Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, July 16, 2012

Hujafa hujaumbika-68 Hitimisho 26



Kila nilipotaka kutuliza kichwa cahangu, sikuweza,maana ile kauli niliyoisikia toka kwa yule dada iliniandama na kunifanya nijione kuwa huenda mimi ndiye mkosaji, ingawajesilijui kosa langu, nikawa nahangaika kuutafuta usingizi, lakini kama niliupata ukawa wa mang’amung’amu. 

Na baadaye nikapata usingizi lakini ndani ya usingizi huo nikajikuta nikiwa situlii, mandoto  ya ajabu, ajabu ya kutisha, na mwishini kabisa, nikaota naelea hewani,kama ndege, huku nikitafuta sehemu ya kutua.

Nikiwa hewani zile nguvu za kukaa hewani zikawa zinapungua, na ghafla nikatua kwenye paa la nyumba. Nilipotua nikajikuta nikiteleza kuelekea chini , maana paa lenyewe ni la bati, na lina umande wa usiku, kama vile kulinyesha mvua.

Kwahiyo nikawa na akzi nyingine, ya kujizuia nisiteleze nakuserereka kwenda huko chini ambapo sipajui papoje,na nikawa nahangaika kutafuta sehemu ya kushika ili niweze kutafuta mwanya wa kushikilia na baadaye nishuke chini taratibu, na wakati nahangaika hivyo, nikaweza kuangalia chini aridhini.

Kule chini kulikuwa na miiba mirefu, kama vile miti iliyochomekwa na juu yake kuna ncha kali kama ya mishale,  ambayo kama ningeliachia pale juu na kuporomoka chini, nikaangukia kwenye hiyo miba,  basi mimi ningelichomwa na ile miba na kuwa kama mshikaki ulichomekwa kwenye miti,  …nilipoona hivyo, nikaingiwa na wasiwasi mkubwa, nikawa najitahidi kushika huku na kule,….na mikano sasa ikawa anachoka kushikilia sehemu ile ndogo niliyoipata.

Nilihangaika kwa muda, na jinsi muda ulivyokuwa ukienda ndivyo name mwili ulivyozidi kukosa nguvu,nikawa nimechoka, na hali ilivyokuwa ilionyesha dhahiri kuwa sitaweza kushikilia tena, kwa vyovyote vile nitaanguka chini, …nikajaribu kutafuta sehemu ambayo hata nikiangukia nisije nikachomwa sana, …..na hapo hapo mikono ikawa imeshachoka, na sikuweza kushikilia tena, nikaachia na kuanza kuserereka….

Nikiwa sasa nipo hewani, naeleeka chini, nikawa namuomba mungu anisaidie ili nikitua chini, nisije nikachomwa na roho ikawa haitoki haraka , na kuanza kuteseka na maumivu,  yaani kama inawezekana nife haraka hata kabla sijapambanana hayo machungu ya kubanikwa kama mshikaki, na mara nikasikia sauti ikisema;

‘Wewe unaomba upate huruma ya mola wako, mbona wewe huna huruma na wenzako?’ sauti ikiniuliza.

‘Huruma kwa watu gani?’ nikauliza huku nikiahangaika kuangalia chini, ….lakini sikuweza maana ilionekana kuwa sehemu ile ndefu hadi kutua chini.

‘Unatakiwa kwanza uwaharumie wenzako, kama unavyojihurumia wewe mwenyewe, je hilo unafanya, hebu chunguza katika maisha yako, ni mangapi mabaya uliyoyafanya yakasababisha wenzako kuumia, hebu jiulize hakuna mtu yoyote uliyewahi kumuumiza katika maisha yako, wewe unaogopa jeraha, je hakuna lolote baya ambalo kwa kulitenda kwako, kwa nafsi yako, likawa ni jeraha kwa wengine,,?’ nikaulizwa

‘Kwakweli sikumbuki,…. je ni nani niyeliyemuumiza hivyo?’ nikauliza.

‘Hebu jiulize mwenyewe , kweli hakuna katika maisha yako, uliyemuumiza sana moyo wake, na kila siku anateseka kwa ajili yako, ….’ile sauti ikasema.

‘Ni nani huyo…mbona mimi simuelewi,…..ni nani huyo?’ nikauliza.

‘Mara ni wepesi sana kujiona hatuna makosa, na wepesi sana kuone wenzetu wana makosa, kama ilivyo wepesi sana kumnyoshea mwenzako kidole. Na pale inapofikia sehemu ya kummwangalia mwenzko kwa jicho la kumsaidia inakuwa ni uzito sana, lakini inapokuja kuwa unataka wewe kusaidiwa kwako inakuwa ni wepesi sana….’ila sautiikasema.

‘Sijaelewa…kwanza ni nani huyo niliyemfanyia hayo mabaya…?’nikajitetea na kuuliza.

‘Ni yule anayeumia ndani ya moyo wake, maumivu ambayo hayadhihiri wazi, lakini maumivu hayo ni makali kwake,kama kuchomwa na miiba mwili mzima,na kubanikwa kama mshikaki,…kutokana na hayo maumivu amekuwa kama mfu,aanyeelea hewani, akitafuta wapi pa kutua, lakini kila anapojaribu anakuta kuna miiba ile ile…

‘Haiwezekani, niwe mnyama kiasi hicho…ni nani niliyemfanyia hivyo….?’ Nikauliza.

‘Hebu jiulize wewe umeonja angalau shida kidogoo tu, ukatamani kufa, ..na sasa hapo ulipo unaomba ufe haraka kabla ya kupata hayo maumivu, umesahau kuwa kuna mtu ambaye amekuwa akiumia miaka mingi,…wapo ambao hawana hili wala lile, hawana macho, hawana masikio, hawana kiwiliwili, na kuna ambao waanteseka mioyoni mwao, mika mingi , hawapati lepe la usingizi, ..na hata kufikia kutaka kujiua ….’ila sauti ikasema.

‘Ni nani hawo ?’ nikauliza.

‘Wapo watu, lakini pia  yupo mtu ambaye amekuwa akiumia moyoni mwake toka udogo wake, hadi sasa, bado anaumia,…akiwa anahangaika  kutunza ahadi yake,… lakini wewe hukuweza kabisa kuitunza ahadi yako,….unakumuka hilo?’ ile sauti ikaniuliza.

‘Sikumbuki….naomba unikumbushe ?’ nikasema.

‘Ni rahisi kwa mtu kusahau wema aliotendewa, hasa pale anapokutana na raha za dunia , ambazo ni za kupita tu, kumbuka kuwa wema katu hauozi, na mtenda mema…aghalabu hana thamani kweney uso wa dunia, lakini….’ila sauti ikawa kama inapotea.

‘Nani huyo alinitendea wema…?’nikauliza.

‘Ni yule anayetunza ahadi yake, anayetunza dhamana, aliyokabidhiwa, na huyo alifanya kwa ajili yako, cha ajabu wewe sasa huna habari na yeye,  wewe unachojali ni hisia zao, je yeye hisia zake atazijali nani….ujue kabisa ili dua za mja zikubaliwe kwa mola wake, inabidi moyo wa muombaji uwe safi, utubu dhambi zako,na ukiri kabisa kuwa hutarudia tena,….je wewe umeshafanya hayo….?’ Akaniuliza.

‘Dhambi gani hizo na nimemfanyia nani…mbona unazidi kunichanganya?’ nikauliza huku nikiangalia chini, na kujikuta ninakaribi akutua…nikasema.

‘Naomba kwanza uniokoe na hili janga,…ninakiri kuwa nitatubu dhambi nzangu, naomba msamaha kwa wale wote niliowakosea, na kama nikipata nafasi nitawapitia mmoja mmoja, niwaombe msamaha….naomba…..’nikawa nalia pale nilipohisi nikigusa ncha moja ya zile miiba, na ule uchungu wake ukanifanya nipige ukulele…..

Na ghafla nikashituka na kuruka kitandani, …nilijikuta mwili mzima umelowana jasho, nikajpapasa ubavuni pale nilipohisi ile ncha ikinichoma, na kwa mbali nilihisi maumivu, na nilipochunguza pale kitandani nikagundua kuwa kulikuwa na sindani ya kushonea nilikuwa nimeishahu hapo kitandani, na ndiyo iliyonichoma.

‘Kumbe ni ndoto tu bwana,…nikajipa matumaini, lakini nfasini nilikuwa nikiwaza mengi, nikijua kabisa hiyo ndoto ina ujumbe maalumu, ambao natakiwa kuufanyia kazi,.

Nikawa najiuliza ni nani huyo aliyekuwa akinipa huo ujumbe, ni mwenyezinungu,….nikawaza sana bilakupata jibu, na hapo hapo nikajiuliza tena, na ni dhambi gani nilizofanya,na nilimfanyia nani, ….hadi inafikia hatu hii, maana kweli nihisi kuwa ni mkosaji, haiwezekani niwe katika maisha ya dhiki kama hayo, na baadaye nikajiandaa maana kulikuwa na kikao nyumbani kwa wakili mwanadada. Alinihitaji niwepo.

Nikiwa najiandaa ndio nikakumbuka tukio la jana, wakati nikiwa nyumbani kwa mwanadada,  ujio wa yule dada rafiki wa mke wa wakili mkuu. Ilikuwa ni tukio nisilolitarajia, ingawaje nilikuwa na hamu ya kumuona huyo mwanadada, lakini alipokuja hapo hakuwa na muda wa kuongea na mimi, alikuja kwa ajili ya kukutana na wakili mwanadada kwa ajili ya kesi yao.

                                                                                        ******

‘Ohh, pole sana nilikuwa nakuja huko kukuona,….’nikasema baada ya kuduwaa kwa muda pale nilipofungua mlango, na kujikuta sina neno la kusema kwa sekunde kadhaa. Yeye alikuwa kasimama pale mlangoni akiniangalia kwa makini, huku akionyesha dhahiri kuwa amechoka, uso wake ulionyesha kuliochoka, na ilionyesha wazi kuwa ana usingizi, …na yela macho..oh.

‘Wakili mwanadada nimemkuta?’ akaniuliza baada ya kuniona nimeduwaa na sisemi kitu kwake.

‘Ndio ume-me-mkuta yuuu-po ndani, karibu..kari---ribu nikuitieee?’ nikasema.

‘Hivi wewe huwa unashida hapa kwake…?’ akaniuliza huku akionyesha kushangaa.

‘Hapana mimi nilikuja mara moja kwa ajili ya kujua nini kinaendelea huko mahakamani’nikasema.

‘Kwanini usifike mwenyewe , unasubiri kuulizia ina maana huna uchungu na hawo wenzako, hujui kuwa mengi yanaweza kuwa wewe ndiye msababishaji ….’akasema na kukumbuka kauli inayofanana na hii aliyowahi kuniambia siku za nyuma.

‘Samahani kama nitakuuliza swali ambalo linaweza kukukazwa, maana nakumbuka uliwahi kusema kauli kama hiyo hiyo, siku za nyuma. Ukanituhumu kuwa mimi na wakili mkuu tunahusika kwa anmna moja au nyingine na sisi ndiye tuliyesababisha haya yote, lakini sijui kuhusika kwangu kukoje, naomba unifahamishe ili nisiwe nawaza jambo nilislolijua…’nikasema.

‘Kama hulijua mpaka sasa, ina maana halikuumizi akilini, na kama hujui lolote mpaka sasa, basi haina maana hata kukuambia lolote,maana haikugusi moyoni,…mimi ninashangaa kabisa,ina maana wewe hunalolote unalolijua kuhusu hii kesi, ..huna lolote unalolijua kuhusu mtu yoyote mle kwenye hiyo kesi, hakuna mtu anayekugusa katika hii kesi,…’akawa kama anapepesuka,….

‘Ooh, ingia ukae naona una kizunguzungu…’nikasema na kutaka kumsogelea lakini akanyiosha mkono kama kunizua nisimsogelee.
Akasema;

‘Ina maana kweli wewe …..hunikumbuki hata mimi,….hapana najua ni kwasababu huna lolote kunihusu mimi….sawa, lakini hata kiubinadamu,….ulitakiwa kufika kuangalia nini kitaamuliwa,?’akasema kwa huzuni, na nikaona kama machozi yanamlenga lenga.

‘Sio kwamba hainiumi kuhusu hii kesi, inaniuma sana,..na nawajali wote,… na ningelifurahi kusaidia kadri ya uwezo wangu, lakini kwa mfano leo, nilikuwa na mzigo naumalizia kama ujuavyo mimi sina kazi, kazi yangu sasa ni pale ninapopata mzigo naufanyia kazi, …., nauuza ukiisha naagiza mwingine, na pesa ninayofanyia hivyo ni ya mkopo, nikizubaa, nitashindwa hata kulipa mkopo wa watu..kwahiyo….’nikatulia nilipomuona wakili mwanadada akitokea.

‘Oh,samahanini, sikujua kuwa kuna mgeni, ooh, endeleeni kuongea… lakini kwanini mnaongelea mlangoni, mkaribishe mwenzako ndani, maana namuona kachoka, ingia ndani muongee kwa nafasi….’akasema.

‘Aaah,mimi sina muda, nitaongeaje na huyu mgeni…., mtu ambaye anajifanya hanijui, hanikumbuki…haina haja, na hata hivyo akili yangu hapa imechoka, nina usingizi wa kupindukia, naomba tu, nijue nini kitaendelea baada ya hii dhamana, maana tumeipata hiyo dhamana, na mimi nimekuja kwako kwa ombi moja kuwa kama inawezekana uwe wakili wangu,…..nitajitahidi kukulipa…’akasema na kuonyesha kweli amechoka, maana hata kuingia pale ndani alikuwa akipepesuka.

‘Upo safi lakini..nakuona kama unapepesuka…..oooh, unaona…upo safi kweli wewe?’akauliza wakili mwanadada huku akikimbilia kumshika.

‘Ni usingizi na uchomvu….’akasema nikiwa mimi nimeshamuwahi, kablahajanguka, akawa mikononi mwangu, nilimuwahi na kumdaka,…na nilivyomsika,  akawa kama kanilalia, na ile hali ilinifanya moyo wangu uzidishe mapigo ya moyo….

‘Oh, samhani….naona hali yako sio shwari..l’nikasema.

‘Hali yangu haina shaka, nahitaji kulala kidogo…’akasema huku akijitoa mikononi mwangu na ikawa kama vile ananisukuma nisimshike.

‘Kwa ajili ya afya yako ni vyema ukajipumzishe, hata kama ukitaka unaweza ukajipumzisha hapa kwangu, …’akasema wakili mwanadada.

‘Hapana nakwenda kwangu, siku ya ngapi sasa sijaweza kuingia kwangu,…nilifika nyumbani mara moja, halafu nikakimbilia kuja huku…kwahiyo ngoja nikaangalia usalama wa sehemu yangu,….hata hivyo bahitaji kujipumzisha nikiwa huru…. usijali mpendwa…’akasema na huku akijiandaa kuondoka.

‘Wewe  kakusanye nguvu, maana kesi yenu ni kesho kutwa, tumeomba ifanyike haraka iwezekanavyo ,maana kila kitu kipo tayari, na hatutaki ipoteze muda tena na matokea yake lolote linaweza kutokea, kwahiyo leo na kesho una muda wakujipumzika,cha muhimu ni masharti ya dhamana, kuwa hutakiwi kusafiri…’akasema wakili mwanadada.

‘Usiwe na sahaka, na je kuhusu wewe kuwa wakili wangu unasemaje?’ akauliza huku akiniangalia kwa jicho la kujiiba.

‘Hilo usijali,na usiwe na shaka, kila kitu kitakwenda shwari, wewe usiwe na wasiwasi wowote,mambo yote yapo shwari,…huhitaji wakili…nakuhakikishia hilo’akasema wakili mwanadada na kuniangalia mimi kama nina la kusema, na mimi nikafungua mdomo na kusema;

‘Ngoja nikusindikize, maana ulivyochoka,unaweza ukalala njiani..’nikasema.

‘Hapana, tafadhali, ninachohitaji sasa ni kufika nyumbani na kulala, sio kuongea na mtu, na wala sihitaji kuwa na mawazo na mtu, nitakunywa dawa zitakazinisaidia nilale vyema, wewe endelea na mambo yako, siku ya kuongea na mimi tutaongea kiukweli, na nahitaji majibu ya maswali yote….’akasema na kuanza kuondoka.

‘Maswali….’nikasema nay eye akageuka na kuniangalia, safari hii alionyesha uso wa kucgangamka, akasema;

‘Ndio maswali…..umeyasahau eehe…kwaheri….’akaondoka.

Majibu ya maswali gani…’nikajiuliza.

‘Unalo hilo, tafuta majibu ya maswali yote uliyowahi kuulizwa,…’akasema wakili mwanadada huku akitabasamu.

‘Maswali gani hayo?’ nikauliza.
‘Utakuwa unayajua ni maswali gani, …ni swala la kutulia na kutafakari kwa makini, wewe nenda katafakari kwa makini,…..’akaniambia huku akinisindikiza nitoke nje,maana na yeye ailionekana kuchoka, alikuwa akihitaji muda wa kupumzika,…nikawa najivuta kutoka nje.

Nikawa sina jinsi, nikatoka nje,na badala ya kuondoka moja kwa moja, nikawa nimesimama pale nje ya mlango, nikijiuliza mwenyewe kichwani, hayo maswali ni maswali gani, na kwanini kila nikikutana na huyu mwanadada ananiacha nikiwa na mawazo mengi,na kwanini iniwie vigumu kwangu kumjua, wakati yeye inaonyesha wazi kuwa ananifahamu….kama ni kweli ndiye huyoo ninayemfahamu, kwanini asiniambie moja kwa moja.

Nikafika nyumbani kwangu,na mwenye nyumba yangu, akaniambia kuna mgeni alifika hapo akiniulizia

‘Mgeni gani na yupoje?’ nikamuuliza.

‘Ni msichana mmoja anasema anatoka kijijini kwenu…’

‘Msichana?’ nikauliza.

‘Ndio…mnzuri kweli, lakini alionekana kuchoka sana sijui ni kwasababua safari ndefu,…aansema atakutafuta kesho…’akaniambia.

‘Yupoje…anafananaje..?’ nikauliza

‘Nimekuambia ni mrembo, mnzuri….siwezi kumueelzea sana, …hata hivyo mtaonana nye kesho, jina lake hakuniambi, ila anasema wewe mnajuana toka utotoni…’akasema.

‘Anasemaanatokea kijijini?’nikauliza.

`Ndio, na alikuwa na begi la safari kabisa….’akaniambia.

  Nikaingia ndani nikiwa an mawazo mengi, huyu mgeni ni nani ambaye tulikuwa tukijuana naye toka utotoni, …isije akawa ndiye Tausi binti Maringo halisi,….

NB: Hii ni sehemu ndogo ambayo inatukaribisha katika kumalizia hiki kisa, nahisi mengi yatakuwa yameeleweka, kilichobakai na hitimisho kamili.

WAZO LA LEO: Mapenzi ya kweli hutoka kwenye nafsi, umbo na sura ni vichachizo vya kuvuta hamasa, lakini matendo mema,na tabia njema ndiyo dira ya mapenzi ya kweli. 

Ni mimi: emu-three

No comments :