Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, August 1, 2012

Hujafa hujaumbika-78 hitimisho-36Nesi akaendelea kusimulia...

Nilitoka pale ofisini na pikipiki, sikujali nimechukua pikipiki gani, na usafiri rahisi hapa Dar ni pikipiki, unaweza kufika eneo unalokwenda kwa muda mfupi, licha ya kuwa ni usafiri wa hatari, lakini mimi nilishazoea huo usafiri na ninajua vipi niende na wakati gani, …

Nilifika maeneo ya Mbezi, na kitu nilichofanya kwanza ni kuangalia maeeno yote ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayenitilia mashaka, na nilipohakikisha hilo, nikaona nizinguke kidogo nione wapi alipoweka wakili mkuu usafiri wake..

Mimi huwezi kunificha kitu, …ni mwepesi sana wa kunusa jambo, sikuchukua muda nikagundua wapi wakili mkuu alipoficha usafiri wake, na sio mbali sana na pale liliposimama gari la mke wa wakili mkuu, nikatabasamu, maana hawa wanawake hawakutaka hata kulificha gari lao. Nilipohakikisha hilo, nikaondoka pale ili kutafuta wapi nitakapoficha usafiri wangu, mara nikaona pikipiki….

‘Hii pikipiki kama ninaifahamu mwenyewe,amekuja kufanya nini huku….?’ Nikajiuliza. Sikutilia maanani sana lakini nafsini mwangu,nikawa na mashaka ….nilikuwa nahisi kitu, na huwa nikihisi kitu kuna jambo, nilikuwa na mashaka sana na ile pikipiki, nikaangaza huku na kule, kumtafuta dereva wa ile pikipiki lakini sikumuona.

‘Hii pikipiki ni ya yule kijana….mchumba wa binti anayeishi kwa wakili mkuu…amekuja kufanya nini huku na alishaniambia kuwa yeye usafiri wake ni mjini tu au maeneo ya karibu na pale kwao, huwa hapendi kwenda maeneo ya mbali…nikajiuliza bila kupata jibu…

Sikumuona huyo dereva, nikaona nipige simu kwa mtu wangu anifuatilie kuhusu huyo dereva,….unapokuwa na tabia kama yangu mara nyingi unakuwa na hisia ya ziada. Akili yangu ilikuwa ikinihimiza kuwa hiyo pikipiki haikufika hapo kwa bure kuna jambo.

Nikaona nisipoteze muda, na kwa vile muda ulishakwenda, nikaona ili nifike kule kwenye majengo mapema, ni bora nikimbie, nikakimbia kuelekea kule kwenye yale majengo kwa mwendo wa kiaskari….eneo hilo limejengwa majengo yaliyoshiba, na ilikuwa ndoto yangu nami niishi maeneo hayo, lakini mbaya wangu akaniwahi, na leo najua itakwua ndio mwisho wake, labda….lakini hiyo labda mimi nitaisawazisha….mara simu ikaita,….nikaipokea,

‘Huyo mwenye pikipiki anasema kaiazima pikipiki yake kwa mtu wake, anayemwamini…’akaniambia, sikujali kumuuliza ni mtu gani, nikaachana na mawazo yahiyo pikipiki, na kuingia kwenye hilo jengo ambalo ninajua ndipo walipo hawa akina mama,na nilihakiihsa kuwa hakuna watu wanaoniona licha ya kuona gari likiwa limesimama,mbali na hilo jengo.

Nilipanda kwenye lile jengo hadi juu kabisa, ambapo niliweza kuona maeneo yote na nikachunguza kule kwa Kimwana, nilichunguza kwa muda, nikagundua kuwa Kimwana hayupo peke yake, kuna watu wengine, na hili lilinipa mashaka sana, …

Nikashuka taratibu hadi kwenye ile gorofa ambayo najua ndipo walipo hawa akina mama, nikawaona wakiwa wanaongea, walionekana kuwa na mzozano fulani na baadaye nikaona wakinya’nganyana ile silaha, nikaona ajabu. Mimi nilijua labda mmoja hataki hilo zoezi lifanyike, nikasubiri, …baadaye kidogoo nikaona niwasiliane na watu wangu.

‘Sokoti, nipo kazini, ile kazi niliyokuagiza umefikia wapi?’ nikamuuliza.

‘Nimeshampa taarifa mtu wangu, na kasema ataifanya bila mashaka, kwani hata yeye ana hasira na huyo mwanadada, na alikuwa tu akisubiri amri yangu…’akaniambia,

‘Sasa sikiliza haya mambo tunataka tuyapange kimahesabu, subiri kidogo, nipe namba ya huyo mtu wako, kuna jambo nataka kulifanya, ila mwambie kuwa amri ya hilo tendo atalipata toka kwangu, nikimbipu tu, afyatue risasi, bila kusita, kama kweli yupo sehemu anapoweza kumuona huyo mtu wetu…’nikamwambia.

‘Kanimbia sasa hivi yupo tayari, keshamuweka kwenye shabaha yake, ni swala tu la kupata kibali kuwa afyatue risasi…’akasema .

Mimi sikutaka sana wakili mwanadada auliwe, mtu wangu ni huyu Kimwana, lakini niliona ni vyema,haya mauaji yakatengenezwa kiasi kwamba, ije ilete utata wa aina yake, hilo wazo likanijia akilini kwahiyo nikawa nawasubiri wale akina mama watulie wafanya kazi yao, ,…

Mimi huwa najulia sana utumiaji wa silaha, na akiwa kashika mtu silaha, naweza nikajua kuwa sasa risasi inatoka au bado, kwa kuangali kile kidole chake anapovuta kile chuma cha  kuachia risasi-trigger, na ndivyo nilivyotaka niwaangalia wale akina mama,lakini  niliwaona kama wanacheza mchezzo wa kuigiza, maana kila mmoja anataka kuishika ile silaha…..

Mara nikasikia sauti za mtu, akipandisha ngazi kwa kukimbia, pale nilipo naona  zile ngazi za toka chini, alikuwa ni kijana tu anatafuta tafuta mabaki ya mbao, sikumjali sana,lakini kumbe wale akina mama wamemsikia, wakaangaliana na mara wakaanza kukimbia kueleekea kwenye vyumba, na wakati huo silaha alikuwa nayo mke wa wakili mkuu.

Wakati wanakimbia kujificha, mke wa wakili mkuu, akapita kwenye sehemu iliyopangwa cements na mabaki ya mifuko iliyokwisha kutumika, akabwaga ile silaha pale na kuweka mifuko iliyotumika juu yake, na kukimbilia huko alikoelekea mwenzake,…

‘Hawa wajinga kweli, hivi wanafahamu vita, ..hawa wamekuja kucheza, …’nikasema na nikaona ngoja nikaimalize hiyo kazi mwenyewe. Nikaanza kushuka kuelekea kule ilipofichwa hiyo silaha, na hata kabla sijashuka hatua mbili, mara nikaona mtu akitokea upande wa pili, wa ile sehemu. Ilee sehemu imejengwa kama ukumbi, na kuna vyumba ambavyo vipo wazi, kwahiyo mtu anaweza akaingia kwenye chumba kimojawapo, na kujibanza asionekane.

Huyu mtu, ni mwanamke, kaavaliakofia kubwa lenye manyoya, kofia hiyo imefunika kichwa chote, kama vile helement wanayovaa waendesha pikipiki….na ikafungwa kwa mbele , na kuachia sehemu ya pua na macho…na kwa vile nilikuwa namwangalia kwa juu nisingeliweza kumgundua kuwa ni nani….nikatulia kumwangalia nini na anataka kufanya nini.

Huyo mwanamke, alionekana sio mkubwa, sana,labda awe na umbile dogo, lakini hata ingelikuwaje ungeligundua tu kuwa ni msichana, …akawa anatembea kuelekea kule ilipowekwa ile silaha, alikuwa akitembea harakaharaka utafikiri miguuu yake ni myepesi sana. Akafika pale bunduki ilipowekwa na ilionekana kuwa aliona wapi hiyo silaha iliwekwa, maana alifunua tu ile mifuko na kuichukua ile silaha,…akaiinua juu kama vile kuashiria ushindi, halafu akaiweka sawa mikononi.

Pale moyo ulianza kunidunda, maana nilijua labda huyo mtu anataka kuwadhuru wale akina mama,labda ni mmoja wa walinzi wa Kimwana, walishagundua hilo na sasa , katumwa kuja kuwamaliza,nikajiweka sawa kama ikibid niende kusaidia, lakini nilishangaa, maana yule mwanamke alikwenda pale walipokuwa wamesimama wale akina mama na kuielekeza hiyo silaha kule walikokuwa wameielekeza wale akina mamahiyo silaja, kule alipokuwa Kimwana…

Mimi nikaona ni vyema nipande kule juu , ambapo nitaweza kumuona vyema huyo mwanamke na pia, niweze kuona huko anakoelekeza hiyo bunduki, na ilikuwa kule kule kwa Kimwana, nikaona sasa mambo yameenda vyema, nikajua kuwa huenda ni watu wa Sokoti,..

Nikajisogeza sehemu ambayo, naweza kumuona vyema…nikaangalia kidole chake na alivyosihikilia ile silaha nikajua kabisa huyu anajue vyema kuitumia, nikaiweka simu ya huyo mtu wa Sokoti hewani nikamuweka sawa, nikaangalia kidole, nikasema

‘Fyatua…..’na mara kule jengo ambapo yupo kimwana, nikasikia yowe, nikajua mambo tayari, sasa sijui vyema yamekuwa tayari kwa vipi, maana mawazo yangu yalikuwa kwa huyu mwanamke, ….nilimuona akiwa kama kachanganyikiwa,….ni kama vile hakujua kuwa ataua, au lile tendo limemshitua kuwa kumbe sasa nimeua, nitakamatwa…akakurupuka na kuanza kukimbia…

Alichofanya ni kuitupa ile silaha, kule alipoichukulia, lakini kwa vile ni nzito kidogo , haikufika kule kwenye mifuko, ikawa sehemu ya wazi, …na kwa vile alikuwa na pupa ya kukimbia, akajikwaa kwenye vipande vya matofali, akaanguka, na ile kofia ikamtoka,…..

Na wakati huo huo mimi nilishashuka na nilikuwa karibu sana na yeye, aliangalia huku na kule, na alipogeuza uso wake, akaniona, …alishituka na kuinua mikono yake kushikilia shavuni, kama vile anataka kupiga yowe,….lakini hakufanya hivyo, alichofanya ni kugeuka na kuanza kukimbia. Kwa vile nilikuwa nimevaa nguo zangu ambazo mtu hawezi kunitambua, nilijua kabisa hakujua kuwa mimi ni nani….’akasema nesi.

‘Lakini wewe ulishamgundua kuwa ni nani….?’ Akauliza wakili mwanadada.

‘Usinichekeshe, nimeshakuambia kuwa mimi ni jasusi, nikiwa na maana ni kuwa nipo kama mpelelezi wa kimataifa, wao walinibania tu,kunipa hiyo kazi,..kama wangelinipa hiyo kazi wangeliona matunda yake. Jicho 


langu moja tu, lilishagundua kuwa ni nani,….na hapo nikaunganisha umbile, ….licha ya kuwa alijibadili katika kutembea, lakini kuna namna mtu hata akijibadili vipi na kutemeba harakaharaka, utamgundua tu kwa jinsi ya miguu yake ilivyozoea kutembea….

‘Kwahiyo uligundua kuwa ni nani ,nataka uniweke wazi hapo…’nikamuuliza nesi.

‘Ina maana unajifanya hujamuelewa, au ndio uwakili huo wa kuuliza majibu, na sizani kama ingelikuwa ni mahakamani ungeliniuliza hilo swali, kwani unakuwa unahitimisha, ngoja tuendelee kwanza…’akasema nesi.

‘Wewe sema tu ,hapa sio mahakamani, uligundua kuwa ni nani…?’ akauliza wakili mwanadada akiwa kmuangalia nesi kwa makini.

‘Ni binti wa kufikia wa wakili mkuu…’akasema nesi na wakili mwanadada, akatulia kwa muda kama anawaza jambo, halafu akasema,

‘Eti nani….ooh, ok, haya endelea….’

NB..Naishia hapa bila kupenda,....kwani muda hautoshi, wenye jembe wameshafika, na sehemu iliyobakia ni sehemu nyeti kidogo, nahitajika kutulia, ili tuweze kuhitimisha vyema, na hutaamini, ukachakisia, kwani kisa chetu kinasema `hujafa hujaumbika,' kila siku mambo yanabadilika, unakutana na mengi y akushangaza na kuajabisha, huwezi amini,.. …

.Je una nini lakusema kuhusu hapo tulipofikia,.... tuwe pamoja, tusicheke, kuwa nami,....

WAZO LA LEO: Mwenye kutoa msaada kidhati, ni yule anayetoa bila kujitangaza, na kama tulivyoambiwa, inatakiwa ukitoa kitu kumsaidia mtu, ni vyema ukatoa, kiasi kwamba kamaulitoa kwamkono wa kulia, basi mkono wa kushito usijue  kuwa umetoa nini. Kusaidia kwa kujitangaza ni biashara, jiulize je wewe unasaidia mtu ili kujitangaza, au unasaidia mtu kibinadamu ,, hata hivyo kutoa ni moyo, na sio utajiri.

Ni mimi: emu-three

No comments :