Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, July 9, 2012

Hujafa hujaumbika-65 Hitimisho 23



‘Ndugu Muheshimiwa Hakimu, kama nilivyoelezea awali kuwa kuna baadhi yetu hapa, nimesikia kuwa wanataak kukiukwa yale masharti  ya kusema ukweli wote, kwasababu moja au nyingine wameamua hivyo, au wameshauriwa hivyo, na hii itatufanya tupoteze muda mwingie kuulizana maswali, lakini nakuhakikishia Muheshimiwa hakimu kuwa ukweli wote utajulikana kwa kila mmoja wetu.

Niasema hili …kama kuwakumbusha kuwa kila kitu tunakifahamu….tunao ushahidi w akutosha, kwahiyo nawakumbusha tena ahadi yenu…..’akasema wakili mwanadada, na kabla hajamaliza yule mwanadada aliyeitwa kutoa maelezo  yake akasema kwa hasira.

‘Kama unajua ukweli wote, na una ushahidi , kwanini unatupotezea muda wetu, kwanini usiusema huo kweli tukamaliza mambo, kwanini…’akasema kwa hasira yule mwanadada na hakimu akamkatiza kwa kusema.

‘Nesi, unachotakiwa ni kuongea ukweli na utaongea pale utakaporuhusiwa kufanya hivyo, huyo hapo ndiye anayeendesha hili jopo hapa, mimi ni msimamizi na msikilizaji tu,kama hutafuata maelekezo yake, utakuwa unafanya makosa….ujue upo wapi hapa….!’akasema muheshimiwa hakimu.

‘Muheshimiwa hakimi samahani sana kwa kufanya hivyo, ila ni yeye kuanza kuleta vitisho, yeye alishatuambai kuwa kila mmoja azungumze ukweli na tukakubali, sasa ana wasiwasi gani na mimi kuwa sitasema ukweli….kwanini aanze kuonge hilo niliposimamishwa mimi, ina maana hana uhakika na mimi kamanitaongea ukweli, …’akasema na kutulia.....

‘Sawa mimi nilikuwa nasisitizia tu,….tutaona kauli yako kama ina ukweli au vipi,  kwa kuanza hebu tuambie, wewe ni nesi , je kuna kazi gani nyingine unayoijua zaidi ya unesi, na ingelikuwa vyema ukatuambai ulijifunzia wapi hiyo kai nyingine kama ipo, na kwanini ulijifunzahiyo kazi nyingine,na kwanini ukachagua unesi badala ya hiyo kazi nyingine,….’akatulia huku bado akitaka kuuliza maswali mengo kwa pamoja.

‘Sawa muheshimiwa maana naona una usongo na mimi,unaniuliza maswali mengi kwa mkupuo kama nina ugomvi na wewe….’akamwanglai wakili mwanadada kwa dharau,na wakili mwanadada akamwangalia bila kusema kitu huku kamkazia macho….na alipoona wakili mwanadada anamwangalia hasema kitu, akamwangalia hakimu halafu akaanza kuongea kwa sauti ya chini;

‘Kwa kuanzia tu,mimi ni nesi, na kama binadamu wengine kuwa wanajaribu hili na lile katika maisha yao, maana katika maisha yetu sisi Waafrika hatuna dira , kuwa kwa vile nina kipaji hiki nitaweza kufanya kazi hii, inakuja tu, umemaliza shule, na umeingia kwenye Nyanja hii unaifutilia tu, hata kama huna kipaji nacho, baadaye unaweza ukajibadili mbele kwa mbele….’akatulia.

‘Nilipomaliza shule kidato cha sita, nilikuwa na hamu sana ya kuwa askari, na hasa uaskari kanzu yaani askari katika idara ya upepelezi, nikaomba, na kweli nikakubaliwa,  nikaingia jeshini kwanza, kama kawaida, nikamaliza mafunzo ya awali, lakini sikupata nafasi niliyoitaka ya uaskari kanzu, nikaingizwa kwenye uaskari wa usalama yaani polisi wa kawaida tu, lakini sikuchaguliwa kule niliko kutaka, na hili likanikwanza sana….nikaona nimekwenda sehemu nisiyoitaka, ila hali ya kupokea amri,sikuipenda,…hata hivyo nikavumilia.

‘Nikiwa huko nikaomba nikasomee udaktari, nikaanzia kusomea unesi, ili baadaye niunganishe na kusomea udakitari,….maana nilikuwa napendelea hilo pia, kwasababau nilipoona mjomba nii dakitari na mara nyingi nilikuwa nasikia yupo nje, na mimi nilitaka sana niende nje. Lakini hayo hayakuwa rahisi kihivyo, nikawa nahaha huku na kule,…nikajiona sina bahati hiyo.  Na ndipo nikakutana na na huyu mnayemuita wakili mkuu. Tukapendana sana,…..’akatulia na kumwanglia wakili mkuu.

‘Akanishauri kuwa yeye kwa vile anakwenda kusoma nje na mimi sina bahati hiyo, basi nitulia nyumbani, yeye hapendi mimi nifanye kazi hasa ya uaskari…aliniomba niache hiyo kazi,akirudi atanio…ukumbuke kuwa kazi ya uaskari bado nilikuwa nayo,lakini nilikuwa mtegaji mkubwa, kwasababu nilitaka niwe askari kaznzu, sio askari wa kawaida, lakini hata hivyo, nikawa ndani kwa ndani naijifunza upelelezi, kupitia kwa rafiki yangu mmoja.

‘Wakuu pale wakaniona nina hamu sana na kazi hiyo, wakaniingiza kwenye hicho kitengo kwa kazi maalumu, na hapo nikaanza kujifunza mabo mengi kuhusu upelelezi, na hayo ni mambo ya ndani siwezi kuyasema hapa, …..

Nikawa nawasiliana na huyu mkuu, na akawa ananisisistiza kuwa yupo na nia yake ile ile lakini kwa masharti kuwa niache kazi,yeye hataki mke askari, na kwa vile nilikuwa nampenda,nikaamua kuacha kazi, na nikawa najishisha na kazi ya unesi, ingwaje hakuwa na maslahi sana….

Mara nikasikia kuwa huyu mkuu kamaliz amsomo, lakini kwa kipindi hiki cha mwisho cha kumaliza masomo yake tukawa hatuna mawasilinao naye, alikuwa kakata kabisa yale mawasiliano tuliyokuwa nayo mwanzoni,nikajua kuna jambo, nikafuatilia mpaka nikasikia kuwa mwenzangu huyu yupo katika hatua za mwisho za kumuoa mmoja wa ndugu wa jirani.

Niliumia sana, nikatafuta mwanya mpaka nikawasiliana naye, naye akaendelea kunidanganya kuwa hayo sio kweli, ila alibanwa na matatizo yake, ndio maana alikuwa hawasiliani na mimi, msimamo wake upo pale pale…kuwa akimaliza elimu yake , tunafunga ndoa, na kipindi hicho nilishahamia huko Kenya,na kuishi na familia yetu iliyopo huko,….na baadaye ndio wakaanzisha hiyo shule na mimi nikajiunga na shule hiyo ya mjomba.

Kweli ilikuwa ndiyo faraja yangu, maana hayo niliyokuwa nikifunza humo yalinijenga sana kiakili, na hapo nikajua uzaifu wa kibinadamu katika hisia na nikichanganya yale ninayojua ya kiuaskari, nikajikuta nina hazina kubwa sana kichwani.

‘Unasemaulijiunga katika shule ya mjomba na wakati huo ulikuwa umeshaingia uaskari,kwahiyo mambo ya silaha, na shabaha kwako haikuwa kitu kigeni?’ akaulizwa.

‘Haikuwa kitu kigeni, na sikuwa nashiriki sana, na kaam nikishiriki, nakuwa nipo peke yangu, maana sikutaka watu wanijue sana kuwa mimi nimepitia jeshini….mambo ya shabaha kwangu nikitu kidogo sana,…..’akasema.

‘Una uwezo gani katika kulenga shabaha…?’ akaulizwa.

‘Kama nilivyokuambia mamboya kulenga shabaha ni kitu kidogo sana, huo kwetu ni kama mxhezo wa kitoto, nilivyowachunguza wote mle hakuna ambaye angliweza kunifikia, hata kama tungeliwekwa kwenye mashindano, kwahiyo sikutaka kuingie kwenye mashindano yao waliyokuwa wakiyaweka mara kwa mara ya kushindana shabaha…’akasema.

Nikapata safari ya ghafla ya kwenda huko kwetu kijijini, kulikuwa na bibi mgonjwa, nikapewa kazi ya kumhudumia bibi akiwa kalazwa, na kumbe muda huo ndipo wenzangu walipanga kuoana, nakiri kuwa kama ningelikuwepo kwenye hiyo harusi isingelifungwa, vumbi lingetimuka, na bahati yao walipooana wakahamia huko Dar, ambapo ndipo  mume wake anapofanyia kazi….

Hata hivyo niliapa moyoni kulipiza kisasi, ..kwanini mtu anidanganye, na hata kunifanay niache kazi yangu, na aheri angeliambia mapema, lakini alinificha kiasi kwamba sijuia kabisa kuwa huyo ndugu wa karibu ni nani,…..’akatulia akiomyesha hisia za huzuni.

‘Nilikuja kugundua kwua huyu ndugu wa karibu ni yule hasimu wangu toka utotoni, ….huyu ndugu wangu wa karibu, yangu utotoni hatuivani,maana kila akiona nina kitu, ataninyang’anya,na kusnisingizia uongo, kwahiyo sikuwa napatana naye , ila pacha mwenzake kidogo tulikuwa hatugombani, na hali hiyo ilibakai hadi tulipokuwa wasichana.

‘Hebu tuambie hapo mlikuwa mnakutana vipi wakati wao walikuwa wakiishi Kenya, na wewe ulikuwa unaishi huko kijijini kwenu Tanzania…?’ akaulizwa.

‘Kijijini kwetu Tanzania nilikuwa nikienda kwa msimu,lakini maisha yetu mengi yalikuwa ni Kenya, hawa mapacha walipoletwa kuishi Kenya mimi niliwapokea, kwasababu kiumri nawapita kidogo, na mimi nilikuwa nikipenda watoto, basi licha ya kuwa mimi bado mtoto, lakini niliwaona wao ni watoto zaidi, nikakua nao kwa karibu sana, kama dada yao…..

Tatizo, au mgongano ulikuja baadaye, hasa waliporejeshwa huko Ulaya walipokuja tena wakiwa wakubwa , maana walikuwa wakija mara kwa mara, sas ile nyodo ya kuishi Ulaya, ikawa inanikera, kwanini wenzangu wao wanaishi Ulaya, na kila hatua wivu ukawa unanikera,.. hadi tulipofika ukubwani, moyoni kwangu nilikuwa sina amani…kwanini kwanini zilikuwa nyingi kwangu,…

‘Kazi niliyokuwa nikifanya ya unesi kwenye hospitali moja, huko Kenya. Ikaleta migogoro, nikaona nikajaribu bahat yangu Tanzania, na wazazi wangu wakawasiliana na Mjomba, mjomba akaniunganishia kwa watu anaowajua, na kwa vile mke wa wakili mkuu yupo huku akaambiwa kuwa ninakuja huko kwahiyo nitakuwa ninaishi kwake.

‘Nilikuwa sina jinsi maana kuishi nyumba moja na mpnezi wa zamani ,mpenzi aliniyenihini, ilikuwa ni kazi kubwa sana. Na sikukaa kwao muda mrefu nikawa nimetafuta chumba sshemu nyingine, nikawa nafika kuwasalamia tu,….

‘Ina maana ulipofika hapo hukupata muda wa kuongea na rafiki yako huyo wa zamani?’ akaulizwa.

‘Niliongea naye, huyu jamaa msikieni tu, ni muongo namba moja, nashangaa kwa nini anafanay kazi ya uwakili, au kwa vile aliniona mimi ni mjinga sijui, maana nilipokuja kwako, muda mwingi tulikuwa tunakutana,….siunajau tena mkewe anakuwa hospitalini.basi aankuja kunibemebeleza kuwa nisahau hayo yaliyotokea, kwani ilikuwa ni bahati mbaya, yeye bado ananipenda…

‘Kwahiyo mkawa wapenzi wa siri….?’

‘Mimi kwangu sikuona kuwa ni wapenzi wa siri, mimi ndiye mpenzi wake wa asili, ..na ukichanganay na uwongo wake, nikawa anye mara kwa mara, na hata nilipohamia kweney chumba changu akawa anakuja huko, nilijaribu kumzuia, lakini jamaa hakukubali, na akaja kuniambia kuwa hawapatani na mkewe,kwahiyo niwe nampa kampani.

‘Hukuona kuwa hilo ni kosa, maana huyo ni mume wa mtu , tena mume wa ndugiu wako wa karibu, halafu manafnya mapenzi ya siri,…..?’akaulizwa.

‘Kwani mimi nilimuita,…. Sijawahi kumuita, hata mara moja, aseme yeye mwenyewe, ukweli wake kama niliwahi kumuita aje kwangu, yeye mwenyewe alikuwa akijileta,….kila akipigana na mkewe anakuja kwangu, kama kiota cha kumfariji,….kuna siku anakuja na majeraha, mimi ndiye nahangaika kumtibia ili asije akaadhirika huko kazini kwake, na kuna wakati mwingine anakuja kalewa hajitambui, mimi nafanya kazi ya ziada.Nilifanya hivyo tu kwasababau ni mtu ninayemepnda, viunginevyo,….

‘Je kwanini hukumwambia mkewe?’ akaulizwa.

‘Kwakeli ilifikia hatua nilitaka kufanya hivyo, nilitaka nimwambie mkewe kama kamshindwa basi amrudishe kwa mwenyewe, …., nilichofanya ni kumkataza huyu mwanaume asike kwangu, na alipokuja nikawa sifungu mlango, kumbe kufanya hivyo ndio niliharibu, nikamshau mbaya wangu, kuwa alikuwa pembeni kama fisi akiutafuta huo mwanya, kwani jamaa huyu, kwanza aliaanzisha urafiki na machangudoa, na ndipo akakutana na huyo Kimwana,….

Kwakeli nilijuta kwanini nililifanya hivyo, ..kumfungia nje, maana hata baaada ya kumbembeleza kuwa nilikosa kufanya hivyo, lakini hakunijali tena, ….akawa anajirusha na huyo Kimwana.

‘Wewe Kimwana ulimjuanaje?’

‘Kimwana nilimjua hata kabla ….kuna siku alikuja kwangu akanikuta nipo na huyo jamaa, wakili mkuu, na alivyomwangalia kwa lile jicho nikagundua kuwa huyu dada keshampenda huyo jamaa, na jamaa yangu kwa vile ni kiwembe, akavutika..nilijua hapo hapo, lakini kwa muda ule, sikujali sana, maana mimi huyo sio mume  wangu na yeye pia sio mume wake, chuki ya nini, nakumbuka alikuja hata kuniimbia huo wimbo siku nilipokwenda kumkanya, kuwa anachofanya sio sahihi….

‘Walipozoeana sana,nikaona lazima nifananye jambo, ndipo nikakutana na Sokoti.Sokoti, alikuwa rafiki yangu wa kazi za hapa na pale maana unajua tena kazi ya unesi unalipwa pesa kidogo, na nilikuwa nahitaji pesa, za kulipia kodi na maisha yangu niliyoyazoea.

‘Kazi gani za hapa na pale…?’ akaulizwa.

‘Mimi kwa siri,bado nilikuwa nafanya akzi za upelelezi wa kujitegemea, kama kuna mtu anataka nichunguze jambo , ananipa hiyo kazi namfanyia, Napata malipo yangu,…ni kazi nzuri, ila ni yamsimu , na kazi nyingi nilikuwa nikipata kutoka kwa huyo Sokoti.

‘Yeye alikuwa akikupa akzi gani?.

‘Mara nyingi zilikuwa kazi za wanandoa,…ingawaje nafanya akzi yoyote inahitaji upepelezi, lakini kutoka kwa huyu jamaa Sokoti kazi zake nyingi zilihusiana na maswala ya ndoa….

‘Kwahiyo alipokupa kazi ya kumchunguza mumewakili mkuuu ilikuwaje,maana unamjau vyema na wewe ni mmoja wa mpenzi wake wa siri…

‘Tuliongea hilo na Sokoti, lakini sikumwambia kuwa mimi ni mmoja wa wapenzi wa mume wa huyo mke wa siri, akasema ninachotakiwa nikumchunguza zaidi huyu mwanaume,  kuna mengi tunahitaji kutoka kwake, ….’

‘Mengi kama yapi?’.

‘Mengi kama hayo, ya kuhakikisha kuwa tuna muweka mkononi,…kwasababu yupo kwenye ngazi za kisheria, tukimweka mikononi tutamvunja nguvu, na akaja kuniambia kuhusu kazi aliyopewa na mke wa wakili mkuu, na mimi nikaambiwa kazi yangu ni kupata habari zote, za wateja wetu na wahasimu wake, kwahiyo kwenye hilo kundi nikawa mkuu wa upelelezi, …na kazi hiyo ikawa ni kazi iliyoweza kuniingizia pesa ambazo sikutarajia, na pia ndipo nikapata mwanya wa kulipiza kisasi kwa mhasimu wangu,mtu aliyenisaliti,…

‘Nani uliyweza kulipiza kisasi kwake, mke wa wakili mkuu, au wakili ,mkuu mwenyewe, au Kimwana?’ akaulizwa.

‘Kwa mke wa wakili mkuu, sikuwa na kisasi anye sana, kwani nilikuwa nahitaji nini tena kwake,kama ni mumewe, kwake ilikuwa ni jina tu , `mume’ na nikiwa na shida naye anajileta mwenyewe,…mumewe ndiye nilikuwa na kisasi naye, kwasababu ndiye aliyenidanganya, kanidanganya akaoa mke  mwingine na sasa kaanzisha mahusiano na Kimwana,…kwahiyo nilikuwa na kisasi naye, na …..’hapo akatulia.

‘Na nani mwingine uliyekuwa na kisasi naye…?’ akaulizwa.

Off course, ni Kimwana, yeye alikuwa kanichefua hasa kutokana na kauli yake ambayo alikuwa akinibwatukia,kila ninapokutana naye,..na cha ajabu yeye hakuninyang’anya tu huyo mke wa mtu, lakini hata nilipimpata mwingine na mwingine,…naye pia alikuwa akimtaka,….na aliyeniuma sana  ni jamaa mmoja ambaye nilimpenda sana, licha ya kuwa yeye alikuwa hajui, ….nikawa na mpango nimpate hata ikibidi anioe ili nitulia…

Jamaa huyu nilipomuona tu mara ya kwanza, nilivutiwa naye sana,nikajaribu kila njia kumpata, lakini haikuwa rahisi na mwenzangu alipogundua tu, akamuwahi, hata kabla sijapaat muda wa kuongea naye,  halafu akaja kunitangazia kuwa huyu niliyekuwa nikimtaka  keshampata yeyemiminilie tu,  kwasababu yeye  ni mrembo,na anajua kukipata kila anachokitaka mimi kwake yeye ni mtoto mdogo sana katika maswala ya kimapenzi, nikaona sasa huyu ananitafuta ubaya, …kwanini ananitafuta kiasi hicho, hanijui mimi ehe…ngoja, ..

‘Je huyo jamaa uliwahi kuongea naye, kuwa unampenda na yeye akakubali hivyo…?’ akaulizwa.

‘Niliongea naye akija kutibiwa, lakini naona hakuhisi kuwa nimemtamanai, na nilijaribu kujibaraguza kwake, lakini nilimuona yupo mbali kimawazo, ….nikawa natafuta njia ya kimshawishi, …lakini sikuwa namfahamu sana, nilichofanya ni kumwambia Kimwana, kuwa kuna mvulanammoja nimempenda sijui kama anamfahamu,

‘Kwahiyo ina maana kwa namna moja,mlikuwa marafiki na Kimwana?’

‘Kimwana na mimi tulikuwa marafiki wa hivi hivi, kukutana na kuongea, tuseme mwanzoni alikuwa rafiki yangu, licha ya haya yote, na watu wengi wanajua hivyo, kwahiyo wakati mwingine tunakutana tunaongea, na kuhadithiana, na kuanza kutambiana nani idi kuhusu hiki au kile, …tulikuwa kama Simba na Yanga….na huwezi amini kuna muda tunakuwa tumeshibana sana, na kuna muda ni kama paka na chui…

Nilipomwambia kuhusu huyo mvulana,akaniambia atanisaidia kunitafutia , na kweli haikuchukua muda akaja kuniambia keshamjua kuwa ni nani,..’

‘Sasa niambie wapi anaishi, na je ana mke?’ nikamuuliza.

‘Wewe unajali nini, kama ana mke, ni mkewe, yeye ni yeye, kwani unamtaka mkewe au yeye, kama huwezi hiyo kazi niachie mimi….’akasema.

‘Usinione mimi wa kuja nimeshajua kuwa umemtamani, mimi kazi ya kumchunguza kuwa yeye ni nani na anaishi wapi sishindwi kuifanya, ila wakati mwingine nalinda heshima yangu, na kwa vile umeshanichukulia huyu jamaa mwingine, nataka ujue kuwa huyo ndiye atachukua nafasi yake, kwahiyo tusiingiliane,…..’nikamwambia.


‘Yeye siku hiyo hatukubishana sana na walahakuniambia kitu zaidi, ila nilipokutana naye siku nyingine, akaniambia kuwa huyo mwanaume keshaenda kijijini kwao na keshaoa,…ila yeye atahakikisha kuwa anampata kwa hali yoyote ile, hata kama keshaoa,  na wote wawili anawajua , anamjua mke na mume vyema kuliko wanavyojijua wao…ooh,nikavunjika nguvu,sikujua kuwa huyo mwanaume keshaoa, na halafu Kimwana anatarajia kuivunja hiyo ndoa.

‘Kwahiyo wewe ulikuwa hujui kuwa bosi wako Sokoti, kafanya mpango na Kimwana kwa ajili ya kuipata nyumba?’akaulizwa.

‘Hilo nilikuja kuambiwa baadaye sana, na mpango wa huo wa nyumba ulikuwa wa kikundi kizima, tulitakiwa tuufanyie kazi, lakini mwenzetu alipofanikiwa akatugeuka,…..kwa kuhusu mapenzi na yeye, sikutaka tena, maaan ni mume wa mtu, na hata niliposikia kuwa  kesharudi hapa Dar, sikuwa na haja tena naye, ila kazi niliyopewa ni hiyo ya kuhakikisha tunafanikiwa kuipata hiyi nyumba….’akasema.

‘Kwani hiyo nyumba ilikuwa na nini cha zaidi?’ akaulizwa.

‘Mpango huo wa nyumba, anaujua zaidi Sokoti, nahisi ni kwa ajili ya kuweka mitambo yake, n anis sehemu nzuri ya biashara,…..zaidi aanjua yeye’akasema na kutulia.

‘Kwahiyo wewe kuhusu Msomali, uliachia ngazi?’ akaulizwa.

‘Kwakweli mimi nina utaratibu wangu,msione kuwa nimemganda sana wakili mkuu, mkazania kwua ninapenda kutembea na waume za watu, mimi ninajiheshimu, ila ni wakili mkuu, alikuwa mpenzi wangu wa siku nyingi, …..’akasema.

‘Kama ni hivyo kwanini uendelee kuwa na uadui na Kimwana?’ akaulizwa.

‘Mimi na Kimwana tutaendelea kuwa madui mpaka mwisho,maana yeye aliahidi mbele yangu kuwa kila mwanaume nitakaye mpata ataninyang’anay, huwezi amini kuwa hata hiyo nyumba aliyojenga mpya, nilikuwa nimepewa mimi mwanzoni, ikiwa inaanza kujengwa, na Kimwana akaja kuipita kinamna ambayo wala sijui ilikuwaje,….’akasema

‘Kwa vipi?’akaulizwa.

‘Ile nyumba na eneo lake lilikuwa la tajiri mmoja,  tajiri huyo aalikuwa kutibiwa siku moja, nikamsaidia sana, kipindi hicho, na alipopona, akahidi kuwa atakuja kunitafutia zawadi, basi siku moja nikakutana naye, akanionyesha hiyo nyumba ikiwa katika ujenzi wa wali kabisa, mimi kwa vilenapenda kumringia Kimwana nikaenda kumwambi kuhusu hilo,kama rafiki yangu …’akatulia kwa muda.

‘Ilikuwa ni kosa, maana wiki haikupita, nilimuona Kimwana akijirusha na huyo mwanaume, kwa muda huo sikujali nakajua hiyo ni tabia ya Kimwana, kwasababuu sikuwa na mpango na huyo jamaa wa kimapenzi, nikaoana kwangu mimi haijalishi sana.

Ukapita mwezi, nilipokwenda kuangalai ile nyumba na kiwanja, nikakuta nyumba imeshafikia juu, na nilipouliza nikaambiwa kuwa ni kazi ya Kimwana. Nikaenda kumuona yule tajiri, nikaambiwa yupo Ulaya, nikatafuta mawasiliano naye, akaniambai kuwa Kimwana kamfanyia kitu kibaya sana, ndio maana kampa yeye hiyo nyumba, ili aije akamuumbua….

‘Je kwanini mkawa katika ushindani wakati wanaume wapo wengi, kwanini mkawa mnagombea wanaume..hamuonai kuwa hiyo ni aibu kwa wanawake, tene warembo kama nyie na kwanini msiongee yaishe…?’ akaulizwa

‘Nilikuja kumwambia wazi wazi kuwa yeye anachezea moto, uliofunikwa na majivu,..yeye hanijui kuwa ni mimi nani,….hutaamini mwanamke yule alikuwa na kejeli na kiburi,alikuwa hajali, aliniambia kuwa yeye hajali kuwa mimi ni nani, kwani hata wakuu wa usalama wanamnyenyekea sembuse mimi kijike kisicho na hadhi..aah, nikaoan lazima bile bifu naye, …ndio hivyo tu…’alisema huyu nesi akionyesha uso wa dharau.

‘Kwahiyo visasi na chuki ni katika ushindani wa kimapenzi kuna jingina lazaidi hadi kufikia hatua hiyo mliyokuwa mumefikia?’ akaulizwa

‘Wewe hujawahi kuwa karibu na Kimwana…..’akasema na kutulia

‘Kwa vipi hebu tueleze wewe uliywahi kuwa karibu nay eye….’akaambiwa

‘Kauli zake, kejeri, na tabia ya kuchukulia wenzake kile unachokipata,… ilionyesha wazi kuwa hanitakiii mema, sio waume tu,hata wa kimaendeleo,kanifanyia mengi mabaya..kuonyesha kuwa etu haniogopi, hata pale alipoambiwakuwa katika kazi yetu hiyo mimi ni bosi wake, yeye akasema hana bosi katikalolote lile.

 Kwa tabia hiyo, tukaanza kumuwinda…yeye alipogundua kuwa namuwinda akaniambia ama zangu ama zake, keshajua kuwa simtakii mema,..mimi nikamwambia kajipalia mkaa, mambo bado ndio yanaanza…., kwanza nilianza kukusanya machafu yake yote, na kila mwanaume anayekutana naye, anaishia kuzalilika, yeye anashangaa kesho yake mapicha yapo hadharani,..na huyu mwanaume wake anageuka kuwa adui yake. ….maana anajua kuwa Kimwana ndiye kapangaiwe hivyo,kumbe sio…..

 Nilihakikisha hakipati hicho anachokitaka , kama alivyonifanyia mimi, na kama akikipata, hakipati kwa raha….`skendo’ zikawa zinamuandama….na wanaume wote aliokuja kuwa mrafiki naye, wakamuona kama nyoka… Hilo lilikuwa pia ni moja ya kazi zetu na Sokoti, kwani Sokoti naye alishamchoka,….lakini hata hivyo, mimi mwenyewe nilikuwa na yangu.  Nikawa napata pesa nyingi kivyangu, lakini kwa nia ya kumkomesha KImwana.

‘Mbona hapo siwaelewi,  mimi najua Kimwana alikuwa kundi moja na Sokoti, na wewe kama ulikuwa kundi moja na Sokoti, ina maana wewe na Kimwana mlikuwa kundi moja, au sio?’ akaulizwa.

‘Mwanzoni kabisa, Kimwana alikuwa hajui kuwa tupo kundi moja, mimi nilikuwa najua Kimwana yupo kwenye kundi, na hakujua nini kinaendelea , maana mimi ndiye mkuu wa upepelezi, na ili jambp lifanyikelazima nilifanyie kazi mimi,…nilikuwa nastahili hadhi yangu namalipo makubwa, lakini hutaamini Kimwana, alikuwa yeye anadai zaidi, na alisema yeye ndiye kila kitu kwenye kundi, na Sokoti akawa anamtizama tu…akasema huku akitabasamu kwa dharau.

`Umesema kulikuwa na mwanaume mwingine uliyempenda,  na Kimwana akakuwahi huyo mwanaume ni nani?’

Nesi akanyamaza kidogo halafu akasema kwa sauti ya nguvu, ‘Wapo wengi, lakini ambaye nilimpenda halafua nikaambiwa kaoa huko kijijini kwao anaitwa Msomali,…’

‘Msomali huyu huyu…?’akaulizwa.

‘Ndio huyu huyu,…huyu mnayemuona hapa mahakamani, lakini alikuwa hajui hilo…’

‘Kwahiyo kuwindanakwenu kulikuwa na malengo gani, kunyang’anyana au zaidi ya hapo, ….maana unasema mliambina ama zako ama zake, hii ilikuwa na maana gani?’ akaulizwa.

‘Kwa vyovyote vile, …kunyang’anyana,kuumbuana,..kuwindanakwakila hali….’akanyamaza
‘kwahiyo hu mpango ulijulikana katika kundi,nikiwa namaanakuwa hata Sokoto alijua hilo?’akaulizwa.

‘Yeye alijua hilo kuwa huyo Kimwana sasa ni adui wa kundi, na kama tukimuachia atakuja kusema kila kitu, kwahiyo nilipewa kazi ya kutafuta njia ay kumziba mdomo,….’

‘Kumzina mdomo kwavipi?’akaulizwa.

‘Kwa vyovvyote vile, lakini cha muhimu asiweze kuongea lolote….’akasema.

‘Hata kumuua….?’ Akaulizwa.

‘Kwani ,nini maana ya kumziba mdomo,kwa mtu kama Kimwana,..hivi nyinyi mnafikiri mngeliweza kumziba mdomo Kimwana kirahisi,rahisi kwa kumfanyoa vitimbwi tu …mtu ambaye aliamua kufanya maasi,kuaharibu ndoa za watu,kuchonganisha watu, kuibia watu kiujanja,….huyu mtu mnamuonaje nyie,….mimi sioni njia nyingine ya kumziba mdomo mtu kama huyu, ….’

‘Kwahiyo ukaamua kumuua?’akaulizwa.

‘Sio rahisi hivyo…..wakili mwanadada…jaribu tena …’Nesi akasema na kucheka.

NB Ngoja niishie hapa maana naona kama mwisho mwisho unakaribia, swali ni je huyu anaweza kuwa ndiye muuaji, hebu rudi nyuma kidogo, uangalie sifa za muuaji, je anazo, kumbuka wakatu maujai yanafanyika huyu nesi aliachwa hospitalini...ua, tukumbushane maana hata mimi husahau

Kuna watu wanasema naandika kwa urefu sana wanataka kwa ufupi zaidi, je mnasemaje kuhusu hilo, niwe nafupisha ziaidi?

WAZO LA LEO:Ubaya hauna kwao, yoyote yule anaweza akawa mbaya au mwema. 


Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Salaam kaka, yaani leo ndio imenoga hasa kwa kuwa umeandika kwa urefu. Hao wanaotaka uandike kwa ufupi nafikiri hawajui riwaya maana yake ni nini. Wewe ni mwandishi wa riwaya na si mwandishi wa taarifa za habari!

emuthree said...

Riwaya ni kazi andishi ya fasihi ambayo kwa kawaida ni ndefu zaidi kuliko hadithi fupi.

Urefu wa riwaya, maana yake ni kwamba msuko simulizi umejengeka vizuri, kuna wahusika wengi, inaenea muda mrefu, na mada zake ni nzito na pana kiasi.

Mifano mizuri ya riwaya kwa lugha ya Kiswahili ni Nagona au Mzingile, riwaya za mwandishi Euphrase Kezilahabi. (imetoka: http://sw.wikipedia.org/wiki/Riwaya)

Anonymous said...

Ole wako utuletee viduchu, hapa ni riwaya zilizoshiba!

Yasinta Ngonyani said...

Mambo yanazidi kukolea hapa...kazi nzuri mie naona si ndefu kutisha Tatizo ni kwamba waTz hatujafunzwa tangu utotoni kusoma vitabu...Pamoja daima!!

emuthree said...

Nawashukuruni kwa kunipa moyo kuwa kumbe nikifanyacho nipo sahihi, hata kama wengine wamekubali kimiya kimiya sio mbaya, na kuna wengine wamenipigiasimu kuniambia kuwa nipo sahihi, yote ni heri.
Nitajitahidi kufanya lile ninaloweza, licha ya kushindwa kuchapisha vitabu, lakini ipo siku.
Tupo pamoja daima.