Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, February 16, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-82 hitimisho-26
Mgonjwa, hilo ndilo jina lake kwasasa, kila mtu anamuita hivyo, `mgonjwa’, ni kweli alikuwa mgonjwa na anawashukuru sana wote waliojitolea hadi kufanikiwa kufika India, hasa….Alipofika hapo alitabasamu, akaiunuka na kwenda dirishani kuangalia nje, hakuona kitu zaidi ya ukuta mrefu mbele yake,na kwa juuu kuna seng’enge zilizozungushiwa nyaya za umeme, ….akaguna na kurudi kukaa kitandani akainama kwa muda akiwaza....

Aliangalia saa yake na kuinuka tena pale kitandani, akatembea huku na kule, alishachoka kulala, na kufungiwa ndani kama mfungwa, na alikuwa pia kachoka kuulizwa ulizwa maswali kama vile yeye ni mkosaji, alishawaambia kila kitu, lakini wanakuwa kama hawaamuamini, kila mara wanamuuliza maswali hayohayo , mara leo kaja huyo , mara kesho kaja yule na kwa mara ya mwisho akakutanishwa na balozi wa nchi yake;

‘Huyu ni balozi wa nchi yenu, tumemleta hapa, ili athibitishe kwa kukuona na ajue kuwa upo hapa, na ili pia tuwe na maandishi yanayokubaliana, na kweli amethibitisha kuwa ilitokea ajali ya meli, na huko …hilo tunalijua hata sisi kwani walikuwepo raia wan chi yetu pia, na ajali ile ilikuwa yeto sote…’akasema yule mpelelezi huku akimwangalia yule balozi, na balozi hakusema kitu kwa muda ule, na huyo mpelelezi akaendelea kuongea kwa kusema;

‘Kwao wengi ambao mpaka sasa, ambo hawakuwahi kuonekana, kwani ni muda mrefu, wanatambulika kuwa wameshakufa na kinachochunguzwa kuhusu wewe kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kweli jina lako lilikuwepo kwenye orodha ya abiria waliokuwemo humo ndani…’akasema huyo mpelelezi ambaye siku zote yupo naye.

‘Huenda lisiwepo maana nilikuwa nisiwepo kwenye hiyo safari, ….niliamua kwenye dakika za mwisho, nikawahi bandarini ziwani, na kwa vile najuana na wahusika, nilipata tiketi hatua za mwisho, sijui kama walikumbuka kuniweka kwenye hiyo orodha yao, sina uhakika na hilo…’akasema mgonjwa.

‘Na hilo ndilo kosa na makosa hayo yanakuja kutupa shida siku kukitokea tatizo, lakini sio mbaya, tutatafuta njia nyingine ya kugundua hilo, ila cha muhimu, usiondoke hapa, hapa utakaa kwa muda, nimekuja kuchukua kumbukumbu na maelezo yako yote, maana upo kwenye nchi ya watu, na kiusalama na kiutaratibu utachukuliwa kama mhalafu, licha ya kuwa umeingia huku pasipo nia yako, ndio maana tunataka kuliweka hili kiutaratibu ili baadaye kusije kukatokea mgongano…natumai unanielewa..’akasema huyo balozi.

Kilichofuata ni yeye kujaza fomu maalumu, na picha yake ikachukuliwa na akaendelea kuulizwa maswali mengi, na baadaye wakaagana, lakini kwa masharti kuwa huyo balazi atakuja kumchukua hadi kwake, ambapo ndipo aatishi hadi ataporudishwa nyumbani…


‘Inabidi uje ukakae ubalozini, kwani ubalozini ndipo kutakuwa nyumbani kwako ukiwa hapa, na huko kuna usalama zaidi, kwani hata hawo magaidi wanaoisumbua nchi, hawaingilii nyumba za ubalozi ovyo, wanaziheshimu, labda wawe na uadui nao, na sisi tunashukuru kuwa hawo magaidi wa hapa hawana uadui na nchi yetu,…hatuna uhakika ila tunajaribu kuchukua tahadhari zote…..’akasema huyo balozi, na baadaye akaondoka nakumuacha akiwa chini ya ulinzi wa huyo anayeitwa Mplelezi.

******

Mpelelezi amekuwa rafiki yake mkubwa, kwani muda mwingi yupo naye, na amakuwa akimdadisi maswali mengi na kila alipotatizwa, alikuwa akiwasiliana na Inspekta, alikuja kuambiwa kuwa huyo Inspekta ni Mtanzania, ila alikuwepo haoa nchini, kufanya akzi maalumu, kwahiyo anawasilina naye mara kwa mara ili apate taarifa za huku kumhusu yeye.

‘Inabidi tuhakiki baadhi ya amelezo yako, kiutaratibu, sio kwamba sikuamini, lakini kutoakana na kazi yangu, kila jambo linahitajika kuhakikiwa…’akasema huyo mpelelezi.

‘Hamna shida, ila kila nilichokuambia ni kweli tupu…’akasema mgonjwa.

‘Hapa utajulikana kama mgonjwa, hatutaka jina lako lijulkanae kwanza, kisualama…’akamwambia huyo mpelelezi.

‘Sawa vyovyote kwangu sawa, ilimradi mambo ayende vyema, ila nina hamu ya kuwaona jamaa zanu, siruhusiwi kuwaona kwa sasa.

‘Huruhusiwi kwasasa, maana tulipogundua kuwa wewe sio raia wa hapa, inabidi tuchukue hatua zote zinazostahili, ungelitakiwa uwe jela…lakini kwa vile wewe sio mhalifu, na hilo lilitakiwa lithibitishwe mahakamni, lakini tutajitahidi hicho kipengele kisiwepo, ….usijali utawaona, lakini sio kwa sasa au kesho….’akasema huyo mpelelezi.

Kesho yake wakiwa wanasubiri achukuliwe kwenda huko ubalozini, mara Mpelelezi akapokea simu, alipoisikiliza , akatoka mle bila kusema kitu, na baadaye alipata taarifa kuwa huyo balozi wake hatakuja tena siku hiyo , asubiri kesho yake, kwahiyo akabakia humo kwa mpelelezi akisubiri.

Alipowaza hayo yote akajiona kama mfungwa fulani, alitamani atoke nje, alitamani akawatembelee ndugu zake aliotoka nao huko India, lakini haikuwa rahisi, hawo ndio ndugu zake, wengine hapo aliwaona wageni kabisa, hata hivyo hakuruhusiwa kuwaona hawo ndugu zake, aliambiwa hataweza kuwaona kwa sasa kwasababu ya kiusalama, kwani kwanza hana kibali cha kuishi humo nchini, kibali chake, ni cha zarura tu, na mambo mengine yanatayarishwa ubalozini, kwahiyo kiusalama ni bora asitoke nje.

‘Na hawa ndugu zangu kwanini hawaji kunitembelea …wao siwanaruhusiwa…?’a akjiuliza , akikumbuka kuwa walipofika uwanja wa ndege, yeye alichukuliwa moja kwa moja hadi hospitalini, alipata muda kidogo wa kuagna an ndugu zake wakimuahidi kuwa watakuja kumchukua, lakini sivyo ilivyokuwa, kwani alipofikishwa hospitalini hakukaa muda mrefu, alichukuliwa kwenda kuishi kwa huyo mpelelezi.

‘Utaishi kwangu kwa hivi sasa, hakuna anyejua kuwa upo hapa, weni watakuwa wanajua upo bado hospitalini, tunayafanya haya kwa usalama wako, na hapa ndipo kwenye usalama zaidi…’alimwambia huyo mpelelezi.

‘Usalama , usalama,…’ imekuwa ni wimbo masikioni mwake, akatafakari, hivi mimi sasa ni mfungwa, maana sio mgonjwa tena, hali yangu imerudi kama zamani, lakini siruhusiwi kutoka nje, na kama ni kutoka nje lazima niwe na walinzi pembeni, …

Akaguna na kuusogelea mlango, akatikisa kitasa akakuta umefungwa, akarui kitandani na kuanza kuwaza,, alianza kuwaza maisha yake tangu nyumbani hadi akafikia kwenye ajali ya meli, hapo akajikuta akikosa mengi ya kuwaza, kwani kuanzia hapo, ilikuwa kama ndoto, hana uhakika na hizo ndoto, kuwa zilikuwa ni kweli au ni ndoto tu, lakini alipofikia sehemu ya binto mrembo, akatabasamu,

‘Mhh, kweli wewe ni binti mrembo, nakuita binti, maana sina uhalali na wewe, na ukizingatia kuwa una ujauzito, ina maana una mtu wako, kwahiyo nitabakia kukuita binti mrembo…’akatabasamu tena na kulala chali, akageuka akalala kifudi fudi, alifanya hivyo mara kwa mara, na alipochoka, akainuka kitandani na kukaa kwenye kiti,..akatulia kwa muda akiwaza mazungumzo yake ya mwisho kabla hawajaachana uwanja wa ndege, aliona amuite hivyo `binti mrembo’ ili kufikisha hisia zake.

‘Mgonjwa, kama tulivyoambiwa inabidi tuachane hapa, nilitakiwa nikusindikize mimi hadi hapo hospitalini, lakini wamenikatalia, sijui kwanini, lakini hakujaharibika kitu, …ila nkuomba ujue tupo pamoja na wewe, mengi tutayaongea tukipata nafasi, naju yapo mengi ya kuongea, ila nikuulize, hivi mgonjwa wetu unakumbuka nini kilitokea, maana umesema umepona kabisa au sio, hata mimi naona, ila nataka nithibitishe, hilo….?’ Akakumbuka swali aliloulizwa na binti mrembo.

‘Nakumbuka mengi, ila baaada ya ile ajali mengi yanakuwa kama ndoto, sina uhakika nayo sana, labda watu wakunisaidia ni nyie mliokuwa karibu na mimi, ili kunithibitisha kuwa ni ya kweli au ilikuwa ni ndoto tu…’akasema huku akimwangalia huyo binti machoni. Na walipoangalia kwa muda binto akageuka pembeni na kucheka…

‘Unajua kwanini nacheka, …..mmh’akauliza kama haulizi. ‘Nakumbuka mbali sana, wakati mwingine natamani ile hali irudie, lakini sio kwa ubaya,…na tukio na kumbukumbu ya aina yake, na nisema ni tukio lililobadili mtizamo wa nafsi yangu….’akasema na kugeuka kuangalia kule walipokaa wenzao, ambao kwa muda ule walikuwa wakinunua zawadi mbali mbali, na Maua alikuwa hayupo upeo wao wa macho, huenda alikuwa maliwatoni.

‘Kwahiyo unakumbuka vyema kuwa ulionondoka kurudi nyumbani kwenu bila kuniaga, ukafika hukoo sijui ilikuwaje ukarudi tena Uganda, unakumbuka vyema hilo tukio..ni tukio lililoniumiza sana, lakini najua ulifanya hivyo kwa nia njema,….je unalikumbuka hilo?’ akauliza huyo binti.

‘Hapo sasa ndio kuna nitatiza kidogo, kuna kitu sikielewi vyema hapo, maana nakumbuka kama niliota hivyo au ilitokea hivyo…, lakini kitu kikubwa ambacho huwa nakiwaza sana, ni pale nilipokutana na jamaa mmoja…, sasa hapo kuna mambo yaninikwaza, sijui lipi lilitangulia, ila nakumbuka, nlifika huko nyumbani na nikakuta mke wangu akiwa anajiandaa kuolewa, na nilimuuliza kuwa kweli kazamiria hivyo na kweli anampenda huyo anayetaka kumuoa, ….na…hapo kumbukumbu inakata kidogo, kila nikijaribu kuwaza kuwa alinijibu nini sikumbuki, ila….’akatulia kuwaza.

‘Kama hukumbuki usijilazimishe mimi nataka kukuweka sawa, kuwa kweli ulikwenda huko kwenu, hiyo haikuwa ndoto, kwani wamethibitisha shangazi na ndugu yangu, lakini uliporudi hukunikuta, sijui nini kilitokea zaidi maana siku ulipoondoka tu, nikapata barua ya kwenda kusoma, barua hiyo ilicheleweshwa makusudi, na sikuwa na muda wa kusubiri tena , au kufuatilia kuwa umeenda wapi, nikaondoka kuwahi hiyo nafasi ya kusoma, …..nilipata simu kuwa umeonekana, na wakati huo nilikuwa nimeshafika huko chuoni, ninaposoma, sasa hebu niambie, hilo linaloingilia hapo mpaka usikumbuke zaidi ni nini..?’ akauliza huyo binti.

‘Ni kwamba, kwa namna nyingine ya kumbukumbu inanichanganya maana kuna mchanganyiko wa ndoto, na matukio ya kweli, ilionekana baadaye kuwa mimi ndiye nataka kuoa, yaani hiyo harusi bwana harusi ni mimi, na wakati nakwenda kumuona binti harusi nikajikuta kwenye nyika , kitu kama msitu, lakini ilikuwa tambarare, unaona miti mingi, na kupo kama hakuna watu wengine, na mara nilikutana na mzee, akaniambia kuwa nipo kwenye mitihani, nikiishinda nitampata mke wangu nikikosa sitampata tena….hapo sikumbuki vizuri kuna utata, kuhusu huo mtihani, nikikumbuka nitakuambia….lakini nikuulize, ndio nimeshajua kuwa ni kweli mke wangu kaolewa na rafiki yangu, lakini kwasababu gani hasa ya msingi sijaijua, najua itakuwepo, kwani namfahamu sana Maua, asingeliweza kunifanyia hivyo, lakini nastahiki kuambiwa hiyo sababu, au sio, sasa wewe kama ndugu yake keshakuambia ni sababu gani …?’ akauliza swali huku akimkazia macho huyo binti.

‘Hilo swali siwezi kukujibu, sio kwamba sitaki, hapana, …ningelifurahi angelikujibu yeye mwenyewe , lakini nakuhakikishia kuwa kama kuna sababu itakuwa ni sababu kubwa ambayo ilimzidi, kwani nakuhakikishia kuwa ndugu yangu anakupenda sana, hutaamini siku zote amekuwa akilia kwanini imetokea hivi, nimejarbu kumweka sawa, lakini….sijui kama hali hiyo itamwishia, Maua anakupenda sio utani…na kama mapacha walivyo, naihisi hiyo hali pia ….aah, sijui…’akakatiza na kuinama chini

‘Sijakuelewa hapo , kama mapacha walivyo….ina maana nyie mna hisia sawa sawa, kila kinachotokea kwa mwingine ni sawa au kinaweza kikamuathiri mwingine…?’ akauliza mgonjwa.

‘Nahisi hivyo, …lakioni sio kila jambo ….nimekuwa nikiteseka hata mimi na kipindi tulipokutana na ndugu yangu huyu, nahisi mambo mengi yakimtokea ninakuwa kama na mimi nimo, …lakini sio kila jambo..….’akasema na kuangalia pembeni, na baaadaye akabenua mdomo kidogo na kusema;

‘Nikimuona ndugu yangu akisononekana nateseka sana….. kama ningelijua njia ya kumsaidia ningelimsaidia kwa gharama yoyote ile,…namuonea sana huruma, maana kakutwa na matatizo juu ya matatizo na yanatokea mambo mengine ambayo hakuyatarajia, na ilimbidi achukue uamuzi mkubwa, licha ya kuwa utamuumiza…’akasema binti.

‘Najua hilo, sitakaa nimlaumu, …ilimradi asiteseke, na ipo siku tutayaweka sawa na huyo rafiki yangu, hata yeye siweze kumlaumu, maana huwezi jua kwanini ilitokea hivyo, lazima ipo sababu, na mengine ni juu ua uwezo wetu wanadamu,….sasa naogopa kama nitakuwa nimewaumiza watu wawili kwa pamoja, …ina maana hisia zenu zinafanana kama sura zenu, ….mmmh, pole sana, nashindwa hata nikuambie nini kwa sasa…’akasema mgonjwa

‘Wakati mwingine, tunakuwa kama tunachangia hisia, nimeligundua hilo….unajua, nilimlaumu sana mwanzoni,lakini hebu jaribu kuwa yeye, utagundua kuwa ilibidi uamuzi huo ufikiwe, hakupenda kabisa, hadi hatua ya mwisho,….lakini ikafikia hatua, akaona hana jinsi inabidi akubali ukweli, maana atafanyaje, ana ujauzito wa huyo mume aliyemuoa, na kakutana na wewe mambo yakiwa yameshaharibika,..na kuonekana kwako, kulikuwa kama ndoto, kwani ulifika mara moja na ukapotea, na kila mmoja aliyekuona alibakia akiwaza kuwa huenda sio kweli….’akasema huyo binti ingawaje hakutaka kusema hayo.

‘Sikutaka kusema hayo, ilibidi akusimulie mwenyewe, ….na kwasasa ndoa imeshafungwa, atafanyaje, na ….yaani akifikia hapo anakosa raha, na nahisi huo uja uzito ndio chanzo cha yote, lakini haya atakuelezea mwenyewe, ila nikuulize swali….’akatulia na wote wakiangaliana kwa muda, na baadaye binti akaangalia chini na kusema;

Sasa utafanyaje maana hali ndio hiyo, na mkeo ndio huyo keshafunga ndoa na mtu mwingine, na mtu mwenyewe ni rafiki yako kipenzi, ….ila, una haki ya kuivunja ndoa yao…sina uhakika na hilo sana, kwani ulitakiwa siku ile ya ndoa ukaweke pingamizi, hukufanya hivyo, …. ila ukitaka unaweza kufanya hivyo,….’akasema binti mrembo.

‘Nikitaka naweza kufanya hivyo, mimi-nikitaka au sio….je yeye asipotaka itakuwaje….?’ Akauliza swali na alipofikia hapo akawa kama anajiskia vibaya, kichwa kikawa kinamuuma,halafu kinakuwa kama kinakakamaa, hakitaki kugeuka…hali hii alishaambiwa inaweza ikawa inamtokea mara kwa mara,

'Lakini hilo ni tatizo la muda litakwisha tu...'aliambiwa na docta wake, kwahiyo yeye alichukua vidonge alivyoambiwa avituie hali kama hiyo ikitokea, akachukua kidonge komoja na kumeza na maji, akarudi pale kitandani, aliona ni bora asiwaze zaidi ni ili afanikiwe hilo ni bora atafute usingizi, maana akiendelea kuwaza ajiumiza kichwa chake, na alipojilaza tu, akapitiwa na usingizi, na mara sura ya binti mrembo ikatanda akilini mwake


*********
Lilianza kama ua, linaelea hewani, mara ua likabadilika na ndani ya lile ua akatokea binti mmoja mrembo.....
‘Unajua hii mimba ni ya kwako, nataka unioe haraka maana kuna mtu anataka kuichukua…’akasema huyo binti.

‘Ataichukuaje wakati sio mimba yake, ..wewe tulia kwanza tuhakikishe kuwa ni yangu au sio yangu…maana hata wewe huna uhakika’akasema yeye.

‘Nani kakuambia kuwa sina uhakika, Ina maana unaikataa hii mimba kuwa sio yako, kama unaikataa sema, nitampa huyo anayeitaka, au hunipendi…?’ huyo binti akasema huku analia.

‘Nani kakuambia sikupendi, nakupenda sana Maua…nakupenda sana Maua wangu…’akajikuta akisema maneno hayo mara nyingi.

‘Unaona hata jina langu unalikosea kwasababu hunipendi mimi….unampenda huyo Maua wako, mfuate huyo Maua wako

Na wakati anasema hivyo, akamuona binti mwingine kama yeye akiwa kasimama pembeni huku machozi yakimtoka, …alikuwa kafanana kila kitu na huyu anayeongea naye, ila yeye alikuwa akilia, hasemi kidogo..analia tu, akaduwaa huku akishangaa, na kusema kimoyomoyo, huyu ndiye…nani tena, sasa mbona analiai, …na kabla hajamuuliza kwanini analia, sauti ya huyo mwingine ikasema;

‘Haya mimi naondoka nampelekea huyo anayeitaka hii mimba hata kama sio ya kwake, lakini ninauhakika ananipenda, kwasababu kasema hivyo… , nimeona wewe hunipendi kabisa…..’yule binti akawa anaondoka kama anapaa vile, alipoona hivyo , akajaribu kuinuka kumzua asiondoke, na huku mara huku nyuma akasikia kama kwiki ya kilio, akaeuka kumwangalia huyo anayelia, na alipogeuza kichwa upende wa huyo anayeondoka, akawa anamuona yule….anapaa kutokomoea mbali kwa sauti akasema;

‘Nani kakuambia sikupendi , wewe ni kama yeye….jamani usiondoke ukaniacha…nakupenda Rose wangu, ua la moyo wangu, wewe umenijali wakati wa dhiki, ni rafiki kwangu wa kweli, oh…..Rose usiniache, usiniache kama alivyoniacha ndugu yako, ukiniacha nitabakia na nani mimi, ina maana nyote mumeamua kunitosa…hapana sikubali, usiondoke,…. Mau…oh, nina maana Rose, usiondoke mpenzi, ….Roseeee’ akapaza sauti ambayo ilisikika hadi nje,

Ghafla….

Oh kumbe ilikuwa ndoto akainua kichwa na kutikia tikisa macho, na akili ilipotulia akainuka pale kitandani, akiwaza kuhus hiyo ndoto, akajiuliza, hiyo ndoto ina maana gani, ni ujumbe, au kuna nini, au ni ndoto tu kwasababu alikuwa akiyawazia hayo, lakini..mbona, nahisi kuna kitu,....

Lazima kuna mtu, nahisi... kwanza hali ya ndani imebadilika, hapakuwa na harufu kama hiyo, harufu nzuri, …mmh, hiyo ni harufu ya kike…., alipotizama mlangoni, akakuta bado umefungwa, lakini alihisi kitu, akataaka kugeuza kichwa pembeni, lakini akaisita kugeuza kichwa haraka, kuna kitu kama kinamzuia, hata hivyo alihisi kuwa kuna mtu …..

Akihisi moyo ukimuenda mbio, akahisi mwili ukisismuka,…akahisi hali ilisiyo ya kawaida, lakini cha ajabu , hakuogopa, hakuhisi kabisa kuwa kuna hatari, kuwa huenda huyo aliyepo humo ndani kama yupo, au kitu kilichopo humo ndani kinaweza kuwa ni hatari….alihisi tofauti, na kwa uhakika alijua hayupo peke yake, kwanza akaangalia mlango kwa makini kuhakikisha kuwa kweli umefungwa, aliuona kweli umefungwa kama ulivyokuwa mwanzoni, sasa huyo mtu, kama ni mtu kaingiaje humu ndani….hapo sasa akaanza kuogopa,…

‘Au bado nipo kwenye ndoto nini, hapana,…’akasema , lakini cha ajabu kichwa hakitaki kugeuka ule upande anaohisi kuna mtu, au kuna kitu… akainua mkono na kupikicha macho, na wakati huo akahisi kichwa kuwa kizito, kama sio chake, hakuweza hata kukigeuza upande ule anaohisi kuna mtu,…

‘Kweli sio ndoto, ni kweli nahisi…’akajikuta akisema kwa sauti na kabla hajamaliza akasiki sauti, iliyomshitua, na ikamafanya azindukane na kujihis kuwa kweli sasa yupo macho akajinyosha kidoo huku akisikiliza hiyo sauti, ikisema;.

‘Inaonekana ulikuwa kwenye njozi ya ajabu , vipi,…upo..safi….maana nimeingia humu na kukuta ukiwa umelala, sikutaka kukuamsha, licha ya kuwa….mmh, maana ulionekana upo mbali, …na, na..oh, najisikia vibaya,…’ sauti ikawa inaongea kwa shida, na baadaye akasikia tena sauti ikisema;

‘Pole na samahani kwa kukuacha peke yako kwa siku zote hizo mbili, sio makusidio yetu…nilikuwa ….oh, nilikuwa…oh, …najisikia vibaya, …oh, …..na… na…ku..pe..nda…’ Sauti nyororo ikatinga masikioni mwake mwa mgonjwa.

Ile sauti mwanzoni ilimfanya ashikwe na hali isiyomithilika, lakini ilikuwa kama imepa uhai fulani, sasa akaweza kutikisa kichwa kilichokuwa kimeganda, sauti ambayo wakati inaongea ilikuwa kama inambembeleza aendelee kulala, na badala ya kugeuka haraka kumwangalia huyo muongeaji, alijikuta akitabasamu, kwani alikuwa kaleweshwa na hiyo sauti, …

Lakini sasa alihisi kuna tatizo, hasa pale sauti ilipofifia, akaeuka haraka kwa kujilazimisha,…oh, alichokiona kilimzindua na kumpa nguvu ya ajabu, kwani alijikuta akishikwa na mshituko, na kwanza alishikwa na bumbuazi, ….lakini ghafala akainuka haraka pale kitandani kumfuta …..

‘Mungu wangu….umepatwa na masihaba gani, …mungu wangu….’ Akamsogelea , pale alipokuwa kakaa pembeni mwa kitanda, na kabla hajamshika, akasikia akisema `na..kupenda ….sana Mhu-jaa, usinia…’ akadondoka na kama asingelikuwa kamshikilia anglidondokea sakafuni,…akajitahidi kumuinua ile alalie kitandani, na mara malango ukafunguliwa….

NB: Muda umekwisha,…..mimi naendelea tu hata kama hakuna wakusema kitu,...Tupo pamoja


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Jamani m-3 tupo wa kwetu, na asante sana kwa kuandika ingawa kwa shida, mungu awe nawe. Kisa ni kitamu sana

Anonymous said...

Jamani m-3 tupo wa kwetu, na asante sana kwa kuandika ingawa kwa shida, mungu awe nawe. Kisa ni kitamu sana