Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, February 15, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-81 hitimisho-25Mpelelezi aliupokea ujumbe wa Inspekta akiwa kajipumzika nyumbani kwake, alipousoma tu, aliinuka haraka, kwanza alichofanya ni kuwasilina na vijana wake anaowaamini kuhakikisha kuwa wamefika kwenye hilo jengo aliloelekezwa na kuwaamrisha kuwa wahakikisha kuwa hakuna mtu anayetoka, na akitoka mtu aweke chini yaulinzi mpaka atakapofika, ila alwiaomba wawe makini, kwani kuna mtu yumo humo dani ambaye ni hatari. Baada ya kutoa maagizo hayo, akachukua pikipoki yake moja kwa moja kwa mkuu wake ambaye kwa muda huo alijua yupo ofisini.

‘Nahitaji kibali, kwani huyu mtu ni hatari, ni vyema kama ikishindikana tutumie nguvu, …’akawa anjisema huku akiwa kweney wmendo mkali.

Alipokaribia kwenye jengo lao maalumu ambapo kuna ofisi zao, akaiegesha pikipiki yake, mbali kidogo na hilo jengo, hakutaka mtu ajue kuwa anaelekea kwenye hilo jengo, akazuga zuga, na baadaye akaharakisha na kuingia ndani ya hilo jengo kwa uficho;

‘Sasa hivi kila hatua natakwia kuwa makini zaidi, maana hata humu ndani siwaamini mia kwa mia…’akajisema huku akipanda ngazi kuelekea ofisi za mkuu wake, na ilibidi kukutana na watu wa usalama, hapo alikuwa hana ujanja, lakini hata hivyo kwa vile walimuamini, hawakumtilia mashaka.
Haraka akaingi ndani hadi ofisi zao maalumu, na alipofika ndani akawa sasa anaelekea kwenye ofisi ya mkuu wao huyo na akausogelea mlango, ulikuwa nusu wazi, kitu ambacho sio kawaida yake, akasogea kwa tahadhari ,kwani kwa muda ule hakuwa na silaha, silaha aliacha kwa watu wa usala, kwani humo huruhusiwi kuingia na silaha ya aina yoyote, …

Mara akasikia mkuu wake akiongea , ilionyesha kuwa alikuwa ndio katoka nje, kutokana na maongezi yake…Mpelelezi yule akaona asubiri kwa nje, kani mkuu anaongea na simu, na huenda hakuhitajika kuiskia. Lakini masikio hayana pazia.

‘Nilikuwa natoka ndio nikapata hii simu yako kuna nini huko, maana nina haraka kidogo,…?’ Akasikia mkuu wake akiuliza.

‘Unasema una uhakika amekugundua, amekugunduaje, amekugundua kwa sura ipi, …hapo sasa lazima kuna kitu ambacho amekigundua kutoka kwako ambacho hujirudia rudia , au ndio huo mwendo wako wa kivita, …’akatulia

Halafu mkuu huyo akasema, `sasa hapo umejichora, kwasababu huyo binti ni mjanja, …umeishi naye muda mrefu, ulikuwa hujamgundua tu, sasa huyo ni nyoka, na dawa na yoka ni kumuua, …usifikiri mara mbili, tafuta mwanya muondoe, halafu badilika haraka na potea kabisa humo ndani, mimi…nitajua la kufanya na hawa watu wangu…au unataka kufanyaje …’akasikia mkuu wake akiuliza.

Mpelelezi alivutika sana na hayo mazungumzo, na alipounganisha akaona hayo wanayoongea na mwenzake lazima yanawahusu Rose na familia yake, akajaribu kusikiliza kwa makini huku akiwa chukua tahadhari nyingine,…akaandika taarifa kwenye simu yake kwa kijana wa karibu kuwa ahakikishe familia iliyopo ndani ya hilo jengo ipo salama, na akazima simu…

‘Bado upo ndani ya hilo jengo la biashara, hujatoka tu,….sasa naona unataka kujichimbia kaburi, …unasema na wao wapo humo humo familia nzima,….mbona sijapata taarifa yoyote, …ndio maana nasema huyo binti hana uhakika, ndio maana hajatoa taarifa, na kama unahisi wamekutilia mashaka, dawa ni moja tu, hakikisha unawaziba mdomo…’akasikia mkuu wake akiongea.

‘Kwanini uogope nchi hii ipo vitani, likilipuka bomu hapo kila watu hawatashangaa, …kwasababu utawezaje kuwaziba mdomo wote kwa pamoja, lakini huyo mmoja ndiye kikwazo hawa wengine ni wakuja tu,…ndio na mama yao….’akakohoa kidogo.

‘Hayo ammbo ya kifamilia tutayamaliza, kwani hukuongea na yule jamaa wako wakaribu, maana naye anatakiwa kuzibwa mdomo, na hilo nitalifanya mimi mwenyewe…kwanini unasema hivyo, huyo ni kikwaza, hilo niachie mwenyewe….kwanini….hapana hapo hatutaelewana, kwani hayo mambo binafsi hayanihusu, sasa ….tusibishane mimi ni bosi wako najua nini ninachokifanya…’akasikia mkuu huyo akifoka.

‘Kwani ndugu yakko huyo, ulishakataa mapema, sasa nini unataka, usione Huruma kwa kipindi kama hiki, mimi nimeshaagiza wale wote ambao wanaonekana kutuweka roho juu tunawamaliza, ni kipndi cha kusafaisha njia maana mambo yameshakamilika iliyobakia ni kuhakikihsa hatuishi kwa mashaka…’akasema huyo mkuu.

‘Huku kikwazo ni mpelelezi wangu, huyu nampa siku moja, kesho utasiki kwenye vyombo vya habari, nimeshamwekea mtego, sikutaka kumharakisha lakini nyendo zake zinaonyesha kuwa atajua mengi, na mwisho wa siku atagundua shina letu, unajua tumebakiwa mimi na wewe wengine wameshapotea, na hili ni muhmu kwetu, hata mambo yakiwa mazuri tutakuwa hatuna vipingamizi…kwahiyo hawo unawaona ni vipingazmizi maliza…hiyo ni amri…’akasema huku akitembea tembea humo ndani.

‘Nishakuambia kila ninayemshuku nimetoa amri kuondoa , mimi mwenyewe nimetokea sehemu kuondoa kikwazo kimoja…hicho kikwazo kilishanigundua,na wewe unasema nisikiondoea umeshachelewa bwana mdogo, ndio ….siwezi kukuambai ni nani…na katika hali kama hii hata kama kikwazo ni ndugu ni heri kukiondoa….’akasema kwa haraka haraka.

‘Nipo ofisini, muda kama huu sina wasiwasi, Jumapili ya leo imeniendea vyema kabisa, kwani kuna mtu alikuwa akinisumbua kichwa, sasa nipo huru, amebakia huyu mtu wangu wa karibu, ana mumkari na kazi, sasa kazi hiyo ataifanyi kuzimu…nitammaliza mwenyewe, najua leo aanweza kufika hapa, kama unavyosema kuwa hiyo familia imo humo, na…lazima kuna jambo litamfanay aje huku, ….hawa watu wangu najua jinsi gani ya kuwamaliza sitaki msaada, wewe maliza wa kwako…’akasema na kukaa kimiya kwa muda.

‘Hakuna kitu kama hicho, kwasababu kama taarifa zingelikuwa hivyo, huyo jamaa yangu angelikwua keshafika, hakuna lolote limefikishwa hapa, kwahiyo kama huyo binti kakushuku, hajatoa taarifa, na akitoa taarifa zitafika kwa kijana wangu, huyu mpelelezi, na huyu mpelelezi hawezi kufanya kazi bila kuniona mimi…na ndiye namhesibia masaa, akifiak tu, ninaye….’akasema na kucheka….halafu akatulia.

********

Mpelelezi hakuamini hayoa liyoyasikia, kumbe alikuwa anakuja kukutana na kifo chake mwenyewe, akageuka haraka na kutoka nje ya jengo, hakutaka kusubiri tena, alipofika kwenye pikipiki yake akatizama kushoto na kulia kuhakikisha kuwa hakuna mtu anyemfuata, alipoona hakuna hatari, akaliondoa pikipkipi lake kwa mwendo wa kasi na kuingia barabarani.

Aliendesha haraka hadi kwenye jengo la biashara alipofika pale akakutana na vijana wake, hapo akachuku tahadhari kwani kama alivyosikia kutoka kwa mkuu wake, humo katika hawo vijana kuna uwezekano mkubwa akawepo mtu wake, sasa afanye nini. Akamsogelea kijana mmojawapo anayemuamini na kumuuliza

‘Vipi kuna lolote, hamjamuona mtu yoyote akitoka….?’ Akauliza

‘Eti, kuna nini, … mauaji, nani kauliwa tena…ooh?’ akajikuta akitikisa kichwa na kukumbuka yale maongezi ya mkuu wake, hakutaka kudadisi mengi, akaingia ndani ya jengo na kukuta kikosi maalumu kikiwa kwenye kazi zao, alisogea hadi kwenye ofisi na kuwaona watu wa usalama wakifanya kazi zao, wakampa heshima yake, naye akaingia kazini.

‘Hebu niambie kumetokea nini, na ile familia iliyokuwa humo ndani ipo wapi?’ akauliza kwa haraka haraka.

‘Inavyoonyesha ni moja ya mauaji ya hili kundi, na mtu huyu hakuzaniwa kabisa kuhusika, na hata kumbukumbu zetu hazimuhusishi, lakini hali ilivyo, inaonekana kama waanzungukana wenyewe kwa wenyewe, …’akasema huyo jamaa, na mpelelezi akamwanglia kwa makini, na kumwekea alama akilini.

‘Na familia ipo wapi….?’ Akauliza

‘Famili tumeiweka chumba kingine, hatujataka kuiambai lolote kwanza, maana inaweza ikavuruga uchunguzi,..’akasema huyo mtu.

‘Nataka nionane nayo haraka hasa wale mabinti wawili…’akasema Mpelelezi.

‘Wapo chumba kile pale, na naomba usiwape taarifa kwanza, maana tunaogopa kelele kwa sasa, na jamaa yetu nafikiri bado yupo ndani…’akasema huyo jamaa, na kumfanya mpelelezii ashituke kwani hakuwahi kumuhusisha huyo jamaa kwenye kampeni ya kumkamata mtu wao wanayemtafuta.

‘Una uhakika na hilo, kwani nani kakuambia yumo humo ndani…?’ akauliza mpelelezi.

‘Kwa taarifa tulizozipata hakuna mtu aliyetoka, na kama akitoka tungelimuona , ngoja nimaliziea kuangalia huko ndani kama kuna lolote la muhimu…’akasema huyo jamaa akionyesha kukwepa kuulizwa zaidi.

Mpelelezi huyo akaona sasa humo ndani kazi itakuwa ngumu, cha muhimu ni kuhakikisha kuwa hiyo familia ipo salama, na mambo ya kumkamata huyo jamaa yataenda kinamna nyingine, kwasababu sasa anshindwa amuamini nai tena, akasogea pembeni na kumtumia ujumbe inspekta;

‘Naona bwawa lote lina ruba, hata papa naye yumo, sina wa kumwamini tena,…’

Baadaye ukaja ujumbe,; `Nilijua, Cha muhimu kwa sasa hakikisha usalama wa hiyo familia, …’
Na hapo hapo akaelekea kwenye chumba kilichowekwa hiyo familia na kuwaambia kwa haraka;

‘Jamani humu ndani hakuna kunaonekana kuna kazi maalumu na watu wa usalama ni vyema tukaondoka na kuwaachia wao wafanye kazi yao…twendeni huku…’akasema huku akiwaelekeza nje.

‘Tunataka kujua kama mume wangu yumo humo ndani au la….?’ Akauliza mama

‘Utaambiwa baadaye, maana ndio nafika, ninachotaka kufanya nikuhakikihsa nyie mpo kwenye mahali pa usalama,…na yule binti mwingine yupo wapi?’ akauliza.

‘Rose, alikuwa ndani nafikiri atakuwa anaongea na baba yake, na Maua kakutwa akdondoka ndani kama walivyotumabia hawo maaskari, yupo anaaptiwa huduma ya kwanza, hatujaruhusiwa kumuona…’akasema shangazi ambaye alikuwa kachanagnyikiwa, alikuwa kila mara akilaani kitendo cha bint yake huyo kumkaidi na kuingia humo ndani ya jengo.

‘Sasa ni vyema tutakaondoak humu kabisa, maana unajua mambo haya ya hawa watu, kutokana na watu wa usalama kunawezekana kukawa na hawo watu humu ndani na waanweza kufanya lolote baya, ni vyema tukachuku atahadhari….’akasema mpelelezi.

‘Kwanza tunataka tuwaone watoto wetu, maana mnatuchanganya..’akasema mama kwa hasira

‘Mtoto weny huyu mmoja keshazindukana, mtaondoka naye, lakini Rose hajaonekana…’akaropoka askari mmoja, na kumfanya mpelelezi amwangalie kwa hasira.

Mara akapata ujumbe toka kwa Inspekta ujumbe ulikuwa ukimwambia kuwa huyo binti mwingine yupo ndani kwenye nyumba vya ndani, kuna meseji imemfikia kuwa yupo kwenye hatari, kwahiyo wafanye kila njia kuhakikisha kuwa wamemuokoa….

Alipomaliza kusoma hiyo meseji, akaanza kazi, akijua sasa hakuna jinsi ilimradi familia imeondolewa humo ndani , kilichobakia ni kumuokoa huyo binti ambaye ni muhimu sana kwake, bila yeye hataweza kumgundua huyo jamaa hatari, licha ya kuwa kubwa lao keshaligundua, lakini huyo aliyepo humo ndani ni hatari zaidi.

Alichofanya kwa haraka ni kuwapanga vijana wake akiangalia nani anayemuamini, kwa kubahatisha tu na yeye mwenyewe akajitosa ndani kwenye hizo ofisi, bastola mkononi, alianza kufungua mlango mmoja mmoja kwa kutumia funguo zake maalumu …..

NB Nimeona nitoe sehemu hii ndogo kwa haraka, maana mambo yameiva, tusubiri sehemu ijayo, munu akipenda. Tupo Pamoja


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Sehemu haijatendewa haki hata ahrante hakuna. Ahsante mkuu