Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, December 23, 2011

Tunawatakia mapumziko mema ya kufunga mwaka 2011
Leo asubuhi wakati naelekea ofisini, nikiwa ndani ya daladala , nilikutana na ajali mbili njiani, magari yamegongana, nikawaza akilini kuwa ndio ajali za kufunga mwaka.

Tunapenda kusema ni ajali za kufunga mwaka, lakini je ni kweli lazima tukifunga mwaka kuwe na jali kama hizi? Au ni kwasababu watu wanakuwa na haraka za kimaisha mpaka wanasahau kuwa makini, ni kweli kuwa mwenyezimungu kazipanga ajali hizi zitokee kipindi hiki? haya na maswalimengi yakanitanda akilini.

Nikakumbuka ule usemi usemao ajali haina kinga, lakini je mtu anaweza kusimama kati kati ya barabara akisema ajali haina kinga,….hapana, hata yule mwenye mtindio wa Ubongo hawezi kufanya hivyo, anajua kabisa kuwa hiy ni hatari. Hata mnyama, au kuku huwezi kumuona akiwa kasimama kati kati ya barabara, akijua kuwa kun agari linakuja, lazima atachepuka pembeni kulipisha, anajua kuna hatari mbele yake. Cha ajabu ni hali ilivyo sasa, kwa watu kujenga mabondeni,ambapo kabisa tunajua hatari yake ni nini kipindi cha mvua kama hiki!

Kwanza pole nyingi kwa waliokumbwa na dhahama hili, na wengi tumeathirika kwa namna moja au nyingine kwasababu ya mvua hii, yote n majaliwa ya muumba.
Hawa waliojenga mabondeni,ambapo kuna mkondo wa maji, naona kama yule mtu anyesimama katikati ya barabara, akiju ahtari iliyopo. Sawa labda ni sababu ya kutafuta unafuu, au kuna sababu nyingine ambazo hatuzijui, lakini tujaribu kutahadhari kabala ya hatari, kwani maji hayana mchezo, yakikasirika, yanaweza yakafanya maajabu, …tumuombe mungu atunusu kwa majanga kama haya, na ikiwezekana tutafute sehemu nyingine za kujenga,..kiujumla tunajua hali ilivyo, lakini wapo wenye uwezo wamejenga majumba ya maana, na mwisho wake ndio..

Nilipofika ofisini, nikapambana na majanga ya wakubwa, nikawaza zaidi hivi `kwanini watu tunatofautiana na kufikiri, maana kuna watu wanaona kila wakifanyacho wao ni sahihi na wengine hawajui, na bila kufikiri tunakimbiliana kulaumiana...sasa labda tunawalaumu hawa waliopanda mabondeni, na kushindwa kuelewa, chimbuka kamili la haya, `maisha magumu'.

'Wewe hujui kazi, mbona unafany amakosa kma haya...'hii ni kauli ya bosi wangu akinishambulia kwa lugh aya dharau, nikamwangali na kusema haya yote ni ile hali ya wandamu kutokupenda kuwajali wenzao, naona nisiseme zaidi, kwani mitihani ya kimaisha ni mingi sana, na iliyobakia ni kumshukuru mungu na kusema yote maisha, na mtoa riziki ni mungu peke yake, na ajali hazina kinga, ila tujaribu kuziepuka, kila iwezekanvyo.
Blog yenu hii inawapa POLE NYINGI WALE WALIOKUMBWA NA MAAFA HAYA na inapenda kuwatakia kila la heri na sikuu zinakuja na heri na fanaka katika kufunga mwaka wa 2011, kwani mengi tumepitia,. mitihani ya kimaisha na wengi wametangulia mbele za haki, yote hayoo ni mapenzi ya mungu. Ni vyema wote tukamkumbuka mungu, na inapofikia miaka kama hi ya kumaliza mwaka, kwa Waislamu wameishaingia mwezi wao wa pili wa mwaka mpya na mwaka huu 2011 ndio unaishilia, je tunafikiria nini,na tumejoanga vipi, au ndio tunasubiri kupiga madebe na kurusha mawe ...

Ni vyema kutokana na mitihani mingi inayotukuta tukafunuka akili zetu kuwa yupo muumba, ambaye leo kupo hivi kesho kunaweza kukageuka na kuwa vinginevyo, ni nani alijua itakuja mvua kubwa ya kisa hcho kwa muda mfupi...angalia mitumbwi inaletwa sehemu ambayo ni nchoo kavu, lakini mvua imetenegeneza lisilotarajiwa, watu walipanda hadi juu ya transfoma, bila kujali hatari ya umeme...je tunataka nini ili tuelewe kuwa yupo mungu mwenye uwezo wa kila kitu.

Ni vyema tukajenga njia ya kumaliza mwaka kwa amani, kwa kumuomba na kumshukuru mungu.

POLENI SANA NA MAAFA HAYA NA TUNAWATAKIA HERI NA FANAKA KWENU NYOTE
TUPO PAMOJA

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Mkuu kuhama sehemu uliyoizoea inakuwa mtihani, hasa sisi wabongo ambao tunaogopa kujaribu kitu kipiya. Sitetei kuishi mabondeni kama ulivyosema ni sawa na mtu kusimama katikati ya barabara ukisema `ajali haina kinga...lakini vipi na vipi utaanza maisha mapya, ukizingatia jinsi ulivyohangaika kupata kiwanja, kujenga, ...duuh, inahitaji ujasiri...

Lakini vyovyote iwavyo, kinga n bora kuliko kuponya, su sio, tujihami kwa hili, ila nina uhakika wakiondoka hawo wamabondeni, mabonde hayo yatachukuliwa na wahindi watajenga maviwanda yao, wao wana bima, wao wana pesa...

Malkiory Matiya said...

Heri ya x-mass na mwaka mpya wa 2012 ndugu Emu-three.

emu-three said...

Na wewe pia mkuu Malkiory ,tupo pamoja