Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, April 16, 2012

Hujafa Hujaumbika-21

 
‘Samahani kwa kukusumbua asubuhi hii ndugu muheshimiwa....’ Ilikuwa sauti iliyomshitua muheshimiwa katika usingizi mtamu, ....alishawaambia walinzi wake hataki kusumbuliwa na simu zote alikuwa kazima, kasoro hiyo ambayo anayeijua ni mke wake tu...alishanga kabisa kusikia sauti nyingine,sauti ambayo hakupenda aisikie tena katika maisha yake.....

‘Nyie watu situlishamalizana na nyie,...niliwalipa hela yote mliyotaka, na mkaahidi kuwa sitawasikia tena katika maisha yangu..ina maana ndivyo mlivyo, hapa sisi mnanitafuta ubaya, sitashindwa kufanya lolote baya hata kama niku....’akaongea kwa hasira.

‘Sikiliza muheshimwa, tunalozungumzia hapa sio kuhusu lile swala lako, lile tulishamalizana kabisa,....na sisi tunatunza ahadi zetu, hili ni swala jingine,kabisa ni kuhusu mkeo..’ile sauti asiyoitaka kuisikia ikasema na aliposikia kuwa ni kuhusu mkewe, aliinuka haraka kitandani na kujiweka vyema, alimtizama yule aliyekuwa kalala naye pembeni na moyo ukamsuta ...

‘Kafanya nini mke wangu...?’ akauliza kwa sauti kali.

‘Tatizo lenu inavyoonekana, nyie wawili, wewe na mkeo,  mlikutana,wote ni kunguru haufugiki..samahani kuwaita hivyo, muheshimiwa...’ile sauti ikasema.

‘Nauliza kafanya nini mke-wa-wangu...?’ ikauliza tena kwa hasira.

‘Kwanza jiulize tumeipata wapi hii namba, ambayo anayeijua ni mke wako tu...’ile sauti ikasema.

‘Kama hamtaki kuniambia kafanya nini, nitakata hii simu na baada ya muda wa nusu saa mtaona nini nitakifanya...hamuniji mimi eehe, lile swala la kwanza, nimkubali hivy hivyo tu, lakini sio kila muda mnataak kunipanda kichwani,...hivi nyi...’akasema kwa hasira.

‘Tutashukuru sana ukifanya hivyo muheshimiwa, maana hata mkuu sana angelifurahi kusikia hivyo, kwani lengo lake ni safi kabisa, kutaka kupata viongozi bora wasaidizi,utakuwa umemrahisishia kazi yake ya kuwachuja, ...ukumbuke mpo wengi ambao wote wanagombea hiyo nafasi, kwahiyo...kwa mtindo huo utakuwa makapi,,’ ile sauti ikatulia kidogo.

‘Hayakuhusu hayo...’akasema mheshimiwa.

‘Ukumbuke, tulishakuabaliana kuwa tutajaribu kuweka njie yako iwe safi, sisi ni moja ya wafadhili wako, je upo tayari kuzalilika,.... wewe unafikiri wenzako hawafuatilii nyendo zako,hasa wale wabaya wako, wakigundua kosa dogo watahakikisha wanakumaliza kisiasa...unajua hilo...’simu ikasikiak ikisema.

‘Kwanini hauniambii....’mheshimiwa akauliza kwa hasira.

‘Mkuu sana, keshakuwekea alama ya kuuliza, ndio unachapa kazi sana, lakini madoa doa kamahayoyanaharibu utawala bora, na akisikia mambo kamahayo,moja kwa moja atakuona hufai kabisa kuwa kiongozi, ni kiongozi gani ambaye haijali ndoa yake....’ile sauti ikasema, na mheshimiwa akageuka kumwangalia yule kimwana aliyelala pale kitandani,...akajiuliza hawa watu wamejuaje mbali kote huku... alitamani kumfukuza yule mwanamke mle ndani,lakini kwa muda ule haingeliwezekana....

‘Lakini tulishakubaliana kuwa hatutafutana-fuatana tena, hasa maswala yanayohusu misha yangu, nyie jukumu lenu ni...mbona..’akalalamika.

‘Hilo tulishakubaliana...sawa kabisa , na tukasema tutahakikisha kuwa hakuna anayekusumbua tena, ili ufanikiwa kupanda ngazi katika maswala yako ya kisiasa,....na tetesi zilizopo ni kuwa huenda ukateuliwa kuwa ....siunajau tena hilo, nchi hii haina siri, lakini kwa mtindo huo sijui,...unajua mheshimiwa sisi tunajitahidi kukulinda,tukijua kuwa ukishika usukani na sisi hatutasumbuliwa tena,...’ile sauti iksema.

‘Ndivyo tulivyokubaliana....sawa kabisa, ... na mimi nimewaahidi kuwa nikishika hiyo nafasi sitavunja ahadi yangu...mbona nyie mnavuja ahadi..’akaanza kulalamika.

‘Sio sisi, hili linamhusu mkeo...na tunafnaya kazi yetu ya kuondoa uchafu utakaokuharibia ....licha ya kuwa wewe mwenyewe hujatulia muheshimiwa, ...tunakuomba ili hizi habari zisivuje,maana ikipita nusu saa waandishi wa habari wataipata hiyo skeno, watamkuta mkeo hapo hotelini...’ile sauti ikasema.

‘Watamkuta mke wangu...unasema wapi, ...hotelini ,anafanya nini....haiwezekani...’akalalamika.

‘Wanasema kuwa dhambi kama hiyo, adhabu yake huanzia hapa hapa duniani, ukizini wake za wenzako, ukizini watoto wa wenzako na wewe pia utafanyiwa hivyo hivyo kwa mkeo na kwa watoto wako..huyo aliye naye hapo ni nani, sio mke wa mtu, unajua kuna usemi usemao,` titi fo tati’, au uovu kwa uovu.’ile sauti ikasema.

‘Mke wangu huko hotelini alifuata nini.....niambieni haraka....?’ akauliza kwa hasira huku akiangalia kule kitandani kwa wasiwaasi.

‘Kwanza tumbukiza kwenye akaunti yetu milioni ishirini haraka, kwa ajili ya hizi gharama...hatutaki malimbikizo zaidi, kumbuka milioni ishirini, ...hiyo ni gharama ya kazi tunayokufanyia ya kukuondolea mauchafu yako, na pili, hakikisha unafika mwenyewe hapo hotelini, na kuondoa mwili wa mkeo,... ‘

‘Eti nini mwaili wa mke wangu...’sauti ya muheshimiwa ikauliza kwa wasiwasi, na mpiga simu hukujali hilo swali akaendelea kusema;

‘Na hakikisha kuwa hakuna kinachojulikana, na futa nyayo zako usijulikane kuwa ulifika mahali hapo, kama huwezi sema usaidiwe, lakini ujue ni gharama...tunakupa dakika tano za kutuambie tufanye weneywe au utafanya wewe ....na kama tutafanya sisi pamoja na kutaka kujua kwanini mke wako alifika hapo tutahitaji shilingi  milioni kumi nyingine...kwaheri..

‘Fanyeni nyi...nyi....ooh, mungu wangu nimekwisha...’mheshimiwa alijikuta akikosa nguvu , giza likatanda usoni,....kitu kikali kiachoma kifuani, ...akainua mkono kujishika kutokana na yalemaumivu, mara uso ukatanda giza akadondoka sakafuni na kupoteza fahamu....

*********

‘Mke wangu kwanini mnanifanyia hivi...?’ nilimuuliza mke wangu nikiwa nimechanganyikiwa.

‘Hebu sikiliza kwanza.., wewe hutakiwa kuwa hapa,....’akasema mke wangu akiwa kasimama mlangoni na khanga moja, sikuwa na najali, nikijua mke wangu alikuwa peke yake humo ndani, kama nilivyomuacha.

‘Ngoja niingie ndani maana, huko...’nikasema nikisukuma mlango ili niingie ndani.

‘Hutakiwi kukanyaga ndani, utaharibu kila kitu,... kumbuka wewe upo kazini,... nenda moja kwa moja kazini kwako, huko ndipo unatakiwa uwepo, ...ulikuwa kwenye zamu ya kazi za usiku...kwanini hufuati masharti, nilishakuamabi usije huku nyumbani,...haya ingia kwenye gari twende nikukimbize huko kazini...’akasema mke wangu bila kujali kuwa kavaa khanga moja, akaingia kwenye gari na kunifikisha sehemu ambayo huwa napofanyia kazi za usiku.

‘Kama ...ikibidi utasema ulichomoka mara moja tukakutana sehemu,...mimi na wewe,..yule mlinzi atakuwa shahidi...’akasema huku akinivutia kwake, tukashikana kwa muda, halafu akasema;

‘Haya nenda haraka, ukajitahidi kufanya kazi..., mengine yaache kama yalivyo...yatasawazishwa...ili mradi uwe umefanya kama nilivyokuambia....’akasema mke wangu bila ya kuonyesha wasiwasi.

**********

Ilipofika asubuhi nilikuwa wa kwanza kuangalia magazetini,...lakini sikuona taarifa yoyote ninayoihitaji, nikasubiri taarifa ya habari ya asubuhi, sikusikia lolote, nikashangaa, ..

‘Ina maana yule.... hakuwa kafariki...haiwezekani....’nikasema

‘Nani kafariki...?’akauliza mmoja wa wafanyakazi.

‘Kuna mtu mmoja alikuwa akiumwa sana,..tulikuwa tunamsikilizia, lakini nasikia bado anadunda...’nikadanganya.

‘Ndio kuumwa sio kufa...mungu ana miujiza yake, wapo watu wabaya, wanaua,..wanafanya machafu, mungu anawahifadhi tu, utajiuliza kwanini hawo watu wabaya wasife...kwa uoni wangu, nafikiri Mungu anafanya hivyo kuwapa hawa watu nafasi huenda watatubia na kuwa watu wema...’akasema huyo jamaa.

‘Kweli ...huenda wakajijua na kuja kutubia...maana madhambi yamezidi duniani...inahitajika kila mtu atubie kwa dhambi zake, kwani kwa ahli ilivyo, kila mtu ana dhambi zake..ingawaje zinazidiana,.....’nikasema nikijaribu kujitetea.

‘Tena haraka sana, usisubiri hadi kesho,maana dunia hii imekwisha,...kama umefanya kosa, ukajijua ni mwanzo mzuri, vyema ukatubu haraka iwezekanavyo, kabla hujachelewa, maana machafu ni kama kuonja asali, ....utapenda urudie tena na tena, na ukizoea , basi utaoana ni jambao la kawaida, nafasi inakuwa haiogopi tena,...bora kama mtu umejigundua ..acha mara moja, tubu kiukweli na usirudie tena, kwani ukirudia utakuwa unamchezea mungu. ...’Akasema yule mlinzi, na kabla sijamjibu akaongezea kusema;

‘Unajua rafiki yangu,  sasa hivi watu wanafanya machafu kila kona,...kutokana na kazi hii ya ulizni, nimeona mambo ya ajabu sana usiku.... usiku kunaharibika, ...unatamani ukimbie, maana gharika ikitokea sijui hiyo ghadhabu ya mungu ita....maana nikuambie ukweli, usiku unaficha mengi sana..’akasema huku akipiga miayo ya usingizi.

‘Kweli ....’nikasema na kutaka kuondoka, lakini yule mfanyakazi mwenzangu ambaye hupenda sana kuongea akaendelea kuniongelesha akasema;

‘Nimesikia kuna watu wanauza mili yao kwa uchafu wa ngono,....sio kusikia tu ,nimeshuhudia hayo...hata wanaume wanarubuniwa, ....na eti kazi hiyo wanalipwa hela nyingi sana, hizo ni pesa chafu hazina hata baraka...sasa fikiria huo uchafu...wanafikiri kwa kufanya hivyo hawataadhibiwa,...adhabu yake inaanzia hapahapa duniani, kwani ukizini mke wa mwenzako na wa kwako atafanyiwa hivyo hivyo...’akasema huyo jamaa.

‘Inawezekana kweli... eti eeeh...inawezekana ni kweli, eeh,  hata mimi nakubaliana na wewe...’nikasema, halafu nikasogea pembeni nikaishika simu yangu, nikiwaza, ...baadaye nafsi ikasema ngoja nihakikishe, nikasogea mbali kidogo na yule mfanyakazi,ambaye aliongeza maongezi ili tu tuwe naye, asipatwe na usingizi,maana kazi za usiku zinachosha....

Nilipohakikisha nipo mbali na yule mfanyakazi nikampigia simu mke wangu, nia hasa ni kutaka kujua nini kinaendelea huko, licha ya kuwa niliambiwa nisubiri mpaka saa tatu, lakini moyo haukuwa na subira tena, nikapiga simu kwa mke wangu...kuhakiki...

Simu iliita kwa muda bila kupokelewa, na kila nilipokuwa nikisubiri, nikiwa nimeweka simu sikioni na wimbo wa simu ukiwa unaendelea kuimbwa masikioni mwangu, kuashiria kuwa mpokeaji hajapokea,na hapo moyo ukawa unajaa mawimbi ya hasira, wivu, na chuki....na baadaye ikapokelewa;

‘Halloh, nani...ooh, ...nimekuambia usinisumbue,...unataka nini asu..su..buhi ooh, .....’akapiga miayo na halafu akasema;

‘Nimeshakuambia kuwa wewe unatakiwa ubakie huko huko hadi saa tatu...unataka nini asubuhi hii....’sautiya mke wangu ikasema ikionyesha bado yupo usingizini,..lakini kwa mbali kwenye simu nilisikia sauti ya kiume ikiuliza ‘Ni nani huyo...’

‘Mke wangu..na nani huyo anauliza huko...’kabla sijamalizia kuongea simu ikakatwa, na kuniacha nikighazibika,na hata nilipojaribu kupiga tena ikawa haipatikani,....

Mwili ulinisisimuka,kwa hasira ,na wivu..kweli tenda mtendee mwenzako, ukitendewa wewe kinauma,... ama kweli mkuki kwa nguruwe...nimesahau kuwa muda uliopita na mimi nilikuwa na mke wa mtu, nikifanya hayo hayo anayofanyiwa mke wangu, niliwaza hivyo, ...ingawaje sikuwa na uhakika wa moja kwa moja, lakini uhakika gani wakati nimesikia kabisa sauti ya mwanaume ikiuliza...huyo mwanaume atakuwa kafuata nini asubuhi hiyo kama sio alilala na mke wangu.

 Kila hatua iliyopita, mawazo yakawa yananitesa moyo wangu, ikafikia hatua najihisi kuwa mimi ni mtu mwenye bahati mbaya, ibu kuwaza kosa limetokea wapi, labda kuna kitu nimekifanya ambacho hakikutakwia kiwe hivyo, inawezekana ni kwasababu wazazi wangu hawajafurahiwa na mkehuyo niliye naye, inawezekana...

Pia inawezekana ni kwasababu ya jinsi nilivyomfanyia mke wangu wa kwanza, nilitakiwa nimtendee haki, lakini sikujali hata pale alipokiri kosa lake na kuahidii kuwa atajirekebisha. Lakini mwishowe alikuwali ukweli , akaona hatutaivana, na sasa yupo katika hali nzuri, kwahiyo hilo halina nguvu sana, kwasaabbau kama tungeliendeela kuishi naye, huenda hiyo hali asingeipata, sasa kosa lipo wapi..

Labda ni kwasababu ya haya mchafu ninayoyafanya, lakini haya mchafu yamekuja kwasababu ya hali ngumu. Kwasababu..ya ooh, labda ni kweli kwasababu ya huyu mke wa pili...hapo nikakanywea, nikaanza kuhsii jambo kwenye nfasi, lakini sikutaka liingie akilini na kukubali moja kwamoja kuwa ni kwasababu ya huyu mke wangu...

Kwasababu hiyo nimejikuta nikifanya yale ambayo hayafai, na matokeao yake na pata adhabu,...ingawaje kwenye nafsi nilijitetea kuwa yote hayo nilikuwa nayafanya sio kwa hiari yangu, ...lakini kwanini nikakubali, ...ama kweli ubaya utalipwa kwa ubaya...nikajiona nitafute shughuli za kujisahaulisha huku nikiwaza nchukue hatua gani, na ni nini hatima ya haya yote, na nikirudi nyumbani hiyo saa tatu nichukue hatua gani, nifanyeje, maana siku zinavyozidi kwenda nazidi kudidimia kwenye machafu, kwenye hatari....

‘Na nikirudi nyumbani, kutachimbika, lazima nijitoe kwenye huu utumwa, ...kama kazi yenyewe ili kuipata ni lazima nijizalilishe, ...sasa itanishinda, lakini hata hivyo, nimeshatimiza kile walichokitaka, kwahiyo lazima niipate hiyo kazi waliyoniahidi, maana nimitimiza kile walichokitaka, lakini kama watajifanya wajanja zaidi, lazima niwachomee,...ndio hata kama wakiniita msaliti sitajali, kama ni kufa, ...kila mtu atakufa tu...’nikawa najipa moyo kwa kuwaza hili na lile, ilimradi saa ziende...

Saa mbili ikafika, nikajua sasa nii muda wa kuanza kujiandaa kwa ajili ya kuondoka, nikijua kamahakuna lolote mpaka muda huo, huenda kila kitu kipo shwari, nikamwangalia mlinzi ambaye kwa muda huo anajifanya yupo kazini, ili mabosi wakiingia wamkute anahangaika, ...ndivyo ilivyo, kazi za namna hii, unatakuwa umuonyesehe bos kuwa unafanya kazi, ...

Nikiwa nimuangalia huyu mlinzi nikakumbuka kipindi nilipokuwa ni bosi ofisini, ilikuwa nikiingia tu ofisini, kila mtu anahangaika kwenye kazi yake,..utafikiri kweli wanafnya kazi kwa bidiii,  lakini ukiwapa kisogo tu, wanafanya mambo yao mengine, wengine wanajisomea magzeti,...nilikuja kugundua kuwa kipato na uwiano wa matabaka ya kipato nayo huchangia hiyo hali, kipato hakirizishi kwahiyo huyo mfanyakazi anafanya kile ambacha anahisi ni sawa na kipato chake na muda mwingie anaigiza tu kuwa anafanya kazi.

Nikiwa ndani ya mawazo, nikainua kichwa kuangaliai dirishani, kwani nilisikia kama honi ya gari, nikajiuliza ni bosi gani kawahi hivyo ofisini, maana kuingia kwao ni kuanzia saa mbili na nusu, mara nikamuona yule mlizni akifungua geti,  nikasubiri kwa hamu, na mara nikaona gari la polisi likiingia,.... hapo mwili ukafa ganzi, miguu ikaisha nguvu,....macho yakaanza kuona giza,  nikajua sasa kumekucha,...yale niliykuwa na wasiwasi nayo ndiyo hayo yamevumbuluka,.... ni lazima watakuwa wamekuja kunikamata mimi...

‘Msomali, ....kuna maaskari wanakuulizaia huku nje......’ sauti ya mlinzi ikasema kwa nguvu, sikuweza hata kumjibu. Nikajikongoja kutoka nje, kichwa kikiwa kikiwa hakifanyi kazi..

Wazo la leo: Fanya mambo yako kwa malengo, usikate tamaa, jitahidi kila siku ufanya jambo katika mpangilio wako, hata kama ni kwa shida, hata kama ni kidogo maana kidogo kidogo hujaza kibaba

Ni mimi: emu-three

4 comments :

elisa said...

Haya asante kwa ku update... Tulimis mwendelezo huu

emuthree said...

Elisa nashukuru kwa kunimiss na wapendwa wengine mungu atajalia tu,

Yasinta Ngonyani said...

Hapa sasa naona utamu unakolea yaani nasubiri kwa hamu kuona /klusoma kinachoendelea...ama kweli mkuki kwa nguruwe...

emuthree said...

Kweli dada yaNGU Yasinta Utamu kolea