Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeSaturday, January 7, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-71 hitimisho 15


Docta alimchunguza yule mgonjwa kwa muda, na alipoona kuwa kila kitu kipo sawa akawageukia wanafamilia na kusema;

‘Inahitaji muda kidogo kurudia hali yake ya kawaida, na atakuwa na matatizo ya hapa na pale na wakati mwingine anaweza akawa asione vizuri, au hata kusikia vizuri, lakini matatizo hayo ni ya muda mfupi, …msijali sana, ila naomba msimsumbue kwa sasa..’akasema Docta na kuondoka, na kuwaacha wanafamilia wakimtizama mgonjwa wao huku kila mmoja akionekana kuwa na mawazo yake.

Baada ya muda mfupi wa kimiya Mama akawageukia wanae kuwaangalia na baadaye akamgeukia Rose na kumuangalia huku akiwa kashika kidevu na kusema na baaadaye akaweka kidole mdomoni kama anayemuonya kitu akasema;

‘Vipi Rose ni kweli uliitwa na dakitari au uliitwa na hawo watu wako wanaokusumbua…’, akasema mama huku akimwangalia Rose kwa makini, lakini Rose hakusema kitu, macho yake yalikuwa yakimwangalia Yule mgonjwa usoni, yalikuwa hayabanduki, kama vile akiombea kuwa akifumbua macho yake awe wa kwanza kumwangalia.

Mama alipoona mwanae kaka kimiya hamjibu akasema,

`Mwanangu nakuomba uwe makini na hii dunia, hawo watu ni watu wabaya sana, na ni bora ukatuweka wazi jinsi ulivyo na hawa watu, na ikibidi tuwaambie polisi, wao watapambana na watu hawo wenyewe…’na alipotaja neon polisi polisi Rose akashituka na kugeuka kumwangalia mama yake usoni na kusema.

‘Mama watu gani hao, unaowazungumzia, mbona sikuelewi….’akajitetea Rose huku ajifanya hajui nini mama yake anachoongea.

Mama yake alimwangalia kwa makini kwa muda , hadi Rose akageuza kichwa na kumwangalia ndugu yake ambaye alikuwa kamwangalia mgonjwa na kuonyesha kuwa yupo mbali kimawazo, na huenda alikuwa hasikilizi kabisa walichokuwa wakiongea mama yake na Rose.

‘Tatizo lako wewe unatufanya sisi ni watoto wadogo Rose…wewe dunia hii nimeiona mapema kabla yako… , utabisha kuwa hiyo simu uliyopigiwa haikuwa inatoka kwa dakitari kama ulivyosema…?’ akauliza mama mama akiwa bado kamkazia macho Rose.

Rose akaanza kukereka na kugeuka kuangaliana na mama yake halafu akasema kwa sauti ya chini chini;


‘Mama mambo mengine sio ya kuongelea hapa,…unakumbuka docta alivyosema, tunatakiwa tusimsumbue mgonjwa, kama unataka tuongee, tutayaongela hayo mambo baadaye…’akasema Rose.

Mama akaangalia huku na kule na akataka kusema kitu , lakini akaghairi na kukaa kimiya akiwaza na baadaye akamwangalia Rose kwa makini, na Rose alipoona kuwa mama yake bado anataka kuongea akasema;

‘Mama hata hivyo , hayo mambo hayakuhusu, ni matatizo yangu mwenyewe, nisingelipenda kumuingiza mtu mwingine na baaadaye niishie kujuta, hapana, mimi nawaombeni sana muniachie hayo maswala mwenyewe najua mwenyewe jinsi ya kukabiliana nayo..’akasema Rose.

Mama mtu akacheka kwa kebejhi na kusema `Mwanangu sasa unajifanya umekua sio….eti tukuachie maswala hayo mwenyewe, wakati matatizo hayo hayataishia kwako tu,…hivi unafikiri ukipata matatizo sisi hayatatuhusu..’akasema huku kakunja uso wa ukali, akatikisa kichwa kuonyesha kusikitika.

‘Hujui kuwa hayo matatizo yanamhusu hata huyo mgonjwa, na kwa taarifa yako, kila kitu nakijua na usipokuwa makini unaweza hata ukamuingiza huyu ndugu yako kwenye matatizo hayo., maana wanashindwa kukutofautisha wewe na yeye…’akasema Mama na hapo Maua akageuka kumwangalia mama na baadaye akamtizama Rose kwa makini akionyesha uso wa mshangao.

Shangazi ambaye alkuwa kimiya akiyasikiliza hayo mazungumzo akawageukia na kusema;
‘Hata mimi naona hayo mazungumzo tukayazungumzie huko nyumbani …eti nyumbani tena, huko hotelini, hapa sio mahala pake,…’akasema Shangazi huku anawaangalia kwa makini na baadaye akamgeukia Rose na kusema;

‘Na wewe Rose, ni kweli anavyosema mama yako kuwa wkati umefika, ni bora haya mambo ukayaweka wazi, ili na sisi tujue jinsi gani ya kusaidia maana kama alivyosema mama yako, watu hawo ni wabaya, …’akasema Shangazi, na Rose akainama chini huku akiwaza, na hakusema kitu, alikaa kimiya kwa muda.

Maua naye akaona ni bora afunue mdomo akasema; ‘Kwani kuna nini kinaendeela ambacho mimi sikijua…’akamgeukia shangazi , halafu akamgeukia mama yake, na baadaye akamgeukia Rose, na alipoona wapo kimiya akamgeukia Shangazi na kusema;

‘Mimi naanza kutishika, maana kweli kila tunapokwenda naona watu wanatufuatilia nyuma, …..kuna nini jamani, kama kuna hatari ni bora tuwaambie polisi…’akauliza Maua huku akiwatizama kila mmoja kwa wakati wake.

‘Mimi naona ni heri usiyajue kabisa haya mambo , maana ukiyajua utaishi kuingia kwenye mashaka yasiyokuhusu, lakini nina uhakika mwisho wao unahesabika,….’akasema Rose huku akiwaza jinsi ilivyotokea baada ya kupokea ile simu….

Alipotoka pale na kuiacha familia yake alichukua taksii ambayo ilimchukua moja kwa moja hadi hospitalini, na alipoingia sehemu ya mapokezi kabla hajamsogelea Yule jamaa wa mapokezi akatokea mtu na kumgusa kwenye bega na kumwambia;

‘Twende huku….’

NB: Nimepitia internet café na kuandika kisehemu hiki kwa haraka, sehemu hii inaendelea


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

pole sana emu3 kwa shida unazozipata.. ila ipo siku mambo yatakaa sawa tuu...