Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Saturday, July 14, 2012

MWAKA MWINGINE UMETIMIA


                         SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA DIARY YANGU


Kila mtu huwa na ndoto zake katika maisha, na kama ndoto hizo zingekuwa kweli, sijui dunia hii ingelikuwa wapi.Lakini Mungu aliyetuumba anajua nini kifanyike kwa wakati gani,kwani yeye hana udhaifi wowote wa kibinadamu, atakalo kuwa huwa

 Nilipoanzisha blog hii nilikuwa na ndoto nyingi sana, nikijua kuwa huenda huo ukawa mwanzo wa ile ndoto yangu ya kuandika mambo mengi yanayotokea kila siku, ikiwemo visa ,mikasa, riwaya na mambo ya kielimu, …lakini mengi yamekuwa kama ile ndoto ya Alinacha na siku zikaenda na leo ni siku ile ambayo blog hii iliweza kuonekana hewani kwa mara ya kwanza.

Rejea niliyoandika siku hiyo hewani kwa mara ya kwanza hapa: 

Masiku yanakwenda na siku hizi tunaona kama kasi ya masaa imeongezeka, maana tunaona kama juzi tu, ambapo tulikuwa tukiitwa watoto, ikabadilika na kuitwa vijana taifa la kesho, ambalo siku hizi ni taifa la leo, na baadaye ooh, …nimekuwa mtu mzima, nakimbiliwa nakupokewa mizigo,huku tukiitwa `baba’ au ‘mama’ …ni kama juzi tu, na mara nyingi unaweza usione tofauti, zaidi ya mabadiliko ya sura …hili halikwepeki. Ukubwa, uzee, hauna dawa!

Leo ni siku nyingine ya furaha ya blog hii, wengine huimba na kusema `happy birthday to you’ na sisi waswahili tunasema `hongera ya kumbukumbu ya kuzaliwa’.

Sina mengi ya kuongea kwa leo ,zaidi ya kuwashukuru wote ambao wanapita katika blog hii, na hasa walewanaotoa maoni , kwani kwa kutoa maoni inakuwa kama sehemu ya kuwasiliana, na kujuana vyema.

Mungu awajalie na awape Baraka tele,…


Ni mimi: emu-three

11 comments :

Anonymous said...

Hongera diary yangu, mungu akuzidishiwe wewe mmiliki uzidi kuwa na nguvu afya na uwezo wa kutuletea visa vizuri zaidi na zaidi

Mama R

Rachel Siwa said...

Hongera sana kwa kuongezeka mwaka mwingine, Uwe wenye baraka, kutimiza malengo,Kuendelea zaidi zaidi zaidi.

Pamoja tunaweza.

wako nduguyo

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hongera sana mkuu!

EDNA said...

Hongera sana jirani,nakutakia kila lililo la kheri katika ulimwengu huu wa kublog.

KEEP UP THE GOOD WORK.

Yasinta Ngonyani said...

HONGERA SANA TENA SANA NA NAKUTAKIA NGUVU NA MALENGO YAKO YATIMIA. TUPO PAMOJA...

Subi Nukta said...

miram3 PONGEZI za dhati kwa kudumu na katika tasnia ya ku-blog. Uendelee kufanikiwa zaidi na zaidi!

HONGERA!!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongera mwandishi wewe.Hongera sana. Nazipenda mno hadithi zako zenye mapenzi tele. Usichoke !!!

emuthree said...

Nawashukuru wote Anony,ndugu wa mimi,mkuu Wambura,jirani yangu mpendwa Edna,ndugu wangu Yasinta,mpendwa mwenza Subi,na Mkuu sana MMN, na wale Kimiya kimiya sana, kwa kushiriki nami katika siku hii muhimu ya kumbukumbu ya kuonekana hewani kwablog hii.
Na hii ni heri na baraka kwetu sote, mungu awabariki sana, na tupo pamoja daima

Anonymous said...

whats up miram3.blogspot.com owner discovered your website via search engine but it was hard to find and I see you could have more visitors because there are not so many comments yet. I have discovered site which offer to dramatically increase traffic to your site http://traffic-for-your-website.com they claim they managed to get close to 4000 visitors/day using their services you could also get lot more targeted traffic from search engines as you have now. I used their services and got significantly more visitors to my site. Hope this helps :) They offer best services to increase website traffic at this website http://traffic-for-your-website.com
To your success James

Anonymous said...

… Unbelievable , but I just found software which can do all hard work promoting your miram3.blogspot.com website on complete autopilot - building backlinks and getting your website on top of Google and other search engines 1st pages, so your site finally can get laser targeted qualified traffic, and so you can get lot more visitors for your website.

YEP, that’s right, there’s this little known website which shows you how to get to the top 10 of Google and other search engines guaranteed.

I used it and in just 7 days… got floods of traffic to my site...

…Well check out the incredible results for yourself -
http://autopilot-traffic-software.com

I’m not trying to be rude here, but I believe when you find something that finally works you should share it…

…so that’s what I’m doing today, sharing it with you:

http://autopilot-traffic-software.com

Take care - your friend George

Anonymous said...

I hаvе been suгfing onlinе more than 3
hоurs thesе dаys, but I by
no meаns fοunԁ any fascinating artіcle lіke yοurs.
It іs pretty value enough fοr me.
Personally, if all sitе оωnеrs and bloggers made
gοod cοntent as yоu ρгоbably ԁiԁ,
the net mіght bе а lot morе hеlpful thаn eveг beforе.
Also visit my web blog ... How to Make extra money from home