Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, April 4, 2012

Hujafa hujaumbika-17



Siku hiyo kabarua karibu kiote majani, maana nilifika kazini mapema, nikawajibik ipasavyo, na kumaliza kazi zangu mapema kama kawaida yangu, nikaona kwa vile nimemaliza kazi mapema, ngoja nikamuone huyu Muhindi anipe mshiko wangu,nikahangaike kwingine....

Nikafika ofisini, huko mara nyingi sisi vibarua haturuhusiwi kufika labdakwa dharura au kuja kulipwa posho yako , mimi sikujali, nikaenda tu, na bahati mbaya nikamkuta mkewe, mwenyewe alikuwa katoka;

‘Weye mbona hufanyi kazi....wakuja huku kufanyia nini..?’ akaniuliza huyo mke wa bosi akiniangali akwa makini.

‘Nimemaliza kazi yangu, nataka malipo na kama ipo nyingine naweza kufanya maana bado muda upo, lakini ukimaliza kazi yako unalipwa kwanza, kabla ya kuanza kazi nyingine...’nikasema.

‘Unajua kazi sana weye, nitakupelaka kwenye duka yangu...na weye nasikia ni mume wayule dada mrembo....?’ akaniuliza.

‘Dada yupi, maana wapo dada wengi..?’ nikadadisi.

‘Yule anaitwa Kimwana....anakuwa pale mapokezi...?’ akauliza huku akisinisogelea.

‘Aaah, ndio ni mke wangu...’nikasema.


‘Unaju akuna jambo nataka kukwambia,....mkewako hana tabia nzuri....nimemfumamara nyingi akiwa na mume wangu, sikujali sana...maana inatakiwa uwe na ushahidi...nimepanga siku nikimfuma, nammaliza kabisa....atajua mimi ni baniani au muhindi...’akasema huku akiniangalia machoni.

‘Mimi sijui hayo....’nikajitetea,na mara akawa ananishika shika,....ooh, nikasema yale yele....nikarudi nyuma na kumwangalia machoni , nikiwa na wasiwasi, na kabla sijasema kitu akasema ;

‘Kamamkewako ananiibia mume wangu na mimi nitamuibia mume wake, unasikia...utakuja kufanya akzi kwangu,...’akanisogelea na kutaka kunishika, na mara mlangoukafunguliwa, wakaingia mume wa huyo mwanamke namkewangu.

‘Wewe unafnya nini huku ofisini,nilishawaambi mje huku kwa taarifa maalumu....’akasema huyu bosi huku akituangalia kwa mashaka, na hata mke wangu naye alikuwa kaduwaa pale mlangoni.

‘Huyu nimemuita mimi, nataka anisaidie kazi kwangu, kule dukani, hapa keshamaliza mpe helayake halafu tunakwenda kule dukani kwangu...’akasema mkewa wahuyo bosi.

‘Kazi bado, ipo kazi mingi hapa ya kufanya, ...’akasema huyo bosi.

‘Kamaipo kazi atafanya mtu mwingine, huyu namchukua mimi, umenisikia vyema, na huyo dadamrembo anakuja kufanya nini huku ofisini...?’ akauliza huku akimwangalia mke wangu.

‘Kuna kazi nataka akaifanye....unajua wiki inayokuja itakuwa ya biashara, sasa lazima ajue jinsi y akuwapokea wageni ...’akasema huku akitoa jarida kubwa lenye picha.

‘Simtaki humu ....sitaki awe anaingia humu, unanisikia, ....weye mwanamke, sitaki uwe unaingia humu ofisini, kama unataka kumpa kazi kampe huko mezani  kwake,na nakuonye tena, kama siku nikiwakuta tena na mume wangu....utajua mimi ni nani...’ akasemahuyo mama.

‘Mimi nafuta maagizo, kaniita kama bosi wangu ningelifanyaje mama mimii sina nia mbaya...’akajitetea mke wangu.

‘Ni hapo nikiwafuma, sitajua kuwa ulikuwa an nia mbaya au nzuri, utakayeumia ni wewe...’akasemana kunishika mkono tuondoke naye, nikasema sijalipwa hela yangu ....

‘Mpe hela yake nataka kuondoka na huyu mtu...’akasema huyo mwanamama,na mumewe akafanya haraka kunilipa pesayangu, na hapo ndipo nikajua kumbe yule mwanamkendiye mweney mamlaka yote ya kazini hapo.

 Bahati tulipotoka kukaja wageni wa huyo mama, ikabidi zoezi hilo lisahaulike, na baadaye akaniambia niondoke tutaonana kesho, basi nikarudi nyumbani mapema.

Nikiwa na vijisenti vyangu, nikapitia gengeni kununua chochote na kila nilivyopiga amehsabu helaikawa haitoshi, nikajiuliza hivi wanawake wanawezaje maana ukimpa pesa, anaweza kununu akitu ambacho mimi nimeshindwa, nikaishia kanunua bamia na nyanya kidogo ili siku ipite, nikazunguka huku na kule kutafuta kingine chochote kwa bei ndogo lakini vitu vingi bei hazikamatiki,...

‘Kweli maisha magumu, wakati nipo ofisini hali kama hii nilikuwa siioni, ukipita sehemu kama hizi unanunua hata kuuliza bei,....leo kitu kidogo tu, nabishana na hawa kina mama, ambao nao wanatafuta riziki yao, kweli maisha ni kupnda na kushuka..’nikajikuta nikiongea mwenyewe kama mtu aliyechanganyikiwa.

Nilipofika nyumbani niliwakuta wazee wamekaa nje,,kwakuwaanglia tu usoni, niligundua kuna jamabo,..kwani mimi niliondoka mapema kabla ya mke wangu, kwahiyo inawezekana kulikuwa na kutoelewana kati  ya mke wangu na wazazi wangu,moyoni nikasema, hivi hali hii itaisha lini, ina maana mke wangu haoni kuwa hawa ni wazazi wetu, anatakiwa kuwatendea wema, kwanza wamechoka wanastahili kupumzika, lakini sio kuwafanyisha kazi kama vijana.

‘Shikamooni wazazi wangu, mbona mpo hivi, ....?’ nikauliza

‘Hilo sio la kuuliza, ulipondoka hapa mlipanaga mtuseme ili tuondoke wenyewe....?’ akasema baba.

‘Mbona mimi sielewi hilo baba, mimi nifanye hivyo nimechanganyikiwa au ....kwani kulitokea nini huku nyuma?’ nikauliza.

‘Huoni tupo nje, tumeambiwa mgeni siku zake ni tatu, sisi tumeshakaa zaidi ya mwezi, nab ado hatufanyi kazi, kazi ni kusubirii kula tu...maneno mengi, sasa tukaona ngoja tukusubiri hapa nje, ili tukuage, hatutakosa sehemu ya kukaa....’akasema baba.

‘Hapaan hapana twendeni ndani, hilomimi sikubali,kwanini awafanyie hivyo,kwani hapa ni kwake, .....twendeni tukaongee ndani, na haondoki mtu hapa,kamanikuondoka aondoke yeye...’nikasemakwa ukali.

‘Aondoke yeye wakati kasema nyumba hii ni ya kwake, wewe upo upo tu,umeshindwa kulipia deni, yeye keshalipia na hati miliki inayoonyesha umiliki wa nyumba katuonyesha....ina jina lake na kila kitu chake....wewe umelala tu,ina maana hujui hilo...?’ akauliza baba.

‘Huyo anatania tu,...eti hati miliki ina jina lake,mbona itakuwa maajabu...’ nikasema huku moyo ukinienda mbio, maana kweli hatii miliki ya nyumba yangu haionekani kabisa,....ina maana aliichukua yeye akaenda kuibadili, lakini kwa vipi....haiwezekani.

‘Huyo anatania tu, tulikuambia mwenzako yupo hapa kwa malengo, na inavyoonyesha lengo lake ilikuwa hii nyumba,sio wewe,hebu jiulize kwanini akugande wewe, una nini cha zaidi kuwashinda matajiri,kuwashinda wanaume wengi anaokutana nao....akili yakoimeganda, hata kuwaza huwezi, unachowaza ni tama zako za kimwili,na huo ni ugonjwa....’akasema mama.

‘Mama hivi kweli mnaamini kuwa mimi na akili zangu nikubali kuiandikisha nyumba hii kwa mke wangu, kwanini nifanye hivyo, wakati nipo hai, ....ndio ni kweli nyumba hii ipo kama rehani,kwani walishakuja wapiga mnada kuinadi....na walinipa notisi ya miezi ....mmh, ikawa imepita, lakini sikuwaona tena wakija, hili lilinitia wasiwasi....’nikasema.

‘Basi labda walikuja wakakutana na huyo mkeo akaongea nao, na huenda keshalipa hilo deni na nyumba imechukuliwa na yeye...’akasema mama.

‘Haiwezekani maana kila jambo linautaratibu wake, hati zote huko benki, huko halimashauri zote zimeandikishwa kwa jina langu...naili zihamishwe kwenda kwa mtu mwingine ni lazima mimi mwenyewe niwepo, ...itakuwa maajabu basi...’nikasemanakuingia  chumbani.

Nilipoingia tu nikakuta karatasi ipo kitandani, ilikuwa nakala ya hati miliki ya nyumba, nikaichukua na kuisoma, kweli ilikuwa na jina la mke wangu, kuwa ndiye mmiliki halali wa nyumba...nakulikuwa na kiambatishi cha wapiga mnada, kuonyesha wao walipiga mnadahiyo nyumba baadaya mimi kushindwa kulipa deni na aliyweza kushinda huo mnada na mke wangu ambaye alilipa pesa taslimu sawa na hilo deni la nyumba....

‘Mungu wangu......’mwili mzima mzima ukaisha nguvu

*******

Nikawa naongea na wazazi wangu maana sikuwa na la kufanya, kama kweli mke wangu kanunua hiyo nyumba sio mbaya, ni kama helakutoka mfuko huu kuingia mfuko wa pili, nikajipa matumaini

‘Mwanangu sisi tumeshindwa,...maana tulijua pamoja na hii shida ya njaa, tungeliweza kukusaidia kuondokana na mnaso ulionaswa nao, lakini kila tulivyojaribu kukusaidia tunaona hunasuki, ...iliyobakia tunamuachia mungu...’akasema mama.

‘Kwani wazazi wangu vipi...?’ nikauliza nikiwa na wasiwasi, ..ndio najua kuwa wazazi wangu hamuishi inavyotakiwa wazazi watendewe, lakini nina matumaini kuwa hali hiyo itaisha tu, na hata hivyo hali yangu itakuwa njema tu, nitapaat kazi tu, sizani kuwa nina mkosi wa kutopata kazi. Nilisema huku nikiwaangalia wazazi wangu;

Wazazi wangu afya zao zilishabadilika, sio kama walivyokuja, angalau sasa wanaonekana akmawatu, jamani msiombee njaa, ....hali iwe vipi, lakini njaa haina muamala, mwili unapukutika na kamaulikuwa kijana unakuwa mzeekablaya umri wako. Wazee wangu walipokuja walikuwa wamechoka sana, nakuzeeka isivyo sawa na umri wao, sasa wanaafadhali licha ya manyanyazo yaliyopo....

‘Mtoto wetu, ndio tumetokea huko kijijini kwa kukimbia njaa, lakini kwa hali iliyopo hapa imetushindwa,....sisi ni wazee, sisi ni wazazi wako, hatupo na umri sawa na nyie tena hata nguvu zetu sio sawa na nyie, kwa umri huu tulitakiwa tukae tufaidi matunda yenu...’akasema mama.

‘Na ndivyo ninavyotaka mama iwe, najitahidi sana, tatizo ni kuwa sina kazi kazi hazipatikani, lakini hiki kibarua ninachofanya kitatusaidia kidogo na kama ikiwezekana nikipata pesa kidogo tu tunafungua genge,...na hata hivyo mwenzangu naye anajitahidi, tunachotakiwa ni kumvumilia, kama mjuavyo kakulia mazingira tofauti na sisi...’nikasema huku nikijitahidi kuficha machozi.

‘Najua unavyojisikiamtoto wetu, lakini yote yanategemea wewe, tulikuwa na matumaini kuwa utazindukana, utajua wapi ulipo, lakini kila tulivyojitahidi haikusaidia kitu ,mwenzako kakuzidi akili, hujijui na hujui wapi unapokwenda na tuna wasiwasi siku ukizindukana utakuwa umechelewa...na hata hivyo umeshachelewa, angalia alivyokufanyia....’akasema baba.

‘Kwa vipi wazazi wangu, nyie ni wazazi wangu hamtakiwi kunitupa,...kama mnaona nipo katika hatari kwanini hamuniambii, na ni hatari gani hiyo....kwasababu kama ni huyu mwanamke , keshaamua kujirekebisha, na hatua liyofikia inatia matumaini, ....tuzidi kumsaidia ...kama ni nyumba, haina shida, kuinunua yeye ni kama kunisaidia tu, isichukuliwe na mtu mwingine...’nikasema.

‘Je alikuambai huo mpango, alikuhusisha, .....?’ akauliza mama

‘Hapana, labda alipitiwa...au sijui hawa watu walifika lini hapa kupiga huo mnada..’nikasema nikiwa na wasiwasi .

‘Ndio hapo tunasema umezidiwa ujanja, maana hujijui, hasa inapofikia kwa huyo mwanamke wako....hatutaki kukuharibia uhusiano wenu, lakini kila tukiangalia mbele kuna giza...sisi ni wazazi wako, na kama ulivyosema siku ile, wewe sasa sio mtoto mdogo tena, unajua nini unachokifanya, na kweli tunaona jinsi unavyoishi na mkeo,mnajua nini mnachokifanya...’akasema baba na mama akadakia nakusema;

‘Sio kwamba kazi za hapa ni ngumu, mbona ni kazi ndogo tu, za kawaida, hatuoni ajabu kufanya kazi zote hizo, kwasababu tumezoea kazi, lakini heshima ni kitu muhimu sana....mimi mama yako katika umri huu nisimamiwe kama mtoto mdogo....hapa hujafagiai vyema, vyombo hukusafisha vyema, chakula hiki hujapika vyema....sio kauli nzuri,lakini sio kosa lake....’akasema mama.

‘Mama hilo nitawalinda hadi mwisho, nilishaongea na mwenzangu na amesema hatawafanyisha kazi tena,...kama hataki nitajua nini cha kufanya maana hapa ni kwangu...’nikasemanikionyesha kujiamini.

‘Hapa ni kwako....ina maana hujaamini kuwa hapa sio kwako tena, wewe subiri,kama hatakuja mwenzako mwingine mwenye sharubu kama wewe, ukaambiwa ishia, kama alivyoambiwa mjomba wako,....aliambia haya chukua msaada huu na ishia...hahaha,jamani kizazi hiki mbonamna vituko...’akasema mama.

‘Mama hii ni nyumba yangu kamani haki yangu nitaipigania mapka hatu aya mwisho..mtaona tu..’nikasema nikijipa moyo.

‘Hayo ni maneno tu mtoto wetu, kauli yako inakushitaki, hata ulivyoitamka, umeitamka kimashaka, tuna wasiwasi, kama ulivyosema nyumba hii uliijenga kwa mkopo,na hukuweza kuulipia tena, ina maana katokea mtu kainunua,ili mkopo huo ulipwe, kwahiyo ni mali yake, sio yako tena,....hapo huoni kuwa mwenzako ni mjanja kuliko wewe.....tulishakuambi kuwa kuwepo kwake hapa ni kwa malengo ambayo mwisho wake yatakuumiza...ndio hayooo’akasema mama.

‘Hapana mama,haniwezi mimi...hilo lisiwatie shaka...huyo namjulia mimi,...haiwezekani, nitaongea naye na nitaona nini lakufanya...’nikasema huku nikiwaza akilini kuwa je hiyo itawezekana vipi wakti sina pesa, sina kazi, asilimi kubwa tunamtegemea mke wangu.

‘Tutafutie nauli, kesho au keshokutwa tunaondoka, tumeshawasiliana na mjomba wako, na yeye yupo mbioni kurudi kijijini, tuna mpango wa wazee ambao keshaufanyia kazi, hatutakufa njaa, na tunakushauri kwa ahtu ailiyofikia ni bora tukaondoka pamoja kabla hujaumbuiwa, ....kama upo tayari tuondoke pamoja,...tuondoke kabla  mambo hayajawa mabaya zaidi...’akasema baba.

‘Baba na mama naona nyie mumeshapanga iwe hivyo, na kama mumewasiliana na mjomba siwezi kuwazuia, lakini lengo langu nilitaka tukae pamoja mpaka hapo mambo yatakapokuwa mazuri,...na naona sio jambo jema kwa nyie kuondoka haraka hivi, .....Basi ngoja akija mwenzangu tutaongea naye tuone jinsi gani tutafanya, ili hata mkirudi nyumbani mpate nini cha kuanzia...’nikasema.

‘Tunaomba kama inawezekana, usimuhusishe huyo mwenzako kuhusu sisi, kama hutaweza kuipata hiyo nauli, usisumbuke, sisi tutajua jinsi gani ya kuondoka, ...ila tulitaka kukuambia yale yaliyopo moyoni mwetu, kama alivyosema mjomba wako, nyumba hii ....haina kizingiti imara,....utakuja kujua baadaye, lakini yote ni wewe mwenyewe, hatutaki kukulazimisha...hatutaki kuingilia maihs yako....wembe ulioulilia unaanza kukukata...’akasema baba.

‘Usimwambie mtoto hivyo, tunatakiwa tumshauri tuondoke naye, mabona tutakuwa tukiishi huko kijijini kwa mashaka, kwa hali kama hii , ...hapana tundoke na mtoto wetu..’mama akawa anamwambia baba kwa sauti ndogo

‘Msijali wazazi wangu, kuhsu mimi, nimeshajifunza sana, ..naona sasa nitulie, na nimeamua huyu mke nitajitahidi tuishi naye na hatua kwa hatua atabadilika tu,...msiwe na mashaka kabisa na mimi...’nikasema.

‘Haya kama ndivyo ulivyoamua sawa, wewe ni mtu mzima, ila ukishindwa maisha karibu sana kijijini, tunataka maendeleo kutoka kwako, maisha ya mjini yana raha zake lakini yana gharama zake,...ili uishi mjini kwa raha unatakiwa uwe na pesa, kwasababu hakuna shamba....shamba la huku ni uwe na kazi, na kazi za hapa ni za kuajiriwa, uwe mtumwa wa matajiri....vinginevyo unatakiwa uwe na biashara ya maana , lakini hayo maisha ni yakwenu, sisi hatuyawezi....’akasema baba.

‘Ni kweli haya ni maisha ya kwetu, nyie maisha yenu ni kijijini...wanakijiji mpo katika kikao cha kijiji...safi sana, na hilo ni jambo jema kabisa....’sauti ikatokea malngoni, Kimwana alikuwa kasimama huku kasika kiuno, akatizama huku na kule akakunja uso, na akawaangalia wazazi halafu akasema;

‘Shikamooni wazazi, ila kabla ya hiyo marahaba yenu, nakumbuka nilisema leo nitakuja na wageni, sasa kama ningelikuja nao siingelikuwa ni aibu tupu, nje kuchafu, ndani ndio usiombe...jamani mnataka nifanye kazi ngapi, niwalishe na bado hata vikazi hivii vidogo nije nifanye mimi, ....haya nitafagia mwenyewe, haina shida, maana nikisema hivyo naambiwa sina adabu...na sina shida ....’akasema na kuchuku ufagio.

‘Usiwe na wasiwasi binti, tunatarajia kuondoka karibuni, ...kesho tutaondoka tu...’akasema mama.

‘Mnanishangaza, muondoke, muache kuishi na mtoto wenu, yupo mjini,...hahahaha, maana mkiwa kijijini mnatamba, tuna mtoto ana kazi, ana nyumba mjini...mumeiona kazi yake...ndiyo hiyo,...nyumba sijui .... kwahiyo ni vyema mkasema ukweli, mkajua ukweli kuwa yale ya zamani kuwa ukoo huu ni bora, familia hii ni bora, haupo tena, yoyote anaweza kuwa bora....’akasema huku akimalizia kufagia.

‘Ubora wako ni wa pesa za msimu, ambazo hazina uhalali, sio sawa na ubora unaojulikana huko kijijini, ndio maana tunataka kuondoa hapa haraka, .....tusije tukajikuta tunakula vile visivyoliwa na mwisho wa siku miili yetu itajaa sumu ya dhuluma...’akasema baba.

‘Hahaha, kama ni hivyo mbona mumeshakula...hamuoni mlivyobadilika...haya hiyo ndio shukurani ya punda, nilijua tu, hata nijipendekeze vipi siwezi kuwatimiliza, mimi mumeshaniweka kwenye kundi baya, lakini sijali, .....unafikiri,.... mimi nina maisha na mtndo wangu, siyumbishwi na hisia za watu,ilimradi sili kwao...kuna mtu nimekula chake hapa, hakuna...huyu mwanaume, sana sana namlisha mimi, asema ukweli....’akasema huku akinigeukia mimi akaniangalia kwa macho tofauti na siku nyingine.

‘Tusianza kuchafuana....’nikajikuta nikisema.

‘Samahani ....samahani bwana mkubwa...’akasemana kucheka,halafu akawageukia wazazi wangu na kuuliza;

‘Haya mnataka kuondoka,nauli mnayo...mtaondokaje hapa,na huko kijijini mtaenda kusihi vipi, maana huko ni njaa ya kufa mtu...nimewasilina na watu huko wanasema wanaishi kwa msaada wa serikali,...’akasema huku akiwaangalia wazazi kwa makini.

‘Hilo tumeshaongea na mumeo...’akasema baba.

‘Mumeo..leondio nasikia hiyo kauli mumeo,siku zote mwanamke wako,....sio mke wako...leo mnaanza kunitambua hahaha..haya yangu macho, ...’akasema  halafu akanigeukia na kuniangalia kwa dharau;

‘Sawa labda ana nauli, ya kuwapa....haya ngoja mimi nikajipumzishe kidogo....maana hakuna kupumua hapa, huko kazini nako mambo  taabu tupu huyo Muhindi ananifanya kama kinyago chake cha bishara zake, unarudi nyumbani badala ya kutulizwa kwa maneno matamu ya faraja, unakatishwa tamaa na watu wasiotosheka....’akasonya na kupitiliza kuingia chumbani,na kabla hajaingia chumbani akasema;

‘Ama kweli kutegemewa ni mzigo mzito sana..na kila unavyojaribu kuweka mambo yawe sawa, wengine wanaona wanaonewa...lakini tutafika tu...haya na wewe mwanaume, ukimalizana na wazee wako njoo tuongee ndani...’akasema mke wangu maana siku hizi neno mpenzi limeshafutika mdomoni, sasa naitwa wewe mwanaume.

‘Sawa nakuja, nisubiri nimalizane na wazazi wangu...’nikasema huku moyoni nimejawa na mawimbi, nikaiangalia nyumba kwa juu na kuangalai kona zote za nyumba, nikasikitika, na nilipogeuza macho kuwaangalia wazazi wangu macho yakafunikwa na machozi.

‘Mtu mzima akilia kuna jambo...mjomba unalia mapemahivyo, bado...usideke kwa wazazi wewe ni mwanaume, angalia sana kizingizti cha nyumba yako....’ilikuwa sauti ya mjomba akiwa mlangoni.

'Una maana gani mjomba...?'nikauliza na mara mlango wa chumbani ukafunguliwa mke wangu alikuwa kasimama pale mlangonii huku kashika kiuno...

Je ni nini kitaendelea...mambo ya kifamilia hayo....mnasemaje wenzangu?

WAZO LA  LEO: Mazoea yakijijenga hugeuka kuwa ni tabia, ama iwe tabia njema au tabia mbaya, ni vyema ukapima matendo yako kwa kuangalia faida na hasara za matendo yako. Na hasa mkiwa wawili mke na mume, ni vyema, mkajaribu kuangaliana matendo yenu, kama hayaendi sawa, shaurianeni mapema,kwani mkiachia tabia ikajijenga, mtashindwa kuelewana baadaye.

Ni mimi: emu-three

5 comments :

elisa said...

Dah ! Nasoma naona kama ni hadithi za kufikirika,ila haya mambo yapo! Binadamu tuna mambo .....

emuthree said...

Elisa inabidi nikukutanishe na huyo jamaa, ili uhakiki mwenyewe. Kuna mataizo mengi watu tunakutana nayo,ukiamua kuyaweka vizuri unaweza usiamini, ..hasa kama hujakutana na matatizo kama hayo.
Mimi aliponihadithia kuwa alikutana na mama wa Kihindi akamlazimsiha, nikaona hiyo ni ongeza chumvi, lakini baadaye nilikutana na jamaa ambaye anakijua hicho kisa vyema, akanithibitishia, hapo ndipo nikaamini kuwa ....duh, ni rangi tu, ndani sote tupo sawa.

Anonymous said...

Kwenye kitengo chako huna mpinzani, lbda watoe kura kwa kujuana, lakini kifani your best writer!

samira said...

haya mambo yapo swali ivi huyu kaka ana elimu mpaka ulaya amefika alikuwa haelewe kama kuna kitu sio kawaida kwenye life yake au ndo kazidiwa maana yapo haya kuzidiwa na wajanja wa mjini
m3 big up dear uko juuuuu sana songa mbele

Yasinta Ngonyani said...

haki ya Mungu ni kama vile hadithi ...kweli UBINADAMU KAZI..