Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, December 26, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-69 Hitimisho 13




Rose alipoondoka, walibakia shangazi na mama wakiwa wametulia bila kuongea chochote, na mara mama akawa kama kakumbuka kitu, alitulia kwa muda, halafu kumbukumbu zikamjia kichwani, akakumbuka siku ile alipofika hoteli wanapoishi na mumewe,…siku ile alirudi ghafla nyumbani kwenye hoteli wanapishi, kwani alisahau baadhi ya stakabadhi zake za kibiashara ambazo zilikuwa muhimu sana, na alipoingia ndani ya vyunba vyao wanapoishi akamsikia mume wake akiwasiliana na mtu kwenye simu, hamu ya kutaka kujua anaongea na nani ikamjia, kwahiyo hakupiga hodi akasimama mlangoni na kusikiliza.

‘Umesema wapo mapacha kweli hapana, hilo sikubaliani nalo,… mna uhakika na hilo…sikumbuki kabisa kitu kama hicho, basi labda ni kufanana tu, jaribuni kufuatilia kwa karibu kama litawasaidia kwangu mimi sina umuhimu nalo sana,…walikuwa pamoja na mke wangu, na unasema na mama mmoja…..oh… kwasababu kama ni mapacha kweli, basi hiyo taarifa sina ….kwasasa hivi haijalishi sana, …’ Akatulia kusikiliza upande mwingine wa simu kwa muda, halafu….

‘Ok, hilo halina umuhimu sana kwasasa, maana nahisi sio damu yangu, ….kwasababu kutokana na ilivyo kama ingelikuwa ni damu yangu, ningepata matatizo, …’akasema na kutulia.

'Ndio ni imani za kishirikina, nakubaliana nalo, ndio maana wewe ulikataa, lakini ina tofauti gani na wewe uliyejiunga na makundi hayo haramu, huoni sasa unavyohangaika…’akasema na kutuli kwa muda.

‘Ndio ikibidi nitakusaidia lakini mambo hayo nilishakukanya mapema, mimi niliyakataa kabisa, kwanza ili iweje, famlia yetu ni tajiri, ..tunataka nini zaidi, wewe na tama zako ndizo zimekuingiza huko, …nilijua kabisa hayo hayana mwisho mwema, na nakuomba uendelee kuwa hivyo hivyo,…na wazee wanajua kuwa wewe haupo hai, sasa ukijitokeza sasa hivi watashituka sana na uanweza ukawaua…sijui kama mizumu yao inajua hilo, na kama inajua labda imeamua kufanya hivyo kwasababu za maalumu…’akatulia kwa muda

‘Hapana, hapana…usifanye hivyo mapema hivyo, hakikisha huko ulipoharibu umepaweka sawa, hasa….hapana sitaki kabisa ijulikane kuwa wewe ni ndugu yangu mapema hivyo, usijibadili mpaka uhakikishe mambo yamemkuwa shwari, uhalisia wako usijulikane mpaka mambo hayo yaishe, yakiisha ndio tutaweza kusawazisha mambo yetu,…’akatuli tena kuskiliza.

‘Wazee wetu hawana matatizo, wewe siunajua masharti yao,…ndio,… mimi nitaondoka leo kufuatilia biashara zangu, sitakuwa na muda wa kuongea na mke wangu kwa hilo, lakini kama kweli ni mapacha nitalijua tu, nahisi ndio mama mambo yangu yalikuwa hayaendi vyema, lakini kwanini wazee hawajaniambia hilo…ndio ni imani na masharti yake yalikuwa hivyo,…ndio lakini ndizo zimenifanya nifikie hapa nilipo, ndizo zimefanya wazee wetu wakawa matajiri, kama kweli wangelikuwa damu yangu, ningepata shida,….’akatulia tena kwa muda akisikiliza kwa makini.

Mama akaangalia saa yake na kuona kapoteza muda mrefu pale alipokuwa akimsikiliza mume wake na hizo stakabadhi ni muhimu sana huko anakokwenda, na ili achukua hizo stakabadhi lazima aingie humo ndani, na kwasasa hakutaka kabisa kuonana na huyo mumewe, kwani wakionana ni lazima kutazuka mvutono hasa kutokana na hayo mazungumzo aliyoyasikia, …anakumbuka walipoachana walikuwa wameagana kabisa kuwa siku hiyo hawataonana, kwani mume wake alikuwa akisafiri,….sasa afanyaje na hizo stakabadhi ni muhimu sana, …mara akasikia mume wake akisema.

‘Haya tuayaache kwasababu sijafuatilia hilo, labda nikirudi nyumbani …ila cha muhimu kwasababu nimeshamuandikisha huyo Rose kama mwanangu, na sina jinsi, itabidi awe hivyo tu, huyo mwingine mimi simjui, na hata hivyo, …ooh, hilo niachie mwenyewe, kwasababu nimemuandikisha kisheria, na ikibainika hiyo italeta picha mbaya, siunajua tena…lakini ili mali hizo zirudi kwenye familia jaribuni kumfuatilia huyo Rose, hakikisha unamshawishi kwa njia zote, umpate…’ akatuli akwa muda.

‘Haijalishi ukimuoa itaharibu nini, kuwa sisi ndugu tumeoa, mama na mwana,…haha, hilo nalo jambo, lakini hayo hayana maana sana, …ukishaoa, ukahakikisha mambo safi, lakini hilo lifanyike kabla haijajulikana kuwa wewe ni ndugu, ukirudi kwenye uhalisia, unapotea , kama ulivyopotea watu wakajua umekufa, au sio, mke atabakia mjane, lakini kila kitu umeshakiandikisha kwenye familia kwa jina lako la uhalisia, au sio, unarejea kwenye uhalisia, hayo mengine yatafuata baadaye..’ akatulia halafu akasimama na kusema kwa hasira

‘Hilo sitaki kusikia, kwanini wewe ushindwe, wewe mwanaume bwana ….sikiliza, huyo mgonjwa yupo kitandani, sawa, fanya ufanyalo umtumie yeye kama chambo, basi ..najua kama kweli anampenda atakubali tu…tunachotaka ni upenyo wa kisheria, na mwezi mmoja tu unatosha…’ Akatulia kidogo na mama akapata nafasi ya kuwaza, ina maana huyo mtu anayeongea naye wana udugu na mume wake, atakuwa ni nani…ni…hapana, mbona hawafanani kabisa..mmh, …

‘Ndugu yangu, kwanza nashukuru kuwa umefanya kazi yako vyema, lakini ninachokuasa ni hilo kundi, achana nalo mapema sana…ooh, sidhani kuwa wana uhakika na wewe, na hata kama wakiwa na uhakika na wewe, sura yako kamili hawaijui,…jitoe huko, na njoo kwa sura nyingine.., sawa huo utaalamu wako unaujua wewe mwenyewe, mimi sio mtaalamu wa mambo hayo…hakikisha hakuna anayejua, kama yupo hakikisha anatoweka…sawa…’akatulia.

‘Ndio hivyo siku ya kurudi kweney sura yako halisi ikifika, wewe rudi nyumbani, lakini lazima kwanza uhakikishe kuwa huyo binti kakubali, na hayo mengine hayatakupa shida, …nilishakuambia, ili tuweze kuweka mambo yetu sawa, hakikisha huyo binti anakuwa wako,…, hakuna kinachoshindikana katika hii dunia, ni akili zetu tu, ...ok, fanya hivyo tutawasiliana baadaye basi maana nachelewa.. baadaye….’ akakata simu na kuchukua briefcase yake.

Mama alisogea mbali na pale na kuhakikisha kuwa mumewe hamuoni, mumewe akatoka haraka akiwa anaonyesha kukasirika, na pia alikuwa mara kwa mara akiangalia saa yake kuonyesha kuwa anachelewa huko anapokwenda, alifunga mlango na bila kugeuka pembeni wala nyuma akakimbilia lifti ya kushuka chini. Mama alipohakikisha kuwa mumewe kaondoka, akaingia ndani na kuchukua stakabadhi zake alizokuwa kazisahau huku mwili mzima ukimtetemeka ….

*****

‘Vipi mbona unaonekana kuwa na mawazo mengi, una wasiwasi na Rose nini….kama kaitwa kikazi ndio kuwajibika huko, napenda sana watoto wanaojituma namna hiyo, na hiyo kazi ndivyo ilivyo, anaweza akaitwa hasa usiku wa manane, mimi naona tusubiri akirudi tutaendelea na mazungumzo yetu, kwa sasa sijui ukatutembeze nje kidogo….’akasema Shangazi.

‘Mhh, moyo wangu haujatulia, akili yangu inanituma vinginevyi, hapa nilipo nina wasiwasi sana, siamini kuwa Rose kaitwa kwa ajili ya maswala ya kikazi, huyu binti kajiingiza kwenye mambo mazito, bila haya ya yeye kujua, na wakati mwingine najuta kuwa mimi ndiye niliyemsukuma katika matatizo hayo, lakini hata hivyo sikujua, ….ni shinikizo la mume wangu…sasa nahisi huko alipoitiwa huenda ndio hawo watu,…’akawa kashika kichwa akiwaza kwa makini.

‘Tatizo gani hilo, mbona unatutisha, na huku ni nchi za watu, hatujui lipi ni lipi, angalau wewe unakujua vyema, sasa tutasaidiaje na hilo, tatizo, kwanza tuambie haraka ni tatizo gani…’akauliza shangazi kwa wasiwasi

‘Kama kweli nilivyosikia ni sawa, kuna tatizo kubwa, lakini nyie hamuwezi kufanya kitu, hilo linatakiwa kutatuliwa kifamilia, ni katu yangu na mume wangu, …haya mengine, nitajua nikifika huko, lazima nimfuatilie huyu Rose kwanza….’akasimama na kuangalia saa, halafu akachukua simu na kutafuta namba, akapiga simu, huku akirudi kukaa, lakini ilionekana kuwa simu hiyo haipatikani, akatulia na kuonyesha kuwa anawaza kitu kwa makini, baadaye akasimama na kusema;

‘Naomba mnisubiri hapa , inabidi nimfuate huyu binti, huko alipokwenda, lazima nikahakikishe kuwa kweli kaitwa huko hospitalini au ndio kaingia mtegoni, tatizo lake huyu binti ni haambiliki, hata kama ningelimkanya asingelisikia, akiamua mambo yake, basi….nyie naomba mnisubirini hapa …’akasema yule mama na kutoka haraka, wakabakia Maua na shangazi, wasijue la kufanya.

‘Shangazi mbona naona tunaachwa kwenye njia panda, …tutakaa hapa kusibiri tu na huku mama kasema kuna tatizo, lazima na sisi tufanye kitu…’akasema Maua huku akisimama na kuangalia dirishani.

‘Wewe unataka tufanye nini kwenye nchi hii ambayo hatujui tuingilie wapi, na tutokee wapi, ukumbuke masharti yetu ya kukaa hapa, tumekuja kwa minajili ya kumuona mgonjwa,….ni kweli ilivyo inonyesha kuwa kuna tatizo, lakini tutafanya nini…’akatulia kidogo na mara wazo likamjia, akasema;

`Kweli inabidi tufanye jambo, na nimekumbuka kitu, unakumbuka Inspekta alitupatia namba yake ya simu kuwa, kama kuna tatizo tumwambie, labda nimpigie simu tusikie atasema kitu gani, ingawaje yupo mbali, lakini alisema wao wana mtandao wa kimataifa wa kupambana na uhalifu na magaidi..’

‘Shangazi hilo wazo ni zuri, lakini tuwe makini, tusie tukawatia matatani hawa ndugu zetu, kwasababu wao sio magaidi, ….huenda hilo swala wanalofuatilia au tatizo hilo halitaki polisi, watu wenyewe hawaeleweki….’akasema Maua, lakini shangazi hakumsikiliza akainuka na kumwambia wakaombe kupiga simu, hapo maulizo.

‘Shangazi…’akalalamika Maua lakini shangazi hakumsikiliza wakatoka mle hadi sehemu ya kupigia simu.

Walipoipiga ile namba, ikachhukua muda kuunganishwa na baadaye akaongea moja kwa moja na Inspketa. Inspekta alipojua kuwa anaongea na wao, alionyesha kufurahi sana, na haraka hataraka aliulizia hali ya mgonjwa…akaambiwa bado hajazindukana walipomuona mara ya mwisho lakini wanatarajia kwenda kumuona baadaye kidogo, halafu shangazi akaanza kuelezea lengo la kumpoigia hiyo simu…, na mashaka yao.
.
‘Unasema Rose alipigiwa simu na akaonyesha mashaka fulani, baadaye akainuka haraka, na kudai kuwa kaitwa hospitalini, lakini mama yake akawa na mashaka naye, akainuka haraka na kumfuata huko alipo, akidai kuwa huenda anaingizwa kwenye mtego, lakini hamkujua kuwa ni mtego gani , …ok, ngoja niwasiliane na watu wangu wa huko, … watajua nini la kufanya, …msiwe na wasiwasi, kwasababu hilo linafanyiwa kazi,…hapa nilipo nilikuwa nawasilina na watu wangu…’akasema Inspekta.

‘Lakini wewe uko huko mbali, mtajuaje nini kinachoendeela huku, wasiwasi wetu ni kuwa hawa ndugu zetu wanaweza kuingia kwenye matatizo, na hatujui tutawasaidiaje,…’akasema Shangazi.

‘Kama nilivyokuambia kuwa hilo linafanyiwa kazi, nyie msitie shaka, hata kabla hamjanipigia simu, taarifa hizo nilishazipata, na hawo watu wanafuatiliwa kwa karibu sana, na uzuri wameingia kwenye anga za watu wenye uzoefu na mambo hayo, ni swala la muda tu, wote wataingia kweney mikono ya sheria,…’akasema Inspekta.

‘Sawa, tunachoomba ni usalama wao , maana sisi tumekuja huku kwa ajili ya kumuona mgonjwa, sio kwasababu hizo, na isije ikamhusu na hata huyo mgonjwa, maana nasikia toka huko alikuwa akitafuwa na watu wenye nia mbaya…’akasema shangazi.

‘Msijali, huyo mgonjwa na Rose, ndio mtego wao, sasa hivi wanatapatapa tu, wamejisahau kuwa za mwizi ni arubaini, na huenda tunavyozungumza hivi watakuwa wameshakamatwa, msitie shaka, na kaeni na amani msiwe na wasiwasi…’ akasema Inspekta.

‘Sawa sasa sisi tufanye ninim tukae tu hapa tusubiri…?’ akauliza shangazi.

‘Sasa militaka mfanye nini, kumbuka Maua na Rose wanafanana, matatizo ya Rose yanaweza yakamgeukia Maua, na ikaleta mkanganyiko, noi bora make hapo msubiri…’akasema Insepkta.

Wakamaliza hayo mazungumzo na kutoka kuelekea kwenye chumba chao walichofikia, wakati wanatembea kuelekea huko, shangazi akawa akiangalia nyuma mara kwa mara, na hisia zake zikawa zimekubali kile alichokiona, alikuwa kamshuku mtu ambaye alikuwa mara kwa mara anawachunguza, na hata wakati wanatembea kurudi vyumba walivyofikia, akamuona huyo mtu akiwafuatilia kwa nyuma, …shangazi akaingiwa na wasiwasi, akamwamia Maua wasirudi chumbani kwao, waondeoke hadi huko hospitalini, wakasubirie huko,…..

‘Kwanini shangazi, …lakini hata mimi nahisi mwili ukinisisimuka, kuna mtu nimemuona, sio mara ya kwanza kumuona, nahisi kama anatuchunguza…’akasema Maua.

‘Hata mimi nahisi hivyo, lakini usijali, twende tukapande taksi…’akasema shangazi huku akiangali nyuma kwa wasiwasi mara kwa mara hadi walipotoka nje ya jengo, na walipokuwa wamesimama kusubiri taksi, mara wakamuona yule jamaa yupo nyuma yao…

Ni mimi: emu-three

14 comments :

Anonymous said...

Yaani hizi picha unazoweka zinanifurahisha sana,maana huwa zinaelezea kitu unachoandika kwa siku hiyo,Big up sana,unakipaji.

Rachel Siwa said...

Duhh baraka zizidimiminika juu yako na familia pia,kazi yako inatisha ndugu wa mimi,PAMOJA SANA TUU!!!

chib said...

Tunakutakia na heri ya mwaka mpya 2012

Faith S Hilary said...

Nimepita kukutakia heri ya mwaka mpya, bado naendelea mpaka nifike hapa :-)

emuthree said...

Wamimi(swahilli), chib na wangu(candy) nawashukuruni sana na kuwatakia mwaka mpya mwema wenye fanaka na baraka!

Anonymous said...

I comment whenever I especially enjoy a article on a site or if I have something to contribute to the discussion.

It is a result of the passion displayed in the article I
browsed. And after this post "Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-69 Hitimisho 13".
I was actually moved enough to leave a thought ;) I do have 2 questions for you
if you do not mind. Could it be simply me
or does it look as if like a few of the responses appear like left by
brain dead visitors? :-P And, if you are writing on additional places,
I would like to keep up with you. Could you list every
one of your shared sites like your linkedin profile, Facebook page or twitter feed?

Anonymous said...

Appreciating the hard work you put into your blog and detailed information you present.
It's good to come across a blog every once in a while that isn't the same old rehashed material.
Fantastic read! I've saved your site and I'm including your RSS feeds to my Google account.


Also visit my website instagram

Anonymous said...

I leave a comment whenever I appreciate a article on a site or I
have something to contribute to the conversation.
It's triggered by the fire communicated in the article I read. And after this article "Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-69 Hitimisho 13". I was excited enough to drop a thought :-P I actually do have a couple of questions for you if it's
allright. Is it simply me or does it give the impression like a
few of the remarks appear like left by brain dead individuals?
:-P And, if you are writing at additional social sites, I would like
to follow anything new you have to post. Could you make a list the complete urls of all your shared pages like your linkedin profile, Facebook page or twitter feed?

Anonymous said...

lovely jubbly fantastic thanks so much

Also visit my blog post: accident claims

Anonymous said...

lovely jubbly fantastic thanks so much

Feel free to surf to my web-site payday loans

Anonymous said...

hello miram3.blogspot.com admin did you know how exactly big corporation websites get massive targeted traffic and exposure in google's top page listings for the most competitive keywords?
Her's answer how you can get same massive targeted traffic to your website and it is straigtforward -

high PR backlinks - http://get-high-pr-links.com, but only quality backlinks which counts as votes for your site giving search engines no option but to shoot your website rankings to top results so your customers can see your website at the top of Google search results. Today is your lucky day because I’m going to reveal you secret place of greatest of the best high pR backlinks from 500’000 website network!
*buy high pR backlinks from actual PR page websites with very low outbound links max 10
* Skyrocket your website rankings for your related search term and obtain insane laser targeted traffic. Buy backlinks at http://get-high-pr-links.com
your friend Rebeka.

Anonymous said...

Hi miram3.blogspot.com admin have you wondered how exactly large company sites get large targeted traffic and exposure in google's top page listings for the most competitive search terms?
Her's solution how you can get same massive targeted traffic to your blog and it is straigtforward -

high PR backlinks - http://get-high-pr-links.com, but just quality backlinks which are considereed as votes for your website giving Google no choice but to shoot your website rankings to results so your customers can find your site at the top of Google search results. Today is is moment of truth because I’m going to reveal you secret place of greatest of the greatest high pR backlinks from 500’000 website marketplace!
*buy Links from actual PR page websites with low outbound links maximum 10
* Skyrocket your website rankings for your relevant keyword and obtain massive laser targeted customers. Get high pr links at http://get-high-pr-links.com
your friend Rebeka.

Ahmad Fahrurozi said...

Thank you for nice information
Please visit our web:
Ahmad Fahrurozi
Ahmad Fahrurozi

Ahmad Fahrurozi said...

Thank you for nice information
Please visit our web:
Ahmad Fahrurozi
Ahmad Fahrurozi