Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, December 15, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-64 hitimisho-8
Shangazi na Maua walipofika hospitalini, waliingia moja kwa moja hadi sehemu wanaposubiria watu kuingia kuwaona wagonjwa, kwasababu walishafikihs taarifa zao kuwa wanakuja kumuona huyo mgonjwa, haikuwa na shaka kwao, kwahiyo walisubiri muda wao ufike, kwasababu taratibu zilivyo pale, humuwezi kingie watu wengi kwa pamoja wanatakiwa watu wachache wachache, na wakati wamekaa kusubiri huo muda dakitari anayeshughuli na mgonjwa wao akafika.

‘Nyie ndio akina nani, maana nimeambiwa kuwa …mmh, ok... basi subirini kidogo, maana kama nilivyokuambia mgonjwa bado hajafiki hatua ya kuzindukana vyema, keshaonyesha hiyo dalili, ila kichwa hakijaa vyema,…kwahiyo nawaomba mkiingia msimsemeshe, nyie mwangalieni tu, halafu kama mtataka kusema nay eye msubiri baadaye sana….sawa, haya karibuni huku…’akasema yule dakitari huku akimuacha Maua akiwa yupo nyuma, akiwaangalia watu wawili aliowahi kuwaona kule hotelini.

Wakati wanaingia ndani mara yule docta akapokea simu, na wakati wanaongea na huyo mtu kwenye simu, akasema;

‘Docta Rose, kwani kuna matatizo makubwa, ni nani huyo, …nitawaarifu polisi, maana dunia hii imeharibika,…’akakata simu na kuongea na sehemu nyingie kuonyesha kuwa anaongea na polisi na baadaye akawageukia shangazi na Maua, akasema ingia chumba hiki, na kama nilivyowaambia msimsemeshe huyo mgonjwa, mtamkuta docta mwenzangu atawasaidia ngoja, nina jambo la kufanya mara moja.

‘Shangazi kuna mtu ana jina la Rose, umemsikia huyo docta akisema, ….na inaonekaan kuna matatizo yanamkabili…halafu shangazi wale watu niliokuamabia wanaonekana kama wanatufuatilia nimewaona wakiwa hapo mapokezi, kila mara wanatutupia macho…nahisi uwoga,isije ikawa wanatufuatilia mimi, na jinsi alivyoongea huyo dakitari inanitia wasiwasi, na alivyoniangalia kama vile ananijua au alitaka kusema jambo….’akasema Maua kwa sauti ya pole pole wakati wanaingia ndani.

Ndani ya kile chumba alikuwepo dakitari akimalizia kazi zake za kumweka sawa yule mgonjwa, akatizam mashine ya kupumulia na ile iliyopo ukutani ikionyesha alama za mapigo ya moyo, na baadaye akawageukia Shangazi na Maua akasema;

‘Mgonjwa hali yake ni njema kabisa, keshaonyesha dalili za kuzindukana, lakini hatutaki asumbuliwe na ningewashaur, kama hamtakuwa na uvumilivu mumuangalia mara moja halafu mrudi baadaye…’akasema yule dakitari, na shangazi akakubali na kumsogelea yule mgonjwa, na wakati huo Maua alikuwa kasimama mbali kidogo kwenye mlango.

‘Maua wewe usimsogelee mgonjwa , ngoja kwanza nimwangalia mwenyewe kwanza…’akasema shangazi na Maua akakubali kwa shingo upande na kusimama mbali kidogo, ambapo huwezei kumuona mgonjwa vyema kwa jinsi alivyolazwa.

Shangazi alipofika pale kitandani alipolazwa mgonjwa, mapigo ya moyo karibu yasimame, lica ya kiwa sehemu kubwa ya kichwa imefunikwa na vitambaa, lakini usoni alioekana dhahiri, akasema kwa sauti ndogo; `kweli hikuwa jinamizi siku ile, ndio yeye…’akatabasamu, lakini moyoni akawa na mshaka makubwa, akasema tena kwa suti ndogo; `utusamehe sana, kwasababu kila mmoja alijua wewe ni marehemu, na mengi yaliyotokea sio makosa yetu, …nasikitika sana kuwa yaliyotokea yametokea, naomba uyakubali tu, kama yalivyo, mungu akujalia upone …’akamsogela na kmgusa mkono, huku akikumbuka siku ile ya harusi alipofika, …

Alikuwa kasimama mlangoni, akigonga, na nia yake ilikuwa kumgongea Maua kuwa anakuja kama yupo tayari, kwani muda ulikuwa karibu unafika ingawaje alipta taarifa kutoka kwa mpambe wake, kuwa amewasilina na msfara wa bwana harusi watachelewa kidogo, ndio maana yeye hajafika mapema huko alikokwenda wasiwe na wasiwasi.

Hakupendezeshwa na hiyo hali ya Maua kubakia peke yake kwa muda mrefu, akaona ni vyema aingie ndani avae na awe naye hadi atakapokuja huyo mpambe, na akiwa anagonga mlango akahisi kuna mtu kasimama nyuma yake, ..na cha ajabu alihisi mwili ukimsisimuka, na kwa uzoefu wake kuna jambo lislo la kawaida, akageuza kichwa taratibu kuangalai nyuma yake, huku akiomba dua yake anayoijua ya kujikinga na mabaya.

‘Shikamoo shangazi, naomba uwe na moyo wa ujasiri, na uikubali hii hali ya kuniona mimi kama kawaida, ingwaje wengi inawashinda, nakuomba sana, utilize moyo wako, ..mimi ni….’ Kabla yule mtu hajamaliza kuongea, shangazi alishaanza kutimua mbio, lakini alitulia hatua mbili akasimama na kugeuka kumwangalia tena yule mtu, huku akijiuliza kama nikikimbia na kumuacha mwanangu na hili jinni au mzuka, itakuwaje kwake.

‘Wewe ni nani na kama umekuja kwa nia mbaya potela mbali huko ulipotoka, nakijinga na ubaya wako…’akaanza kusoma dua yake ya maombi, lakini yule mtu akasema kwa sauti ya chinichini..

‘Shangazi usipoteze muda, kwani kwa taarifa nilizozipata ni kuwa Maua anaolewa na rafiki yangu Maneno, na nilikuwa naomba niongee naye kwa dakika chache, kwanza ni kutaka kujua kweli kaamua kwa moyo wake iwe hivyo, na pili ni kumtaarifu ukweli waangu kuwa sikufa kama nilivyoskika watu wakiongea, bahati nzuri nilioongea nao hawanijui kama wangelikuwa wananijua kungetokea matafaruku, na anomba wasinijue wengi, kwani hata ndugu zangu sitaki wanijuw akwa hivi sasa,…tafadhali shanagzi, mimi sio mzuka, jini au kibwengo, mimi ndiye haswa…nimponea kimiujiza ya mungu.

‘Wewe ni mhuja kweli…?’akauliza kwa sauti ndogo.

‘Ndio mimi shangazi , niliponea nchi ya jirani, nikawa naishi huko bila kuwa na kumbukumbu yoyote, hadi majuzi tu, nilipopata fahamu zangu, nikasafiri kibahati hadi hapa, yote yaliyotokea huko kwa ujumla siyajui, kwasababu kwa muda mwingi nilikuwa sijijui,..ndio maana sikuweza hata kuwapigia simu, nashangaa mwenzangu hakuweza kuvumilia na kuamua kuolewa, imekuwaje shsngazi hadi kunifanyia hivyo….?’ Akasema Mhuja,

Shangazi kwa kuchelea kuwavuta watu kuja hapo, akamvuta pembeni huyo mtu, na kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeweza kuwaona, na akaanza kumhoji vyema, ili kuhakikisha kuwa huyo ni mtu kweli au ni jinamizi la mtu, akikumbuka tukio la yule Tajiri, na alipomhoji na hata kujaribu kurizika kuwa kweli huyo ni mtu, wala sio jinamizi, akasema kwa kauli ya kusua sua;

‘Mhu-ja , bado naogopa hata kutaja jina lako, maana sijaamini,…ni muda umepita na sijui kwanini , hata simu… ila nakumbia hivi, haya yaliyotokea ni mapenzi ya mungu, na kilichopangwa na mungu huwezi kabisa kukizuia, sio kweli kuwa mwenzako alishindwa kuvumilia, ungelijua kazia aliyopitia hadi kufika hii leo usingelisema hayo kabisa, na nakuomba, umuachie kabisa aolewe, kama kweli unampenda, nasema hili kama shangazi yako, vinginevyo, …anaweza hata kujiua, nakuomba ukubali hilo, na kwanini nasema hivyo, ipo siku nitakusimulia mwenyewe, lakini sio leo,…’akasema shangazi, ambaye walijuana vyema na Mhuja na alijua Mhuja atamuamini, kama kweli ndiyo yeye.

‘Shangazi wewe nimekuchukulia kama mama yangu na katika watu ninaowaamini wewe ni namba moja, na uisemapo jambo lako naliheshimu sana, ..lakini nakuomba tafadhali,na mimi nakuomba unisikilize na uniamini kama tunavyoaminiana, naomba tafadhali, ningelifurahi, angalau nionane na Maua, …kwanza nina hamu ya kuona sura yake, kama kweli ndiyo yeye, maana akili yangu imeingiwa na utata fulani, …’akasema huku anatikisa kichwa kama vila anaondoa kitu fulani kimeganda kweney ubongo ambacho hakieleweki.

‘Pili shangazi nataka kusikia kauli yake mwenyewe , nataka kuskia kutoka kwenye kinywa cheke Maua akitamka kwa mdomo wake, kuwa kweli kakubalina na ndoa, ili moyo wangu uridhike, ..najua kama mumefiki hii hatua, sitaweza kugeuza kitu, hasa ikizingatiwa kama nlivyosikia anayemuoa ni rafiki yangu mpendwa, …’ akasema huku moyoni akiwaza, kuwa kama ataamua kuweka ubabe na kusema hakuna ndoa hapa, mimi ndiye mume halali, matokeo yake kutazuka mgongano, na vyovyote iwavyo, hawatakuwa na mahusiano mema tena kati yake na rafiki yake.

‘Nimewaza mengi shangazi, …na inabidi nikubali kushindwa ili kuondoa migongano, ….hayo yote nimeyawaza kwa undani, lakini hata hivyo ndoa yangu ipo, …na mimi ndiye natakiwa kuivunja, kwahiyo kabla haijafikia hatua hiyo naomba nionane na Maua, nitaongea naye kidogo tu, akitoa kauli ninayoihitaji, basi nitaondoka bila kupingamizi…nakuahidi hilo shangazi’akasema Mhuja, lakini shangazi hakukubali kwa haraka, kwanza bado alikuwa hana imani kuwa huy mtu kweli ni mtu haswa.

Walibishana kwa muda hadi shangazi akaona haina haja ya kumzuia ndipo wakakubaliana kuwa aingie aongee naye na asilete kipingamizi chochote na akubali kuivunja hiyo ndoa, kwasababu kubwa ambayo shangazi hakutaka kuisema, lakini Mhuja alijua ipo sababu kubwam ndio maana shangazi akafiki auamuzi huo, na moyoni alisema lazima ataitafuta hata kama kakubali kuivunja hiyo ndoa, …hata kama itachukua miaka mingi lazima atarudi kuja kuulizia ni kwanini akatendewa hivyo…

Baada ya muda mwingi wa Mhuja akiwa ndani akiongea na Maua, shangazi aliingiwa na wasiwasi na ilionyesha dhahiri kuwa msafara wa kuona unakuja, na wakati ule mpambe alishafika, lakini, shangazi akamuita pembeni na kumwelezea mambo mengine, ili kupoteza muda, na alipoona muda unazidi kuisha akamtuma mpambe kiujanja kuwa akanunua kifaa fulani duka la jirani, halafu akwagongea Maua na Mhuja, na hata kuufungua mlango, kuwaMhuja atoke.

Mhuja alitoka akiwa kanyong’onyea, kabisa kuonyesha kuwa alikuwa hajapata jibu alilolitaka, yeye akamvuta pembeni na kumwambia aondoke maeneo yale, na yeye bila ubishi akasema;

‘Shangazi nimekubali ombi lako, najua una sababu ya msingi, ingawaje nitaumia sana, ila ipo siku nitarudi, na nahitaji maelezo ya kina, nimekubali kuivunja hii ndoa kutokana na wewe na pia Maua hakuwa tayari kunijibu swali langu,najua ni kwasababu ya mshituko,bado hajaamini, natumai akiniona mara ya pili ataamini….hata hivyo, sina ubaya naye, kwasababu nampenda sana, na nitaendelea kumpenda kwa moyo wangu wote,…najua shangazi huwezi kunifanyia hivyo kama kweli hakuna sababu nzito, naitaka kuijua hiyo sababu, hata kama sio leo…nakwenda huko nilipotoka, nikija tena nataka kuijua hiyo sababu…’akasema Mhuja.

‘Ipo Sababu kubwa sana,…. tafadhali kubali na hili, na vunja ndoa yako, na nakuomba uondoke haraka iwezekanavyo, kwani nakuhakikishia kuwa ipo sababu kubwa sana, niamini hivyo mwanangu,mimi nisingeweza kukubali jambo kama hili litokee, niamini hivyo…’akasema shangazi huku machozi yakimlenga lenga.

‘Sawa nimekuamini shangazi,…hata hivyo tafadhali msimwambia Maneno, au ndugu zangu kuwa mumewahi kuniona, kwani inabidi nirudi huko, nikaage, na kujua nini kilitokea, najua kuna watu nina deni nao, na…nakumbuka kuona jambo kubwa huko ambalo nataka kwenda kulihakikisha, …najua kuna mtu ananisubiri sana,ngoja nirudi huko kabla hakujahribika. Na naahidi kuwa nikiwa tayari, nitakuja tena kuonana na nyie, hasa kwako na Maua….’akasema na kuondoka huku naye machozi yakimlenga lenga, hakuamini kuwa ni kweli...

Baadaye shangazi akawa kama haamini, kuwa kweli huyu mtu alikuja kwake, aliona kama ilikuwa ni jinamizi au ndoto, kwani kilichomshangaza zaidi ni pale alipokwenda kuulizia kwao, na kujikuta watu wakimshangaa, na walipomuulizia zaidi akasema aliota ndoto kuwa kamuona huyo jamaa, na yeye mara nyingi akiota ndoto zinakuwa kama kweli, watu wakiishia kumcheka, na akiwa njiani kurudi kwake akawa anawaza hilo tukio, na kujiuliza kwanini hakuta kuwaona ndugu zake kama kweli alikuwa ni yeye, mwisho wa siku alichukulia kama ni moja ya majaribio tu yalitokea ambayo alitakiwa kuyasahau, kama kweli yupo hai atakuja tena, kama ni jinamizi, basi liishie huko huko lilipotokea.


‘Nawaombeni msimwambie chochote rafiki yangu, nina maana, rafiki yangu Maneno au hata mkionana na ndugu zangu msiwaambie lolote kwa hivi kwa sasa, kwani sijajiandaa kwa hilo, hata hivyo afya yangu bado ni tete, sitapenda kuja kuwaumiza mara ya pili....’ haya maneno yalimkaa sana kichwani kila mara anapotaka kusema lolote kuhusu huyu mkwewe aliyepotea, na yalikuwa yakimuumiza sana moyoni.

Shangazi alijitahidi sana kutokusema lolote, kama alivyoahidi hata kumshauri Maua naye kutokusema lolote kwa Maneno kuwa alionekana mtu kama Mhuja, na hapo alijaribu kumuonyesha Maua kuwa huyo anaweza aisiwe ni Mhuja, ni mtu kaja anafanana naye na kurubuniwa tu, kwahiyo asiwaze sana kuhusu kuwepo kwake, labda itokee mara ya pili.

‘Lakini mimi nimemuona kwa macho yangu, na akasema mumeongee na kukubalina hili, kweli shangazi tunyamaze hivihivi, mimi naona kuna haja ya kuwaambia ndugu zake, ili atafutwe …’akasema Maua.

‘Utawaambia yupo wapi, na je una uhakika kuwa ndio yeye, na kama ndio yeye, mbona umekubali kuolewa na mtu mwingine…na hata hivyo, mwenyewe katuomba tusiseme lolote, na hiyo inaonyesha kuwa kuna jambo, au kama ni yeye kweli, ana maana yake…timiza wajibu kama alivyoweza kutimiza wake, kwa amepnzi yake kwako, akaacha kuleta fujo, au kufanya lolote, na wewe kaaa kimiya…sawa?’ akasema shangazi mtu.

Na wote wawili wakakubalina kukaa kimiya, na hili kweli lilifanikiwa hadi pale walipokutana na Inspekta alipoileta hiyo taarifa ya kuwa yupo mgonjwa nchi ya jirani. Na huyo mgonjwa huenda anwahusu, kwani alielezwa na Inspekta kama mume wa Rose, na hili jina likawa chachu ya kugundulika mengi yaliyokuwa yamejificha ndani ya hii familia.

‘Shangazi vipi nije hapo na mimi nimuone huyo mgonjwa, maana nakuona unaongea peke yako…?’akauliza Maua na kumfanya shangazi ashituke toka katika lindi la mawazo mazito, na wakati huo huo,aliuona vidole vya mkono vya yule mgonjwa vikitikisika na hapo akawa kama kashikwa na mshituko na kigugumizi, huku moyoni akisema, `sio wakati muafaka wa kuonana uso kwa uso na huyo mgonjwa’, akaanza kurudi kinyume nyume.

‘Kwa hali niliyoiona hapa wewe usije kwanza huku kaa hapo hapo, …unajua Maua nakushauri, twende kwanza tukirudi baadaye ndio utamuona huyu mgonjwa, …hasa akizindukana, … nakuomba unielewe hivyo Maua, wewe huhitajiki kupata mshituko wowote kwa sasa, …umenielewa Maua, kaa hapo hapo…’akasema shangazi na wakati huo alikuwa akirudi kinyume nyume hatua moja moja bila kuangalia nyuma, kwani akili yake ilikuwa ikitafakari kuhusu huyo mgonjwa, na alipogeuka kumwangalia Maua akajikuta ypo naye sambamba na macho yake yakiwa yanaaanglia kitandani.

‘Wee Maua mbona hunielewi, nikmekambiaje, sasa unaona…ohh, balaa hili sasa..’akasema shangazi akiruka kusimama mbele ya Maua ili asiweze kumuona huyo mgonjwa pale kitandani, lakini alikuwa keshachelewa, macho ya Maua yalishatua kitandani na akiiona ile sura…sura ikamwingia akilini, ….

‘Oh, jamani kumbe ndiye yeye…oh,….’ Maua akasema maneno hayo, na alipojaribu kuvuta subira, ikakataa, na ingawaje wakati huo shangazi alikuwa keshawahi kusimama mbele yake lakini hikusaidia kitu, alishaoana, giza likatanda machoni na kujikuta akielea hewani,…shangazi akamdaka, lakini uzito ulikuwa mwingi kwa shangazi ,wote wakaenda chini, …

‘Sasa hili balaa ndani ya nchi ya watu, sasa…’shangazi akawa anahangaika kuinuka na kumweka sawa Maua na mlango ukagongwa na kufunguliwa, shangazi alipoinua uso kutizama aliyeingia, akajikuta akiziba mdomo, kwa mshangao na kutahayari…!

NB: Mambo yanaelekea mwishoni, unaonaje seheu hii, je unaweza kukisia aliyeingia ni nani?

Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Nahisi aliyeingia ni Dk Rose

emu-three said...

Rose kapata kura moja wengine mnasemaje unahisi ni nani aliyeingia humo?

Anonymous said...

wow ni rose kaingia huyo pls m3 tupe utamu

Anonymous said...

huyo ni rose kaingia dah pameishia patamu.

Swahili na Waswahili said...

Duuhhh ndugu wa mimi,yaani wewe ni mwisho duuhh mtu wangu Mungu akubariki sana tuu,Pamoja ndugu yangu!