Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, May 8, 2012

Hujafa hujaumbika-33



Nilisogea na kukaa pembeni ya kitanda alipolala huyu mwanadada wakili, nikamuangalia machoni akiwa bado kajilaza huku akiangali juu, alionekana mwingi wa mawazo,na mimi hapo hapo mawazo yakaenda mbali zaidi, lakini sikutaka kusema kitu, ...namuheshimu sana huyu mwanadada, na nilichofanya nikugeuza kichwa na kuangalia pembeni, na yeye akasema,

‘Najua una hamu sana ya kutaka kujua kuwa nimeolewa na kama nimeolewa mume wangu ni nani, na kwanini siku ilesikuwa na pete, …pete yangu hii hapa,mara nyingi siachani nayao tangu siku ile nilipovalishwa na mtu nilipyemepdna sana…..’akajigeuza na kulala upande upande.

‘Una maana mume wako au sio ,basi nipe namba  yake nimpigia aje….ni muhimu sana ajue kuwa upo hapa, sizani kuwa keshapigiwa simu, au sio….?’ Nikualiza na kuchukua simu yangu tayari kwa kumpigia nikipewa namba yake.

‘Huwezi kumpata, usihangaike…..’akasema na nilipomuangalia usoni niliona nuru ya huzuni ikitanda na kitu kama machozi yakija kwa mbali, lakini aliyazuia, akasema;

‘Wengi wana hamu sana ya kumjua mume wangu, lakini …..’akatulia na kujinyosha.

‘Kama hupo tayari kuongea kusu hilo,usijilazimishe …unataka utilize kichwa ili upone haraka…’nikasema.

‘Nimeshapona, mimi sio mtu wa kulala-lala, hapa naona uzia tu,….akija docta nitamwambia niondoke, sipendi kuwahivi, nataka niwe mhakamani napambana na kutetea haki, sio kulala,…kilamuda ukipita naona kama napoteza haki za watu wengi ambao wanastahili kusaidiwa….’akasema na kujaribu kuinuka.

‘Ni kusaidia kuinuka….’nikasema huku nikimsogelea na kumsaidia kukaa vyema.

‘Usihanagike, nipo fiti….hapa nilipo nahitaji nipate mazoezi kidogo, huwa nikilala,nikiamuka lazima nipate mazoezi,….’akasema na kunyosha nyosha mikono na kweli alionekana mkakamavu.

‘Natamani sana nimuone huyo mume wako,….’nikasema

‘Kwanini….na wanini kwako?’ akauliza huku akiendeela kujinyosha.

‘Ana bahati sana kumpta mke kama wewe…’nikasema.

‘Unichekesha kweli,bahati ipi, na wakati wanaume mpo wachache na mnaringa, na wanawake tupo wengi, hatuna soko….’akasemana kugeuza geuza kichwa kujinyosha.

‘Mpo wengi, lakini watu kama wewe wapo wachache sana….’nikasema.

‘Watu kamamimi wapo wengi sana, ila hawapewi nafasi ya kujiweka kama mimi….huo ndio ukweli, kama wanawake wangelipewa nafasi ya kusoma, ya kuwa katika hali inayostahili, mbona dunia hiiingekuwa sehemu bora…lakini wapi…’akatulia na kuangalia mlangoni.

‘Niambie basi kuhusu huyu mume wako, maana nilizania kuwa nitamkuta hapa, na mpaka sasa hajafiak au yupo nje ya nchi?’ nikamuuliza.

‘Naona sasa ni bora nikuhadithie kisa changu,….cha mume, au sio, ili nikuondoe dukuduku lako,..kisa change sipendi kuhadithia,sitaki kujitia unyonge, lakini ngoja tu nikuhadithia. Ni kisa cha kunyang’anywa tonge mdomoni, sio mbaya ndivyo dunia ilivyo na unatakiwa ukubali ukweli…namshukuru mungu kwa hilo, kuwa licha ya kuwa niliumia mwanzoni, lakini nilikuja baadaye nikajipa ujasiri na kuyasahau yale machungu….’akasema na kuinua mkono wake ukiwa na ile pete.

‘Huwa napenda kuivaa hii pete, ….tangu siku ile nilipovalishwa, naiona kama ni sehemu yangu ya mwili,…najua ipo siku nitaitoa, lakini ni mpaka hapo nitakaporizika, na kwanini niitoe wakati nimevalishwa, ilitakiwa aliyenivalisha ndiye aje aitoe..ni mawazo tu….’akasema na huku akiizungusha zungusha ile pte kidoleni.

‘Una maana gani kusema hivyo….?’ Nikamuuliza huku nikiwa natafakari,….

‘Hahaha…waanume bwana,..kwahiyo unataka nikuhadithia kuhusu maisha ya ndoa,..halafiu iweje,au na wewe unafanya utafiti wa ndoa za watu,..kamani hivyo tupo sawa, sio mbaya nikikuhadithia hivi sasa, ….upo tayari?’ akaniuliza name nikamgeukia a kusema;

‘Nipo tayari muheshimiwa wakili….’nikasema huku nikitabasamu….Na hapo akaanza kunihadithia kisa cha maisha yake ya ndoa,…..

************

‘Wakati nipo chuoni, nilitokea kupendana na mvulana mmoja, tukawa tumeshibana kweli, , kwasababu ya upole wake , na tabia yake, ilinifanya nimuone ni mtu muhimu sana katika maisha,natumai hata yeye ililkuwa hivyo hivyo, na haikupita muda akanitamkia kwa kinywa chake kuwa kanipenda na angelifurahi niwe rafiki yake.

‘Nakuomba sana tusianze mambo hayo,maana nimetokea kwenye historia ambayo nisingelipenda , kujitonesha kidonda kilichoanza kunywea, na hata kuyahatarisha maisha yangu ya baadaye…’nikamwambia huyo mvulana.

‘Kwani kupendana kunahatarisha maisha yako, mimi sina nia mbaya kwako, nia yangu ni nyeupe kabisa, Sitaki kukudanganya,….ninachotaka ni kuwa tuwe marafiki wa kweli,..na  hata ikibidi ukirizika na mimi tuje tufunge ndoa…’akaniambia waziwazi.

‘Muda huo bado,nia na lengo langu ni kusoma…. hadi nifikie sehemu ambayo nitarizika nayo, tupo marafiki tangia hapo,..kwani hatupo marafiki?’nikamuuliza. Unajua tena wanaume hawakubali kushindwa,alinibembeleza,na ikawa kama kero, kila tukipata nafasi ya kuongea inaipenyeza hiyo hoja yake.

‘Sikiliza mimi nitakupa jibu baada ya kumaliza mitihani yetu…naomba unipe nafasii ya kusoma, nisingelipenda jambo jingine liingile akili yangu kwa sasa…’nikamwambia. Na yeye akanielewa ,na basi ikafikia muda wakumaliza mitihani, na kabla hatujaondoka maeneo ya chuo akanifuta na hapo hapo akadai jibu nililomuahidi…..wanaume mking’ang’ania kitu,….

‘Jibu langu kwa sasa ni hapana, nahitaji muda wa kujiweka vyema, kwanza maisha yetu ya kujuana ni ya hapa hapa chuoni,sikujui huko utakako, na huenda mila na dsuturi zetu zikasigishana, …wazazi wako wanaweza wakawa na malengo mengine ikizingatia kuwa wewe ni mtoto wakwanza wakiume,…sitaki kuleta migangono katika familia za watu..’nikamwambia.

‘Basi tupange siku twende kwetu, ….na mimi nipo tayari kwenda kwenu, unaonaje,…mimi nakuhakikishia kuwa nitakulinda na utaiona familia yetu ilivyo,ni wakarimu na hawana shida kabisa….hawapendi kuingilia maisha ya watoto wao yenye faida,…hilo nakuhakikishia…’akasema nami nikakubali kuwa anipe wiki mbili za kujiandaa, maana lazima nikapate kibali toka kwa walezi wangu.

Kwakweli nilishampenda huyo mvulana na moyoni mwangu nilisharizika naye, mengine yalikuwa ni mambo tu ya kujirizishana kwa nafsi zetu, ….na siku hiyo tuliyopanga kuwa nitakuwa tayari kusafiri,akaja kwetu nilipokuwa nikiishi na alinikuta nimeshajindaa, tukafunga safari hadi kwako mikoani.

Kwakeli ni familia iliyojitosheleza,kwani nilikuta kwao wana nyumba nzuri, wana miradi ya kuwakimu, na hata usafiri wa familia, na wenyewe walionekana wakarimu tu,…nikafurahi sana na yeye akanitambulsiha kwako kamamtarajiwa wake,sikupenda iwe hivyo haraka, lakini angesemaje kwa wazazi wake, …

‘Mbona haraka hivyo,kwanza hatujamjua huyu binti vyema …’akalalamika baba baada ya kumuita mtoto wake pembeni, na mimi nilibakia pale na mama, baadaye mama naye akaitwa na nikasikia akisema;.

‘Baba Nanihii unataka kumjua vyema kwa vipi,, ..wao walishajuana toka huko chuoni,sisi hatuhitaji kumjua zaidi,hebu niambie utafunga safari hadi huko kwao anapotoka ili umjue maisha yao na familia yao ,maisha ya siku hizi ni kuelewana, ..kama mwanetu karizika naye, hewala’akasema mama kwani alishanipenda .

Basi tukakaa hapo kwa wiki moja halafu nikaomba nirudi kwetu,na mwenzangu akadai kuwa kabla ya kuondoak hapo lazima tufunge uchumba. Ujue nilikuwa sijakubaliana na hilo ombi,na hakutaka kunilazimsha, na siku hiyo akalitamka tena hilo ombi,….nikamwambia bado muda muafaka, hakukata tamaa.

Kumbe wao kama familia waliandaa sherehe, waliyoiita ya kuniaga, lakini kumbe sio kuniaga tu, ila walivyoniambai mwanzoni ni kuwa wameamua kunifanyoa sherehe maalumu kwa ajili yangu.

‘Kwanini muahangaike hivyo…’nikasema na yeye akaniambia hilo ni swala dogo tu, na akaniomba nijiandae vyema, na hata nguo maalumu ikanunuliwa kwa ajili yangu.

Basi nikiwa chumbani kwangu, mara huyo mvulana akaja,….alikuwa akiniheshimu sana, tangu tufike hapo, alihakikisha hafiki chumbani kwangu mpaka kwa ruhusa yangu, na siku hiyo hiyo alifanya hivyo,akagonga mlango, nami nikamuitikai aingie ndani.

‘Unaonekana mrembo kuliko siku zote,sitamani uondoke, kabisa…’akasema
‘Nashukuru,hata hivyo lazima niondoke,ujue mimi ni mtoto wa watu, hatujafunga ndoa itakuwa ni maajabu nikikaa huku kwa muda mrefu…’nikasema.

‘Ni kweli lakini kabla ya kuondoka , kuna hicho kijisherehe kidogo ,tunataka kukuaga kama familia…tumekupedna sana hata wazazi wangu wamefurahishwa na tabia yako, wanasema kweli wewe unastahili kuingia nyumba hii…’akasema nami nikasema hakuna shida, muda ndio utakao-ongea.

Tukiwa ndani ya sehemu maalumu waliyoiandaa kwa hiyo sherehe fupi, wazazi wakongea na kutoa nasaha zao huku wakinisifia kwa maneno mengi na abadaye wakasema kijana wao ana la kuongea ;

‘Kijana wetu katuambia ana maneno ya kuongea mbele yenu,….hebu njoo huku mbele maana wewe ndiye ulitakiwa uongee sana kwa ajili ya mwenzako anayeondoka….’akasema baba

Yule mvulana akapita mbele, na kusalimia kwa adabu, akaongea kidogo,halafu akaniita nipite mbele.Bila hili wala lile nikaenda na tukawa tumesimama mbele ya wanafmilia na wageni waalikwa, nikashngaa mwenzangu anapiga magoti mbele yangu, akatoa kiboksi chete pete, na kusema ananiomba uchumba…watu wakashangilia na mimi hapo nikaingiwa na aibu,, maana sikutegemea kabisa kuwa itakuwa hivyo, na kwa heshima ya familia yao nikashindwa kusema lolote zaidi ya kukubali, nikavalishwa pete.

Basi sherehe ikaendelea na baadaye tukaeleeka kila mtu chumbani kwake, na kabla sijajiandaa kulala mara mlango wangu ukagongwa, akaingia huyo mvulana.

Na kwa vile tulishakuwa wachumba tena , mipaka ya kuingia kwangu ikawa imelegezwa kidogo, na usiku huo alipokuja tuliongea sana, na hata kufikia hatua ambayo sikuweza kumkataza kulala humo, na kawa mara ya kwanza nikaweza kukutana kimwili na huyo mvulana, sikutaka iwe hivyo kabla ya ndoa, lakini kwa hali ilivyokuwa nilishindwa kusema hapana….sisi wanawake tuna mitihani sana, lakini inatakiw auajsiri kusema hapana….

Basi kesho yake tukaagana na hapo ndipo nilipoona kuonja mitahani ya mapenzi, maana sikutamani kabisa niondoke, nilitaka nibakie naye, moyo, mwili akili ilishakubali kuwa naye, lakini ndio hivyo tena safari ilishapangwa na ikabidi niondoke. Yeye alitarajia kuja huku mjini baada ya mwezi na kitu hivi, kwani walikuwa na mipangilio yao ya kifamilia. Kwakweli njiani nilikuwa nikimuwaza yeye tu. Ndio mapenzi ya mwanzo yalivyo, ….

Sikuamini tukawa tukiwasilina kila siku kila muda nilipopata nafasi, na mwezi ukaisha,na hapo nikahisi mabadiliko ya mwili,nilikuja kugundua kuwa nimepata uja uzito nisio utarajia….nikahamanika, sikupenda kabisa iwe haraka hivyo na pia nikaona aibu kumwambia huyo mwenzangu ukweli. Na baada ya mwezi na nusu akaja hapa Dar, alipokuja nilishindwa kumwambia lolote kuwa nina uja uzito wake. Hakukaa sana akarejea kwao.

Alipoondoka kilipita kipindi cha miezi mwili, nami nikawa na wasiwasi jinsi gani nitamwambia na muda mrefu ukapita tena, na siku moja akanipigia simu kuwa ana mazungumzo muhimu na mimi….nikajua ndio hilo swala la kufunga ndoa,nami nikafurahi moyoni,….

‘Utakuja au tutazungumzaje na wewe upo mbali………..?’ nikamauuliza.

‘Tutaonge kwenye simu maana hata hivyo nina safari ya kwenda nje ….naenda kusoma zaidi…..familia yangu imenishauri hivyo nami siwezi kuikatalia, nitapita huko mara moja, uje uwanja wa ndege….maana sitakuwa na muda w akuja kukuonanyumbani kwenu,….natamani iwe hivyo, lakini safari ilivyopangwa imekuwa kama haraka, kinyume na matarajio yangu…’akanimbia nami nami nikamkubali ingawaje nilipenda aje tukutane uso kwa uso…

Basi siku hiyo ya safari yake, nikafika uwanja wa ndege, na alifika kwa ndenge ndogo, na siku hiyo hiyo anaondoka kwenda ulaya, kwahiyo hatukupata muda wa kuongea vyema, tuliongea mambo ya kawaida na pale nilipotaka kumgusia hilo swala langu akaja tafiki yake, wakawa na mazungumzo ambayo yaliishia muda ndege inataka kuondoka na yeye tukaagana tu.

‘Usijai nikirudi tu tunafunga ndoa….’akasema na pale pale akakumbuka na kuniachia simu yake. Akasema ;

‘Najau wewe ni mtu muhimu kwangu , nakuachia hii simu yangu, …sihitaji kusafiri nayo huko nitanunua nyingine..kama kuna mawasiliano yoyote waambie kuwa sipo’akanipa nami sikuwa na kipingamzi.
Akaondoka na nikabakia nikiwa na mtihani, maana nilijiona mjinga, kwanini sikumwambia muda wote huo, na nitawambiaje wanafamilia hasa familia yangu au familia ya mwenzangu, na wakati umeshapita muda mrefu kama huo,nikasema potelea mbali, nitamwambia mwenyewe kwenye simu,

Hutaamini hilo, kila muda tulipokuwa tukionge kwenye simu, kila nilipotaka kumgusia hilo swala,kunatokea kizuizi fulani,ama mawasiliano yanakuwa mabovu, au salio linakwisha au sababu yoyote ambayo inafanya tuahirishe mzunguzmo yetu, siku sikazidi kwenda mbele, ….

Ikafika muda hakuna mawasiliano na yeye tena akipatikana anadai kuwa yupo na shughuli nyingi za masomo na mara hata simu yake ikawa haipatikani tena….nikaona sasa hili litakuwa tatizo siku moja nikaona ni bora niifahamishe familia yao kuwa nina ujauzito wa mtoto wao, na siku hiyo nikaamua nitumie simu yake ambayo tangia aondoke nilikuwa siitumii, nilikuwa nimeizima kabisa.

Nilipoiwasha tu, kukaingia ujumbe, na ujumbe, ujumbe, na mtumaji alionekana ni yule yule  na nilipousoma huo ujumbe mmoja nikajikuta nikipepesuka, nilijisikia vibaya sana, nikawa na hali mbaya ambayo sijawahi kuihisi, na ukizingatia na hali niliyokuwa nayo,basi mambo yakazidi kuwa mbaya.
Baadaye nikajipa moyo nikasoma huo ujumbe vyema, ulisema hivi;

‘Mpenzi tangu uondoke mimi sijisikii vyema, unakumbuka nilikuambiai kuwa nahisi nia uja uzito wako, na sasa miezi miwili, ….naomba uwafamishe wazazi wako ili taratibu zote zifanyike, ….’, nIliusoma ule ujume  vyema ,labda iwe umetumwa kimakosa, lakini jina la mtumaji lipo waziwazi  na jina la mtumiwa katajwa kabisa kwenye hiyo simu, jina na la huyo mvulana.

Nikaona isiwe tabu , nikaamua kumpigia huyo mwenye ujume nikijifanya mimi ni dada wa huyo mvulana , na huyo mwadada akaupokea tukaongea kama mawifi, nikamwambia simu yake kaka kaiacha kwangu na nimeona ujumbe wake, je ni kweli kuwa yeye ni mjamzito.

‘Ndio ni kweli unajua tulipendana sana na kaka yako,…kila akija likizo tunakutana, mara nyingi nilimshauri tutumie kinga lakini hapendelei hivyo, na sasa safari hii mambo yameharibika, nimejikuta na ujauzito wake,…lakini hata hivyo alishaniambia kuwa nisiwe na wasiwasi…atanio tu…hataki mtoto wake azaliwe bila baba’akasema.

‘Mbona nilisikia kuwa ana mchumba mwingine toka huko Dar, na aliwahi hata kumtambulsha kwa wazizi wake…?’ nikamuuliz a kiujanja.

‘Ndio ilitokea hivyo, na iliniuma sana, na sikutana kumwingilia,…nikijua yeye ndiye muamuzi,… ila baadaye alikuja kwangu na kuniomba samahani kuwa alipitiwa tu, sasa yupo tayari kuwa na mimi, name sikujivunga, nahisi hapo ndipo mimba ilipoingia….kwakweli nampenda sana kaka yako, kama angelinidanganya,ningelikunywa sumu….’akasema.

Fikiria mwenyewe hali kama hiyo, hata hivyo sikukata tamaa, nikawapigia wazazi wake simu kuhakikisha hilo na wao wakasema kuwa ni kweli kuwa mtoto wao alikuja akawaambia kuwa anapenda amuoe mchumba wake wa zamani kwasababu alitaka mtu anayetoka kwao….na alishaharibu…keshampa ujauzito…’wakaniambia hivyo na siku niliposikia kauli hiyo toka kwa wazazi wao, tumbo lilinikata sana…nikawa najisikia vibaya kuliko, na siku hiyo hiyo nikapokea simu toka kwa huyo mvulana.

‘Haya niambie kwanini umefikia hatua hiyo ya kunidanaganya kumbe una mtu mwingine…’nikamwambia mapem kablahatujaanza mazungumzo mengine.

‘Ndio maana nimekupigia,nilitaka kukuambia kuwa bahati mbaya nimempa mtoto wa watu mimba, na nimeona nisimtese, …na nisingelipenda awe na mtoto asiye na baba, kwahiyo nitamuoa yeye tu…samahani sana….ila nakuomba tuzidi kuwa marafiki,nakuomba sana unisamehe, ..najua nitakuwa nimekuumiza sana, lakini imetokea hivyo..nashindwa hata la kukuambia….tufanyeje’kwakweli hayo mazungumzo yaliyofuata sikuweza kuyasikia, nilidondoka chini…huku nasema.

‘Je na mimi kama nina mimba yako utasemaje?’ nikasikia akisema.

‘Hiyo itakuwa siyo mimba yangu…’niliposikia hivyo, kiza kikatanda usoni, na mara nikadondoka chini na kupoteza fahamu huku maumivu kwenye tumbo, yakiwa makali sana….


NB: Jamani leo nimebanwa na mtandao unasua sua...kidogo kidogondio mwendo.


WAZO LA LEO: Unajiskiaje pale mwenzako uliyemtegemea anakumabia mimi na wewe basi, au ukasikia kuwa kapata mwingine ...inauma sana,....lakini ukumbuke yote ni majaliwa ya mungu, huenda imetokea hivyo kwa kukuokoa na jambo, au ili ukutane na mwingine ambaye ndiye chagua la mungu. Kama imekutokea hivyo, shukuru na usihamanike...vuta subira
Ni mimi: emu-three

1 comment :

Yasinta Ngonyani said...

Nimependa wazo lako la leo. Inauma ndiyo lakini inabidi iwe hivyo itabidi uyakubali yaliyotokea na kuendelea na maisha. Ahsante na nakutakia kazi njema maana kila ukiingia hapa unatoka na faida.