Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, June 14, 2012

Hujafa hujaumbika-52 hitimisho-10



Tukiwa katika maongezi yetu, tukiwaa tumemgeukia  muongeaji mkuu ambaye alikuwa wakili mwanadada,mara mlango ukagongwa, na wote tukageuka kuangalia ni nani aliyegonga, maana mimi mwenyewe nilimsikia mkuu akitoa amri kuwa asisumbuliwe na mtu yoyote, kwasababu yupo kwenye maongezi muhimu. Akageukia kule mlangoni na kusema kwahasira;

‘Nani wewe, ….?’ Akauliza mkuu kwa sauti.

‘Mkuu kuna dharura,….’sauti ya askari ikasema, na hapo mkuu, akajua kuna jambo, akainuka haraka nakufungua mlango, na tukasikia sauti ya mkuu ikiguna, kukawa na mazungumzo huko nje,ambayo hatukuweza kuyasikia na mara mlango  ukafunguliwa, akaingia mkuu, na kusema;

‘Haya yule mtu wetu muhimu tuliyekuwa tukimtafuta kajileta mwenyewe,…ingawaje hali aliyo nayo, intisha tuvumilie hivyo hivyo…’ akageuka mlangoni nakuangalia ,na sisi macho yetu yakawa yanaangalia kwa hamu kumuona huyo aliyetambulikana kama `mtu muhimu’

Harufu ya pombe kali ilianza kusikika, na ….mara akaingia jamaa akiwa kachafuka kweli, anatoa harufu ya pombe, kama vile alimwagiwa mwili mzima, akasogea, huku anayumba yumba, na kukaa kwenye kiti kilichokuwa wazi, na hata kukaa kwake alikaa upande upande ,ilionyesha kabisa kuwa hana nguvu, ..ama kutokana na ulevi aliokuwa nao,au hajala,au anaumwa…au vyote.

‘Mkuu kwanza naomba maji baridiiii….’akasema huyo jamaa huku akiwa kama kafumba macho, macho yalionekana mazito kuyafumbua,…akawa kama anayalazimisha.

‘Maji yatapita kwei hapo, maana inaoena kama hujala ,…kwanini unajitesa hivyo, ..kwanza angalai ulivyo, huoni hali kamahiyo nikutazalilisha sisi…na kitengo kizima cha sheria…’akalalamika mkuu.

‘Kula sitaki, chakula changu sasa ni pombe….nitakunywa hadi kieleweke, maana sioni umuhimu wa kuishi tena, kuwaabisha, sijaabisha mtu, tatizo lenu hamjui nini kinachoendelea....kuna watu hawanitakii mema,lakini kaba sijafa nimeamua kuwamalizawote waionifanya hivi….’akajiangalia huku akiyumba kwenye kiti

‘Hivi…hivi wewe mkuu  unanionaje, unafikiri napenda hii hali, ukiona hivi ujue, maji yamezidi unga,…mwanaume, tena mkwe kaingia choo cha kike na kumkukuta mama mkwe wake…..’akasema huku akijaribu kukaa vyema kwenye kiti.

‘Mwanaume mzima naonekana hivi,zalili….nazalilika mwenzenu, eti… kwasababu ya...eti kwasababu ya kijike,…mwanamke…hapana, tutafikishana mbali…mmmh, sasa mkuu maji utanipa au hunipi mkuu au ndio nimeshaanza kifungo,….bado, hafungwi mtu hapa….kesi itasimama, na waliofanya haya yote, ama wawe hai au mfu, watasimama kizimbani, mimi ni mwanaume bwana,wazazi wangu wanajua kuwa walizaa dume….’akasema huku akipiga kifuani.

‘Mmmmh, ngoja nimalizie hii,…haya maji ya uhai….hii ndio chai kule kwetu, lakini ndio hivyo, kule inaitwa gongo, lakini wenzetu, wameifnaya hivi, …na kuuita wiski…hii ni chpa ya mwisho, basii….’mara akatoa chupa ya pombe, aliyokuwa kaweka mfukoni na kunywa.

Kila mmoja alikuwa kaduwaa, na hakuna hata mmoja ambaye moyo wake hakuingiwa na simanzi, huwezi amini. Mtu ambaye siku kazaa nyuma, alikuwa na afya yake, mtanashati, na mwenye hadhi, leo hii anaonekana kama mtu aliyetindikiwa na ubongo,…kweli hujafa hujaumbika.

Mkuu aliinuka na kuchukua gilasi ya maji na kumpa huyoo jamaa, akaipokea huku mikono ikitetemeka, akaiangalia kwanza na halafu akainua kichwa, akatuangalia mmoja baadaya mwingine, akatikisa kichwa, hakusema kitu, akainua ile gilasi akawa kama anaongea kitu, au kuomba, akainua kichwa tena na kutuangalia kwa muda,…machozi yakaanza kumtoka.

‘Mungu wangu nisamehe…..najua jinsi gani nilivyokukosea,….sijui nini kiliiningia hadi yakanifikahaya yote, sijui….naomba kwa nguvuu ya haya maji, unipe ujasiri niweze kuitenda haki, niweze kuwafikisha wote walionifanyia hivi mbele ya mahakama,….ndugu muheshimiwa, nataka kukutambulisha jambo…kuwa mhusika mkuu wa haya yote, nimeshammaliza, ….’akainua maji na kuanza kunywa.

‘Tulimwangalia kwa makini, akiyanywa yale maji, na mara mlango ukagongwa tena, na mkuu hakusemaneno akainuka na kuufungua mlango, akaingia dada mmoja,……wote tukageuka kumwangalia na Yule dada akatuangalia kwa mashaka huku akiwa kashika kichwa kwa aibu, alipomuona yule jamaa alivyo. Ilionekana wanajuana, lakini hakupenda ile hali aliyomuona huyo jamaa, lakini akajifanya hajali, akamsogelea yule jamaa na kukaa karibu yake. Yule jamaa aliinua uso na kumwangalia, akasema;

‘Umefika mpenzi,…ahsante sana kwa kutimiza ahadi yako, na mimi nimetimiza ahadi yangu kama tulivyopanga, nakuomba unyoshe mikono juu, maana hapa upo chini ya usalama, upo chini ya nini, ya usalama, kwa utambulisho tu,mmh, ngoja nikutambulishe wahusika humu ndani….’akajaribu kuinuka, lakini hakuweza, akarudi  kukaa,na kaunza kucheka…alicheka hadi akadondoka kwenye kile kiti.
Yule mwanadada akamfuta pale chini na kumsaidia kumuinua,…na Yule mwanadada akasema kwa uchungu;

‘Yeye tangu afike kwangu ndio hivii hivi, kunywa pombe tu, hataki kula, hajijali, namimi sina muda wa kumuogesha kama mtoto mdogo,hataki hata kubadili nguo, nimembeleza sana, ajitoe kwa polisi hataki,….lakini ikafika muda nikasema basi liwalo naliwe,ikabidi nivunje ahadi yangu, kuwa nitamlinda hadii mwisho nikamwambia kama hataki kujitoa, mimi nitakwenda kuwaita polis waje wenyewe….’akasema Yule mwanadada.

‘Tulia, usianze kuongea wewe,..mimi ndiye wakili wako nitaongea, mwenyewe…usijitie matatani kwa jambo ambalo nimelisababisha mimi mwenyewe, kwasababu ya huyo jamaa anayejiona ana akii sana....sasa wewe tulia…’akawa anaongea huyo jamaa kilevi levi.

‘Lakini kwa hali kama hiyo naona sio wakati muafaka ,ngoja tuangalie afuya yako kwanza….’akasema mkuu.

‘Wewe unajau nini kuhusu afya yangu, usicheze na muda, hapa naweza kukata kamba, nikafa, mtajua wapi ukweli wa haya yote, simtabakia kuwafunga watu wasiohusika, mimi najua kila kitu, mimi nilijua yote yaliyokuwa yanakuja juu yangu, na aliyesabibisha haya yote….lakini kila jambo lina mwisho wake,…niliyempenda naye hanipendi..sasa ningelifanyaje, na Yule, …..aliyeninisaliti awali, akapata jaza yake,hatunaye tena….nitamfuata huko huko…..’akataka kuanguka kwenye kiti.

‘Mimi nashauri kwanza tumfikishe huyu mtu hospitalini akapate, matababu, hali aliyo nayo sio nzuri, alipoteza fahamu masaa mengi, nikahangaika naye sana, na alipozindukana akaja na wazo hilo la kuja hapa, akidai kuwa anataka kuwafahamisha ukweli,kwani anaona kifoo kinamjia….’akasema Yule mwanadada.

‘Tatizo lako unajitia kimbelembele…wewe hujui sheri,utajiweka kitanzi mwenyewe….shauri lako ngoja mimi niongee mwenyewe, sitakufa mpaka nimalize  kazi yangu, kwanza mkuu waambie vijana wako wakamchukue huyo jamaa ndani ya gari, asije akafa kabla hamjajua nini …unasikia mkuu, haraka, sio swala lakufikiria…’akasema namkuu kweli akaamrisha vijana wake wakaangalie kwenye gari kuna nini.

‘Mkuu, kuna jamaa, sijui kamayupo hai, kafungwa pingu, na kamba kwenye gari, anavuja damu….’akasema huyo askari.

‘Waite watu wa huduma , wamshughulike, kwani ni nani huyo….?’akauliza mkuu huku akimwangalia Yule jamaa.

‘Mhusika mkuu wa hii kesi,..huyo ndiye chanzo cha haya yote….aje mbele yenu akiri mwenyewe…maana keshakubali, hana ujanja tena,…hana mbele wala nyuma, wenzake wamemkimbia, hana pesa, hana nini…..’akasema.

‘Mbona wanasema hali yake ni mbaya..’akasema mkuu.

‘Hali yake ni mbaya ndio, ni njaa….lakini hata hivyo haijawa mbaya bado, nione mimi hapa, nina hali nzuri…mimi ni kama yeye tu, na alijifanya kichwa maji ndio maana akawa vile, angekuwa mtiifu, yasingelimfika hayo yaliyomfika,sikuwa na jinsi, nikamfinya kidogo,akaropoka yote…hii hapa kanda niliyomrekodi kama mnataka kuiskiliza, na kama hataki kuongea ,au..kama kafa, lakini ushahidi huu hapa….’akatoa CD’S  nakumkabidhi mkuu.

‘Ila nataka mke wangu, na rafiki yake mpendwa wafike hapa,…nataka hili swala liishe  leo hii hii, na ukweli uwe wazi, na….hata nikifa nijue naenda kutulia,sio kwenda kuteseka,….unaweza kufanya hilo mkuu, au nikalifanye mwenyewe….?’akaninuka huku akipepesuka.

‘Hebu tulio hapo kwanza, tulia hapo kwenye kiti, hali uliyo nayo sio nzuri…’akasema Yule mwanadada.

‘Unajua hali nzuri wewe,tatizo lako unanipenda sana,lakini mimi kuna mtu nampenda zaidi, kwanza mke wangu, lakini….mapenzi yaipungua,..macho yakaona mwingine…mmh….lakini nitafanyaje, nafsi imeumbwa kupenda vizuri, baadaye…., nimependa …mwingine, mmh,kweli huyo, hata kama ni kuoa mke mwingine nitamuoa yeye, na wewe pia, nataka wake hawa…’akaonyesha kwa vidole vitatu huku akimshika yue mwanadada.

‘Sawa, lakini hayo yote yanahitaji afya yako kwanza…’akasema huyo mwanadada.

‘Umekubali sio, …basi kwanza aje mke wangu wa kwanza,…akikubali, na akikubali huyo rafiki yake, tukafunga ndoa, aaah, mimi tena, nitatulia nyumbani kimiya, nataka nini tena,…lakini huyo rafiki yake, hanitaki,….anasema ana mtu wake,…mtu wake gani huyo, nikimuuliza ni nani hamtaji….’akainama kama vila kichwa kimekuwa kizito, akainua kichwa na kumwangalia mkuu.

‘Mkuu, nimekuambia nawataka hapa, mke wangu, narafiki yake,waje hapa tuyamalize…na huyo mfu keshapona…?’akageuza kichwa kuangalia nje.

‘Mfu gani huyo….?’akauliza mkuu.

‘Huyo muhusika mkuu,huyo ndiye aliyejifanya anajua sana, eti ana akili …akawapagawisha hawa akina dada, na…na kutaka kutuzalilisha, ..mkuu unakumbuka ile kanda ya Cd,uliyoichukua kipindi kileee…huyo ndiye muhusika, mleteni hapa….hata kama ni maiti yake, nataka iongee…hajafa huyo, nimemfinya kidogo tu, tatizo ni kuwa hajala,ana njaa…mpeni chakula.’akasema huku akiinuka kwenye kiti.

Safarii hii alisimama vyema kabisa, na kugeuka kutuangalia mmoja mmoja, aliponigeukia mimii akaniangalai kwa muda, akasema.

‘Na wewe umefuata nini hapa…mkuu huyu hahusiki hapa, nataka hili swala tuliongelee kikazi, wahusika ni mimi, wewe, mke wangu, rafiki yake, huyu mwanadada, nataka awepo hapa, ili athibitishe, ni shahidi yangu muhimu….hata wewe wakili, msaidizi wangu,…wewe utakuwa wakili wangu mtetezi, au sio…hata kama hutaki sijali….lakini huyu jamaa, sijui anahitaji au vipi, lakini mmmmh,labda awe kama shahidi tu, sijui,mnamjau nyie….’akanisogelea na kunishika begani.

‘Huyu ni mtu wetu….’akasema mkuu

‘Kwani wewe ni nani….aaah, nimeshakukumbuka,ndio wewe eeh, tumeshakufunga mara mbili, samahani sana,sasa nimekukumbuka usiondoke,nataka uyasikie mwenyewe, utaona ni nani mbaya wako…’akasogea pale aliposimama wakili mwanadada.

‘Sasa unasemaje unakubali kuwa wakili wangu..nitetee rafiki yako….aah, hata kama hutaki sio mbaya, …mkuu watume vijana wako wawalete hawo watu hapa haraka tumalize haya mambo, hakuna muda wa kupoteza tena, kesi imefika penyewe, na ikibidi muite na hakimu, …na wazee wa baraza, au…nina wazo, sote twendeni mahakamani tukayamazie huko huko…’akasema huku akiyumba.

‘Mimi natoa wazo, kama unataka haya yote yafanyike, wote hawo uliowataka watachukuliwa na kusimama mbele ya mahakama, na kama unavyotaka kila kitu kitafanyika hivyo, kwanza tuhakikisha kuwa umekula, una afya,hujalewa….utasimama je mbee ya hkimu ukiwa na hai kama hiyo,….hebu fikiria kwanza….kila kitu kitafanyika kama unavyotaka, tena kisheria unasemaje…?’ akasema Yule mwanadada.

Yule jamaa alitulia kwa muda kama anawaza jambo,halafu akamwangali Yule mwanadada, akatabasamu, halafu akamgeukia mkuu akasema;

‘Mkuu unasemaje ,maana hapa nakuheshimu wewe tu….utakalosema nitalisikiliza,lakini je hiyo kesho itafika, maana nimeshamuona izraili akinichungulia,anasubiri muda, aichukue roho yangu, sasa nyie mnamwekea kiwingu,….ongeeni naye, kamatakubai kuahirisha kazi yake, sawa…..maana kaja kasema nina kesi huko mbele, Kimwana ananisubiri…’akapepesuka hadi kwenye kiti chake na kabla hajakifikia akayumba, na mara akadondoka chini ….

Yule mwanadada akamsogelea nakujaribu kumuinua,lakini haikuwa kazi rahisii akatugeukia na kusema;

‘Keshapoteza fahamu, naona huu ndio wakati muafaka tumpeleke hospitalini,maana akizindukana hapa tunaweza tukashindwa kumsadia,ni kweli ana mengi ya kuwaambia, ….lakini afya yake kwanza, amekuwa kama kachanganyikiwa….’akasema huyo mwanadada.

‘Na huyo jamaa huko nje ni nani maana sijawauliza watu wangu vyema namlimpatia wapi…?’akauliza mkuu.

‘Jamaa gani huyo?’ Yule mwanadada akauliza kwa mshangao huku akihagaika kutoa hudum ya kwanza kwa huyo jamaa aliyedondoka chini.

‘Huyo aliyekuwa kwenye gari…ambaye wanasema kazimia kwa kupoteza damu nyingi…?’ akauliza mkuu.

‘Yupi huyo mbona sielewi, unajua mimi nimekuja kivyangu,…huyu …aliondoka mapema hapo ninapokaa,…ooh,au ndioo huyo  Sokoti…..mmh, …kwakweli  sin auhakika kuwa ni nani, labda akizindukana atawaambia mwenyewe, …maana alisema anakwenda kumkamata mbaya wake….’akasema huyo mwanadada huku akimweka sawa huyo jamaa aliyedondoka chini bado akiwa kapoteza fahamu.

‘Unasema ni huyu Sokoti tunayemtafuta….!?...hebu niwauize vijana wangu,…..’Mkuu akauliza huku akiwa kashangaa akapiga simu kwa vijana wake kuulizia.

NB: Nimeona siku isipite bure, japo kwa shida, nimewaletea sehemu hiyo. Tutakuja kuhitimisha kisa hiki,inabidi kwanza nikipitie kidogo,….na kama kuna kitu nimekisahau naomba mnifahamishe,…tuweni pamoja,….shukurani kwa wale mnaokuwa pamoja nami,hata kama ni kwakimiya kimiya, sio mbaya, Tupo pamoja.

WAZO LA LEO: Zarau sio jambo jema, hata kama unacho, hata kama unajua sana, hata kama umesoma sana,...hata kama,....lakini usipende kuwazarau wenzako, kwani pamoja na hayo mpaji ni mungu, huwezi jua kuna leo na kesho, leo kwako kesho anajua mwenyewe Muumba.. Hapa nikaumbuka usemi usemao; aliyekupa wewe kiti, ndiye aliyenipa mimi kumbi, na pia mzarau mwiba guu huota tende.



Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

1 comment :

Anonymous said...

Tupo pamoja,mara nyingi tupo kimiya kimiya!