Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, January 19, 2012

Kisa kinaendelea lakini.....



Kama nilivyokwisha sema tangu awali kuwa mtiririko wa kisa chetu utakuwa ukichelewachelewa kwasababu zilizopo nje ya uwezo wangu. Lakini hata hivyo, kuna jambo ambalo lilinifanya nikawie kidogo kuiweka sehemu inayofuata kwani ilihitaji utafiti fulani, kwani mambo yaliyotokea hapo yalikuwa hayaniingi akilini, na wengine natumai itakuwa hivyo hivyo, lakini yapo, na yanatokea..

Nilipofika sehemu hii hata mimi mwenyewe nilijiuliza hivi kweli haya mambo yapo,...na siku kadhaa nikayakuta yakitokea kwa mtu....nikajiuliza haya mambo kama yapo kwanini hayajawahi kuwekwa kitaalamu na dawa zake zikawekwa wazi, maana asikuambe mtu haya mambo yapo pia hadi huko uzunguni, lakini kwa silimia ndogo, ...pengine wenzetu hawayajali sana, na wakati mwingine, ikitokea mtu kapatwa na hayo mambo, wao wanaishia kumpeleka mtu huyo kwenye hospitali za wenye mtindio wa ubongo.

Nikajiuliza pia kwanini hayo mambo hayapo kwa kiasi kikubwa huko uzununi, yapo ndio, lakini ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na huku kwetu, ... Na ni ukweli usipingika kuwa wenzetu nikimaanisha wazungu, hawafuatilii sana dini, ili tuseme wao hawayajali hayo mambo kwa vile ni watu wa dini…, lakini huku kwetu, watu wanajitahidi kwa dini, na bado yapo, kwanini, ina maana hayo mapepo, mashetani yanahitaji watu masikini...nikajiuliza, na kujiuliza, je nyinyi wenzangu mnasemaje kwa hili?

Swali langu kwenu linakuja hivi, je kuna mizimu au mashetani?, Na kwa wale waliowahi kukutana nayo au kuwaona ndugu zao waliowahi kutokewa na mambo hayo, ilikuwaje na je walitumia njia gani kupambana nayo. Najua kwa ujumla njia pekee na ya uhakika ni kwa kutumia uwezo wa mungu(dini), lakini uwezo huu unahitaji imani kamilifu kwa muathirika, bila imani utaweza kweli kuyashinda haya matatizo sijui, nakuachia wewe useme uonavyo wewe au ukweli unaoujua wewe….

Wapo watu wanataabika kwa matatizo haya yanayojulikana kama kukumbwa na mapepo au mashetani na wapo watu wanayatumia kujipatia utajiri, na wengine wanakuwa ni mawakala wa mashetani , kwani wanayatumia mambo haya kuwachawia wengine,…na wengine wanayatumia mambo haya kujipatia riziki zao kwa kutibia mambo hayo, ….swali langu ni watu hawa wanaotumia mambo haya kihasi, kuawadhuru wengine, …. sijui nini kikubwa wanachofaidi hapo, na je kwanini wasingeliweza kuyatumia mambo haya katika njia chanya, wakafaidii na kuwasaidia wasio na uwezo.

Kisa chetu cha Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli, kimepiga hodi katika sehemu hiyo, kwani sehemu inayokuja itaingilia mambo hayo, nimeona niliweke wazi mapema, msije mkafikiri mimi napendeela hayo mambo au kuyaamini, hapana,…lakini kwa vile visa vyetu vimetokea kwa watu , nikaona ni vyema, pamoja na kupata maelzo ya kina, lakini ni muhimu na mimi mwenyewe nifanye utafiti kwanza, nisikie zaidi kuhusiana na mambo hayo ya mizimu, mashetani na nguvu za giza, kabla sijaiweka sehemu hiyo ambayo itakuwa ikitisha kidogo, lakini ndivyo ilivyotokea kwa jamaa yetu huyo , na waliomshuhudia wamesema ndivyo ilivyokuwa, sio kwamba kajitungia hadithi ….

Mkumbuke yote haya yalitokea baada ya ile ajali ya MV Bukoba, na hayo mengine yalifuatia badaye….

Swali kwako wewe mpendwa wa blog hii, tunaomba mchango wako kuhusiana na mambo haya ya mashetani na kwanini hapa Dar sasa hivi watu wengi, hasa wanawake wanakumbwa na matatizo haya, na utashangaa hata mashuleni kwa watoto, yanatokea haya mambo, kuna lini kulikoni?

Hebu soma sehemu hii toka wikipedia

Ni mimi: emu-three

8 comments :

Anonymous said...

Mambo hayo siyaamini sana, ila kwa ukweli nimeshuhudia watu wanapandisha mashetani, wanahangaika kweli, na utakuta wanabadili hata sauti na kuongea sauti ya mtu mwingine, utakuta mwanamke anaongea kama dume, au dume linaongea kama jike....ajabu kabisa,....dawa na kuiingi akatika ibada,
Maoni yangu ni kuwa mamboo hayo huzidi sana kwasababu ya adui ujinga , na pili umasikini. Watu badala ya kushinda kwenye maabara kugundua madawa ya kitaalamu watu wanashinda kwenye mauchawi kuangamiza wengine,wewe utanunua uchawi kumuangamiza mwenzako, ....au hutaki mwenzako aendelee,kwanini...huo wote ni ubinafsi...au mtu anafuga majini au mashetani, ya nini, yakija kukugeukia itakuwaje, hawo wanaofanya hivyo ni kama wale wanaofuga nyoka,ipo siku atakugeukia, ...mungu atuepushie na udhaifu huo,...
Chombe emu-three tunaomba utuendelezee kisa chetu, maana umetuacha kwenye utamu, najua hali uliyo nayo, lakini kidogo kidogo sio mbaya, na mungu atakujalia upate sehemu ya kujishikiza na hata kukujalia kupata nyenzoo za kukamilisha kitabu na kuiendeleza blog yako.
Samhani nakuuliza kwanini huongeii na watu wa voda, zaidi au tigo wakakuzamini,naona kuna watu wanazaminiwa, na kwenye blog zao hakuna cha maana...hebu ongea nao, au ndio mambo ya kibongo mpaka uongee kwa herufii kubwa, sipo siku watakuona mkuu....

Simon Kitururu said...

Nje kidogo ya topiki:

Nimerudi mkuu! Niko nyuma kidogo katika mafunzo uliyoandika hapa kutokana na muda kadhaa wa kadhaa kutoona Komputa!

Pamoja sana M3!

Subira said...

Asikudanganye mtu Em3 haya mambo hata kwa wazungu yapo tena sana tu. Ila wenzetu wao wameyaweka wazi hawafanyi kificho. Kwa mfano kuna sehemu wanakwenda Stonehenge kuabudu mizimu, na wako wanaokwenda inapokutana mito mitatu, mji ninaoishi kuna mahali mito mitatu inakutana na wao wanasema hapo ni sacred place.

Tukirudi kwenye kupunga au kutoa majini hata wazungu wanafanya, google exorcism hata kwenye you tube uone. Na kama ni uchawi yaani wao wachawi wao hawana uficho ila wanasema kuna good witches na bad witches.

Na tukija kwenye kuabudu mashetani hapo ndio umewafikisha ndio wengine wanapatia utajiri, kama kundi la illuminati na mengineyo. Hawana kificho kusema kuwa mtu yeye anaabudu shetani au yeye ni free spirit. Na utakuta nembo yao ni skull, skunk, au nguo nyeusi. Na wengine mpaka wanaweka makeup nyeusi usoni kama machozi.

Mwisho kuna makundi ya dini ambao wanaamini uwepo wa Mungu kwa dini mbali mbali na kundi la atheist ambao hawaamini uwepo wa Mungu. Kwa hiyo suala la kuamini au kutoamini ni mtu mwenyewe jinsi anavyojiweka lakini asikudanganye mtu haya mambo yako sana kwa wazungu. Ukitaka kujua kuwa wazungu ni washirikina ingia kwenye yahoo au msn horoscope pages uone jinsi watu wanavyotangaziwa wakatabiriwe au kusafishwa nyota zao! he heheehee!

Anonymous said...

M-3 haya mambo yapo, ila ukiyafuatilia sana unaweza kujikuta unamkufuru Mungu, so kikubwa ni kujikita kwenye ibada na kumtegemea mwenyezi Mungu

Anonymous said...

mambo, mbonna huko kwenye wikipedia sioni mwendelezo.kama vipi tuwekee kwenye blog tulioizoea au tueleze kwa kina tunapataje kwenye wikipedia. mdau

Anonymous said...

Tupo pamoja M3 kaza buti tunasubiria huo mwendelezo wa kisa chetu maana umetuacha patamu sana mungu atakusaidia tu utapata chako one day

emuthree said...

Nawashukuruni sana kwa kuwa pamoja nami, na kunifanya niingiwe na moyo wa kuweka sehemu inayofuata. Sehemu hiyo ipo jikoni, lakini natafuta internet cafe isiyo na longolongo, nyingi computa zao sipo `slow' sitaweza kuandika kile nlichokikusudia,...
Huko kwenye wikipedia ni maelezo ya maana na maaana ya kuingiwa na mashetani, niliiweka ili uweze kujua kuwa sio mambo ya kujitungia,yapo na kama alivyosema Subira, wenzetu wanayafanya waziwazi, sio huku kwetu wanafanya usiku, na kuwatesa wenzao, bila faida. Nashukuru sna Subira kwa kutuweka wazi zaidi.
Mkuu Kitururu, karibu sana, nilizania umesafairi kuhesabiwa, ...

Oh, na wengine...Tupo pamoja.

Nashukuruni sana, ila sijamsikia Samira,upo kweli, au umekwenda `vacation' au upo `honeymoon'..lol
Tupo pamoja

Rachel Siwa said...

Ahsanteni wote mliochangia kwa kutoa maoni yenu nasi twajifunza mengi,Ndugu wa Mimi Ubarikiwe sana kwa Yote kwani siwezi kuyahesabu, ilo la Internet, linanikwaza sana, sina jinsi tuu,Lakini Mungu yu mwema sana ndugu yangu ipo siku yataisha tuu,PAMOJA SANA SANA SAAAAANA!!