Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, June 5, 2012

Hujafa hujaumbika-47 hitimisho-5



Mwanadamu ni kiumbe mwenye huruma sana, lakini ile huruma ikimtoka na ikatawala chuki,anaweza akageuka akawa na nafsi mbaya kuliko unavyofikiria, hili niwaambie muelewe,….’akaendelea kuongea mwanadada wkili tukiwa tunamsikiliza kwa makini,, akaendelea kusema;

‘Chuki iliyopandikizwa kwa sababu ya mapenzi, inakuwa haraka kama isipozibitiwa, nasema hili nikiangalia visa ndani ya kisa hiki ambavyo matukio yake yalitokana na mapenzi. Kusalitiana kwa mapenzi, kutokuzijua ndoa zetu, na mmoja kati ya wanandoa kutenda kinyume na makubaliano ya ndoa.

Tumrudie mmoja wa wahusika katika kisa hiki ambaye tunaweza kumuita binti wa docta, huyu mwanadada ambaye alitoka katika familia ya madakitari walioijua ndoa na wakawa walimu wa kuzijenga ndoa za watu, lakini….

*******

Kwakweli huyu mwanadada licha ya kuwa alijitahidi sana kuijenga ndoa yake, na taka kutaka kugundua nini kilichombadilisha mumewe, lakini alijikuta kigonga ukuta, ila kimoja alichokigundua mapema, na ambacho aliona kuna njia mbadala ya kuweza kuwasaidia, ni kuchoka kwingi kwasababu ya majukumu ya kazi yake, lakini hata alipogundua njia mabadala,bado alijikuta akishindwa kutokana na kikwazo cha mumewake,….

‘Mume wangu kazi hii  ya kuajiriwa naona inanichosha sana, na naona inawezekana ikawa ni moja ya chanzo cha mimi na wewe kuwa mbali kimwazo, na hata kimwili..nimeonelewa kuwa,…’siku moja alimwambia mume wake na kabla hajamaliza alichotaka kuongea akakatishwa kauli yake.

‘Kwahiyo unataka kusema nini…?’ akakatishwa na mumewe, huku akiwa kaangaliwa kwa uso wa dharau.

‘Nataka tulijadili hili kwa pamoja, ili kama inawezekana nisiwe nafanya kazi masaa mengi, hili linawezkana mume wangu, kama tutakubaliana,… lakini ili liwezekane, ina maana mimi mshahara utapungua…’akasema.

‘Hata ukipungua mimi linanihusu nini mimi, toka lini nikaishi kwa kutegemea mshahara wako,…hatuna watoto, ni huyu binti yako, ambaye hahitaji gharama…ni uamuzi wako kuamua….fanya utakalo?’ akasema kwa hasira.

‘Tatizo lako wewe hutaki kuwa karibu na mimi, kila nikjaribu kukuweka sawa, ili tuwe pamoja, unanisukuma kwa maneno makali, unajua mimi ni bindamu, itafika sehemu na mimi nitasema basi,liwalo na liwe…nitachoka mume wangu…na haitasaidia kitu…..’akasema huyo binti.

‘Useme basi au usiseme basi, mimi sijali,wewe amua unalotaka,…kwanza unanipotezea muda wangu hapa bure….’akasema na kuinuka kutaka kuondoka.

‘Sikiliza mume wangu, wewe ni mtu mzima,….kwanini hutaki kuniskiliza amimi hata mara moja tu, nini nimekufanyia kibaya mpaka unione siona maana kwako,….niambie ili nijue, ili tuweze kuishi maisha ya raha kama mume na mke……’akasema.

‘Siwezi kusikiliza utumbo, kila unachoongea hakina maana yoyote,….kwanza wewe unataka raha gani, hebu jiulize nini hasa unataka mimi na wewe tukae tuongee, utanipa nini cha kunifurahisha, huna mtoto, umejikalia tu hapa,….raha gani unataka wewe….’akasema na kumwangalia mkewe kwa hasira.

‘Mume wangu kuhusu swala la kupata mtoto  nilshakuambia twende tukapime ili tujue nini kinafanya tusiwe na mtoto, umelipinga hilo, na hutaki kabisa kuhangaika nalo, …au una mipango yako, ya kuniletea watoto wa nje,…..’akasemahuyo binti  wa docta.
‘Nilishakuambia mimi na mwanaume humu ndani, nini nafanya ni juu yangu,hata nikileta watoto hapa yanakuhusu nini….wewe si huzai, acha nikatafute watoto nje..’akasema huku akiwa keshafika mlangoni.

‘Unajuaje kuwa mimi sizai, huenda tatizo liko kwako,….mimi ni docta,kama ningelikuwa na tatizo ningelishajua,na ningelishakuambia ….mimi sina tatizo lolote, kama lipo tatizo huenda lipo kwako, au linaweza likahusu sote wawili, katika kukamilika kwa swala zima la uzazi,….ndio maana nashauri twende sote tukafanay uchunguz wa kina,….kwanini hilo liwe gumu kwako….au umeshajipima ukajigundua kuwa una matatizo mwenyewe….’akasema huku akimwangalia.

‘Eti unasema nini wewe mwanamke…’akageuka kwa hasira,

‘Nasema hivi, kama hutaki kupimwa huenda umeshajigundua kuwa una matatizo, ….’kabla hajamaliza jamaa alishamfikia kwa hasira akiwa kainua mkono kutaka kupiga kofi, lakini mkewe akasogea mbali na kushika kiuno.

‘Hivi wewe unaona kupigana sio suluhisho la haya matatizo,….au kwasababu ya mila zenu ambazo kupiga wanawake mnaona ni ufahari,….nakuomba mara nyingine tena, kuwa sitavumulia hii hali, ….kwanza nakushangaa wewe ni wakili , una jua nini maana ya sheria, …’akaongea na kabla hajamaliza akaone mwenzake akiondoka, na alipofika mlangono akasema;

‘Kama unaona mimi nina matatizo, subiri,….si unaona mimi nina matatizo, eeeh, nitaanza kukuleta watoto wan je,uje ulee, nafikiri ndio dawa yako,….’akasema na kuondoka.
Binti Docta, alikaa kwenye kiti, akashika kichwa, akawaza, na kuwazua, akawa anajisema akilini mwake kwa huzuni,

‘Hivi jamani ndoa inakuwaje ngumu, kwanini tushindwe kuelewana, …hivi kuna tatizo,..hivi, mimi nina tatizo gani kwa mume wangu, sina mvuto, sijui mapenzi…au kuna tatizo gani…mungu wangu lini na mimi nitaipaat raha ya ndoa, nimeosa nini mimi mungu, naomba unisaidia , …naomba uisaidie ndoa yangu,…kama kuna kosa nimelitenda naomba unionyeshe njia….’akawa anaongea huku machozi yana mtoka.

*********

Profesa Sokoti , kama anavyojulikana, alitizama tarakilishi (komputa) yake kwa makini, akawa anaangalia sura za mabinti mbali mbali aliowaweka humo ndani, amekuwa na tabia ya kuweka kumbukumbu za wateja wake kwenye tarakilishi yake, na sasa alikuwa akiweka kumbukumbu ya mteja wake wa hivi karibuni, huku akikumbuka mahojiano yake na yeye;

‘Mume wangu nampenda sana,na nimejaribu kila njia ya kutaka tuongee naye, ili tuweze kusaidiana, lakini imekuwa vigumu sana, kama unavyojua kuwa mimi ni docta, na pamoja na udakitari wangu,nimezaliwa ndani ya familia inayojua vyema maisha ya ndoa, …..ningekuwa huko ,nafikiri tatizo hili lingeshaisha, lakini sitaki kuihusisha familia yangu kwanza…..

‘Lakini nimeshakupatia mtu ambaye alishafanya hiyo kazi, na jana tu nimeongea naye akasema alikupa mjina yote, ya wanawake wanaoonekana kuwa wana mahusiano ya karibu na mumeo, …unataka nini zaidi….tuwafanye kitu mbaya…?’akauliza

‘Hapana sitaki kumfanya mtu kitu mbaya, mimi tatizo langu ni mume wangu, hawo, nitajua nini cha kufanya baadaye,kwanza nikutane nao mwenyewe. Kwasabbu gani, tatizo hili limekuwa kubwa sana sio kwangu tu, nimekutana na akina mama wengi waliopo kwenye ndoa wakilalamika kuhusu swala kama hilo ….sasa nimetuliza kichwa changu nikaona kuna haja ya kufanya jambo….’akatulia.

‘Jambo gani..?’ akauliza.

‘Kule Kenya mama yangu ana kliniki ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya ndoa, sasa na mimi nataka kuanzisha kitu kama hicho hicho hapa nchini,….lakini kinamna yangu, na malengoyangu..’akasema na kuwa kama anawaza kuhusu hilo jambo.Na Sokoti akasema kimoyomoyo, ` na mimi nina malnego yangu hapo hapo….tutabanana hapo hapo…’ halafu akasema;

‘Wewe unanishangaza kweli, kama mwenyewe umesema ndoa imekushidna utawezaje kuwashauri wenzako….hebu niambie unataka tufanye nini, labda wazo ulilonalo ni sawa na wazo langu, ila nilikuwa naogopa kukuambia,…’akasema huyu mtaalamu.

‘Nimegundua kuwa wanaoharibu ndoa za watu ni hawo wakina dada wanojipitisha mitaani,,...mimi nataka nianzishe kitu kama shule, ambayo hatua ya kwanza ni kuwakuasanya hawo akina dada, na mpango wangu wa mwazo ni kuwapata hawo akina dada wanaotemeba na mume  wangu..’akasema nakutulia.

‘Mambo si hayo,….hilo mbonakazi rahisi tu….enedelea kuleta vitu,…maana leo wewe ndiye mtaalmu wangu,….’akasema huyo jamaa akiegemeza kichwa kwenye kiti chake.

‘Kwanza itaonekana kama nawasaidia, lakiini baadaye,….tunawaita hapo shuleni,…tunawafunda, huku tukiwajau undani wao,…lazima kilammoja ajieleze, najua umeshawajua kiundani, lakini mimi kuna jinsi nataka kuwajua, …halafu hawo hawo tutawatumia kama fimbo ya kuwachapia hawa wanume wasiotulia kwenye ndoa zao….’akatulia na kumwangalia huyu jamaa.

‘Safi kabisa…wewe kichwa,…nakuaminia docta, sikujua kuwa wewe jembe la nguvu, mke wa shoka…naona tukiwa pamoja, tutafaya jambo kubwa sana, niambie ..ehe, hebu ongea, sasa umafika pale nilipopataka,…..’akasema akiwa na shauku.

‘Usije ukawazia tamaazako, ukaweka  njaambele, sitaki uhuni huo,…nakukanya mapema, maana wewe nakujau tabia zako….sitaki kufanya ubaya, mimi sitaki kufikai hatua ya ubaya, lengo langu lina maana ya kuwapa fundisho hawo wanaume, na pia, kuwa karibu na hawo mabinti. Kwahivii sasa nataka unisaidie kuhusu hili, wewe ni mtaaalmu wa saikolojia, …..au sio..?’ akasema kama anauliza na jamaaakadaikia  kwambwembwe…

‘Na wewe ni docta, ….au sio?’ akasema huku akitabasamu.

‘Nataak unielewe, usilichukulie hilijambo juu kwa juu, nataka utaalmu wa hali ya juu, nataka tumtafute mwanasheria ambaye ataliweka kisheria, na awe tayarai kujibu mapigo ya kisheria, na nitajitahidi kitengo cha sheri anachofanya mume wangu nikidhibiti kinamna,unaweza hilo….?’ Akauliza.

‘Hiyo kwangu ni kazi rahisi, hao hao mabinti watatumika, wewe utaona ….mimi sio mchezo, huwa nikipata upenyo kidogo tu, utacheka, huku wengine wanalia,….’akasema huku akitingisha kichwa.

‘Tatizo lako, una tamaa, naomba sana usije ukaweka tamaa mbele, utaharibu kila kitu…unaona, lengo langu ni kujenga mtandao ambao utaweza kufanya jambo, lisiingilie sheria, na sheria ikiingiliwa tujue jinsi gani ya kupambana nalo…kwasababu ujue mume wangu ni mwanasheria, ni mwanajeshi,…anajua kupeleleza, akija 
kugundua , utafia jela….sasa nataka asigundue lolote,….huku anapata kichapo ….mpaka arudi kwenye msitari….


‘Unajua wewe nilishakusoma tangu awali, ulikuwa ukizunguka zunguka, hata mimi nilikuwa na wazo kama hilo,….lakini nilikuwa naogopa,maana mumeo ni sio mtu wamchezo. Kwahiyo kwanza kuna akina dada wengi wanahitaji hilo somo, tunaweza tukawapata kwa wingi….kwanza tunawavuta kama njia ya kuwaboreshea amisha yao, ili wapate ndoa,…..mwisho wa siku, wanakuwa chambo,…..hilo wazo niachie mimi,…..hapa umefika, ila tunahitaji pesa ya kuanzia, nyingi kidogo…’akasema.

‘Sasa hapo ndio tatizo,na mimi kwa ujumla sina pesa ya kuanzia….lakini nipe muda…’akasema huyu mwanadada

‘Sikiliza dada yangu, pesa sio shida, , ….mmmh, …hiyo itapatikana kwa hawo hawo wanaume uchwara, kwasababu pesa zao ndizo zinazowavuruga….mimi hilo nitajua jinsi gani ya kulifanya,…..kwanza yupo rafiki yangu karudi ni mitambo ya nguvu…..wewe utaona, usiwe na shaka……wewe jiweek sawa kimwalimu, mengine niachie mimi…’akasema huyo jamaa

‘Sawa, kama umenielewa hamna shida, lakini mimi sitaki nijulikane sana kuwa nipo kwenye kundi hilo, nitakuwa nakuja kama mtaaalmu wa kufunda, na kwasababu nimepata mafunzo kidogo toka kwa mama,nitajua jinsi gani ya kuongezea maarifa,…..nikija kwenye hiyo shule,nitakuwa tofauti sitaki kabisa mtu anijue mimi,utakayelijua hilo ni mimi na wewe tu,  wewe uwe msimamizi wa kila kitu….sawa?’

‘Mimi nimekuelewa kabisa, usiwena shaka…’akasema huku akiandika kitu kwenye kumbukumbu zake.

‘Nafikiri ili twende sawa, nataka umtafute mwanadada anayefanana na mimi, awe anashika nafasi yangu kama sipo….hilo unalionaje ….?’akasema

‘Huyo mbona yupo tu….wewe utaonavitu vyangu,…wewe utakuwa kama kivuli….nyuma ya pazia,…mambo yanaenda kimiya kimiya…safi kabisa’akasema.

‘Haya naona wewe kila unakijua , unakielewa,….ngoja nikiachie wewe…’akasema huku akitaka kuondoka

‘Sawa, lakini kuhusu mumeo itakuwaje, maana kweli nitafanya hivyo, na wateja wetu, au wanafunzi wa mwanzo watakuwa hawo wanawake wanaotembea na mumeo…lakini mumeo ni mkali wa kupeleleza, atakuja kulijua hilo,..huoni ni bora nianzie kwake, kumuweka sawa kwanza…..?’akasema na kukatishwa.

‘Hayo kuhusu mume wangu niachie mwenyewe, cha muhimu ni jinsi ya kuwakusanya hawo wote wanaotembea na mume wangu, wakikubali,….na nikakutana na wao uso kwa uso, …nitajua nini la kufanya….utaona matokea yake baada ya miezi kazaa, ikifikia hatua ya kuwachapa viboko hawo wanaume wasiotosheka an ndoa zao, nitakuachie wewe na….’akasema huku akiangalai nje,

‘Na wataalamu wenzangu ambao wapo, hilo lisikutie shaka,…hapo tupo pamoja….kama utadhibiti huko kwenye usalama, shwari kabisa …na hilo ni rahisi tu, …hawo hawo akina dada tutwatumia kuhakikisha kuwa hakuna cha usalama au jeuri yao, watanywea wenyewe….hilo niachie.’akatikisa kichwa  na yule mwanamama akamwangalia huyo jamaa kwa mashaka, lakini akasema kimoyomoyo, nitahakikisha kuwa hafanyo baya lolote, akasimama na kuondoka.

Alipoondoka huyu mwanadada , huyo jamaa akainua simu na kumpigia mmoja wa rafiki zake akaongea naye kwa muda mrefu halafu, akampigia na mwingine, na mwingine….alipohakikisha kuwa kawasiliana na watu wake maalumu, akairudia komputa yake na kuanza kuangalia zile picha,alipofika kwa picha mojawapo, akatabasamu, na kusema;

‘Sasa pesa nitapata, nikiwa na pesa, nitafanikiwa, ndoto yangu, warembo wote…..hasa huyu,….’ Akawa anaangalia picha mojawapo kwenye komputa yake….akaanza kucheka kama mtu aliyechanagnyikia, akasema;

‘Sasa mambo yanajileta yenyewe, kipindi kigumuu kimmeshapita,…wanajileta weneywe,….na huyu ndiye mke wa kuoa,…..sijui kwanini anapata shida…na mwanume ambaye wala hajui kuwa yupo hai….sasa hiki kidume kisichotosheka na mke wake eti kinamtaka….nitakikata ulimilimi wake,….sijali cha usalama wake…nikigusa pale penyewe,atatulia,….mfuko ataufungua kilaini…’akasema na kukumbuka siku alipokuja huyu mwanadada ambaye anamtaka awe mke wake,…

*********

‘Kaka yangu mimi nimekuja hapa kwako baada ya kupata ushauri toka kwa rafiki yangu, sikupenda sana, kuja sehemu kama hizi, ila nahisi kila siku zinavyozidi kwenda nazidi kuchanganyikiwa, hasa nilipogundua kuwa mtu niliyempenda keshaoa,….

‘Nilishakuambi kuwa mtu kama huyo , najua jinsi gani ya kumweka sawa, lakini nikupe ushauri wa bure,kama keshaoa,huna haja ya kuhangaika naye,…wewe kwanza mzuri,…wanaume wengi wanakutafuta, ….yaani mimi mwenyewe kama ungenipenda, mbona utawaoan wanaume wengien hawana maana,…pili wewe una kazi yako ya maana, …udakitari, kwanini ujihanganisha na mtu ambaye sasa ana mke wake na …

‘Huo ndio ushauri wako..au ndivyo unavyowafanyia wateja wako?’ akauliza.

‘Ushauri wangu utategemea kuhusu historia yako, naomba tafadhali usinielewe vibaya, haya ngoja nikuhoji kidogo, na uniambie kila kitu nitakachokuuliza, bila kificho….utaona maajabu yake…na kuhakikihsia kuwa nitakusaidia ufanikiwe katika maisha yako…’akasema.

Alimuhoji yule dada, na hatiamye akagundua kiini cha tatizo hilo,akampa ushauri, kwamba, kwanza anatakiwa kuhudhuria hapo kwake, kwa ajili ya `kuweka mambo sawa’ ….pili, yeye anataka atafute mbinu za kuonana na huyo mwanaume, ili ajue jinsi gani ya kumfungulia njia, na hata ikiwezekana, ataichafua hiyo ndoa iliyopo na hatimaye huyu mwanadada anaweza akarudi tena kwa huyo mume…

‘Sitaki kuharibu ndoa  za watu, keshaoa, haina haja, ila ninachotaka ni kupata ushauri w ajinsi gani nitaondokana na hayo mawazo, maana kila mara namuwaza yeye tu,….nakuwa kama nimechanganyikiwa,….’akasema huyo mwanadada.

‘Hilo tutalimaliza ….usitie shaka,….limefika kwa mwenyewe, mimi nitahakikisha nakusaidia wewe, na kuna jambo moja  muhimu, nahitaji akina dada kama nyie waliosoma, kuna wazo limenijia sijalifanyaikazi kwanza, nikiliweza hilo, nataka kufungua shule au sehemu ambayo, nitakuwa antoa semina na ushauri nasaha wa mambo hayo ya ndoa, sijaweza kuliweka sawa hilo….’akasema huku akiwaza .

‘Hilo ni wazo jema,…kama nilivyokuambia nimewahi kuhudhuria shule kama hizo najue mengi kuhsu ndoa na mataizo yake, lakini wakati mwingine unazidiwa maana kama wasemavyo kinyozi hajinyoi….’akasema.

‘Ni kweli,mimi kama nitafanikiwa hilo, nataka nikuombe wewe tutakuomaba uwe nafika, unajau wewe ni mwelevu, na msomi, ukikutana na akina dada ambao wanahitaji ushauri wa misha, itakusaidia na wewe kuyasahau machungu yako, ….kama upo tayari nitawasiliana na wewe….’akasema.

‘Kwanza tutatue tatizo langu,…hayo mengine yatafuata, mimi napenda sana kazi ya namna hiyo, kama  kuna shule kama hiyo, nitajitolea, haina shaka, itanatajai kufunguliwa lini?’ akauliza.

‘Hivi karibuni, nitakujulisha….’ akasema huku akiwa haamini, maana kila anayekutana naye na kumwambia jambo hilo anakubali kiharaka sana. Akajua sasa mambo yanajileta yenyewe.mlakini katika wateja waliowahi kufika kwake, huyu aliweza kuiteka nafsi yake, na akaona kuna haja ya kumjua vyema, …kwanza alitaka kumjua huyo mume wa huyu mwanadada ambaye anapendwa kihivyo...

Alitaka akimjua awe ni mmoja wa chambo chake katika mambo anayoyakusudia, na ikiwezekana ahakikishe kuwa huyu jamaa anakuwa hohehahe kiasi kwamba hakuna mwanamke atakayemjali tena,…kila atakalolifanya limwingiza pabaya,....na hatimaye huyu atamweka huyu mwanadada kwenye himaya yake. yake.

‘Mjini hapa, mtoto mzuri kama huyu anahangaika na lijanaume lisilomjali,….kwanza nachafua huyu mtu,na huyu dada,nitajua jinsi ya kumhadaa, atajileta mwenyewe…cha muhimu huyu mwanaume, nitamchanagnya kabisa, kazi hapati, …nuksi itamuandama, kitaalamu….mpaka ajitie kitanzi……anacheza na Profesa …..mmh,sasa pesa nje nje….

Baada ya kumalizana na huyu mwanadada, akaingia dada mwingine….dada huyu alipoingia, alismama kwanza bila kusema neno, akamwangalia hho la dharau, huku kakunja uso,kinamna bila kusema neno, halafu baadaye akasogea na kukaa kwenye kiti..

‘Haya niambie umeniitia nini….

‘Kimwana unakumbuka tulipotoka….mimi najua siri zenu zote, na kama nitawafikisha polisi mtafungwa wewena huyo kidume chako, mtafungwa kifungo cha,maisha,…..nimekuambia achana na huyu muhuni,njoo nikuoe tuishi pamoja,……’

‘Niambie ulichoniitia, usinipotezee muda wangu….’akasema huyu mwanadada huku akiangalia saa yake.

‘Poa mtoto,…nakuona sasa huna muda wakupoteza, sawa siku hizi wewe matawi ya juu…sio mbaya, ila sasa kuna dili ya nguvu, kama utatulia vyema, tutatengeneza pesa ya nguvu….na hapo ndipo utakapo niona kuwa mimi nina akili ya ziada, hili jambo nilikuw nalo siku nyingi, lakini nilikuwa sijaliweka kwenye kazi zangu, sasa kaja mtu wa haja, ana  pesa, ana wadhifa,…..na ni wale watu walioshikilia mpini katika serikali….

‘Niambie nini umeniitia..

‘Wewe siunataak pesa, kwa mfano ukiwa unaingiza shilingi milioni kadhaa kila mwezi na hizi ni lazima uzipate, na kila kazi utakayoifanya unaweza ukaingiza milioni haya ishirini,…..

‘Wewe sasa umechanganyikiwa,kazi gani hiyo ya kuweza kupaat pesa nyingi kiasi hicho, na utazipaat kwanani,…, sisi tumejitadi kufanya kazi ya kufumaniwa kwa kupanga, na kudai pesa nyingi, lakini hatujawahi kupta psa nyingi kiasi hicho,hiyo ni ndoto ya Alinacha,…….’akasema.

‘Sikiliza hii dili ni ya majembe ya nguvu, wewe mweyewe utaona….wewe nisikilize kwanza, nitakuonyesha hatua kwa hatua….ninakuhakikishia kuwa kama utatulia na kufuata hayo utakayoelekezwa, utamiliki nyumba ya kifahari, utamiliki gari, na kila ukitakacho, lakini kwanza utimize hayo nitakayokuambia, …unasikia kwanza kabisa,unatakiwa uende shule maalumu ya kujua nini huyu mwanaume, ujua nini ndoa, ujua nini kuhusu mahusiano, na……

Mambo ndipo yalipopikiwa hapo……wajanja wakatumia udhaifu wa ndoa za watu, na hatimaye,...yakatokea yaliyotokea……lakini je yalitokeaje,.....! Tuwe pamoja katika sehemu nyingine ya hitimisho la kisa hiki..

WAZO LA LEO:Mpango wowote wa kujichumia mali usio halali ,mwisho wake ni madhara.  Watu sasa hivi hujiingiza kwenye njia nyingi za kutafuta mali, bila kujali `uhalali wake’….hata kama kwa kufanya hivyo wataumiza watu wengine, ilimradi kama wao wamefanikiwa, basi wanaona ni halali yao,…na hata kufikia kunadi kwa kusema `mjini hapa’.

Kumbuka, kuwa utajiri wa namna hiyo hauna mwisho mwema,kwasababu kupata kwako ni kuumia kwa wengine, …na hujui maumivu gani waliyoyapata  hawo wenzako uliowadhulumu, ujue hukumdhulumu yeye peke yake, kama ana familia basi hata familia yake imeumia. Je unajua wamumia kiasi gani, na hujui wamelia kilio gani kwa mungu, na ukumbuke kuwa dua ya mwenye kudhulumiwa haina kizuizi,  ..najionya kwanza mimi mwenyewe na wewe pia kuwa tuwe makini katika kutafuta rikiki zetu.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Precious said...

Nimependa sana wazo la leo...tuko pamoja M3

emuthree said...

Precious tupo pamoja,nashukuru kuwa nami kama kawaida