Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, April 3, 2012

Hujafa hujaumbika-16




‘Kimwana namba moja, nimekuita hapa kwa jambo moja kubwa ambalo nahisi wewe peke yake ndiye unaliweza, wenzako wanaweza wakaogopa...najua ulishaniambia kuwa wewe umeamua kubadilika,na hata umeolewa..safi kabisa maana najua huyo mume ataishi maisha ambayo ilitakiwa wake wawe hivyo....’akasema Mama D, kama wanavyomuita, wengine humuita Docta tu.

‘Mimi nilipenda kusikia nini huyo mume wako angesema baada ya kukutana na mtu kama wewe...najua kuwa kuna taarifa za kuwazalilisha kuwa mnajiuza na vitu kaam hivyo, lakini hiyo ni kawaida na ni chamgamoto kwenu....na hili nilijua litatokea ,lakini ndio gharama za hii kazi...’akatulia na kuangalia nje.

'Hiyo kwangu ilikuwa hatua ya kwanza, maana nilikuwa na malengo, kuwa ikifika hapa, kukitokea hiki nichukuea hatua gani...sasa hatua inayofuata inahitaji ujasiri na...

Na mara akaingia dada mmoja ambaye ni mmoja wa walinzi akamnong’oneza Docta na docta akatoa macho kuonyesha kuwa alichoambiwa ni jambo la kutisha kidogo, akawaeukai mabinti aliowaita na kusema kwa sauti ya haraka;

‘Kuna jambo limetokea....juzi, na hili sikutegemea kuwa litawahusu nyie naona kumbe kuna miongoni mwenu wamehusika na hilo...nilishawaonya kuhusu mambo hayo,kuwa katika kazi yetu hatutaki kutumia nguvu,...hauhitaji silaha, sisi wenyewe ni silaha, kama ukitumia akili...na mambo kama haya yanavuruga mpangilio wangu. Nakumbuka ndio niliwafundisha ujasiri, na jinsi gani ya kujihami, lakini sio kutumia silaha...sasa naona miongoni mwenu kuna mmoja kajihusisha na ujambazi....’akasema na wale mabinti wakaguna.

‘Ndio huo ni ujambazi, kama mlitumia silaha, kumtisha yule Mhindi ili atoe pesa, na kumjeruhi mlinzi, ina maana gani, huo ni ujambazi, na wahusika wameshabainika,na kibaya zaidi wananihusisha na mimi, eti wakisema mabinti zangu...hilo halipo, maana mimi sina mabinti....nyie ni watu walioamua kukodi majengo yangu kwa kazi zenu ambazo mimi sizijui...’akasema na kuangalia nje.

‘Hilo ndilo nataka wote mliweke akilini na mseme hivyo....vinginevyo, mimi sitahusika na yoyote yule atakayewekwa ndani kwa uzembe wake....mimi niliwafudisha kuwa mkono wa mwanamke muda wote ni laini...kivutio...au sio, sio mkavu wa kutisha, kumbe wengine hawakunielewa na hilo somo...sasa ..ooh, ngoja nikaongee na hawo maaskari kwanza nisubirini hapa...’akasemana kutoka.

‘Ina maana ndilo alilotuitia huyu mama au kuna jingine...?’ akauliza mmoja wa wasichana.

‘Lipo jingine lakini hili la polisi naona limeharibu utaratibu ...’akasema msichana ambaye yupo karibu sana na huyo mwanamama.

‘Lipi hilo..?’ wakauliza wengine.
‘Atawaambia mwenyewe...mimi siruhusiwi kuongea jambo ambalo sijaambiwa niseme...

Mara Kimwana akakumbuka jambo, na haraka akainuka pale alipokuwa kakaa na kusema anataka kuondoka kuna jambo muhimu analifuatilia huko kwake..

‘Huwezi kuondoka ..subiri mpaka mama arudi...’akasema mmoja wa walinzi.

‘Hapana kuna jambo muhimu sana, akija mama mwambieni nina zarura...’akasema na kuondoka 
haraka.

********

Nikiwa njiani huku nikiwaza nilichokifanya, nikakaribia nyumbani,....akilini nilikuwa sijaamini nilichokiona mlendani,..nakilanililowaza, sikuweza kupata picha. Nilipoufikia mti wenye kivuli nikajipumzisha kidogo, maana jua lilikuwa likichoma hadi mfukoni, ....nikaangalia kule nyumbani kwangu,na mara nyingi nikiingalia nyumba yangu kwa mbali, moyo unaniuma sana, nikijua kuwa siku yoyote itakuwa sio yangu tena.

‘Hivi kunaweza kukatokea miujiza gani nikalilipa hiloo deni...sijui, hata nikipata kazi leo, sio rahisi benki kukubali kunivumilia tena, na nikawa nalipa kidogokidogo...namuomba mungu hawa wapiga mnada waendelee kusahahu sahau....’nikajikuta nikiongea peke yangu.

Mara macho yangu yakagundua gari ambaloo halikuwa mbali sana na pale nyumbani lilikuwa hatua chache kutoka nyumbani kwangu, lakini kwa muonekano lilikuwa ni gari la polisi, hapo mwili ulisisimuka, utafikiri nimefanya uhalifu fulani, nikajiuliza moyoni, kwanini nimefanya hicho nilichokifanya, kwanini ninakuwa na huruma na mtu asiyejihurumia....

‘Ningelikaa kimiya nione mwisho wake ni nini, lakini je....mara nikaona pale mlangoni kwangu akitoka askari...Kumbe askari wapo nyumbani kwangu, kwanini wameliweka gari mbali na nyumbani kwangu, au walifanya hivyo makusudi, ili waliopo hapo wasijue kuwa wanakuja maaskari. Janja yao.

******

‘Mnasema wenyeji wametoka, na hamjui watarudi muda gani, ina maana nyie tangu mfike hawow wenyejiwenu wakiondoka hawasemi wanakwenda wapi, au watarudi saa ngapi?’ akauliza askari mmojawapo.

‘Kuna siku wanatuambia, kuna siku hawasemi, ....hatuna muda mrefu tangu tufike hapa....kwani kuna tatizo gani?’ akauliza baba.

‘Kuna maswali machache tunataka kuwauliza, hasa kuhusiana na mke wa mwenye nyumba hii...’akasema askari.

‘Mimi nilisema huyu mwanamke atamuingiza mtoto wetu hatiani,....sasa unaona...’akalalamika mama.

‘Kwani umeambiwa kuna hatia....huyo ni mwanaume na matatizo kama hayo ni kawaida katika maisha, hebu tuambieni kuna tatizo gani, maana sisi ni wazazi wa huyo mwenye nyumba..’akauliza baba.

‘Ni vyema tukawauliza wao wenyewe, msiwe na wasiwasi,wakija waambieni tunawahitjai kituoni...wafike haraka, vinginevyo tukija wenyewe litakuwa swala jingine...’akasema askari na kuondoka.

********

‘Hebu niambie kuna tatizo gani mpaka maaskari wanafika hapa, ...wamekuja hapa ukiwa haupo na lengo lao kubwa ni wewe....hasa baada ya kupokea ile simu, hebu niambie ilikuwa simu ya nani, na jinsi ulivyoondoka hapa jana,uliondoka bila kuaga,ina maana ile simu ilikuwa ya matatizo gani?’ nikamuuliza.

‘Hayo hayakuhusu, nilishakuambia kuna mambo yangu ya kimasiha hutakiwi kuyajua, na nafanya hivyo kwa nia njema....’akageuka na kuangalia kwenye droo ya kitanda, na kusema;

‘Kwanza niambie pale kwenye droo, kulikuwa na pesa na vitu vyaagu vingine,...niliondoka bilakufunga,sasa hivi naona droo haina kitu,  pesa na vitu vyangu vingine vipo wapi?’ akauliza Kimwana akiniangalia machoni.

‘Pesa zako hizi hapa...., nilipoona droo zipo wazi na afunguo haupo, nikaona nikuhifadhie...’nikamwambia na kumkabidhi zile pesa, alizipokea na kuanza kuzihesabu, na alipomaliza akauliza tena;.

‘Na vitu vingine...?’ akauliza kwa ukali.

‘Vitu gani vingine....mimi nimekuambia ni pesa ndizo nilizoziona ,lakini sikuona kitu kingine...’nikasema huku nikimkazia macho.

‘Sikiliza...wewe  mwanaume, mimi sio mjinga kukuambaia kulikuwa na kitu kingine, usijifanye mjanja , unaweza ukafanya jambo ukaja kujijutia baadaye, hicho kitu kilichokuwa hapo ni hatari, ni bora ukanirudishia nikajua mwenyewe jinsi ya kukihifadhi...’akasema huku akikagua mle kwenye droo.

‘Mimi sijaoan kitu kingine...zaidi ya hizo pesa..’nikasema huku nikimwangalia kwa makini.

‘Tusitaniane...nakuambia ukweli hicho kitu kitakuletea matatizo....mimi mwenyewe nimekabidhiwa tu... na kama polisi wakija hapa, na wakakiona umekwenda na maji, usije ukasema sijakuambia.....’akasema huku akitafuta kila kona ya chumba.

‘Kitu gani hicho, ...mpaka polisi wahusike,....mbona husemi kulikuwa na kitu gani humo...mimi sijaona kitu zaidi ya pesa, kama kuna kitu kingine ambacho mimi sikijui niambie....’nikasema na baadaye wazazi ambao walikuwa njewakaingia, na kutupa taarifa kuwa polisi wanatuhitaji kituoni haraka iwezekanavyo.

‘Haya ndio mambo tuliyowahi kukukanya....unaona jinsi unavyojiingiza kwenye matatizo ambao kamaungelitusikiliza mapema yasingelikukuta...’akasema mama.

‘Mama usijali hakuna tatizo hapa,....’nikasema nikijipa moyo.

‘Msijali wanakijiji,...haya ni mambo ya mjini...tumeshazoea matatizo kama hayo...nyie endeleeni na 
shughuli, maana wanasema asiyefanya kazi asile....sasa hata vikazi vidogo vidogo vya hapanyumbani mpaka mtu aambiwe....sio kwamba nawaamrisha mfanye, lakini ni swala la....’nikamkatiza kabla hajaongea zaidi.

‘Kimwana, unataka nini kwa hawa wazazi, unataka wafanye nini,mama kila siku ndiye anafanya kazi zote za hapa nyumbani utafikiri ndiye mfanyaakzi wa hapa nyumbani, ulitaka akufanyie nini zaidi....au unataka baba naye afanye nini...?’ nikauliza kwa ukali.

‘Kuna usafi wa nje, angali majani yalivyoota nje....kwasababau wapo hapa wanaweza wakasaidia...aah, ngoja ninyamaze maana ulishasema antakiwa kuji....kufnaya nini vile, maana sijui kuigiza mambo hayo, haya twende huko polisi ukajichanganye huko, na ole wako kama ulichukua hicho kifaa na ....ole...wako kamaunataka kwenda Segerea, jifanye mjanja...’akaniamb huku akininyoseha kidole.

‘Twende , mimi sina wasiwasi, tutayajulia huko mbele...’nikasemana tukaondoka kuelekea kituoo cha polisi.

Tulifika kituoni tulikutana na huyo askari aliyekuja nyumbani na moja kwamoja tukaingizwa kwenye chumba maalumu, na kuanza kuhojiwa kwa saa nzima, na hatimaye tukaongozana nao hadi nyumbani ili kufanya msako...mimi sikuwa nakipingamizi,ingawaje mke wangu aliwapinga kwa nguvu zote,

'Hakuna kupekua humu ndani, .....kwa uhalifu gani, ...'akasemamke wangu, na hata hivyo ilibidi akubali baadaye alipoona mimi sina kipingamizi akakubali shingo upande huku akiniangalia kwa wasiwasi, na msako ukafanyika kila kona ya nyumba, wakitafuta silaha inayosaidikiwa kuwa imehusika katika ujambazi na silaha hiyo aliporwa kutoka kwa mmoja wa maaskari akiwa kazini..

‘Na waliompora na hawo machangudoa....’akasema askari mwingine.

‘Kwani huyu askari alikuwa wapi, kama hakuwa na hawo machangudoa...?’akauliza jamaa mmoja aliyekuwa karibu akisikiliza.

‘Hata kama alikuwa nao,alikuwa akitimiza majukumu ya kikazi....kwanini unaingilia hapa, kwanza wewe haikuhusu ..hebu ondokeni hapa...’askari wakaanza kutimua watu wasiohusika, lakini ujumbe ulishafika. Kwani inavyosadikiwa askari huyu na mwenzake walikuwa eneo hilo wanakopenda kukaa hawo wasichana wanaoitwa machangudoa. Wasichana wale walipogundua kuwa maaskari wanawafukuza eneo hilo,wakapanga mbinu za kuwahadaa hwo maaskari kimapenzi, na walipowanasa, ndipo wakachukua silaha mbili bastola na bunduki....bunduki ilipatikana baadaye,lakini bastola haikugunduilika wapi ilipo.

‘Sasa kwanini mje kwa huyu mke wangu...?’nikauliza.

‘Kuna taarifa kuwa silaha hiyo ilikuja kufichwa hapa...na kwa taarifa yenu, hizo silaha zilipochukuliwa zilitumika kufanyia ujambazi....mnaona hatari iliyopo hapo...naomba mlifikirie hili kwa makini....’akasema askari.

‘Mimi nauliza kwanini mhusi kuwa hiyo silaha imeletwa kufichwa hapa, ...ina maana mke wangu alikuwa huko kwa hawo machangudoa,au anashirikina nao...?’ nikauliz akwa hasira.

‘Sikiliza sisi tumewakamata washukiwa na tulipowabana sana mmoja akasema silaha hiyo walimpa dada mmoja akaifiche,  na akasema ni huyu mkeo, ...kwahiyo tunaomba kwa usalama wake kama anayo aitoe, vinginevyo tukihakikisha kuwa ni kweli alipewa, atahusishwa na huo ujambazi,....’akasema askari mmoja.

‘Lakini mumetafuta kila kona hakuna, ...endeleeni kutafuta mpaka mjirizishe wenyewe...’nikasema huku nikigeuka kumwanglia mke wangu ambaye alikuwa katulia akivuta sigara. Huwa kukiwa na jambo linalomkera sana hupendelea kuvuta sigara, na tabia hii nimejaribu kumkanya kuwa sigara sio njema kwa afya yake, lakini haambiliki.

‘Usituvutie sigara hapa....’akasema askari kwa ukali.

‘Hapa ni nyumbani kwangu, kama sigara inakukera ondoka,... nani aliyekuambia uje nyumbani kwangu, ..sio kwasababu wewe ni askari  ndio unituingilia hadi sheria za nyumbani kwangu, ..kwanza nyie maaskari, mtatumwaje na hawo wasichana wenu kuja kwangu kuwa eti wamenipa silaha, na muwaamini, hamjuii hawo wanaweza kusema hivyo ili kuniharibia maisha yangu ...mimi ni mke wa mtu nina heshima zangu, au mnalenu jambo....?’ akauliza mke wangu kwa hasira.

‘Hatuna maana hiyo kwako,... ila siku hizi kuna mtindo umezuka, ...Hawo wanaohusika, siku hizi hawakai barabarani,wanachofanya  ni kukodi nyumba kwa siku, wiki au mwezi, wanawasiliana na wateja wao muda wakukutana...’akasema

‘Mimi nimeshakuambia kuwa mimi ni mke wa mtu,...unanielewa ...tokalini mke wa mtu akafanya mambo hayo, au nikuulize wewe mke wako anaweza kufanya mambo kama hayo?’ akase mke wangu na yule askari akakunja uso kwa hasira, na kusema;

‘Hatuzungumzi habari za mke wangu hapa, usiharibu mada, unataka kuharibu jambo la msingi...’

‘Jambo la msingi ni lipi, hilo maana sikuelewi elewi mimi ....?’ akauliza mke wangu.

‘Jambo la msingi ni hilo tukio lililotokea,...na ni kawaida kukitokea uhalifu lazima tuufanyie uchunguzi, na hapa ni moja ya  kazi zetu, kutafuta ukweli na kufichuka ukweli ulipo, kujua chanzo cha uhalifu huu, hatujakunyoseha kidole wewe moja kwa moja kuwa unahusika,ila ninachotaka kusema ni kuwa uhalifu umefanyika, na kama umefayika ni lazima tutafute wahusika, ....na ndani ya uhalifu huo kuna silaha ye polisi iliyochukuliwa...je mnajua lolote kuhusiana na sil’akasema askari huyo akiwa kamkazia Kimwana macho.

‘Je huo uchunguzi umelengaje hapa kwangu, na isiwe kwa mtu mwingine....?’ akauliza Kimwana.

‘Kutokanana vyenzo vyetu vya habari na mahojiano kati ya mmoja wa wahusika tukaeleekzwa kuja kwako....ni moja ya taratibuu na wewe kama raia mwema unatakiwa ushirikiane na sisi...ni kawaida, huna haja ya kujishuku....’akasema polizi.

‘Sina haja ya kujishuku wakati nyie mumeshanishuku...ina maana kinachotakiwa ni mimi kujitetea, siwezi kukaa kimiya tu....mwisho wa siku mnaweza mkamshika asiye na hatia, ....imeshatokea hivyo....’akasema na kabla hajaendelea mara akaingia askari mmoja.

‘Afande, unaitwa huku na mkuu ...’akaja askari mmoja,na kuondoka na huyo askari na baadaye akarudi na kusema;

‘Bahati yako, hiyo silaha imepatikana,lakini hatujamalizana na wewe unaweza ukahitajika kituoni muda wowote , kwasabbu kwanini utajwe wewe...lazima kuna kuhusika kwa namna yoyote ile,na nitahakikisha kundi lenu na huyo mwanamama, mnafikishwa mbele ya sheria...’akasema yule askari.

‘ Ni mpaka....hahaha....umeshindwa babu wee...hapa ni maji marefu, nakuambia hivi kama ni kwa matindo huo yatakushinda....mjini hapa...’akasema mke wangu bila kujali.

‘Hivi wewe huoni unawapandisha hasira hawa watu, wenzako wapo kazini,na kuna huo uhalifuu umefanyika, wewe unaleta mzaha, hawo ni wanausalama, wanaweza wakakulinduika ndani kwa usalama wa taifa...’nikasema.

‘Sio rahisi hivyo, tatizo lenu na Wananchi wengi ni uwoga,...hakuna sheria ya kumshika mtu ovyo ovyo, bila kuwana ushahidi kamlifu kuwa ni mhalifu..ukiwaogopa hawa watu watakunyanyasa...na mara nyingi uwoga ni dalili mbaya sana ya kutokujiamini...’akasema mke wangu.

‘Hebu niambie hicho ulichokuwa ukitafuta kwenye hiyo droo ni hiyo silaha....?’ nikamuuliza.

‘Wewe mwanaume, sema ukweli ulikwenda kuiweka wapi, maana umevuruga mambo ya watu, unafikiri hawo wanye nao wakija kuniuliza nitasema nini hapa...aah, watu wengine bwana..waoga...’akasemabila kujali.

‘Yaani badala ya kushukuru kuwa umeokoka na hilo janga, ...unafikiri wangeikuta hiyo sailaha hapa ungelikuwa wapi sasa hivi...na mbona kila hatua inaonyesha wewe kuwepo kwenye makundi hatarishi...kumbe na hata silaha unajua kutumia?’nikamwambia.

‘Silaha, ina maana wewe hujui kutumia silaha,....tuachane na hayo, hebu tuangalia jinsi ya kusihii na hiki kijiji, maana mambo ndio hayo yameharibika, kwa mtaji huu hakuna sehemu ya kufanya dili la pesa, hata huyo Muhindi atakuwa mbendembende...hiki kijiji kitakuwa hapa mpaka lini?’ akauliza.

‘Nilishakuambia hiki sio kijiji, hawa ni wazazi wangu wanahaki ya kukaa hapa hadi hapo watakapoamua kuondoka wenyewe....’nikasema.

‘Sawa sio mbaya maana mama ni jembe, anavyopiga mzigo hapa nyumbani, nimemkubali, ....lakini baba mmmh, ananiboa, muda wote kakunja nne, anasubiri sahani mezani, huyu tutakosana naye....wewe subiri..na leo tunaongozana hadi kwa huyo Muhindii anahitaji kibarua wakubeba mizigo...’akasema huku akiangalia saa.

‘Mimi nikabebe mizigo naelimu yangu hii...hivi wewe unanionaje mimi...?’ nikamuuliza.

‘Kula hiyo elimu yako...elimu bila kazi ina maana gani, elimu ni jinsi ya kupata mahitaji yako, elimu sio kufa na tai shingoni, umekaa ndani na makaratasi yenye mapambio makubwa, eti shahada, au stashahada, au sijuii nini...lakinii mfukoni hakuna kitu, hayo ni mkaratasi tu, yanastahili kutupwa shimoni..elimu ni pesa,....elimu ni mipango, elimu ni kuwa na uhakika wa mkate wa kila siku....’akasema huku akionyesha mkono mdomoni.

‘Unajua sana kuutumia mdomo wako...’nikasema na mara  simu yake ikaita na alipokea bilakuiangalia

‘Kuna nini tena Docta....?’ akauliza

‘Mimi ....hapana,huoni hali ilivyo huko nje...’akasema na kusogea mbali na pale nilipo.
Mimi ni mke wa mtu mama, kwanini usiwatumie wengine....najua sana, lakini wapo ambao ni wajanja, wanaweza kuifanya hiyo kazi....oooh, mama,tafadhali...mbona hunitakii mema, ...ooh,...mkuu wa usalama, hapana, huko tunakwedna mbali...huko,...unamjua eti nini, uliwahi, ... haya nakuja ...’akakata simu na kunigeukia.

‘Huyu mama sasa ananipanda kichwani, lakini sina jinsi, maana ameshika mpini, ....haya mimi natoka,ila kesho ujiandae tutakwenda kwa huyo Muhindi, lakini huko uwe makini maana mke wake naye simuamini,....’akasema nakuchukua mkoba wake.

‘Sasa unakwenda wapi?’nikamuuliza.

‘Kwa wanaojua hii dunia, ....huyo ni mama, yeye ndiye alinilea, ..sio mama yule wa kijijini, hapana huyu ni mama wa mjini, mama wa maisha, akikohoa unatetemeka....sina jinsi, ila akijifanya kuniburuza, nitamuhesabia masiku, hata mimi nina data zake...yeye anajifanya ana kila kitu chetu, hajui hata mimi ni mjanja....tutaona mwalimu na mwanafunzi nani zaidi....’akasema na kuondoka.

‘Siamini ....’nikajikuta nikisema .

 NB: Nimechelewa kuiweka sehemu hii kwasababu ya matatizo ya blog, nashukuru mungu ile hali imetangamaa, tuzidi kuwemo,ingawaje sehemu hii nimeiburuza kwa harakaharaka , lakini natumai ujumbe utakuwa umefika.

WAZO LA LEO: Mabaya yapo na watendaji wa ubaya ni hawo hawo wanadamu, tunaposikia jambo tusizarau, tulifanyie uchunguzi kwanza,  kwani lisemwalo lipo kama halipo laja....na hata hivyo tusiwe na pupa na maamuzi , kwani maamuzi ya haraka yanaweza kuleta majuto baadaye, kama walivyosema wahenga, haraka haraka haina Baraka na majuto ni mjukuu.


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Pam said...

wanakijiji what a name to call ur inlaws!!! wanawake sie hii ni aibu tujifunze kupitia hii story na kujirekebisha nina uhakika tupo wenye haya mapungufu haya na wandoa dawa ya tatizo ni kulikabili na si kulikimbia
thanks m3 kwa kutupa kitchen party ndoani...

Precious said...

Ujumbe umefika M3 na umeeleweka kabisa

emuthree said...

Pam,...Kuna jamaa aliniambia kuwa wanawake ni watu wa ajabu sana, wao wana huruma sana, lakini wakibadilika wanakuwa wabaya zaidi ya mnyama...sin auhakika na hilo, nawasikiliza nyie.

Nashukuru Precious, tupo pamoja

Na wengineo mungu awabariki kwa kuendelea kuwa nami.