Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, May 29, 2012

Hujafa hujaumbika-43 hitimisho-1




‘ Kila mtu hakuamini ,hata mimi mwenyewe sikuamini hilo, hadi pale nilipopata ushidi wa waza kutoka kwa wahusika wakuu,….maana ilikuwa kama mchezo wa kuigiza, au pwagu na pwaguzi,…mchezo uliochezwa ndani ya famila moja kila mmoja akimtenda mwenzake bila ya mwenzake kujua,….lakini athari zake zikawa zinawaumiza watu wengine ambao….kwa namna moja walikuwa na matatizo kama hayo, wakaingizwa kama ngao …..’akasema wakili mwanadada, huku tukiwa na hamu kila mmoja alikuwa na maswali mengi kichwani ambayo majibu yake tulitarajia kuyapata kutoka kwa huyu wakili mwanadada.

‘Mimi hapo sielewi,matatizo ya familia yanakwenda kuwahusisha watu wengine ….kwa vipi, kama mimi nahusika vipi na matatizo ya familia nyingine, ambayo hata siijui vyema….?’ Nikauliza.

‘Jambo kubwa,ambalo nililigundua ambalo ndilo kiini cha hili tatizo, ni swala la  ndoa na mapenzi, ….’akasema na wote tukabakia tukimwangalia huku tukiwa hatuelewi kabisa nini anachotaka kusema, iweje ndoa na mapenzi yazae vifo vya watu....!
.
‘Ndoa na mapenzi yalete maafa hadi kuuana, kwa vipi na ni nao hawo walisababisha hayo, usiniambia chanzo ni mimi, sikubali kabisa….?’ Nikauliza.

‘Ndoa na mapenzi ni swala nyeti, na tatzio hili limekuwa likiathiri watu bila wenyewe kujua, na hata wanaolisababisha hilo,wanaweza wasijue kuwa chanzo na tatizo ni ndoa yao…..’akatulia na kuniangalia mimi, nikawa kimiya kumskiliza.

‘Bosi anaweza akakorofishana na mkewe huko nyumbani, kwasababu za kindoa, kwasababu za mahusiano ,hasira zile akazipeleka ofisini, na mkamuoana bosi kabadilika, hasira tele, au ukimiya usio wa kawaida au ….hata utendaji mbaya, kiini chake ni ndoa,….hili watu hawajui, na huenda wakataka kujifanya kuwa sio sababu….’akatulia kidogo, na kuinama chini.

Hii ni kuonyesha kuwa wanawake niwatu muhimu sana,…katika jamii, kutokana na wanawake tunaweza kuwa na taifa tulivu na la amani, kwani ndoa ndio chimbuko la kizazi ambacho kinaweza kikawa chema au kibaya, kutokana na malezi, kutokana na masikilizano ya wanandoa, kutokana na sintofahamu inayoweza ikajijenga ndani ya ndoa….’akatulia an kutuangalia …

‘Mimi nazungumzahili baada ya utafiti wa kina, huwezi amini hata viongozi wa nacho wanaathiriwa na hili,…ndio maana watafiti wanapendekeza kuwa ili kiongozi awe bora, lazima nandoa yake iwe bora,…kama ndani ya ndoa yake kunamsuguano, lolote linaweza likatokea…huko kwenye siasa sitaki kupaendea, ila ninalotaka kusema ni kuwa tukio hili, limagubikwa na msuguano, wa ndoa, ….ndoa mbayo iliwakutanisha mafahali wawili, wakawa wanapigana na zinazoumia ni nyasi….’akasema wakili nakutulia.

‘Samahani,….mimi bado umeniacha njia panda….’nikaanza kulalamika.

‘Nilitaka kuwaweka kwazi kuhusu hilo kwanza, kabla sijawaelzea kazi nzimaya hili tukio,…tukio ambalo ni kielelezo kwa jamii, kuwa ndoanimuhimili muhimu katika maisha ya jamii, …tujiribunii kuijua , kuiheshimu, na wanadoa wasikubali tu kuitwa wanandoa, wawe wakiifanyia kazi,….waziboreshe nda zao kwa kujifunza ….kamazilivyo Nyanja nyingine…’akatulia tena kidogo, na mimi nikaoan akma anaipoteze muda nikauliza swali kwa haraka.

‘Tuambie ulivyogundua , maana hadi sasa mimi bado unanichanganya tu, uligunduaje hayo yote maana ukiangalia ilivyo huwezi hata kukisia, wengi walijua kuwa chimbuko la tukio hili zima ni kutoka kwangu, …kwasabbu ya damu yangu moto…..maana kila jambo lililotokea limekuwa likinigusa mimi sio chanzo cha yote, mimi ni kama mhanga mwingine wa ….ndoa za watu wengine.’nikasema na hata mkuu akakubali kwa kichwa huku nikikosa neno sahihi la kumalizia.

‘Dunia hii ina mengi, na binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, kila mara anajaribu kuutumia ubongo wake,  akiona kuwa kuna upenyo wa kuutumia, bila kusahau kuwa na wenzake wana ubongo huo huo na wanafikira hizo hizo,ila pengine kwa njia nyingine….na ndivyo ilivyokuwa kwenye hili tukio zima,….tukio ambalo chanzo chake ni ndoa, hasira zikazaa visasi, na visasi vikawa vinaumiza watu wengine, ambao nao wana matatizo yao kama hayo, na hilo lilipikwa kitaalamu…...’akasema wakili mwanadada akijaribu kutafuta njia ya kutuelewesha maana hadi hapo tulikuwa abado hatujamuelewa vyema , licha ya kuwa mshukiwa wa tukio zima alishajulikana.

‘Ili muelewe hili tukio kwa undani, naona nielezee kwa kupitia wahusika,nikianzia kwako wewe mtoto wa Msomali ,ambaye nitakuita muhusika, ambaye kwa usoni mwa watu ulionekana kama mhusika  mkuu, ….lakini kiundani wewe sio muhusika mkuu, wewe ulikuwa kama tawi kwenye shina,….wapo wahusika wakuu wawili ambao ni shina la tukio zima,…tutakuja kuwajua, ila nataka nianzie kwako wewe ili kukuweka sawa…’akasema wakili mwanadada.

‘Nilishakuhoji sana, na katika kukuhoji huko nilgundua mengi dhidi yako…..mambo haya yanaweza yakaanza mwanzoni tu mwa ndoa, watu hamkai mkaongea, kila mmoja anajiona anajua zaidi ya mwenzake, na likitokea jambo, kila mmoja anakuwa na maamuzi yake,…na hatimye lile pendo linageuka kuwa chuki, wivu, usio na tija,…nakulipizana kisasi,….

Mimi nikakaa kimiya, nikisikiliza ,lakini kwa upande mwingine akili yangu ikawa ikitamani kusikia mengi kwa wkati mmoja, hapo nilikuwa na mawazo ya yule mgonjwa aliyekufa kule hospitalini, nilikuwa nikitaka kwanza aniambie ukweli kuhusu huyo mgonjwa, kabla hajaongea kuhusu mimi, kwahiyo wakati anaanza mimi akili yangu ikazama na kujiuliza,…

Hivi,…..huyo marehemu ...imekuwaje....mbona siambiwi lolote kuhusu yeye, maana kila nilipodadisi lini atazikwa nimekuwa nikipigwa danadana, na kuambiwa hilo nitaambiwa baadaye……na hata ndani ya mahakama sikusiki hakimu akiligusia,….kuna nini kinaendelea,…akili yangu ikasema `hapo kuna kitu nafichwa..na kwanini nifichwe, hata hivyo huyo mtu mbona sijajua umuhimu wake kwangu…’ sikuvumilia nikauliza;

‘Kabla hujaendelea nataka kujua jambo moja,kuhusu huyo marehemu,…..kitu cha ajabu ni kwamba, sijasikia lolote mpaka sasa kuhusu yeye, na maandalizi ya mazishi yake, …., jana nimewauliza mkasema hilo nitaambiwa baadaye, sasa leo naona mnanipiga danadana, kwanza sijamjua ni nani, na kwanini alikuwa akitaka kuongea na mimi, na alitaka kuniambia nini,hamuona mnanitesa mimi kiakili…..’nikalalamika.

‘Ndio maana nawataka mtulie niwape tukio zima , huko kwa huyo anayekutesa akili yako,tutafikia, kwani ni mmoja wa wahusika , sijui tumuiteje , tiutamuita muhusika mashuhuri, kama ulivyo wewe…..maana huyo unayetaka kumjua ni nani, yeye ndiye kiunganishi cha tukio zima, …sasa niwaulize mpo tayari niwaambia nini kilitokea, au bado mna maswali mengine….’akauliza wakili mwanadada na kutuangalia machoni kwazamu, na sisi tulibakia kimiya ….

*********.

 Hiki ni kikao maalumu ambacho tulijikuta tupo mimi, mkuu na wakili mwanadada, hapo tulikuwa  kwenye chumba maalumu cha maongezi, baada ay kutoka kwenye chumba cha  mahakama ambapo tulikutana na hakimu, ambaye alitaka kujua hatima ya kesi inayonikabili mimi, …na baada ya maongezi na hakimu, ilionekana kuwa mimi sina hatia, ila nilishikiliwa ikioanekanna kuwa mimi ndiye muhusika , lakini baada ya uchunguzi , iligundulika kuwa mimi nilitegewa ionekane kuwa ndiye muhusika kiujanaj wa huyo mhalifu, …

‘Sio kwa vile umeambiwa wewe huna makosa ndio uondoke hapa jijini,hapana wewe ni shahidi muhimu sana katika kesi hii, usije ukaondoka, unahitajika sana….’akasema wakili mwanadada.

‘Nimekusikia muheshimiwa ,….’nikasema nakumwanagalia hakimu ambaye alikuwa akimsikiliza wakili mwanadada akiwa anatoa maelezo yake kuhusi kesi niliyokuwa nimekamatwa nayo,…, na alipomaliza kutoa hayo maelezo hakimu akaanza kumhoji wakili mwanadada akuliza swali,

‘Je huyo mshukiwa mumeshamkamata…?’akauliza hilo swali na kumwangalia mkuu, mkuu  ambaye kwa muda mwingi alikuwa kimiya, akionekana mwingi wa mawao akasema;

‘Hajakamatwa muheshimiwa, ila tumeshagundua wapi alipo na mtego umeshawekwa , …nia na lengo letu akamatwe bila umwagaji wa damu…’akasema mkuu.

‘Kwahiyo mnataka kusemaje,maana nimewaita hapa kuwasikiliza nyie,kutokana na kesi zenu ambazo zinakuwa haziishi, kila mnapoleta kesi izenu zinakuwa hazijakamilika, …na hili halinifurahishi, kwanini msitafute ushahidi wa kutosha kabla hamjazifikisha hizo kei zenu kwangu, msifanye kubahatisha, ….hilo sitaki lijirudie tena,mnanielewa…?’akasema muheshimiwa hakimu.

‘Tumekuelewa muheshimiwa, imetokea hivyo kwasababu, kesi hizi zimajisokota , ni watu wajanja walibuni mbinu zao, kwa kuichezea sheria, na saikolojai za watu, wamekuwa wakitumia uzaifu wa wenzao na kujifanya hawahusiki,…na matokeoa yake wakawa wanakamatwa watu wakijulikana wao ndio wahusika, kumbe wahusika wamejificha kiujanja,  na jinsi walivyojipanga isingelikua rahisi kuwajua kuwa ni wao wahalifu,….lakini ubaya hauna kwao wamepatikana…..’akasema wakili mwanadada.

‘Unatakiwa uliweke hilo wazi, na hakikisha kuwa unakuja na ushahid uliokamilika, maana hapa tu umeongea kimafumbo, kitu ambacho sitakitaka kwenye mahakama yangu, uweke uweke kila kitu wazi, ….na hakikisheni kuwa huyo mshukiwa anakamatwa haraka iwezekanavyo, sitaki kusikia matendo macahafuyakitendeka tena, na wakati mumesemamnaushaidi wa kutosha, mkameteni na haki itendeke ,….’akasema muheshimiwa na kuwaangalia  wakili na mkuu kwa kila mmoja kwa wakati wake.

‘Sawa muheshimiwa, leo au kesho utapata taarifa kamili, na tunakuhakikishia kuwa ushahidi wote umekamilika, ndio maana huyo mshukiwa akakimbia,….yeye alichofanya ni kujaribu kuvuta muda ili azima yake ikamilike,  lakini tutahakikisha kuwa hafanyi lolote baya..’akasema mkuu.

‘Sawa hilo tumemaliza, na nini mnataa kusema kuhusu huyu mshukiwa Msomali, maana leo mlisema mtakuja na kauli sahihi, kuwa yeye ndiye mshitakiwa na tunze kusikiliza kesi yake, na kama ndio hivyo ni nani wakili wake, …..?’ akauliza muheshimiwa Hakimu.

‘Kama nilivyosema awali, muheshimiwa, kesi hizi zilijisokota, na hawa watu walikuwa wakitumia mbinu, ambazo zimetufanya tuwakamate watu, tukijua wao ndio wahalafu, kumbe, wao wamejikuta wakiwa kwenye tukioo kama chambo tu, …..’akasema wakili mwanadada.

‘Kwahiyo hapa unataka kusema nini, kuwa kesi dhidi ya Msomali tuifute….nawaonya tena, mjue kwa mtindo huu mnatupoteze amuda wetu, kuna kesi nyingi za kusikiliza, na isiwe kila tukipanga muda wa kesi yenu, mnadai hili halijakamilika na sasa mnadai huyu mshukiwa sio yeye, ni yupi basi mshitakiwa, ili,tuyamalize haya matatizo…?’ akauliza muheshimiwa hakimu akimwangalia wakili Mwanadada, na wakili mwanadada akamgeukiwa mkuu,akiwa anataka yeye aliongelea hilo, na hakimu alipoona wanatupiana macho, akasema;.

‘Kwahiyo mnachotaka kusema hapa ni kuwa kesi dhidi ya Msomali, ifutwe, kwa masharti kuwa, muda wowote atahitajika kama shahidi, ila sasa yupo huru,….sawa?’akasema muheshimwa hakimu na wakili mwanadada akasema;

‘Ndio Muheshimwa, tunaomba kesi hiyo ifutwe dhidi yake,….hana hatia, ila atahitajika kama shahidi…

‘Sawa, mshitakiwa Msomali, kuanzia sasa upo huru,… ila kama ulivyoarifiwa utahitajika kama shahidi, hilo mtaliongelea wenyewe huko, naona hatuna zaidi, …nasubiri mumulete huyo mshitakiwa anayehusika…...’akasema muheshimiwa Hakimu na akawatizama kwa muda wakili na mkuu na alipona wote wapo kimiya akainuka kwenye kiti chake nakuondoka.

Mimi na wakili mwanadada na mkuu, tukatoka na kuingia kwenye chumba cha maongezi, ambapo mimi nilikuwa na mengi ya kujua, na hapo ndipo wakili mwanadada akaanza kuelezea jinsii ilivyokuwa kwenye kisa hiki hatua kwa hatua…..akianzia kwangu,na malezo yake yalijifanya nijijue …. na hapo akili yangu ikama kama mtu aliyezibuliwa,,…ni kama mtu aliyekuwa kaingiwa na maji masikioni, na yale maji yakatolewa……

NB: Haya wapenzi wa blog hii, naanza hitimisho la hiki kisa…..zipo njia nyingi za kuandika visambalimbali,  unaweza ukaandika kisa ukikianzia kwenye shina au aukakianzia mwishoni,ukakianzia kwenye  matawi yake,….kisa hiki ni mtindo mwingine ambao tumeaniza  kwenye matawi, na sasa tunaingia kwenye shina…mpo hapo…
WAZO LA LEO: Dunia ni starehe, na starehe iliyo bora ni maisha ya mume na mke ndani ya ndoa. Na  ili starehe hiyo ikamilike na kuleta matunda bora na mema, matunda ambayo nikiini cha amani na upendo duniani, ni bora wewe unayatarajia kuingia kwenye ndoa ukatafuta mke au mume mwema, na pia ni muhimu ukaijua ndoa na misingi yake vyema.  

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Yasinta Ngonyani said...

Ndoa ni mawasiliamo, masikilizano, utulivu= UPENDO WA NDOA...nasubiri hitimisho la kisa hiki kwa hamu kwelikweli...Kazi nzuri na nakutakia nguvu na kheri.