Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Saturday, December 17, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-66 hitimisho-10



Maua alipozindukana na alipofungua macho tu kitu alichokiwaza ni kuhusu ile ndoto, na macho yake yalikuwa yameganda kuangalia mlangoni ambapo kila mtu mle ndani alikuwa akiangalia huko kwa mshangao,...na baada ya muda watu wengine wakageuka kumwangalia yeye pale alipolala, na hapo ndipo akaanza kukumbuka ile ndoto,... na wakati kumbukumbu za ndoto hiyo zikigubika fikira zake, akawa anajaribu kuangalia huku na kule, ili ahakikishe ukweli wa ile ndoto, kwani ndani ya ndoto ile alijiona akiwa kizimbani, akishitakiwa kwa kosa la kumuua mumewe, na ushahid mbalimbali ulishatolewa, sasa ilikuwa zamu yake ya kujitetea, Lakin cha ajabu hakimu alikuwa yeye mwenyewe akijuhukumu mwenyewe.

‘Haya Maua unapewa nafasi ya mwisho ya kujitete, ukijua kuwa kuua ni makosa na adhabu ya kuua nawe ni kuuliwa, tunakupa dakika chache za kujitetea kabla adhabu yako ya kifo haijafikia…’akasikia hakimu akisema, na hakimu mwenyewe ni yeye mwenyewe.

Maua akajarubu kusimama kizimbani, lakini mwili wake ulikuwa hauna nguvu, hakuweza kusimama, ilioekana kama vile miguu na mikono yote vilikuwa vimevunjwa vunjwa, akataka kuuliza kwanini imekuwa hivyo, na ile sauti ikamjibu hata kabla hajauliza.

‘Wauwaji kawaida ni lazima wavunjwe vunjwe viungo, ili wasije wakapata nafasi ya kukimbia, wewe jifanya tu kama umesimama kwenye kizimba, sisi tutakuona, …’akashangaa hayo maelezo na kweli alipijifanya kasimama kwenye kizimba, akajiona kama kweli kasimama pale, alafu akaambiwa haya jitete, maana muda unakwisha. Akawa anagwaya gwaya, akiangalia njia ya kuitetea, akaangalia mlangoni ili kama kuna upenyo akimbie, …

Na wakati huo huo, Maua alikuwa akifikiria ajiteteeje, kwani hakuwa na cha kusema, ushahidi uliotolewa ulionyesha kuwa yeye kaua, lakini hakumbuki lini alifanya hivyo, akawaza aseme nini, aseme kuwa hakumbuki kufanya hivyo, hata akisema hivyo atauliwzwa shahidi wake ni nani, akageuka upende wa kushoto kwake, akamuona Adam, akitabasamu kwa dharau huku akisema bila kutoa sauti, nikubalie matakwa yangu, nami nitakusaidia kuwa shahidi .

Maua akauliza matakwa gani, akajibiwa umeshahu kuwa tulikubaliana kuwa tutaoana, na mimi nitakuwa tayari kukupa kila kitu hata kukusimamia katika kesi yako hiyo, umesahau kuwa mimi na wewe tulipanga njama za kumuya mumeo, ili nikuoe mimi, sasa sema umekubali mimi nikuoe, ili nikusaidie kukutetea….Maua akaondoa macho yake haraka kwa mtu yule.

Akageukia upande wa kulia akamuona Maneno, katulia kimiya, hasemi kitu, lakini uso wake ulionyesha alama ya kushangaa, alikuwa akijiuliza kumbe kaoa mke muuaji, hakuamini yale aliyosikia, na macho yake yaliyoonyesha kukata tamaa, na mara nyingi alitaka kusiki kauli ya Maua kuwa atajiteteaje, ili asionekane kuwa yeye ni muuaji.

‘Maua tunakusubiri wewe ujitete, na muda ukiisha tutachukulia kuwa una kiburi, umeua na umetakiwa ujitete., lakini umekaa kimiya…’akaambiwa, lakini kila alipojaribu kuinu amdomo, mdomo haukufunguka, akawa anajiuliza atajiteteaje wakati madomo haufunguki, au anachotakiwa ni kujifanya anajitetea kwa kuwaza yale yakuongea…

Kooti, Maua unahukumiwa adhabu ya kifo, kama ulivyomuua mwenzako, …akasiki asauti ikisema, na hapo kauli ikamjia ghafla na kusema, ….`sijamuua mimi mume wangu, mume wangu yule pale hajafa…’ na hapo akazindukana.

Maua alipofumbua macho akajikuta kazungukwa na watu warefu wamevalia mavazi meupe, na kila wakiongea meno yao yalikuwa meupe marefu, na kila kiuongo chao kilikuwa na ukebwa wa ajabu, akaanza kluogopa akijua ndio hawo waliokuja kumuua kama alivyoambiwa kuwa kamuua mume wake, akainuka kutaka kukimbia, na wale watu wakamshikilia kwa nguvu, ikawa mshike mshike, na mara macho yakaondoa kile kiwingu na kujiona yupo kashikiliwa kitandani.

‘Zawadi yako ni hii, …’akasikia sauti ya mwanamke ikiongea, na hiyo sauti ikamfanya mwili wake usisimukwe na kuinuka kutamani kumuona huyo muongeaji ni nani mbona alikuwa miongoni mwa sauti alizozisiki azikitoa usahidi kuwa yeye ni muuaji, na kwahiyo anastahili kunyongwa, akawa na hamu ya kumuona, na hapo akainua kichwa na mara kwa muda huo akaona watu wote wakiwa wanaangalia mlangoni, akamuona….

Alimuona yule Maua aliyemuona kwenye ile ndoto akishitakiwa kuwa ni muuaji wa mumewe na muhukumu wa kesi hiyo akiwa ndio yeye mwenyewe Maua, akashangaa na kujiuliza akilini, ina maana ile ilikuwa sio ndoto, akajiangalia jinsi alivyosimama pale mlangoni, huku watu wakiwa wamemkodolea macho, akasema kumbe kweli ilikuwa sio ndoto, kaua na anatakiwa kuuliwa, akiwa kashikwa na butwaa huku haamini, kuwa kweli anasubiri kunyongwa akataka kugeuka upande ule ambao kwenye ndoto,ulionyesha maiti ya mumewe ikiwa imelazwa ka ushahidi, na kabla hajafnaya hivyo, mara akawaona watu waliokuwa wakiangaliana mlangoni wamegeuka kumwangalia yeye na hapo hapo akasema kwa sauti ;

‘Siyo mimi ni yule…’

Docta ambaye ambaye alikuwa akimshughulikia, yeye alikuwa muda wote anamwangli ayeye na kumpimapima, lakini aliposikia sauti ya huyo mgonjwa ikisema sio mimi ni yule, akageuka na kuangalia kule mlangoni, akashikwa na butwa, na mara akamgeukia Maua pale kitandani kuhakikisha, Maua akasema tena, nimewaambia `sio mimi ni yule kule, sio mimi kabisa…, docta akasema; `kweli sio wewe, usiwe na wasiwasi…’

***********

Shangazi na wifi yake waliposikia mgonjwa wao kitandani anaongea na ule mshangao wa kuona huyo aliyeingia mlangoni, wakainuka pamoja bila hata kuambiwa, shangazi yeye akitaka kueleeka kule alipolala Maua, lakini mwenzake akwa kashikwa na kigugumizi, aelekee wapi kwanza, na yup hasa ni Rose,

`Wifi tell me who is Rose, …niambie ni nani Rose, ni yule kule mlangoni au ni huyo huko kitandani…?’ akauliza.
Shangazi akacheka na kumwangalia kwa makini, halafu akamuuliza `je ni yupo mwanao kati ya Rose na huyo mwingine…’kabla hajaendelea kuongea, wifi yake akasema.

‘Na Maua…of course, wote ni wanangu, na wote nina uchungu nao, lakini ninachotaka kujua ni yupo aliyedondoka hapo sasa hivi, ili nijue kipi cha kuongea, ili nisionekana emjinga mbele ya wanangu mwenyewe, nashindwa kutofautisha, nisaidie haraka…’akawa anamnong’oneza sikioni wifi yake, na waifi yake akanyosha mkono na kusema `kwanza nipe zawadi yangu, ahadi ni deni…’

‘Aaah, zawadi yako nimesahau, akachuku apocho na kutoa ufunguo, …’akainua juu na kusema

‘Hilo ni gari jipya kabisa la kisasa, na gharama za kulisafirisha juu yngu, usiwe na
wasiwasi,….haya niambie yupi ni Rose na yupi ni Maua, tafadhali, maana hapa natamani kulia, sijawahi kujiskia hivi kabla…’na kweli machozi yakaanza kumbubujika.

‘Unalia nini sasa, sasa unajifnya unahuzuni, hukumbuki sike ile upo chumba kile unasubiri nikuletee mmojawapo, ukawaita majina mwenyewe, ….’shangazi akasema.

‘Ndio niliwaita mwenyewe majina yao, Rose nikamchukua na Maua ukamchukua wewe, sasa…ooh, tufanyeje hapa , maana wote wanahitaji maelezo, na sikutarajia wote watakutana pamoja, na inaniwia vigumu…haijatokea hali kama hii, kushindwa kujua nini ha kuongea, hapana,…’ akasema wifi mtu, na wakati huo, yule aliyekuwa mlangoni akawa anaingia, na hakutaka kujua nini kimetokea, hakutaka kujua kwanini watu wanamuangalia, hakutaka hata kuongea na mama yake, akafululiza kuelekea kule alipolazwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji.

Shangazi akawa kasimama na wifi pia, wakasogea mbele, na kuwafanya wasimame kati kati ya huyu anayeingia na kitanda cha yule mgonjwa, ….

‘Hebu mzuie asieje na yeye akazimia…’akasema shangazi.

‘Kama ni Rose , sina wasiwasi naye , kwani yeye ni Docta, ..’akasema wifi na shsngazi akamtupia jicho huyo binti, alishangaa, nguo ile ile aliyovaa Maua ndio hiyo hiyo aliyovaa huyo binti mwingine, hata nywele zilivyofungwa, inagwaje wote waliamua kuzifunika na kitambaa chepesi, lakini kila kituu kilikuwa sawa sawa, ila yeye alikuwa kagundua kitu kidogo sana, wakati aanwachukua pale lkitandani na hiyo peke yake ndiyo inayoweza kuwatofautisha, …hakuna mwingine anaijua…

*********
Rose aliharakisha kuingia pale hospitalini, na alipofika akamuulizia docta wake ambaye aliwasilina anye kwenye simu, akaelekezwa wapi alipo, na kwa haraka akaelekea huko, alipofika kweney chumba chake, mara akakutana na docta akitoka mbio mbio, na alipomfikia akashituka na kusimama ghafla, …na kabla hajasema kitu nesi wake akamshika mkono na kumwambia mgonjwa yupo huku kazimia…

Basi yule docta akasema; tafadahli nisubiri hapo nakuja…’akamwambia Rose na kukimbili ahuko alipoitiwa. Rose akabakia pale kwa muda, na moyoni akasema yeye ni Docta, kwanini asimame pale badala ya kutoa msaada hata kama sio hospitali yake , lakini kutoa msaada ni muhimu, akaelekea kule walipoingia nesi na yule docta.

Rose alipofika mlangoni akasita kuufungua kwanza, akikumbuka kuwa aliambiwa amsubiri huyo docta kwenye ofisi yake, akatizama nyuma, na hapo akamuona mlinzi akimjia, akamsubiri kwanza asikia atamwambia nini, na yule mlinzi akamwambia kuwa huko ndani kuna mgonjwa anahudumiwa, na pia wameshaingia watu wengi isivyo kawaida, asubiri kwanza kidogo.

‘Mimi mwenyewe ni docta, ninamuhitaji doacta mwenzangu, na kama kuna msaada wa kidakitari naweza hata mimi kusaidia, naelewa unachoniambia, lakini pia tunakwenda na muda, au sio..ngoja niingie, kama inawezekana na mimi nitasaidia hilo linalowezekana …’akasema Rose, na kabla yule mlinzi hajasema lolote, kwani alishaanza kulalamika, yeye hakujali, akausukuma mlango na kuingia ndani,…

Alijikuta kwenye chumba kikubwa, na chakwanza ilikuwa kufauta wapi mgonjwa wake lipo, kwahiyo akazungusha macho kwa haraka ndani ya kile chumba na kumuona, lakini hata hivyo, alijikuta akishiwa butwaa kwanza, kwa jinsi alivyoona watu mle ndani, maana wote walimgeukia kumwangalia kama vile ni mtu maalumu, akawaza su mimba yangu imeshaanza kuwa kubwa nini, hakujali akaangalia kule pembeni kwenye mashine ambapo mgonjwa anayemfuta akalzwa, na macho yalipoangalia ile mashina, akajua kuwamgonjwa wake hana matatizo.

Lakini akagundua kuwa kuna magonjwa mwingine,amabye kwa muda huo alikuwa akihudumiwa na yule docta aliyemwambi asubiri, kwa jicho la haraka akaangalia kama anaweza akatoa msaada wowotea, akaona hahitajiki, maana pale kulikuwa na docta na wasaidizi wawili. Kuna kitu alikigundua kwa haraka kuwa huyo mgonjwa pale kitandani kavaa nguo sare kabisa na nguo alizovaa ..hakuweza kumuona vyema usoni mwa huyo mgonjwa kwa sababu docta alikuwa kamziba, hakujalai hilo, kwa muda huo akasogea kwa msahaka, kuelekea kwa mgonjwa wake…

Kila aliposogea aliona watu wakimwangalia kwa mshangao, akajiuliza kwanini hawa watu wananishangaa, hakutaka kuwaangalia watu wote waliokuwemo mle ndani, lakini kitu kimoja kingine kilichomvuta awaangalie baadhi yao, ….ni kuwa alimuona mama yake, alikuwa kasimama na mama mwingine wakiongea kwa kunong’onezana, inaonekana wanajuana, oh, hakutaka kabisa kukutana na mama yake humo ndani, maana anamjua sana mama yake huyo, badala ya kusema maneno mema, wataanza kubishana na mwisho wa siku ataihia kulaumiwa mbele ya mgonjwa wake, …akaona hapo sio mahala muafaka hata wa kumdsalimia, ngoja akamuone mgonjwa mara moja, atoke akasubiri kule alikoambiwa asubiri.

Alipofika katikati ya chumba mara akamuona mama yake na mama mwingine wakija na kusimama mbele yake..akataka kuwambia kuwa ana haraka ataongea nao baadaye, lakini macho yake yakageuka na kuangalia kile kitanda kingine, akijaribu kutafuta uso wa wa yule mgonjwa, lakini ilikuwa sio rahisi maana madakitari walikuwa wamemzunguka, akaona haina haja, ila kafurahia uvaaji wake maana ni kama yeye…, akajiangalia tena yeye mwenyewe alivyovaa, akatabasamu, na kusema, tumevaa sare, na ingekuwa vyema tungelifanana pia, …akageuka na kuwaaangalia mama yake na huyo mama mwingine, akatikisa kichwa….na kabla hajasema kitu mara mlango wa mle ndani ukafunguliwa akaingia mtu na kusimama katikati ya mlangoni…

Ni wakati huo huo Maua naye alikuwa keshatulia na alikuwa kaamua kutoka pale kitandani na kusimama, docta akamruhusu kuwa anaweza kuondoka, naye mawazo yake yalikuwa kule kwa yule mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji,akagueka kuangalia muelekeo wa kile kitanda alicholazwa huyo mgonjwa na akawa anageuka kuelekea huko alipolazwa huyo. Shangazi alishamuona akataka kumzuia, lakini docta akamwambia amuache tu, hakuna shaka…
Rose aligeuka na kumuona yule mtu aliyesimama pale mlangoni, na mara moja akamtambua, akaanza kuingiwa na wasiwasi, moyoni akasema ndiyo yeye kaja tena huku, sasa atafanya nini, achukuea hatua gani , kabla hajasema kitu yule mtu akashika kwenye eneo la kiuona, Rose akaelewa ana maana gani, alikuwa akihakikisha kuwa silaha yake ipo au anataka kuitoa hiyo silaha na hapo inamaanisha kaja kwa shari…akamua kumsogelea docta na nia yake ni kumwambia kuwa `yule aliyesimama pale mlangoni ni jambazi anataka kumdhuru mgonjwa kabla hajamfikia yule docta akasikia akilini mwake sauti ikisema…

‘Rose , usifanye lolote, kumbuka uhai wa mgonjwa wako upo mkononi mwako…’ akamgeukia yule mtu aliyesimama mlangoni, lakini cha ajabu alimuona yule mtu kapigwa na bumbuwazi, anashangaa..alikuwa akimwangalia yeye na mara anamwangalia yule mgonjwa alyekuwa kalazwa kitandani ambaye sasa kainuka anaeleeka kule alipolazwa yule mgonjwa wa aliyefanyiwa upasuaji, na hapo ndipo Rose naye akagundua ukweli , kwanini yule jamaa alikuwa kashikwa na butwaa, na yeye akashikwa na butwaa..

NB Zawadi ya jumamosi hiyo, kutatokea nini hapo, tuzidi kuwemo, tukimalizia kisa hiki hiki, je kuna sehemu tumesahau? Kuna mtu kanishauri ninunue moderm, bada la ya kiguu na njia kwenye internet cafe..sijajua gharama yake na kama nitaimudu!

Ni mimi: emu-three

3 comments :

samira said...

m3 tupo pamoja na swala la moderm ni zuri muhimu ungeuluzia na sisi wapenzi wako tukakuchangia ingawa nipo mbali ya tz lakini naweza kutowa mchango wangu

Anonymous said...

asante kwa zawadi nzuri ya jmos.tuko pamoja

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Wallahi hadithi hizi tamu zimenipita nikiwa napigana vita vyangu...Nisamehe mkuu!
==============>
Nilikuwa napita hapa kusema kwamba sasa nimerudi tena rasmi. Tupo pamoja !!!

http://matondo.blogspot.com/2011/12/wanablogu-wenzangu-na-wapenzi-wote-wa.html