Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, March 26, 2012

Hujafa hujaumbika-10



Siku zikawa zinaenda nami nikawa nasota rumande, na kuna siku moja, mmoja wa maaskari aliniambia kuwa wiki ijayo kama kesi yangu itakuwa bado, inabidi nihamishiwe gereza kuu, maana hairuhusiwi mahabusu kukaa hapo kwa siku nyingi, hiyo ni sehemu ya muda tu, walinisaidia tu wakijua kesi yangu itaisha mapema, lakini inavyoonekana sio ya leo au kesho.

Nilivyosikia hivyo, jasho lilinitoka maana huko gereza kuu, kile aliyepitia huko huja na hadithi yake, na wengi hawakatishi mwaka,kwanza anakumbwa na kifua kikuu, ukurutu usioisha, na wengine huishia kuchanganyikiwa kabisa....nilipowaza hayo, nikajikuta nikitetemeka mwili mzima, ina maana maisha yangu yamekwisha...haiwezakani....na baadaye mjomba akafika, ikabidi nimuulizie mjomba kuhus hilo;

‘Sasa kwanini hawanipi hiyo dhamana, wakati kila kinachohitajika kimeshawasilishwa kwao, au ndio wanataka kunikomoa kwa vile wanajua hawana kesi ya msingi juu yangu...’nikalalamika kwa mjomba,ambaye hakuonekan na raha, lakini ibidi kwa hali ilivyo anipe moyo tu.

‘Utatoka tu, ...hilo nakuhakikishia, wewe vuta subira...’akasema mjomba.

‘Mjomba hiyo lugha yenu inanitia wazimu, sasa toka leo sitaki kumuona mtu akinitembelea hapa, kama hana habari njema za mimi kuachiwa, mwambie huyo wakili sitaki kumuona kama hana habari njema kwangu, sitaki kuja kunipa matumaini wakati naona hakuna lolote linalofanyika....’nikamwambia mjomba.

‘Watu wanahangaika mjomba wangu, unafikiri tumekaa tu, kila siku ni kiguu na njia kwa hakimu na kila sehemu tunayohisi inaweza kutusaidia, lakini nahisi wenzetu wameshatuwahi kwa nguvu ya dunia....’akaema mjomba.

‘Nguvu ya dunia, nguvu gani hiyo wakati sina hatia.....’nikasema kwa hamaki.

‘Wanajua kuwa huna hatia, na hawajampata aliyefanya hicho kitendo, kwahiyo hasira zote zinashushiwa kwako, ...ndivyo ilivyo hata kwa mataifa makubwa, yakipigwa yanamkimbilia mnyonge wake hata kama hana hatia...’akasema mjomba na kabla sijamwambia kitu akasema.

‘Nguvu ya dunia mjomba wangu, ...ni pesa,kama ukiwa na pesa wewe dunia yote unaitawala tu...hata hivyo mitihani yake ni mikubwa, na pesa ikitumiwa vibaya madhara yake ni makubwa, ....mimi ninachokushauri usikate tamaa, maana hujui kwanini mungu anakuchelewesha usitoke haraka,....muda utafika utatoka tu....’akasema mjomba.

‘Mjomba ni rahisi sana kuongea hivyo, kwasababu hamjui ni adhabu gani ninayoipata humo ndani ya
hicho chumba,...ni kwasababu hamjui, na hamjakutana na mateso haya ndio maana mnarahisisha tu, nawaomba msije hapa kuniona labda mkiwa na habari njema,....na habari njema kwangu ni kutoka humu ndani yah ii jela ndogo,... basi....je mumeongea lolote kuhusu Binti Yatima...?’ nikamuuliza kupoteza muda.

‘Tumeongea mengi, lakini hakubali kuja kukaa kwenu, najua kwanini, binti yule krithi tabia ya mama yake, ana maaadili mema, hakubali kwenda kwa mwanaume mapakakuwe na uhalali,hata hivyo y
eye anasingizia kuwa baba yake yupo peke yake nani atampikia, tukamuuliza je ukiolewa utakuwa anarudi kumpikia baba yako, akasema ni hapo nikiolewa, kwasasa sijaolewa,lazima nitii na kuwajali wazazi wangu.

‘Kwahiyo ili aje kukaa kwetu ni mpaka ndoa ipite, je mumeshalipa mahari kama tulivyopanga?’ nikaluliza.

‘Kila kitu tayari, kilichobakia ni ndoa tu, na isingelikuwa hili tatizo sasa mngekuwa pamoja...lakini kama nilivyokuambia, kila jambo lina muda wake....’akasemamjomba.

‘Mimi mjomba nina ombi, na hili ni muhimu sana, mwambie wakili wangu, aombe kwa hawo waheshimiwa, kuwa nataka kufunga ndoa,....kutokana na muda , maana nikitoka hapa natakiwakzini, siku za likizo zinaanza kuisha, ..... sizani hilo kisheria linakatazwa, aje huyo binti na mfungisha ndoa na watu wao tupate saa moja tu, fufunge ndoa naye, ikiisha sawa mimi nitaendelea kusota humu rumande, na nasikia kuwa kesho au keshikutwa napelekwa gereza kuu...hapa ni mahabusu,.....’nikasema.

‘Hupelekwi huko, hilo tumehakikisha kuwa hupelekwi huko, kama ingekuwa kupelekwa ungeshapelekwa siku nyingi, ...’akasema mjomba akijiamini. Na kuhusu kufunga ndoa, ...ni wazo zuri, lakini ...mmh, sijui kama wazazi wako watalikubali, lakini hata hivyo,nitalifikisha kwa wazee, kama
wataafikiana nalo...’akasema mjomba huku akionekana kuwaza sana.

‘Hata mimi nilikuwa na wazo hilo, lakini sikupenda kulisema awali, .... , basi ni jambo jema, ili huyo binti aje akae ndani ya familia yetu, na itakuwa vyema kiusalama wake maana huyo mama yake wakambo mpaka sasa hajulikani wapi alipo,na kwanini kakimbia nyumbani kwake...’akasema mjomba.

‘Mimi nina mashaka naye, nahisi anahusika na hayo mauaji....kwasababu alivyonisimulia Binti Yatima, inawezakana kuna mpango ulisukwa...kati ya huyo mama na marehemu, kuhusu huo ubakaji, sijui kw amalngo gani, na inawzekana kwasababu haukufanikiwa, ndio wakahujumiana...

‘Yawezekana, lakinii mbio za sakafuni husihia ukingoni,....atashikwa tu...’akasema mjomba ambaye alionekana kuwa na mawazo mengi sana.

‘Mjomba,kama alivyosema binti Yatimani kweli, ....mama, anasema kwaza waliondoka baba mama na marehemu, haikupita muda marahemu na mama wakarudi,lakini mama akajifanya kasahau kitu, na kumuacha huyo merehemu akiwa kakaa ndani, ...’nikawa namsimulia mjomba, ingwaje nilishamsimulia hayo yote lakini nilitaka kumwambia tena, huenda tukagundua jambo ndani yake.
‘Sasa huku alisahahu nini, na kwanini alimuacha huyo marehemu ndani,....hayo ndio maswali yakujiuliza...’nikasema na kumwangalia mjomba machoni.

‘Nakusikiliza na najaribu kuwaza hata mimi...hata huko kurudi sokoni, au wapi, mbona hakufika huko, kwasababu tumeulizia huko sokoni...’akasema mjomba.

‘Sasa tuangalie hapo, ....maana binti Yatima anasema alipoingia kuweka vyombo , ndipo marehemu akafunga mlango na kumshika huyo binti , kwa nguvu na kumsukumia kwenye chumba cha watoto...na uone huo muda uliochukuliwa na huyo mama....je alirudi muda gani, ...au hakurudi kabisa, na alikuwa wapi muda huo, ...’nikasema huku nikiwa bado namwangali mjomba.

‘Sokoni hakufika, aliishia mahali, na hapo huenda ndipo walipoagana kukutana...sasa kwanini waliamua kumuua huyomarehemu,....ni kwasababu ya pesa, au ni kwasababu zoezi halikufanikiwa, kwahiyo malipo yakakataliwa kutolewa..?’ kauliza mjomba.

‘Kwa kauli ya bintii Yatima, anasema kuna muda alisikia sauti yake mama huyo, akisema `baado, ....unaweka kiwingu..’lakini kwa vile alikuw akatik hali ya kuhangaika kujiokoa hakuwa an uhakika moja kwa maoja kuwa nai sauti ya mama yake hasa au ilikuwa sauti ya mtu mwingine, lakini alijaribu kumuita mama yake huyo kuomba msaada, lakini hakuisikia hiyo sauti tena, ..hadi hapo nilipofika mimi....’nikasema.

‘Ina maana basi huyo mama na watu wengine, walikuwa wamemsubiri mahali...na huenda kwa vile hakufanikwia lengo lake, marehemu alikataa kuwalipa, ...na kwa muda huo alikuwa na pesa tayari,....wajamaa wakaona isiwe shida, wakaamua kum-maliza kabisa jamaa na kuchukua pesa, na wote wakatokomea mjini, au wapi sijui walikojificha.....’akasema mjomba.
‘Watakuwa mjini hao...unafikiri watu kama hawa watakwenda wapi.., na ulisema huyo mama alikuwa ana tabia ya kuwarubuni mabinti wa wenzao kwa huyo merehemu na huwa analipwa pesa nyingi kwa ka hiyo, ...hivi nikuulize ni kwa starehe au kuna imani nyingine hapo..?’ nikamuuliza mjomba.

‘Inavyosadikiwa ni kuwa huyo jamaa utajiri wake, ni wa mshetani,...hutaamini mambo haya sasa yanashika kasi, ...nimesikia kuwa ili afanikiwa ni lazima kila mara akutane na mabinti bikira. Awazalilishe...sijui hapo inakujaje...na nini kinatafutwa hapo, ....lakini ndivyo wanavyohadithia watu wanaomjua huyo jamaa...’akasema mjomba

‘Hizo ni imani zao, na tamaa zao huku wanasingizia hivyo,mjomba unaamini hayo..kuwa utajiri unakuja kwa kumpata binti bikira....?’ nikamuuliza.

‘Hayo ndio mambo ya washirikina, hapo wanacheza na ibilisi ...na ibilisi kazi yake ni kukutumbukiza kwenye maasi, ndio kazi yake kubwa duniani, kwahiyo atakushauri mambo ya kishetani, mambo ya maasi, uzidi kuzama huko huko, na kweli unaweza kufanikiwa kuupata utajiri kwa njia hiyo, ili tu uzidi kupumbuzika....’akasema mjomba.

‘Mjomba naomba mkliongelee hilo swala la ndoa, na mwambie wakili alifanyie kazi hilo , kama kashindwa kupigania dhamana yangu ,na hilo pia litamshinda,basi hafai, tafuteni wakili mwingine ...kufunga ndoa haichukui hata nusu saa....nawaombeni sana mlifanyie hilo kazi...sitakuwa na muda tena wa kumfuatilia huko kijijini....’

‘Muda umekwisha, .....’mara askari akafoka, na mjomba akaondoka, na mimi nikarudi kwenye mateso yangu,

**********

Binti Yatima, akiwa anafunga funga nguo zake tayari kuondoka, huku mawazo yakiwa yamemtinga kichwani, hasa baada ya kuongea na mtoto wa Msomali,na kumwambia anataka wafunge ndoa huko huko mahabusi,kitu ambacho alikiona sio cha kawaida ...

‘Mbona haiji, ..ndio kweli, nataka kuolewa, lakini sio kwa hivyo,.... hata hivyo wazazi wake watakubali mtoto wao afungie ndoa mahabusu...,hapana, ngoja nisiwatie katika mihangaiko isiyo na maana, dawa ni kuondoka hapa,....naenda huko kijijini, kama kweli wana nia ya kunioa watanifuata huko huko,...maana inavyoonekana wanachofanya kwa sasa ni kunionea huruma...’akakusanya nguo zake na kuzijaza kwenye bgi la nguo. Lakini akakuta begi hilo limeliwa na panya sehemu kubwa na nguo zinaweza kudondoka.

Kila alipojitahidi kuziba ziba akakuta halifai, kabisa, ndipo akakumbuka maagizo ya baba yake kuwa kuna begi mzuri la mama yake, anaweza kuliazima,....baba yake alimshauri hivyo kabla hajaondoka kwenda kwenye shughuli zake , akisema kuwa anakwenda kumtafutia nauli, maana hata hela ya kula ndani ilikuwa haipo, ....

‘Baba mimi sipendi kugusa kitu cha mama, siunamjua mama, akirudi akigundua hilo, atanitafuta popote nilipo....’binti akamwambia mama yake.

‘Atarudi hapa,labda niwe maiti...wewe angalia huko chumbani toa minguo yake na chukua hilo begi, nasema mimi kama baba yako....’akasema baba yake kwa hasira.

Waakati anwaza hayo, akajipa moyo na kusema, kweli baba kaniagiza, hivyo, kwanini niogope, lakini hata hivyo kwanini namuogopa sana huyu mama, jinsi ninanvyomuogoa huyu mama, hata nikitaja jina lake au nikisia mtu akilitaja jina lake mwili mzima unashikwa na hofu, kwanini kanifanyia hivi...namuona kama shetani...mungu nisaidie na nisamehe kwa mawazo haya, lakini naombea mungu apotelee huko huko, asirudi hapa tena kwa baba...

Akaingia chumba cha wazazi wake hao, akamalizia kufagia na alipoliona lile begi ambalo baba yake alimuagiza alichukue, akaingiwa na hamu ya kulichukue akweli, licha ya mawazo yake ya mwanzo ya kutokuchukua kitu chochote cha mama yake huyo, Akalisogelea lile bgi, na wakati analichunguza macho yake yakatuoa mvunguni mwa kitanda, akaona begi jingine, sawasawa na hilo, lakini lilionekana ni dogo kidogo, akainama mvunguni na kulivuta kwa nje,...

‘Hili begi ndio zuri, linanifaa mimi, nitamuomba baba kama inawezekana niliazime hili, baadaye nitalirudisha, maana mama akirudi, kutakuwa ka kazii hapa.........’akasema huku akilifungua, na baaadaye akaanzaa kuhamsha nguo kuziweka kwenye begi hilo kubwa, huku bado akiwa na mashaka.
Mara akaona nguo ya ndani...gagulo jekundu, limefungwa fungwa sana,.... akaingiwa na hamu ya kuifungua, maaan ilionekan nzito, na kilichofungwa hapo kitakuwa kitu kizito kidogo, mara akaona gazeti,....limezungushia kitu kwa ndani, na kilikuwa kiziti kidogo, akalifungua na mibulungutu ya pesa ikadondoka chini...


‘Mungu wangu, .....’akajikuta akishangaa, katika msiha yake hajawahi kuona pesa nyingi kiasi hicho, akagopa hata kuzishika tena,lakini kwa haraka akaziokota na kuzirudishia kama zilivyokuwa, lakini haikuwa kazi rahisi, akajikuta hata lile gazeti likichanika.....

‘Hivi baba analalamika kila siku kuwa hana pesa, na mihela yote hii imo humu ndani, ina maana kweli hajui ...au ni mama kazificha huku...na hata hivyo mama kazipatia wapi hela nyingi kiasi hiki...? ‘akasema na mara akasikia mlango ukigongwa, haraka akaziweka zile pesa kwenye lile bagi alilotaka kuondoka nalo, na kwa kuogopa akaliacha lile begi kubwa likiwa na nguo za mama yake pale chini na kutoka humo chumbani haraka,...huku akiwa kalishikilia lile begi dogo mkononi likiwa na hzio pesa.

******

‘Upo tayari....’ilikuwa sauti ya baba yake.

‘Nimechukua mfuko huu, naona ni mdogo unanifaa...’akasemabinti.

‘Sawa wewe chukua tu, mama yako ana mifuko mingi, na sijui nguo zote hizo anazivaa saa ngapi...umetoa nguo zake zote, kama inawezekana ningekumabia hata nguo zake zinazokufaa uzichukue, lakini hazitakutosha, labda ukazipunguze.

‘Sawa, naogopa asije akawa kaweka vitu vyeka hapo,...akivikosa anaweza kuniua...’akasema binti.

‘Ataweka nini huko...zaidi ya minguo yale iliyozidi ukubwa...mimi sitaki hata kuziona, kwanza zote nitazichomamoto, maana nikiziona zinanitia kichefuchefu...sikujua kuwa mwanamke huyu ni mbaya kiasi hicho,nimesimuliwa mambo mengi ya huyo mama mabaya mabaya...yaani mwanamke wa mtu unakuwa kuwadi, ....unauza mabinti za watu kwa matajiri....hata huyu nimkimuona nitajua la kufanya...’akasema baba yake huku akiingia chumbani na mara akatoka na ule mfuko mkubwa uliojaa nguo.

‘Hizi naenda kuzitia moto, kama nguo inakufaa chukua, sitaki kitu chochote chake, ngoja nikanunua kibiriti....’akasema nakutoka nje.

Baba yake alipoondoka, akabakia akiwaza, ‘Sasa sijui nifanyeje na hizi pesa, ngoja,... huko ninakokwenda kijijini kuna njaa, hizi zinaweza zikanisaidia nikafanyia msingi wa biashara,... lakini hapana, kufanya hivi sio zambi. kweli..hapana...ngoja nifikirie’akatulia kidogo huku akizaingalia zile pesa na baadaye wazo likamjia akasema;

‘Mimi natachukua hili bulungutu moja ...Yapo, moja mbili tatu nne, hapana mimi nitachukua mabulungutu mawili, na mawili natamuachia baba, na haya yangu mawili, nitakachofanya, lazima nimlipe yule kaka wa watu fadhila, najua bado anasota rumande kwasababu labda wamekosa hela ya kutosha, mimi nitampa mtoto wa Msomali hili bulungutu moja, likamsaidie kwa dhamana.....’, akasema nakuzigawa harakaharaka , na yale mafungu mawili akaweka kwenye mfuko wake.....hayo mengine mawili akayafunga kama alivyoyakuta.

‘Ehe sawa kabisa, nimekja kwa kazi moja, nataka kuzichoma moto hizi nguo na chochote kilicho chake,... hebu angalia kama kuna nguo za maana zinazokutsha chukua haraka..’sauti ya baba yake ilimshitua akiwa anaingia mlangoni.

‘Baba kuna kitu nimekiona humo kwenye mfuko mdogo....na nikakiweka humo kwenye huo mfuko mkubwa....’akasema binti Yatima.

‘Sitaki kitu chochote kutoka humo,vitu vyote humo vinanuka ushetani ushetani, uchafu usio faa, na dawa yake ni kuchomwa moto...hata kama ingelikuwa ni pesa,sizitaki....’akasema huku akikusanya kusanya vyema zile nguo na kuzisindilia ndani ya mkoba mkubwa, tayari kwenda kuzichoma.

‘Kuna pesa kweli baba....’akasema binti na baba alivyosikia hivyo akasimama na kumwangalia binti yake.

‘Unasema kuna pesa ,... zipo wapi...?’ akauliza hamasa, huku akianza kuzitoa hizo nguo kwa fujo na kuzitupa chini moja moja.
Angalia vizuri hapo, nguo hiyo nyekundu, hebu fungua hapo....’akasema binti, na baba akafungua kwa haraka haraka kama vila anaona kinyaa kuishika ile nguo, na mara mabulungutu mawili ya pesa yakadondoka na karatasi.....haikuiona ile karatasi alichoona ni zile pesa.

‘Mungu wangu ....pesa zote zote hizi zinatoka wapi....sasa binti yangu naona safari yako haipo tena , unajua nini tutakifanya, hizi pesa, nitanunua mitumbwi, na kazi yake itakuwa kukodisha, mimi nakaa ufukweni, wakirudi wavuvi wananipa mshiko wangu....nyingine, nafungulia duka, hakuna shida tena, kwanini uondoke, maana kuondoka kwako hapa ilikuwa ni kwasababau ya hali ngumu, sasa pesa ipo...’akasema baba mtu.

‘Na tena nitakufanyia sherehe kubwa ya harusi yako... chukua hizo khanga mpya ...hapo, hiz0 kwanza zilikuwa hazimtoshi mama yako....’akaongezea na kuzichuku akhanga mpya zilizouwa bado zimefungwa na kumkabidhi binti yake, na baadaye akazigeukia zile pesa na kuzibusu, huku akisema;

‘Hizi khanga nitachukua, lakini baba mimi sitakaa hapa, kumbuka mama akirudi hapa na kukuta pesa hazipo,... unafikiri nani atamshambulia, utanikuta mimi hapa nyumbani vipande vipande..hapana,kama wewe una mipango yako hiyo endelea tu, lakini mimi leo naondoka...kama hawo waowaji wana nia kweli watanifuata huko huko kijijini...’akasema binti.

‘Sawa, vyovyote iwavyo, lakini ujue binti yangu nakupenda sana, wewe ni mtoto wangu pekee,angalia mama yako huyo alivyo, alijua kuwa atanitoroka, kawachukua watoto wake wote kawapeleka kwao, huko kwa bibi yao,utafikiri hatujazaa naye,kwanza watoto wenyewe hakuna hata mmoja ninayefanana naye, wanafanana na....’mara mlango ukagongwa na harahara baba mtu akakimbilia chumbani,...

Binti Yatima, mawazo yake yote yalijua ni wageni wamekuja kuhsu maswala ya ndoa, kwahiyo alichukua khanga za mama yake mpya, akajitanda haraka haraka....halafu aakajificha chumbani kwako kusikiliza, lakini aliposikia sauti ya mjumbe akajua hakuna cha ndoa, labda ni mambo ya kesi, akatoka na kusimama, mlangoni mwa chumba chao,akiwa kajitanda vyema khanga....hajawahi kuvaa khanga mpya ....lao kazifuma, ngoja naye ajionyeshe kuwa anajua kuzivaa.

‘Subiri nakuja....’akasema kwa sauti, halafu akasema kwa kunong’ona kwa binti yake, `usiwafungulie kwanza mlango, mpaka nitoke mwenyewe...’akaingia chumbani .
Na mara binti akaiona ile kartasi iliyodondoka pale chini wakati baba yake anazichukua zile pesa, akataka kuiokota, lakini mara baba yake akatokea, na kuwakaribisha hawo waliopiga hodi....

‘Karibuni jamani, ooooh, leo mumenitembelea, mnataka nini maana nyie watu wausalamahamna dogo, mumempata huyo mnafiki, au mnataka kusema nini...

‘Mnafiki gani huyo...?’ akauliza mjumbe.

‘Si huyu mke wangu,maana kila kona Napata habari ambazo sijawahi kuzisikia kabla...’akasema.

‘Tatizo lako ulioa,....na nasikitika kusema, uliolea wenzako, ....ndio naweza kusema hivyo, ilikuwa kama umeolea wenzako,wewe kutwa, kuchwa ziwani,unafikiri yeye angeliishije,niliwahi kukushauri hilo siku moja, ukasema nakuchimba na familia yako...lakini sikulaumu, maana lazima mume uhangaike au sio..’akasemamjumbe na kumwangalia baba mtu.

‘Sikuelewi mjumbe...’akasema baba mtu.

‘Inbidi kama mjumbe wako, nikupashe maana mambo yalianza kidogokidogo sasa yamefikia kubaya, wewe ulizidi....mbona wenzako wanafanya kazi hiyo hiyo,lakini wanafika nyumbani kwao, siku moja moja wanashinda na familia zao, lakini wewe utafikiri huko ziwani ndio nyumbani kwako....’akasema mjumbe.

‘Sasa mumekuja kunisamanga, au muna lenu jambo, kwanza nina haraka sana, nataka kwenda kuhangaika, semeni shida yenu, maana wewe umewaleta hawa maaskari hapa najua mna jambo muhimu,....haya mna shida gani?’ akauliza.

‘Tumekuja kuulizia kuhusu mke wako...kuna taarifa kuwa kaonekana huko mjini, una habari hiyo...?’ akauliza mjumbe.

‘Ningelikuwa na habari hiyo, ningelishafunga safari na kumfuata huko huko, na cha moto angelikiona...mwanamke gani anakuwa kama changudoa...hapana huyu sasa kazidi... ’jamaa akwaambia kwa hasira.

‘Hahaha, hivi wewe unaweza kufanya lolote kwenye ule mwili, umbo lake na wewe ni kama mtu na mtoto wake, ...tuyaache hayo,hebu tuambie kwa mara ya mwisho mliongea nini, wakati anaondoka, hamkuagana kuwa ankwenda huko mjini, au ana mpango wowote, au hebu taumbai ilikwuaje...?’ akauliza yule askari.

‘Maswali hayo nimeulizwa sana, na nimeshajibu , kwa marefu na mapana,sijui kipi kingine cha ziada ninaweza kuongeza, naona hamna jipya,huyu mwanamke, kwa mara ya mwisho tuliachana naye sokoni, baada ya kununua vitu vya nyumbani, tukaagana, na mimi nikaelekea zangu, ziwani, kilichofuata huku nyuma mimi sijui zaidi ya kusimuliwa...’akasema huyo mvuvi.

‘Wakati unaondoka nyumbani ulimuacha marehemu,..?’ akauliza askari.


‘Maswali yale,yale,...sijui yatawasaidia nini, maana na majibu ni yale yale, ... Wakati tunaondoka nyumbani,tuliondoka pamoja,mimi mke wangu na marehemu, nyumbani nilimuacha binti yangu akiosha vyombo, tulipofika eneo la soko, marehemu akaingia kwenye moja ya duka lake, mimi na mke wangu tukaingia sokoni kununua vitu, kwahiyo mimi na marehemu kwa mra ya mwisho tuliachana hivyo akiwa hai, hapo alipoingia dukani kwake....’akasema mvuvi.

‘Unajua kuwa mke wako alikuwa akifanya biashara ya kuuza mabinti kwa huyu marehemu,na kesi hiyo ilishafikishwa polisi na wazazi wa hawo watoto, ...?’ akauliza mjumbe.

‘Hilo ndio nimeambiwa jana, nilipokwenda polisi...nashangaa hawa polisi wanamsaliti mtu wao kwa sasa...,mbona wakati yupo hai, hawakuweza kusema hivyo,...mbona hawakuwahi kunihoji swala kama hilo, sasa kafariki mtu wao, wanaanza kuropoka ovyo...hebu niambieni, mimi nina kitu gani cha kujibu hapo, naona hamna zaidi, kwaherini, au mnasemaje?’ akauliza huku akitamani kuwaambia waondoke.

‘Taarifa nyingine ni kuwa marehemu wakati anatoka huko dukani kwake alichukua kiasi kingi cha pesa, na inasadikiwa ndizo hizo anazozitumia mke wako huko mjini, kwani huko anaishi kwenye hoteli ya kifahari, na mambo anayoyafanya huko ni ya aibu tupu...una habari zozote kuhus hilo? ’akauliza mjumbe, badaka ya hawo polisi, mjumbe alishwahi kuwa skari, kabla hajastaafu.

‘Eti nini,....mjini ipi, yaani nyie mnajuwa wapi alipo, badala ya kumkamata mnakuja kuniambia mimi,....Sasa hivi napanda basi, niambieni ni mjini ipi, nikimuoma ama zake ama zangu...’akasema baba mtu.

‘Hilo sio muhimu kwa sana, kuna watu wanamfuatilia, sisi tunachotaka ni kuona kama tutapata ushahidi zaidi kuhusika na hayo mauaji, na kama una tetesi zozote au unajua lolote kuhusiana na hilo,kwasababu kama unatuficha kitu ,mwisho wa siku utaishia na wewe jela kwa kuwa mkishirika wake...’akasema askari.

‘Mimi kama alivyosema mjumbe, asilimia kubwa ya muda wangu ulikuwa ziwani, mke wangu na shughuli zake, sikuwa nazijua, kama ningelikwua nazijua ningeshampa talaka yake muda mrefu...ningeoa mke mwingine haraka sana, kwani dunia hii yupo peke yake bwana....kwanza sitaki kumuona tena...’akasema huku akitaka kuwaambia waondoke.

‘Tunaweza kupekua ndani , maana huenda tukapata kistu cha kutusaidia kuhusu yeye, kama hujui wapi alipo, na hizi nguo zake unataka kuzipeleka wapi...?’ akauliza mjumba.

‘Nataka kuzitia moto, zinanitia kichefu chefu....’akasema baba mtu,na mara askari akaona kile kikatarasi kilichokuwa kimedondoka pale chini, akainama kukiokota, na akakikunjua na kukisoma, halafu akampa na mwenzake ....

‘Hii karatasi imetoka wapi?’akauliza askari.

‘Karatasi, mbona sikumbuki kuiona kabla....’akasema baba mtu na kumwangalia binti yake.

‘Nimeiona ikidondoka wakati unaziweka hizo nguo vizuri humo ndani ya huo mkoba....’akasema binti.

‘Sawa, hii karatasi itatusaidia mbele ya safari....ni kielelezo kingine, kuhusu hii kesi yetu...’akasema askari.

‘Kwani imeandikwa nini cha muhimu.....?’akauliza baba mtu.

‘Kuna maelezo ambayo yanathibitisha hilo tulilokuwa tukilifuatilia, lakini kunkosekana kitu muhimu...je una uhakika kwenye hizo nguo kulikuwa hakuna kitu kingine?’ akauliza huyo askari.

‘Ni nguo zake tu,....sinajipekua sana, labda kipo ambacho mnakihitaji,... kama mnazihitaji chukueni,mkazipekulie huko mbele ya safari, mimi sizitaki tena humu ndani kwangu......, vinginevyo nitazichoma moto...’akasema baba mtu.

‘Hata sisi hatuzihitaji sana..., tunachohitaji ni hicho kilichokuwa pamoja na hii karatasi,inavyoonekana kulikuwa na kitu kimeweka pamoja na hii katarasi, kama kuna kitu kilikuwa pamoja na hii karatasi ulioandikwa humu,ni vyema tukajua maana itatusaidia kwa kiasi kikubwa sana....’akasema huyo askari.

‘Mimi wala sikuiona hiyo katarasi hadi mlipoiona nyie, mawazo yangu yote yalikuwa kuzichoma hzo nguo, sasa....ooh, ...hivi huyu mwanamke ni binadamu kweli....mimi naona tupekue humo kwenye nguo zake labda tutaonahicho mnachokihitaji...’akasema baba mtu.

‘Haina haja kama ulishapekua na hukuona kitu,.., ila zirudishe hizo nguo ulipozichukulia na hakikisheni kuwa hamgusi kitu chochote cha kwake tena’, ...akasema askari.

‘Mimi nashauri tufanye upekeuzi kwenye vitu vyake kabla hatujaondoka,..huenda tukagundua mengine zaidi ....kama wanavyodai hawa kuwa hawajaona kitu, na ndio mara yao ya kwanza kukagua huoo mfuko,u humo tutagundua tu..’ akasemammoja wa maakari.

‘Tunaweza kufanya hivyo kwasababu mumewe yupo, ...lakini vyemaupekuzi ungefanyika mwenyewe huyo mwanamke akiwemo, ....lakini kwasabanu mumewe yupo, tunaomba ushirikiano wako, upekuzi huo utafanyika ukiwepo ili uhakikishe mwenyewe....hiki hapa ni kibali cha upekuzi...’akasema askari ambaye alionekana ndiye kiongozi wao, na mjumbe akakubali, baba wa binti akasita kidogo, ....

‘Lakini hii hapa ndio mifuko yake yote, sizani kwamba kuna kitu chake kingine ndani...’akasema baba mtu akionyesha wasiwasi....

‘Hamna shida, ...sisi tunachotaka nikujirizisha tu, ..kutimiza wajibu wetu...tafadhali turuhusu tuingie....’akasema huy o askari...

Je nini kitatokea tuendelee kuwepo sehemu ijayo.TUPO PAMOJA DAIMA

WAZO LA LEO: Unapotenda mabaya ukagundua ubaya wake, ni vyema ukatubu ukweli wa kutubu kwa kuacha kabisa,na kujisahihisha,....lakini kama utarejea tena kosa lile lile, basi hapo wewe ni mkosaji. Kama wanenavyo wahenga, kuwa kutenda kosa sio kosa bali kulirudioa hilo kosa.


Ni mimi: emu-three

3 comments :

EDNA said...

Jirani yangu kwema? nakutakia siku njema.

Precious said...

Pesa ni shetani mbaya sana inafanya binadamu wawe wabaya maana wako tayari kuua, kusaliti na kufanya lolote baya kwa ajili ya pesa. M3 tuko pamoja mpendwa Allah azidi kubariki kazi za mikono yako.

emuthree said...

Hallo jirani yangu Edna, na mpendwa Precious, nawashukuru sana kuwa nami, Mwenyezi mungu awabariki sana. Tupo pamoja