Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, April 23, 2012

Hujafa hujaumbika-26




 Ilikuwa muda wa saa sita za usiku, eneo lote lilikuwa kimiya, kilichokuwa kikisikia na sauti za mingurumo ya wafungwa, mimi sikuweza kupata usingizi kabisa, kama nilivyokuambia nilitakiwa nipambane kiume, nilikuwa nasubiri huyo mtoa roho aje tukutane naye…lakini kulikuwa kama siku nyingine nami nikakata tamaa na kujua kuwa huenda hakimu hakufikishiwa ujumbe wangu…..nikajibanza pale nilipokuwa nimejificha.

Nilikumbuka jinsi nilivyohangaika ili nimuone hakimu, lakini haikuwezekana, na matokea yake nikakutana na Yule wakilianayetetea akina mama, na hata yeye alikuwa kama haniamini tena, nikakumbuka jinsi alivyokuja wakati nikiwa nimepiga magoti mbele ya Yule askari.

‘Vipi huyu jamaa ana matatizo gani mbona anapiga magoti kama anatubu dhambii zake…?’ .

‘Eti anataka kuonana na hakimu…?’ akasema Yule askari kwa kebehi.

‘Unataka kuonana na hakimu,…? Mbona muda mwingi ulikuwa naye ndani ya mahakama, una lipi jipya la kuonana naye, na wakili wako yupo wapi maana yeye ndiye njia yako ya kufika kwa hakimu…’akasema huyo wakili.

‘Ni muhimu nionane naye, na hili nataka niongee naye mwenyewe, sio kwa kupitia kwa wakili, …maana hakuna ninayemuamini kwa sasa….’nikasema.

‘Kuna jambo gani unataka kumwambia hakimu, ….na kwanini usimwamini wakili wako?’ Akauliza na baadaye akamgeukia Yule askari na kumwambia ampe nafasi aongee na mimi. Yule askari akasema muda wa kuondoka umefika hakuna nafasii tena ya maongezi…aongee harakaharaka..’akasema afande.

‘Unasikia anavyosema afande, hata wao sio kosa lao wanafuta sheria,kama kuna kitu muhimu wewe niambie harakaharaka, nitajitahidi nifikishe huo ujumbe kwa hakimu…kuna jambo gani sema haraka gari linawasubiri nje…;akasema huyo mwanadada.

‘Ni kuhusu usalama wangu, ….sizani kama nitaweza kufika kesho, sihitajiki tena kusimama mahakamani , sina amani tena, nimeonekana msaliti…nimesikia kwa amsikio yangu wakili akipigiwa simu….’Nikasema.

‘Tulishakuambia hilo hukutuamini, sasa unaona….lakini usiwe na wasiwasi, hayo tunayajua, na tunayafuatilia kwakaribu sana…na kuhusu huko mahabusu,tutaangalia jinsii usalama wako utakavyokuwa, lakini wewe sio mtu wetu, tunaogopa kukuingilia….’ Akasema na halafu aakmgeukia Yule afande;

‘Afande hili ni muhimu sana, kama hutaliweza tunaomba utuitie muhusika, huyu mtu ni muhimu sana katika kesi yetu na huko gerezani anahitajika awekewe ulinzi mkubwa…’akasema huyo mwanadada.

‘Mbona huko kuna ulinzi wa kutosha…hakuna shida kabisa, hata mimi naweza kufuatilia hilo kuhakikisha kuwa hakuna matatizo,mbona ndio kazi zetu….’akasema huyo afande.

‘Kama unatuhakikishia tunaomba utuhakikishie kimaandishi…maana kama litatokea lolote wewe utakuja kujibu mahakamni…’akasema huyo mwanadada.

‘Kama ni hivyo ngoja nikaonane na mkuu wa huu msafara….’akasema Yule afande na baadaye akaja na mkuu msafara,wakaongea na huyo mwanadada kwa siri pembeni, sikujua wameongea nini, na baadaye tukaondoka hapo mahakamani.

Tulipofika gerezani, tukaendeela na shughuli zetu kama kawaida na muda wa kulala ulipofika, kila mmoja alikwenda mahali pake, lakini nilipofika chumba ambacho nilikuwa nalala…nikashikwa na butwaa, kwani kulikuwa na mtu mpya…labda ni mfungwa mgeni..labda,labda..zikawa nyingi, lakini sikuwa na amani.Nikaingia ndani….

 Chumba hicho tulikuwa wawili nilipofika mara ya kwanza,..lakini siku mbili hivi za karibuni , nilikuwa nalala peke yangu kwani mwenzangu ambaye tulikuwa naye hapo alihamishwa baada ya kusikilizwa kesi yake na kuonekana ana hatia. Sasa leo nafika hapo namkuta mtu mgeni,na huyo mtu akawa kalala sehemu yangu. Kwasaabbu nilishakuwa mwenyeji nikauliza kwa ukali.

‘Mbona umekuja kulala mahali pangu….?’ Nikauliza.

‘Wewe una kwako hapa, hebu ishia huko nisije nikakumaliza…kila mahali kuna mtu,mimi nitakaa wapi…kwanza utoke humu ndani, humu nalala peke yangu, sitaki usumbufu, au nikuonyeshe kuwa mimi ni nani, huko nje wananijua, hata hivyo sizani kama nitamaliza siku mbili hapa….’akasema huyo jamaa na yeye kwa ukali, na mimi kwa kuogopa purukushani, na kwa vile nilikuwa bado na wasiwasi wa kuuliwa usiku, nikatafuta sehemu nyingine, …nikjabanza kwa shida shida, nikiwaza jinsi ya kupata sehemu nyingine kamaile.

Kwa hali ilivyo, usingizi haukuja kabisa, kwani sehemu hiyo niliyojibanza,sio sehemu rasmi, na ukakaa kama hakuna chumba maalumu, ni hapo hapo kwenye hicho chumba, lakini ni kwa nje kando kidogo, na sio sehemu nzuri, lakini nikaona nijibanze hapo hadi kesho, na nilipapenda kwasababu watu hawakuoni wakipita kwa nje, nikajifunika vipande vya godoro,….

Hata hivyo kwa shida shida usingizi ukanijia na mara nikajikuta nikitembea pembeni mwa ukingo,  ni kama njia nyembamba….ipo kama daraja, lakini ni njia, upande mmoja ni ukingo wenye shimo refu ajabu.

Nilikuwa naangalia kwa kujiiba, maana hata kuangali lile shimo unaogopa,unaweza ukapatwa na kizunguzungu ukatumbukia, na kwa kujiiba huko nilijaribu kuangalia urefu wa lile shimo , lakini sikuweza kuona mwisho wake,lilikuwa ni shimo refu ajabu, na pana sana, ina maana huko mbele lilipoishia kwa upana huwezi kuona, ilikuwa ndio kama mwisho wa dunia.

Ilivyo nilitakiwa kupita pembezoni hadi mwisho wake, ili nifike barabara inyokwenda huko ninakotakiwa nifike,na walasijui ni wapi, na upande mwingie ambao nilikuwa sijauona, kulikuwa mto wenye mamba na kila aina ya wadudu , ….na ukijsogeza karibu na ukingo wa huo mto, harufu yako ikiwafikia hawo wadudu , mamba na mijoka wanaweza kukurukia, kwahiyo hutakiwi ukaribie huko ukingoni,….

‘Huku ni kuzimu nini…..?’nikauliza.

‘Unauliza jibu,…’sauti nyingine ikanijibu, lakini sikumuona aliyenijibu, huenda alikuwa nyuma yangu,na huwezi kujigeuza, unaweza ukakosea mguu ukakanyaga kusipofaa ukateleza, kwahiyo wewe unachotakiwa ni kuangali mbele..

Mara ukasikika upepo,….na kelele zikaanza kusikika kwa nyuma,ina maana ilikuwa ni vilio, labda ni kwa wale waliokosea wakadondoka, au walikamatwa na mamba, ….mikoromo ya watu wakikata roho, huwezi kugeuka, wewe unatakiwa kwenda mbele, na muda tulipangiwa unaanza kuisha….

‘Mkichelewa kiza kikiingia wadudu kama mamba wanatoka mtoni, mtashindwa kupita…kwani watakuwa wameziba njia wakisubiri mawindo….’tuliposikia hivyo, tulianza kusukumana, na hapa watu wakaanza kudondoka huku na kule, na hata aliyekuwa nyuma yangu akawa anhema na kukoroma kwa uwoga, nikamwambia asinisogelee karibu kwasababu anaweza kunisukuma,lakini hakusikia akawa anakoroma kama samba…

‘Bwana wee  acha kukoroma, unawaita simba….’nikasema, lakini hakusikia, na ile sauti ya kukoroma ikazidi hata ikanitisha, nikasema huyu asije akawa ni samba yupo nyuma yangu, ngoja nimwangalie, nikageuza kichwa, na pale ikawa ni kosa, maana nilipogeuza kichwa, mguu wanguukakosea njia, na haukukanyaga sehemu inayostahili, nikajikuta nimekanyaga hewa na niliojaribu kujiweka sawa huyu jamaa anayekoroma akanisukuma…..

Nilijikuta nikielea hewani,…ina maana nilikuwa nikizama kwenda huko kuzimu, kwenye shimo lisilolokuwa na mwisho,nikaanza kupiga ukulele….

‘Wewe mbona unasumbua watu…mikelele ya nini..’sauti ikasikika, kwa muda ule sikujua ni ya nani, haraka haraka nikainuka..ooh, kumbe ilikuwa ni ndoto…nikakumbuka kuwa nipo mafichoni,nikajibanza vyema,nikitafuta usungizi tena.

Mara wakaja majamaa wanne, mmojawapo alikuwa mku wa wafungwa hapo gerezani, akasogea hadi pale alipolala Yule jamaa, ambapo nilitakiwa nilale mimi,  akagonga na rungu lake, kwa nje kwenye nondo zinazotuzunguka,maana vyumba hivyo vimezungukwa na nondo, ukitaka kuotoka unafunguliwa na afande, wakamuamusha Yule jamaa na mazungumzo yao nikayasikia wakiongea

‘Wew Unaitwa chumba cha wageni…’nikasikia sauti ikisema,huku Yule msemaji akiwa kashika ufunguo, kuonyesha kweli anaweza kuufungua huo mlango,lakini nikajiuliza usiku kama huu kuna nini hado mtu aitwe chumba cha wageni. Nikasubiri kusikia zaidi….
‘Chumba cha wageni usiku huu…?’akauliza huyo mfungwa kwa hasira.

‘Ndio…usiki huu,wewe unaujua usiku hapa ….unasikia  afande anakuita….’akasema Yule mkuu wa wafungwa.

‘Mimi huko siendi…’akasema Yule mfungwa.

‘Unaleta ubishi sio…unafikiri bado upo uraiani, hapa ni amri amri….hujajifunzamisha ya haa muda wote huu, au kwa vile hatukuwahi kuja kukukaribisha ulivyofikahapa..sasa tutakukaribisha rasmi,…..’akasema huyo mkuu wa wafungwa, alikuwa pande la jitu, na pembeni yake wapo wasaidizi wake na wao ni mijitu inatisha, …..

‘Mimi huko siendi na kama ni mgeni mwambieni nitaonana naye kesho..’akasema Yule mfungwa naye alionekana ana mwili, sio haba, lakini huwezi kuwalinganisha na hawo jamaa wengine.

‘Sio mgeni ni afande anakuita..hujatusikia au huna masikio, ..ngoja tuingie huko tukuzibue hayo masikioa’akasema huyo jamaa huku akifungua mlango.

‘Nimesema huko siendi kama ni kuniua niulieni hapahapa…maana nyie mna lenu jambo…hata hivyo nimeshachoka na maisha, ila ole wenu, nitakwena na mmojawenu…’akasema huyo jamaa akijiweka tayari.

‘Nani kasema anataka kukua wewe,…unaleta uzushi hapa ndani..’akasema huyo mkuu wa walinzi.

Mara akaja afande mmoja, akauliza kuna tatizo gani, yule mfungwa akajitetea kuwa hawo jamaa wanamwambia kuwa kuna mgeni wake chumba cha wageni,usiku kama huo,na ahwaamini kuwa kweli kuna mgeni, huenda wanataka kumfanyia kitu kibaya….

‘Tumemwambia unamuita  afande,….lakini analeta ubishi..’akasema huyo mkuu wa wafungwa na Yule afande akawaangalia kwa hasira wale jamaa na baadaye akamgeukia huyo mfungwa na kumwambia;

‘Ina maana hukusikia ujumbe wangu kuwa ninakuita….?’ Akauliza huyo afande

‘Lakini afande muda kama huu ni wa kulala, mnaniamusha usiku usuki, kuna nini cha muhimu,….mbona ni kinyume cha sheria,sio kwasababu tupo hapa ndio mchukue sheria mkononi mwenu,sio wote wenye makosa hapa, wengine tumeshikwa kimakosa…kuna nini unaniitia muda kama huu?’ akauliza.

‘Hapa unafuta sheria hata kama ni saa ngapi ukiambiwa kuja unakuja mara moja…hujaja kulala hapa kamaulikuwa unataka kulala ungelilala huko nyumbani kwako, ….’akasema huyo afande.

‘Sasa mimi huko siendi afande,…fanyeni lolote mnalotaka kufanya….’akasema huyo mfungwa.

 Wale jamaa waliposikia hivyo, wakamuiingilia humo ndani na kuanza kumbeba juu, juu, na jamaa hakukubali, kukatokea mapigano,….ilikuwa vurumai, lakini kwa vile wao walikuwa wengi wakamdhibiti, na ilichukua nusu saa, Yule jamaa akawa chini sakafuni,na mara wale jamaa wakato mbio,na kukimbia, na Yule afande akasogea pale alipolala Yule mfungwa na kumgusa kwenye shingo, nafikiri ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kafa au vipi.

 Baadaye Yule afande akaondoka..humo nilipokuwa nikawa natetemeka kwa uwoga, nikazidi kujibanza, maana kesi ianweza kunigeukia mimi kuwa ndiye niliyeua, lakini mara Yule afande akarudi na maafande wenzake wakamchukua huyo mfungwa,akionekana kabisa hayupo hai,….moyoni nikashukuru mungu, nikijua kuuwa huenda lile lengo lilikuwa kwa ajili yangu sasa sijui ilipangwa, au ni mungu mwenyewe kajalia ikatokea hivyo.

Siku ya pili yake nikashikwa na homa kali sana, ikabidi nipelekwe hospitalini, huko nikapata mapumziko chini ya ulinzi, hadi jioni nikajikuta hali ina nafuu, na kuruhusiwa kurudi gerezani, nilipofika huko gerezani nilijaribu kuuliza wenzangu kama wakili yangu alifika, wakasema hawajamuona, nami sikujali sana, na kwa vile nina kibali cha kazi ndogo ndogo, nikawa nimepumzika ndani ya gereza hadi usiku ukaingia.

Sikulala kabisa ile sehemu yangu ya kawaida,nikichelea kukutana na hawo jamaa waliommaliza mwenzetu, na cha ajabu sikusikia lolote kuhusu huyo mwenzetu, na hata nilipowauliza wenzangu, hawakutaka hata kuliongelea, kama vile wanaogopa kuliongelea hilo jambo , kuwa wakiongea na wao litawakuta. Nami nikaona haina haja ,ni bora nijikalie kimiya nisubiri nini kitatokea baadaye. Nilitafuta sehemu nyingine na kuifanya ndio mako yangu mapya, hadi kesho yake asubuhi.

Majina ya wanaokwenda kwenye kesi zao kwa siku hiyo yakaitwa,lakini cha ajabu sikusikia kabisa jina langu likitajwa,nikashangaa maana nilikuwa na uhakikakabisakuwa siku hiyo ndiyo siku ya kesi yangu,licha ya kutokuoenekana kwa wakili wangu,….nikaona hapo kuna jambo,nikasubiri hadi kila kitu kilipokuwa tayari nikaenda kukutana na mkuu wa msafara.

‘Afande mimi nina uhakika leo ndio siku yangu ya kesi, lakini jina langu sijalisikia likitajwa…’nikasema.

‘Labda kesi yako imeahirishwa,  jina lako nani maana mimi nimekabidhiwa hii orodha leo asubuhi nilikuw akituo kingine, na mwenzangu ambaye ni mweneyji hapa kapatwa na dharura, kwahiyo sina uhakika zaidi na mambo ya hapa.

‘Naitwa Mtoto wa Msomali…’nikasema na huyo afande akaangali majina na alipofika sehemu ya jina langu akakuta limepigiwa msitari mwekundu, akaniangalia kwamakini, na muda huo huo dereva akawa anapiga hino,kwani tulikuwa  tunachelewa.

‘Mambo ya hapa bwana,…mimi nhukulia juu kwa juu, kuwa nitakuwa mkuu wa msafara lakini dereva anajiona yeye ndiye mwenye mamlaka,….na mambo mengine sijakabidhiwa, lakini hakujaharibika kitu tutatumia uzoefu,…haya kaingie kwenye gari  twende, tutajua hukohuko….’akasema na mimi nikaingia kwenye gari.Na Yule mkuu wa msafara akaomsogelea mwenzake  na kuchukua nyaraka za kumbukumbu akawa anaziangalia na baadaye akawa anateta na mwenzake, na wakawa wanaonyeshana lile daftari na nyaraka lenye majina na mara wakageuka kuniangalia.

Baadaye kukawa na mambo mengine mengi ya kufuatilia, na kwa vile Yule afabde alikabidhiwa mambo mengi juu kwa juu, hakuwa anayajua ilibidi kila mara kwenda kuuliza na kufuatilia na baadaye tukaondoka kwenda mahakamani. Tulipofika mahakamani Yule mkuu wa msafara akanichukua hadi chumba maalumu, wanapowekwa watu ulinzi mkali, akasema;

‘Wewe uje huku,maana mambo yako yana utata, ni kweli kuwa leo ni siku yako ya kesi,lakini maelezo yaliyopo hapa yanaonekana kunichanganya,  cha ajabu inaonekana kuwa wewe haupo hai…..sasa sijui nini kinaendelea,….itabidi nifuatilie swala lako kwa karibu,na  kwahiyo utakuwa kwenye ulinzi mkali mpaka nionane na wahausika….’akasema na kuniangalia kwa makini,akachukua jaridalenye picha yangu,akalitaizama na karatsi iliyoweka hapo akaisoma na kuniangalia machoni. Akasema.

‘Sawa wewe utakaa hapa na usije ukajidanganya kwa lolote lile, upo kwenye ulinzi mkali,….tusubiri maelezo zaidi…wewe kaa hapa….nitakuja baadaye .’akasema huku  akiondoka kufuatlia maswala mwengine.

Siku ikaanza na kesi yetu ilikuwa ndiyo ya kwanza,na watu walijazana kama kawaida, ingawaje kilechumba kilikuwa sehemu ambayo huwezi kuona vyema nje, hata hivyo nilijitahidi hadi nikapata sehemu yenye upenyo na kuweza kuona nje.Pale nilipokuwa nimewekwa ni sehemu ambayo mawakili hukutana kwa dharuara labda kwa kujadli jambo au kuhifadhiwa wafungwa hatari.

‘Huyu ni nani….mbona hakuna orodha ya wafungwa hatari…?’ Akauliza mwendesha mashitaka, na wakili wa mshitaka akaniangali a kwa makini,halafu akageuka upande wa pili,…akiwa kashikwa na mshangao, na wakati huo Yule mwanadada wakili alikuwa akiingia ndio anaingia hapo kwenye chumba, ilionekana walikuwa na kikao chao maalumu,…akaingia moja kwa moja pale tulipokuwa, akasalaimiana na wenzake, na kusema;

‘Unajua hapa nilipo nimechanagnyikiwa, na bado nasikitika sana moyoni, na najuata sana, maana siku ile ya mwisho wakesi hii,Yule mshitakwa namba moja,aliniambai kuwa ana wasiwasi na uaslaam wake kuwa watamua hawo wenzake, na mbinu hizo zitafanyika huko gerezani, ….sikumwamini sana, kama mjuavyo kuwa ni mtu niliyemtegemea mwanzoni , lakini alikuja kunigeuka….sasa’ Akasema na akaingiwa na wasi wasi na mimi, maana alichotaka kuongea pale huenda hakikutakiwa kusikiwa na mtu mwingine, kwanza, aliangalia saa yake.

‘Kwahiyo kama ulivyonielezea jana, tutaendelea kama kawaida, bila hata ya yeye….si kila kitu kipo sawasawa,  ?’akauliza mkuu wa mashitaka.

‘Ndio kwasababu ushahidi wa kutosha tunao,ila Yule mwanamama ambaye ndiye kiongozi,wa haya yote, na kuwatumia watu wengine, katoweka kinamna,…. tangu jana haonekani alipo,licha ya kupokea amri ya mahaka kuwa awepo leo hapa mahakamani kama shahidi…hatukuweza kumkamata moja kwamoja, kutokana na kesi yenyewe ilivyo,…lakini kwa mtindo huu inabidi atafutwe  na akamatwe,….’akasema Yule mwanadada.

‘Kibali kila kitu si kipo tayari…sasa mnasema tena haonekani,…jamani,muwe makini na hili, mimi sio kazi yangu kufuatilia kila kitu, mimi nataka mkifika hapa kila kitu kipo tayari,tunaweka mambo sawasawa,…sasa tuanza kuongea maana muda unakaribia….’akasema mkuu wa mashitaka.

‘Lakini jana tulikutafuta sana, ukawa na …’akasema halafu mara akageuza shingo kuangalia uapnde wangu, kwani muda wote huo alikwua hajaniangalia, akaniona…..’alaivyoshituka karibu adondoshe lile jarida alilokuwa kalishikilia mkononi, akaniangalia kwa makini halafu akanisogelea na kuniangalia  usoni, akafungua jarida alilokuwa kalishikilia na kuanglai kitu,halafu akawageukia wenzake, na baadaye akanigeukia mimi wenzake wakafanya hivyo hivyo…

‘Wewe ..mbona, …..sielewi, usiniambie kuwa,…mpo mapacha,maana dunia hii ina mengi…’akasema Yule mwanadada.

‘Kwani kuna nini…maana toka huko gerezani kuna utata,jina langu halijaitwa, na kwenye orodha jinalangu limekatwa kwa wino mwekundu,na mkuu wa msafara naye hajui zaidi…sasa kuna ninikinanendelea…?’ nikauliza.

‘Ahsante sana mungu, maana nilishaanza kujijutia, siku ile nilimpakazi yuleafande kuwa ahakikishe kuwa upo salama, na siku hiyo hiyoi huyo afande akapatwa na dharura na kwendakwao,….nilikuja kupata taarifa siku ya pile yake wakati tukio lilishatokea,…’akasema huyo mwanadada.

‘Tukio gani…?’ akauliza mkuu wa mashitaka.

‘Mkuu huyu ndiye mshitakwa mkuu, ambaye tulipata taarifa kuwa kajiua…kumbe haikuwa hivyo, nafikiri kuna makosa yalifanyika huko gerezani,na wahusiak wa huo mpango wanajua kuwa imekuwa hivyo, ….inabdi uchunguzi wa haraka ufanyike,na Yule mlinzi wa siku ile, akamatwe akahojiwe….’akasemahuyo wakili.

‘Hiyo siyo kazi yako,ongea kuhusu kesi ya leo, ..’akasema mkuu wa amshitaka.

‘Kesi ya leo, iendelee kama kawaida, na mengine tukatete ndani..’akasema na wakachukuana huko ndani mimi nikabakia palenikiwa an ulinzi mkali, huku moyoni nikijiuliza nini itakuwa hatima yangu, ….

WAZO LA LEO TOKA KWA MDAUHakuna jambo litamkuta mwanadamu isipokuwa limepangwa na Mwenyezimungu muweza wa kila jambo. Hivyo Utashi wa binadamu hauna nafasi, mbele ya makadrio ya mweneyzimungu. Kwani yeye kila alipngalo liwe huwa.


NB Shukurani kwako mdau,na wewe kama una wazo lako unataka liwe hewani litoe ili kunogeza kisa chetu, na kama inawezekana liendane na kisa cha siku hiyo.

Ni mimi: emu-three

6 comments :

samira said...

m3 ya leo kali inasikitisha lakini alipangalo mungu binadamu haliwezi na pahala popote ikisimama haki basi ushindi upo
huyu kaka yamemkuta nampa pole
nawe m3 unajitahidi kuwa na sisi
siku njema dear

Rachel Siwa said...

Mmmmhh kazi nzuri ndugu yangu,pongezi tele,daima mbele.Pamoja sana sana ndugu wa mimi!!!!!

Anonymous said...

Ngoja mie niweke neno la leo, maana umetuacha juu ya mawe leo, yaani nilikuwa natamani kuendelea kusoma zaidi na zaidi mara ghafla vuum kimya.

Neno la Leo

Hakuna jambo litamkuta mwanadamu isipokuwa limepangwa na Mwenyezimungu Subhana wa Taala. Hivyo binadamu wanajisumbua tu sijui nimfanye nini nani sijui nimtoe roho nani hakuna anayeweza kuyafanya haya kama Mwenyezimungu hakupanga.

emuthree said...

Nashukuru Samira tupo pamoja

emuthree said...

Ndugu wa mimi tupo pamoja

emuthree said...

Wazo la hekima hilo nitaliweka, shukurani sana