Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, March 13, 2012

Hujafa Hujaumbika-2



MAISHA YALIPOANZIA


‘Nikiwa bado mdogo, mara nyingi nilikuwa napendelea kwenda kukaa kwa mjomba, hata kulala huko, kama unavyojua tena kule kijijini, huwa kutembeleana ni jambo la kawiada,na hasa kwa watoto, na tulipapenda sana kwa mjomba kwasababu ni mtu aliyekuwa na uwezo kidogo, redio vitu vya anasa anasa kwa enzi hizo vilikuwa havikosekani nyumbani kwake.

Mjomba yeye kwa bahati nzuri, aliwahi kuajiriwa na baadaye akaachishwa kwa sababu ambazo hatuzijui, na alikuwa na kabati lake la vitabu, name mara kwa mara nilikuwa nikichukua vitabu na kuvisoma, hasa vya hadithi, ...na nikajikuta nimevutika zaidi na vitabu vya hadithi za mapenzi

‘Nilipofika sekondari nikawa siachani na viatbu `novels’ na jinsii nilivyozidi kuvisoma ndivyo nilivyoshawishika na vitendo vya kimpanzi, nikawa na wapenzi wengi wa kike,na pia nilikuwa mtaalamu mkubwa wa kuhadithia hadithi za kimpanzi,hata wanzetu wakawa wananiita docta wa mapenzi.

Na ujuavyo shule hasa za bweni,mambo hayo yapo sana, ya kuita wasichana kwenye madisco, au kuwatembelea basi mimi nilikuwa mkali wa kutafauta wasichana, na kwa tabia hiyo nikpata nikachaguliwa kuwa waziri wa starehe na utamaduni. Madisco, kutembelea shule za wenzetu hasa zawasichana ikawa kila mwezi sikosekani.

‘Naweza kukiri kuwa hapo ndipo akili yangu ilipoharibikia, maana muda mwingi nilikuwa nikiwaza mambo hayo, sikupata muda wa kusoma sana shule, na matokeo yake miaka mine ikapita ,akili ikiwaimejaa mapenzi starehe na manno mengi mdomoni. Mtihani wa kidato cha nne,ukadhirisha hayo maana nilipata `division four’ ya karibu na kufeli. Hata wazazi wangu hawakuamini , maana kila mara nikirudi likizo nilikuwa nikiwafunga kamba za kuonyesha kuwa mimi ni mkali wa masomo darasani.

Kinachonisikitisha ni kuwa mara nyingine nilikuwa nikiwadanganya kuwa nimeharibu kitu, kwa mfano nilikuwa nikiwaambia nimvunga `paramecium’ au amiba’ yaani ni uongo usio na hata maana,na wazazi wanauza kile kidogo walicho nacho ilimradi helahiyo ipatikane,mimi nikipta ni kwendea madisco,na kuhongea mabinti.

Siku matokea yalipotoka, nilikuwa kwa mjomba, na mjomba tulikuwa tukielewana sana nay eye,kwahiyo nilikuwa sibanduki kwake, na siku hiyo walikuwepo mama na baba , wakawa wanasomewa matokeao yangu na mjomba alipofika mwisho akasema;

‘Kafaulu katika kundi la wajinga, katika wajinga bora yeye anaongoza kapata divisheni four ya kufutia machozi..’akasema mjomba na kunirushia karatasi yangu ya matokeo.

‘Hiyo divisheni four ndio kafaulu kawa wanne,au ...?’ akauliza mama.

‘Kafulu kafeli,alibakiza kidogo tu kupata sifuri..kajitahidi maana atapata cheti chake, lakini kwa maksi hizo hata ualimu hawezi kwenda....’akasema mjomba,

‘Ina maana waalim ndio wanachukuliwa walio na maksi za chini...?’ akauliza baba.

‘Ndivyo wengi wanavyoamini hivyo, na hilo ni tatizo...’akasema mjomba.

‘Sasa hilo ni tatizo maana tulijitahidi na kukung’uta mikoba yetu ,hata kuuza vile vimbuzi vyetu ili mwanenti asome, aje atukwamue,sasa ndio huyo kafeli, tutamfanyaje maana huyu akikaa hapa tutaambulia kesi za kuwapa mabinti wa watu mimba....’akasema baba.

‘Dawa aoe ili atulie,tusje kupigwa mapanga,unakumbuka juzi tu alikuja jirani yetu na panga kuwa kamfuma huyu mwaneti na binti yake ambaye yuko darasa la sita....hebu niambie tutawezana naye kweli...’akasema mama.

‘Mimi huyu nitamsomesha, msiwe na wasiwasi ...ila ajitahidi maana sitapoteza pesa zangu bure...’akasema mjomba na kweli akajitahidi nikapata shule za kiufundi , huko kwa vile nilikuwa nakipaji cha ufundi nikafaulu vizuri sana na kiudogo niliazna kutuliza kichwa nikijua sasa maisha yananjia kwa kasi, hasa nikiwaangalia marafiki zangu wakirejea toka kidato cha tano na sita iliniuma sana,nikasema mimi nawawahi kabla hamjaanza kazi.

‘Na mungu bariki nikapata kazi kampuni ya maana, na kutokana na ujuzi wangu na utundu wa kimaisha nikaweza kufanya vyema kazini,na kujikuta Napata wadhifa wa juu, na haikupita muda nikachaguliwa kwenda kusoma nje, ...’akasema huku akimalizia soda yake.

‘Hapo nimeruka ruka maana ile tabia yangu ya uzinzi na ulevi sikuweza kuviacha, nilikuwa nabadili mabinti kama mtu anayebadili nguo, na umbile langu ni hii sura yangu ya mvuto kwa mabinti, utanashati na kuongea niliweza kufanikiwa sana kuwa ‘handsome boy’. Siku hizi hizi wanaitwa `ushari-baro’...’akasemana kucheka.

`Niliporejea toka kusoma nje, huku nina gari la kifahari, nikaona sasa nimeula, ...lakini akili kikanicheza, kuwa nikiwa na gari huku nina kazi nzuri, nitaishia kubaya, dawa ni kuoa mke. Hapa nikatuliza kichwa na kutafakari ni yupo kati ya mabinti niliokuwa na urafiki nao ananifaa kuwa mke wangu.

Kwaweli sikuweza kumpata anayenifaa,na wengine niliowagusia walifurahi na kutafuta kila mbinu ili niwaoe, lakini kila nilipowachunguza vyema, iligundua kuwa hawatanifaa,nitaishai kugonganisha magari tu, mwisho wa siku nikarejea kijijini na kukutana na wazazi.

Nilimuelezea mjomba, naye akaandaa shughuli ya kimila, ambapo wazee wa familia wanaitwa, unawakarimu chai na waakti mwingine soda au vinywaji vikali, lakini mjomba alinishauri kuwa nitayarishe cha ya mziwa na siku ikapangwa na mambo yakawawekwa hadharani.

‘Haya wazee wangu hapa nimepewa jukumu kama baba mlezi, maana mtoto wetu msomi toka Ulaya kaja kunipa habari kuwa sasa keshakua,....tunajua alishakua kiaina yake mwanzoni,hayo ya zamani yalikuwa ni ujana, maana hapa kwetu kesi nyingi zilikuwa zikimhusu yeye,lakini sasa amepevuka na ameona atulie na ikibidi apate mwenzake....ni jambo la kushukuru sana’akasema mjomba na kuanza kumiminia watu ile chai.

‘Ahsante sana mweneyzi mungu...’akasema mama na kunyosha mikono juu.

‘Ni vyema sana tukadumisha mila na desturi zetu na kwa utaratibu tunaoujua ndio hivyo, kuwa mwana akikua anatakiwa kuwaarifu wazee, na zamani walikuwa wakitumia pombe, siku hizi kwasababu tumeijua dini na mambo mengine kuwa hapa wanakusanyika watu wa imani tofauti, kinywaji kizuri ni chai ya maziwa, kusadidisha upevu wa elimu....na asali kidogo maana jambo lenyewe ni tamu kama asali. ...’akasema mjomba akitoa akitoa maneno yake toka kwenye vitabu, kwani alikuwa mpenzi sana wa kusoma vitabu.

‘Kwahiyo hii hapa chai maalumu, ya kidesturi, name kama mzazi nawanywesha kwa niaba yake, na kwa hapa ...tutaiita sadaka, ya kujitangaza kuwa yeye keshakua,...haya nimemaliza hilo zoezi’akasema mjomba.

Mama na shanagzi wakapiga vigelegele,

Walipomaliza kunywa kidogo ikafuata sehemu ya maswali, maswali hayo ni muhimu kutathimiwa kuwa kweli umekuwa na kama umkua umkua,kuaje, na nini nia yako, na kama unayo nia ya kujitangaza tua kuwa umekuwa basi wanamaliza, lakini kama nia yako ni zaidi ya hapo,kuwa unataka kuoa, utaulizwa maswali ya ziada , je kama unatka kuoa umeshapata mchumba, kama huna unahitaji kutafutiwa....

‘Mimi kweli nia yangu ni kutafutiwa...’nikasema, na wazee wakahema kwa kutokuamini.

‘Ina maana hawo wasichana wote uliokuwa ukitemebea nao hakuna aliyekuvutia, hakuna anayefaa kuwa mke mwema...ooh, mjomba usiniangushe bwana....?’ akauliza mjomba na kunisogela akanipiga piga mgongoni.

‘Mjomba, sikuwa nawazo la kuoa kipindi hicho, ilikuwa ni ujana kama ulivyosema, na sikuwa nawachunguza , nilichokuwa najua ni kujirusha nao tu, starehe za siku moja moja, na hata hivyo kwa hivi sasa nilipojaribu kuwachunguza mmoja mmoja nimegundua mengi, na kuthibistisha kuwa kati yao hakuna anayefaa kuwa mke wa nyumbani , nataka mke wa kikweli kweli...‘nikamwambia mjomba na kikao kwa ujumla.

‘Ndio tatizo lenu wanaume kutuzalilisha na mwisho wa siku mnatuambia hatufai..’akasema shsngazi kwa utani.

‘Usiingilie mambo kwanza, hivi unajau maana ya hiki kikao,nyie hamtakiwi kuongea kwanza,muda mtapewa , au ndio hayo maendeleo, hata kama ni maendeelo mnatakiwa kumuheshimu mwenyekiti,na wazee waliohudhuria.....sawa mke wangu....’akasema mjomba.

‘Saamhani nimekosa mwenyekiti, lakini ujumbe umefika...’akasema shangazi.

‘Hapo umenenakijana wetu....’akasemamjomba huku akiniangali kwa macho ya kutafakari, akasema tena;

‘Tuliona tukiachie wewe mwenyewe , maana siku hizi hakuna cha kuchaguliwa mke, ni wewe na maisha yako,ili usije ukatulaumu,...maana kuishi ndani ya ndoa sio mchezo, ukizingatia kuwa mnakuja kukutana watu wawili ambao kila mmoja anaweza akawa na tabia na hulka au hata mila na imani tofauti....sasani vyema ukalijua hilo mapema, ....’akasema mjomba na kuwaangalia baba na mama.

‘Lakini kama umeamua hivyo, basi sisi tumefurahi sana, na katika jambo ulilowahi kufanya la maana ni hilo, lakwanza kujaribu kudmisha mila na desturi zetu na tunakupa Baraka zote kwani tutahakikisha unapata mke wa kweli....’akasema mjomba, na baba naye akaomba aongee kidogo,na mjomba akampa nafasi.

‘Mtoto wetu, hilo uliloamua ni jambo jema sana, na kama alivyosema mjomba wako,ni jambo la heri na zawadi kubwa kwetu wa wazazi, lakini ujue sisi ni wazazi, sisi ni watu wa huku kijijini,maamuzi yetu yanaweza yakawa kinyume na ulivyotarajia,kwahiyo tunakuomba ulifikiri sana, sio kwamba hatutaki kukutafutia mke,....tunataka sana, lakini je ni vigezogani vilivyopo moyoni mwako,...’akasema baba.

‘Baba nikuulize swali, samahani lakini, je mama ulimpataje,au hata mjomba shangazi ulimpataje...?’ nikadadisi.

‘Sisi enzi za zamani sio sawa na enzi zenu,mimi mama yako nilimpata kama ulivyofaya hapa,baaadaya kujitambulisha wazazi wangu walinitafutia mama yako,na wao walishafanya uchunguzi kabla, walijua ni nani atanifaa, kuna mambo mengi wanayaangalia, kwanza ukoo, upoje, maana historia inajirejea,kuna ukoo hazijatulia, ...hilo tuliache, lakini kuna mambo ya magonjwa ya kurithi, kuna tabia mbaya kama uchawi na umalaya, ...hayo yote wazee wetu waliangalia kwa makini, na cha muhimu zaidi ni tabia njema...’akasema baba huku akimwangalia mkewe.

‘Kweli baba nawasifu maana namuona mama alivyo, nitashukuru sana nikimpata mke sawa na mama au na shangazi...’nikasema na kuwaangali wazazi wangu hawo wa kike.

‘Mungu atakusaidia kijana wetu...’akasema mama.

‘Nafikiri umemaliza mzee..?’ akasemamjomba akimwangalia baba , na baba naye akatingisha kichwa kukubali kuwa kamaliza yale aliyokuwa akitaka kuoengea.

‘Sasa kijana , ni kipindi cha maswali na majibu,... karubuni wazee ....’ akasema mjomba, maana hakutaka kuongea yeye mwenyewe na kulikuwa wazee wengine, baba wadogo, na wakubwa katika familia,na akaanza kuongea baba mkubwa, akakohoa kwanza na kusema;

‘Kijana ni muhimu sana ukalijua hili kwa ajili ya vizazi vyenu, hebu tuambie wewe unataka mke wa namna ipi,mrefu ,mfupi, nk, tabia na mengineyo tuachie sisi,ila kimtizamo wako ungelipendelea wa maumbile, au sura ipi...?’ akauliza baba mkubwa na kunifanya niingie kwenye ndoto za kuwazia mke huyo ninaye mtaka nataka aweje.

Ilichukua dakika chache nikiwaza,na hapo nilikuwa nikiwawaza wale mabinti niliowahi kuwa na urafiki nao,je akiwa kama vile,mrefu,mwembama, au mfupi,au awe mnene, au awe.....nikajikiuta siwezi kutathimini hayo, nikasema;

‘Mkitaka nichambue namtaka wa namna ipi nitawafanya mshindwe kunichagulia na kumpta huyo aliye kwani taswira ya akili yangu,maana hata mimi mwenyewe sio rahisi kusema awe katika maumbile gani,....hiyo kazi nawaachia nyie,...na tatizo nataka ambaye damu inachemka,maana naogopa kusema kuwa huenda mke mmoja hatanitosha....’nikasema nikionyesha wasiwasi.

‘Unasema nini...?’ akauliza mjomba.

‘Acha utani huo, unaongea hayo wakati wapo akina mama, unawadharau....utashindwa mwenyewe...’akasema baba.

‘Nasema hivyo baba kwasababu najijua, mke mmoja sitaweza kuvumilia naye, naona kama nitamkosea, mimi damu inachemka sana ....kama ingeliwezekana, maana pesa sio tatizo, wake wawili,au watatu naweza kuwamudu na kuishi nao....sijui lakini ngojeni kwanza nioe huyo mmoja , halafu tuone...’nikasema,huku wazee wakiniangali kwa mashaka.

‘Sikiliza mjomba, mke sio pipi au chakula au nguo, mke ni kitu cha heshima, ukishaoa unatakiwa utulie naye, usiruke huku na kule tena, cha muhimu ni maelewano,...nichukulie mfano wa nyama, kwani wewe kula nyama, hata uwe na uchu vipi , ukisha ila nyama siku mbili tatu utakinahiwa tu, halikadhalika ukioa, utaishi naye, mwishowe utagundua kuwa nyama ni ile ile hata uende wapi, ....’akasema mjomba huku akiangalia huku na kule.

‘Kijana wetu swala ni mapishi tu, kama alivyosema mjomba wako,nyama ni ile ile, uruke huku na kule, nyama ni ile ile....’akaongezea baba mmojawapo.

‘Mjomba,kama kweli una nia ya kuoa, hakikisha unajituliza, kiukwelii sisi tulikuwa na tabia hiyo tukiwa vijana, hasa mimi , wananijua sana hapakwetu, au huko nilipokuwa nikifanyia akzi, lakini siku ile nilisema sasa nimeoa, nina mke ndani,nilitulia na nikaheshimu ndoa yangu, maana ndoa ni kitu cha heshima na thamani kubwa sana...’akasema mjomba.

Na kweli sifa za mjomba ni nyingi,alikuwa moto wa kuotea mbali, ndio maana kwenye kabati lake la vitabu , vitabu vingi ni vya kimapenzi mapenzi.

‘Ukishaoa ujue huruhusiwi tena kuruka ruka, nikuambie kitu, ndoa inakuwa imekufunga, kama kifungoni, unatakiwa kufuatilia masharti yake,...hilo ulijue, na ukiyavunja,ujue unaivunja ndoa...kuna usemi usemao kuwa, ukifanya ufisadi ndani ya ndoa, mfano uzinzi, ujue na wewe utafnayiwa hivyo hivyo, kwa mkeo au kwa watoto wako, hilo uliweke akilini....’akasema shangazi.

‘Kweli ili uyashinde majaribu kama umepatwa na mitihani, jaribu kuwaza, nafanya hili kwa binti au mke wa mtu, ina maana na mimi nitafanyiwa hivi hivi kwa mke wangu au binti yangu...je nitafurahi nikigundua, au hata nisipogundua,...kwasababau ndivyo itakavyokuwa...hayo hulipizwa hapa hapa duniani...’akasema mama.

Baada ya kuaswa na karibu kila mtu, na ilipoonekana hakuna zaidi la kuongea kuhusu maadili mema, mjomba akasema;

‘Sasa kijana umeskia, je unasemaje upo tayari kutafutiwa au unahitaji muda wa kuchunguza mwenyewe, sio kwamba sisi tutakutafutia tu, na kusema huyo hapa mkemuoe, tuna taratibu zetu safi kabisa, mwenyewe utafurahia, ....hilo tunalijua wazee wako, je unasemaje..?’ akauliza mjomba.

‘Nipo tayari wazee wangu, nimeyasikia yote na nimeelewa,nipo tayari, maana mimi kwasasa ninachotaka ni mke,na nina imani kuwa nyie kwa hekima zenu nitampata mke ambaye atanifanya nitulie nyumbani, ....nisiwe naruka huku na kule tena....’nikasema.

‘Sasa kijana umetupa kazi , na hili ndilo tulikuwa tunalitaka, kwanza tulia wiki moja, sisi tulifanyie kazi,halafu tutakuambia nini cha kufanya....usiwe na wasiwasi tutakupatia mke ambaye atahakikisha kuwa damu yako imetulizwa na kwa ajili ta familia yako ya baadaye....eti kuwa mkemmoja hatakutosha, hayo ni mawazo yako na hisia zako tu...haiwezekani ukaoa wake wawili kwa siku moja...’akasema baba mkubwa na Mjomba akacheka huku akiniangalia.

Rafiki yangu alipofika hapo akatulia kidogo name nikapata muda wa kumuuliza swali;

‘Duuh, ina maana na ujanja wako wote huo ulitafutiwa mke,...na mke mwenyewe ndiohuyo unayemlaumu kuwa kakuingiza kwenye matatizo au ni yupi huyo?’ nikamuuliza
Akapiga miayo ya njaa,halafu akaangalia kule kwa wahudumu, chupa yake ilikuwa tupu, nikajua nini kinachotakiwa, nikajipigapiga mfukoni, na baadaye nikaona ni vyema tuagize chakula cha bei rahisi ,na tulipomaliza kula akasema;

‘Lete soda nyingine...ili nikupe habari za jinsi nilivyotafutiwa mke, ....niakumbia jambo wazee wetu wana busara sana kwa hilo, sio kwamba wanawake wanaletwa mbeel yako halafu unaambia haya chagua , unamataka nani kati ya hawo, ....hekima ilitumika, kujali hisia za huyo anayetafutwa,maana ikitokea humuhitaji,na yeye keshaambiwa kuwa yupo jamaa anataka kukuoa,itamuuma sana...’akasema rafiki yangu huku akichokoanoa meno yake na kijiti.

‘Sasa ilikuwaje...?’ nikauliza.

`Kwanza hebu fikiria mabinti wa kijijini, ...hawajajipodoa,...na unajua pilika pilika za kule...na mimi nimeishi mjini nimewaona mabinti wa mjini walivyo, nimeishi Ulaya,nimewaona mabinti wa kizungu, na...halafu upo kijijini unatafuta mke, unakutanishwa na binti katoka shamba, kachooka, mchafu...lakini tabia ni mia kwa mia....utasemaje....?’akaniuliza.

‘Kwakweli mimi hapo sina jibu la kukupa, nataka kujua wewe ilikuwaje,ulimpataje huyo mke uliyemuoa...?’nikasema.

‘Haikuwa kazi kubwa kumpata huyo mke wangu wa kwanza ,kwani moyo wa huruma na upendo ndivyo vilinisukuma nimchukue huyo mke wangu wa kwanza, na sikujua nini kitaathiri hayo baadaye, lakini kwa hali niliyomkuta nayo wakati huo nilidondosha machozi....hadi leo nikiwaza nijalaumu,nakujiona mtenda dhambi mkubwa....kweli ishi na omba yajayo yawe mema,maana ya leo ni ya leo ya kesho huwezi kujua yatakuwaje...`hujafa hujaumbika...’ akasema rafiki yangu na kunifanya name niwaze kidogo.

‘Siliza rafiki yangu ngoja nitulie kidogo niwaze , maana nikifika hapo na kumkumbuka mke wangu wa kwanza nasononeka sana moyoni,...kweli nilimtendea isivyo haki, sijui nitatubuje dhambi hizo, sijui....’akasema na kuinama kidogo huku akionyesha hisia za kuwaza.

NB.Hebu na sisi tuwaze kidogo, ...ilikuwaje...Tupo pamoja, au nimechemsha? Tatizo lenu mnakaa kimiya hamsemi, ili nijue nipo na watu wananifuatilia. Haya tusubiri sehemu ijayo.
Swali kwako: Je wewe au nyie ilikuwaje mpaka mkaoana?

WAZO ZA LEO: Ndoa ni kitu cha hesima na kitakatifu,tuziheshimu ndoa zetu kama tunataka baraka,kinyume chake ni mikosi, kwani ndoa hujengwa na wanandoa wenyewe na wakuivunja hiyo ndoa ni hawo hawo wanandoa wenyewe.

Ni mimi: emu-three

7 comments :

Anonymous said...

Wewe mkali, sikupatii mfano, licha ya kuwa unajitolea, huenda hata kazi hujapata, bado watuletea hivi vitu...mawazo ya kimaisha bado watujali

Anonymous said...

kaka yaani sichoki kusoma visa vyako inshallah MUNGU akutunze daima

Rachel Siwa said...

Mmmmmmhhh Ndugu wa mimi naishiwa maneno!!pia asante kwa wazo la Leo, siwanasema pia Mjenga Nchi ni mwanaNchi na Mvunja Nchi ni MwanaNchi!!!!!!Mungu akubariki sana kwa kazi za mikono yako,Mikono yako inakazi kubwa na yenye Thamani!!!Pamoja sana ndugu yangu.

emuthree said...

Nashukuru sana ni kweli najitolea kama moja ya malengo yangu huenda nikaja kufanikiwa

emuthree said...

Insha-Allah, akujalie na wewe tuzidi kua pamoja

emuthree said...

Amin, ndugu wa mimi . Nawe mungu akubariki pia kwani mikono yako ni tunu kwetu, ibarikiwe tuendelee kuwa pamoja

Anonymous said...

Undeniably believe that which you said. Your favorite reason seemed to be on the net the easiest
thing to be aware of. I say to you, I certainly get irked while people
consider worries that they just don't know about. You managed to hit the nail upon the top and also defined out the whole thing without having side effect , people could take a signal. Will likely be back to get more. Thanks

My web-site; todo