Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, March 22, 2012

Hujafa hujaumbika-8




Polisi walifika haraka hata isivyotarajiwa, hikuwa kawaida yao kuitwa kwenye tatizo na kufika haraka hivyo, wengi walihisi kwasababu ilimuhusu mtu tajiri anayejulikana sana. Watu wakawa wamezingira lile eneo, na kila mmoja alikuwa akiongea lake;

‘Unafikiri kauliwa na nani huyu mtu...?’ kauli hiyo ilinishitua sana, na kuangalia huku na kule kama kweli kuna mtu ananiona, na pole pole nikahesabu hatua hadi nyumbani, nilipofika karibu na nyumbani nikaona sare za polisi zikiwa zimetanda mlangoni, nikashituka.

‘Hivi kumetokea nini, nikamuuliza jamaa mmoja aliyekuwa katokea huko kwenye tukio.

‘Yule tajiri mkuu wa ziwani kakutwa amekufa, na inasadakiwa kauliwa na majambazi, kwani huenda alikuwa na pesa....’akasema huyo jamaa.

Sikurizika na hizo kauli, nikajisema moyoni, kama kauliwa na majambazi mbona askari wapo nyumbani kwetu, haiwezekani, na akilini nikakumbuka tukio lililopita na hapo moyo ukanienda mbio ina maana polisi wananitafuta mimi kuhusiana na hilo tukio, mbona huyo jamaa alitoka mle akiwa mzima,....

Nikumbuka sana hali ilivyokuwa baada ya kuingia mle ndani ya chumba.

Nilimkuta jamaa kavua suruali nusu na huku mikono ikiahangaika na miguu ya Yule binti, Yule binto hakukubali kirahis akawa anapigana kwa kutumia miguu yake,

‘Hebu tulia nikuonyeshe raha ...ni kidogo tu tnamaliza....’akasikia huyo jamaa akisema.

‘Unataka kunifanya nini wewe mzee, niachei sitaki...jamani huyu mzee ananibaka....’sauti ikasikika wakati name nimeshaingia, na panga mkononi,...nikalipiga mgongoni kwa huyo jamaa kiubapa, nakumbuka kabisa sikumkata, nilimpiga kwa upaba, na alishituka sana na kugeuka haraka;

‘Hapana, simbaki, tumekubaliana tu....’akasema huku akiniangalia kwa wasiwasi

‘Wewe mzee mzima huna aibu, unataka kumbaka huyu binti wa wau halafu unadai mumekubaliana,kama mumekubaliana mbona anapigana na wewe....’nikasema na kumpiga tena na ubapa Yule mzee, na akatoa mguno wa maumivu, na haraka akaanza kuvaa suruali yake huku akikimbilia nje.

‘Sikumkata kabisa, hilo nina uhakika nalo...’nikasema

‘Kwani alikutwaje ?’ nikauliza.

‘Alikuwa kakatwa na mapanga, tena sio moja, zaidi ya moja, na kilichomuua ni kutokwa na damu nyingi, na alikutwa akiwa kabakiwa na chupi tu, ina maana waliofanya hivyo, waliamua kuchukua hadi suruali na shati, na koti lake la bei mbaya...’

‘Sasa polisi walijuaje kuwa ulikuwa huko nyumbani kwa binti Yatima, au ilikuwaje, hebu tuhadithie vyema...’nikamuuliza jamaa na kumpa nafasi atohoe kisa chenyewe kilivyokuwa.

**********

Kuna mtu mmoja alikuwa akiwinda, na alipofika kwenye njia panda, aliona kitu kimetuna, akajua ni mnyama, akaweka mshale vyema, ....lakini akasita kwanza mbona mnyamamwenyewe hatikisi, ndipo akaamua kumsogelea na mara akaona mtu akiwa uchi...kama alivyodai, lakini hakuwa uchi kabisa, alikuwa na chupi, ....

Muindaji Yule akaingiwa na udadisi, akaona ajariu kumtambua kuwa ni nani,...alipomsogelea akamgundua,....maana jamaa huyo ni maarufu kila mtu hapo kijijini anamjua, ..... na hapo hapo akapiga mayowe, na watu wakakusanyika.

‘Ni nani huyo....?’ watu wakauliza.

‘Huyu ni tajiri wa ziwani, ..bila shaka, kafumaniwa nini maana huyu jamaa ni mwingi wa wake za watu...’akasema mmojawapo.

‘Iteni mjumbe haraka, na msiguse kitu chochote....’akatoa wazo mzee mmoja. Na kweli mjumbe akaitwa haraka na kwa muda huo watu walikuwa wameongezeka, kila mmoja akitaka kumchngulia huyo marehemu...., alikuwa keshajulikana kuwa ni marehemu, maana mjumbe alipofika alitumia ujuzi ake, na kugundua kuwa jamaa hayupo hai.

Na baadaye polisi ikafahamishwa na kufika eneo la tukio. Kama ujuavyo polisi wananusa kama mbwa, wakaanza kazi yao ya upelelezi, haikichukua muda wakagundua kuwa jamaa huyo alionekana akiwa nyumbani kwa binti Yatima, na mimi nilionekana nikiingia humo.

‘Nani alitoa hizo taarifa....?’ nikauliza.

‘Kwakweli mpaka leo sijui, ila polisi wakaelekea kwetu , hawakunikuta, na kipindi hicho mkutano ulishakwisha kutokana na hilo yowe. Unajau kijijini tena hakuna dogo, kila mmoja alikimbilia huko lilipotokea yowe, na pale walibakai wazee wachache tu. Baada ya taarifa kupatikana Wazee wakakutanika na walinzi wajadi kuanza kuchunguza wakishirikiana na polisi, na hapo kwa kauli ya polisi ni mimi nitafutwe ili kuisaidia polisi,lakini sikuonekana.

‘Huyu jamaa yupo wapi, maana kwa mara ya mwisho alionekana akiingia nyumbani kwa huyo mnayemuita binti Yatima, na huko ndipo alipoonekana huyu marehemu kwa mra ya mwisho akiwa hai, na hata huyo binti Yatima mwenyewe haonekani, inaonyesha kuna uhusianao wa hicho kifo na wao, kwanini watoweke ghafla...’akasema polisi.

‘Hizo ni hisia tu,maana hawo watu unaowataja hawana tabia hiyo unayoifikiria, watu wenyewe wanaogopa hata kuua mdudu sembuse kuua mtu...hapo kuna walakini, nahisi huyo jamaa kauliwa na mjambazi au kafumaniwa maana huyo jamaa tunamjau sana....’akasema mzee mmoja na wengi wakasadiki maneno yake na kusema ni kweli.

‘Kama ni kweli au sio kweli, cha muhimu tunataka tuonane na huyoo kijana,na huyo binti, tukiwahoji kama hawahusiki basi, tutaendelea kumtafuta muuaji, lakini hawo wanahitajika kituoni haraka....’akasema polisi mmojawapo huku akiwaamrisha vijana wake wanitafute mimi na binti Yatima.

Siku ikaingia doa na maandalizi ya harusi yakabadilika na kuwa msako msako wa kunitafuta mimi,kila nyumba ilipekuliwa. Na ilipoonekana ni kazi kubwa polsi waliitwa polisi wengine ili waje kusaidia kunitafuta mimi,....walikuja wanjeshi na silaha kubwa kubwa,...siunajau tena kesi ya mauaji, na tena familia ya huyo Tajiri ilikuja juu na kusema lazima mimi nitafutwe nikajibu hayo mashitaka.

‘Atakuwa ni huyo huyo muuaji,kwanini atoweke...’akasema mmoja wa jamaa za marehemu.

‘Hata zawadi tutatoa kwa yoyote atakaye mpata...’akasema mtu mwingine mmoja wa jamaa za marehemu.

********

Huko nilipojificha sikujitokeza kabisa, kwani nilijua nini kitanipata nikikutana na polisi, siunajau polisi wetu walivyo, wakikushika, ukifika salama kituoni ushukuru mungu, labda utafika ukiwa umevunjika mkono, au mguu, huo ndio usalama wako,...

‘Kwanini sasa tujifiche huku, kwani tuna kosa gani..?’ akaniuliza binti Yatima.

‘Hatuna kosa, lakini ni bora kujificha ,kuliko kujitokeza,kwani polisi wakituona wataanza kutupiga hata kama hatuna kosa, ikizingatiwa kuwa aliyeuwawa ni mtu tajiri...’nikamwambia binti Yatima.

‘Tajiri gani wa kubaka watu, nakushuru sana kaka, maana pale nguvu zilishaanz akuniishia,na nilisema akinifanya lolote baya, najiua, niende nikaonane na mama yangu, nilishachoka na mateso, nakushukuru sana kaka, sijui nitakulipa nini, mungu mwenyewe atakulipa badala...’akasema huyo binti huku machozi yakimtoka.

‘Usiajali, nshukuru kuwa hakuwahi kukufanya lolote...au aliwahi kukufanya lolote maana sijapata hata muda wa kukudadisi...?’ nikamuuliza.

‘Zaidi ya kuniangusha chini, na kunibana miguu, hakuweza kunifanya lolote, nilikuwa nikipigana kwa kutumia miguu, ...alikuwa an inguvu, lakini mungu alinisaidia....na niliona kama mama akiniangalia akisema mwisho wa yote haya unakuja...kwahiyo nikajua ndio mwisho wangu wa kuishi...’akasemahuyo binti.

‘Ndio mwisho wa yote hayo umekuja, usiogope tena, ....nakuahidi hilo...nikasema, na mara akaja mweneyji wetu .

‘Vipi kuna nini kinaendelea huko kijijini..?’ nikamuuliza.

‘Usiombe, polisi waliomwagwa hapo, utafikiri kuna tukio kubwa,....’akasema huku akiweka mizigo yake aliyokuja nayo , na aligeuka kutuangalia na kusema

‘Ni kwasababu mtu mwenyewe ni tajiri na alikuwa akimwaga pesa kwa maaskari kama njugu wakati wa uhai wake,.... sasa wanajua hayupo tena watakosa pesa za bure, hata hivyo ndugu zake na wao kwa vile wana uwezo wanataka kuonyesha kuwa wanamjali jamaa yao, licha ya kuwa wanajua tabia zake mbaya...’akasema huyo mwenyeji wetu.

‘Sasa unatushauri nini...maana polis wakigundua kuwa tupo hapa na wakaja kutushika na wewe utakuwa hatiani....?’nikamwambia huyo jamaa.

‘Wewe usijali, wewe ni rafiki yangu nitahakikisha kuwa upo salama, na mambo ya polisi mimi na yajua sana, hasa hawa polisi wetu , ukilogwa kujitokeza tu utapokelewa kama mpira wa kona, kama mtapona ni bahati yenu, bora mjifiche huku huku, hakuna anayeweza kugundua kuwa mpo huku....’akasema rafiki yetu huyo.

Siku kadhaa zikapita, na polisi wakaanza kuondoka kurudi kwenye vituo vyao, huku wakiacha matangazo kuwa atakayeniona atoe taarifa haraka, na zawadi ikitangazwa milioni kumi kutoka kwa ndugu wa familia hiyo...

Alipotuletea taarifa hizo huyo mwenyeji wetu pale tulipokuwa tumejificha nikajikuta nikiuliza kwa mshangao;

‘Milioni kumi...?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Tena...., kwao milioni kumi ni sawa na elifu kumi...kwahiyo haikuwa ni gharama sana, walisema huyo atayeniona na kutoa taarifa polisi wanamlipa wao wenyewe pesa tasilimu....’akasema jamaa.

‘Sasa ina maana uchunguzi haufanyiki mpaka watukamate, kwa mtindo huo huyo muuaji au wauwaji watakuwa wameshapotea mbali...?’nikamuuliza jamaa yetu.

‘Unawajua polisi wana mbinu nyingi, hiyo ni mbinu yao mojawapo, ...usifikiri wao ni wajinga, uchunguzi upo unafanyika, lakini ili kuwafanya hata hawo wauwaji wahadaike ndio hivyo wanajifanya wanatafuta mtu mmoja huku wakiendelea kuwahoji watu nakutafuta ukweli zaidi kisirisiri,...’akasema rafiki yangu a baadaye alipoondoka binti Yatima akaniuliza.

‘Ina maana huyo rafiki yako hazitaki hizo milioni kumi...?’

‘Hapo nami najiuliza,...hatuwezi tukamwamini moja kwa moja, ....ndio huyu ni rafiki yangu maana nilisoma naye shule ya msingi, tulikuwa tukicheza naye, ..... lakini hali zetu zilivyo ...na ukaweka pesa ambayo ndiyo kila matu anaifukuzia,....lolote linaweza kutokea ...lakini kwa hivi sasa tuvute subira, na naona wewe kapike,ili mimi nitafakari la kufanya...’nikasema huku nikishika kichwa sehemu ya machoni,kuonyesha anawaza jambo.

Binti Yatima, aliondoka kushughulika, na wakati anashughulika, mawazo yangu yakawa yanakwenda na baadaye yakarudi kumtizamahuyo binti,...kwa siku hizi tulizokaa hapo, niliona mabadiliko ya haraka kwa binti huyu,mwili wake ulianza kurejea,na sura yake ikawa inaonekana...kweli ni mzuri, na binadamu huchakaa kutokana na shida, akikaa vyema, ...

‘Chakula tayari kaka....’akanishitua binti Yatima.

‘Hiyo kaka unaipenda sana, hujui wewe sasa ni mchumba wangu....’nikamwambia.

‘Hata nikiwa mchumba wako, kaka ni heshima tu,...na namuomba munguiwe hivyo kwasababu wewe ni mtoto wa watu, sizani kwamba wazazi wako watakubali unioe mtu kama mimi....hali niliyo nayo, na mazingira yetu...sijui namuomba mungu tu, anisaidie....’akasema Yule binti huku akiinama kwa huzuni.

Nilimwangalia kwa makini hutuma, upendo vikaniingia, nikamsogelea na kumshika, nilimvuta kwangu nikawa kama namkumbatia, lakini kiupande upande...kwani hata hivyo, haikuwa rahisi, akawa anajitahidi kujitoa mikononi mwangu.

‘Sikiliza mrembo, mimi nimezamiria hivyo, na sio siri,hilo limepitishwa kweney kikao chetu,ingawaje niliodoka wakati bado wanalijadili, kitu cha muhimu ni wewe kujiamini, kuwa u binti mrembo na una sifa zote za kuolewa na mtu kama mimi...kama tulivyyongea awali, nataka nikuoe, nataka uwe mke wangu, sio utani...kwani wewe hunipendi...au una mtu mwingine ..?’ nikamuuliza.

‘Mhhh, unanichekesha kweli, niwe namtu mwingine, hivi wewe hujamsikia mama Bonge, hakuna mtu anayeruhusiwa kunioa mimi bila ya kupitai kwake,...wote waliojaribu walinyosha mkono, mapaka yeye akubali na alisema mpaka amjaribu kuwa kweli anafaa...sasa sijui kujaribu huko ni kwa namna gani....’akasema huyo binti.

‘Mwanamke balaa huyo, sikuamini alivyotaka kunishika kwa nguvu, hivi ana akili kweli...lakini huenda sio kosa lake, unajau binadamu tunauzaifu , kila mtu ana uzaifu wake, na....mkishakuwa mke na mume mnatakiwa kujuana vyema, ...je yeye na mume wake hukaa na kulijadili hili, wanapaya muda huo kweli...?’ nikamuuliza huyo binti.

‘Aaah, mimi sitaki kujadili maisha ya wazazi wangu, lakini muda mwingi baba anakuwa hayupo, kama akiwepo sikjui kama wanajadiliana,....sijui maana naona akiwepo baba ni mzozo tu...sijui lakini hayo hayanihusu mimi kama mtoto...’akasema binti.

‘Sio kwamba nataka uongee maswala ya baba na mama yako, hapana, ninachotaka kukuonyesha hapa ni jinsi gani mke na mume wanavyotakiwa wawe, mimi napenda sana uwe huru ...tukiwa ndani kama ken a mume, nataka uwe unajadiliana na mimi, kama kuna jambo ambalo unahisi linatufaa, basi tukae tujadili, na ....’mara mlango ukagongwa kwa nguvu na sisi tunainuka haraka....

**********

‘Mimi nimewaiteni hapa makusudi, maana kama mnavyoona polisi wamatanda kila kona na lengo lao nikumtafuta kijana wetu,...eti kwa kushukiwa kumuua huyo tajiri...lakini cha ajabu hawamtafuti Mwanamke Bonge ambaye naye katoweka nyumbani kwake, mumewe anamtafuta kila kona hajui wapi alipo....’akasema mjomba.

‘Hivi kweli huyo mama kaenda wapi, maana mimi simwamini kabisa Yule mama, ana tama sana ya pesa, ana weza kufanya lolote kukiwa na pesa,.....na naona ajabu watu hawamzungumzii huyu mama, ...hivi kweli kaenda wapi, maana katoweka kiajabu ajabu...’akauliza mzee mmoja.

‘Kama sio mbinu za polisi basi kuna jambo limejificha hapa, ndio maana nimewaiteni hapa tulijadili hili swala kwa makini, na hapa nimemualika mjomba wa binti Yatima,....natumai wote tunamfahamu. Sasa kama kikao chetu kilivyoamua kuwa tunataka kuunga udugu, na yeye na ndugu zake wameliunga mkono hilo jambo na wamesema watatoa ushirikiano wa kila hali, ila sasa limezuka hili kubwa lao....’akasema mjomba.

‘Na hili linatuchanganya maana hatujui kuwa huyo binti yupo wapi, yupo na huyo kijana wenu, au yupo na mama Bonge, au kuna nini kimemtokea, ...ya mungu mengi....’ akasema mjomba wa binti Yatima.

‘Tetesi ni kuw yupo salama na kijana wetu,....hilo hatutakiwi kuliongea sana, na kwa kuwatonya tu, ilivyotokea ni kuwa,....kijana wetu ana hisia za hatari, labda tuseme mungu kamjalia hicho kipaji, alihisi kuna hatari inataka kumtokea binti yenu, na akaondoka hapa haraka, ... alipofika huko kweli akakuta hiyo hatari, jamaa huyo alikuwa katika harakati za kumbaka binti yenu,....hatujui zaidi ya hapo...’akasemamjomba.

‘Kuna watu walisikia kilio cha huyo binti akiomba msaada, na ndipo akafika kijana wetu na kumuokoa...’akasema mzee mmoja.

‘Ina maana polisi hawajui hayo...?’akauliza mzee mmoja.

‘Watakuwa wanajua,ndio maana nasema kama sio ujanja na mbinu za polisi kutaka kujifanya hawajui huku wanamtafuta muuaji kinamna basi kuna jambo, maana dunia hii inatawaliwa na pesa,pesa inaweza ikabadili mazingira...’akasema mjomba.

‘Hata iweje,haki ni haki tu, sheria itachukua mkondo wake,sio wote weney ibilisi ya pesa...’akasema mjomba mgeni.

‘Ndilo tunaloomba, lakini sasa nini tufanye maana hali ndiyo hiyo, mimi nina uhakika leo nitapata fununu wapi alipo mjomba wangu, na najua atakuwa nab into yako,lakini ujue wale ni vijana, damu zinachemka, sio vyema tukakaa hivi hivi, na mwishowa siku wakaharibu mila na desturi, si unajua tena,...'akasema mjomba na kuwaangalia wenzake.

'Kwahiyo kwa vile tunauhakika kuwa wanapendana na wapo tayari kuoana,na swala tu lamuda, sisi tuanze taratibu zote zinazohitajika....na ikibidi hukoo walipo, tunaweza kumtumamtu wakufunga ndoa ...au aunsemaje....?’ akasema mjomba.

‘Hilo lamuhimu, nd ndilo tulilojadili huko na baba yake amekubali bila pingamzii, kwani lifikia kusema yupo tayari aolewe hata bila ya mahari...’akasema mjomba mgeni.

‘Hiyo ni kawaida kwawazazi, ikizingati na hali aliyo nayo sasa...maana mke hamuoni,binti naye haonekani, lazima takuwa kachanganyikiwa, sasa tuanze taratibu zetu...’akasema mjomba na mambo ya kimila na desturi yakaanza, na mahari ikakubalika ikabakia jinsi ya kujua wapi walipo hawo walengwa na wakati wanatawanyika mara gari la polisi likaingia....

‘Wote mpo chini ya ulinzi mnahitajika kituo cha polisi...

‘Kwasababu gani....?’ akauliza mjomba.

NB Ngoja nikumbuke kidogo, ilikuwa kwasababu gani...tuone sehemu ijayo.

WAZO LA LEO: Katika dunia hii jaribu sana kutenda wema, usiseme mbona yeye hajanifanyia hivyo...na usifanye ukisubiri shukurani, kumbuka usemi usemao `tenda wema uende zako usingoje shukurani...kwani wema hauozi na mwisho wa wema ni faraja'

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Precious said...

Usione kimya M3 tuko pamoja kwenye mkasa mpya kama kawaida yako unaibua mambo mazuri zaidi na zaidi. Keep it up & God bless you.

emuthree said...

Tupo pamoja Precious, ahsante sana. Jazakallah haira