Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, August 3, 2012

Hujafa hujaumbika-79 hitimisho-37



Aliendelea kuongea nesi....

                                                     *****
‘Niliogopa, ….yaani nilihisi mwili mzima ukiniisha nguvu , kwanza akili haikuamini kwa haraka kuwa ni yeye, pili nilikuwa nikijiuliza kwanini afanye jambo kama hilo, maana mimi nilijua kama ni mbaya wake ambaye angeliamua kumfanyia hivyo, angelikuwa baba yake, aliyembaka, …..

Akili ya haraaka ilikuwa jinsi gani ya kumsaidia huyu dada, nilichofanya nikwenda pale ilipokuwa ile silaha, na kuiweka kwenye mfuko wake, na mawazoni mwangu, ilikuwa niichukue, nikatafute sehemu ya kuificha, kama sio kuipoteza kabisa…ikibidi nikaitumbukize baharini.

Kuna kitu kimoja nimejifunza , silaha iliyofanyia mauaji inakuwa kama imenasa damu ya mtu, na ile damu inailinda ile silaha, maana mimi nilijua ni kazi rahisi, tu,nitaichukua ile silaha, na njia nitakuwa na muda wa kuiifua alama za vidole,maana huyu mwanadada, hakuwa amevaa chochote mikononi, tofauti na wale akina dada wawili, wao walijua nini wanakifanya.

‘Na wewe ulikuwa umevaa chochote mikononi, maana hatukuona alama zako za vidole?’ akauliza wakili mwanadada.

‘Hilo sio swala la kuniuliza mtu kama mimi, professional..mimi ni askari, najua nini ninachokifanya, ….nisingeliweza kwenda sehemu kama hizo nikiwa na mikono mitupu, najua nini kitatokea abadaye,sifanyi makosa kama hayo…’akasema.

‘Je huenda huyo mwanadada alikuja kuikamata hiyo silaha baadaye kwa mipango yako, ili ionekane kuwa ndiye kaishika…’akasema wakili mwanadada.

‘Hayo ni mawazo duni,..kama hujafuatilia vyema, nenda kafuatilie tena, kama unahitaji zaidi nenda kaanzie kwa huyo aliyemuazima hiyo pikipiki ,nenda hadi kule alipoiweka, kuna watu walimuona,…na hata wakati anatoka kuna watu wawili waliweka gari lao, walikuwa wamesimama nje ya gari lao, wakishangaa nini kimetoeka kule kwa Kimwana, waligeuka kumwangali huyo mwanadada wakati anatoka pale na kupanda pikipiki…

‘Kwanini wao hawakuiarifu polisi kuwa wameona mtu kama huyo?’ akauliza.

‘Hilo swali ungeliwauliza wao, na najua nini unachofikiria, kuwa labda niliwaweka mimi, ili waje kuwa mashahidi wa kuonyesha kuwa walimuona huyo binti…nakuambia ukweli hivyo ndivyo ilivyokuwa,…amini , usiamini, ..na hata hivyo, mimi sijali,nipo tayari kwa lolote lile ilimradi  niweze kusaidia …’akasema .

‘Haya endelea na maelezo yako, maana hujamaliza,…..’akasema wakili mwanadada.

‘Hata nikiendelea anona kama huniamini, lakini sio mbaya, amini usiamini, nitakuambia tu ilivyokuwa, …’akasema na kutulia kwanza kwa muda, kama vile anawaza jambo.

‘Kwenye hiyo barua yeye alikuandikia nini…maana unavyonibishia nahisi huenda kakuandikia tofauti na maelezo yangu,…?’ akaniuliza.

‘Haya aliyoniandikia yananihusu mimi,na siwezi kukuambia kwa sasa, ninachotaka ni kuhakikisha kuwa maeelzo yako yapo sawa na alichoandika yeye, …..au umeshaanza kujishitukia?’ akauliza wakili mwanadada.

‘Kwanini nijishitukiea wakati ninayokuelezea ndivyo ilivyokuwa,….sina wasiwasi na hilo, kwasababu nimejiandaa kwa vyovyote vile, mimi nilishakuw atayari kubeba yote, na hata wakati nakunywa sumu, nilitaka niondoke, nikiwa najulikana kuwa mimi ndiye niliyemuua Kimwana, ….lakini naona haikufanikiwa, hata hivyo, kama tutakuabliana nipo tayari kukubali kuwa mimi ndiye niliyehusika, laini kawaida yangu, huwa sikubali moja kwa moja, hiyo ni kazi ya usalama kuthibitisha…

‘Makubaliano gani hayo unayotaka tuyafanye mimi na wewe?’ akauiza wakili mwanadada.

‘Uiharibu hiyo barua, na usiseme  lolote…..mambo yaishe kimiya kimiya, mimi nitakwenda kukitumikia kifungo, kama ni cha maisha hewala, kama ni kunyongwa, hewala,…nipo tayari…’akasema.

‘Kwanini uwe tayari kubeba makosa ya mtu mwingine, ilihali wewe mwenyewe unajua kuwa hilo ni kosa, sio kwamba wewe unajiona kabisa ni mkosaji mkuu, kwa kumrubuni binti wa watu, asiye na hatia, kiujanja,ili mwisho wa siku afanye lileulilotaka kulifanya wewe,…au hujui kuwa tumehsligundua hilo,..ama usingelikuwa wewe huenda huyo unayemuona anakosa asingelifanya hilo kosa….kama kweli alifanya yeye….’akasema wakili mwanadada.

‘Hebu nikuulize swali moja, kwanini wewe unaniona kuwa mimi ni mkosaji,..tangu mwanzo nakuona huniamini na hunipendi, kwa kauli zako na maswali yako, nimekukosea nini mpendwa…mimi ninajaribu kukuambia ukweli wewe unaniona na kudanganya..kwanini lakini..?’ akauliza.

‘Ina maana huoni kosa lako toka mwanzo,wewe unaona makosa ya wenzako, ya wengine huyaoni, hebu nikuulize, kama nisingeliinama siku ile, mimi sasa hivi ningelikuwa nani….?’ Akauliza wakili mwanadada.

‘Ungelikuwa maiti….hiyo ni vita, huwezi kunilaumu kwa hilo, pale sote tulikuwa kazini, tifauti yetu ni kuwa mimi nilikuwa upande wa maadui, na wewe upande wa serikali….lakini lengo letu lilikuwa ni moja kuwa tupo vitani, huwezi kunilaumu kwa hilo, cha muhimu ni sheri ikufuata mkondo wake,….’akasema kwa kujiamini.

‘Na kweli itafuta mkondo wake,…hilo nauhakikishia…na huo mkono wako, uliofunga plaster ulifanya nini…?’akasema wakili mwanadada na kuuliza swali kwa kiujanja.

‘Hili sio siri, niliumwa na nyoka…..’akasema.

‘Uliumiwawapi na yoka..?’akaulizwa.

‘Niliumwa siku ile wakati naificha hiyo silaha, kwenye kabati pale kwa nyumbani kwa wakili mkuu…’akasema

‘Siku ile wakati unaificha huyu binti alikuwa wapi?’ akaulizwa.

‘Mimi sijui maana nilifika pale na kukuta hakuna mtu…na wakati nahangaika kutafuta sehemu ili nikafute hizo alamaza vidole, nikasikia mtu akija ,nami kwa haraka nikaificha hiyo silaha kwenye hilo kabati, kumbe kulikuwa na nyoka…akaniuma…’akasema.

‘Wewe unajifanya mjanja sana, uumwena yoka, na uwe na ujasiri wakufanya hicho ulichokifanya…ile silaha kama ilivyo, na jinsi ilivyokuwa humo ndani,ingeliweza kuufungua ule mlango,…haingelichukua muda, ilesilaha ingelidondoka,….’akasema wakili mwanadada.

‘Una maana gani kusema hivyo?’akauliza nesi kwa kushangaa.

‘Nina maana kuwa huyo nyoka pale ulimweka wewe, …na slikuwa sio nyoka wakweli, ni nyoka bandia, ni plastic, ambayo kama kweli huijui utasema kuwa ni nyoka, ….uliitupa kwenye jalala, siku ile ulipoona haina kai tena,…lakini tulikuja kuipata, na ukumbuke wakati unaituoa ulikuwa umeshavua soksi za mikono, na hapi tukazipata alama zako zamikono….utabisha nini hapo…’akasema wakili mwanadada,

‘Sasa unataka kusema nini hapo kuwa mimi ndio ….?’ Akauliza nesi nakukatisha kile alichotaka kusema.

‘Ile silaha uliiweka vile ,pale kimakusudi, ule  mlango ulifunguka kwa sababu ya uzito wa ile silaha, ikatokeza nje, yote hiyo uliipanga mapema,  ili huyo binti aione, aishike na aache alama za vidole kwenye hiyo silaha…..na kweli huyo binti alipoiona wakati anafanya usafi, aliogopa sana, akijua lolote atakaloongea kwa baba au mama yake hataeleweka, akairudishia pale kwenye kabati na kuiweka vizuri,ili kama ni baba yake kaiweka, aje aikute mwenyewe, hakutaka kusema lolote kuhusu kuiona hiyo silaha hapo....’akasema wakili mwanadada.

‘Hivi wewe unafikiri haya yote ninayokuambia nimeyatunga kichwani mwangu,…hiyo barua ilisema nini, maana ndiyo msema kweli?’ akauliza nesi.

‘Hiyo barua uliindika wewe…..na ulichofanya ni kubadili barua aliyoiandikia huyo binti ya kweli, ambayo uliichana, lakini hukuichana ipasavyo, tumeiunganisha vipande vyake…na kuona nini alichokuwa kakiandika huyo binti, ….wewe ulijua ni nini ataandika kwani ulishaongea naye, ukaongezea hayo yakeo mengine uliyabuni wewe,….’akasema wakili mwanadada, na nesi akacheka kwa dharau.

‘Na huo mwandiko wake je….maana uwongo wako hauna maana…’akasema.

‘Wewe unajua kugushi saini za watu, sembuse ushindwe kubuni mwandiko wa mtu…kwenye kundi unajulikana kwa kuigiza matendo, hadi kuandika….uliigiza mwandiko wa huyo binti, na ipo siku ulimwanikia kitu akashangaa na kujiuliza umejuaje kuandika mwandiko wake,..au unajfanya hukumbuki hilo…’akasema wakili mwanadada.

‘Hivi nani atakuamini hilo, mimi nimelazwa hapa, ni nani aliipeleka hiyo barua huko nyumbani kwa wakili mkuu….?’ Akauliza kwa mshangao.

‘Ni docta, …aliyeipeleka ni docta, bosi wako, yeye kwa kutokuwa makini, alishindwa kuvaa kinga za mikononi, alama zake zimeonekana juu ya bahasha…na vipande vile alivyochana zipo alama zake…’akasema wakili mwanadada.

‘Wewe ulistahili kuwa mwandishi mzuri wa riwaya, hivi unajua nini unachokisema…hapo unatunga kitabu cha riwaya ya uwongo…nani ataamini huo uwongo wako….’akasema nesi huku akikunja uso kama anawaza jambo.  Wakili mwanadada akaendelea kuongea na kusema;

‘Na yote kuhusu kuwa umeambukizwa ukimwi  na, wakili mkuu, ni ujanja wa kiini macho ili jamii ikuonee huruma. Huna ukimwi, wala wakili mkuu hana ukimwi, yote hayo yameshagundulikana….kwani wakili mkuu keshapimwa na kugundulika kuwa hana huo ukimwi, na tulipogundua hilo, tulikwenda kuangalia kumbukumbu za afya ya Kimwana, tukagundua karatasi mliloligushi wewe na dakitari wako, kuwa Kimwana ana ukimwi, lakini sio kweli,hakuwa nao…..’akasema wakili mwanadada.

‘Eti nini…?’akasema kwa kushangaa.

‘Cheti ulichosema ulikikuta kwa Kimwana, ulikigushi wewe, ….kwa kumtumia huyo huyo docta wako, ambaye imegundulikana kuwa mlikuwa kundi moja…yote hayo yameshagundulikana….’akasema wakili mwanadada.

‘Eeeh, tatizolako hunijui, hayo yanaweza yakakugeukia, na ninaweza kufungu amshitaka juu yako kwa kunipakazia uwongo, …hunijui mimi wewe, lakini ya nini, mimi sijali amini uaminivyo, ilimradi najua sio kweli kwanini nijali…’akasema huku akikunja uso kwa hasira.

‘Siku ile ulipofika na silaha kule hospitalini, ulitoka naye kwenye gari , ukiwa umejificha nyuma na silaha yako, walinzi hawakuwa na sababu ya kulikagua hilo gari lake….na ndio maana hawakukuona ukitoka,….ulisahau kuondoka na kofia lako la manyoyanyoya, na hili lilikua kuonekana na nesi msaidizi wako,nikuuliza hilo kofia lilifikaje huko kwenye nguo zako?.’akasema wakili mwanadada.

‘Hivi wewe unajifanya kuwa hunielewi, au ni mbinu zako za kunipakazia..hata hivyo mimi nimeshasema sijali, nipo tayari kuhukumiwa kwa hayo, lakini nafanya hayo kwa ajili ya kumlinda huyo binti…hilo kofia silijui mimi…na kofia kama hizo zipo nyingi,hukumbuki nilikuambai kuwa mimi nilikuwa na makofia mengi kwa ajili ya kujificha nikifanya mambo yangu…’akasema.

‘Kama hayo ya kufanya uhalifu na kuwasingizia watu wasio na hatia….’akasema wakili mwanadada.

‘Huyo binti kama anglikuwepo angelisema yote angelikiri mbele yako kuwa yeye ndiye aliyeua, na mimi nimjitolea kumlinda,….kwa hali yoyote…’akasema huyo nesi.

‘Kumlinda au kumtumia kama kinga yako….wewe ulimuhadaa, ili aondoke hapa jijini,ili uwongo wako ufanye kazi, ….lakini hujui kuwa njia ya muongo ni fupi…na za mwizi ni arubaini, ujanja wako wote umefikia ukingoni…..’akasema wakili mwanadada.

‘Kama unakana maelezo yangu kwanini huendi kumuuliza yule kijana muendesha pikipiki….kuwa kweli alimuazima huyo binti pikipiki, sasa jiulize huyo binti alikwenda wapi, na alikwenda kufaya nini….’akasema.

‘Ni kweli kuwa huyo binti alikwenda kuazima pikipiki kwa huyo kijana, na huyo binti alifanya hivyo, baada yaw ewe kumpigia simu ukiigiza kuwa wewe ni mke wa wakili mkuu, unamuita huyo binti aje huko Mbezi,….’akasema wakili mwanadada, na nesi akainama kidogo kufichs hisia zake, halafu akamwangalia wakili mwanadada akiwa na uso wake ule wa ujasiri, huku akitabasamu kwa dharau.

‘Unatunga hadithi, sio, endelea kutunga hadithi yako….’akasema.

‘Huyo binti akijua kuwa kapigiwa simu na mama yake, alikwenda kwa huyo mchumba wake akaazima pikipiki, na kweli alifika huko….wewe ukavua ile kofia uliyokuwa nayo mwanzoni, ukavaa kofia hiyo ya manyoyanyoya, ambayo ulisema alikuwa kaivaa huyo binti,ukafanya hayo uliyayasema kuwa aliyafanya huyo binti, ulipomaliza….kwa haraka ukashuka chini kwenye lile jengo, ukampiga simu kwa huyo binti kuwa arudi tu nyumbani….’akasema wakili mwanadada.

`Huo ni uwongo nambari moja, wewe unalako jambo…haya tuyahakikishe hayo mahakamani kama unataka kushindana na mimi,lakini sina muda huo…mimi nimeshasema nipo tayari kwa lolote lile…kwa ajili ya huyo binti…kumlinda…’akasema na kutulia huku akiangalia chini.

‘Tatizo lako, unafikiri sote tumefumba macho na msikio, kuwa akili zetu haizifanyi kazi,…hii kazi sikuianza leo, na ninajua nini ninachokifanya, yote ninayokuambia yana ushahidi…na mwisho wako umefikia ukingoni, nilikupa muda wa kujikosha, ukajifanya wewe mjanja, sasa nimeona nikufunulie ukweli anagaliu kidogo tu, ili ujue kuwa najua kila kitu…..na mengi yatafuta…’akasema wakili mwanadada.

‘Hiyo ndiyo kauli naitaka kuisikia,mimii sitaki mtu  wa kunionea huruma mimi, ili iweje,…mimi nilishajiandaa kwa hili, najua mwisho wa yote haya ni nini,nilijua kabisa kuwa nitakuja kukamatwa, na huenda nikanyongwa, 
lakini lengo na mdhumuni yangu ..ni hayo niliyokuelezea, kumlinda huyo binti,..najua wengi watazungumza mengi, …., lakini ni kwa vile  hawanijui dhamira yangu ya kweli,..mimi sio mnyama kama unavyodhania wewe…mimi nina huruma zaidi yako wewe…’akasema kwa macho yaliyojaa ukali.

‘Huruma gani hiyo ya kuua watu,kuwachonganisha watu ndani ya ndoa zao,, kuwa-blackamail…Hiyo ndiyo unayoiita huruma, na ikizingatia kuwa wewe uliwahi kuwa mtu wa usalama, unatumia ujuzi ulioupata kutokana na jasho la wanyonge, kodi yao ilikusomesha, na sasa unakuja kuwatende sivyo ndivyo..’akasema wakili mwanadada.

Yule nesi akacheka kwa dharau…na kuangalia chini, na baadaye akasema;

‘Hivi huruma yangu na ya kwako unaweza ukailinganisha,…’akasema wakili mwanadada.

‘Kama wewe una huruma kweli, fanya hilo nililokuambia, hakikisha kuwa unaiharibu hiyo barua, na hakikisha kuwa haijulikani kabisa kuwa huyo ….’kabla hajamaliza mlango ukagongwa, na mara akaingia dakitari, akiwa na mkuu….

‘Natumai mumeongea vya kutosha….’akasema docta.

‘Na yote tuliyoyataka tumeyapata, ….’akasema mkuu.

‘Yote yapi…’akauliza wakili mwanadada akionyesha mshangao, na nesi akamwangalia wakili mwanadada kwa jicho la hasira, akizania huenda yeye ndiye aliyepanga hayo yote, akasema neno moja.

‘Ina maana….’kabla hajasema zaidi mkuu akasema;

‘Mimi sio mjinga, sisi tulichofanya ni kuwasiliana na wenzetu, ambao wanamjua vyema huyu binti, tuliambiwa yote, na kwanini walimsimamisha kazi huko,kwenye idara ya usalama. Haya mambo hakuyaanzia hapa,huko ndio ilikuwa kazi yake kubwa. Alipoona kuwa hana nafasi tena ya kufanya machafu yake huko, ikiwemo kublackmail, …..akaona akimbilie huku kwa visingizio vya kusalitiwa kwenye penzi.

‘Wakili mkuu hakujua kuwa alikuwa kitumiwa kama ngao,..ndio huenda kulikuwa na kupnedana ndani yake, lakini mwenzetu alikuwa akitumia huo mwanya kwa kutimiza malengo yake. Yote hayo tuliyajua, na tulikuwa tukisubiri wakati muafaka. Na wakati muafaka umefikia, …..’akasema mkuu.

Wakili mwanadada akasogea nyuma na kumuachia mkuu apite mbele yake, karibu na kitanda alicholala nesi,na nesi alikuwa akijaribu kuficha uwoga wake, akaangalia kwa yale macho yake ya dharau…

‘Mimi na idara ynagu tulishajua kuna kitu kinaendelea, tulishajua kuwa wewe wakili mwanadada unajua mengi, lakini hukutaka kuyaweka wazi mapema kwa mtindo wako wa huruma,…tulikupa muda , ili tuone, jinsi gani utakvyowahurumia hawa watu, lakini tumeona hiyo njia yako haiwezi kusaidia, tukaona bila kukuwahi unaweza hata ukaficha ukweli mwingie kwa kuwaonea hawa watu huruma, …’akasema na kusogelea pale kitandani, akafunua godoro nakutoa kifaa kidogo, halafu aksema;

‘Hapa kitandani tumeweka chombo cha kunasia sauti,na ukiangalai pale juu kuna kifaa kingine kinachukua picha, na matukio humu ndani, hii ni kuhakikisha kuwa kila kitu tulichokihitaji kwa ajili ya kuhitimisha uchunguzi wetu kinapatikana, yote mliyokuwa mkiongea tumeyasikia,na kwa vile tunajua kuwa huyu jasusi wa kimataifa, tulichukua tahadhari zote, asije akapotea. ….’akasema mkuu.

‘Ni nani aliyekuambia kuwa sikutaka kuyaweka haya wazi, ni mambo gani unayosema nayataka kuyaficha mkuu, mbona unaniingilia wakati nilikuwa nataka kupata kila kitu kwa uwazi….?’ Akasema wakili mwanadada, akionyesha kutokufurahishwa kwa tukio hilo la mkuu.

‘Hisia zangu zimenituma hivyo….nilishafuatilia yote, huyo kijana mchumba wa huyo binti nilishaongea naye, nimekwenda hadi huko juu, Mbezi,nimeongea na wote waliokuwepo hapo,….najua kila kitu..lakini nilikuwa nasubiri nijue nini mwisho wa yote haya, najua mbinu zako, na huruma yako, najua nini kitakachofuatia baada ya hapo na tuna mjua huyu nesi, na tumekuwa tukimfuatilia kwa karibu sana, na kwanini alifukuzwa kwenye kazi yake ya usalama….’akasema mkuu.

‘Sijakuelewa mkuu, maana naona sasa unaanza kunigeuka, nilijua unanifahamu taratibu zangu zakuyamaliza haya, ili mwisho wa siku kila mtu ajutie kosa lake, akiri mwenyewe..mimi sivyo kama unavyonizania,kuwa labda nataak kuwaficha hawa wahalifu kinamna ….na kwanini useme kuwa unajua mbinu zangu, na huruma zangu, …?’ akauliza wakili mwanadada akiwa katahayari.

‘Samahani sana ,kwa kuwa nimekuingilia katika taratibu zako za kikazi,…,lakini mimi kama mtu wa usalama ninapohakikisha kuwa mkosaji kapatikana na ushahidi upo wa kutosha, natakiwa nilipeleke hili swala mahakamani,wao watajua nini cha kufanya, hatuwezi tukayapeleka unavyotaka wewe, hatuwezi kuwabembeleza hawa wahalifu tena maana tumegundua mengi mabaya ambayo yangelifuatia, ….haiwezekanitukasubiri zaidi..huyu mtu sivyo kama unavyomzania, ni jasusi kweli….’akasema mkuu.

‘Kwahiyo sasa unataka kusemaje, maana umenivurugia utaratibu wangu….?’ Akauliza wakili mwanadada.

‘Muhalifu wetu ndio huyu hapa, na tunashukuru kuwa shahidi muhimu ambaye alitakiwa kupotea na hata ikibidi auliwe, akifika huko kijijini, sasa tunaye ….….’akasema mkuu na kumbonyeza mwenzake ambaye alikwenda akafungua mlango, ….

Mara akaingia  yule binti wa kufikia wa wakili mwanadada, wakili mwanadada hakuonyesha kushangaa sana, ingawaje moyoni, alijiuliza ni kwa vipi walimuwahi huyu binti, kwani yeye alikuwa na uhakika kuwa keshaondoka kwenda huko kijijini, …kumbe ilikuwa mbinu ya nesi, ili huyo binti akifika huko kijijini, amaliziwe huko huko…..Yule binti akaingia, na kusimama mlangoni, akasita na kuonyesha uso wa uwoga, akatizama kule kitandani…

Nesi ambaye alikuwa kashikwa na butwa, na hasa lipomuona yule binti, akatoa macho kwa woga akasema `Ssshiti…hawa watu wamefanya nini….’ na mara , akabadilika sura kwa hasira, akataka kusimama pale kitandani, lakini akasita, akamwangalia yule binti huku akiwa kakunja uso,…Yule binti akamsogelea pale kitandani, na kusimama karibu na kitanda, akamwangalia kwa uso wa mashaka, akamgeukia wakili mwanadada , halafu akamwangalia tena yule nesi, akasema;

‘Kweli mimi siamini,….ina maana hata wewe dada yangu niliyekuamini, unanifanyia hivyo, ina maana hukuwa unanionea huruma, kumbe ulikuwa na lako jambo, ulikuwa ukinifundisha kutumia bunduki, ili mwisho wa siku, nionakane nimeua kwa bunduki,…yaani jamani kumbe upo hivyo, umeamua kunisingizia mauaji, hata mimi…’akawa anatoa machozi akimwangalia nesi.

‘Sikuwa na nia mbaya na wewe kabisa, ipo siku utanielewa….lakini kwa leo wafuate hawo watu wako unaowaoana wa maana,….mimi nilikuwa na kusaidia tu….’akasema huku akimkwepa kumwagalia yule msichana machoni.

‘Siwezi kukuamini tena, kunisaidia mimi kwa kunisingizia kuua,….unanisingizia mimi kuua..hapana wewe siomtu mwema,…, hata kama nilikuwa namchukia vipi yule dada nisingelikimbilia kumuua, kwanini nimuue binadamu mwenzangu….jamani toka lini mimi nikaweza kuua mtu, ….’akawageukia wakili mwanadada na mkuu, na wao wakawa wanamuangalia tu.

‘Wewe…hukumbuki uliniambia kuwa ukipata silaha utamuua huyo dada, lao hii unanikana ..’akasema nesi.

‘Nilisema tu kwa hasira, lakini sikufanya hivyo, na nisingeliweza kufanya hivyo..mimi kule nilipigiwa simu na mama kuwa niende huko alipo, na mara nikapigiwa simu tena nirudi…sikujua nini kinaendelea, kumbe ..ni wewe uliyafanya yote hayo…siamini….’akasema huku akilia.

‘Usiwasikilize hawo hawana lolote, …’akasema nesi huku akionyesha wazi kuwa keshashindwa, akajaribu kujifunika uso na lile shuka, lakini hakuweza, akawa kama kamwagiwa maji. Yule binti akamwangalia halafu akasema;

‘Hivi hii dunia  nimeikosea nini, ina maana kuzaliwa masikini ndio kosa, …nawashukuru sana, nyie mlionifanyia hivi….sina cha kuwafanya, kwanza nitawafanya nini mimi kiumbe zaifu, na huenda hata nitakaloongea halitasikilizwa, ila mungu wangu ni shahidi, …mimi hata siku moja sijawazia kumuua mtu….kama nilitamka neno kama hilo ilikuwa ni hasira tu, kwa vilenilijua hata mimi nimeambukizwa huo ukimwi kutokana nay eye……’akageuka na kumwangalia wakili mwanadada,ambaye alikuwa akimwangalia kwa uso wa huzuni.

‘Eti dada mpendwa, kuna siku niliwahi kukuambia kuwa nataka kumuua huyo dada marehemu…?’ akauliza huku machozi yakitoka, na wakili mwanadada akawa kimiya .

‘Najua wewe peke yako ndiye utakayeniamini maneno yangu, wewe peke yako ndio ndugu yangu wa kweli, mungu atakuzidishia …..hawa maaskari wananikamata eti ….’akageuka kumwangalia mkuu, na akataka kusemakitu, lakini akawa kama anaogopa, akageuka na kumwangalia nesi ambaye alikuwa katulia kionyesha hasira za wazi wasi usoni.

Mkuu akasema, ‘Usiwe na shaka binti, ukweli umshadhihiri, na kwa taarifa ni kuwa wahalifu wote wa hilo kundu, akiwemo, Sokoti, na wengi ambao walipandikizwa, kila mahali, mahospitalini na maofisni wote wameshakamatwa, na wote wanatakiwa wakasimame mahakamani, na sheria ndiyo itawahukumu, kama kuna msahamaha, hilo litajulikana mbele ya sheria, na sio kwa njia hii….’akasema mkuu akimwangalia wakili mwanadada.

‘Sawa kwani mimi nimekataa, …ilimradi kila kitu kipo wazi, na wahusika wenyewe tuliwapa muda wa kujitetea lakini wamejitia wanajua zaidi , mimi nimenyosha mikono, ila huyu binti wa watu anahitaji ushauri nasaha, ili asijisikie vibaya, …ni vyema hili likafanyoka mapema, kwani alishahamanika na kuzania kuwa kweli kaambukizwa,…’akasema wakili mwanadada.

‘Ndio, niliskia kwa masikio yangu, sizani kama mama anaweza kudanganya….na, hata huyu dada alinishauri niende kijijini …kuna hisia zilinijia kuwa huko nitapona,…na yeye kanishauri kuwa kweli nitaponyeshwa kwa dawa za asili…eti kweli jamani ina maana mimi ndio basi tena usichana wangu umekwisha sitaolewa, tena, maana mchumba wangu akisikia kuwa…..’akatulia na wakili mwanadada akamshika mkono na kumwambia.

‘Usiwe na shaka mpendwa, wewe hujaumbukizwa ugonjwa, na ili uwe na uhakika twende ukapime, leo hii lazima ukapime, ili uondokane na hizo zana potofu, huyu dada yako alidanganya watu, hata huyo Kimwana mwenyewe hakuwa na huo ugonjwa,..usijali yote utayasikia mahakamani…’akasema wakili mwanadada, na huyo binti akabakia kushangaa.

‘Ina maana kweli..sina ukimwi, ina maana kweli hata baba hana ukimwi,…ooh, …asante mungu,…’akanyosha mikono juu na kushukuru.

‘Sasa natumai umeshamuelewa dada yako alivyo, yeye alitumia udhaifu wa watu ili kufanikisha malengo yake, lakini sasa uwongo wake umegundulika,….kwahiyo wakili  mwanadada kuanzia sasa, ngoja sheria ichukua mkonod wake,….’akasema mkuu.

‘Kama hivyo ndivyo utakavyo, mimi sina zaidi, njia yangu ilikuwa na nia njema, ili kuwafanya watu wajijue, na wakiri makosa yao,…’akasema wakili mwanadada.

‘Hiyi njia yako hapana, haifai kwa watu kama hawa walikubuhu, hawa ni wahalifu sugu, watatumia kila upenyo kufuta madhambi yao, bora kuwawahi ili wakatumikie vifungo vyao, kabla hawajaiharibu jamii yetu, je ulijua huyu mtu, nesi, na pia alikuwa mtu wa usalama, wewe ungelijua kuwa mtu kama huyu angelidiriki kumpandikizia binti  mnyonge kama huyu madhambi ya uuaji, na kuwapandikizia watu wangine magonjwa yasiyokuwepo, na wangi wao kuathirika kisaikolojia na hata kupoteza maisha kwa mshituko…..inasikitisha, sana….’akasema mkuu.

Nesi akawaangalia kwa makini, halafu akamwangalia yule binti akainuka pale kitandani, na nywele zale zilikuwa zimetawanyika kichwani, akashika  kichwa kuanza kuongea kwa  uchungu, akasema;

‘Samahani sana binti, wewe hukujua lengo langu, nisingekutosa, ni katika mbinu za ushindani tu, na ujue kabisa…hayo yote hutokea unapokuwa kwenye uwanja wa vita, inabidi utumie kila njia ili ufanikiwe malengo yako, najua hakuna atakaye nielewa kwa sasa, …ninachoweza kukuomba kwa sasa ni msahama na hasa kwa ambao hawatanielewa, na wataona nimewakosea,….'akasema kwa uchungu, na kabla mtu mwingine hajasema lolote akaongezea kwa kusema.

'Ila yote haya niliyawafanya kwa ni njema ya kupambana na watu wasiotosheka, na nisingeliweza kufanya bure, kwani natangaza, dini, ...haiwezekani hawa watu wachume, sisi tuumie, wanaju ni matatizo gani niliyopata waliponifukuza kazi,....hiyo hela waliyoichuma kwa dhuluma, na sisi tumeichukua kwa mtindo huo, .na hata hivyo ni kweli nilimpenda wakili mkuu, na yeye ilibidi atumike, Ili kumkomoa, kwa tamaa yake ya kiwmili..na kwa kunisaliti,...najua hamtanielewa hata nikiwaambia nini, lakini ukweli ndio huo…’akasema na pale pale akashika kichwa na kuanza kulia….na kwa mara ya kwanza huyu mwanadada lionekana akiwa analia kwa hisia. Ile dharau na ujasiri ukatoweka….!

Mkuu akamwangalia kwa macho ya ukali, halafu akageuka na kumwangalia wakili mwanadada,akasema;

‘Hata hivyo,nashukuru sana kwa kazi yako nzuri, bila wewe tusingeliweza kugundua mengi,…..na sasa upo huru kuwatetea watu wako mahakamani…natumai watakuwa wanakuhitaji sana..ila huyu mtu wetu hastahili kubakia hapa inabidi tuondoke naye akalazwe hospitali zetu zenye ulinzi wa kutosha,….’akasema mkuu, na mara wakaingia ma-askari wengine, ambao walimwamrisha nesi atoke pale kitandani, na wakamshia mikono huku na huku na kutoka naye nje.

Wakili mwanadada akamshika yule binti mkono na kumwambia;

‘Tunakwenda kwangu , wewe utaishi na mimi ,toka sasa wewe ni mdogo wangu.

‘Ahsante wewe kweli ni ndugu wa kweli…sitakusahau katika maisha yangu.

NB: Hapa sio mwisho, kuna sehemu ya mwisho ambayo itatoa ufafanuzi hasa kwanini KImwana aliuwawa, tuungane na wakili mwanadada kwenye sehemu hiyo muhimu, tukijaliwa tena. Na pia tutajua nini hatima ya Msoma na Tausi, na ndoa ya wakili mwanadada. Na kama kuna sehemu yoyote nimejichanganya naomba wale mliofuatilia hiki kisa mnifahamishe ,maana ni kisa kirefu naweza nikachangaya.

WAZO LA LEO: Ndugu wakigombana chukua jembe ukalime, maana ogomvi wa familia sio wa kukingia kifua, na kulalia upande mmoja, unachotakiwa ni kuwapatanisha, kwani ukijifanya kulalia upande mmoja,wakija kupatana utaonekana wewe ndiye chanzo.


Ni mimi: emu-three

12 comments :

Anonymous said...

I see! naona kama naangalia bonge la movie. hongera sana, kwakweli sikutegemea ingekuwa hivi. unaonaje ukiuza hizi stori zitengenezewe movie? na wazo la kutoa vitabu limeishia wapi ndugu?

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

bomba sana mwanawane...nakumbuka ndani ya kisa hiki Msomali alipigiwa simu kwenda Sinza kwenye nyumba moja hivi lakini akakuta mdada kajeruhiwa na kupelekwa hospitali.

sijaona (labda macho yangu yana kengeza) mahali ktk simulizi ameelezewa yeye ni nani, anahusikaje, na alomtungua! Na kama alikufa ama la!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

M3,

Nakumbuka wakati fulani ndani ya kisa hiki Msomali alipigiwa simu kwenda kwenye nyumba moja huko Sinza akakutana na kisa cha mdada mmoja kupigwa risasi na kukimbizwa hospitali.

Sijaona (labda nina kengeza) mahali kuhusu huyo mdada ni nani, anahusikaje na sakata hilo, kama alipona, na nani muhusika wa kumtungua na kwa nini!

emuthree said...

Ni kweli,labda nije kuelezea baadaye ilikuwaje , lakini zote hizo
zilikuwa mbinu za kiujanja za kundi, ...walikuwepo watu walioweza
kuigiza mtu, matendo, na kuonekana kama muhusika fulani...tutaielezea
hiyo kwenye sehemu ijayo!

emu-three said...

Ama kuhusu kitabu/vitabu na movie hilo ni moja ya malengo yangu. Lakini mambo bado magumu, maana mtegemea cha ndugu,au cha mtu ni mavi.
Jembe linalonisaidia ni la ofisi, muda hautoshi, ukiwa ofisini, na cafe nako ni gharama,...lakini bado tuna nia hiyo!

Anonymous said...

Mimi sijajua kwanini hutumii majina,na kutumia mdada, mke wa,huoni hiyo inachanganya zaidi?

emuthree said...

MSINIONE NIPO KIMIYA, JEMBE LINAKOROFISHA, NA KAMA WEHENGA WALIVYOSEMA CHA MTU NI NINI? NA NGUO YA KUAZIMA HASITIRI NINI...
Tuombe mungu, atujalie, maana haya yapo juu ya uwezo wangu, hata hivyo Tupo pamoja!

Yasinta Ngonyani said...

Kazi nzuri ndugu wangu..nawe usiona nipo kimya nipo nawe...

Precious said...

Nilipotea kwa muda majukumu M3 yamenizidi ila nashukuru nimepata muda kdg ya kuendelea na riwaya yetu mpka mwisho..Tuko pamoja M3, Mungu azidi kubariki kazi ya mikono yako.

emuthree said...

Mkuu Wambura, ndugu wangu Yasinta na mpendwa Precious na wengineo ambao hawakutaja majina yao na wale wa kimiya kimiya, nawashukuruni sana kuwa nami.

Kwa ujumla nyote Mumenipa faraja, maana ukiandika huwezi jua nini wenzako wanafikiria mpaka akitoa maoni.

Pole na majukumu Precious, karibu sana tuungane pamoja, na halikadhalika Yasinta ulisema ulikwenda `kalikizo kidogo' karibu tena!

Kay said...

hongera m3 kwa hadithi zako tamu, name nilitaka kuulizia ile part ambayo msomali alienda akakuta mwanadada amelala chini kwenye dimbwi la damu, ila naona ushaitolea ufafanuzi hapo juu.. Big up brother..

Anonymous said...

однокласник mail ru группа
одноклассники ry
сообщение на одноклассниках
одноклассники online игры ipad2
удалить одноклассниках