Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, January 25, 2012

Uso wa binadamu umeumbwa na haya




Siku hiyo nilikuwa nyumbani, nikawa nawapa kuku wangu wa kienyeji dawa na chakula, kati ya hao kuku mmoja alikuwa katotoa vifaranga karibuni, nikawa nawaangalia wale vfaranga , ambao kwa muda ule walikuwa wakimzunguka mama yao huku na kule. Mama yao alikuwa kalala na aliponiona akalia ule mlio wa tahadhari, mlio wa kuwaashiria watoto wake kuwa wawe makini, na mara kweli wale vifaranga wakakimbilia ndani ya mabawa ya mama yao kujificha na kutokeza vichwa tu.

Wkati nahangaika kuwapa chakula, baadhi ya wale vifaranga wakawa wanatoka ndani ya mabawa ya mama yao na kukimbilia kile chakula, licha ya mama yao kulia mlio ule wa tahadhari, lakini wengine hawakuajli, ikabidi mama yao ainuke na kuanza kutanua mabawa kwa kunitishia mimi nisiwakaribie watoto wake, hakuniamini hata mimi ambaye nawajali nakuwalisha, alikuwa akitimiza wajibu wake wa mama mzazi.

Nikiwa namalizia kazi ya kuwapa chakula na dawa na wakati huo mama wa wale vifaranga akikwakura chakula nilichowawekea, ambacho kilikuwa safi, tu lakini kama wajibu wa mama wa vifaranga lazima ahakikishe anawatengenezea watoto wake kile ambacho anaona kinafaa, na pia kuonyesha kuwa anawajali, na kweli watoto walikuwa wakimzunguka na kudonoadonoa kile chakula mama yao alichoshikilia mdomoni, nikasema kweli nani kama mama.


Wakati huo mara akazuka jogoo toka nyumba ya jirani, jogoo yule alikuwa hajaniona, akafika pale aliposimama yule mama wa vifaranga na kuanza kumbugudhi yule kuku mama wa vifaranga, yule mama kuku akawa anatanua mabawa kujihami, lakini jogoo yule hakujali akawa anataka kumparamia mama kuku yuke, na mama kuku hakukubali, akaanza kukimbia na hapo watoto wake wakawa wanakimbia huku na kule kujihami, na ghafla akashuka kunguru na kumchukua kifaranga mmojawapo.

Mama kuku yule huku akihangaika kukimbizana na yule jogoo, huku akitafuta mwanya wa kuwalinda watoto wake, na yule jogoo naye akawa kashituka na kuanza kulia mlio wa tahadhari kuwa kuna adui. Baadhi ya vifaranga wakakimbilia kujificha, ila mmoja ambaye alikwua bado mdogo akashindwa kujificha haraka, na kunguru akashuka kumwahi. Mana kuku hakubalai akaruka juu naye kumwahi yule kunguru na mimi kwa vile nilikuwa karibu nikarusha jiwe, yule kunguru kwa woga akamuachia yule kifaranga, kikadondoka chini na kilikuwa hoi.

Baadaye nikamfukuza yule jogoo na mama kuku akaingia kwenye banda na kulala na watoto wake, na mara vifaranga wawili wakamrukia mama yao juu na kusimama juu ya mgongo wa mama yao, hawa ni majogoo, ndivyo inavyoaminika kuwa ukiwaona vifaranga wanamrukia mama yao na kukaa juu ya mgongo wake watakuwa ni majogoo.

Nilijaribu kufanya uchunguzi huo kwa kuangalia alama za wale vifaranga. Na kweli hapa karibuni wale kuku wameshakuwa wakubwa, sasa hawaishi na mama yao, mama yao ana vifaranga wengine wakubwa tu, wale niliowaona siku ile wengine wanatetea na majogoo yanaanza kuparamia mitetea, na cha ajabu sasa wanaparamia hata ndugu zao, na cha ajabu zaidi wanamfukuza hata mama yao,…hiyo ndiyo hulka ya wanyama, wakishafikia umri fulani hawatambuani tena, mama hajuani na watoto wake tena, watoto nao hawajuani na wazazi wao, mtoto atampanda mama yake!


Wakati nawaza hili nikakutana na baba mmoja akiwa kamshika mtoto wa kike mkono, mtoto huyu wa kike alikuwa kavaa sare za shule, na mfuko wa vitabu upo mgongoni, binti yule alikuwa akilia, na wote tuliokuwa karibu tukageuka kumwangalia baba yule kulikoni.

Wengi wetu mawazo yalitupeleka mbali maana dunia hii imeharibiwa na watu wabaya, na mwisho wake unakuja na mambo ya ajabu ajabu, ukiona jibaba limemshika mtoto na ukalitilia mashaka chukua hatua haraka, kuna visa vingi vya kubakwa watoto wadogo wa kike an wa kiume kwani watu hawa waliolaniwa wanafanya unyama wao kwa mtoto yoyote kwahiyo ukiona jibaba limemshika mtoto wa kiume usizarau, maana wengine tunatilia mashaka tu kwa watoto wa kike, liwe limemshika mtoto wa kike au wa kiume, ukamtilia mashaka, chukua hatua za haraka, uokoe hawa watoto wasio kuwa na hatia.

Sisi tulipoona vile tukaamua kumfuatilia yule baba nyuma, kusikiliza nini wanachoongea, na mara tukasikia yule baba akisema;

‘Wewe binti yanu, jana uliniambia kuwa umekwenda shule, nimeuliza walimu wako wamesema hukufika shule, ulikuwa wapi, leo tunaenda mguu kwa mguu hadi shuleni kwako, kama kweli unanidanya nitakupiga mikwaju mbele ya walimu wako…’akasema yule baba.

‘Baba mimi nilifika shuleni, kwasababu nilikuwa naumwa, muda mwini nilikuwa darasani, ndio maana mwalimu uliyemuuliza anasema hakuniona….’akajitetea yule binti huku akilia,

‘Nitayajulia huko huko kwa walimu wako kwani hakuna kitabu cha mahudhurio, na sasa hivi nitakuwa nikifanya hivi hivi, kuhakikisha unasoma, unafikiri mimi hili litanisaidia nini, haya ni kwa ajili ya maisha yako ya baadaye , na sana sana ni kwa ajili yako na mume wako na watoto wako…nahangaika kutafuta ada, nihanaike kukufuatilia kusoma, hivi mnataka mimi nianguke kwa shinikizo la damu, nife, au…'

‘Hapana baba, siku hizi nimebadilika, nasoma baba, …’akawa analia yule mtoto huku baba wa mtoto kamshikilia mkono na mwendo wake kwasababu yeye ni mtu mzima ulikuwa ukimzidi yule binti kwahiyo muda mwingi alikuwa kama anamvuta ili wawe sambamba,…tulipoyasikiliza yale mazungumzo weni tukaridhika kuwa huyo ni baba yake na hana nia mbaya na yule mtoto. Na kwa muda ule dada mmoja akaanza kulia na kasema;

‘Baba huyo ananikumbusha mbali anafanya kama nilivyofanyiwa na marehemu baba yangu,..nilipomuona nikakumbuka maisha yangu, yalikuwa hivyo hivyo, sasa baba ni marehemu, mungu amlaze mahali pema peponi, asingelikuwa yeye, sijui sasa hivi ningelikuwa wapi, kama sio kuwa changudoa, na kuzalilika mitaani, maana hawa machangudoa wanatembea na mibaba sawa na baba zao, ni kama binti kutemeba na baba yake.

Aliposema hivyo `sawa na baba yake’ ndipo nikawakumbuka wale kuku zangu, ambao sasa wanatemeba na mama yao, hawakumbuki tena kuwa huyo alikuwa mama yao aliyewalea kwa shida na taabu sasa wao ni vijogoo, wanamfukuza hata mama yao. Lakini hayo ni maisha ya wanyama, sio sisi binadamu, binadamu tuna haya zetu, huwezi kumkuta baba akitemba na binti yake au mama akitembea na mvulana au kijana . Labda hawo wanaoitwa machanudoa, na wanaume sijui wanaitwaje….


Kama unabisha hili, muda wa jioni na kwenda mbele nenda mitaa ya Ohio hapa Dar, na huko Moshi kama sikosei kuna mtaa wa Mafuta, na kila mji sasa una mitaa fulani ambapo wapo wakina dada, nasiki hata wanaume wanajiuza, …wanajizalilisha kwa kufanya biashara hiyo haramu, na mwisho wa siku wanakuja kutembea na mibaba sawa na baba zao waliowazaa, mabinti hawa au wanaume hawa uso wao umevuka haya ya kibinadamu,…tumegeka kuwa wanyama au kuwa kama kuku….

Jamani tunakwenda wapi? Na hii hali iliyozuka sasa hivi ya watu kuwazalilisha watoto, na kila kukicha hukosi kusikia visa kma hivi, jamani tutauliwa wazazi, tutaulizwa katika swala hili la ulezi, kwani kila mmoja ni mchungaji, kila mmoja ni mlezi, watoto wote ni wetu sote, tuhakikishe jukumu hilo tunalitekeleza sote.

Ngoja niishie hapa maana, muda ni mali...naishia hapa huku nikitafakari kisa cha huyu mwanadada aliyeangusha kilio baada ya kumuona huyo binti akikokotwa kwenda shuleni na baba yake, kama nitapata nafasi hiyo nitakiweka hewani. Tukumbuke blog hii ni `diary' niliwajibika kila mara kuweka vitu kama hivi,lakini ipo siku ndoto ya blog hii itakamilika. TUPO PAMOJA

NB: Kisa chetu cha `akufaaye kwa dhiki ...' akinaendelea na kinafikia ukingoni, lakini sijapata mahala muafaka pa kuweza kukimalizia vyema.



Ni mimi: emu-three

3 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Imekuwa kama tuliwaza kitu kimoja leo. Nimesema hivi kwa vile nami katika pitapita nimekutana na mada inayofanana na hii. Ila yenyewe ni kinyume kijana kumbaka mama yake mzazi. Kweli sijui binadamu ni wanyama au ndo tamaa pia. Fikiria Baba anamtamani binti yake mdogo tena pengine hata alikuwa akimbadili nepi...Yaani kwa kwali nashindwa hata kutafakari jambo hili, Sijui ni wapi tuendako???

emuthree said...

Nashukuru sana sasa Yasinta tupo pamoja. Na leo mtandao umegoma, kila ukiweka kitu hakikubali,...sijui ni kwangu tu, au kuna tatizo huko Google kwenyewe, sehemu inayofuata ipo tayari, mtandao ukiwa makini nitaweka sehemu yetu ya 76 ya akufaaye kwa dhiki -hitimisho 20

Anonymous said...

Huyo bint,alishajua utamu ulivyo,kwa hiyo kuacha ni shughuli pevu,mzee amepata kibarua cha ziada,ambacho akina malipo.Wazazi,mbona mna kazi.Huyo bint,amuonei huruma baba yk,na maisha yalivyokuwa magumu hivi,unaendekeza utamu au raha?Pengine huyo,anayempatia huo utamu,hana kitu chochote cha maana,yaani,angejua thamani yk,wala acngeichezea hivyo.Wenzie,tunatamani kurudia enzi ya udogo,tusome nk,lakini ndiyo hivyo tena,tunakumbuka shuka,wakati kumeshakucha zamani.Huyo baba,cjui atafanya kazi gn,maana kwenda kuwatafutia chakula na mahitaji mengine,inabidi aende kzn kuwajibika na huku nako ampeleke huyo bint(kicheche)shule,sasa atajigawa vipi yeye,mtu mmoja?Yaani,ningekuwa namjua hata cmjui,ningemshauri amnunulie daftari la maudhirio.Kila mwalimu wa kipindi,anapotoka,asaini,kuwa alikuwepo kwenye kipindi,kila cku,na pia kabla ajarudi home,inabidi apitie kwa mwalimu wk wa darasa,naye asaini,kuwa kweli ameudhuria,la sivyo,mzee atakufa kwa BP tu,aache watoto wengine,ambao bado wanamuhitaji,kisa ni huyo mpuuzi.Vipi,umeshapata sehemu ya kujishikiza kwa muda au?

Mimi C. nduguyo