Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, June 29, 2012

Hujafa hujaumbika-60 hitimisho-18




Mara ghafla akasimama wakili mwanadada, na kusema;

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, kabla mke wa wakili hajaendelea na maelezo yake, naomba nimuulize maswali machache, na kama inawezekana nitoe baadhi ya vifaa ambavyo ni muhimu katika maelezo hayo…’akasema na hakimu akamwangalia kwa muda, …halafu akasema;

‘Vifaa gani wakili, maana hapa tunachosikiliza ni maelezo kwanza, hayo mengine ,tutaangalia kuwa kama kesi ipo basi vitu vyote vya ushahidi vitawakilishwa mbele ya mahakama….?’ Akauliza hakimu.

‘Ndugu muheshimiwa hakimu,licha yakuwa hapa tunasikiliza maelezo ya awali kwa ajili ya kesi hii ambayo imekuwa na utata, lakini pia ni vyema nikawakilisha hivi vithibiti ambavyo vitaweza kutumika kama ushahidi , kesi ikifika mahakamani….’akasema wakili mwanadada, na kupitisha macho yake kwa haraka kwa wote waliofika hapo.

‘Nasema kesi ikifika mahakamani ,maana inavyoonyesha ,wengi wataishia kukana kuwa hawakuhusika na haya mauaji, na lengo letu lilikuwa jema tu, kuwa muuaji,mshirika na yoyote yule aliyehusika azungumze ukweli ,akiri kosa na ikibidi tuone jinsi gani tutamsaidia….lakini jinsi tunavyokwenda naona inaweza wengine wakaficha ukweli, …kwahiyo mimi nimeona tutoe huo ushahidi hapa ili mwenyewe aone kuwa kweli tunajua nini kilichofanyika…..’akasema

Hakimu alitulia kwa muda, halafu amwangalia wakili mwanadada, alitaka kusema jambo, lakini akasita, akamgeukiwa mkuu, na baadaye akasimama na kusogea mbele akasema;

‘Hebu nawaomba wakili mwanadada na mkuu mje hapa mbele ….’akasema muheshimiwa hakimu. Na wakili na mkuu wakasogea pale mbele aliposimama muheshimiwa hakimu na kuanza kuteta, na baadaye hakimu akarudi kwenye sehemu yake aliyokuwa kakaa mwanzoni.

********
Watu wote mle ndani walikuwa kimiya baada ya mke wa wakili kuongea kwa muda, na alikuwa akisubiri maswali, na kabla hakimu hajaruhusu hayo maswali aliwaita kwanza mkuu na wakili mwanadada akateta nao, na walipomaliza kuteta, ndipo akaruhusu maswali kwa mke wa wakili mkuu.

Wakili mkuu ambaye alikuwa katahayari kwa maelezo ya mke wake, alikuwa muda mwingi kainama huku akitingisha kichwa, ilionekana wazi kuwa ana dukuduku fulani, ambalo kila mmoja wetu mle ndani alikuwa nalo maana muheshimiwa hakimu alikatisha sehemu ambayo kila mmoja alitaka kujua ni nini kiliendelea baadaya hapo, ….

Mimi mara kwa mara nilikuwa nikijiiba na kumtizama yule mwanadada, rafiki wa mke wa wakli mkuu, na nilimuona yule mwanadada akionekana kuwa na mawazo mengi, tofauti na awali alipokuwa anatabasamu, na hakuwa akinitupia kicha tena, alikuwa anaangaliai chini au kumwangalia rafiki yake akiongea…..nikahisi kuna jambo…

‘Najua wengi mna hamu sana ya kutaka kujua nini kitafuta na wengi naona mna dukuduku kwa vile nimemkatisha huyo mzungumzaji wetu, lakini mjue mimi ni msikilizaji , na anayeendesha haya maelezo ni wakili mwanadada na mkuu, nia na lengo lao ni kuhakikisha kuwa kesi hii haitaleta migogoro tena.

‘Niwaambie kiukweli, kesi nyingi sasa zimekuwa na migogoro mingi, na kupigwa tarehe, kwasaabbu zinaletwa kwetu bila kuwa na ushahidi wa kutosha, na hili sio jambo jema, kwani unaweza ukamtesa mtu kwa kumweka mahabusu kumbe hana hata kosa…na pia minong’ono mingi inakuaj kuzagaa kuwa kuna lolote limetendeka ili mwisho wa siku mtuhumiwa aachiwe huru….sisi siolengoletu hilo….

Sasa hili wenzetu hawa wameliona na wakaona ni vyema tukawa na haya maelezo ya mwanzo, na kama kesi ipo wazi basi tutaipeleka mahakamani na kama bado, inabidi wao wajipange vyema,….’akamgeukiwa wakili mwanadada.

‘Haya uliza hayo maswali…maana na muda unakwenda kasi..!’akasema huku akiangalia saa yake
Wakili mwanadada akasimama na kumsogelea mke wa wakili mkuu, akamwangali kwa muda halafu aakgeuka na kurudi sehemu alipokuwa kaweka vifaa vyake, akachukua kitu, ilikuwa ni silaha iliyokuwa imewekwa ndani ya mfuko wa nailoni, akaiinua kwa makini, na kusogea nayo, akaiinua juu,…

‘Mke wa wakili mkuu, unaikumbuka hii silaha…?’akaulizwa.

‘Ninaikumbuka, sana, hiyo ni salaha ya mume wangu….’akasema

‘Unajuaje kuwa ni silaha ya mume wako wakati silaha kama hizi zipo nyingi…..’akaulizwa

‘Kwasababu ya hicho kitako chake, kimepakwa rangi ya nyekundu bluu na manjano, hizo ni alama ambazo zizani kama zipo kwenye silaha nyingine, ….’akasema.

‘Uliwahi kuona silaha kama hii kabla?’ aakulizwa.

‘Ndio, wazazi wangu wana silaha kama hiyo, wanzo mbili, wanazitumia kwa ajili ya kuwindia pia, …na walikuwa wakituundishia shabaha…’akasema.

‘Ina maana nyie mnajua kulenga shabaha? Akauliza.

‘Ndio tunajua, na katika shule ambayo wanamiliki wazazi wangu, huwa kuna mazoezi ya shabaha, na mimi na ndugu yangu na baadhi ya wanafunzi waliotaka walikuwa wakihudhuria mqzoezi hayo….’akasema.

‘Katika mazoezi hayo, uligundua nini…..?’ akaulizwa.

‘Niligundua nini…,sijaelewa swali lako muheshimiwa….’akasema

‘Katika kulenga shabaha mlikuwa wanawake watupu au na wanaume, je ni watu gani walikuwa walengaji wazuri wa shabaha?’ akaulizwa.

‘Ni wanawake,….na sisi wanafmailia tuliongoza sana katika kulenga shabaha, inaonekana familia yetu, imerithi hicho kipaji, kilichotoka kwa familia ya baba….’akasema.

‘Ina maana familia ya baba inahusisha watu gani, au una maana gani kusema hivyo, kwani mama yeye hakuwa na shabaha ukilinganisha na nyie…?’ akaulizwa.

‘Mama hakuwa an shabaha sana,ukilinganisha na sisi au na familia ya baba,familia ya baba hapo nina maana baba na ndugu zake na watoto wandugu zake.

‘Ina maana pia walikuwepo hawo familia ya baba yako, yaani watoto wa baba yko mdogo, watoto wa dada zababa yako?’ akaulizwa

‘Ndio walikuwepo, maana hapo kulikuwa na familia za ndugu wa baba, na wao walikuwa wakijumuika, na kulikuwa hakuna uabaguzu wowote…’akasema.

‘Kwahiyo uligundua kuwa familia ya baba yako ina kipaji cha shabaha, na unasema kuwa katika hiyo familia ya baba yako kulikuwa na wanaume na wanawake, na wote walijumuika, ….?’ Akauliza

‘Ndio walikuwepo?’

‘Na wote walikuwa na shabaha sana…?’ akaulizwa.

‘Ndio,hasa wanawake, ….wanawake walikuwa wakiongoza sana kwa shabaha kuliko wanaume, ingawaje kwa ujumla familia ya akina baba wana shabaha sana, na wanapenda kuwinda, naona ni asili yao….’akasema.

Wakili mwanadada akamwangalia muheshimiwa hakimu ambaye alikuwa akifuatilia hayo maswali, na hakimu akatulia akiwa anashangaa kumuona wakili mwanadada bado kashikilai ile silaha na alitaraji zaidi kuhusiana na hiyo silaha. Na wakili mwana dada akaligundua hilo na kusema;

‘Hii silaha umesema ni silaha ya mume wako, je uliwahi kuitumia kwenda kuwindia na mume wako?‘akaulizwa.

‘Mara nyini sana,ndio maana nasema naifahamu sana…..’akasema.

Wakili mwanadada akaiinua ile silaha juu, na kuiangalia kwa makini, akaishika kama vile anaipima uzito….halafua akasema;

`Muheshimiwa hakimu, nia na lengo letu ni kusikiliza maelezo ya kila mmoja, na tangu awali niliwaambia kuwa kila mmoja aseme ukweli wake wote, na hili nimelirudia mara kwa mara kuwaambia hawa washiriki hapa, ….hii silaha ni muhimu sana katika tukio hili maana ndiyo iliyotumika , na risasi yake ndiyo iliyosababisha kifo cha Kimwana.

‘Awali kulitokea sintofahamu, maana wengi tulijua kuwa risasi iliyomuua Kimwana ni ile iliyotoka kwenye bastola ya dereva na mlinzi wa Kimwana,lakini hili lilithibitishwa katika kesi iliyofikishwa mbele yako, iliyokuwa ikimkabili dereva na pia mlinzi wa Kimwanda kuhusiana na kifo cha Kimwna, kuwa siyo risasi iliyosababisha kifo cha Kimwana,…

‘Ilikuja kugundulika kuwa risasi iliyotoka kwenye silaha hii ndiyo iliyosababisha kifo cha Kimwana, ndio maana tukawa tunangaika kumsaka wakili mkuu kama mshukukiwa muhimu…..sasa ninataka ieleweke wazi kuwa tunachohitaji hapa ni ukweli,ukweli mtupu, maana ushahidi wote tunao hapa…naoba tena kila mmoja aseme ukweli, kwani ukweli ndio utakaomsaidia yeye na mwishowe tutafikia hatima ya haya matatizo....’akamwangalia muheshimiwa hakimu ambaye alionekana anataka kuongea,na wakili mwanadada akatulia kumsikiliza

‘Nakumbuka wakili mwanzoni, uliniambia kuwa wote wamekubali kuwa watasema ukweli, lakini naona kama una wasiwasi, vipi tena…..?’ akauliza hakimu.

‘Nahisi kuna wengine wanataka  kubadili mawazo, labda kutokana na ushauri potofu toka kwa watu wengine, au kwa dhana zao wenyewe, maana nimejaribu kuwapitia kila mmoja kujua kuwa bado wapo tayari kuzungumza ukweli, nikakuta kuna baadhi wanaanza kusita…..lakini kila kitu kitawekwa wazi, muheshimiwa, hakimu….’akasema wakili mwanadada. Na baadaye akamgeukiwa mke wa wakili mkuu, na huku kaishikili ile silaha.

‘Kwa mara ya mwisho uliishika hii silaha lini?’akauliza hilo swali, na wakili mkuu aliyekuwa kakaa huku kainamisha kichwa akataka kuinuka, kama vile anataka kulizuia hilo swali,alishajisahau kuwa yeye pale sio wakili tena, yupo miongoni mwa washukiwa na hakutakiwa kuongea, mpaka aruhusiwe....

Muheshimiwa hakimu akamuona na akatabasamu, lakini hakusem neno akamgeukia wakili mwandada ambaye slihauliza swali, halafu akamwangalia mke wa wakili mkuu ambaye hakuonyesha wasiwasi,akajisema;

 ‘Ni siku ile alipouliwa Kimwana……’ Wakili mwanadada akageuka na kuangalia washiriki, halafu akaguka na kumwangalia mke wa wakili mkuu,akasema;

‘Hebu tueleze ilivyokuwa…..

NB: Nilijua leo nitaandika kwa kirefu, lakini nimejikuta na majukumu yaliyopo juu ya uwezo wangu, tuwepo pamoja kwenye sehemu ijayo.

WAZO LA LEO: Wengi wetu tunapendelea kuhamaki, na kuhitimisha mambo bila ushahidi kamili, tukisikia jambo tunakimbilia kulivumisha na kuona ndivyo ilivyo, …kuna watu wanasikia waume au wake zao wanatembea nje ya ndoa, na bila ushahidi wanaamini,….mambo mengi yanatokea hapa na pale na bila ushahidi watu wanaamini,...na kuanza kunyosheana vidole

Jamani tuweni makini na matukio, uvumi na maelezo ya watu, na habari mbali mbali zinazotolewa kwenye vyombo mbali mbali vya habari. Tuamini tu pale tunapokuwa na ushihidi yakinifu, dunia hii imegubikwa na sintofahamu nyingi kwa masilahi ya watu wachache,…. ingawaje kuna usemi usemwao lisemwali lipo kamahalipo laja….

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Nilisngaa mara 68, ooh, sasa umejishitukia, tunakwenda pamoja mkuu

Yasinta Ngonyani said...

Pamoja sana ndugu yangu. Nimelipenda wazo la leo ni ukweli haswa. Ahsante

emuthree said...

Ndugu `Anony' wa hapo mwanzo kabisa, nakushukuru sana kama uliliona hilo kosa,...tupo pamoja.

Ndugu wangu mpendwa Yasinta nashukuru sana kuwa nami, najua tupo sote wakati wote, ...

Kama ombi,hawa watu wanaandika bila kutaja jina lao tuwaite Anony...au vipi?

chib said...

Nilikuwa nimepotea, kwa sasa ninarudi rudi.
Nimeona blog yako ipo kwenye mchakato wa tuzo.
Nimeshakupigia kura, kila la heri

chib said...

Nilikuwa nimepotea, kwa sasa ninarudi rudi.
Nimeona blog yako ipo kwenye mchakato wa tuzo.
Nimeshakupigia kura, kila la heri

chib said...

Nilikuwa nimepotea, kwa sasa ninarudi rudi.
Nimeona blog yako ipo kwenye mchakato wa tuzo.
Nimeshakupigia kura, kila la heri