Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, March 2, 2012

Binadamu hatosheki
Kuna kitu muhimu sana ambacho wengi tunaho katika maisha yetu, hili ni kutokana na asili ya binadamu, kuwa kaletwa hapa duniani, pamoja na kumcha mungu,lakini pia lazima ahangaike, na hii yote ndiyo inayomuingiza binadamu katika mihamaniko ya kimaisha, iliyojaa mitihani anuia.

Katika hili, kila mmoja anapambana ni vikwazo mbali mbali, kila mtu ana matatizo yake. Hutaamini kuwa hata yule tajiri unayemuamini sana duniani, naye ana matatizo yake, na hakeshi kulalama au kumuomba mungu wake, kama ana imani hiyo, ndio maana anahangaika, licha ya kuwa ana pesa ambazo anaweza kuzitumia hadi anaingia kaburini, lakini bado hatosheki.

‘Ama kweli binadamu hatosheki hata ukimpa nini milele hataridhika....’ nayakumbuka sana maneno ya wimbo huu toka katika moja ya bendi zetu kama sikosei inaitwa Ochestra Makassy.

Ama nikiwaza haya, nilimkumbuka rafiki yangu aliyenitembelea karibuni, alipofika moja kwa moja alianza kulalamika, akisema;

‘Mwenzangu nataka kuacha kazi, maana hapa nilipo kichwa kinaniuma....’akasema na kuniacha hoi, kwani mimi natafuta kazi, leo mwenzangu anasema anataka kuacha kazi, moyoni nilitaka kumwambia anipe mimi hiyo kazi, nikasahau kuwa kazi yake haiendani na taaluma yangu.

‘Kwanini unataka kuacha kazi..?’ nikamuuliza.

‘Bwanawe , najituma, nafanya kazi kama punda lakini bosi wangu hanithamini, yeye kila dogo kwake ni kubwa, kila nifanyalo kwake halikosi kasoro, nashindwa hata kuwaza jingine, zaidi ya kumuwaza yeye, ni ni lipi jema nitende ili anione nafanya kazi...’akasema huku akionyesha uso wa huzuni.

‘Ndio kazi ndugu yangu we,unahitajika kuvumilia maana wewe wasema hivyo , na kulalamika kwasababu kazi unayo, je ungelikuwa huna kazi kama sisi ungelisemaje....?’ nikamwambia.

‘Ni heri ujue huna kazi, kuliko kuwa na kazi ikutoe nyongo, hata raha ya kazi huna,.....unajua karibu nishikwe na kiarusi,maana siku hiyo bosi alinisema mpaka shinikizo la damu likapanda, karibu nidondoke maana mwili uliisha nguvu,na maumivu makali yakanipata kwenye moyo.....hapo kilichokuwa kimebakia ni nini kama sio kushikwa nakiharusi...weweusiseme, kuna watu wana roho mbaya....sijui nikuelezeje...’akasema rafiki yangu huyo.

‘Kwani yeye anataka nini, au anataka ufanye nini ili aone unafanya kazi, labda mnasigishana katika mawasiliano...?’ nikamuuliza.

‘Sijui, anachotaka nini, nini, labda anataka aonekane anafanya kazi kwa kuongea sana, kwa kugeuka kuwa mnyapara....maana hatosheki kila unalomfanyia....hatosheki hata na juhudi zetu, hana jema kabisa...’akasemarafiki yangu.

Ndugu wapendwa wa blog hii, maisha ni magumu, na kila mmoja anatafuta usiku na mchana, na hakuna hata mmoja atakayesema sasa nimetosheka, kila mmoja ana ambalo analikosa, na anaomba kwa kila hali alipate...hiyo ni sawa na ndivyo tutakiwavyo tuwe, cha muhimu kwetu ni kujenga subira, huku unatenda wajibu wako.....

Je mnamkumbuka rafiki yetu anayeitwa Subira, nampenda sana rafiki yetu huyu maana akijaa moyoni, hutahangaika sana, na pili tusimsahau rafiki yetu mwingine anayeitwa `kinaa...’ huyu mara nyingi hatumkumbuki, kinaa inasaidia maana hata ukipata kidogo kinatosha, unakinahiwa na uchu wa kupat a zaidi..mafisadi hawampendi kabisa huyu jamaa....

Nimeona Ijumaa isipite hivi hivi bila kuwasabahi kwa wazo hilo la leo, kuwa Binadamu katu hatosheki hata umpe dunia na vilivyomo atasema aaah, ningelitaka na ahera...

NB Kisa kinaendelea lakini ...ndio hivyo tena, nashindwa hata la kuongea, ...Tupo pamoja daima

Ijumaa njema.
Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Hii ni kweli kila mtu hatosheki

Anonymous said...

Hii ni kweli kila mtu hatosheki

Yasinta Ngonyani said...

Ubinadamu tumeubwa kipekee kabisa hakuna tunachoriki kwa kila jamba..aliye mene anataka kuwa mwembamba na halfu kinyuma aliye na mke/mume anataka zaidi sijui mwisho wake nini?

emu-three said...

Mwenyewe,kama ulivyosema kuwa,hakuna maisha yasiyo na mitihani,na mafanikio hayaji kwa njia ya rahisi,pasipo na majaribio na mitihani.

Ndiyo,maana kwa sasa,kila ukitaka kupata kitu,kam kazi,lazim ufanye mtihani,ukifaulu tu,kazi umeipata,hata kama baba yako au mama yako ni fisadi.Ila,tumetofautiana sana,kimaisha na familia ya kifisadi,

Kuna watt wengine,wamezaliwa hadi wanazeeka,hawajui shida ni nini?Mfano,familia ya viongozi wt wa kiafrika,jinc wanavyong'ang'ania vyeo,kuachia madaraka hawataki,hata km wakiachia,wanawapatia watu wao,ili kulinda maslai yao. Hebu angalia vyama tawala wamejaa wenyewe tu,kila mtu anamsogeza taratibu mtt wk.Cna wivu wala nini(Usiseme kuwa mimi,nawaonea wivu,mafisadi)Hapana.

Kuna,mwezi au miezi,ilishapita,nilisoma kwenye blog mmoja,wameonjesha big house ya mtt mmoja wa mkubwa mmoja, jina nalihifadhi,aliyojenga,ina thamani ya bilioni moja na ushee,je,huyo ndugu yetu,pesa yt ya kujengea house ameitoa wapi?C,ndiyo hao ambao wanahujumu uchumi wa nchi? Hebu jiulize mwenzangu na mie,hapo hata shilingi huna,huku ada ya watt inakupiga chenga,hicho kibanda chako hata thamani yk,milioni 30,haifiki,je,utalinganisha na hao waliobarikiwa duniani?

Kwa hiyo,kwenye maisha,kuna tofauti ya ngazi au madaraja.Usemi wako,naukubali nusu na ninaukataa nusu.Wengine,wameshatayarishiwa kbs,utukufu wa kwenye dunia hii,mie na wewe ndugu yangu,tuzidi kumuomba Mungu,atupe tu,riziki yetu ya kila cku.
Hapa bado najiuliza,cpati jibu,mtu anaweza kuwa na house zaidi ya 10,vitu vya thamani ndiyo usiseme,lakini,kuna cku moja tu,itafika,ataenda na nguo moja,km yule maskini na atalala nje km yule muhitaji wa barabarani,vitu vyote,alivyoviahangaikia anaviacha hapa hapa duniani.
Oh, najiuliza tena, hivi,kwanini,cye binadamu,hatuna roho ya kushukuru,kwa kila kidogo,ambacho Mungu ametujalia?Mtu,anakuwa na gari moja,lkn alimtoshi,atataka kuwa na lingine nk.Kwa nini,ndani ya mioyo yetu,kuna shimo kubwa sana,ambalo alitosheki?Hata ukilifanyia nini ni bure tu.
Oh, tena leo,kuna habari,cjui madoctor wamegoma,nk.Hivi,kwa maskini wenzangu,c,watakufa tu,eeh Mungu,tunusuru na janga hili,mgonjwa wetu na wagonjwa wt,Mungu,nyoosha mkono wk tu,kugeuza mioyo ya hao viongozi na madoctor,roho za watu,wenye mahitaji zisiangamie,kwa kosa la watu wachache.Nackia uchungu ndugu yangu,usifikilie,nakuandikia maombi,hakuna.
Kwa hali iliyofikia hapo home,ni mbaya sana.Viongozi wetu,wamegeuka km mashetani,hawana huruma na wananchi wao.Hivi hawa viongozi,wanaapa kwa kutumia vitabu vitakatifu,c,wanamchezea Mungu,ila ndani ya mioyo yao,wanamuapia shetani. Sijui wanamuapia mungu yupi…?
Kweli dunia imefikia mwisho.Katika maisha yangu ya ndoa,nimejifunza mengi sana,na soma kubwa ambalo nimejifunza na hata wewe ndugu yangu,ambalo unalipenda sana ni neno la SUBIRA….kuna dada anaitwa Subira, sina maana yeye, hapana, ila matendo yenyewe ya kusubiri.
Km Mungu,akikujalia kukupa zawadi hii ya subira,hakuna kitu ambacho kitakushinda chini ya jua.Kwani muovu shetani,anapenda sn,kukupatia udhaifu wa kukata tamaa,lkn ukiwa na huyu dada Subira,jua wewe ni mshindi tu,cku zote za maisha,hata mawimbi,mafuriko yaje kwa kila njia,ukimshikilia tu huyu,umeshinda.Hata km majaribu,yatafululiza kukujia kwa kila njia,kama Ayubu,lkn ukiwa na subira,mambo ni poa tu.

Ipo cku,tutafanikiwa,ushindi upo njiani.Saa ya Mungu,ni tofauti na saa ya shetani au ya binadamu.Na zawadi au kitu ambacho Mungu,anakupatia ni chema zaidi.Kwani vitu vyote ni mali yk na hakuna jambo lililo gumu ambalo linamshinda kutenda.Yeye,anatenda kwa muda wk na majira yk,km ukiwa na subira,utafaidi sana matunda ambayo Mungu,atakupatia kwa wakati wk.
Nafurahia sana kwa ndugu yangu kuwa na mpenzi,anayeitwa subira.Ipo cku,utapata kazi nzuri sana na machungu yt utayasahau kwa kumzingatia huyo subira,km mwenyewe ulivyosema.Nakutakia mchana mwema na mafanikio mema
Mimi dada C.

Anonymous said...

I couldn't refrain from commenting. Perfectly written!

Also visit my web page :: http://paydayloanspup.co.uk