Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, March 5, 2012

akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-86 hitimisho 30
‘Wote mpo chini ya ulinzi, naomba msiguse chochote, sitasita kufanya lolote bila kujali wadhifa wenu najua wewe ni bosi wangu, lakini hapa natimiza amri ya serikali.....’akasema mpelelezi huku aki wa kaishika bastola yake vyema,huku akihakikisha amekaa swa ili kama litatokea lolote aweze kukabiliana nalo.

Licha ya kuwa alihakikishiwa usalama wake na akaombwa kuwa asiue, kwani watu hawo wawili wanahitajika sana, lakini moyoni alikuwa na jeraha ambalo hatalisahau maishani, jereha lililomsukuma kujiunga na kazi ambayo hata baba yake hakuipenda, na pia alikuwa keshaapa kuwa akimpata aliyemua baba yake, kama haki haitapatikana, basi ataichukua haki hiyo mikononi mwake,

.....

Alimwangalia mkuu kwa jicho la hasira, ....akataka kumuuliza asikie kauli yake, lakini akaona hakuna haja, ipo siku itafika haki iliyopotea itapatikana, ipo siku tu, na inavyoonekana siku yenyewe imeshafika ni swala la muda...alipokumbuka hilo alimwangalia mkuu wake kwa macho ya chuki, na aliomba litokee jambo, ili iwe sababu ya kuondoa kovu ambalo limekuwa kama donda ndugu.

Asingelijua hilo kama asingelisikia mazungumzo ya mkuu wake akitoa kauli yake mwenyewe mdomoni kuwa yeye ndiye aliyemuua baba yake, hakuamini siku hiyo alipofika hapo ofisini akamsikia akiongea na simu na mwenzake, na hakuweza kuonana naye siku hiyo kutokana na hasira zilizomzonga....

*********

Baba yake Mpelelezi, alikuwa mmoja wa watu muhimu sana serikalini, na alikuwa kikwazo kikubwa kwa wale wasiotii sheria za nchi, na hili lilimuumiza sana Mkuu, na akawa akitafuta kila njia ili aweze kumuondoa, ili iwe rahisi kwake kufanikiwa mambo yao, na mipango ya siri ikafanywa bila watu kujua,na kwa vile mkuu alikuwa akiaminika sana serikalini, hakuna aliyekuwa na wazo kabisa la kumshuku huyu jamaa.

Maiti yam zee huyu mashuhuri, mchapakazi hodari iligundulika porini, ikiwa na majeraha ya risasi na ilionyesha dhahiri kuwa muuaji, alikuwa ni mtu anayemfahamu sana huyo mzee, kwani macho yake yalikutwa yakiwa yanaonyesha mshangao....

Mpelelezi alimaliza chuo akiwa mwanasheria kama baba yake alivyotaka, na kipindi hicho baba yake alikuwa bado yupo kazini, na lengo la baba yake ni kumfanya mtoto wake awe wakili wa kijiegemea, hakutaka ajiingize serikalini, ....

Lakini lengo la baba huyo halikuweza kukamilika, na hata hakuwahi kufaidi mshahara wa mwanae kwani hata hivyo mtoto huyo alikiuka ile kauli ya baba yake na kuwa maji kufuata mkondo..

Mpelelezi alisukumwa na dhamira ya kujua ni kwanini sheria haikufuata baba yake alipouwawa, na alipofuatilia kama mwanasehria kugundua kiini cha mauaji hayo,alijikuta akipata vikwazoo vingi, mwisho wa siku akaona ili aweze kugundua yote ni lazima aingie huko huko taarifa zinapopatikana , akajiunga na chuo chamafunzo ya upepelezi. Alifanya vizuri sana na hata kuchukuliwa na serikali kama askari kanzu,..

Alikumbuka siku ile alipomfahamisha mama yake kuhusu dhamira yake hiyo, mama yake alipinga vikali, lakini alikuwa keshaamua akamwambia mama yake;

‘Mama mimi najiunga na polisi ili nihakikishe kuwa namkamata huyo muuaji wa baba, hata kama itachukua miaka kumi, lazima ashikwe na nione haki inatendeka....’akasema kumwambia mama yake.

‘Wewe, unasema nini hukumbuki baba yako alivyokuwa akisema, hataki mtoto wake awe askari...au ndio manata wote muuwawe, mniache sina mbele wala nyuma...’akasema mama yake.

‘Mbona yeye alikuwa askari,....hapo huniambii kitu, lazima niwe askari ili niweze kupata nafasi ya kuchunguza kifo cha baba yangu, najua lazima nitamgundua muuaji...’akasema na kesho yake alichukua fomu za kujiunga na mafunzo ya upolisi, na kweli akafanikiwa kwani dhamira njema huzaa matunda.

Akiwa mafunzoni , mara kwa mara alikuwa akikumbuka kauli ya baba yake ambaye kila mara akirudi kazini, akiwa kachoka, alikuwa akipenda kuisema;

‘Mwanangu kazi hii ni ya hatari na hutaamini kuwa ndani ya wenzako ambao mnaaminiana ndipo humo humo kuna maadui zako, na uadui wenyewe utaukuta hauna hata maana, ni kutoakana na kitu kidogo tu, labda ni kutakana na kugombea madaraka, au kutokana na kugombea wanawake...hakuna cha muhimu sana, lakini binadamu anajisahau na kuanza kujenga chuki, na kwa vile keshazoea kutoa roho za watu basi haoni shida kukulenga risasi...

Siku alipoisikia kauli hiyo kwa mara mwisho ndiyo siku kesho yake alipopokea taarifa kuwa baba yake kakutwa amekufa porini kwa kupigwa risasi, na hata uchunguzi ulipofanyika, haikuwahi kugundulika sababu ya kifo cha baba yake na ninani aliyehusika na kwasababu gani,...na kwa vile nchi ilikuwa imegubikwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, basi ikachukuliwa kuwa huenda kauwawa na wapiganaji wa msituni.

Hata alipojiunga na polisi na kulifufua hilo jalada, hakuweza kabisa kupata kitu, ilionekena kuwa kila kiti kilifutwa kabisa, kama vile hakukuwa na jambo kamahilo, na taarifa zilizopo ni maelezo mafupi tu, kuwa mzee huyo huenda aliuwawa na majangiri wa msituni. Hadi siku ile, aliposikia mkuu wake akiongea na huyo asimu wake, na kusema kuwa katika watu atakaojivunia kuwa ni ushindi kwake ni kuwaondoa watu walikuwa kikwazo kwake kufikia malengo yake na mmojwapo ni baba yake.
Aligeuka kumwangalia simu wa mkuu wake na kusemamoyoni, kama na wewe usingelikuwa unatafutwa ningekuambia kuwa lengo letu ni moja, lakini wewe na yeye hamna tofauti....
Akiwa na jicho lililojaa hasira za kulipiza kisasi aliwaangalia watu hawo kwa makini sana, na akijua kabisa hawo anaokabiliana nao ni watu wanaoijua vyema kazi yao, na kama wataamua kuleta ubishi, hana budi ya na hatasita kuzimimina risasi zote zilizopo kwenye ile bastola....akamwangalia mkuu kwa jicho moja na jicho jingine likimwanglia huyo asimu wake ambaye bado amekuwa kitendawili kwao kuwa ni nani mtu huyu...na ndugu kwa vipi na marehemu Tajiri Mzungu.
*********
Mkuu alikuwa kashikwa na butwaa hakuamini hili lililotokea, hata hivyo moyoni alijpa moyo kuwa huyo mpelelezi hajui lolote na huenda anafanya hivyo ili aweze kumkamata huyo mhasimu wake, ambaye hakuonekana kujali, na mawazoni mwa mkuu alihisi kuwa huenda mhasimu wake hajali kwasababu kaja na lengo moja la kulipiza kisasi.
‘Vipi kwanini...mbona unaingia ofisini kwangu na bastola mkononi,.... sijamuita mtu kuja huku, au mnadhani nimevamiwa na huyu mtu...’akasema huku akimwangalia yule jamaa ambaye alitulia kimiya akiwa kaangalia mbele tu, utafikiri sanamu.

Huyu ni mtu wangu nilikuwa namjaribu tu, ukakamavu wake, kwahiyo usitie shaka,unaweza kuondoka maana tuna mazungumzo muhimu na huyu mtu wangu, au jingine limekuleta, kama lipo utabidi usubiri , na hii tabia ikome, sipendi mtu kuniingilia ofisini kwangu bila taarifa..’akasema mkuu huku akijaribu kusogea karibu na droo ya meza ili aweze kuifungua na kuchukua bastola yake.

‘Sikiliza mkuu, sijawahi kufanya hivyo kabla, unanijua taratibu zangu,...nafikiri umenisikia kuwa hapa nipo natimiza amri ya serikali, nyote mpo chini ya ulinzi naomba usisogeze mguu hata hatua moja,maana sitasita kuitumia hii silaha, na unaijua silaha ilivyo....’akasema mpepelezi.

‘Mbona sikuelewi, nipo chini ya ulinzi, kwa vipi....wewe unakosa nidhamu hujui naweza kukuchukulia hatua mwenyewe hata bila kuomba kibali,kwanza usinionyeshe hiyo bastola, ...unanielewa lakini...’akasema huku akitaka kusogeza mguu, na kilichofuata hakuamini, kwani risasi ilimkosakosa mguuni na kumfanya aruke nyuma na hapo akawa kasogea mbali na meza yake, na ndivyo mpelelezi alivyotaka.

‘Hilo ni onyo mkuu, hapa natimiza wajibu wangu na kwa taarifa yako tu, kikosi kipo nje, kinasubiri amri nyingine, na pia haya yote yaliyokuwa yakiendelea hapa ndani yamekuwa yakionekana moja kwa moja, ...simnajua tena utaalamu wa siku hizo...’akasema mpelelezi akionyeshea kidole chombo kilichopo eneo la juu ambacho hakikuwepo hapo kabla na hata mkuu hakuwa na taarifa hiyo, kwani hakumbuki kiliwekwa lini na moyoni akawa anajilaani kwanini hakuwa muangalifu kama ilivyokuwa kawaida yake.

Aliinua kichwa kuangalia sehemu ya juu na kweli aliona chombo kidogo ambacho hutumika kuchukua matukio na kunaswa kwenye vyombo vya hawo walioviegesha, kwahiyo alikuwa na uhakika kuwa kweli hayo yote yaliyokuwa yakitendeka humo ndani yameoneekana au kuhufadhiwa mahala Fulani , lakini hakuwa na uhakika kuwa ni nani alifanya hiyo kazi, kwani chumba chake hakuna mtu mwingine mwenye ufunguo...

‘Nani kaweka vitu hivi....?’ akauliza huku akihamaki.

‘Hilo sio muhimu kwa sasa, ...kwani mengi yameshagundulika, nayo sio muhimu kwa sasa,kwani tukiyachambua zaidi tutajikuta tukipiziana visasi...’akasema mpelelezi, na kabla Mkuu hajasema kitu, akasema;

La muhimu ni ni wewe kukubaliana na hali halisi kuwa hayo uliyokuwa ukifanya kwa siri na kwa dhahiri ambayo ni kinyume cha wadhifa wako na dhamana uliyopewa na jamhuri, yamefika mwisho, ukumbuke kuwa ubaya haulipi, na katu dhuluma huwa haidumu,....mengi uliyofanya yote yamegundulika..’akasema mpelelezi huku akibonyeza simu yake, kutoa ishara nje kuwa jamaa zake waingie...

‘Sikiliza mpelelezi, ...usichukulie mambo kiharaka kihivyo, ...kwanza tuelewane, mimi ni mtu wa heshima zangu, heshima yangu ipo pale pale,kwahiyo nakuomba utoke humu ndani kwanza...’akasema huku jasho likimtoka, na alipotaka kusogeza mguu, risasi ikapiga karibu na vidole vyake, akaruka nyuma na kumwangalia mpelelezi, ....alijua kweli huyo jamaa sasa hana mchezo...

‘Sikiliza mpelelezi, ...’kabla hajamaliza, mlango ukafunguliwa na vijana waliovalia rasmi kikazi wakaingia bunduki mkononi, ...

‘Hii nini sasa...?’akasema mkuu, na kabla hajajibiwa vijana wengine wakaingia na kumshika mkuu na jamaa yake na kuwatia pingu mkononi..
Mhasimu wake hakuonyesha dalili kabisa ya kuogopa, utafikiri hahusiki, na wote wawili wakasukumiwa nje ya ofisi na walipofika eneo la wazi ambapo ni mapokezi, mpelelezi akasema;

‘Mkuu unajua kabisa nchi yetu ilivyo sasa hivi, hali hii imekuwa tete kutokana na nyie wakubwa mliopewa majukumu, na badala ya kutimiza dhamana mliyopewa na wananchi ya kuwalinda wao na mali zao, mumekuwa mkitumia wadhifa huo kuhujumu nchi....umewaua watu wengi kisiri bila hatia, na mmojawapo ni baba yangu, lakini hayo tuyaache kwanza, tusema sasa basi,.... imeonekena kuwa ni bota mambo haya yakamalizika kisiasa zaidi kuliko kijeshi...’akasema mpelelezi.

‘Mpaka sasa hivi sikuelewi nani kamuua baba yako, kama aliuwawa ni kwasababu labda, aliingili mambo yasiyomuhusu.....’akawa kashikwa na uso wa mshangao lakini baadaye akasema;

‘Naona kama unapoteza muda wako, na hili nitahakikisha kuwa unapata adabu yako, nitakuonyesha kuwa mimi sikuchaguliwa katika wadhifa huu kiholela tu...na mikipata mwanya unaweza ukamfuata baba yako..’akasema mkuu kwa jicho la hasira.

‘Hilo lisikuumize kichwa, ila ninachotaka kukuambia ni kuwa, ili kujenga taifa imara la nidhamu, na sheria, inabidi tuanze mahala, na kusahau yaliyopita, ni hili litawezekana kama tutakuwa na baraza la maridhiano...inajulikana kuwa kuna wakosaji wakubwa, kuna watu wameuwawa bila sababu, na wengi wana kinyongo cha kulipiza kisasi, lakini hivyo visasi vitatufikisha wapi, maana unapilipiza kisasi kwa mwenzako na y eye pia atataka kulipiza kisasi kwako, sasa hayo yatatufkisha wapi....’akasema mpelelezi.

‘Kwanza kabisa tukae tukubali kuwa tumekosa,na ikibidi kila mmoja akiri makosa yake, asisubiri kuingizwa mahakamani, pili tukae katika baraza la usuluhisho na maridhiano, ili tuone jinsi gani tutayamalzia haya, msamaha utolewe, na kila linalowezekana lifanyike ili kila mmoja aridhike...tuanze kuijenga nchi yetu....jamani hamjachoka kumwanga damu za watu...’akasema mpelelezi.

‘Nani kamwanga damu za watu wewe....tatizo lako unajifanya unajau sana, ....eti baraza la maridiano, hamna kitu kama hicho , eti baraza la maridhiano, hiyo sheria kaanzisha nani, ninajua nini kitafuata baada ya hapa, lakini lazima nife kiume....utaona nini kitafuata...na olewako, ..nasema, ...ole wako....’akakatizwa kwa kusukumwa na mmoja wa vijana waliovalia kikazi ....

Mkuu aligeuka kumwangalia yule kijana kwa hasira, kwani haijawahi kutokea hivyo katika maisha yake, yeye siku zote amekuwa mtu wa kuogopwa,....mtu wa kutoa amri,leo hii anadhalilishwa...

‘Usijali mkuu, hili linafanyika kwa manufaa yako na vizazi vijavyo,....ipo siku utalikumbuka hili na badala ya kunichukia utanipa mkono.....kwani kama ingelikuwa mimi ni wewe, ungeshanimiminia risasi, ..’akasema mpelelezi .

Mpelelezi, akaingia tena kwenye ofisi ya mkuu kuhakikisha kuwa kila jambo limekwenda sawa. Akafungua ile kabati na kuchukua `briefcase’, hakuamini kuiacha humo, Alipomaliza, akatoka nje , na mara ghafla akasikia milio ya risasi, alipogeuka uoende ule walipokuwa wamesimama mkuu na mwenzake,, akamkuta mkuu akiwa chini, damu zilikuwa zikimvuja kifuani, ...na alipotaka kumkimbilia kuona nini kimetokea, mara mlipuko mkubwa wa bomu ukatikisa eneo lote la ofisi, naye akajikuta akirushwa hewani alipotua chini akapoteza fahamu, ....

WAZO LA LEO: Asiyekubali kushindwa katu si mshindani...

NB: Kila lenye mwanzo haliosi kuwa na mwisho...tuwe na subira tu, kisa kinamalizikia, ila sijui nyie mnakionaje, ....!Ni mimi: emu-three

No comments :