Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, March 30, 2012

Hujafa hujaumbika-14




 Ukiwa huna kazi...na ulikuwa umezoea kazi, asubuhi upo ofisini na mwisho wa mwezi unakinga, ni taabu kweli kweli. Ikabidi nijifiche fiche, na wakati mwingine naamua kutembea sana, kwenye maofis hadi jioni, narudi wafanyaakzi wakitoka...lakini nikaanza kuishiwa nauli hakuna, ikabidi kiguu na njia, viatu viakisha soli....ikabidi ninunue ndala....

Mwanzoni tulikubaliana vyema na kimwana, kuwa tuwe tunatoka asubuhi, kila mtu akahangaike kivywake, na jioni tunakutana tuoena tumeppata nini, hakuna kufuatana, ilimradi tunakutane jioni kila mtu anaonyesha kile alichojaliwa nacho, mimi sina kazi, sina biashara nitapata nini....ikawa kila siku anayeleta kitu nyumbani ni mke wangu kimwana....anapatia wapi sijui, ilimradi tunakula...

‘Sasa mimi ni mume, maana nakulisha wewe, huji na lolote, hata angalau tunda, kila ukija unanuka jasho tu...’akaanza kunisamanga.

‘Sasa ndio unanisamanga, nimejitahidi kila ofisi ninayoijua sijapata kazi, na biashara mitaani haitoki, kila mtu ana biashara hata wale wenye kazi wameanzisha biashara, sasa sisi tusio nakazi tutafanya nini...yaani hapa nimechananganyikiwa mke wangu, nahisi dunia imenilemea...sijui ni balaa gani...’nikasema huku nikiwaza mengi.

‘Sikiliza, huwezi kupata kazi kwa mtaji huo, ili upate kazi inabidi ufanye kazi, mimi kama ningelitaka kuajiriwa ningelishaajiriwa muda mrefu tu, lakini sitaki kazi za ofisini tena, siku nilipoachishwa kazi na yule meneja aliyenitaka.... nikamtolea nje, nikasema basi , kama kazi ni lazima ujitoe mwili wako, bora nikaifanyie huko mitaani, huko nje,...sio huku ofisini... nitapata maslahi zaidi lakinii sio kwa yule meneja,..mtu mwenyewe mzee halafu, sura mbaya...’akasema huku anacheka.

‘Eti sura mbaya, hivi hawo wanaojiuza huko mitaani wanaangalia sura....si maslahi tu,.....lakini hata hivyo ukiongea hivyo uanataka kusemaje,....., ujue mimi ni mwanaume, kama lengo lako ndio hilo,....sijakuelewa hapo, maana hata kama pia ni pesa, sina pesa kama ni kuhonga au sijui kujiweka vipi....sasa nifanyeje..?’ nikamuuliza.

‘Dunia hii usipokuwa mjanja utalala na njaa, cha muhumi ...nikupe maarafa...eehe,... nyumba, ukiwa na nyumba, halafu una hati miliki, .... ukatumia akili yako vyema, hulali njaa, hata siku moja...tatizo lako hutakii kutumi akili yako vyema, nikuambie kitu...hii hapa ni nyumba yako, una hati una kila kitu...kwanini huiweki bondiukapata mkopo benki...?’ akaniuliza.

‘Nyumba....ungelijua...’ nikatulia na kuwaza, kwani alikuwa hajajua kuwa nyumba hiyo ipo tayari kupigwa mnada, nilikuwa nimemfica kabisa, nikasema;

‘Lakini hata hivyo mkopo una masharti yake, unaweza ukauchukua ukaishia kunywewa tu sasa mimi sitaki kurejea huko, nakunywa, lakini sitaki niwe mlevi tena....’nikasem ahuku nikiwa sina raha, maana aliponigusia nyumba, nikakumbuka kuwa wale wapiga mnada wa nyumba za wadaiwa sugu wamenipa miezi mitatu tu, niwe nimelipa deni la watu....miezi mitatu tu...nikawaza....na hiyo inaishia.

‘Sasa unasemaje.....?’ akaniuliza kimwana.

‘Miezi mitatu ..nimepewa...’ nikajikuta nikisema.

‘Miezi mitatu tu, yaani uchukue mkopo uurudishe kwa miezi mitatu tu, sio mbaya nenda kachukue mimi nitakuonyesha jinsi gani ya kuuzungusha, nakuambia ukweli, ukiwa na akili,utakuwa tajiri...’akasema huku anaiagalia nyumba kwenye paa, akizungusha kichwa hku na kule .

‘Hivi nikuulize na wewe kule ulipokuwa umepanga niliona vifaa vingi vya thamani, umemuachia nani hivyo vifaa..?’ nikamuuliza, na swali hiloo likamshitua kidogo  na mara ghafla akainuka na kuchukua mkoba wake.

‘Swali zuri sana lakinii sasa nina miadi na bosi mmoja...., huyo najua atatupa hela ya kutusukuma hadi mwisho wa mwezi na akizubaa, ataingia choo cha kike, wewe tulia, ngoja mwanaume nikhangaike, unajua mimi watu wanafikiri ni Malaya, hapana mimi ni mjanja,... mwili huu unakuwa kivutio tu, lakini mwisho wa siku inakuwa akili kichwani mwangu, ni kama kutamani ndizi, ...lakini kuila huili kamwe, wanakula wengine   ndivyo ninavyowafanyia hawa wakubwa...’akasema.

‘Eti nini mbona sikuelewi, wewe umeniambia kuwa una dili zako za kibiashara, hukuwahi kuniambia kuwa unauza mwili...au sikukusikia vyema...huko kwa huyo bosi unakwenda kufanya nini..?’ nikamuuliza kwa hamaki.

‘Nimeshakuambia, akili zitumie vyema, unafikiri hata hawo wanaofanya kazi maofisini pesa zinawatosha, haziwatoshi, lakini utashangaa wanaojenga majumba mazuri  kwa sasa wengi kwasasa ni wanawake....na wengine hawana waume, ni nini wanatumia, nia akili...mwili huu ni kitega uchumi tu...lakini hauuzwi...kama mtu akitaka kuona ndani atakuwa an ujasiri wa hali ya juu sana kama wewe...hakuna mwingine...' akanisogelea na kunikumbatia akilala kifuani kwangu.

'Sasa tutaliongea hilo baadaye, wewe nenda kauchngamkie huo mkopo, chukua hati ya nyumba, kaongee na mameneja kweney benki..mkopo upo nje nje....’akasema huku akijirmba mdomoni.

Maneno ya mke huyu yalianza kunitia wasiwasi, inawezekana kweli ni changudoa,na mimi ananitumia tu, lazimanimchunguze, haiwezekani, kwanza alishaniambia nikimuoa atajituliza na kuwa mke mwema, sasa kila siku anaaga kuondoka, ...lakini hata hivyo asipoondoka, tutakula nini....nikajiuliza bila jibu...wazo likanijia kama mke wangu huyo kule alikuwa na vitu vya thamani na sisi hatuna kazi, kwanini tusiviuze baadhi ili tupate pesa.

Kwangu nilishauza karibu kila kitu na gari ambalo tunalifanya kama taksi bubu, nimeliweka rahani, ina maana ikipita muda wa deni gari, sio langu tena, nyumba sio yangu tena, nitabakiwa na nini...Nilipofika hapo nakatoka na kuingia mitaani. Mkaa bure sio sawa na mtemeba bure, tembea tu hata huna kazi huenda ukaokota,...

*********

Nikafika mitaa ambayo kimwana alikuwa akiishi, nilioana nifike hapo kutizama vifaa vyake, na kujua nani anaishii hapo kwasasa, maana vile vifaa mle ndani vilikuwa vy athamani, sizani kwamba aliviuza vyote kabla ya kuja kwangu, ...

Nilipofika pale, nikakumbuka jinsi nilivyoibiwa gari langu , nikajikagua mfukono, maana hapa pakumbusha mengi, halafu nikagonga mlango...kwa mbali nikasiki kama mtu anaongea, au wanaongea an sauti ya runinga,...nikajua kuna mtu anaisha hapo kwasasa, isije ikawa ni mshikaji wa mke wangu wa siri, leo nitapambana naye...

‘Halloh, mpenzi, karibu, unahitaji huduma....au sio,halafu umependeza kweli, na hapa ukitoka, jasho lote litakuwa limekauka, kuna maji safi ya kuoga, ni mpango wako tu...’sauti nyororo ya kimwana ilifanya masikio yangu yaingiwe kiwi, na jinsi alivyovaa, ni heri tu angeacha kuvaa, gauni ipo karibu kuonyesha chupi...

‘Huduma....namulizia ...mmmh, hapa alikuwa akiishi kimwana,au sio..?’ nikajikuta nikigwaya.

‘Swali kabla ya jibu,nimekuuliza kwanza unahitaji huduma, maana muda nii mali, anaweza akaja mtu mwingine,akazania unahitaji huduma, akaondoka, ukanikosesha bahati...kama unahitaji huduma,karibu ndani, lakini, kila kitu ...’akaonyeshea vidole kwa ishara , ambayo inamaanisha pesa....

Nikabakia bado nimeduwaa, nikaangali mlango kwa juu kuwa huenda kumebadilishwa na kuwa sehemu ya huduma fulani, lakini mimi sikuwahi kupitahapo karibuni, nilipoona hakuna maandishi yoyote nikamtizama yule kimwana, akajirembua....

‘Mhh, wanionaje, .....kwani una ngapi wewe....maana nisje nikaitupa bahati....wewe sema una ngapi, ulicho nacho kinaweza kikakusaidia hata chapu chapu....ongea wewe mwanaume usiwe kama demu bwana, kasema na kunsihika sehemu za siri...nikaruka kwa nyuma..

‘Vipi wewe...unataka kunifanya nini, nimekuja hapa nikiwa na maana ya kuangalia vifaa vya mke wangu, Kimwana, alikuwa akiishi hapa kabla, wewe unaleta mzaha,...unafikiri wanaume wote ni wakutaniwa,mimi nina mke wa maana, sio kama ....kwanza wewe ni nani kwake...’ nikauliza kwa hasira.

‘Mimi ni Kimwana pia,...ukipenda niite Kisura....nani mwingine kimwana zaidi yangu...sikio wewe lofa, kama huna kitu ishia na usije tena hapa kunipotezea muda wangu...mijanaume mingine bwana utafikiri waume kweli, kumbe milofa...haya ishiia usije ukanifukizia kibosile wangu yupo njiani anakuja...hata hivyo umeshanitilia nuksi za mapema,watu kama nyie mkifika hapa wa kwanza mnaharibu siku nzima....aah...’akaubamiza mlango kwa nguvu na mimi nikageuka na kurudi barabarani.

‘Vipi ulikuwa unapata huduma nini..?’ mara nikasikia jamaa akiniuliza nyuma yangu, name bila kugeuka kumwangalia nikasema;

‘Huduma....kuna huduma hapo, ni kuchanganyana tu, kwanza huduma gani hiyo unayozungumzia, maana hata yule binti pale kaniuliza nataka huduma...kwani pale kuna huduma gani?’ nikageuka na kuangaliana na huyo jamaa, alikuwa kabeba nguo za mkononi, ni mmachinga.

‘Wewe unauliza kuwa kuna mate mdomoni...au wewe wakuja nini, ..maana watu kamanyie ndio mnalizwagwa....pale kuna huduma maalumu, huwa wanakuja machangu wenye nazo, wanakodi kwa masaa, wiki na wengine hata kwa mwezi,....kwa ajili ya kutoa huduma....hahaha, ulikuwa hujui wakuja eehe..’akaziweka nguo zake vyema na kuniangalia kwa hamu.

‘Mimi sio wakuja bwana....wewe unafikiri utajua huduma zote hapa Dar, huna kazi nini, iwe kazi ya kujua kila kitu kinachofanyika hapa Dar....’ nikajitetea.

‘Nimeshakujua, hujuii huduma hiyo ni kitu gani, ...ukija mwanaume na vihela vyako, unahudumiwa pale, hakuna longo longo, hakuna eeh, nakupenda sana, hapana, hapeendwi mtu, inapendwa pochi yako...ukizubaa, unachukuliwa jumla jumla, na mwisho wa siku tunakukuta mitaani ukiokota makopo...kuna laana pale....’akasema huyo jamaa akaelekeza macho yake kwenye ile nyumba.

‘Mhh, siamini...kipindi fulani alikuwepo msichana mmoja anaitwa Kimwana, ....sasa kaolewa, alisema kapanga hapo, na...’nikaanza kuongea.

‘Hahaha...sasa kaolewa, maajabu,huyo kampata lofa, ...kaolewa, wanaolewaga hawo ....mmh, visura...sijui labda...maanake huwezi jua ya mungu mengi.....’akaguna na kuziweka nguo zake vyema, na akawa kama anawaza huku akingalia pale kwenye jingo, akasema;

‘Pale majina yao ndio hayo visura,vimwana, mrembo..., ukifika pale wote wanajiita majina hayo, ila leo yupo huyu,kesho yule.....lakini hayo yote ni majina ya bandia,....kweli ni warembo wamejichubua utafikiri wazungu....na wapo wana urembo wa asili, wazuri huwezi amini, ...lakini kama wesamavyo wehenga, sio vyote ving’aavyo ni dhahabu, chunga sana, utalizwa....’akasema jamaa yangu akizichambua nguo zake kama vile ananionyesha ipi bora nichague.

‘Unajua wengi ni mabinti waliotoka hukoooo,makwao, labda wameshindikana, labda,....hatujui, tusema hatujui , ....wakifika hapa bongo....wanachofanyalabda kwa kuelekezwa, au kwa kunaswa na maisha au kwa kupitia mawakala, wanaingia kwenye shule ya huyu mwenye haya majumba, wanafundwa kisawasawa,...unajua kufundwa wewe, hkokwenu mnaitaje, unyago, au...?’ akaniuliza akiniangalia kwa makini.

‘Sijui nini unachoongea....’nikasema huku nikiiangalia ile nyumba, na huku nikimuwaza kimwana wangu, maana siamini,...ina maana hata yule binti mrembo anafanya ....hapana kwanini...siamini...

‘Siamini....’nikajikuta nikisema.

‘Huamini nini hapo.....wale wapo kazini, ...sasa sijui tafsiri sahihi ya kazi ni ipi, maana unaonekana msomi kidogo...hebu niambia wale wanasema wapo kazini, maana mwisho wa siku wanapata mshiko wao, kwa vipi, ....hebu kwanza nikupe jinsi inavyokuwa kwa hawo vimwana, ...kamahuyo kimwana wako, .....’akaweka nguo zake vizuri na kuiangalia machoni.

‘Wakikutana na huyo mwanamama, wenyewe wanamuita Docta....sio Docta wa hivi hivi, ....kaisoema hiyo fani na ana mashahadanamadigrii,sijui na maprofesa....anamjua bindamu, anaijua hisia ya binadamu, anajua tabi na maumbile ya bindamu, kivitendo, kihisia, ...’akasema huku akifikiria neno jingine la kuongezea hapo, na mimi nikaingiwa na hamasa ya kutaka kujua..

‘Kwahiyo ni mwalimu,...akiwapata hawo mabinti, kwanza sifa ya kwanza ili uwe mwanafunzi, ...uwe mrembo, na kamahujakamilika,unatengenezwa....huwezi kumjua akishatengenezwa, hutaamini,...halafu anaanza kufundwa....nyie kule mnaita unyago, lakini tofauti yake, ni kuwa unyagoo huo sio wa amlengo ya kuishi na mume na mke.....unanielewa hapo...’akaniangalia kwa makini, lakini mimi sikumjibu nilikaa kimiya.

‘Anafundishwa  jisni ya gani ya kumpagawisha mwanaume, ...na siri za uzaifu wa wanaume...unafikiri wanaume tuna kitu sisi,....kitu kidogo, eeh, ooh, wewe ni kila kitu, chukua zote, unatoa mihela yako yote...ni kushindwa tu kwa wanawake kutujulia, wangelikuwa wanaijua hiyo siri, mwanamke angekuwa anatamba katika hii dunia....’akaanza kunifunua ubongo huyu jamaa anayeonekana kuijua sana sehemu hiyo.

‘Ina maana....kumbe, wana.....lakini inakuwaje mpaka mwanaume asijijue, ..kwaninii sisi ni wajinga, hapana, lazima kuna dawa wanatumia kumpagawisha mwanaume.....?’ nikauliza.

‘Hakuna dawa kabisa...ni hayo manjonjo tu...ndio maana nakuambia kuwa wanawake wetu wangetujulia, kusingekuwa na hiyo wanayoiita mfumo dume....wana silaha kubwa mungu kawajalia,lakini hawataki kujifunza, wakishaolewa basi, wanajua wamefika,...kazi yao kupika, kufagia..umbea..huku wenzao wanawasoma...na wanaweza wakaja kwako kama rafiki,....nikupe hiyo mapema..’akasemana kuniangalia kwa makini.

‘Akikutana na mkeo,  anamdadisi, na udadisi huo unalenga maswala nyeti....kuanzia ofisini, hadi chumbani...kuna mambo wameshafundishwa, wayajue, wakishayajua,kazi ni ndogo kwao, wanakukokota kama mbwa anavyojipeleka kwa chatu,.....mwisho wa siku unasema dawa, dawa...hakuna daa hapo, ni akili....usicheze na binadamu, nakuambia, binadamu nikiumbe wa ajabu kabisa....’akajionyeshea kwa kidole kichwani mwake.

‘Wenzenu kila kukicha wapo kwenye maabara, sio lazima maabara ya madawa, ya kutafiti ugonjwa, lakini pia kuna maabara ya kumtafiti binadamu, na hidia , hulka na nyendo zake....wanakuchambua juu chini, ...akikuangalia hivi tu, keshakujua udhaifu wako...mwishowe unasema ooh, mazingaumbwe, oooh, wachawi..ooh, dawa, ooh, limbwata..hakuna, ni akili kidogo tu...’akasema na kuchuchumaa .

‘Sasa huyo mama anapaat faida gani....sio kwamba anachumamazambi tu...’nikasema

‘Ndugu yangu wee, matajiri, na utajiri, unanuka zambi...pesa ndio ibilisi wetu mkubwa, pesa imewafanya wengi wakasaliti, na hata vitabu vikubwa vimeandika, ila sitaki kwenda huko....ukisema nikifanya hiki nitapaat zambi, ni wewe na imani yako....mwenzako hamjui wala kuamini hayo....dini yake ya mali, ...mungu wake ni pesa...eti zambi..shauri lako, kaa na imaniyako hivyo hivyo...’akainuka kama anataka kuondoka, lakini hakuondoka.

‘Kuhusu huyo mama anapata faida gani, ....ni mfanyabishara, ala leseni na analipa kodi, kwa kukodisha majengo yake....mengina nini kinafanyika, yeye hajui....akili kichwani mwako, ...kitu anachofanya ili kufanikiwa zaidi ni hivyo kuwa anawafundisha hawo mabinti,kwa nakubaliano ya siri....mwisho wa siku atakata hela yake sijui, au ndio anajua kuwa ataipata kwenye kodi.....’akatulia kama anawaza.

‘Sasa huyo mama mwenye mijumba, kasoma, na kumjulia mwanaume, yeye sasa anatumia huo ujuzi kujiingizia hela, yeye kakaa kwenye kiti chake tu , na hata watu wa kodi wakija, anasema anafnya biashara ya nyumba, kukodi nyumba, ...unaweza ukaita nyumba za wageni, lakini kinaman iliyojificha......kodi zinaingia.....wanalipa hela nyingi sana kukodisha hapo....mama anatajirika,docta anaheshima zake...kwenye ngazi za juu, ana sifa ya mtetezi wa akina nani.....utajaza mwenyewe....’akaniambia huyo jamaaa.

‘Wewe sasa umejuaje hayo...?’ nikamuuliza.

‘Mimi nimejuaje hayo,... kwasababu mimi ni mtoto wa mjini, nimesoma ahdi chuo kikuu, lakini sio cha kukaa darasani,..akili iliyopo hapa ingelikuwa Ulaya au Marekani ningeliitwa docta....naujua kuutumia mdomo, najua mengi, nasikia mengi na nawajua watu...wenzako wanaonijua wananitumia,naitwa mtaalamu wa kujua mengi..mwanzoni nilikuwa wakala wa huyo mama...baadaye nikaona ni ushetani....nikajitoa....’akaniangalia kwa makini halafu akacheka.

‘Unajua nimekungali na kukupima kwa makini..nimegundua kitu, na wewe umelizwa, nina uhakika huo, semausaidiwe...maana unavyodadisi naona kabisa umeshaingia mkenge, na ukinaswa ni kama ulimbo wa kumtegea ndege.. ukinaswa hunasuki, umenaswa....?’akaniuliza akiniangalia usoni kwa mshaka.

‘Hpana, ila huyo dada niliyekutajia, namfahamu sana,....huyo ninayemzungumzia, nilimfahamu kwa jina hilo la kimwana nilifika hapo kwake na akaniambia amepanga hapo siku nyingi,...nilimshangaa maana sizani kama alikuwa na uwezo wakununua vifaa vya tahamani kama vile na kupanga nyumba kubwa ya thamani kama hiyo, tukaongea tukaachana, tulipnaga tukutane humo, sasa hayupo, namkuta msichana mwingine, ana jina hilo hilo...’nikasema

‘Hivyo vifaa ni vya mwenye hizo nyumba sio moja tu,...anazo nyumba nyingi seehmu tofauti....hivyo vifaa kavinunua kwa pesa yake, na anavibadili kila siku , kwahiyo ukifika hapo utakuta mabadiliko ya mara kwa  mara...kutokana na watu wake, na ni moja ya mipango ya kuwavutia wateja,na kuwahadaa mijanaume isiyo na wake, na hata kama ina wake, haitosheki  na hata kama inatosheka, lakini ni limbukeni, wakilegezewa basi, wamelainika....mijitu haina akili ya kufikiri....mimi kama ningelikuwa na uwezo wangu, ningeichapa midume ya namna hiyo viboko....’akasema huyo jamaa.

‘Lakini siumesema ni utaalamu wa shule kidogo uliotumika, ina maana hawo vimwana waliwekwa mahala wakapatiwa shule na nini siri ya kumpagawisha kidume, ina maana wamesomeshwa, na wakamjua mwanaume, na mwanaume hajijui, ...na matokeo yake alipoguswa huko...akajiona kama kafika sehemu ambayo hajawahi kufika,na hakuwahi kufikishwa na mke wake au sio...mimi sioni kuwa ni ujinga....’nikasema kama vila najitetea.

‘Ujinga, huo ni ujinga ...kwanini hukukaa na mkeo mkaongea,na kumwambia  mwenzako vipi unataka iwe,....ni kama chakula, au wali , unaweza ukautengeneza ukaonekana wa ajabu, kutoka hali fulani inayojulikana na kuwa tofauti,  mfano wali hadi pilau, hadi biriani, lakini ni wali ule ule...mkafundishana, ....mtaona ni kitu cha ajabu sana...lakini hamtaki kukaa na kuongea, matokeao yake ndiyo hayo...watu wajanja wamegundua, sasa wanachuma, watu wanaumizwa...sijui mpaka lini, watu wanalia na ndoa zao, hawaelewi sababu ni nini ..’akatikisa kichwa.

‘Nikuambie ukweli, mapaka wakijua tatizo ni nini huyo mama atakuwa tajiri wa kupindukia, na mwisho nasiki anafungua hospitali, au sehemu ya ushauri nasaha wa maisha ya ndoa....sio bure, ni pesa..hayo walikuwa wakifanya mabibibi mashangazi, ....unyagoni, ..siju wapi, lakini tumeyazarau, ....tunawazarau hata hawo mabibi..mashangazi...matokeo ndiyo hayo....’akasema na kukuna kichwa.

‘Tunawazarau kwa vipi...?’.nikauliza

‘Utaoaje, hujui ndoa ni nini,....lini mtu akaendesha gari bila kujifunza...lini mtu akawa docta bila kusoma shule, kwanini hatuisomi hiyo ndoa ni nini....nini cha muhimu na nini kinatakiwa nimfanyie mwenzangu,ili....hapa ujue kuna mambo mengi ya ndoa, lakini kuna jambo kubwa limesahaulika, ambalo ndilo kiini cha ndoa....hata wenyewe wanaita...mmh, la ndoa....’ akaguna na kunionyeshea kwa kichwa kule kwenye hiyo nyumba na tukawa kimia kuangalia nini kianendelea huko.

`Unaona mambo hayo, sio mchezo wewe sikia tu...’akasema huyo jamaa akiangalia kule mlangoni wakati gari la kifahari likisimama mbele ya mlago na jamaa mmoja, aliyevalia suti yake ya kifahari, akatoka harakaharaka na kuingia ndani ya ile nyumba,....mlango ulishafunguliwa mapema, ilionekana alishawasilina na huyo kimwana auache wazi maana gari lilifika, mlango wa gari ukafunguka haraka, na mtu akatoka na kuingia ndani ya nyumba haraka, na lile gari likaondoka haraka, lakini tulimuona alikuwa mtu mzima tu, tena anaonekana ni mheshimiwa...

‘Unaona wanaoingia hapo ni watu wazima,watu wazito, watu wenye wake zao.....sasa jiulize wake zao wanayajua hayo, hawajui, na kwanini inatokea hivyo.....akili ni mali....’akasema na kushika kichwa kwa kidole.

 ‘Ndio maana nika kuambia midume humu hakuna, ....mimi ni mwanaume, lakini nilikuja kugundua hilo...wanawake wanaweza wakatuchezea sana wakitaka..na sisi midume na akili zetu mbovu, tunatamba mitaani maofisni, wapi kuwa mimi sibabaishwi....nyumbani ukifika hakuna kitu....siri ya mtungu aijua kata, ndio maana nasema ni heri tuchapwe viboko....’akasema.

‘Kweli tunastahi kuchapwa viboko....na hata hivyo haina haja ya kuchapwa viboko kama fimbo, dunia yenyewe itatuchapa viboko...’nikasema huku nikiwa nimenywea na kujiona kweli sina akili na kwelii nastahili kuchapwa viboko...

Baadaye jamaa aakondoka akitafuta wateja wa nguo zake, na mimi taratibu nikaondoka pale nikiwa nimenywea kama mtu aliyemwagiwa maji, nilitemeba nikiwa kama sio mimi, ...na baadaye nilijikuta nimeshafika nyumbani hata bila kujijua ,....nilipoikaribia nyumba yangu nikaiangalia vyema huku moyo ukiniuma, ina maana kesho tu wajamaa wa kupiga mnada wanaingia....nyumba hiyo inakwenda, na gari hio linakwenda, sasa nifanyeje, ..akili ikanijia....

Lazima nyumba hii niitafutie mteja chapu chapu, mjini hapa.....na hata gari nitaliuza kinamna...’ nikasemana kushika kitasa cha mlango...nikakuta mlango unafunguka...upo wazi, nikajua mke wangu keshafika, nikajitahidi na hata kupiga mlunzi kama vile baba mwenye nyumba umefika, na unahitaji mke aje akupokee...

Kwanza nilisikia sauti za ajabu ajabu chumbani....na baadaye vicheko vya ....nikashituka, kwanza kwa hasira nikaangalia huku na kule, nikakipata kisu,....mwili uakanichemka,zilehasira zilizokuwa zimejificha zikafumuka, .....nikatamani kuua, .... kwa haraka nikakimbilia mlango wa chumbani...nikausukuma kwa kishindo....

 Je nini kilitokea....tuwepo kwenye sehemu ijayo Ijumaa njema. Nawashukuru sana waliochangia, nilitaraji kisa hiki wangelichangia wengi, hasa wanandoa,....lakini sio mbaya :Tupo pamoja

WAZO LA LEO: Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, huwezi kumdhibiti, huwezi jua nini anakiwaza, na kila siku kuna matendo ya ajabu ajabu yanayotokea duniani na anayeyafanya ni biandamu, nafikiri hata shetani atakuja kuturuka na kusema ‘hayo mimi sikuwahi kumfundisha huyu binadamu,hata mimi nashangaa nijawahi kuwaza hivyo....kwani wahenga walisema `ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Frauni..


Ni mimi: emu-three

8 comments :

samira said...

da m3 makubwa sana yamemkuta huyu jamaa mtu unaweza kupata wazimu
mkasa unavutia sana tatizo binadamu wapo tofauti wengine wakingangania kitu huna la kuwambia mpaka yawakute ndo wanaambilika saa nyengine ndoa ndoana
any away tupo pamoja

Anonymous said...

Duuh, hii kali, lakini sio wanaume wote wanaoweza kunaswa...ni kila mtu na tabia yake.Tutakupigia kura muda ukifika

elisa said...

M3 kama ulivyosema ,binadamu ana mambo makubwa na moyo wake ni kama kichaka ,hujui awazalo wala anapanga nini juu yako, kwenye ndoa tumetokewa na mengi japo kila mtu ana lake. Mmh wengine ni imani tu ! Kwamba Mungu ni mkuu,anatulinda na kutuongoza, kuna wakati mlango mmoja unafungwa ,tunapoteza muda mwingi na kujuta kwa ajili ya mlango mmoja uliofungwa na kusahau kuangalia mbele kwenye milango saba iliyo wazi.
Wikiendi njema wapendwa.

Anonymous said...

Tuchangie nini kaka yangu, maneno yametuishia kwani umemaliza kila kitu. Yaani vijana wengi hasa wa kiume wanaingia bila ya ndoa bila kufundwa kuelimishwa ndoa ni nini na niyepi yakufanywa ndani ya ndoa na ni yepi hayapaswi kufanywa ndani ya ndoa, matokeo ndio kama hayo.

Na hata wanawake pia wanaingia ndani ya ndoa kwa kufuata mkumbo tu, fulani kaolewa ngoja na mie niolewe. Wako wanaofundwa lakini hayo mafunzo yanaingia sikio la kulia na kutokea la kushoto. Mimi nikirudi Bongo nitafungua kliniki ya ushauri wa masuala ya ndoa/mahusiano, kwani nimefanya utafiti kwa muda mrefu kwenye suala hili na sasa ninaelekea ukingoni. Hii bwana weka kwenye kitabu ili kisomwe na wengi walau inaweza kuwafungua watu macho.

emuthree said...

Samira nikweli asiyesikia la mkuu huvunjika guu.

Kweli kuna blog iitwayo Tanzania Blog awards humo kuna kupigia kura blog kutokana na vipengeel vilivyowekwa, nawaomba muipigi kura blog yenu hii, ni moja ya kuitangaza.

Na kweli Elisa, ndoa ndoana, yaliyopo kwenye ndoa, ayajuaye ni mwana ndoa mwenyewe.

Anon. 31 March 2012 9:22 AM, Umeshachangia, uliyonena ni mchango mkubwa sana tunakusubiri sana uje utupe utafiti wako ili uziokoe ndoa za watu.

Na wengine wote TUPO PAMOJA DAIMA, nawashukuru sana kwa maoni yenu na kuwa pamoja nami, ....mbarikiwe sana

Anonymous said...

powerful material Cl. Salt provide is enthusiastic, not hot, release with your entropy.

If you privation to score a purchase with them.
Registering ordain encourage you strike fatty tissue.

The adrenal cortical steroid secretion is produced through emphasise.
This internal secretion makes your limit fresh freshby mailing on cultural media.
Canada Goose Jacket Canada Canada Goose Outlet
a news story, don't let a losing positions so you can intercommunicate the seller may say,
valuableness occupied adornment. No content what the seller straight off.
score certain to cater. Do national leader search on your act-about?
When you go out of your determine judge, is
practically easier to get discounts on foreordained products.


Also visit my web-site :: Canada Goose Coats

Anonymous said...

I really like your blog.. very nice colors & theme. Did you create this website yourself or did you hire someone to do it for you?
Plz reply as I'm looking to construct my own blog and would like to find out where u got this from.
kudos

My homepage ... The Price Is Right Manuela's Blooper

Anonymous said...

I’m not that much of a internet reader to be honest but your
blogs really nice, keep it up! I'll go ahead and bookmark your website to come back later on. Many thanks