Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, February 14, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-80 hitimisho-24



Rose alikuwa wa kwanza kuingia ofisi ya baba yake, na kuwaacha wenzake wakiwa wamesimama nje, alifungua ule mlango wa mkuu wa jengo, na kuingia kwenye sehemu kubwa ya mapokezi , hakukuwa na watu wa mapokezi, kwani siku hiyo ilikuwa ni ya Jumapili, …akasogea upande wa pili ndipo kwenye ofisi za baba yake, akausogela mlano na kuufungua , na kukuta upo wazi, akawa na uhakika kuwa kuna mtu ndani hata kama sio baba yake lakini kuna mtu.

Aliwaza siku ya jumapili atakuwepo nani, kama sio baba yake, haraka akachepuka na kuingia ndani, kwenye sehemu ndogo ya mapokezi, akasimama pale kwa muda, na mlango ukajifunga kwa nyuma, kwani ule mlango hujifunga kwa haraka, vinginevyo uushikilie, …na kabla hajaangaza macho vyema, mlango wa ofisi ya baba yake ukafunguliwa, akasimama kuangalia ni nani, ni baba yake au ni mtu gani..?

Rose alikuwa kaizoea hiyo ofisi kabla, kipindi cha mwanzo alikuwa akifika hapo mara kwa mara, hasa kipindi akiwa shule, alikuwa karibu sana na baba yake, kwahiyo alikuwa akimtembelea mara kwa mara ofisi kwake, a wakati mwingine alikuwa akifika kujisomea hapo, na baadaye yalipoanza kutokea matatizo akaacha kabisa kufika hapo ofisini, hadi leo hii, lakini kila kona ya hiyo ofisi alikuwa akiijua.

Aliyetoka pale hakuwa baba yake, alikuwa mtu mgeni kabisa katika macho yake, akamtizama kwa makini, lakini inavyoonekana yule mtu hakutaka aonekane usoni, maana alipoangalia mlangoni na kumuona Rose kasimama kwanza alificha kitu alichokuwa kakishika mkononi , Rose hakuweza kukiona ni kitu gani, na mkono ulipotoka mfukoni, ukawa umeshikilia miwani ya jua, hakuivaa kwanza alikuwa akiitikisa tikisa mkononi, huku akiangalia saa ya mkononi.

Rose alikuwa na uhakika kuwa hiyo miwani siyo aliyokuwa kaishikilia mwanzoni, kuna kitu kingine alikuwa nacho mkononi kabla, lakini kwa haraka alikificha kwenye mfuko wa koti, na alifanya tendo hilo kwa haraka, pale alimpomuona yeye kasimama pale mlangoni, ….na kutoa hiyo miwani kujifanya kuwa ndiyo aliyokuwa kaishikilia mwanzoni.

Rose aliingiwa na wasiwasi, kwanza huyo mtu katokea ofisini kwa baba yake, na kutoka kwake kunaonyesha ni kwa haraharaka, na pili, mtu huyo anaoenekana kabisa ni mgeni, hajawahi kumuona kwenye ofisi hiyo kabla, inawezekana walikuja kuajiriwa watu wengine, kwani ni muda hajafika hapo, lakini akili ya Rose lihisi kuwa kuna jambo lisilo la kawaida, ukizingatia viendo alivyovifanya huyo mtu kwa harakaharaka, vile vitendo vilimtia wasiwasi, akawa na shauku ya kujua usalama wa baba yake. Hakutaka kumjua yule mtu kwanza alichotaka yeye ni kukimbilia huko ofisini, aangalie usalama wa baba yake.

Akaanza kuongeza mwendo, kuelekea kwenye mlango wa ofisi ya baba yake, na yule mtu aliyetoka pale, alipoona Rose anakuja uelekeo wa mlango wa ofisi kwanza alivaa ile miwani ya jua haraka, halafu akaanza kutembea kwa haraka, kuelekea kushoto kama vile anamkwepa Rose apite, wasikutane ana kwa nana, na kuelekea pembeni mwa ile ofisi ambapo huwekwa magazeti, akainama na kuchukua gazeti moja wapo, akachukua simu na akawa kama anataka kumpigia mtu, huku analiangalia lile gazeti, kama anasoma, akageuza kichwa kwa haraka kumtizama Rose, na alipogundua kuwa Rose anamtizama, akaondoka kwa haraka na kuelekea kwenye mlango na kutoka nje huku akivaa ile miwani ya jua.

Rose akamfuata kwa nyuma, na alipofika pale mapokezi yule jamaa hakutoka nje kabisa, alielekea kwenye mlango mwingine ambao unatokea kwenye ofisi nyingine maana jengo hilo lina ofisi nyingi, ila mlango wa kutokea nje ni mmoja. Kwahiyo kwa vyovyote akitaka kutoka ni lazima atapita hapo, Rose akaona amsubiri, ili amuulize vyema yeye ni nani, lakini kwa wakati huo huo alitaka kumuona baba yake kama yupo pale ofisini, akawa njia panda, aende kumuona baba yake amkose huyo mtu, au amsubiri huyo mtu, na hajui usalama wa baba yake….na ghafla kitu kikamjia akilini.

Kuna kitu kama mshituko ulipita akilini mwa Rose, mara akahisi kichefuchefu, na kizungu zungu, akasimama na kujiweka imara ili asije akaanguka, na wakati huo huo macho yake yalikuwa hayabanduki kule alipoelekea yule mtu, akahisi jambo, akili yake ikaanza kufanya kazi kwa haraka;

Ule muondoka, …na ingawaje alivaa miwani haraka, lakini akayakumbuka yale macho, ….akakumbuka kitu, huyu mtu , atakuwa yule….haraka haraka mawazo yakamjia. Kwanza alikumbuka kuwa simu yake ilikuwa imewekezwa sehemu ya ujumbe wa haraka kwa Inspekta, kwahiyo alichofanya ni kuishika simu yake, na kubonyeza namba mbili, na hapo alijua itakuwa imeshafunguka kwenye namba ya Inspekta, akaibonyesha mara mbili, akajua hapo ishafunguka sehemu ya ujumbe, na haraka haraka mkono wake ukaaandika ujumbe…

‘Inspekta, nahisi nimekutana na yule mtu, kwenye ofisi ya baba, hajatoka bado….’akatupa jicho haraka kwenye simu kuhakikisha na kubonyeza namba mbili, hii ndio namba yenye namba ya simu ya Inspekta na haraka akaituma ule ujumbe, na huku bado akiangalia pale mlangoni alipopitia yule mtu, akijua kwa vyovyote atatoka tena, hakutaka kugeuka sehemu nyingine, hakutaka kabisa kumkosa, alitaka kuthibitisha kuwa kweli ni yule yule, ….

Ghafla ujumbe ukaita kwenye simu ya Rose, Rose akaiinua simu yake kwa haraka akausoma huo ujumbe uliosema;

‘Kama hajatoka hakikisha unasimama mlangoni, ..na usifanye lolote, huyo mtu ni hatari, ninawasiliana na watu maalumu…’

Rose akasogea kwenye kiti kilichopo mlangoni na kukaa, akawa macho yake hayabanduki kule alikoingilia yule mtu, na alikuwa na uhakika kuwa hataweza kutoka mpaka apitie pale mlangoni, lakini hakuamini, hivyo, alihsi kuwa anaweza akatoka na mtu mwingine, au akatoka kwa haraka bila ya yeye kumuona vyema,….hata pale akijua kuwa mlango wa kutoka ni huo mmoja, na madirisha ya ofisi zote humo ndani yamejengewa nondo, na viyoo, huwezi kurukia dirishani.

Rose akiwa katulia akili yake ilijaribu kumkumbuka vyema huyo mtu, kitu cha kushangaza ni kuwa kila, akikutana na huyu mtu, kama ndio yeye kweli, kwanza anajisikia vibaya, halafu moyo wake unamwenda mbio, lakini hilo aliliona labda ni sababu ya ujauzito alionao. Lakini kitu kikubwa ambacho kinamfanya amkubuke huyu mtu ni jinsi anavyotembea,…

Huyu mtu anatembea kama askari anayetembea gwaride la mwendo wa pole, lakini hutembea kwa haraharaha, kama ingelikuwa ni kwa askari ingelikuwa ni mwendo wa pole, lakini kwa huyu jamaa sivyo, yeye miguu anayoitembeza hivyo lakini anatembea kwa haraka haraka,…anahakikisha anakwenda mwendo ulionyooka, kana kwamba hataki kugusa sehemu nyingine, akapoteza ushahidi, kwahiyo mwendo wa sehemu ya mguu mmoja, na ni mwendo unaofurahisha kwa Rose, unaonyesha kuwa huyo mtu alijizoesha kutembea hivyo tangia akiwa mdogo, kwani sio rahisi kwa mtu wa kawaida kutembea kwa mwendo huo kwa haraka haraka kiasi hicho.

Akiwa anawaza hili akakumbuka kitu, …, siku moja, alimuona jamaa mmoja…akitembea hivyo….oooh, ghafla akasimama ka mtu aliyeona kituu cha ajabu, …alikuwa kakumbuka kitu, mbona wazo hili halikuwepo toka awali, akainuka pale alipokuwa kakaa na kukimbilia pale kwenye mlango alipoingilia yule mtu, akaufungua, …hakumuona yule mtu, kulikuwa kimiya, na kwa vile ni jumapili , ofisi nyingi zilikuwa hazina mtu, na akajaribu kuangalia milango ya zile ofisi zilivyojipanga na majina ya wamiliki, lakini hakukumbuka kumuona huyo mtu kabla kuwa huenda ni mmoja wa wamiliki wa ofisi yoyote pale..

Hamu ikamjia, kukagua kila ofisi, akaingia huku akiwaza nini atasema akikutana na yule mtu tena, akajaribu mlango wa kwanza, ulikuwa umefungwa, wa pili, halikadhalika, wa tau, nne….mara simu yake ikamuumbua, akaikata bila kuangalia, na kabla hajashika kitasa cha mlango mwingine, simu ikaanza kuita tena, akaangalia akakuta ni meseji ya Inspekta imeingia na kwa haraka akaisoma, ilisema;

‘Kuna watu wanakuja, usifanya jambo jingine lolote, wala usiongee naye, au kuonyesha dalili kuwa umemtambua, huyo mtu ni hatari….’Rose akashituka alipousoma ule ujumbe, na haraka akageuka na kurudi kule alipokuwa mwanzoni, huku akiwaza;

‘Mbona sikuwa na wazo hilo kabla, ….inawezekana, …hapana, mbona haiji akilini, hivi kweli, kwanini wazo hili halikuwepo akilini, hapana, akaitizama simu yake, akataka kutuma ujumbe, lakini akasita, taratibu akarudi pale alipokuwa amekaa, akifuata maagizo ya inspekta na kukumbuka yale maneno, na usifanye lolote, huyo mtu ni hatari….

Kila alivyotafakari ndivyo alivyoingiwa na hamu ya kumuona tena yule mtu, kwani kama ni yeye, alikuwa na hamu sana ya kuongea naye, alikuwa na maswali mengi ya kumuuliza, kwanini…..na ghafla akainuka akitaka kurudi kule kwenye zile ofisi kuendelea kukagua zile ofisi moja bada ya nyingine..na kabla hajainua mguu, mara mlango mkubwa wa nje ukafunguka, akatupa jicho mara moja kuangalia ni nani, na alipomuona kuwa ni ndugu yake, hakusema kitu, yeye akaendelea kutizama ule mlango wake,na hukuu akijisema kimoyomoyo, sasa ni muda muafaka wa kukagua hizo ofisi, ni lazima amuone tena huyu jamaa, haiwezekani, lakini vipi kuhusu baba yake….

Alipomuwaza baba yake akamgukiwa Maua ….

***********

Wakati huo huo wenzake walikuwa nje, walikuwa wakimsubiri Rose awape taarifa kuwa baba yupo ndani au hayupo, na walipoona anachelewa kutoka, wakaona na wao waingie ndani, …lakini hawakuingi a wote kwa pamoja, kwani shangazi na mama walikuwa wamesimama mbali kidogo na jengo la ofisi, wakiteta, na baadaye mama akijaribu kumuonyesha shangazi mazingira ya ile ofisi kwa nje, na lengo ni kupoteza muda, ili binti yao aingie na kuwapa taarifa yoyote.

‘Unasema hukumpigia mume wako kuwa tunakuja na ndege ya pili..?’ akauliza shanagazi

‘Hapana kulikuwa hakuna muda huo, cha muhimu ni kuwa tumeshafika…naona sasa tuingie humo ofisini, sizani kama kuna shida, mimi namjua vyema mume wangu, hakuna shida kabia….’akasema mama

‘Unajua wanaume ni watu wa ajabu, nimejifunza hilo, hasa wanapokuwa kwenye ofisi zao, unaweza ukaingia ghafla bila hodi, ukakuta kakumbatiana na katibu muhutasi wake,…na hata kama mume wako hana tabia hiyo, lakini sisi wenyewe, tunapenda kujizalilisha,….na kama ukiwaona hivyo utafikiria mume wako ana tabia chafu, kumbe…’ akatulia kidogo akimwangalia Maua anavyohangaika, halafu akasema;

‘Matokeo yake ni nini kama sio kupatwa na ugonjwa wa moyo bure, huku wenzako waanfurahia, ya nini yote hayo….’akasema shangazi.

‘Kama ikitokea hivyo, niingie ofisini nimkute huyo, …binti, au mwanamke gani sijui, nitahakikisha huyo katibu muhutasi hana kichwa, ….tena unanitia wasiwasi, twendeni ndani, tunasubiri nini hapa,. Na huyu Rose anakawia sijui anaonea nini na baba yake, …lakini hata hivyo mume wangu namuamini, hana tabia ya uzinzi, labda ulevi….’akasema mama.

‘Subiri kidogo, usiwe na pupa, kama ni wivu utulize kidogo, …unasema ni mlevi, oooh, na ulevi huendani sana na uzinzi, lakini tuyaache hayo, ngoja tusubiri huyo binti akitoka ndio tuingie, maana sio vyema kuingia kwenye ofisi za watu bila taarifa, ..labda Rose, kakuta wapo kwenye mkutano, ndio maana anasubiri, kwani kama kungekuwa na tatizo angetuambia hata kwa simu…’ Akasema shangazi huku mara kwa mara akimwangalia Maua kwa kujiiba.

‘Kwani mumeo alikuwa akijua kuwa tutafika sa hizi…?’ ghafla akauliza shangazi tena.

‘Alikuwa anajua kuwa tutafika kwa ndege ya mwazo, na tulipobadilisha ndege hatukuwahi kumpa taarifa, na huenda alipooona hatukufika na ndege ya mwanzo, atakuwa kafikiria kuwa tumeahirisha safari hadi kesho…’akasema mama.

‘Hawezi kufikiria hivyo angelikupigia simu, kukuulizia imekuwaje, lakini hata kama kakupigia, ungeliipataje, na wakati tulikuwa ndani ya ndege….hakukuta simu iliyopigwa kutoka kwake…?’ akauliza shangazi, na kumgeukia Maua, alipomuona katulia kidogo, akamgeukia wifi yake na kumuuliza maswali ya kupoteza muda;

‘Hili jengo mumekodisha, inaonekana kuna ofisi nyingi humo ndani, naona mlango wa kutokea ni mmoja tu huu wa mbele, au kuna mlango mwingine kwa nyuma…?’ akauliza mama.

‘Hakuna mlango mwingine wa kutokea kwa nyuma, ni huo wa mbele tu, kwahiyo hata mtu akitokea ndani utamuona tu, na leo sio siku ya kazi, sizani kama mume wanu atakuwa na katibu muhutasi ….’ Akasema mama kwa shauku.

‘Wivu huo….’akasema shangazi na kucheka, na kumfanya Maua ageuke kuwaangalia.
Mara mama akaangalia simu yake ailiyokuwa ikiita, akagundua kuwa ni mmoja wa wafanyabiashara wenzake akaanza kuongea na huyo mfanya biashara, na kumuacha shangazi akiangaza macho huku na kule, na alipomtupia macho tena Maua, akagundua kuwa hayupo kwenye hali nzuri, akataka kumsogelea kumuuliza , lakini akasita na kusimama pale alipo. Na alipomuona akiinua mguu kuelekea kule mlangoni, akamfuata nyuma…

*****

Maua pale aliposimama alihisi kitu, mwili ulikuwa haupo vyema, akawa anajisikia vibaya, na hali ile ikampa ishara kuwa huenda mwenzake ndani hayupo vyema, akataka kumwambia shangazi, lakini aliwaona wakiwa kwenye mazunguzmo yao, na hakupenda kuwaingilia au hata kuyasikiliza, akawa anahesabu muda tu, huku hali ikiendelea kuwa sio nzuri. Akasema kimoyomoyo;

‘Nahisi Rose ana tatizo huko ndani, lakini sasa nifanyeje….’akageuka kumwangalia shangazi na kumuonyeshea ishara ya saa. Shangazi naye akamuonyesha ishara ya kuwa atulie asiende popote, …..lakini kadri muda ulivyokwenda, subira ya Maua ikaanza kutembea mdogo mdogo kuelekea mlangoni, na alipogeuka akamuona shangazi akimjia kwa nyuma, yeye hakumsubiri tena akausogelea mlango na kuanza kuufungua,

‘Wewe mbona una kimbelembele, hujui hizi ni ofisi za watu utaingia utolewe mkuku, achia wenyeji waingie kwanza….’Maua alisikia shngazi akiongea nyuma yake , lakini alishachelewa, Maua alishafungua mlango na kuingia ndani, maana hali aliyokuwa akiisikia alijua kabisa kuna tatizo.

Tangu akutane na ndugu yake huyo alishagundua jambo kuwa ndugu yake akiwa na jambo, au tatizo nay eye huhisi, na kama ni maumivu na yeye atayasikia, na mra nyingi imekuwa hivyo, mwenzake akisema anajisikia vibaya na yeye anajihisi hivyo hivyo, kwahiyo alikuwa na shauku sana ya kuingia ndani amuone ndugu yake hata pale shangazi yake alipojaribu kumzuia hakujali kabisa.

Maua alipoingia ndani na kumkuta Rose kakaa kwenye kiti, karibu na mlano, akasita kwanza kumsemesha, alimtizama kwa makini, na hali aliyomuona nayo, alihisi ana jambo,alishangaa kumuona kakodoa macho kuangalia kwenye mlango uliopo mbele yake, akamsogelea haraka na kuuliza;

‘Vipi upo safi kweli wewe….?’ Lilikuwa swali la kwanza alilouliza Maua, na Rose akatikisa kichwa kukubali bila kusema kitu, alichofanya ni kuonyesha kwa Maua, ishara ambayo mwanzoni ilimtatanisha Maua, lakini alipotuliza mawazo, ikawa kama waanonea wote akilini, aliona Rose, akionyesha mkono wake na kumuelekeza mlango uliopo upande mwingine, sio ule ambao Rose muda wote walikuwa akiuangalia, na Maua bila kusema kitu, akaugeukia.

Halafu akauangalia ule mlango kwa muda kuwa una nini, na baadaye akamgeukia, Rose , alijua kuwa Rose anamuelekeza aende kwenye huo mlango , lakini alitaka uhakika, akamwangalia Rose kwa muda, na Rose akawa anamuonyeseha kwa ishara Maua naye, akaugeukia ule mlango na kuanza kuufuata.

Bila kusita Maua akaufikia ule mlango na alipofika akasimama kwanza kwa muda, halafu akagonga mara tatu, akaona kimiya, akamgeuka Rose, akamwangalia, Rose akamuonyeshea ishara kuwa aufungue, na Maua akafanya hivyo, akaufungua, na ulipokuwa wazi kiasi , aakaingia ndani, na Rose naye akaanza uondoka kuelekea kweney hizo hizo ofisi za ndani. Maua hakugeuka nyuma kuangalia kule alipokuwepo Rose, na alipogeuka akakuta mlango umeshajifunga, hamuoni Rose tena wa kumuelekeza.

Akiwa ndani ya hiyo ofisi akatizama huku na kule, akagundua kuwa hapo ni sehemu ya mapokezi, ni sehemu ndogo tu, lakini ilijitosheleza kama sehemu ya mapokezi, na alipoangalia vyema kwenye chumba kilichojengwa kwa mbao na kua dirisha, akakuta amandishi yameandikwa `mapokez, uliza hapa’ lakini kulikuwa hakuna mtu, kupo kimiya kabisa, akageuka upande mwingine, akaona mlango, umeandikwa `mkurugenzi mkuu, ..’ na chini yake akaona jina limeandikwa `Tajiri mzungu….’ Akatatikisa kichwa kuwa hapo ndipo anatakiwa kuingia, akausogelea mlango na alipoufikia akasita kidogo.

Akagonga mara moja, akaona kimiya, akagona tena, hakusikia kitu, akageuka, kama vile akikumbuak kuwa atamuona Rose amuelekeze, lakini alichoona ni mlango ulifungwa, na kabla hajaeuza kichwa vyema kuangalia hapo mlangoni alipokuwa akigonga, akashika kitasa na kukizungusha, malango ukafunguka.

Maua akahisi mwili ukimsisimuka, …akaachia ule mlango, na ile milango ilivyo, ukiuachia uanajifunga, akajiuliza kwanini anajihis hivyo, au ndugu yake aligundua kitu ndio maana akawa vile, na huenda alichogundua ni kibaya, na kashindwa kuamini, ndio maana kamtuma yeye ili aje kuthibitisha,akasema kijasiri, kwanini apoteze muda kujiuliza , na wakati ushahid upo, akashika kitasa na kukizungusha, na akausukuma mlango kwa nguvu.

‘Hodi …..’akasema.

Hakusikia jibu, akatizama ndani, na macho yake yalipotia kwenye meza, na kuangalai kwenye kiti, hakupenda kuangalia tena, alijikuta mwiliukiisha nguvu, na mara akahisi vinyota, na kabla hajadondoka, akapanua mdomo, na kilichosikika ni yowe…..
Je kuna nini, ….tuwepo pamoja kwenye sehmu ijayo.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Rachel Siwa said...

Duuhh ndugu wa mimi yaani sijui niseje,yaani kazi yako ni yako tuu,Mungu azidi kukubariki sana.Pamoja sana ndugu yangu!!

Anonymous said...

comprar cialis precio cialis