Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, March 6, 2012

Hujafa Hujaumbika-Utangulizi




Maisha ni kupanda na kushuka, na mitihani ni jadi ya binadamu, sizani kuna mtu kazaliwa hadi kufikia utu uzima, hajawahi kupambana na matatizo,sijui kama wapo. Na ili kujifunza, ni vyema tukaaangalia yale yaliwasibu wenzetu,na kama wewe hujakutwa nayo, ni bora ukachukua tahadhari.

Visa ninavyojaribu kutoa ni matukio halisia, ili mimi na wewe uweze kujifunza. Katika rudia yangu kusoma yaliyopita nikakutana na utangulizi wa kisa hiki, ambacho niliahidi kama tukijaliwa tutaweza kukiweka hewani, naona albda ni wakati muafaka wa kuja kukiweka machoni mwenu ili tuweze kutafakari pamoja.

Kisa hiki kilikuwa na utangulizi huu:


Ilikuwa ni siku ya Jumamosi ya tarehe 19-09-2009, nikiwa nasubiri daladala nifike Kariakoo,kuangalia kuwa sikukuu itaendaje.

Sikuamini niliyemuona mbele yangu kuwa alikuwa mmoja wa `Collage-mate wangu', nakumbuka kwa mara ya mwisho nilikutana naye akiwa ndani ya Benz lakifahari na my wife wake na kiti cha nyumaa cha hilo gari aliweka mbwa-mkubwa. Niliogopa hata kumsimamisha, siunajua tena ukikutana na wenzako unaowajua halafu ukajikuta wewe ni TZ 11, unajisuta mwenyewe. Lakini yote ni makadrio ya Mungu hamuwezi nyote mkawa sawa.

Nakumbuka tukiwa shuleni jamaa huyu alikuwa kati ya vijana watanashati, na pamoja na utanashati alikuwa nazo, na zaidi ya hapo ni mnato. Na hii ni hulka ya kibinadamu unapokuwa umejaliwa kipato, uzuri , au cheo mnato haubanduki, hata sauti hubadilika, utaongea kama mzungu hata kama kizungu hukijui, utaongea kama bosi hata kama hujawahi kushika nyazifa yoyote kwenye ofisi yoyote, hii ni hulka ya kibinadamu.

Mara lile gari likasimama mbele kidogo na niliposimama, nikajifanya sikuliona na kuangalia upande wa pili wa barabara, lakini haikusaidia kitu, kwani honi ya lili gari ilisikika, na mara nikasikia sauti yangu ikiitwa. Ilibidi nisijivunge, niligeuza kichwa na kuelekea pale gari liliposimama, huku moyoni wangu ukijisemea huenda hata kama sitapata lifti,lakini senti kidogo nitapatiwa, hii ni hulka yetu sie matawi ya chini, kuomba upate msaada kwa unayemuona anauwezo, kwasababu huna jinsi.

Nilichepuka hadi pale gari liliposimama,na mara kiyoo kikashushwa, na nilijikuta nikihema kwa woga, sio kwamba mimi ni mwoga, lakini lile jibwa, siunajua mijibwa mikubwa ilivyo, basi lilie likuwa miongoni mwa hiyo mijibwa. Lilikuwa limetulia kiti cha nyuma na macho yake yakiniangalia kwa hasira, na kusubiri nini bosi ataliamurisha.

`Usija-ali, rafiki yangu, vipi unaelekea wa-api, manake nampeleka wife kidogo shooping,na halafu...' alipofika hapo akaangalia nyuma ya gari, nikamuelewa ana maana gani.

`Usijali rafiki yangu, mimi nami namsubiri jamaa mmoja hapa, halafu nitaelekea huko ninakokwenda, usijali, hali zenu lakini' nilisema kwa hali ya kutojiamini kidogo

`Ok, basi chukua elifu kumi hii utachukua teksi , halafu, hii ni bussiness kadi yangu tutawasiliana' Alinipa business kadi yake wakati huo mai-wife wake alikuwa akiniangalia kwa dharau, na alimgusa begani mumewe kuonyesha kuwa wanachelewa.
Hii ilitokea takribani miaka mitano iliyopita, leo sura ninayoiona mbele yangu inafanana kabisa na yule rafiki yangu, lakini...

Nilimsogelea ili kuhakikisha, ni kweli ni yeye, pale alipo alikuwa kachoka kwakusimama,na mbaya zaidi alikuwa kashikilia fimbo iliyokuwa ikimsaidia kusimama, kuonyesha kuwa ana matatizo katika mguu au nyonga, chini kavaa ndala. Niliingiwa na simanzi kwasababu hata ndala alizovaa sio zile zakifahari kama ninavyomjua tabia yake. Jamani acheni Mungu aitwe Mungu, ina maana binadamu unaweza ukabadilika ghafla kutoka hali moja kuwa nyingine kiasi kwamba hata sura inabadilika kabisa.

`Ndio rafiki yangu usishangae sana, mimi ndio yule yule uliyemjua, ila mambo yamekwenda kidogo vibaya,lakini ninaimani kuwa baada ya siku kadhaa,mambo yatanyooka, siunajua tena fitina za watu, wameniharibia mipango yangu yote kiasi kwamba najuta hata kumwamini mtu. Wamefanya hata mke wangu kanikimbia..' alianza kuongea kama kaseti iliyofunguliwa.

'Fitina ipi bwana isije ikawa ndio nyie mafisadi, ....simesikia ulikuwa kwenye mkondo wa....'nikaanza kumtania.

'Najua mengi yatasemwa, lakini ukweli unabakia pale pale kuwa yote niliyokuwa nikifanya ni kwa juhudi zangu, ....yaani sina hata cha kukuambia, maana hapa nilipo naumia sana...we acha tu, kama una chhote nisaidie nipate nauli ya kufika nyumbani...'akasema na kweli nilimuonea huruma.

Jamani nia kubwa hapa sio kumteta rafiki yangu,lengo kubwa ni kuonyesha hulka zetu wanadamu,ambazo wakati mwingine naweza kusema kuwa tunamkufuru mungu pale tunapojiona tunahali nzuri kikipato , kiuzuri kiwadhifa nk. Tunapenda kujisahau nakujiona tumefika....tunapokuwa katika hali hiyo hata mungu hajulikani tena.

Hivyo ni kujidanganya,kwani katu hatujafika kwasababu kabla hujafa hujaumbika, huwezi jua nini makadrio ya muumba,leo mzima kesho mgonjwa taabani kitandani,. Wakati ukiwa na nguvu zako, afya yako, uwezo wako kikipato, hebu jaribu kuwekeza, angalau kiubinadamu, ili hata ukikwama, wenzako hawatakusahau, .... lakini leo hii unajona una miguvu, unatamba huko na huko,kesho unatembea mguu mmoja haupo. Yote hii ni kudura za muumba.
Nenda Muhimbili, uone miujiza ya mungu, nenda kwenye mahospitali, utakiri kweli sisi sio kitu,ni wakupita tu, jana yule alikuwa na afya yake, hana shida, anatamba kila kona, leo hii kalala hata kujigeuza hawezi, ...jamani tumuogope mungu, sawa, tumia leo ya kesho huyajui, lakini siku ukiyajua utaishia kusema `ningelijua, kwani Hujafa hujaumbika.

Tunatakiwa tukiwa katika hali nzuri au mbaya tumshukuru muumba kwani yote hayo hutokea kwa sababu, na sababu mojawapo ni ili tupate fundisho. Kama wewe unacho wakumbuke wasio nacho,watendee wema na punguza kunata,kwani huwezi jua huo mnato unaweza kugeuka kuwa mchatomchato. Kama wewe ni bosi, usiwadharau wafanyakazi wako, watendee haki, bila kujali mapungufu yao, kwani kila mmoja anayoriziki yake , ndio maana unapata unachokipata.

Na kama wewe huna kitu basi mshukuru mungu kwasababu huenda mwenyezimungu anakukwepesha na mitihani kama hiyo inayowapata walio nacho,huenda ungapata kama wao ungekufuru zaidi na hata kugeuka fisadi wa kutupwa.

Kisa hiki nakitafakari kidogo, kabla hatujamaliza kisa kilichopo cha Akufaaye kwa dhiki, ambacho kiliaznzia hapa sehemuu ya kwanza.

Kwanza Itabidi kumuomba rafiki yangu huyo aliyefikwa na mkasa huo, kama ataniruhusu nikielezee au la...



Ni mimi: emu-three

1 comment :

Yasinta Ngonyani said...

ndivyo ilivyo aliyeshiba hamjui mwenye njaa...na pia huwa wengi hawataki kuamini kama inaweza kuwapata walio na uwezo...