Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, June 8, 2012

Hujafa Hujaumbika-48 hitimisho-6


‘Swali kubwa mpaka kwa sasa ni nani aliyemua Kimwana? Maana nini kilichosababisha kifo inajulikana, na ni kwanini kundi kama hilo lilianzishwa tumeshaona, na kwa mtaji huo Kimwana alikuwa na maaadui wengi,….” akaanza kwa kuuliza swali hili,wakili mwanadada,na huku akituangalia sisi kama vile anatuuliza hilo swali sisi, ambao tulikuwa na swali kama hilo kichwani mwetu,tukamwangalia tukisubiri atupatiejibu. Alipoona tupo kimiya akasema;


‘Ni rahisi sana kumnyoshea mwenzako kidole, palekosa linpotkea, ni rahisi sana kuhisi kumuhisia mwenzako kuwa ni yeye pale tunapoona kuna kitu kibaya kimetokea. Lakini sisi kama wasimaizi wa sheria,,watetezi wa haki, na mawakili, ni vigumu sana kufanya hivyo,labdakama huijui kazi yako vyema…’akaniangalia mimi mtoto wa Msomali, mpaka nikahisi vibaya, halafu akamgeukiwa mkuu na kusema;

‘Mpaka sasa nashindwakuelewa hawa wenzangu waliokuja kuhisi kuwa muaji wa Kimwana ni Mkuu wetu wa upelelezi kirahisi tu, …..sina uahkika na ushahidi mlio nao,sijui kama kweli kuna ushahidi wa kimatendo, kama sio hisia tu,eti mkuu mna ushahidi ganii kuwa mkuu wetu wa kitengo cha upelelezi ndiye mnyemshuku kama muuaji…?’akatulia na kumwangalia mkuu. Mkuu hakusema kitu, alitulia kama vile hayupo.

‘Kitu ambacho nimegundua katika muda mfupi wangu wa hii kazi ya uwakili ni kuwa mara nyingi wenzangu nyie, wa idara ya polisi, na hata usalama, mnakimbilia sana kukamata watu kwa hisia tu, na hata kabla upelelezi haujakamilika kwa kisingizio cha kuisadia polisi…mimi hapo kama mtetezi kama wakili naona tunaharakisha sana….hasakwenye hii kesi yetu…’akatulia huku akikwepa kumwangalia mkuu machoni.

‘Naona wakati mwingine sio sawa, maana kwanza unamtesa mshukiwa kisaikolojia, mshukiwa ambaye ambaye labda hana kosa, lakini umemkamata kwa kisingizio cha kuisadiai polisi, haya umefanyahivyo umemuweka ndani miezi kdhaa, humo kaumia kwasaabu hizi na zile, kaumwa na mambo kama hayo, mwishowa siku unamuona hana kosa, …..jiulize utamlipaje huyu mtu….au kwa vile ni mkuki kwa ngururuwe,….’akatulia huku akiwa bado hamuangalii mkuu machoni.

Pili mimi naona wakati mwingine kama ungelivuta subira, ukafanya upelelezi wa kimiya kimiya ungeliweza kugundua mengi yaliyojificha…kamakesi hii ilivyo, na pia ungeliweza kumpa nasaha,au kumtambau mshukiwa undani wake, na hata ukamsaidia na hata akifika mbele ya mahakama, anakuwa huru kujieleza, kwasababu keshaona kosa lake,…..sio rahisi kihivyo, lakini inawezekana…’akatulia kidogo.

‘Sisemi kuwa watu wa usalama kwa kufanya hivyo wanafanya makosa, hapana, wakati mwingine ni vyema kwasababu unaweza ukazuia uhalifu usisambae, au mhalafi isipate muda wa kutoroka, lakini kama kweli ni mhalifu haina shida, …nasema kama kweli unayemuhisi ni mhalifu, unaweza ukafanya hivyo,…..lakini je kama umemkamata mtu ambaye sio mhalifu , ikaja kugundulika baadaye kuwa kakamatwa kimakosa, utawezaje kufidia yale mateso aliyoyapata hasa ya kisaikolojia…wengine wakanakaa jela miaka,halafu wanatoka wakiwa hawana kosa….hebu niambie kweli hiyo ni haki?’ akauliza swali huku akimwangalia mkuu.

Mkuu alikuwa kimiya akimwangali huyu mwanadada, na hakutaka kusema kitu kwa wakati huo, ingawaje alikuwa na majibu mengi ya kumjibu , lakini aliona sio mahali pake, yeye alikuwa akisubiri wakati muafaka, maana ana uzoefu na akzi hiyo,

‘Wewe bado mchanga kweney kazi, hii mhalafu umpe mwanya, humapti tena, na hata ushahidi utafutwa kinamna….’akasema kimoyomoyo, huku akimsikiliza mwanadada huyu.

Mkuu kwa wakati huo, alikuwa akisubiri yale anayoyataka kwenye kesi hii, mengine aliona kama kuptezewa muda, ingawaje amejifunza mengo ambayo alikuwa hayajui kuhusu hisitoria na watu wanaohusika katika janga hilo, lakini yeye alikuwa akisubiri yale aliyokuwa nayo kichwani, hasa yanahusiana na kesi iliyope mbele yake, hasa aliposikia kuwa huenda mtu wanayemshuku anaweza asiwe ndiye muuaji ,…

‘Kama huyu mtu tunayetaka kumkamata sio muuaji, …..nani ni muuaji, na kama tutamakamata huyu jamaa bila kosa, na huyu ni mtu anayejua sheria, kesi inaweza ikatugeukia sisi,na kujikuta tunapoteza kazi, oooh, hapa nahitaji maelezoo ya kina, ili nijipange upya, huyu dada kichwa,….lakini hata hivyo hajajibu swali langu, kama sio huyu jamaa tunayemshuku basi atakuwa nani, anaweza akawa ni ni Sokoti,…’mkuu kichwa kikawaka moto kwa mawazo.

********

‘Tuna washukiwa wawili muhimu katika hii kesi yetu, washukiwa ambao usalama unawatambua, na kama nikufikishwa mahakamani sasa hivi hawo ndio watafikishwa mahakamani, kutokana na ushahidi uliokusanywa, na sijuii kama ni kweli, au la, lakini tutaweza kuona kwenye maelezo yangu, naomba mtulia na mnipe muda….’akasema wakili mwanadada.

Mshukiwa wa kwanza ni muheshimiwa mkuu wa kitengo chetu cha upelelezi, huyu amepewa nafasi kubwa, kwasababu nyingi tu, lakini sababu muhimu ni kutokana na madhila aliyotendewa na hawa watu kwa kutumiaudhaifu wake wa kibinadamu, udhaifu ambao, unawanasa wengi, ingawaje hatutaki kunyoshewa vidole, lakini weneywe ni wepesi kuwanyoshea vidole wengine.

Kimwana, alitumiwa na kundi hili, kuwa ajifanye , au ajirahisi kwa muheshimiwa kimapenzi, ilii wenzetu waweze kumweka huyu jamaa mkononi, hilo ndilo lengo lao kubwa, lengo la kipesa kwa huyu lilikuwa ni kipenegel cha pili, nia ni kumvunja nguvu, …kwahaiyo wakimtumia Kimwana,na kwa maelezo ya upelelezi, huyu mkuu, alimuua Kimwana kwasababu ya kisasi, na pili kwasababu ya kuondoa ushahidi kuwa huenda akatumiwa tena mahakamani kumchafulia jina lake kama akifikishwa mahakamani, kwa udhaifu huo.

Ni kweli, Kimwana alitoke kuwa mpenzi wa siri wa mkuu wetu huyo,, na kutokana na yeye picha chafu zikachukuliwa na kutumiwa kama silaha, wenzetu wanaita,`blackmail’ . Kuwa tuna siri zako hizi hapa, ambazo tukiziweka hewani, au kuzifikisha mahala kadhaa, kazi huna, au mke huna, au hata mali huna ..kwahiyo ili tukilinde na ili tuziharibu hizi siri, tunahitaji shilingi kadhaa,….na hawa watu usfikiri wanataka pesa bila kujua kuwa unazo auu huna, wameshafanya utafiti kuwa unazo…

‘Ndivyoo ilivtokea kwa mkuu wetu wa kitengo, walishagundua udhaifu wake, na pia walishagundua kuwa huyu tumkimnyaka, kutokana na utendaji wake, tukamuweka mkononi, hakuna mwingine wa kutufuatilia, …na pia ni vyema tuvunje nguvu zake za kimali, ili aipate tena pesa zakuhingea, hapo unaona swala la ndoa linajipeneyeza.

Akapelekwahizopicha na kuambiwa atoe pesa nyingi, na asipotoa pesa,picha hizo zitasambazwa, na hata kufikishwa kwa wakuu wake wa kazi, …kwa mtizamo huo, wapelelezi wakaona kuwa huyu ndiye mshukiwa wakifo cha Kimwana, kwani alimuona kama ndiye aliyemuingiza matatani, ukitizama hoja hiyo bado ina walakini, ….’akamwangalia mkuu kwa huku akitabasamu.

‘Nasema ina walakini kwasababu Kimwana, sio yeye aliyechukua hizo picha, na kama tulivyoona yeye alitumiwa tu, na kundi hili,…ndio,..labda huenda alishirikiana na hawo watu kamatulivyo-ona awali. Lakini kama alishirikiana na hawo watu, kwanini huyu mshukiwa asiwaue hawo watu ambao ndio walipanga hiyo mipango ya kuchukua hizo picha, akimbilie kumuua huyo Kimwana peke yake, au ndio ilikuwa mwanzo wa kulimaliza hilo kundi mmoja mmoja, au labda tutasema alikuwa hajawajua hawo watu wengine na kwa hasira akamuondoa huyu binti duniani….?’ Akamgeukia mkuu kama vila anamuuliza hili swali.

Haya tuchukulie ni yeye, …kama ni yeye aliyafanyaje hayo mauaji, maana lazima tujenge hoja kimatendo, hatua kwa hatua, jinsi alivyofanya hadi kuyafanya hayo mauaji, hebu turejee kipindi cha hayo mauaji ,….’akageukia upande mwingina huku akiwa hamuangalii mkuu au mimi, aksema;

‘Wote tunajua kuwa muheshimiwa alikuwa mgonjwa, na mauaji hayo yalitokea kipindi mwenzetu huyu yupo kitandani mgonjwa, kwa mshituko baada ya kupelekewa mkanda huo unaoonyesha matendo yake aliyokuwa akifanya na huyo binti. Ukiuona huo mkanda …aah, jamaa hana ujanja,sijui kama kazi atakuw anayo tena, sijui….hilo sio jukumu langu tena, lakini je kuhus mkewe, je kuhusu jamiii, ndugu, na wazazi wa mke, watamuelewaje husuani ndoa yake,….hapo akili ikagota akadondoka …..na kipondi cha mauaji alikuwa bdo yupo kitandani….

Nilipeleleza kiundani hadi kwa nesi ambaye alikuwa akimhudumia huyu muheshimiwa kwa karibu, maana unaweza kusema labda alikuwa na nafuu, akachomoka na kwenda kutekeelza mauaji hayo, huyu nesi kwa kinywa chake, alithibitisha kuwa mgonjwa huyo siku hiyo alikuwa katundikiwa dripu za dawa, na vyeti vinaonyesha, masaa dawa ilipoweka hadi ilipoishia…..kwahiyo asingeliweza, na haikuwa rahisi kwa hali aliyokuwa nayo, kutoka hapo kitandani na kufanya hayo mauaji.

‘Wapelelezi wanasema hata kama sio yeye aliyefanya hayo mauaji, basi atakuwa kamtuma mtu wake, kuyafanya hayo mauaji, swali likaja huyo mtu wake ni nani, …na tukifika hapo, tunamweka muheshimiwa pembeni, maana hapa tunakisia kitu, tunakuwa hatumzungumzii yeye, na inakuwa batili kiushahidi mahakamani,….`irrelevant and immaterial,…hakuna ushahidi wa kimatendo, ni ushahidi wa kuhisi tu….mtuhumiwa huyooo anaonekana hana kosa.

Mkuu akamtizama huyu mwanadada kwa macho ya mshangao, na alitaka kusema kitu lakini akanyamaza na kujifanya anakohoa tu, na kutulia akimskiliza huyu mwanadada. Alitaka kutetea hatua yao ya kumkamata mshukiwa huyo, kwani walikuwa na ushahidi wao mwingine, lakini hakutaka kubishana kwa muda huo,akatulia kimiya.

*******

Mshukiwa namba mbili ni Sokoti, huyo pamoja na makosa mengine, naye anatafutwa kuwa huenda akawa ndiye aliyesababisha kifo cha Kimwana, au hata kuhusika kumuua ,kwasababu kubwa kuwa Kimwana kasaliti kundi, pia alikataa kukabidhi mali kama vile nyumba, ambayo aliambiwa, kuwa kama anajitoa basi hizo mali alizopata kwa mgongo wa kundi, azirejeshe kwenye kundi akakataa.

Pili kama mnamkumbuka, Sokoti kwa kauli yake mwenyewe alisema kuwa kuingia kwenye hilo kundi ni rahisi, lakini kutoka ni vigumu, na alisema njia rahisi ya kutoka kwenye hilo kundi ni kifo, …ama huyo mtu anayetaka kutoka, ajiue mwenyewe, au kuuwawa kinamna. Sasa je kama Kimwana alishasema kuwa anatoka kwenye hilo kundi, hatuoni kuwa aliuwaliwa na hilo kundi.

Na kama aliuliwa na hilo kundi,ni nani alitumiwa akafanye hiyo kazi,au ni Sokoti mwenyewe aliyefanya hiyo kazi,,….Kama ni Sokoti mwenywe kwa vipi maana siku hiyo ya tukio hakuwepo hapa mjini, kwa ushahidi uliotolewa na yeye mwenyewe, lakini kama mkuu wa kundi aliweza kumtumia mtu wake, na kama alimtumia mtu wake, huyo mtu wake ni nani,..tunajikuta bado hatuna ushahidi wa kumbana huyu mtu kama muuaji wa Kimwana,atashikwa kama muudaji wakundi haramu lenye malengo kama hayo.

Wakili mwanadada akamwangalia mkuu, kama vile anataka maelezo kutoka kwake,lakini sivyo hivyo, nia yake ni kutaka kuhakikisha kuwa anaelewa nini kile anachokielezea, na hakutaka maelezo yake yachukuliwa kijuu,juu, ndio maana akatumia njia hiyo ndefu ya maelezo,ndio kazi yake , …

Tangia awali nishawaambia kesi kama hizi zinazofungamana na maswala ya ndoa, mapenzi, na kusalitiana, ambazo zinafungamana na mauaji, zinahitajii uangalifu wa kina, na zinahitaji busara, ili mwisho wa siku hata kama utampata muhusika, uwe umemsadiai kuliko kumwangamiza, na ndio maana mimi nikatumia njia ndefu ambayo natumai kama tutaitumia tutakuwa tumewasaidi wahanga waliojikuta wanatumbukia katika kisanga cha kesi hii bila hata wao wenyewe kutegemea.

Ili tuweze kuwatambua washukiwa na ili mwisho wa siku tumpate muuaji, mimi kwa uchunguzi wangu, nilianzia kuangalia shinikizo la haya yote, kiini cha haya yote, na ni rahisi tu kusema haya yote yalitokana na tatizo la ndoa,tatizo la wnandoa kutokutimiza wajibu wao, tatizo la kimapenzi,na cheche za mataztizo haya zikasambaa na kuleta maafa sehemu zisizohusika…..huwezi amini hili lakini ndivyo ilivyokuwa, kwani wanadamu ….usiombe,akili zetu zina mengi, …..

Hebu kwanza tuangalia kifo cha Kimwana kilitokeaje, huenda hapa tukasaidia kugundua kile nilichokigundua mimi, hebu jikurubishe kwenye hilo tukio, nashukuru kuwa mimi nilikuwepo hapo kweney tukio, sasa hebu tuliangali lile tukio natumai tunaweza tukapata mwanya wa kumtambua muuaji,……..

NB: Jamani hili jembe nimeliazima kwa masaa mwenyewe analitaka, ngoja niishie hapa. Ila nalitupa swali kwenu, ni nani anaweza akawa muuaji wa Kimwana?

WAZO LA LEO: Tunapokuwa makazini, au katika shughuli zetu za utendaji, ni vyema tukasimamia misingi ya kazi zetu, na sio kutenda kwa ajili ya kumuonyesha bosi, kwa kufanya hivyo, kuwa eti nifanye hivi ili bosi anione kuwa ninafanya kazi, unakuwa hujaiva kiutaalamu wa kazi yako. Huko kunaitwa ni kujipendekeza.



Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

5 comments :

Precious said...

Nimependa wazo la leo M3 tuko pamoja sana

Rachel Siwa said...

Asante sana kwa Wazo la Leo;Mmmmhh kazi ipo pouwa ndugu wamimi nafarijika sana,Mungu azidi kukubariki ndugu wa mimi Pamoja daima!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Hapa pana utamu kila ukija hapa unatoka na kitu. Shukrani na kazi nzuri . Pia kama kachiki hapo juu nimependa pia wazo la leo yaani umenena hasa.

Anonymous said...

Ni kweli usemayo ila Kama kawaida binadamu Wendi humuogopa boss

emu-three said...

Nawashukuru sana jirani zangu: Precious, ndugu wa mimi,ndugu wangu na unknony kwa kuniunga mkono.TUPO PAMOJA.
Swali langu wapendwa ni nani muuaji wa Kimwana