Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, June 20, 2012

Hujafa hujaumbika-54 Hitmisho-12


`Ndugu hakimu, hawa wote ni wahusika wakuu kwa kadhia hii nzima ambayo ilifikia hadi watu kupoteza uhai wao na wengine sasa wapo kitandani wameshikwa ni kiharusi. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa kuna watu wanabuni mambo kwa maslahi yao, bila kujali athari zake kwa wengine.

Tumeliona tulionglee hili hapa, kabla hatujasikia uamuzi wako, kwasababu ni jambo la kijamii, na ni vyema tukawasikiliza hawa wakosaji, ni kwanini walifikia kutenda haya waliyotenda, na tukapeana nasaha, ili mwisho wa siku kila mmoja aone ubaya wa hilo jambo, na ajirekebishe, kuliko kumpelea mtu jela, akasota huko na akitoka hajajifunza lolote.

Mimi katika utafiti wangu nimeona kuwa ni vyema taratibu kama hizi zikafuata, mkosajai ajue kosa lake akiri na ajute, na apewe nasaha,ambazo zitamsaidi kuliko kumuhukumu tu. Na pia wakosaji waanpokuwa jela,ni vyema kukawa na shule nasaha, kwa kila mmoja kutokana na kosa lake akalishwe chini ajieleze ni kwanini alifikia hatua hii.

Akimaliza kujieleza ,aelezwe madhara yake kwa mwenzake, na ni nini kwa athari kwa jamii, hili lifanywena watu waliosomea mambo hayo, na pia watu wa dini, wahusishwe kutoa mambo ya kiroho, ili yamjeneg huyu mtu, na hata akitumikia kifungo chake ajue ni halali, na akimaliza hatarejea tena.

Angalia wengi waliofungwa, wakirudi uraiani, wanajiona kama sio binadamu tena,hawajui hata waanzie wapi maisha, na hata wengine kuimba kuwa ni `ni heri tena warejee jela,..’ ni maneno ya kukata tamaa,ina maana huko jela kuliko sio chuo chamafunzo,ni sehemu ya kukomoana.

Mimi kwa mtizamo wangu tuanze kubadili mtizamo wa jela, jela iwe sehemu ya mafunzo, wakifika wahukumiwa, kwanza tujenge imani za hawa watu,kuwa kufanya kosa ni dhambi, hili lifanywe nawatu wa dini, pili tangalia makosa yao, kwanini wamefikia hapo, hawa watu wa ushauri nasaha wawepo,waangalie jinsi gani ya kumshaurii huyu mtu. Halafu kila mtu ana kipaji chake, humo vipaji viendelezwe na kazi ziendlezwe kama kawaida.

Nimegundua jela nyingi, zinakuwa ni sehemu ya kuharibu watu kisaikolojia, watu wanaingie humo wanafanyiana uchafu, wanazalilishana, wanaambukizana amgonjwa, sasa hapa tunakuwa tunafanya nini. Ndugu muheshimiwa,kuna wau wengine wamehukumumiwa hata kosa hawajafanya, ni kutokana na sababu za kujieleza, au kutegewamakosa, hawa watu wanaumia sana,na mwisho wa siku wanajiona hawana thamani katika hii dunia, tutakuja kujibu nini mbele ya muumba.

Pamoja na kusema hyo, kuna jambo jingine ni vyema tukaliangalai mapema, hasa kunapotokea jambo, kama la mauaji,au uasi wowote, imekuwa ni destruri kukimbilia kukamata, kutesa, kuweka watu ndani, na kutoa hukmu kutokana na vigezo vilivyoonekana, lakini hatuchunguzi haya makosa kiundani, hili utaliona katika kesi hii,.

Labda tuanze kwa wahusika kujieleza , na tukianzia na mkosaji , ambaye wote tulimnyoshea kidole yeye, na kutokana na akzi yake, hakustahili kufikia huko,lakini kwa udhaifu wa kibinadamua akjikuta kifanya hayo aliyoyafanya, na hili katika utafiti wangu niligndua kuwa limetokana na maswal ya kindoa, naona tisirejee naomba kwa nafasi yako muheshimiwa tumruhusu mkuu wetu wajieleze, kwani yeye ndiye anaonekana ndiye mkosaji, je kweli yeye ndiye mkosaji…

Hakimu akatulia kwanza kwa muda, akafikiri, na baadaye akauliza;

‘Kwahiyo tunakubaliana kuwa hapa tunasikiliza maelezo ya mwanzo tu, ambayo baadaye yatatusaidia katika kesi hii, mimi sikupendelea hii hali,maana ipo kinyume na utaratibu, lakini kutokana na hali ya kesi hii ilivyo, naona iwe hivyo, ili tusisumbuane tena, na kesi zenu zisizo na ushahidi wa kutosha…’akasemanakutulia.

‘Kama mnavyojua utaratibu, haya yote yalitakiwa kusikilizwa mahakamani, hapa inabidi tufanye kama utangulizi wa kujua kuwa kesi ya kujibu ipo kwa hawa watuhumiwa aua la,..ina maana tunafanya kama mashauri nje a mhakama, …..sawa maana kwa mtizamo huo alioelezea wakili mwanadada, naona inaweza ikasaidiahusuani hii kesi ambayo naona inakuwa kama mchezo wakuigiza, haya wakili wetu mkuu,tuambie, kwanini ulifikia huko ulikofikia.

Wakili mkuu ambaye muda mwingi alikuwa kainamisha kichwa chini, …..alinua kichwa chake na kuwatizama watu waliopo mle ndani, leo alikuwa kabadilika,alikuwa, kabadilika na kuonekana Yule wakili anyejulikana, mtanashati na nguo zake safi kama  wakili, akageuka na kuangalia wote waliohudhuria humo ndani, na wa mwisho kumwangalia alikuwa mke wake,pale akatulia kidogo, akayapepesa macho, halafu akasema;

‘Kabla ya yote, naomba kwanza nimuombe radhi mke wangu,kuwa nimemkosea kiasi kikubwa sana, kama hatanisamehe yeye bado hakijafanyika kitu, na mimi nitakuwa ni mtu wakuangamia tu, ….' akasimama na kwenda kupiga magoti mbele ya mkewe. Na yule mwanadada akakunja uso kwa hasira alipoona wakili mkuu akifanya lile tendo, akageukia dirishani asiwaangalia.

'Mke wangu.mimi nimekuwa mkosaji wa ndoa yangu mwenyewe,kwasababu ya tamaa zangu za kimwili, …nakuomba unisamehe  mke mke, nisamehe, kwa yote, najua umeumia sana kwa haya yaliyotokea, hata kama nitatoa sababu nyingi zilizonisukuma kufanya hivyo haitasaidia kitu,…’akamwangalia mke wake kwa macho yaliyogubikwa na machozi.

Mke wake, alimwangalia kwa muda kwa macho yaliyojaa hasira, akasema ;

'Eti nini....nikisamehe wewe...ehe, ehe....'ondoka mbele yangu akaangalia kwa mbele huku akijifanya hamuoni.

Ule moyo uliokuwa umejaa chuki, hasira na kusalitiwa katika ndoa ukawa unamcheza akilini, alitamanii kutapika maneno mabaya, lakini akasita, akamwangalia Yule mwanaume na kauli aliyotoa, akageukia nyuma, na huku akikumbuka yale aliyokuwa kadhamiria moyoni.

Alipoitwa hapo, yeye alikuja na dhamira moja tu, kuwa ndoa haina haja kwake,alishaona bora aiombe talaka yake, ajue ataishije mwenyewe,hatua hiyo ilifika hapo pale alipoona ule mkanda wa video uliokuwa kwenye chumba ambacho mume wake huwa anaweka kumbukumbu zake za siri.Na licha ya kujaraibu kuongea naye, ili ajue nini kinaendelea mume wake akawa hakubali.

 Yeye kuwa hana tabia ya kuingi ingia humo,hakuwa akipenda kuingilia maswala ya mume wake. Lakini siku moja, Yule binti anayeishi naye alikuja mbele yake akamwambia ;

‘Mama, kule ofisi kwa baba kuna mkanda ambao nahisi una jambo…’akasema.

‘Jambo gani,na umejuaje hayo,…wewe nilishakukanya kuwa huko ofisni kwa baba yako hakutakiwi kuingi- ingia, unakumbuka alivyokuwa akisema kila siku….huo mkandaumejuaje kuwa una jambo….?’akamuuliza kwa hamaki .

‘Mama…nilimuona baba akiuangalia, …nilikwenda humo kwasababu alinituma sigara….na bahati wakati naingia sikupga hdoi nikaona anauangalia, nikarudi nyuma haraka, na nikapiga hodi, akazima …nimekuamua kukuambia, kwasababu, nilitaka kukusaidia wewe, nakushauri sana ukauchukue huo mkanda uone kilichomo…’akamshauri  mama yake wa kufikia, na kweli mke huyu akavutika na kwenda kuuchukua huo mkanda wa CD, na alichoona humo, kilimvunja nguvu, hakuamini kuwa mume wake alifikia hatua hiyo,….alishindwa kuvumilia na nguvu zikamwishia na kudondoka chini.

Wakatii huo huyo binti alikuwa nje,akiosha vyombo, akahitaji sabuni, akaingia ndani, akamuita mama yake, lakini kulikua kimiya akaona amfuate huko chumbani kwake, akashituka kumuona yupo chini, kazimia, akahaha na kuanza kuita;

‘Mama…mama….mungu wangu….’yule binti akawa analia hakujua ni nini kimefanya iwe hivyo kwa ule, na akili zilipotulia akakumbuk kuwa huenda ni kwasababau ya ule mkanda aliomshauri auchukua, na wakati ule ulikuwa umefika mwisho, kwahiyo Yule bintio hakuona nini alichokuwa akiangalai huyo mama yake…, akaenda pale kwenye `DVD player' na kuangalia, kweli akauona mkanda, akautoa na kuuficha.

Baba mtu akaja kwani ilibidi huyo binti ampigie simu baba yake huyo wa kufikia, na alipokuja wakamuwahisha hospitalini na haikuchukua muda hali yake ikawa njema. Na hata alipoulizwa tatizo ni nini,hakusema kitu, alichoweza kufanya ni kumwangalia mume wake kwa jicho la chuki.Mume wake hakujua kuwa kuna nini kinaendelea na kwa vile walishakuwa hawaivani, akaona ni kawaida tu .

Na huyu mke hakukubali akaanza kulifuatili hilo swala kwa karibu sana licha ya kutoweka kwa ule mkanda ambao alitaka uwe kama ushahidi. Na alichunguza sana bila kujua nani kafanya vile, akili yake ikamshuku Sokoti kuwa huenda ndiye alitengeneza hayo, kinyume na makubaliano yao. Akamuuliza Sokoti ambaye alipinga kuwa hakupanga yale, yeye hata kama angefnay hivyo, kwanza angemuonyesha yeye.

'Mimi nilishafnya kama tulivyopanga, ....huyo atakuwa mtu mwingine...'akajitetea vikali…..na hapo akaona kuwa hilo alilokuwa kadhamiria huenda likasababisha mambo mabaya, ndipo wakati ule akamwambia Sokoti kuwa huo mpango waliokuwa wamepanga uvunjike.

Tangu siku ile chuki ikawa imemtanda akilini, na kila anapowaza ile taswira ya ile ule mkanda na yale matendo aliyoyaona kwenye ile Cd’s, yakawa yanamuandama akilini, na mbaya zaidi mume wake akawa analewa kupita kiasi, akimuuliza anakuwa mkali,.....akaona lazima afanye jambo, akaanza kumuandama Kimwana, amabye naye likuwa akimjibu kijeuri kila alipomuuliza. Ndipo akaweka nadhiri, akasema;

‘Lazima nitafute mbinu za kummaliza huyu mwanamke,halafu tunaachana na huyu mwanaume, naomba talaka yangu, na kurudi kwetu,sina haja ya mume…..sina haja tena na huyu mtu,….lakini lazima nimmalize huyu mwanamke…..’akajikuta akisema kila mara.

Akageuka kumwangalia huyu mwanaume akiwa kapiga magoti mbele yake, akiomba msamaha huku akitoa machozi, …akamwangalia kwa muda,…..nasijui kwanini…moyo wa huruma ukamtanda , na akajiskia vibaya  kwa ilechuki aliyokuwa nayo, akajikuta akilengwa lengwa na machozi huku akiyakumbuka ya nyuma, …lakini akaona haina haja, yaliyopita ni ndwele , kinachotakiwa ni kuganga yajayo, ingawaje hajui hatima ya yote, lakini ni vyema akakiri kuwa keshamsamehe, akasema;

‘Mimi nimeshakusamehe leo na kesho ahera, lakini  …’akataka kusema jambo,nahakimu akaingilia kati na kusema;

‘Mambo mengine utakuja kuongea zamu yako ikifika, cha muhimu hapa ni wewe, je umeshamsamehe kwanza, , ….’akasema muheshimiwa hakimu.

‘Mimi nimeshamamehe, ila tu ninachohitaji…...’kabla hajaongea wakili mwanadada akamtuliza, akijua nini anataka kusema.

‘Wewe tulia tu kwanza, usiwe na papara,…..msikilize muheshimiwa hakimu ….’

‘Endela kuongea wakili mkuu, mtuhumiwa…maana wewe hapa ndiye mtuhumiwa mkuu, tunataka tulione hilo, kuwa je unastahili kutuhumiwa,…au la…su sio?’ akamgeukiwa wakili mwanadada.
Wakili mwanadada akatingisha kichwa kukubali, hakusema neno, na kumgeukiwa wakili mkuu, ambaye aliaanza kuongea kwasauti ya unyonge;

‘Mimi kutokana na tamaa zangu nilijikuta nikiwa na mahusiano ya nje ya ndoa,hili kwangu nililiona kama ni sehemu ya sifa ya mwanaume, licha ya elimu yangu, ….nilikuwa na nyumba ndogo, niliona kama vilekupata chakula tofauti na kile nilichokizoea, hasa ninapofika kwa mke wangu akasema kuwa kachoka au hajisikii, basi hapo nilipata kisingizio. Ni kweli mke wangu alikuwa anachoka kutokana na kazi zao, lakini hilo sikulielewa.

‘Wenzetu wajanja wakaligundua hilo wakatumia uzaifu wangu, wakatutegea wasichana,na kutuchukua picha mbaya, ambazo walinitishia nazo kuwa nisipotekeleza matakwa yao watanizalilisha,kwakweli nilipoona zile kanda za video niliogopa sana, nikijua kabisa zikifika kwa bosi wangu, muajiri wangu, kazi sina, na pia nitazalilika hasa kwa mke wangu na jamii kwa ujumla….

Mtu pekee niliyemuamini tangu awali ni huyu mwandada sijui kwanini. Kwa ufupi yeye alikuwa ndiye mpenzi wangu wa awali kabla sijamuoa mke wangu...na ana udugu na mke wangu. ....Cha ajabu ni kuwa yeye nimekuwa nikumwamini sana kuliko hata mke wangu,...sijui kwanini, maana kila nikiwa nimetatika na jambo, huwa nakwenda kwakwe kupata ushauri, na yeye amekuwa mtu wangu  wa karibu, kuliko hata mke wangu,maana mke wangu muda mwingi yupo kazini….na maswala kama haya nisingeliweza kwenda kumuomba yeye ushauri…ningesemaje…

Nilipopatwa na haya matatizo, sikuwa na mtu mwingine wa kumwamini,mwanzoni nilitulia sikumweleza yoyote, nikajaribu kulimaliza kimiya kimiya,lakini hawa watu walipozidi kunifuta tena, ndipo maji yakanifika shingoni, sikuwa na pesa walizohitaji, nikawa kama nimechanganyikiwa na kutumbukia kwenye kunya pombe kupita kiasi, na hali ilivyokuwa huyu mwanadada akanigundua, na baada ya kunishawishi sana ni kamwambia hali ilivyo.

‘Hivi kweli wewe unamwamini mkeo?’ akaniuliza.

‘Kwanini unasema hivyo,?’ nikamuuliza.

‘Mimi nahisi kuwa huenda ni mkeo anakufanyia hivyo, unakumbuka awali nilikuambia kuwa mkeo anakutana na jamaa mmoja,ambaye wengi wanamtambua kama mtaalamu wa maswala ya mapenzi…’akaniambia.

‘Sasa hayo yanahusiana vipi na hizi picha chafu?’ nikamuuliza.

‘Anaweza akawa kashauriwa hivyo….yule mwanaume simwamini, …na nilishakuambia kuwa mkeo hakufai…wewe hunisikii,…angalia sasa mwaka wa ngapi hamna watoto…umeniacha mimi, sasa unaona….’akaniambia huyu mwanadada, na Yule mwanadada akamwanagalia kwa mshangao,nafikirihakutarajia hayo.

‘Basi naomba ujaribu kunifuatulia hilo,kama ni yeye anafungamana na haya mambo ,itakuwa ndio mwisho wake wakuishi na mimi…na ….aah, hayo tuyaache kwanza…’nikamwambia.

‘Alifutailia lakini hakuona ukweli wa hilo, ni wakati huo hawa jamaa wakazidi kunisakama, na chaajabu kila ninachopanga, wanakijua, ….na mtu pekee aliyekuwa akiyajua hayo ninayopanga ni huyu mwanadada, ….nilijaribu kumbana kama anaweza kuwa ndiye anayetoa taarifa zangu, lakini niligundua kuwa sio yeye, nikahisi kuwa kuna jambo jingine…

Niliamua kufanya mambo yangu menginebilakumuhusisha, lakini kila nililofanya bado wakawa wanajua na kutoa vitisho vya kila namna,hapo sasa mawazo msongo na hali ilivyokuwa ikanifanya nipatwe na huo mshituko, uliosababisha hali yangu kuwa tete…

‘Nilipoona mambo yanazidi kuwa mabaya, nikanona nitumie njia ambayo ni ya hatari,niliona ni bora kuwamaliza hawa watu mmojabaadaya mwingine, nilijaribu kutafuta ni nani yupo nyuma ya haya yote, ikawa vigumu, basi nikaona bora nianze na hawa akina dada ambao walishiriki na mimi hadi mikanda hiyo mibaya ikatolewa, maana wao watakuwa wanajua, licha ya kuwa kila nilipowahoji, walisema wao hawajui lolote kuhusiana na hiyo mikanda..

Kutokana na hali yangu kuwa mbaya ,nikaona nitafute msaada, na hakunamwingine niliyemuamini, nikamtumia huyu mwenzangu….nikamuomba anisaidie…’akasema na Yule mwanadada akasema kwa hasira;

‘Hivi wewe vipi, ina maana umeamua kunisaliti, ndivyo tulivyokubaliana hivyo, ina maana unataka kuniingiza kwenye mambo yako….’akasema kwa sauti ya hasira, na wakili mwanadada akamkatisha kwa kuuliza swali;

‘Akusaidie kwa vipi?’

Mkuu wa wakili akamtizama Yule mwanadada ambaye alikuwa bado akamuangalai kwa hasira akasogeza mkono kutaka kumshika, lakini Yule mwanadada akarudi nyuma, kwa hasira na kuukwepa ule mkono, ilionyesha wazi hakutaka kabisa kuhusishwa au hakutarajia kuwa wakili mkuu angafikia hapo. Wakili mkuu akaendelea kuongea;

‘Siku hiyo nilikuwa nimetundukiwa madripu ya dawa,lakini ilikuwa kama ushahidi wa kuficha hayo niliyokuwa nimekusudia kuyafanya. Ndio nilikuwa anumwa, lakini kwa muda haikuhitajika dawa ya namna hiyo,  nikamuomba anipe dawa itakayonipa nguvu,niweze kuinuka hapo na kwenda kummaliza mwanadada mmoja ambaye niliona ndiye yupo karibu na hawo watu ingawaje hakutaka kuniambia….
‘Mwanadada yupi huyo…?’ akauliza muheshimiwa hakimu
‘Wote mnamjua , haina haja ya kumtaja kwa sasa…’akasema.

‘Ni vyema ukamtaja, kwani tunataka kuweka haya mambo sawa…’akasema  muheshimwa Hakimu.

‘Ni mwanadada Kimwana….’akasema nakutulia,na wote mle ndani wakageukiana, lakini wakili mwanadada alikuwa katulia kimiya akisikiliza yale mazungumzo,

‘Mnaona nilishawaambia kuwa ndio yeye aliye muua Kimwana mkawa mnanibishiamnoana sasa kakubali mwenyewe….’akasema Mkuu.

‘Sijasema kuwa nimemuua mimi, sikumuua mimi, …..hilo nawaambia ukweli….’akasema mkuu wa wakili huku akionyesh akwakidole…

‘Aaah,….unapinga tena…’akasema mkuu kwa kuhamaki na Muheshimiwa hakimu akamtulia mkuu, kwa mkono, kuwa aache mwenzake aendelee kuelezea.

NB; Kumbe bado mambo yapo, nilijua leo tunamalizia, tuonane sehemu ijayo ya hitimisho la kisa hiki.

WAZO LA LEO: Urafiki wa kweli hauna msimu, na pendo la zati hutoka moyoni, nadhahiri yake ni matendo mema. Mpende akupendaye,asiyekupenda,.... kama ni mumeo au mkeo, jitahidi akupende kwa kujiuliza huyo anayempenda ana nini cha zaidi ambacho wewe huna.

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Duuh, kila ninayemfikiria kuwa ndiye muuaji anachomoa, hapo tunakuachia wewe mkuu. Tupo pamoja, kura yangu ipo, na kama wanaruhusu,nikakupigia mara mia..

Anonymous said...

Τhe write-uρ has established helpful to us.

It’s very іnformative and you're certainly extremely educated in this region. You have opened up my eyes in order to various views on this particular topic together with intriguing, notable and solid written content.

Feel free to visit my page ... buy viagra

Anonymous said...

Thank you for sharing your info. I really appreciate your efforts
and I will be waiting for your next post thanks once again.


Feel free to visit my blog ... debtconsolidationinsider.com