Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, July 2, 2012

Hujafa hujaumbika-61 hitimisho -19



Hakimu akasema;

‘Mimi naona tumsikilize kwanza rafiki yako, maana nimeyasiliza mazungumzo yako mengi umekuwa ukimuongelea huyo rafiki yako, na nilitarajia kuwa wakili angekusimamisha kuwa uongelee mambo yako, lakini nimeona labda ina sababu fulani, …..lakini kwa vile mwenyewe yupo hapa, mimi ninaona ingelikuwa ni bora yeye akaongea kwanza kabla hatujafika huko unapotakiwa uongee, …au unaonaje wakili …?’ akauliza muheshimiwa hakimu.

‘Muheshimiwa hakimu, ….lengo letu ni kila mmoja aongeee kikomo cha yale anayohusika nayo,ndio maana hatukutaka kumkatisha, ni kweli seehmu kubwa amekuwa akimuongelea rafiki yake, hii ni kwasababu seehmu kubwa tunayoihitaji, ni ile ambayo yeye na rafiki yake walihusika,….mengne meng yanayomuhusu huyu muongeaji tumeshayasikia toka kwa mzungmzaji wa kwanza na wa pili, 

Hata hivyo sio mbaya,tukimsimamisha rafiki yake akaongea kuhusu yale yanayomuhusu, kabla hatujafikia sehamu hiyo muhimu…’akasema wakili mwanadada na kumgeukia rafiki wa mke wa wakili mkuu, ambaye alionekana kuwa mbali kimawazo.

‘Ni zamu yako kukisikia …’’akasema na alipogundua kuwa huyo mwanadada yupo mbali kimawazo aakmsogelea na kumshika bega.

‘Unaweza kuongea yale ambayo mwenzako kayaacha , naona sehmu kubwa inayokuhusu wewe imeshaongelewa, hebu tuanze kwa wewe kutuambia mlijuana vipi na Kimwanaau ulimjuaje Kimwana?’ akamuuliza.

Yule mwanadada akainuka pale alipokuwa kakaa na kuanza kwenda mbele, na wakati anapita pela nilipokuwa nimekaa akaniangalia , halafu akatabasamu,…Nilijiuliza sana akilini , mbona huyu mwanadada anakua kama vile namfahamu.

Kabla hajaanza kuongea, simu yangu ikaashiria kuwa kuna ujumbe wa maneno, nilipoaangalia nikagundua kuwa ni mmoja wa jamaa zangu ambaye niliahidiana naye kuniletea mzigo,na ujumbe ulisema kuwa mzigo umeshafika kwahiyo nahitajika bandarini haraka….ooh, nilishikwa na butwaa, maana sikupenda kabisa kumkosa huyu mwanadada akiongea, …..lakini huo ujumbe ni moja ya maisha yangu ya baadaye, nikainuka na kumuonyeseha ishara wakili mwanadada, akaja karibu yangu;

‘Vipi kuna nini,…?’akaniuliza,nikamuonyeshea ule ujumbe, maana nilishmafahamisha kuwa nina biashara nimeianzisha na yeye mwenyewe akacnagia kiasi fulani cha mtaji.

‘Oooh, ina bidi uondoke, maana huo mzigo ni muhimu na ukichelewa utakuta faini kubwa, mimi nitakuhadithia nini kimeendelea, kamautafanikiwa kuutoa haraka ,rudi hapa huenda ukakuta bado tunaendelea,….’akasema na kunishika mkono.

‘Usijali ….’nami nikamwangalia yule mwanadada akiwa anaendelea kujieleza, huku natembea kutoka nje, kwahiyo yale mengi aliyoeleza mwanzaoni nilisimuliwa na wakili mwanadada. Na wakati natoka yule mwanadada alikuwa katizama mbele , ya washiriki,hakuniona nikitoka…..

                              *****
‘Nilifika hapa Dar na wazazi wangu  kutoka Kenya. Wazazi wangu waliamua kufanya hivyo, baaada ya kuona kuwa biashara kule Kenya haiwaendei vyema,wakaona kuwa ni bora kubadili mazingira, na kuja hapa Dar, na kwa vile wazazi wangu walikuwa an ndugu zao hapa, haikuwa vigumu kwao, walichofanay ni kuwasilina na ndugu zao mapema, kabla hawajafika hapa.

Mimi nilipata kazi moja kwa moja kwenye moja ya hospitali hapa Dar, na muda mwingi nilikuwa nautumia kujisomea, …sikupendelea sana marafiki au kujumuika na makundi, nikawa kama mpweke fulani na hata wanaume waliojaribu kuniongelesha walinikuta sina maongezi nao.

‘Mawazo mengi yalikuwa yakiniandama mara kwa mara, na waakti mwingine, ilibidi niwe nakunywa dawa  za usingizi.

‘Ulikuwa unawaza nini?’ akaulizwa.

‘Historia yangu ni ndefu, inaanzia utotoni, na huko haina haja kuwaelezea hapa kwa sasa,naona ni mamb yangu binafsi, ila ninachoweza kusema hapa ni kuwa, akili yangu ilikuwa ikimuwaza mtu niliyotokea kumpenda, ….’akasema na kugeuka kunagalia pale alipokuwa kakaa mtoto wa Msomali, akashangaa kuona ile sehemu ipo wazi.

‘Mtu huyo tuliahidiana naye toka utotoni,hadi …..naweza kusema ni utoto, lakini akili yangu toka sasa inaona kuwa lile tendo lililotokea pale ni la halali, na moyo, akili na mwili ukawa unaamini hivyo kuwa tendo lile ni haki yangu, na sikutakiwa kuwa na mume mwingine zaidi yake…’akasema.

‘Tendo gani hilo?’ akauliza hakimu.

‘Tendo la ndoa…..’akasema na watu wengine wakaguna.

‘Kila mtu ninayemuhadithia kuhusu hilo anatokea kunicheka na kuniona sina akili, lakini kama mtua ngeliingia kilini mwangu akanichambau angeligundua kuwa mwili wangu wote ulikuwa umamshiba huyo jamaa…na niliona kuwa kweli huy ndiye mwenzangu katika maisha.

‘Hata mimi mwenyewe kuna muda najilaumu nakusema kuwa huenda kuna kasoro kichwani mwangu, maanamichezo ya kitoto ni utoto tu, ikishapita umri huo huwezii kutazamia kuwa yale yanaweza kuwa kweli,lakini mimi tendo lile nililina kama kweli na katika umri wangu wote toka siku ile niliojiona kam make wa mtu.

‘Fikiria tokautoto, hadi usichana ,hadi umri kama huu, bado namuwaza mtu huyo huyo, na abadaye uanjikuta yeye hana habari nay eye, yeye yupo na watu wengine, halafu unasikia kabisa kuwa keshaoa,….kwakweli niliteseka sana,…..na hali kam hiyo ilipokuwa ikijinia akilini nakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa…

Nilipofika hapa Dar na wazazi wangu , wao walinishauri kuwa niachene kabisa na hayo mawazo , hata kama nitamuona huyo jamaa nihakikishe kuwa siongei naye, maana ninaweza kuchanganyikiwa, kama keshaona, ni nini natarajia, ….nivunjendoa ya watu, hapana, ni bora kuishi bila yeye, ingawaje moyo unaumia. Hata hivyo sikuwezakuvumilia, kwani nilianza uchunguzi wa kumtafuta yule aliyekuwa akiutesa moyo wangu.

‘Nilikuwa najua toka siku nyingi kuwa mtu huyo yupo hapa Dar, lakini sikuwahi kuwasiliana naye …ningeliwasilina naye vipi wakati nilijua hana habari ni mimi. Na mbaya zaidi ni aple niliposikia  kuwa keshaoa binti wa huko kijijini, lakini hata hivyo nilikuwa na nia ya kumuona tu, ili tu nijue yupoje, na nijue kwanini kaamua kunifanya hivyo.

Nilijua kuwa akiniona hataweza kunikumbuka kwa haraka, maana sura yangu ilibadilika sana, hata ndugu zangu wa huko kijijini ambao nilikuwa nijakutana nao muda mrefu, walishanisahau,…labda ni kutokana na hali ya hewa,…sijui, ilamimi nilijiona kama kawaida tu.

 Nikawa kila mara nikipita muda nazunguka sehemu mbali mbali hadi siku moja nikafika kwenye jengo moja, ambalo nilisikia  ni maarufu kama sehemu ambayo wakina dada waliwekeza kwa ajili ya kujiuza kwa wanume, na hapo hukutana na wanaume wenye pesa, na kuwahadaa, ndivyo nilivyosikia lakini sikuwa na uhakika na hilo.

Nilipofika hapo moyo wangu ulikaribia kupasuka,…..nilimuona mtu ambaye  nilikuwa nazani ndio yeye, mtu huyo alikuwa kasimama mlangoni mwa ile nyumba na baadaye akaingia ndani, kwanza moyo wangu ulikuwa ukihakiki kuwa ndio yeye au la, na kw aupande mwingine ukawa unamshuku kuwa huyu mtu kumbe ana tabia hiyo ya kutembea na hawa akina dada,ambao jamii ilikuwa ikiwaona kuwa wanafanya mambo mabaya.

Nikasubiri kwa muda, na alipotoka nilihakikisha kuwa ndio yeye, kwakweli niliumia sana , nikajiuliza ina maana huyu mtu ndio kaharibika kiasi hicho, nikaahidi kumtafuta ili nijue ni kwanini kawa hivyo, na nilitamani niwasiliane na wazazi wake, maana kama wangelijua hili sizani kama wangemvumilia kwa jinsi ninavyojua familia yao ilivyo. Nikaona ni vyema kwanza nihakikishe hilo kabla sijawasilina nao.

‘Lakini nakumbuka niliambiwa kuwa huyo jamaa keshaoa, binti wa kijijini, sasa imekuwaje,….’nikajiuliza sana hilo swali bila jibu, na nilijua njia njema ni kukutana na huyo jamaa, lakini haikuwa rahisi kiasi hicho. Na nikakata tamaa kabisa.

Siki kadhaa nikapata habari toka kwa mtu anayemfahamu kuwa keshaoa msichana mmojawapo wa hawa wanaoendesha hiyo biashara ambayo jamii haikubaliani, nayo, sikuamini, na siku hiyo nilikuwa kaam mtu aliyechanganyikiwa. Sijui kwanini nilikuwa hivyo maana baada ya yote hayo nilitakiwa kuachana na huyu mtu, na kuamua moja,lakini ilishindikana.

Basi siku zikaenda na mara nikakutana na huyu mke wa wakili mkuu,kipindi hicho nilishaamua kutokuhangaiak tena, na nishaamua kuwa mimi sitaki wanaume, au kuolewa na mtu yoyote.Kila mwanaume aliyenijaribu kuniomba niwe rafiki yake, nilikuwa kama mbogo, na kutokana na hali hii wengi walifikiri nimechanganyikiwa.

Siku fulani nilikutana na huyu jamaa, kwakweli sikutaka hata kumuona, na sijui ilikuwa ni kitu gani, maana nilimuona kama shetani fulani hivi, nikamkimbia,….’hapo wakili akamsimamisha na kumuuliza swali.

‘Ulimuonaje huyo mtu kama shetani,…?’

‘Nilimuona hana sura ya kawaida, na kama ana mtu mwingine nyuma yake…lakini nilikuja kujua kuwa ni ile chuki iliyokuwa imejijenga akilini.

‘Je uliwahi kukutana na huyo jamaa mara nyingine, au ilikuwa hiyo mara moja, na ukamkimbia?’ akaulizwa.

‘Kukutana naye uso kwa uso ni mara moja tu, sehemu nyingine nilikuwa nikimuona kwa mbali, na nilijaribu kila uwezo wangu kuwa mbali kabisa na yeye, …

‘Je uliwahi kufungwa , kushikiliwa na polisi kwasababu zinazohusina na huyo mtu au jambo jingine?’akaulizwa.

‘Hapana, mimi sijawahi na kama nilivyokuambia baadaya hilo tukioo la kukutana naye na kumkimbia sikuwahi kuwa naye karibu tena…’akasema.

‘Je uliwahi kuumizwa kwa risasi au kupata jeraha kama hilo, kutokana na  yeye?’akaulizwa.

‘Hapana ,sijawahi, ….ndio nilikuwa na upendo wa dhati na huyo mtu, lakini nilishafikia sehemu nikaamua basi sio huyo mungu eliyenipangia, na hata pale niliposikia kuwa kamuacha mke wake wakijijini na kuoa mke mwingine,…nikaamua kuachana naye….’akasema.

‘Haya hebu tuambie ilikuwaje mpaka ukawa mmoja wa walimu wa kufundisha hawo wasichana?’ akaulizwa.

‘Siku moja nilisikia kuwa yupo jamaa ambaye ni mtaalamu wa kusaidia watu walioathirika kimawazo kama yangu, maana kwa ujumla nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, nilijaribu sana kujizua bila mafanikio ,sijui ni kitu gani kilikuwa kimewekwa akilini mwangu, ….niliwahi kusaidiwa na madakitari bingwa lakini haikusaidia kitu,….basi nikaoan ngoja njaribu kumuona huyo jamaa huenda akanisaidia.

Nilipokutana naye na kumhadathia matatizo yangu, akanichimba undani wangu,…. kijumla niligundua kuwa ana kipaji hicho, maana alivyokuwa akinipa zile nasaha na kutambua nini kilichokuwa kikinisibu, nikajua ni mtu ambaye anayeweza kunisaidia,sikujua ana nini nyuma ya pazia…

Baadaye huyo jamaa akaniambia kuwa ili kuondokana na mawazo ya mara kwa mara ni bora niwe nafundisha shule za kuwahudumia watu wanaohitaji msaada wakindoa,… sikupenda tena kazi kama hiyo, nilikuwa nimeshatosheka na kazi yangu ya udakitari.Nilikuwa nikijiuliza,kama mimi mwenyewe nimeshindwa kujisaidia nitawezaje kuwasaidia wenzangu.

Huyu jamaa alinipa moyo akasema kuwa mimi nina kipaji hicho na pia nina utaalamu wakuosmea,sio vyema kuupoteza hazina hiyo hivihivi tu, ni bora niwasaidie wengine ili nipate ujasiri wa kupambana na matatizo ya kimaisha. Na pia inaweza kunisaidia kugundua mengi katika maisha ya watu na mhusiano yao. Nikaona ni jambo jema, kwahiyo nikaamua kufanya hivyo ,kama sehemu ya kuniondolea mawazo,na kweli nilipojaribu tu,nikawa na hamasa kama ile niliyokuwa nayo huko Kenya.

‘Je ulipokutana na Kimwana kama mmoja wa wanafunzi wako,na kugundu ndiye alikuchukulia mpendwa wako ilikuwaje?’

‘Kitu cha kwanza ambacho niliona ni cha ajabu kwenye hiyo shule ni pale nilipopewa masharti , nivae vipi, niwe vipi. Niliambuwa kuwa mwalimu wa hiyo shule, alitakiwa asijulikane sura yake, nikaelekezwa jinsi gani ya kuvaa, na kuwa nihakikishe kabisa wanafunzi hawanitambui hata mara moja, kwasababu ninaweza kushindwa kuwasaidia , na mimi nilikubaliana na hilo maana sikutaka hata kazini kwangu wajue kuwa nafanya hiyo kazi ya ziada,….

‘Kimwana nilimgundua hapo hapo,...sikuwa namjua sana kabla ya hapo, nilikuwa nasikia jina lake tu watu wakimuongelea. Na sikujua mwanzoni kuwa ni mpenzi wa huyo jamaa ninyemtafuta, nilimuona kama mwanafunzi ambaye ni mwepesi kujua mambo, mcheshi muelekevu,…nikawakaribu naye sana, na hata hivyo, ilionekana kuwa huyo mwalimu aliyekuwepo hapo mwanzoni alikuwa naye karibu, maana maongezi yangu na yeye yalikuwa yakiashiria kuwa ananijua sana.

Nilimdadisi sana kuhusu maisha yake, na nilikuja kugundua kuwa anatokea huko kijijini kwetu,na nilipowauliza wazazi wangu kuhusu huyo Kimwana, walisema hamjui, lakini watajaribu kutafuta wapi anatokea, baadaye walikuja kuniambia kuwa nisiwe na urafiki naye, wanasema familia yao haina muelekeo mwema , na hata huyo msichana mwenye inasemekana alitorokahuko kwao….

‘Nilipogundua hilo nikaona nilitafutie uhakika wake, na kweli nillipomdadisi sana huyu mwanadada akanifunulia maisha yake ya toka utotoni, …..nilichoka.

‘Sasa hivi nimempata bwege mmoja, ana nyumba,…..anatokea huko huko kijijini kwetu,….huyo jamaa ana sura nzuri, anavutia, lakini hana pesa sana, kamuoa binti mmoja toka huko kijijini, binti mwenyewe namfahamu,….mshamba wa kutupwa, hajui mapenzi, ….mapenzi kwake ni kazi za nyumbani, kuwajibika kama punda, lakini nini amfanyie mumewe hajui….sasa mtu kama huyo utamsaidiaje…’akaniambai siku moja.

‘Kwani kakuomba umsaidia kama kakuomba,mshauri aje hapa, ndio watejawe hawo, mlete hapa shuleni. Sisi tutajua jinsi gani ya kumfundisha…’nikamshauri.

‘Eti nini,nimlete hapa, ili afunguke , ….hapana aliyelala usimwamshe, ukimwamsha, ooh, huyo mwache kama alivyo, nilisoma naye, ana katabia ka uzamani,…hapendi mabadiliko, sasa nimeona ni bora nimuingize mjini ….ninachotaka ni kumpata mumewe, …ile nyumba ni nzuri sana, ….ukiiona mwenyewe utaamini maneno yangu,  na ipo sehemu nzuri ya biashara, ukiipata, na baaadaye unaweza ukaiuza kwa hela nyingi sana,…mimi naona mbali , sio hapa….’akasema.

‘Mimi kama mwalimu wako nakushauri kabisa uachane na waume za watu, hebu fikiria kama wewe ungelifanyiwa hivyo ungelifurahi….’nikamwambia.

‘Mimi nilishakuambia toka siku nyingi, hapa nimekuja kusoma, maisha yangu ya mitaani sitaki mtu ayaingilie,…nimekumabia hili tu kwasababu umeniuliza, vinginevyo nisingelikuamabi kwasababu hayakuhusu..’akasema kwa ukali na kuondoka zake.

Baada ya siku kadhaa tukawa hatuongei sana kuhusu maisha yake, lakini siku moja tukajikuta tukiongelea maswala hay o hayo, akaniambia sasa hivi keshafanikiwa kumpata huyo anayemuita bwege wa kijijini, na ndoa ya huyo jamaa imeshvunjika,….

‘Mungu wangu umefanya nini…’nikasema kwa huzuni.

‘Wewe unajali nini, kwani ni mume wako….wajinga ndio waliwao, ..mjini hapa, kama mke kashindwa kuwajibika, nani wa kulaumiwa, huyo mwaume kajileta mwenyewe, sikutumia nguvu, ni yale yale mahaba …mvuto, na ule mkao wangu wa siku ile , aliponiona kwa mara ya kwanza ….siunajua tena….sasa nifanye nini…mungu akupe nini,..kwahiyo mimi nimekuja kwako kukuambia tu, kuwa kuanzia leo, nitapunguza siku za kuja hapa darasani, maana natarajia kuwa mke wa mtu…

‘Ina maana mumeshapanga kufunga ndoa tayari….?’nikamuuliza

‘Sasa,.. ndoa imeshapangwa ,na hilo ndilo lengo langu, hiyo ni hatua ya kwanza, kitakachofuata ni urithi, nyumba lazima iandikwe kwa jina langu, baadaye jamaa hana lake, namfukuzilia mbali….kwanza sasa hina kazi,namlisha mimi….na atabakia hivyo hivyo, baba wa nyumbani….’akasema huku akijiandaa kuondoka.

‘Mimi ni mwalimu wako, na itakuwa ni mtu wa ajabu nikikiufundisha ubaya, hayo unayoyafanya sio mambo mazuri…hebu niambie ni nani huyo mwanaume?’nikamuuliza.

‘Ni bwege mmoja wa huko kijijini,….eti wamekosa majina mpaka wanajiita majina ya nchi nyingine…’akasema kwa dharau.

‘Jina gani hilo…?’ nikamuuliza.

‘Anaitwa Msomali……wengi wanamuita mtoto wa Msomali…’

‘Eti nani….?’nikasema na kujikuta nikipepesuka…….kiza kikatanda usoni, na kupoteza fahamu.

NB: Usipende kumwamini kila rafiki, na ukawa unaongea matatizo yako kwa kila mtu…hasa matatizo ya ndani ya ndoa. Huwezi jua ni nani adui yako, maana siri ya kila mtu ipo moyoni mwake, inawezekana kabisa rafiki yako wa karibu akawa ndiye adui yako…


Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

2 comments :

Anonymous said...

Kazi nzuri ujumbe mzuri, kaka keep it up, na tunga kitabu,mbona kazi zako nzuri sana

Anonymous said...

Tatizo weye unakatizia patamu!