Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, April 25, 2012

Hujafa hujaumbika-27



Nilikuwa hata sijui nifanye nini ili niweze kuishi, maana tangu niachiwe huru, nimekuwa mtu wa kuzunguka huku na kule kuwatafuta marafiki wa zamani lakini sikuwahi kumpata mtu ninayemfahamu na wa kuaminika, na hata Yule anayenifahamu kidogo, akaniona ananikwepa na hata kunikimbia, ….sijui ni kwanini.

Basi nikaona nihamie maeneo ambayo nitaweza kuishi, huku nikifanya bishara ya kuokota chupa na kuuza,ili angalau niweze kuishi,na siku nyingine nakosa pesakabisa na kugeuka kuwa omba omba, sina mbele wala nyuma,na hapo nikakumbuka na kujijutia ile hundi  niliyoahidiwa, ambayo hata hivyo nisingeliweza kuipata tena, kwa jinsi mambo yalivyokuwa.  Walishaniona mimi ni mbabaishaji,….

 Siku hiyo nilikuwa na mawazo sana, nikawa nakoswa koswa na magari,…na mwishowe nikaona nisije nikaambulia kilema, ni aheri ningeligingwa nakufa,lakini naweza kuambulia ukilema, na hali niliyo nayo nitaozea Mumhimbili, nikaona ni bora niingie kwenye jengo moja, ambalo tulizoea kuliita kijiweni, siku hizo labla sijawekwa ndani.Humo kweneye hilo jengo tulizoea kukutana baada ya kupigika kwenye vibarua, …ukiwa ni vijisenti vyako kidogo,aah, utapata supu ya ngozi, ukoko,na vyakula vya bei ndogokutoka kwa mama Ntilie, ambao wanauza kwa kujiiba wakiwakwepa watoto wa mjini, au wengine huwaita `cite’ au watoto wa mkuu wamkoa. Ukiingia hapo unachojali ni kujaza tumbo hujali usafi au ubora wa chakula.

‘Ohh, mshikaji, upo, ….’jamaa mmoja akanisalimia akiwa anaharakisha kuingia ndani, utafikiria anakimbilia kuingia kwenye daladala, lakini nilijua kabisa ni njaa, inayomkimbiza, nami wala sikumjibu, nikijisogeza malngoni,….palishaanza kubadilika , naona usafi umeboreshwa,….nikashangaa, ina maana hiyomiezi niliyokuwa nasota jela, kuna maendeleo kidogo.

Nilikuwa nayaangali haya wakati naingia mlangoni, huku nikiangaza angaza wapi nikajibanze, natembea huku macho yangu yako huku na kule,  na wakati natemba eneo lamlango, kwa bahati mbaya nikapigana kikumbo na mwanamama mmoja,aliyekuwa akitoka nje. Niligeuka kumwangalia huku nikitafuta lugha ya kuongea,maana humu ndani hakunalugha safi, kila neon linamatusi ndani yake, watu humo utazani wamechanganyikiwa, au hawana adabu.

Yule mwanamama, au mwanadada, alikuwa na  nywele ndefu ajabu,nafikiri ni za bandia, maana zilikuwa ndefu kiasi cha kumfunika  sehemu kubwa ya kichwa hadi mebagi, sikashuka hadi nyuma mgongoni, na usoni zilikuwa kama mtu kajifunika khanga ya nywele, na kuachia sehemu ndogo tu ya macho.

‘Wewe huoni nini….unatembe ahuku nanihii yako mbele kama …..’akasema na lugha ile ninayoijua ikafuata …..akainama kuchukua mkoba wake uliodondoka chini, nami wakati huo huo nilikuwa  nimeinama kumsaidia kuukota, akauwahi kabla yangu,na kama vile anaogopa kuwa nitamuibia akaushikilia barabara mkononi. Na kunifyoza…..sikujali ndivyo palivyo hapo, kama unahasira utaumia mwenyewe bure ,maana humo hakuna kupigana, ukipigana unamwagiwa maji au matakataka…olewako ujifanye mwamba….matusi yote yatakuangukiwa wewe…

‘Saamhani dada yangu, ni njaa tu inatufanya hata tusione mbele,…ukiniazima elifu mbili tu nitashukuru sana…kwanini nanhii….’nikasema namimi nikaporosha neon linalolingana na humo ndani, ambalo nisigeliweza kulitamka sehemu nyingine zaidi ya humo ndani....

‘Elifu mbili kwa kazi gani uliofanya…ukiwa an nguo zako hivyo hivyo…. ,wewe unafikiri pesa ni za kuokota tu hivihivi,…. dume zima huna hata haya, kuombaomba pesa…halafu uanomba mwanamke pesa, kawaombe wanaume wenzako wakuonyeshe mji….’akasema na likafuata tusi la nguoni, na mimi sikujali nikacheka, maana ndio lugha za hapo.

‘Na wewe hutekenywi au shemeji kakuchoka, hujui mapenzi….nipe hiyo elifu mbili, nikaongeze …..’nikatamka tusi na Yule mwanadada akasema kwa lugha ile ile ya mle ndani, lugha ta matusi...

‘Haya chukua hizi hapa usije ukanipa nuksi ya bure maana wewe nina mashaka na wewe, sizani kama….’akasemanalikafuata tusi la nguvu,na mimi nikacheka na kuipokea hiyo pesa huku nikashangaa nikikabidhiwa pesa ambayo sikutegemea,nikaipokea huku siamini macho yangu, nikijua atadai chenji yake, na hapo tukakutanasha macho yetu na Yule mwanamama…akaurudisha mkono wake haraka, utafikiri alishika kaa la moto, ….lakini kwa muda huo nilishaichukua ile noti ya shilingi elifu tano…..

Nilishikwa na mshangao,maana macho yetu yalipokuatana na yule mwana mama ilikuwa kama kaona  kitu cha kumshitua, kwanza aliniangalia mara moja, halafu ikawa kama vile kuna kitu kimepanua macho yake , akayakodoa kwa usoni akaonyesha wazi kuwa anaogopa,kama vile mtu aliyeona kitu cha kutisha,halafau akarudi kinyume nyumehuku akiwa kakodoa macho yam domo,kama vile anataka kupiga yowe,lakini sauti haitoki, na mara akageuka nyuma na kuangalia mlango upo wapi,mbio akatoka akikimbia…

‘Ahsante dada yangu…naku….oh, vipi…’nikasema, na kushikwa na butwaa,na vile vitendo, name nikawa natoa macho kwa mshangao, nikimwangalia huku sijui kimemsibu kitu gani,yule mwanamama, siwezi kumuita mwanadada, labda nimuite mwanamama,ingawaje mwili wake kauweka kiafya, hajajiachia kiasi cha kuonekana mwanamama inaonekana ni mtu wa mazoezi, au ni mtu anayeujua mwili wake vyema, na kuutunza ipasavyo.

‘Oooooooh…..’ndiyo sauti aliyota huku akiishia mlangoni.

Cha ajabu hata ile pochi yake akaiodondosha tena, kwa jisni alivyoshituka, nami nikaikota haraka na kushikilia mkononi, huku nikiwa namfuatilia kwa nyuma,….ulikuwa nimikoba hii ya akina mama, wanayopenda kutembea nayo, lakini ilionekana ni ya bei mbaya, haiendani kabisa na sehemu kama hiyo, nikajiuliza moyoni, kuwa huyu mwanamama, na huu mkoba mbona haviendani,ukiangalia na sehemu yenyewe, au kauiba na alikuja humu kuwakoga wenzake.

‘Wewe dada umedondosha mkoba wako….’nikawa namkimbilia nikimpigia ukelele, lakini ilikuwa kama ndio namfukuza,akawa anakimbia huku anaangalia nyuma, na kila akiniona namfuatilia ndio naye anaongeza mbio, ikafikia mahali akawa anakimbia kabisa kama mtu aliyechanganyikiwa na mimi nikasema,hapana, … dada mwenye huruma kama huyu, hastahili apoteze mkoba wake, na humo ndani ilionekana kuna simu na vitu vyake vingine….nikamfuatilia huku nikimuita kwa sauti kuwa asimama ili achukue mkoba wake…hakusimama,….

Alipofika upande mwingine wa bara bara,akaona bajaji,akaisimamisha na kuondoka nayo,nami nikjaitahidi kumuita kuwa kadondosha mkoba wake,lakini hata hakujali , akaondoka na ile bajaji, nikabakia nimeduwaa, nakujiuliza ina maana haunisikia,na kwanini anakimbia, ina maana ananikimbia mimi,na kwanini anikimbie mimi,…..nikasimama kwa muda nikiwaza, na mara ikaja bajaji na kusimama mbele yangu…..

Sijui kwanini nilifanya hivyo, kwani pale palenikaingia ndani ya ile bajaji, nikamwambia mwenye bajaji anisaidie kuifukuzia ile bajaji iliyoondoka,…kwani Yule abiria mle ndani nina mzigo wake, ..hapo moyoni nikijua sitalipa pesa nyingi zaidi ya ile niliyopewa,  na hata kama nikilipa pesa nyingi, huyo mwanamama, anaoenekana ni mtu mwema, ataniongeza chochote, kwa wema niliomfanyia,….basi Yule jamaa akakubali tukaifutilia hiyo bajaji mpaka tukafika maeneo ya nyumba za wakubwa……wenye nazo….

Ile bajaji aliyokuwa nayo Yule mwanamama, ikasimama na Yule mama akatoka mbio, nakuingia ndani ya nyumba tuliyokuwa tumesimama mbele yake. Kwani na sisi tulikuwa tumeshafika na kusimama karibu na hiyo bajaji,….nafikiri Yule mwanamama, hakujua kuwa nimemfuatilia nyuma na hiyo bajaji ,kwani nikipindi namlipa huyo mwenye bajaji pesa yake ndipo Yule mwanamama aliyeingia ndani ya lile jengo akawa anatoka nje, akiwa na pesa mkononi,akamlipa  Yule mwenye bajaji  pesa yake,na mimi nikawa namsogelea,….

Akageuka kuondoka akiwa na haraka na kukimbilia ndani , na mara akaniona…alipanua mdomo na kutaka kupiga yowe, na alichofanya ni kusema; `mungu huyu hapa tena….ooh’....

Alikurupuka na kukimbilia ndani haraka,na mimi nikasema lazima nikamtoe hofu kuwa mimi sio mtu mbaya,nikaelekea kule kwenye mlango wa hilo jengo. Lilikuwa ni jengola bei mbaya, mageti yenye alama za ulinzi na maneno ya kutisha kuwa kuna ulinzi mkali,mimi sikujali, nikalifikia lile geti na kugonga mlangoni....

‘Wewe ni nani, na unataka nini….?’ Akauliza mlinzi huku akiwa kafungua nusu upenyo wa mlango.

‘Mimi nina taka kumuona huyu mwanamama aliyeingia hapa sasa hivi….’nikasema

‘Hapa haparuhusiwi mtu yoyote kuingia,na huyo mwanamama uliyemuona hana mamlaka ya kuruhusu mtu kuingia hapa,….unasikia ….tunakuomba uondoke haraka, kabla hatujakushughulikia,unaijua jela wewe,utaenda kuozea huko jela sasa hivi…ondoka mara moja eneo hili….’akasema huyo mlinzi.

‘Nilikuwa na mko…kibegi,…..’kabla sijamaliza mlango ukafungwa usoni mwangu na sauti ikasema;

‘Sitaki nikuone hapo nje,….nenda zako, hatuhitaji chochote kutoka kwako…..’akasema na mimi nikaona haina haja, nikageuka na kuondoka zangu,huku nikiwaza hilo tukio , maana huyo mwanamama, alionekana kabisa ananiogopa mimi,hasa nilipomuona kwa mra ya pili, mwanzoni sikuwa na uhakika huo, lakini safari hii ya pili, nikajua mara moja kuwa ni mimi anyenikimbia.

‘Kwanini anikimbie, ninatisha nini….hapana,sizani kukaa jelamiezi hiyonimebadilika kiasi cha kutisha watu, huyu ana lake jingine, ‘nijajikuta nikiongea mweneywe huku nimeushika ule mkoba mkononi, sikujua niufaye nini….

Nikiwa natembea mbali ya lile jengi nikawa nawaza kuhusu haya maisha maana tangu nitoke jela, imekuwa mimi kama kioja fulani, maana huyo sio wa kwanza kuonyesha dalili ya kunikimbia, kila nikikutana na mtu anayenifahamu kidogo,, mtu huyo hunikimbia,na wala hataki kuongea na mimi, nikajiuliza kuna nini,au nimekonda sana,au nina nini cha ajabu cha kuwafanya watu wanikimbie.

Kwa maisha kama haya nikajikuta nikilala kwenye majengo wanayolala wachuuzi au wafayabiashara wanaoleta mizigo toka mkoani,na wakati mwingine nafanya akzi ya kupakua hiyo mizigo na kupata chochote, na siku zinakwenda.

Niliwaza sana, nilipotokea, maana nilikuwa mtu wa watu, nlikuwa na nyumba yangu nzuri, kazi nzuri, lakini sasa nipo mitaani , ombamba,…kweli hujafa hujaumbika, na hapo hapo nikaumbuka siku ile nilipotoka kwenye huo mkasa ulionifanya nisweke jela kwa miezi zaidi ya sita....

*******

Siku ile nilipotoka jela, nilitokea mhakamani, ….moja kwa moja niliongoza kiguu na njia hadi mahali pale palipokuwa na nyumba yangu, nikitarajia nitamkuta mke wangu, ingawaje ni siku nyingi sijamuona, tangu kesi ianza, hakuweza kukanyaga mahakamni, nikajau labda anaumwa, na hata nilipomuuliza wakili wangu, hakunipa jibu la maana, ….alisema hajui mke wangu alipo , mimi nisimuwaze yeye, niwazie kesi yangu.

Nilipotoka jela, sikuwa na mahali pakwenda, zaidi huko nyumbani kwangu,nikatumia pea kidogo aliyonipa Yule mwanadada wakili. Alinigaia hiyo pesa, pale aliponiona nikiwa nimeduwaa, aliponiambia kuwa kuwa,nipo huru, sina hatia, kamamahakailiviyosema, kwahiyo naweza  kuondoka.

‘Naweza kuondoka….?....., ina maana haina haja ya mimi kurudi kule gerezani…?’nikauliza.

‘Haina haja, hukusikia hakimu alivyosema, ….wewe nenda nyumbani kwako , kajipange vyema, uachane na hawo watu , hasa huyo mke wako,…’akaniambia.

‘Ni kweli sijui yupo wapi maana sijamuona akija kweney kesi….’nikasema.

‘Achana naye, chukua nauli hii,nenda nyumbani kwako, kamuommbe mungu wako….maana huko ulipokuwa ukienda sio mahali pema…nakutakia maisha mema,na kama utakuwa na tatizo chukua kadi yangu hii hapa nitakusaidia…’akasema na kunipa kadi yake na pesa ya nauli.

‘Nashkuru sana, na ubarikiwe sana, kweli wewe ni mtu mwema sana….’nikasema huku nikimwangalia kwa uso wa huruma.

‘Usijali yote ni maisha….nia yetu ni kuwasaidia wote,…lakini lengo letu hasa ni kwa akina mama,na nyie wanaume maliojikuta kwenye huu mtego….’akatulia kwa muda, na baadaye akasema;

‘Nakushauri tena, …achana na hawo  watu,… jipange kimaisha na ukijitahidi maisha yatakuwa mazuri bila kutafuta njia za mkato, wengi ndipo wanapokosea, ….utatajirikaje kwa kutumia mgongo wa mwenzako, hali ujue kapataje mali aliyo nayo…..kwaheri tukijaliwa tutaonana tena lkini iwe kwa heri, sio kwa shari, au sio …?’akasemana kuingia kweney gari lake akaondoka zake.

 Nikafika maeneo ya ilipokuwa nyumba yangu, lakini nilipofika hapo nilikuta jengo limebadilika kabisa na limekarabatiwa kivingine,…hutaamini kuwa pale ndipo ilikuwa nyumba yangu,nilifikiri nimpotea, lakini nilipotizama vyema, nikawa na uhakika ni hapo hapo,maana zipo alama nyingine zipo vile vile…..

‘Huyu mwenye hili jengo yupo wapi…?’ nikauliza.

‘Hatujui, yeye anakuja mara moja moja kwa mwezi kuchukua pesa yake,na kuishia zake, hatujui wapi anapoishi,kwanza itatusaidia nini,kama tunalipia kodi yake….mtu kama huyo huhitaji we anakuja mara kwa mara, anaweza akakupandishia kodi,kwanza ukimuona moyo unalipuka paaah, unajau sasa kodi ya watu inahitajika……’akasema jamaa mmoja mwenye duka kubwa la vifaa vya simu.

 Nililiangalia lile Jengo lilivyorabatiwa kwa muda mfupi,moyoni nikasema, kweli watu wana pesa, usiseme hata siku moja, kuwa na kuwa la kibiashara, sio nyumba ya kuishi mtu tena, sikukata tama nikajaribu kuwauliza watu mbali mbali hadi nikampta mtu mmoja anayepajua vyema hapo mahali , ndipo akaniambia kuwa hilo jingo lilikuja kuuzwa kwa muhindi mmoja,alaiyelipa pesa nyingi kwa dadammoja aliyekuwa akimiliki hapo, na huyu dada hajaonekana tena hapa mjini tangu alipouza hilo jingo.

‘Huyo dada umafahamu vyema?’ nikamuuliza.

‘Kwanini nisimfahamu, Yule Malaya…alikuwa akijiita kimwana, kumbe kazi yao ni kujiuza na akimpata bwege anamuweka ndani, na mwisho wa siku anamuibia huyo bwege, …na hata hii nyumba ilikuwa ya bwege mmoja,aliyemchukua huyo kimwana,…eti mpaka wakafunga ndoa, …mwisho wa siku, akatapeliwa…’akasema huku akicheka.

‘Akatapeliwa nyumba nzima,….siamini…’nikajifanya kushangaa.

‘Unashangaa mjini hapa, kashangae juu, ndege inaelea hewani,…., hapa mjini  bwana, kama umekuja leo utashangaa sana. Hii nyumba nakumbukakabisa ilikuwa na bwege mmoja, ambaye alijenga kwa mkopo,nakumbuka kabisa,na huyo kimwana akafanya mambo yake, na watu wao huko sijui wapi, na mwisho wa siku nyumba ikawa yake…’akasemahuyo jamaa.

‘Kweli hapa mjini, ina maana huyo kimwana alikuwa na pesa nyingi sana…au alizipata wapi?’ nikadadisi.

‘Usiniuliza kazipata wapi, wakati nimekuambia kuwa kazi yao ndio hiyo ya uatapeli, inawezekana kuna njia zao walitumia,au alimtapeli mtu mwingine kinamna, kwasababu alipouz ahii nyumba akapotea kabisa, nakumbuka kuna jamaa alikuja kufungua kesi na huyu mhindi akidai kuwa nyumba hiyoni yake, lakini alishindwa kesi.

‘Ohh, kumbe basi hii nyumba ina hsitori ndefu…’nikasema...huku nikigeuka pembeni ili asije akanijua huyu jamaa,ambaye alikuwa akionge huku akaifanya shughuli zake.

‘Huyu bwege aliyekuwa akimiliki hii nyumba mwanzoni sasa hivi yupo wapi…?’ nikauliza.

‘Sizani kamayupo hai, maana hawa akina dada akikutapeli ukajifanya mjanja, utaondoka hii dunia,…sina uhakika kamayupo hai,na kamayupo hai atakuwa jela, au kakimbilia kijijini kuogopakuumbuka…’akasema huyo jamaa.

‘Ukimuona unaweza kumtambua…?’nikamuuliza.

‘Kwanini nisimtambue…kama kweli yupo hai, maana wngi walionaswa na hawo watu, utasikia mara kajiua ,mara kafa  kwa shinikizao la damu,wengine wanakumbwa na kiharusi,….kwakeli Yule jamaa siwezi kumashau,….’akasema na kuinua boksi alilokuwa akijaza vitu.

Akatulia kidogo kama anawaza jambo, halafu akasema; ‘Hata kama kabadilika kimaisha nikimuona tu nitamfahamu…unajua ndugu sasa hivi watu wanahangaika na maisha, hakuna mtu anayejali kuhusu mwingine,  unahangaika kuangalia maisha yako nay a familia yako. Nikuulize kwanini unamuulizia huyo bwege,una shida na yeye…?’ akauliza na safari hii aliinua kichwa kidogo kuniangalia, na haraka nikageuza uso upande mwingine,na kuanza kuondoka, huku nikisema;

‘Sina shida na yeye…..,nilikuwa natafuta sehemu ya kuweka biashara …..sasa naona huku hapanifai tena…’nikasema na kujiondokea hapo haraka, nisije nikaumbuka, na  nilipogeuza kichwa nikiwa mbali, nilimuona yule jamaa akiwa kaduwaaa akiwa ananiangalia, …nikageuza kichwa haraka na kuangali huko ninapokwenda, na sikugeuka nyuma tena, na toka siku hiyo nikawa sitembelei maeneo hayo.


 **********

Nikiwa na ulemkoba wa Yule mwanamama nikaondoka hadi kwenye jingo moja lililokuwa linajengwa, na nikatafuta sehemu yenye amani, nikakaa, hapo nilipokaa, kulikuwa na shomo la maji taka, lilikuwa refu na naona lilikuwa likitumika,….na lilikuwa refu sana, nikaachana nalo na kukaa juu yake, huku miguu nimeiningiza kweney shimo,….nikawaza, sasa nifanyeje, nikakumbuka kuwa sijala,….

‘Oooh,huku kukaa na njaa kutaniua, pesa bado , nikajipapasa, na kujikuta nina elifu tatu,…kabla sijainuka, wazo la kuukagua huo mkoba ukanijia,….sikupenda kufanya hivyo, jela ilishanifunza,..sitaki tena kureeja huko,huko sio pa kwenda, jamani..

Lakini moyo uuitamani kitu, na kitu kikiwa karibu nawe, unashindwa kuvumilia, nikauchukau ule mkoba na kuufungua,….nikakuta simu ya bei mbaya…nikaiangalai,ilikuwa hewani, ina maana kulikuwa na mtu anapiga, lakini mlio ulikuwa hautoki, ….na mara bila kutarajia nikakuta nimeshaipokea ile simu;

‘Ule mzigo nitakuletea huko huko kijiweni,uje na pesa yangu taslimu,….ni mara mbili ya ule, na uwe makini maana mandata wamecharuka, ila hapo kijiweni hawajapashitukia, watumie wale wale akina mama….’simu ikakata……

‘Mzigo gani huo….?’ Nikajiuliza.

‘Nikairudishia pale pale,na kukagua vitu vingine, nilichokuta cha zaidi ni mfuko wa plastic, ndani kulikuwa na mfuko mwingine,una vitu vimefungwa kama vibunda vya binzari, ni unga ungamweupe,sikuangalia zana,maana vilikuwa vingi tu,….moyoni nikasema,ina maana huyu mwanamama na ujanja wake wote anafanya biashara ya viungo vya kupikia,maana hii inaweza ikawa ni hamira....

Nikaufungua vyema, na kutoa kimoja…ulikuwa kama `glucose’ ulaini wake,…nikalamba…mmh,mbona haina aldha, nikatema, na kukirudishia humo,sikuwa na wazo jingine lolote, na kwa vile nilikuwa na njaa,nikaona nitafute kama kuna pesa.

‘Nitachukua pesa….siiibi, nachukua tu kwa gharama ya kuhangaika kwangu,….nikikutana naye nitamwambia….nikachukua elifu kumi,…na mara kwa pembeni nikaona pesa za kigeni,zilikuwa kwenye kimfuko cha pembeni….nikachomoa dola mia,nikaichunguza, nikaiweka kwenye kiatu changu….

‘Ngoja nitaichunguza vyema, huyu mama anaweza akawa ana dola za bandia, ukishikwa nayo unaishia jela….’nikatulia kwaza, nikiwaza…sikuahangaika na huo mkoba tena, maana vitu vingine vilivyokuwa humo ndani vilikuwa vikorokoro vya akina mama,nikaufunga ule mkoba, na kumbe kulidondoka picha mbili za `pasipoti size’, nikaziokota, na kabla sijaitizama vyema, mara kwa nyuma nikasikia sauti, na picha moja ikaniponyoka,nikabakia na moja, sikuweza kuiokota tena, mawazo yangu yakawa kwa hawo watu wanaoongea….

‘Ndio Yule pale….ndio…. yule, Yule….yule pale….’nikageuka,….walikuwa ni askari..’mmh,nikasema hapa ndio balaa la kurudi tena jela,nikauangalia ule mkoba, nikajua hiki ni kidhibiti cha kuwa nimeiba, labda ndio wanaoutafuta….nikageuka kule walipo wale maaskari….kabla hawajanikaribia nikaanza kurudi nyuma, kutafuta upenyo wa kukimbilia.

`Wewe simama hapo hapo….’ Akaamrisha mmojawapo wa wake maafande.

‘Kwanini bwana afande…?’ nikauliza

‘Kuna kitu ulicho nacho, ambacho sio mali yako,….’akasema.

‘Ni kitu gani afande na ni mali ya nani… bwana afande, ….maana…’nikasema na kusogea mbali na wao, ….wakaja hadi pale nilipokuwa nimesimama, na kile kimkoba nimekishika kwa uficho.

‘Ni mkoba wa mama Yule pale aliyesimama pale barabarani,anauhitaji mkoba wake tu,hana haja na wewe,….tunauomba na uishie zako….’akasema huyo afande.

‘Kama ni hivyo tu, haina shida, aje mwenyewe auchukue…lakini sio nyie….’nikasema.

‘Anakuogopa….wewe tupe tumpelekee…’akasema huyo afande.

‘Kwanini aniogope na nitakuwa na ushahidi gani kuwa nyie mtamfikishia….’nikasema na huku nimesogea mbali na wao kama vile naeleeka kule barabarani. Na kule alipokuwa Yule mama nilimuona akiwa kama anarudi kinyume nyume….hasa pale aliponiona nikiwa namsogelea yeye….

‘Yule afande akatoa bastola, nakusema…lete huo mkoba au nitakushughulikia kama jambazi…’akasema na mara akaja afande mwingine aliyekuwa mwanzoni kasimama na yule mama akawaambia;

‘Msimuue,…..hakikisheni mnauchukua huko mkona tu na yeye muwacheni aende zake,…‘ akasema.

Niliposikia hivyo kuwa kumbe hawana haja ya kuniua mimi,nikaanza kuwachezea shere, walipokuwa wakinifuata huku, kwa kasi wakitimiza amri ya bosi wao nakimbia upande mwingine kuwakwepa,…..wakija huku napitia huku, na wakati nakimbizana nao, nikajikuta nimefika pale palipokuwa na lile shimo la maji taka,.na muda huo wazo langu halikuwa limekumbuka hilo shimo tena,….tahamaki nikajikuta nimekanyaga sehemu ya lile shimo, na kuporomoka  kwenda ndani, ...nikazama, na bahati nzuri, mikono ikawahi kudaka chuma kilichokuwa kimiejitokeza, nikabaki naelekea ndani ya hilo shimo….

‘Aaaah,  nisaidieni, ....mungu wangu……’kukuru kakara, ule mkoba ukaniponyoka na kutumbikia ndani ya lile shimo,na hata Yule afande aliponikaribia naye huyo akaserereka,na kutumbukia…hata alipojaribu kuudaka ule mkoba ikashindikana,tukawa tunauangalia ukizama,…huku tumeshikilia kile chuma, ….haraka nikajikakamua na kupanda juu….nikatimua mbio…

‘Wewe mpumbavu kweli….’akasema huyo afande, ikajaribu kuutoa mguu wake ulionasa, na mimi bila kusema kitu nikatimuka mbali kabisa na wao, …..nilipogeuka kuwaangalia, niliwaona wakiwa wamejikusanya wakiangalia ndani ya lile shimo,na Yule mwanamama alikuwa mmojawapo.

Wazo la kuwafuata likanijia, nilitaka nimuombe Yule mama masamha ….nikawa nawajia, …yule mama akaniona akawaambia kitu wenzake….wenzake wakasimama kuniangalia, ….wakaniona nawajia, ….mara wote wakawa wanarudi kinyumenyume…mara wakageuka, wakwaza kukimbia alikuwa Yule mama, halafu mara wale maafande na wao wakafuatia na kuanza kutimua mbio….

 Nikabakia nikishangaa, ….vipi ina maana hata maafande wananiogopa…kuna nini jamani…..nikakumbuka ile picha niliyokuwa nayo,….bado ilikuwa mkononi,nikaigeuza sehemu inayoonyesha sura…..kwanza nikashituka,…nikakadoa macho kuiangalia vyema…..mapigo ya moyo yakaongezeka…..

Je kwanini wanamuogopa huyo jamaa…na je huyo mwanamama ni nani?


WAZO LA LEO: Kumbuka kumshukuru mungu kwa kila jambo, liwe la heri au la shari liwe jema au baya, kwani yote hutokea ili iwe sababu ya jambo fulani.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

samira said...

m3 na mimi nafikiri ni kwa nini watu wanamuogopa jamaa huyu sipati jibu lolote
i cant wait kujuwa mungu akujalie kila kheri m3

Rachel Siwa said...

Ndugu wa mimi kazi yako ni yakipekee, Mungu azidi kukufunulia, pia Ahsante kwa WAZO LA LEO!!!Pamoja Daima ndugu wa mimi!!!!!!