Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, July 6, 2012

Hujafa hujaumbika-64 hitimisho-22Hakimu alichelewa kuingia na hatukujua ni nani atasimamishwa kujielezea, …na leo kulikuwa na watu wengine wameongezeka,….sikujua ni nani hawo watu, nakwamba je ni miongoni mwa wahusika wa hiyo kesi au ni watu wa sheria tu. Nhunguza kwa macho kama kuna ninayemfahamu, lakini wote walikuwa an sura ngeni kwangu.

Kwamuda ule sikuwa ninajali sana kuwepo kwao,nilikuwa na mawazo yangu kichwani, na nilipotua jicho langu upande wangu wa kulia nilimuona kumwangalia yule mwanadada, rafiki wa wakili mkuu, naye ilionekana alikuwa akiniangalia maana nilipogeuka kumwangalia aligeuza kichwa chake na kungalia mbele kwa haraka.

‘Haya wakili mwanadada, tuambie ni nani anahitajika kwasasa kuleta maelezo yake maana naona muda umekwenda sana….?’ Akauliza hakimu.

‘Wazungumzaji wetu wawili waliopita mke wa wakili mkuu na rafiki yake,walikuwa hawajamaliza malaezo yao,  naona ni vyema kwanza tukamsimamisha mke wa wakili mkuu, na baadaye tutamsimamisha rafiki yake, tuendelee kusikiliza yao, sehemu tuliyoachia.

Mke wa wakili mkuu, aliposimama kwanza aligeuka kumwangalia rafiki yake, ambaye aliinua mkono na wakashikana kama vile wanapeana moyo. Kweli walionekana ni marafiki alioshibana. Yule mwanadada, alikwenda moja kwa moja pale mbele  na alipokaa kwenye kiti akageuka kumwangalia mume wake ambaye kwa muda huo alikuwa kainama chini.

Na mimi kwa muda ule nikawa nimwangalia kwa makini yule mwanamke, nikajaribu kujiuliza kwanini aliamua kufanya jambo kama lile, na kwanini ni rafiki mkuu wa huyo mwanadada mwingine, au ni kwa vile wanasema waliwahi kukutana huko Kenya. Nilipofikia hatua hiyo, ya kuwa walikutana huko Kenya, nikajaribu kumuwaza mtu niliyemfahamu, ….lakini sikuweza kuwaunganisha kuwa huenda akawa ndiye huyo ninayemuwaza.

Nikamwangalia yule mwanadada akiwa katulia, haonyeshi wasiwasi,….nikawa najiuliza  ni nini ataulizwa na wakili mwanadada, ….maana kwa mtizamo wangu, huyo mwanadada huenda akajaribu kupindisha habari zake ili wasije wakaonekkana kuwa wao ndio walioua, wau waliua kwa bahati mbaya,….naikawa na matumaini kuwa huenda leo ndio mwisho wa maelezo yao, na ndio diku ya kumjua muuaji, ….vinginevyo itakuwa ni kupotezeana muda tena.

Kwangu mimi niliona kama kupoteza muda, ….maana kila kitu kipo wazi, watu wamekubali kuwa walizamiria hivyo, wkachukua bunduki, sasanini kitafuta kama sio kuua, …ngoja nimsikilize huyo mwanadada kamaatasema nini leo,maana …..dunia hii kuna mambo, kama walivyosema, hujafa hujaumbika…..

Wakili mwanadada akasimama na kumsogelea yule mke wa wakili mkuu pale mbele,akamwangalia ,nilihis ni yale macho ya uwakil, yasiyo nawoga, yenye ujasiri, kama askari aliyena djamira ya kweli, akauliza swali.

‘Hebu tuambie, siku ile mlipoamua kwenda kufanya yale mlioyokuwa mumekusudia kuyafanya wewe na rafiki yako ilikuwaje,?’

‘Siku ile tulipanga tukutane nyumbani kwangu, na kwa vile rafiki yangu alikuwa likizo , ilikuwa ni rahisi kwake, na mume wangu alikuwa anaumwa kalazwa hospitalini. Na mimi siku hiyo ilikuwa siku ya mapumziko. Rafiki yangu alikuja nyumbani mapema, na tukapata muda wakujipangavyema, na kupeana majukumu.

‘Kwakeli kila mmoja alikuwa na hasira zake moyoni dhidi ya Kimwana, maana taarifa nilizozipata mimi mwanzoni ni kuwa huyo mwandada hayupo hapa jijini, …lakini mwenzangu aliniambai kuwa bado yupo, na anatamba kuwa hawezi kukamatwa na polisi, kwa vile  wote wapo mikononi mwake,…akiamua anawalipua mara moja,…na pia atahakikisha waume za watu wenye wake lakini wake zao hawajui kutunza waume, yeye ataifanya hiyo kazi, kwa thamani kubwa…

‘Una maana gani kusema kwa thamani kubwa..?’ akaulizwa.

‘Yaani hawo wanaume watamlipa gharama kubwa, kamaunavyoona anajenga nyumba ya gharama kubwa, anagari la kifahari…..navitu kama hivyo…’akasema huyoo mwanadada aklionyesha wivu usoni.

‘Hebu tukumbushe, mlijuaje kuwa yupo wapi,kwani kama sikosei kwa muda ule Kimwana alikuwa anatafutwa na polisi?’ akaulizwa.

‘Rafiki yangu alikuwa keshapata taarifa zote, na kama unavyokumbuka kwenye maelezo yangu ya mwanzo nilivyoelezea,tulishakwenda kule kwenye nyumba iliyopo karibu na nyumba ya Kimwana na kugundua wapi anapojificha ,kwahiyo, hilo halikuwa gumu kwetu tena, na tulishajua kuwa ni siku gani anakuwepo hapo, na kwa muda gani…’akasema.

‘Haya endelea na maelezo yako,….’akasema hakimu alipoona wakili mwanadada katulia.
Basi kwanza tuliangalia mkanda mmoja wa ujasusi, mkanda huu unafundisha jinsi gani ya kufanya upelelezi,jinsi gani ya kumuwinda adui yako,na pia jinsi  gani ya kuweza kumuwinda adui yako bila hata ya yeye kujua, na jinsi gani gani ya kutumia silaha, ili usije ukajulikana kuwa ndio wewe uliyeitumia.

Kwahiyo jambo la kwanza tulilolifanya, licha ya kuwa na uhakika, kuwa mara kwa mara tulikuwa tunafanya hivyo na mume wangu, tunapoirudisha ile silaha, tukiwa tumetoka kuwinda, …..Tukaifuta ila silaha vyema, kuhakikisha kuwa haina alama za vidole na hapo nyumbani kulikuwa na vitambaa mbali mbali vya kufutia alama za vidole, ….’akasema.

‘Ulijuaje kuwa ni vitambaa maalumu vya kufutia alama za vidole?’ akaulizwa

‘Mimi na mume wangu mara kwa mara tunakwenda kuwinda na mume wangu alishanifundisha kuwa ni vyema kwa usalama wa silaha ni kuhakikisha kuwa ni safi na haina alama ya mtu yoyote, ili kama itatokea hatari,mtu kuitumia,  iwe ni rahisi kumgundua….kuwa ni nani aliyeitumia kwa mara ya mwisho….

‘Ina maana hizo silaha zilikuwa zinzwekwa wapi, …?’ akaulizwa

‘Kulikuwa na chumba maalumu ambacho hata msichana wetu palenyumbani haruhusiwi kuingi, na mimi na mume wangu ndio wenye ufunguo wa hicho chumba..’akasema.

‘Endelea kuelezea…’akaambiwa.

Kwahiyo mimi na rafiki yangu tulihakikisha hayo yote tumeyafanya, na baada ya kuisafisha ile silaha, na kuiweka risasi,…tukiwa tumevaa soksi za mikononi,…tulivaa hizo soksi za mikononi mapema, kabla hatujaishia ile  silaha, na tulihakikisha kuwa hakuna anayeigusa hiyo silaha kwa mikono mitupu, tukiweka ile silaha kwenye mfuko wake, ambao kama umeubeba inaonekana kama mtu aliyebeba gitaa, na sio rahisi mtu kujua kuwa umebeba silaha.

Tulichukua gari langu hadi huko Mbezi, na tulipofika hapo tuliliacha hilo gari, mbali kabisa na nyumba zile, na tukatembea kwa miguu hadi kwenye lile jengo, na bahati nzuri, kulikuwa hakuna watu kwenye hilo jengo, kulikuwa kimiya kabisa, tukapanda hadi gorofa ya juu, ambapo ungeliweza kuona kule ilipo nyumba ya kimwana.

Tulipofika tukatafuta sehemu yetu ambayo tuslihaichagua tukawa tunasubiri muda muafaka, tulipoangalia kule kwenye nyumba ya Kimwana, tulimuuona Kimwana akiwa anatembea huku na kule,ilionekana alikuwa akikagua nyumba yake, na hakuonyesha wasiwasi wowote, na hili likawa faraja kwetu.

Tulipoona kuwa muda muafaka umefika na Kimwana yupo kwenye kile chumba chake,..tukajiandaa kufanya lile tulilokusudia, na mara tukasikia gari likija eneo lile la jengo tulimuokuwa, lakini likapita na kwenda kusimama kwa mbele,…kweye lile gari, walitoka watu wawili, wakawa wanatembea kuja kwenye lile jengo, walifika wakawa wanakagua kwa nje, lakini bahati nzuri hawakupanda juu, na baaadaye wakaondoka, lakini hatukujua wameeelka wapi, maana walipita kwa nyuma ya jengo ambapi tusingeleiweza kuwaona..hata hivyo gari lao, tuliliona likiwa bado limesimama pale pale.

Mara kwenye eneo la nyumba ya Kimwana kwa nyuma nikaona mtu anaelekea kwenye dirisha, na kusimama pale dirishani, akiwa anaangalia ndani ya chumba alipokuwa Kimwana, ni nyuma ya lile jengo.Nilipomchunguza vyema nilimgundua kwa haraka kuwa anafanana ni mume wangu.

Sikuwa na uhakika sanakwa muda ule,  alikuwa kasimama akichunguza huku na kule, kila nilivyomwangali vyema niliona kabisa ni mume wangu, niliona ajabu, maana najua kabisa kuwa mume wangu ni mgonjwa, kalazwa hospitaloni, sasa amekujaje pale, na baadaye sikumuoan tena, nikahisi walipanga na huyo Kimwana, na atakuwa kaingia ndani,na uchungu,wivu na hasira vikanizidia.

Wazo langu kwa muda ule lilikuwa ni kwamba mume wangu ananidanganya kuwa anaumwa, kumbe anakuja hapo kukutana na hawara yake, Hasira na chuki dhidi ya Kimwana zikazidi kunipanda, nikaichukau ile silaha kwa hasira na kuielekeza kule alipokuwa Kimwana, …..na rafiki yangu,akawa kama anaogopa, nikamwambia;

‘Kama unaogopa, ondoka mapema, mimi siwezi kuona huyu Malaya anatembea na mume wangu, nimuache hivii hivi, sasa hivi nimemuona mume wangu akiingia kwenye hilo jengo, ina maana wanakutana humo, huku mimi najua kuwa mume wangu ni mgonjwa, ….’nikasema kwa hasira na rafiki yangu akaniambaia kuwa sio huenda sio yeye, lakini mimi nilikuwa na uhakika kuwa ni mume wangu. Lakini kabla hatujajiweka sawa mara tukaona watu wengine wawili , mke na mume wakielekea kwenye hilo jengo, nje ya geti.

Yule mwanaume alikwenda moja kwa moja kule kwenye geti wanapokuwa walinzi, na tulimuona akiongea na walinzi, na cha ajabu yule mwanamke yeye alikwenda nyumba ya ile nyumba na kupanda kwenye ukuta kwa nyuma ya jengo na kuingia ndani ya lile jengo,…na mwenzangu kwa wakati huo, alikuwa anamwangali yule mwanaume aliyekuwa akiongea na walinzi na ilionyesha kama anamfahamu,naakaniambia kwa hasira.

‘Ina maana huyu mwanamke Malaya anawapanga wanaume kwa zamu,…kamamumewako yupo , ndani huenda anasubiri mume wako atoke na huyo mwanaume aliyepo pale mlangoni ataingia zamu yake ikifika,….. kweli huyu ni Malaya hastahili kuishi.. hata mimi siwezi kumuona akiwachukua wanaume wa watu bila aibu, nipe hiyo silaha maana mimi nina shabaha kuliko wewe..

‘Hapana niachie mimi maana ndiye mwenye hasira na huyu mtu….kanichukulia mume wangu …hapana hii ni kazi yangu…wewe kaa pembeni maana hata mimi nina shabaha…’tukawa tunaigombea ile silaha, na mara tukasikia sauti y akingora cha polisi ikilia kwa nje, na muda huo huo tukasikia kama mtu anakuja pale tulipokuwa, tukakimbilia kwenye chumba kingine kijificha.

‘Ni nani huyo? Nikauliza

‘Sijui, …’mwenzagu akasema.

‘Mbona umeiacha ile silaha pale, mtu anaweza akaiona na kuichukua..’nikamwambia mwenzangu.

‘Pale nilipoificha sio rahisi kuoenekana, lakini nenda kaichukue wewe…’akaniambai mwenzangu, akionyesha uwoga,….nikawa na wasiwasi sana, na kwa muda huo nje kile king’ora cha polsi kilikuwa kikikaribia sana maeneo tuliyokuwa na ikabidi tujifiche , tukawa na mashaka,…tulijificha pale kwa muda,hadi tulipohakikisha kwua hicho king’ora kimepita, na hakuna shaka tena.

Mara tukasikia sauti kama ya yowe…mara moja, kamaa `aah, nakufa….’ Likitokea kwa nje, na nahisi kama lilitokea kule kwenye nyumba ya Kimwana….na nahisi kama niliskia sauti ya kitu kama kuvunjika kwa kituhivi, …mimi nina ufahamu sana na mlio wa bunduki yetu,…. moja kwa moja nilihisi ni sauti ya silaha iliyopigwa ,ambayo ina kiwambo,kuna mlio fulani kama umeshaitumia sana unaweza kuujua, sio mkali sana, lakini kuna mlio wake,,nahisi kmaniliusikia, na hapo nikawa na wasiwasi, kuwa huenda kuna mtu kaitumai silaha yetu,…

Nikatoka pale tulipokuwa na kunyemelea kule kwenye chumba ambapo tulikuwepo kabla, na ambapo ndipo kwenye silaha,…nikafiuka pale ambapo nilimuona rafiki yangu akiificha, nikapatwa na mshituko wa ajabu,….sikuamini macho yangu,nikamuita mwenzangu, …

‘Silaha mbona siioni pale ulipoiacha una uhakika hukuiweka sehemu nyingine??’nikamuuliza

‘Usinitanie, silaha niliweka pale pale, umeangalia vyema kwenye ile mifuko ya cementi iliyotumika…,maana  sio rahisii mtu kuioana umeangali vyema, ?’ akaniulzia mwenzagu bado akiwa na waasiwasi akiw abado kajificha,nalionekana wazi anaogopa kutoka  pale alipojificha, na baaadaye  akatoka na wote tulikwenda pale tulipoiweka ile silaha, na kweli hatukuikuta…maana mifuko ilikuwa imeondolea kuonyesha kabisa kuna mtu kaichukua...’

‘Mna uhakika kweli wakati mnakimbia mliiweka hpo mlipokuwa mnasema, huenda…..?’akauliza wakili mwanadada.

‘Nina uhakika huo, hatukuondoka nayo wakati tunakimbia,, silaha hiyo kwa wakati huo alikuwa kaishika mwenzangu, na wakati tunakimbia,nilimuona kabia akiisokomeza ndani ya mifuko ya cementi iliyokuwa imepagwa humo,…kulikuwa na mifuko ilitumika, ikaachwa hapo,ilikuwa mingi…. na tuliporidi tulitafuata kila sehemu yote haikuwepo..tukachanganyikiwa na ukumbuke nilisikia kabisa sauti kama ,mlio ambao naujua kabisa ni mlio wa ile silaha inapopigwa ikiwa imewekwa kiwambo cha kuzuia sauti, kuna sauti ndogo unaisikia.

‘Ina maana unahisi ilitumiwa wakati mumejificha…?’akaulizwa

‘Nilihisi hivyo,lakini sikuwa na uhakika, maana silaha haikuwepo, ….lakini hata hivyo, kuanakitu kingine kilizihirsiha kuwa imeshatumiwa,….’akasema

‘Kitu gani?’akaulizwa

‘Harufu ….harufu kama ya baruti, huwa silaha ikitumika kuna ule moshi wake, unanuka ….niliusikia, na hata mwenzngu aliuhisi, tukawa tumeduwaa, na mara.. tukasikia nyingi upande ule wa nyumba ya Kimwana, tukaangalia, na kule tuliona yule mwanamke aliyekuwa akipanda ukuta, akiwa kainama na pale chini kuna mtu kalala…

‘Unaona kule, inaonyesha Kimwana kalala chini,isije ikawa, kuna mtu kaitumia silaha yetu, na kumuua Kimwana….’nikasema nikiwa na mashaka nauwoga mwingi

‘Haiwezekani, ni nani mwepesi kiasi hicho na alijuje kuwa tupo hapa, na akajua kuwa tutakimbia akaichukua 
ile silaha na kuitumia,haiwezekani,…’akasema mwenzangu.

‘Sasa hapa sio salama tena, lakini siwezi kuodno kabla ya kuipata hiyo silaha, ni silaha ya mume wangu na inajulika kuwa yeye ndiye anaimiliki, lazima tutafute kwanza….’nikasema.

‘Muda huo haupo,kama kuna mauaji , na polisi wanakuja, huoni kwamba tutakuwa hatiani,na mfano kama kweli Kimwna kauwawa, na polisi wakatuona tupo hapa, tutasema nini,tuasema tulikuwa tunafanya nini huku, hebu twende zetu, tuondoke  hapa haraka…’aliniambia mwenzangu….’akasema mke wa wakili mkuu.
Wakili mwanadada akageuka na kumwangalia rafiki wa mke wa wakili mkuu,halafu akageuka kwa hakimu na kusema;

‘Muheshimiwa hakimu, naomba nimsimamishe rafiki wa mke wa wakili mkuu, aendeleze sehemu hii, ni shemu muhimu sana tunahitaji  kuyasikia maelezo ya pande  zote mbili, na kama kuna kitu mwenzake kasahau tupate kukisikia’

Hakimu akasema ni sawa lakini mke wa wakili mkuu arudi kwanza kukaa, na kama atahitajika tena ataitwa. Mke wa wakili akarudi kukaa na walipisha na mwenzake, wakakumbatiana kidogo na kuachana,
Rafiki wa mke wa wakili mkuu akaelekea pale mbele na kwenda kukaa kwenye kile kiti kilichoweka pale mbele, alionyesha uso usio na furaha, nikadhania kuwa labda huenda ni kwa vile niliongea naye nab ado alikuwa na hasira na mimi…..au ni kutokana na hayo maelezo aliyotoa rafiki yake, huenda hayakumfurahisha, au kuna sababu nyingine anayojua yeye mwenyewe….nilimwangalia akiwa katulia pale mbele akisubiri kuulizwa swali;

‘Kama ulivyomsikia mwenzako yeye anasema wewe ndiye uliyekuwa na hiyo silaha,kabla haijatoweka,je kwa muda wote ulikuwa umevaa soksi mkononi?’ akaulizwa.

‘Ndio,sikuwahi kuzivua hadi niliporudi nyumbani kwa rafiki yangu, yaani mke wa wakili mkuu….’akasema.

‘Wakati mpo pale uliwahi kumuona mtu yoyote …?’ akaulizwa

‘Kwa pale kwenye jengo, sikuwhi kumuona mtu, ili tulisikia sauti za watu,wakipanda, kuja juu, na hata baadaye tulipokuwa tunaitafuta ile silaha, tulisikia sauti za nyayo za watu,wakishuka au kupanda juu,lakini hatukuwahi kuwaona.

‘Hamkujaribu kuangalai kuwa ni watu gani?’ akaulizwa

‘Kwa hali tuliyo nayo, hatukuwahi,maana mawazo yetu yote yalikuwa kwenye kutafuta hiyo silaha,na hata tulipohisi huenda Kimwana kauliwa, hatukuwa na mawao ya kuangalia zaidi, na nilipomshauri mwenzagu kuwa tukimbie, tulitoka hapo haraka, nakukimbilia pale tulipoweka gari letu.

‘Je mlipofikakwenye gari, mlilikuta kamalilivyo, na hapakuwa na gari jingine, au pikipiki?’akaulizwa.

‘Tulilikuta kama lilivyo, ..nakumbuka vyema ,kulikuwa na alamaza michoro ya kuonyesha kuwa kulikua napikipiki iliyokuwa imepita hapo,….maana kulikuwa na mchanga, na kitu kikipita kinaacha alama…’akasema

‘Una uhakika alama hizo hazikuwepo kabla?’akaulizwa.

‘Hazikuwepo kabla, nina uhakika huo, maana tulipoteremka kwenye gari, nilimwambia mwenzagu tuhakikishe kuwa tunaliacha mahali ambapo hata mtu akilisogelea tunaweza kujua,kwahiyo tuliangalai sehemu zote kwa makini….nina uhakika kabisa alama hizo hazikuwepo kabla.

‘Swali hili ni muhimu sana, maana katika maelezo yako sikusikia ukimuelezea huyo aliyekuwa akikusadia kukupa taarifa, na kwa maelezo ya mwenzako alisema wewe ulimwambi kuwa kuna mtu anawasaidia kuwapatia taarifa ambazo ulikuwa ukimpa mwenzako,….je ni nani aliyekuwa akiwasaidia kuwapa hizo taarifa?’akaulizwa.

‘Ni..ni nesi,…yule pale…’akasema nakumuonyeshea yule mwanadada nesi kidole, yule nesi kwa muda huo alikuwa katulia,na aliponyoshewa kidole akaonyesha kama kushituka. Na kusema kwa sauti ya kujihami;

‘Mimi…’

Wakili mwanadada akamwangalia huyo mwanadada kwa muda, halafu akageuka kumwangalia huyo rafiki wa mke wakili, na kusema;

‘Kwahiyo ina maana huyu nesi, alikuwa akijua kuwa mtakwenda huko kwa Kimwana, na pia ina maana kuwa yeye alijua yote ambayo mlikuwa mkiyafanya?’ akaulizwa.

‘Ndio kwasababu yeye ndiye aliyekuwa akinipa taarifa na mipango yetu, yeye ndiye aliyekuwa akinisaidi  katika uchunguzi wa kujua wapi alipo Kimwana, na kilaninalotaka kulifanya nilikuwa namwambia yeye, na yeye alikuwa akinishauri nifanye nini kwa wakati gani.

 Na kipindi nilipomwambia lengo letu , alifurahi sana, na akasema yupo tayari kutusaidia maana hata yeye ana hasira na huyu Kimwana,….na akasema yeye atakachofanya cha kutusaidia ni kuhakikisha anamtafuta huyo 
Kimwana,na kujuwa wapi alipo, kwani kwa tetesi za watu wengi, ilijulikana kuwa hayupo hapa jijini, lakini yeye alisema lazima atakuwepo humu jijini, lakini anajificha tu,….’akasema nakutulia, na alipomuona wakili mwanadada hamuulizi swali akasema’

‘Na kweli alitusaidia sana maana sio kujua tu wapi Kimwana alipo, lakini pia alichunguza na kugundua ni muda gani Kimwana anakuwepo hapo kwenye jengo lake. ...’akasema huyo rafiki wa wakili mkuu. Na mimi nikajaribu kumwangalia yule nesi ambaye alionekana kama kukerwa na yale maelezo maana kuna muda alikuwa akipanua mdomo kutaka kubisha,lakini hakuweza kutoa sauti.

Wakili mwanadada akamgeukiwa yule Nesi akamwangalia, na yule nesi naye akamwangali huyo wakili mwanadada kwa macho ya kujifanya haogopi kuangaliwa na yupo tayari kwa lolote, na baadaye wakili mwanadada akageuka na kumwanglia hakimu na kusema;

‘Ndugu Muheshimiwa, naomba sasa tumsimamishe huyo nesi, tusikie upande wake, kama unavyoona yeye anahusika….,ukikumbuka kuwa yeye ndiye aliyekuwa na wakili mkuu hospitalini, na yeye alijua kuwa wakili mkuu katoka hospitalini, na kwenda huko kwa Kimwana, na pia yeye alijua kuwa hawa akina dada wawili watakwenda huko kwa Kimwana,…na pia yeye ni mpelelezi wa Sokoti, ….kwahiyo yeye ni kiungo mzuri wa matukio haya yote.

Hakimu akamwangalia nesi kwa muda halafu akasema;

‘Sawa,..haya Nesi tunakuomba upite mbele…ni zamu yako, tunataka kuskia maelezo yako’
NB Je huyu nesi atakuwa na nini cha zaidi, ukumbuke kuwa yeye aliachwa hospitalini na wakili mkuu…sasa ilikuwaje? Na je wewe unahisi ni nani muuaji?

WAZO LA LEO: Mnapoishi zaidi ya mmoja, ni vyema tukajenga tabia ya kuhurumiana,kujaliana na kuoneana huruma. Katika nyumba nyingi hasa za wapangaji, au kwenye mjumuiko wa watu, kuna baadhi ya watu wanafungulia redio au runinga zao, au simu zao kwa sauti kubwa, kiasi kwamba inakuwa kero kwa wengine. Huu sio uuwangana.
Tujue kuwa sote hatupo sawa, kuna wengine wagonjwa , hawapendi sauti kubwa.Kuna watoto wadogo wamelala, kuna wengine wanahitaji kutuliza vichwa vyao hawapendi sauti kubwa sana,yote hayo tujaribu kuyafikiria, kwani ni vyema ukampenda jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Lete ,mambo mkuu, naumia kwa kusubiri!