Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, February 7, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-79 hitimisho-23‘Haina haja ya kushika hiyo bastola, kwanza wewe huna utaalamu nayo, waachie wenye kazi hiyo waifanye, …irudishe kwenye droo, tuna mambo muhimu ya kuongea, na bila kupata majibiu ya uhakika, udugu utavunjika….natumai mpaka hapo umenielewa….’ikasikia sauti hiyo ikipenya kichwani kama mwangwi fulani, mwili ulikuwa umekwisha nguvu kiajabu, na alijua nini maana ya ile hali ikitokea, akaangalia pembeni kule ukutani, alichoona ni meno yakioneysha kucheka kwa kebehi.

‘Huko ukutani uanaangalia nini usiniambie ulikuwa na mizimu yako, maana nyie watu washirikina hamuishi vituko, sikuja hapa kwa mambo ya kishirikiana sisi ni wanasatansi kamili….’yula jamaa aksema

‘Usijifanya kuwa hujui mambo hayo wakati hata wewe ulikuwa ukishiriki katika mambo hayo…’akasema Tajiri na mara kitu kikamtuma kuangalia ukutani na alichoona sasa hivi ni kidole kikiwa kimekwekwa mdomoni kikiashiria kuwa anaymaze asiongee hilo alilotaka kuongea.


‘Mimi, nani kakudanganya, hayo niliyakataa kata kata, na ndich kilichonifanya nipotee kwenye familia yetu iliyojaa ushirikina, ….’akasema huyo mtu/

‘Unajidanganya bure, unamkumbua mwali wako ni nani…?’ akauliza Tajiri.

‘Mwalimu wangu..,!’kasema kwa mshangao halafu aakuliza `mwalmu wangu anahusikaje na ushirikina huo..?’ akauliza kwa mshangao.

‘Basi mwalimu wako ungelimjua vyema, ungelijua kuwa na wewe ulikuwa katika njia ile ile niliyokuwa mimi, njia ya kwuatumikia hawo mizimu , njia ambayo mwisho wa siku ni kuangamia tu, mimi sijaona faida yake….maana wanachotaka wao ni ufe ukajiunge na kundi lao, sioni jingine…’akasema Tajiri.

‘Hilo silo lililonileta hapa, nimekuja hapa na maswala ya mali yangu, haki yangu ambayo umemua kuigawa kwa eti inayoitwa familia yako, hvi kaka huoni aibu, kwanini umatekwa na yule mwanamke na kumuona bora kuliko ndugu yako, hadi unachukua mali ya ndugu yako na kuiandikisha kwake. Ili iweje, hebu niambie ili iweje?’ akasema yule jamaa huku kasimama kama mwanajeshi

‘Leo unakuja kudai mali yako, umeshahu kuwa ulishasema huna haja na mali za kishirikiana, leo hii sio za kishirikina tena….uinichekeshe, au kwa vile umefirisiwa,…lakini hata hivyo, nilichofanya kilikuwa na malengo, ndio maana nikakushauri , nilikushauri sana, kuwa umuoe yule binti, lakini umeshindwa mwenyewe, ungelimuoa, mali ingerudi mikononi mwetu….’akasema Tajiri.

Hilo usiniambie kabisa kwanini usingeliwagawia kutoka katika mali zako , hilo sikubali fanya ufanyalo, uhakikishe kuwa hiyi hati ya kuwagawia mali za familia umeharibiwa, nakupa siku mbili baada ya hapo tutazungumza mengine….akasema huyo jamaa.

‘Tatizo lako unaongea bila kutafakari, hilo litakuwa gumu kiharaka kiasi hicho, kwasababu hato zote za mke wangu alishazituma kwao na kuhakiisha kuwa wakili wake ambaye sio mtu wa hapa amezisimamia, ila kuna hicho kipengere cha kuwa kama mmojawapo atafariki mwingine atakuwa na mamlaka na hiyo mali…na kama binto ataolewa, mumewe atakuwa na mamlka na hiyo mali, ….wakati tunaandikishana hiyo hati nilikuwa kama nimfungwa, nilikubali bil kujali…..’akasema Tajiri Mzungu

‘Kwasababu ulikuwa umezingwa akili na huyo mwanamke wako….kazi ni kwako, nahitaji mali yangu haraka, nimesema siku tatu tu…..unanijua nilivyo, …unajua nini nitakifanya , …..na ok, ngoja nitakusaidia kazi moja, kama kuna kipengele kama hicho kuwa mmojawapo akifa mwingine ana mamlaka na hiyo mali,basi nitakusaida kwa hilo, ila tusilaumiane, baada ya hapo hakikisha umeweka sawa hiyo hati,..ali yangu ni yangu, andikisha mali yako , siyo yangu….’akasema huyo jamaa.

‘Sasa unataka kufanya nini, unataka kuua , hapana, kama utaua familia yangu hatutaelewana, kumbuka hilo, sitakubaliana na hilo, ….’akasema Tajiri kwa kung’aka.

‘Eti familia yako,…ni nani familia yako hapo, utasema mkeo, lakini nakuambia ukweli mke huyo anakupena kwsababu ya mali,….ukisema mtoto, mtoto huyo sio wako,…umebambikiwa na wewe unakubali tu, …mtoto huyo sio damu yako, au unajiita baba mlezi, kama ni hivyo sawa. Lakini kitu ninachojiuliza hapa, ni kwanini usizae mtoto wa kwako, na hata hivyo, kama umeamua kutoa sadaka ni kwanini usiwape mali yako wewe! Sasa kwa vile kuna kipengele hicho kuwa mmojawapo akifa mwingine ndiye mrithi,ina bidi tufanye jambo….’akatulia kidogo halafu akasema, `Hilo limeptishwa kaka, wewe subiri matokeo, na hilo ni kukusaidia tu, kama una njia nyingine hakikisha umeifanya kabla ya siku hizo tatu…’akasema huyo jamaaa.

‘Kwanini mnapenda kumwaga damu, tena damu za watu wasio na hatia, eti kwasababu ya mali, hamjatosheka tu, mimi hilo sikubalian nalo, katu…’akasema Tajiri Mzungu.

‘Eti sasa unajifanya mtakatifu, umesahau damu mlioyokuwa mukiimwaga, eti mnatoa kafara..hiyo damu ilikuwa ina hatia gani, …acha kunichekesha, …hebu niambie utakwenda kuwapokea hawo unaowaita familia yako,au uko busy ….nakuomba usiene kuwapokea kabisa….’akasema huyo jamaa.

‘Ina maana kweli umedhamiria na unajuaje kuwa watakuja leo, umepata wapi hiyo taarifa, …?’ akauliza kwa mshangao.

‘Mimi kila kitu nakijua hata huo mkataba wa mali nilikuwa naujua kabla, hata huo mpango wa nilishaupanga kabla sijaja hapa kukuaona, nilikuwa nataka kusikia kauli yako, kwahiyo wewe subiri matokea, …’akasema na kuiegemea kiti huku akikunja miguu mfano wa nne.
Tajiri akawa hana raha, hakupenda kabisa mpango huo, na alitamani achukue simu ampigie mke wake ajihami, au atafute walinzi wake wakawalinde , lakini hataweza kufanya kitu akiwemo huyo jamaa hapo mbele yake akaangalia kule ukutani, hakuona kitu, akafikiri afanye jambo gani la haraka, ….na mara akasikia watu wakiongea nje ya ofisi..

‘Ni nani hawo ,… siuliniambia hakuna mtu atakaye kuja leo humu ofisini….?’ Akauliza yule jamaa hukua akinuka pale alipokuwa amekaa na kutoa bastola yake kwenye koti, akajisogeza malngoni na kusikiliza kwa makini, sauti alizosikia zikamfanya atulie kwanza kwa makini kutafakari, na baadaye akafungua mlango kwa haraka na kutoka nje….

*******

Mbona tumebadilishiwa ndege kwa haraka hivyo, kwani ile ndege ya mwanzo ina matatizo gani…?’akauliza shangazi wakiwa uwanja wa ndege

‘Nafikiri kwa ajili ya usalama, sizani wamefanya hivyo kwasababu ya hitalafu ya ndege, nimeiona ndege tuliyopangiwa akiondoka mapema kabisa,…’akasema Rose huku akimwangalia Mgonjwa aliyekuwa kakaa mbali na waliposimama wao, mgonjwa alichelewesha kufika, mpaka wakaingiwa na wasiwasi, kumbe wao walikuwa wanajua kuwa hawataondoka na ndege waliyopangiwa mwanzoni, ndio maana wakamchelewesha mgonjwa…

Na hali ile ilimfanya Maua akose raha akikumbuka kuwa walipoondoka pale hospitalini, hakumuona mgonjwa kitandani, na kila alipojaribu kuwaeleza wenzake, akajikuta akishikwa na kigugumizi, na kwa vile ndugu yake alimuhakikishia kuwa hakuna tatizo lolote, moyoni akaridhika kuwa huenda ni madocta walimchukua kumuogesha, au ….akawa anshindwa afirie sababu nyingine, na wakati anataka kusema hisia zake na alichoona kule, mara gari maalumu la wagonjwa la hospitli hiyo likawasili .

Na mara wakamuona mgonjwa wao akitoka kwenye gari, hakuwa anahitaji msaada kwani alionekana na afya, ....alikuwa akitembea peke yake na wote walipoona hivyo, wakatabasamu huku wakimpokea kwa bashasha….na ghafla aakasimama na kuonyesha uso wa kushangaa akasema,...

'Oooh, nyie ni akina nani, mbona siwajui....'akasema magonjwa na wote wakashikwa na butwaa na nyuso za furaha zikaanza kuyeyuka, na pale pale Maua machozi yakaanza kumtoka. Mgonjwa alipoona vile akacheka, ....wakashangaa tena anacheka nini tena....

'Jamani samhani nilikuwa nawatania, nilitaka kuwashitua kidogo,mimi sijambo kabisa, msitie shaka, sina la kusema kwasasa, kwani moyo wangu una furaha ya ajabu, na unahitaji muda wa kutafauta maneno ya shukurani...lakini kwa sasa nahisi usingizi..sijui ni hizo dawa...'akasema mgonjwa na kuwafanya wanafamili hwo kupumua kwa nguvu....

Baadaye mgonjwa alipata sehemu nzuri akakaa, na hakutaka kuongea sana, aliwaambia wenzake anahitaji kutulia bila kuongea kwani alikuwa akijiskia usingizi, wakamuelewa na kumuacha atulie….na wao wakawa wanatemba huku na kule ilimradi wapate kuujua ule uwanja vyema, na baadaye akarudi pale walipomuacha mgonjwa wao, lakini kwa mbali kidogo na kuanza kuongea…

‘Una uhakika ni kwasababu ya usalama au ni kuingizwa mtegoni, ….maana hatari zinatuandama utafikiri sisi ni familia za mkuu wa nchi, hivi wanatafuta nini kwetu…?’akauliza mama ambaye alikuja dakika za mwisho na kusema kuwa mambo keshayamaliza atakuwepo kwenye msafara.

‘Tukuulize wewe mama,….au ulibadili ndege bila kutuambia ili tuondoke pamoja, ….vinginevyo ni mambo yenu mnayotuingiza kutokana na maisha yenu, ambayo hatuyajui mwanzo wake ni nini…’akasema Rose.

‘Nilipata taarifa hizo wakati najiandaa , sikuwa najua mapema kuwa ndege imebadilishwa na hata nilipojaribu kuwapigia mkawa hampatikani, sijabadilisha mimi….’akajitetea mama.

‘Sasa nani kafanya hivyo,…?’ akauliza shangazi.

‘Mkumbuke tunandoka na mgonjwa, na tuliambiwa kama tupo naye utaratibu wote watapanga wao, tunachohitajika ni kuwapa fedha zetu za usafiri,….’akajitetea mama.

‘Lakini yote hayo umepanga wewe bila kutushirikisha….mama mbona…’akasema Rose , na baaadaye akakatiza mazunguzmo alipogeuka kumwangalia ndugu yake ambaye alikuwa kashika shavu, akimwangalia mgonjwa….

Maua muda wote alikuwa kimiya kashikilia shavu, na safari hii alijikwatua kama ndugu yake, na walaimua kuvaa sare, …mara kwa mara alikuwa akimwangalia mgonjwa ambaye wakati wote alionekana katingwa na usingizi, huenda ni kwasababu ya madawa au uchomvu mwingi na hakuna aliyetaka kumsumbua. Maua akageuza kichwa na kumwangalia kwa mara nyingine, na safari hii macho yao yakakutana, na akatabasamu, na mgonjwa naye akatabasamu na wakabakia kuangalia kwa muda, huku kila mmoja akiwaza lake.

Maua alikuwa akiwaza mazungumzo yake na ndugu yake , mazunguzmo yao yaliishia katika mzozano hadi shangazi yao alipokuja kuingilia kati, kwani Rose alihamaki, kwanini Maua akimbilie kuolewa bila ya kuwa na uhakika kuwa mumeo yupo hai au keshakufa,....

‘Wewe Rose unasema tu, hujui nilipambana na maisha gani, hujui jinsi gani nilivyoteseka miaka miwili kwangu ilikuwa kama mtu mfu, niliishi kwa mateso makubwa sana, hadi nilitamani kujiua, asingelikuwa huyo mume wangu mpya, ningelikuwa maiti……..haya yaliyokuja kuyokea sikupenda kabisa yatokee hivyo,naweza kusema imetokea hivyo nje ya makusudio yangu…na kama ungelikuwa ndni ya moyo wangu, ungelijua ni jinsi gani ninavyoteseka, lakini sina jinsi, nifanyeje wakati yameshatokea….’akajitetea Maua.

‘Eti mume wangu mpya, unatamka bila aibu, sikuelewi, ina maana ulilazimishwa kuolewa, si ulikubali mwenyewe, sizani kuwa huyo Maneno alikulazimsiha kuwa kwasababu nimeokoa maisha yako ni lazima nikuoe, hapana, wewe umekimbilia, inavyoonyesha wewe umekimbilia kuolewa kwasababu uliogopa kuwa mjane, au kuna sababau gani nyingine, …?’ akauliza Rose kwa hasira.

‘Hajanilazimsiha baba wa watu, kilichotokea ni nje ya uwezo wangu, nishakuambia, na sikupenda kuwa na mtoto asiye na baba, na hata tunafikia uamuzi huo, tulishajua kuwa Mhuja hayupo duniani, unataka nikuambie vipi, hebu wewe fikiria, miaka miwili hatuna habari yoyote kuwa Mhuja yupo hai, na taarifa za ajali ya hiyo meli zilishasema wale ambao hawakuonekana ni kwamba wamepotelea majini wamekuwa chakula cha samaki, …’akasema Maua kwa huzuni

‘Kweli wewe mwepesi kukubali, …haya sasa mtu mwenyewe ndiyo huyo hajaliwa na mamba, au samaki, utamwambia nini, maana mpaka sasa natumai anaamini kuwa wewe ni mkewe, hajawahi kutoa talaka, mtafanya nini wewe na shangazi, mtafanya nini habu niambieni…?’ akauliza Rose.

‘Tutafanya nini, hiyo ndio kauli njema, …’akasema shangazi baada ya kutuliwa kwa muda kitafakari, akatulia kidogo na kuwaangalia wale mabinti wawili, huku akiomba hicho anachofikiria yeye kiwe kweli, akasema;

`Watoto wangu acheni kuzozana, haya yameshatokea, na hatuna jinsi nyingine, kitu cha muhimu nikutafuta ufumbuzi utakaosaidia, Rose usikimbilie kumlaumu mwenzako, maana hata wewe naona kama umekumbwa na janga kama hilo, habu niambie huo uja auzito ni wa nani, utaniambia kuwa umeupta kwa kupenda au ilitokeaje…?’ akauliza shangazi.

Rose akainama chini kwa aibu akaliangalia tumbo lake halafu akageuka kumwangalia Maua na hapo akajikuta akiwaza mengi, kwani kila alipofikiria sana, alijikuta njia panda, mwanzoni alijipa matumaini kuwa ujauzito huo ni wa mgonjwa wake, lakini akakumbuka tukio lililotokea katika mwezi huo huo, tukio ambalo lilimfanya amchukua sana Docta Adam, …

‘Naomba tusichanganye mada, hapa tunamzungumzia Maua, haya yangu hayawahusu, na nitajua jinsi gani ya kupambana nayo, lakini kitu kikubbwa hapa ni kuhusu huyo mgonjwa wetu, na hili limefungamana na Maua, hatuna ujanja wa hilo, je tutamrizishaje huyo mgonjwa, …tusikimbilie kwangu kwanza..’akasema Rose kwa hamaki.

‘Kwanini haya yako hayatuhusu, ina maana wewe sio mwanafamilia, tunataka kujua ukweli, kwani huenda nalo linafungamana na mgonjwa, wewe siulikuwa ukiishi naye…?’ akauliza Maua naye kwa hamaki.

‘Kwahiyo unaongea hivyo kwa kunilaumu au kwa wivu…mimi niliishi naye kama mgonjwa wangu na ukumbuke kuwa sikuwa namjua kuwa ni shemeji yangu, hakuwa an kumbukumbu zozote, sasa hayo ni mengineyo, hayahusiani na hili tunaloliongelea ni muhimu sana, usiingize …wivu hapa’ akasema Rose na mwishoni aliyatamka yale maneno ya mwisho kiutani.

‘Wivu, wivu gani tena, ..?’ akasema Maua na kumwangalia shangazi yake, ambaye muda mwingi hakutaka kuyaingilia hayo mazungumzo, lakini hali ilivyokuwa ikienda, akaona ana umuhimu wa kuingilia kati, na washukuru kuwa mgonjwa hakuruhusiwa kuondoka nawo , waliambiwa kuwa mgonjwa ataondokea huko hospitalini.

Na wakati hawo ndugu wawili wakiongea, shangazi kichwani, alikuwa akiwaza hali halisi kwa makini, na muda ule akawa anakumbuka maongezi yake na wifiye ambaye ndiye alitakiwa kuwepo kuyajibu maswali mengi yanayowakwaza watoto wake. Akakumbuka kuwa jinsi wifi yake alivyowaaga pale, i huenda pia alitumia mwanya ule, akwepe kuwajibika kwa watoto wake , kwani kwa hali halisi, watoto walimuhitaji sana, walihitaji kusikia atawaambia nini, na huo ndio ulikuwa wakati muafaka, maana wakitoka hapo huenda kila mmoja akatawanyika kivyake…akawageukia watoto , huku bado akiwaza pale alipoachana na wifi yake.

********

‘Mimi sijawa na uhakika kuwa tutaondoka pamoja….’akasema wifi mtu kwa kunong’ona, alikuwa akimnongoneza wifi yake, na ilionekana hakutaka watoto wasikie, lakini haikuwezekana kwani Maua aliyekuwepo karibu aliwasikia,

‘Mama unataka kuondoka, mbona bado mazungumzo yetu yalikuwa hayajaisha….’akasema Maua.

‘Kama nilivyowaambia, mume wangu kaniigiza nikamalizie kazi zetu za biashara, ili tuondoke na mzigo wa kutosha, yeye aliondoka haraka, na mambo mengi aliyaacha hayajamazika, kwahiyo mimi ninahijitajika kuyamalizia, na mambo mengine aliyoniagiza mume wangu, nikiyamaliza haraka tutaondoka pamoja, vinginevyo, itabidi muondoke na mgonjwa…’akaongea kwa sauti ya masikitio kuonyesha kuwa hakutaka kuachana na familia yake, lakini hakuwa na jinsi.

‘Kajitahidi umalize hizo biashara zenu haraka, maana tunakuhitaji sana….’akasema Rose.

‘Nitajitahii niwezavyo, inategemea wapi baba yako alifikia, kama kuna mambo yatahitaji muda, itabidi niwaachie vijana wetu wayamalizie, lakini yale ya muhimu itabidi niyamalizie mwenyewe…ila nawaomba , kama hatutaongozana, mkifika Uganda msiondoke mpaka nifike, na wewe Rose, inabidi uongozane na mgonjwa, maana hatujui afya yake itakuwaje, na pia kuna mambo mengi ya kifamilia tunatakiwa tuyamalize pamoja, …’aliongea mama huku akiangalia saa yake.

‘Sawa hilo ni muhimu sana,lakini ukumbuke sisi tunaishi kwa vibali, kwahiyo muda ukiisha inabidi turudi makwetu, na ningelifurahi sana kama ningelisikia hatima ya haya yanayoendelea na kama hakuna muafaka, mimi nitaondoka na watoto wote nirudi nao Tanzania…’akasema shangazi.

‘Uondoke na watoto….hapana,…..lakini hayo tutayajadili baadaye, maana sio rahisi kama unavyofikiria wewe, Rose ni mtoto wa Tajiri Mzungu, …unalielewa hilo na Maua ni mtoto….’akasema mama na kabla hajamaliza Maua akadakia kwa hanaki na kusema;

‘Hapana, usitugawe mafungu mafungu, ina maana mimi sio mtoto wako, kama unanikana niambie hapa hapa, …na ndivyo ilivyo, kwasababu hukunitaka tangia mwanzo, sasa nakubaliana na hisia zangu…’akasema Maua kwa huzuni.

‘Maua wewe ni ndugu yangu na mama huyu hapa ni mama yetu, haya yametokea tu,yasitukwaze tukavunja udugu, hakuna kitu kama hicho, mengine ni mambo ya makatarasi tu, hayana ukweli wa kuvunja udugu, kitu cha muhimu ni mama kutuambia ukweli, je mimi aliniandikisha vipi, maana sote tumezaliwa Uganda, je vyetu vyetu vya kauzaliwa vimeandikishwa vipi….hayo yanahitaji sheria, na ni rahisi kuyaweka sawa, na pia kuna mambo ya mirathi, na mengineyo….hatutakiwi kuakimbilia maamuzi ya haraka…’akasema Rose.

‘Mirathi ya nini kwani nani kafa hapa..ngojeni nikimaliza hayo mambo ya kibiashara tutakaa
tuyaongee, msianze kuleta mambo mengine…., hamjui sisi wazazi wenu tumepitia maisha gani, hayo yaliyotokea hayakutokea kirahisirahisi tu, kama mnavyofikiria, …ilibidi mtu uchukue maamuzi magumu , huku unaumia, hutaki unataka, lakini lazima uamuzi uchukuliwe…..lakini yote hayo yalikuwa na nia njema, ni kwa ajili yenu, ….tutaongea zaidi , ngojeni niwahi,…’akasema huku akiwatizama kila mmoja machoni, halafu akachukua kibegi chake na kusema;

`Haya jamani, naondoka, lakini nawaomba, haya mambo yetu msiyayazungumze mbele ya mgonjwa, ….’akasema mama na kuondoka.

Baada ya mama kuondoka, waliobakia wakawa wanamwangalia mgonjwa, na kwa kipindi hicho mgonjwa alishapitiwa na usingizi, na docta aliwaambia wamsimsumbue, kwahiyo wakakae sehemu ya kusubiria nje ya hicho chumba, aliebakia ndani alikuwa Rose, na aliendelea kuonea na dakitari akitaka kujua baadhi ya mambo, baadaye alitoka nje na kuonana na familia yao, akasema;

‘Kutokana na hali ilivyo, mgonjwa yupo tayari kuondoka, kwani matibabu mengine yanawezekana kufanyika huko huko kwetu, ila wamesema kuwa mgonjwa ataondokea hapahapa hospitalini, haturuhusiwi kuondoka naye huko hotelini kwetu, ….’akatulia kidogo huku akikaa vizuri kwenye kiti cha wageni.

‘Ina maana wao watamchukua na ari la wagonjwa hadi uwanja wa ndege, mbona mimi naona ni haraka sana, mgonjwa alistahili kukaa kama wili ili wahakikishew kuwa hajambo….?’ Akasema shangazi.

‘Hatua iliyofikia haihitaji tena uangalizi wa hali ya juu, hatu ahiyo anaweza akakaa na docta yoyote, kwani sasa hana matatizo yoyote….’akasema Rose.

‘Sawa kwa vile wewe ni docta, tutakusikiliza wewe hata kama hatupendi….’akasema Maua, Rose akaguka na kumwangalia ndugu yake kwa macho ya udadisi, alimwangalia kwa muda bila kusema kitu , baadaye akasema;

‘Kwahiyo kesho tutakutana naye huko uwanja wa ndege, kwa hivi sasa haturuhusiwi kubakia humu , kwani usalama na afya ya mgonjwa ipo mikononi mwa utawala wa hii hospitali, nishahakikishiwa hilo, tafadhali tuondokeni….’akasema Rose hata pale wenzake walipojaribu kulalamika, lakini yeye alikuwa wa kwanza kuanza kuondoka, kwani ilionekana haiwezekani kabisa wao kubakia humo ndani, au eneo la hospitali kwa muda ule, akawa anaondoka kwa ahtua ndogo ndogo akisema.…

‘Nimejaribu kila njia lakini wamekataa, wamesema hawawezi kuendelea kuvunja sheria ya hii hospitali, na sasa wamezidisha ulinzi wakutosha, na wamedai kuendelea kuwepo watu wasiohusika humo ndani ndiko kunakosababisha kutokuwepo na usalama….kwahiyo mimi naona tuondoke tu, tusiwe na wasiwasi, mgonjwa wetu yupo kwenye usalama , tutakutana naye kesho uwanja wa ndege…’akasema Rose na kuanza kuondoka.

Maua akageuka na bila kusema kitu akarudi hatua mbili nyuma, akaufikia mlango wa kila chumba, bila kujali amri waliyopewa akaufungua mlango na kutizama ndani,…hakuamini macho yake, akajikuta kashikwa na butwaa,… pale kitandani alipokuwa kalala mgonjwa, palikuwa patupu, hakuona mtu, …..haiwezekani mgonjwa kaenda ,…..akageuka kuwaangalia wenzake, walikuwa hawapo kwenye upeo wake wa macho, na kwa vile walikuwa wakiongea bila kuangalia nyuma, walikuwa hawajui kuwa yeye alikuwa karudi nyuma, na alipotaka kuwaita akaja mlinzi na kumfukuza….

NB Samahanini kwa kuchelewesha muendeelzo wa kisa chetu, ni sababu zilizo nje ya uwezo wangu, hata sehemu hii imeandikwa katika mazungira magumu, mtasahihisha pale nilipokosea, ….naona tunafikia ukingoni, ili tuanze kuwaza kisa kipya, …

Wazo la leo: Tupende kusikilizana, kwani kila mmoja ana hoja au ana hisia zake, na kama hisia zako hazikubaliani na wenzako, au unaziona ni zaidi ya wenzako, usiwakatishe au kuwakatalia wenzako kuongea, kwani huenda watakachokizungumza kikawa na manufaa kwako pia. Huwezi ukajua kila kitu na Ukumbuke kwenye wengi pana mengiNi mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Kwanza mkuu nikupe hongera zako, kwani licha ya kuwa upo kwenye mazingira magumu, umeenfelea kutujali...hongera sana nakuambia hivi, hilo unalofanya ni kama kujitangaza, siku utaibuka tu.
Wazo au ushauri, neno hitimisho uliliweka mapema sana, nionavyo mimi, lakini mambo mazuri. tupo pamoja mkuu