi utapambana nayo, kwani hujafa hujaumbika.

%%%%%%%%%%%%%% %%  MWISHO.   %%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%

NB. Nawashukuru wote mlioshiriki nami kwenye kisa hiki, sina uhakika na hisia zenu , jinsi gani mlivyokipokea hiki kisa, kama kimekaa sawa basi mungu atujalie tukifanye kiwe kitabu,kama kuna kitu kinahitajika zaidi ,basi wewe kama mdau muhimu kwangu, na mshiriki muhimu nakuomba utoe maoni yako. Tupo pamoja daima.

WAZO LA LEO:Wengi wa watendaji wetu, au wale walipo kwenye nyazifa fulani,  hujali sana maslahi yao binafsi, bila kuangalia maslahi ya watu wengine, inapofikia kwenye maamuzi ya maslahi, hatukumbuki kuwa cheo hicho ni dhamana, na tunaotakiwa tuwajali nao waliotukabidhi dhamana hiyo, tukumbuke kuwa Ubinafsi ni uchoyo na mwisho wake ni kudhalilika tu. 


Ni mimi: emu-three

11 comments :

Anonymous said...

Umefunga kazi mkuu nakuaminia. Tunasubiri kisa kipya, naomba usichelewe maana nina hamu sana na hichokisa kipya , sijui kitakuwaje, wengine huo ndio ulevi wetu.

Anonymous said...

HONGERA SANA ndg yangu.

Yasinta Ngonyani said...

Kazi nzuri sana na wala huhitaji kuongeaza wala kupunguza hivi hivi kilivyo kinafaa sana sana kuwa kitabu. Ukikitoa kitabu nitakinunu na kukisoma tena kama marudio kama ilivyo desturi yangu kurudia. Ama kweli watu wamejaliwa vipaji una kipaji ndugu wangu unajua kuchonga kalamu kufikiri na pia nakusifu sana si MCHOYO. PAMOJA DAIMA!!

samira said...

comment inasumbuwa kila nikiweka inarudi may be network ,i hope upo ok m3 mungu akuzidishie kipaji unacho sana na tunakushukuru sana kuwa nasi mwanzo hadi mwisho ,tumejifunza mengi sana muhimu binadamu ni subira na kustahamili maisha mzunguko na hujafa hujaumbika
hata ivo thank you m3 na ramadhani kareem kwa wote
ni mimi samira

Rachel Siwa said...

Mmmhh ndugu wa mimi kazi yako nizaidi ya nzuri yaani nashiwa maneno.
Mungu azidi kukubariki sana sana kwa kazi za mikono yako na mengine meeengi.

Nakutakia Mfungo mwema na kila lililojema.
Pamoja daimaaaaaa!!!!!!!

Subira said...

Hongera sana kwa kumaliza kuandika hiki kisa. Kina mafundisho mengi na mazito hasa kwa watu walio kwenye uhusiano au wanaotaka kuingia kwenye uhusiano.

Rai yangu iko pale pale, anza kukipanga kwenye mtindo wa manuscript ya kitabu, wakati huku kwenye blog ukiweka visa vifupi vifupi ambavyo baadae vitakuwa short story. Kazi ya manusrcipt si ndogo na ni ngumu lakini huna jinsi ili kiwe kitabu lazima uanze kuipanga kuanzia chapter 1 mpaka ya mwisho. Usiwe na papara kuwa uifanye leo itaisha kesho. Ukimaliza mie nitakusaidia kufanya editing wakati tukimtafuta Publisher. Kumbuka end of September uwe umeshafika somewhere kwenye manuscript na mimi ndio angalau kipindi hicho naweza kusema ninaweza kuwa nina nafasi ya kuipitia InshaAllah.

Nakutakia kila la kheri, waswahili wanasema mambo mazuri hayataki haraka na Mola yu na mwenye kusubiri.

emuthree said...

Ohh, sijui niseme nini, nmefarijika sana, kuwasikia ndugu zangu wapendwa. Ndugu wangu Yasinta, ndugu wa mimi Rachel, tupo pamoja.

Samira,nilijua upo likizo maana sijakusikia, nashukuru kama upo salama, na tupo pamoja tena. Lini utakuaj huku bongo tena?

Subira meneja wangu, nashukuru kwa wazo lako jema kabisa, nalifanyia kazi tutawasiliana. Tumuombe mungu atupe uhai.

Na wengineo wote, Anyon, na wale wa kimiya kimiya, tuwe pamoja na kila mwenye wazo asisite kulitoa, maana kwenye wengi hapaharibiki kitu.

Precious said...

Hongera sana maana mkasa umetufundisha mambo mengi sana ya maisha na changamoto tunazokutana nazo majumbani, makazini n.k. Lakini M3 samahani kwa kukurudisha nyuma Wakili Mdada hukutumalizia mambo ya ndoa yake au uchumba wake ilikuwaje?..tunasubiri kwa hamu mkasa mpya najua utakuwa moto kama kawaida yako. Tunakuombea sana Mungu asikie sala zetu siku 1 nawe ufaidi kazi ya mikono yako.

emuthree said...

Mmmh Precious,ungenikumbusha mapema,lakini hata hivyo, huyu mwanadada hakutaka sana kusimulia mamo yake, licha ya kuwa alitaka kujua ya wengine, lengoolake ni kujifunza kwa wengine, kuwasaidia na ili ajua nini cha kufanya kwenye ndoa, yake.

Niliwaza kuongeza mambo yake hapa, lakini mambo yake ni kisa kingine,...siji kwenye kitabu itakwuaje, maana nahisi kitakuwa kitabu kikubwa sana,labda kiwe sehehe sehemu, yaani cha kwannza , cha pili na cha tatu, nitajaribu kuweka mamboo yake kidogo, ndani ya kitabu kuelezea nini kiliajiri kuhusu yeye,...nashukuru sana kwa kunikumbusha hilo.
Tupo pamoja

Precious said...

Nimekuelewa M3 na tuko pamoja sanaaaaaaa

samira said...

m3 nashukuru my dear nipo ila nilikuwa mbali kidogo na makazi yangu ikawa ngumu japo napita kimya kimya sasa nipo home ila bado nipo sijaja nikija nakutafuta
ramadhan kareem