Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, July 4, 2012

Hujafa hujaumbika-63 hitimisho -21
Wakili mwanadada akanielekeza kwa kichwa nyuma yangu huku akisema

‘Sawa,…yule kule anakuja na rafiki yake, unataka muongee naye sasa hivi?’ akaniuliza, na nikageuka nyuma na kujikuta tukiwa tunaangaliana na wanadada hawa wawili wakiwa wanakuja taratibu, huku wakiongea kwa furaha.

Walivyokuwa wakiongea hawakuonyesha dalili yoyote kuwa wapo kwenye matatizo, na hili likawa linanipa mawazo mimi, na kujiuliza bila majibu, ina maana hawa akina dada hawajioni kuwa wapo kwenye matatizo, hawajioni kuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji, mbona hawana wasiwasi, au ndio kwa vile wanahisi watasamehewa…

Nikawa nimeguka nusu mwili,na kichwa kikawa kinawaangalia wao wakiwa wanakuja taratibu huku wakiongea na kutabasamu, na macho yao yalikuwa yakituangalia sisi kama vile wanatuongelea sisi  wawili, mimi na wakili mwanadada.

******

Ilikuwa ni kama unaangalia zile sinema ambazo unafika sehemu tukio linaonyeshwa kwa mwendo wa taratibu .  

Ndivyo akili yangu ilivyokuwa ikiwaangalia hawa wanadada wawili, wakiinua mguu kwa hatua ndogo ndogo, na huku midomo yao ikionyesha tabasamu la namna yake.Mimi kwa ujumla nilikuwa nimeduwaa huku sana sana namwangalia yule mwanadada rafiki wa mke wa wakili mkuu, anavyokuja na sikuwa na mawazo na rafiki yake.

Na wao walijua kabisa kuwa tunawaangalia  wao ,maana mimi nilikuwa nimegeuka na kuwaangalia sijui mwenzangu wakili mwanadada kama naye alikuwa kafanya hivho hivyo au la, maana sikuwa na mawazo ya kugeuka kumwangalia. Hata hivyo yeye kwasababu alikuwa moja kwa moja anawaona wanavyokuja haikuonyesha dalili ya moja kwa moja kuwa anawaangalia wao, sana  sana itaonyesha kuwa ananiangalia mimi.

Nahisi yule mwanadada alijua kabisa namwangalia yeye, kwa jinsi alivyokuwa akionekana, maana nilihisi macho yake yalikuwa yakiniangalia moja kwa moja, na hapa nikawa najaribu kujiuliza macho kama haya niliyaona wapi, sikuwa na wazo la zamani sana, mawazo yangu yaligota kwa matukio ya hapa karibuni. Na nikahisi kama anatabasamu kwa kule kuniona namwangalia.

Labda tabasamu lile lilitokana na yale waliyokuwa wakiongea, lakini kwangu mimi tabasamu lile lilikuwa maalumu, maana liliganda kichwani kwangu na kunifanya nizidi kuduwaa,na moyo ulikuwa ukinienda mbio  isivyo kawaida yake, na niliduwaa vile hadi walipotufikia,bila ya kugeuka kama nilivyokuwa awali.

‘Habari zenu…’wakatusalimia kwa pamoja baada ya kutufikia, na wakili mwanadada akaitikia,na kuwakaribisha.

‘Naona nyie mumewahi sana, ….’ Akasema mke wa wakili mkuu.

‘Ni kawaida tu, hatujawahi sana…’akasema wakili mwanadada.

Walisimama pembeni kidogo na pale tulipokuwa tumesimama, na wakili mwanadada akamgeukia mke wa wakili mkuu na kusema

‘Bosi, wangu, ….’akasema na kumgeukia  mke wa wakili mkuu, na mke wa wakili mkuu akacheka.

‘Usicheke, wewe ni bosi wangu, maana mumeo niibosi wangu, au unaukataa ubosi?’ akasema kwa utani.

‘Wala sijaukataa, ila huo ubosi iuwezi, najua mambo ya hospitalini,….lakini hayo ya kupambana na wahalifu, siwezi kabisa,….’akasema.

‘lakini unaweza, mbona unapmbana na wagonjwa, unawauliza shida zao mpaka unagundua tatizo lipo wapi ,ni sawa na sisi kupambana na watu hadi kugundua tatizo lipo wapi,…huoni ni yale yale….’akasema.

‘Hapana kwako ni kugumu, maana kumjua mhalafu, ni kazi kubwa sana, kwasababu mhalafu hawezi kukubali kuwa ni mhalafu, lakini kwangu mgonjwa anakubali kwua ni mgonjwa, kazi ni kutafuta ugonjwa gani….’akasema rafiki yake.

‘Sasa bosi wangu ninataka kuteta na wewe, unaonaje tukienda pale, maana nataka tutete wawili tu mimi na wewe, samahani kwa rafiki yako…’akasema na nikajua ni njia ya kuniacha mimi na yule mwanadada ili tupate mwanya wa kuongea. Na kwa muda huo moyo ulikuwa ukidunda, nikijiuliza nitamuanzaje. Sio kwamba mimi ni mzaifu sana wa kuongea, hapana, ila kwa huyu mwanadada hali ilikuja kuwa tofauti kabisa kwangu, sikuelewa kwanini.

Wakili mwanadada na mke wa wakili mkuu wakasogea mbali na pale tulipokuwa tumesimama, mimi nikasogea nakukaa kwenye kiti,nikamkaribisha huyo mwanadada aje akae, kwanza alisita baadaye akaja na kukaa,tukawa tutizamana, uso kwa uso,tulibakia kimiya kwa muda, na yeye akawa wa kwanza kuuvunja huo ukimiya,na kuniuliza hali na maisha yangu kwa ujumla.

‘Hali nzuri tu mungu anasaidia na maisha ni kama safari kuna kupanda na kushuka, vipi wewe?’ nikamuuliza.

‘Kama ulivyosema maisha ni kupnda na kushuka,mimi kwa ujumla ni kazi ngumu tu, kama unavyojua kazi a udakitari, ukishafika kazini huna muda wa kupumzika, …na tena ndio limezuka hili tatizo yaani akili haipumui, …..’akasema.

‘Lakini hili tatizo, kuzuka kwake ni kutokana na nyie, kwanini warembo kama nyie mkaamua kujiingiza kwenye matatizo haya?’ nikamuuliza.

‘Kwani wewe huoni ni kwanini, mbona hata wewe upo kwenye tatizp lenyewe, au kwa vile hujasimamishwa 
kujieleza, na ingelikuwa bora wewe uwe wa kwanza kusimamishwa kujielezea tukusikie upande wako , maana huenda wewe ni muhusika mkuu namba moja, na huenda ukawa pia msababishaji wahaya yote…..’akasema kwa sauti ya kukasirika.

‘Kwa vipi mimi niwe msababishaji,…mbona unanitwika mzigo ambao wala sihusiki nao,….mimi nimekuwa nikiingizwa kwenye haya matatizo bila hata kujua, najiona kama mnyonge wa kutolewa chambo, …’nikasema kwa unyonge.

‘Labda kama kweli umesahau au unajifanya kuwa umesahau, na maranyingi nyingi mla ndizi hasau, ila mtupa ganda ndiye anashau….lakini nionavyo, wewe na wakili mkuu mna kesi ya kujibu, leo na kesho ahera…’akasema huku akininyoshea kidole kwa hasira, na mimi nilibakia nikishangaa, huku najitetea kwa kunyosha mkono kuwa sijui nini anachokiongea. Yeye alinuka kwahasira na kuanza kuondoka huku akionyesha kukasirika.

‘Sikiliza nilikuwa na maongezi na wewe….’nikamwambia, lakini hakunisikiliza akawa anatembea kwa haraka na kuingia ndani ya jengo la mahakamani, na kuniacha nikiwaza hiyo kauli kuwa;

‘Mimi na wakili mkuu, tuna kesi ya kujibu , leo na kesho ahera….’nikawa naongea peke yangu na wakili mwanadada akawa keshafika huku akionyesha uso wa kushangaa;

‘Vipi mwenzako yupo wapi, mbona maongezi yamekuwa mafupi sana?’ akaniuliza.

‘Mwenzangu yupi, ….mmh yule mwanadada, kaondoka , na kuniacha nikiwa na mawazo, tulianza kuongea vyema, na tukafikia sehemu ambayo nilimwambia kuwa wao wasingelistahli kujiingiza kwenye mambo haya, na akaanza kunilaumu mimi na wakili mkuu kuwa sisi ndio chanzo cha haya yote ….’nikasema.

‘Kwanini alisema hivyo?’ akaniuliza.

‘Nilimuuliza kwanini,…, akasema najifanya nimesahau, na ndipo akamalizia kwa maneno ambayo yameniacha njia panda…’nikasema

‘Maneno gani hayo?’ akaniuliza.

‘Eti mimi na wakili mkuu tuna kesi ya kujibu hapa duniani na kesho ahera…’nikasema na wakili mwanadada akaniangalia kwa makini na baadaye akaangalia saa yake.

‘Naona muda tayari,twende ndani, …labda kwa kuyamaliza yote hayo kama tutapata muda, nitakusimamisha ujibu hiyo kesi, maana mwenzako wakili mkuu keshaongea imebakia wewe….’akaniambia.

‘Utanisimamisha kwa kwesi gani sasa,nitaongea kuhusu nini….?’ nikauliza huku nikiwa kama mtu aliyechanganyikiwa.

‘Wewe huoni kuwa wewe umelaumiwa kuwa ndiye msababishaji, ina maana isingelikuwa wewe , wao wasingelifanya hilo walilolifanya, nina maana wewe na wakili mkuu…’akaniambia.

‘Mimi na wakili mkuu!’nikasema kwakushangaa.Na wakili mwanadada akawa anaondoka kuelekea ndani, bila kusema neno, mimi nilisimama pale kwa muda nikiwa nimeduwaa, huku nikiwaza, hiyo kauli, na nikawa najiuliza kuwa lini mimi na wakili mkuu tukawa pamoja hadi kufikia kuwaingiza hawa wanadada wawili kwenye matatizo.

‘Kweli nitaomba na mimi nisimame mbele,  ya mahakama nijue kosa langu ni nini , nitaomba iwe hivyo,..’nikasema na kuingia ndani.

NB: Samahani kwa kukatisha hapa, kwasababu ya majukumu na mambo juu ya uwezo.

WAZO LA LEO: Usikate tamaa unapotatizwa na mambo,ambayo huenda yanakukuta hata bila kutarajia, na wengine hukimbili kusema `ooh,labda ni mkono wa mtu', …tusikimbilie huko, tuwe na subira, tujue kiini ni nini, na je ni ipi njie nyepesi ya kuyatatua hayo mataizo bila dhana potofu, tukumbuke kuwa mwenye kusubiri ni mpenzi wa mungu.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Kuna mkono wa mtu m3, ni tabia ambayo imekithiri sana siku hizi.

Nashangaa hata wasomi wakubwa wana tabia hiyo ya imani za kuamini kuwa kalogwa.kuna hata waumini wa dini wanaita hivyo, eti kuna mapepo.

Hata kama yapo , kama ukiyaamini, basi yatakuathiri, cha muhimu ni kumwamini mungu, atakusaidia
Na kumwamini mungu sio uchangenye na imani zako .

Anonymous said...

Ndugu m3 nakuonea huruma sana. maana unatumia muda wako lakini sijui unapata nini, sisi wenzako tunajisomea tunafurahi je wewe....angalia hili kwa makini, tunakupenda sana.