Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, December 14, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-63-Hitimisho-7




Rose nguvu zilimuishai kabisa, kwani ile sura ni ngeni sana kwake, ..ana midevu mirefu, na alipotoa ile miwani machoni alionekana mtu wa kutisha, na ile sura ina fanya mwili unasisimuka kwa woga. Akawazia mbali kuwa huenda ni hao magaidi aliwahi kusikia wapo maeneo ya huku, ambao wanaweza kulipua hoteli, akamwangalia kwa makini, kuona kama anasilaha nyingine zaidi ya ile bastola, hakuona kitu kingine…

‘Haya hebu niambieni maana kazi niliyowapa nimeifanya mwenyewe…’akasema kwa sauti ya kikakamavu, ambayo ilioneakan kikwaruza, ni kama mtu kaweka kitu mdomoni, ili kupoteza lengo la sauti ya sili, …akawa anasikiliza kwa makini hiyo simu upande wa pili, na akageuka kumwangalia Rose, huku anasikiliza anachoambiwa, alionyesha uso wa mshangao…halafu akageukia upande mwingine na kusema ;

‘Mna uhakika na mnachokisema, umesema amevaa nguo gani, ?’akauliza na kumgeukia Rose, huku usoni akizidi kuonyesha uso wa kushangaa, huku akimkodolea macho Rose, na kusema kwa hasira

‘Hivi kwanini mnanichezea shere, hayo mnayozungumza mumeyafanyakuyakariri kuwa kava nguo hizo, ili mje mnidanganye mimi, mna uhakika kweli mnayoyazungumza, eti unasema unasema amevaa nguo ya pinki ya Kihindi, na mumemuona akipanda kwenye taxi na mama mmoja, wakati nipo naye hapa, msinichezee, …naona kuwa hamtaki kazi, …’akafoka, na aliposikia yale wanayomuelezea kwenye simu akabakia kushangaa kila anachoambiwa, akaizima ile simu kwa hasira na kumuangalia Rose kwa muda halafu akasema;

‘Sshiti, ….hawa hivi watu hawanijui mimi, …’akageuka pembeni kama vile anamkwepa kumuangalia Rose usoni moja kwa moja kusema tena, `Ajabu kabisa wanasema kuwa wamekuona wewe Rose ukiingia kwenye taxii na mama mmoja, mkiwa mnaeelekea hospitaini, ina maana Rose mpo wangapi, hawa watu wananichezea kweli wanafikiri mimi ni mjinga, sifuatilii kazi zao…’ Akamsogela Rose ambaye alikuwa kasimama akiwa kakunja uso kwa hasira, akaangalia saa yake....

‘Wewe ni nani na unataka nini kwangu, naomba usinicheleweshe,…’akasema Rose na kumwangalia kwa makini, akagundua kitu, kumbe ndio maana huyu jamaa alipokuja akigeuka pembeni kwa muda akawa anafanya kitu, zile ndevu zinaonekana hakuzibandika vyema, …

‘Nakuuliza tena wewe ni nani na unataka nini kwangu, maana naona umejaribu kuficha sura yako kwa kujibandika hiyo ngozi ya bandia, na sijui ni joto au ni kitu gani, kilishaanza kukuumbua,…’aaksema Rose, na yule jamaa akageuka pembeni na kujirekebisha vyema, halafu akasema;

‘Haijalishi utakavyo, kwangu mimi yote ni sawa, cha muhimu ni kukufikishia ujumbe …’akasema yule mtu huku akashika shika zile ndevu zake.

‘Ujumbe gani, na unataoka kwa nani..?’akauliza Rose, huku akiwa hajiamini, kwani kila mra akimwangalia huyu mtu anahisi nywele kumsisimuka, na ilionyesha kuwa huedna huyu anamfahamu, lakini akili yake ilishindwa kugundua ni nani…

‘Wewe kama ni jambazi au gaidi, huwezi kunifanya lolote, na sasa hivi nitapiga ukulele wa wizi au nipige simu polisiwaje kukuchukua, najua watagundua kuwa hiyo sura uliyovaa siyo ya kwako…aliendelea kusema.

‘Sikiliza Rose, ujumbe niliotumwa kwako ni kwa mtu anayekupenda sana, amesema kuwa yote aliyokufanyia ni kwa vile anakupenda, hebu ujiulize ni nani angelichukua hatua zote hizo, ni nani amejaribu kuwa karibu nawe , .. hata kuhatarisha maisha yake , hata kuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yako kama yeye,..amefanya hayo yote kwa vila anakupenda sana Rose, …ujumbe ni kuwa vyovyote ufanyavyo, kokote uendapo, yeye atakuwa nawe, na anaomba kwa moyo wake wote ujaribu kumpa nafasi katika moyo wako…na hutajutia …’akasema yule jamaa.

‘Umemaliza …?’ akauliza Rose.

‘Nikitaka kuelezea yote hayo nitamaliza siku nzima, ndio nimemaliza kwa hilo, ila lipoo jambo jingine , ambalo ni muhimu sana…’akasema yule mtu.

‘Jambo gani hilo, maana sioni la maana lililokuleta hapa hadi kunionyeshea bastola, san asana ni kunipotezea muda wangu bure, tafadhaki toka nifunge mlango, nawahi …’akasema Rose akimuonyeshea yule mtu kidole kuwa aondoke.

‘Usinilazimieshe kuondoka, naweza kufanya lolote na nisipate lolote, nina uazoeufu nah ii, kazi tulia nimalize kazi iliyonileta, unasikia sana, na sema hivi, zile pesa ulizozitumiwa na ukaona ni vyema kuwasaidia wale wasiojiweza, anaulizwa nani alikupa hicho kibali, je kama mwenyewe atazihitaji hizo pesa zake utazirudishaje…wewe utumie pesa tu, ambazo hujazifanyia kazi, au niambie umezifanyia kazi gani, mapaka ulipwe pesa zote hizo, kwanini hukutafakari kaba ya kuchukua hatua hiyo…?’akauliza yule mtu huku akishika shika pale alipoweka ile bastola yake.

‘Sikumbuki kabisa kumuomba pesa huyo mtu, kama alizitoa hizo pesa kwangu, hilo alilifanya kwa utashi wake mwenyewe, na mwambie namshukuru sana, na kama anazo pesa nyingine anitumie tena, kwani bado wapo wagonjwa wengine wanazihitaji sana…na huenda pesa kama hizo ni jasho lao,…’akasema Rose, na kumfanya yule jamaa amwangalia kwa hasira, halafu akatabasamu, …lile tabasamu, …likamshitua Rose, na kuanza kuhis jambo, akaanza kumhisi kuwa huyu mtu anajifanya kutumwa, lakini huenda …

‘Eti jasho, lao, mtu anahangaika usiku kucha , anazalisha anapata pesa zake ,anataka kuziwekeza, ….Rose, hizo pesa zimetoolewa kwa kukuamini kuwa ukizipata utazitunda hadi hapo utakapoambiwa nini cha kufanya, ni kwasababu huyu mtu anakuamini, anakupenda, na hukutakiwa kuzitumiwa kama ulivyofanya wewe, lengo lake lilikua kinyume na ulivyofanya na hata kama ungelikuwa na nia hiyo, kama mtu mwenye busara, ungeliomba ushauri kwanza…’akasema yule mtu, huku akiangalia huku na kule, na alionyesha kuwa hana waiwasi na anachokifanya.

‘Ningeliomba ushauri kwake, ningelimpatia wapi huyo mtu, wakati alishatoweka, akijua anataka kukamatwa, alifikiri atafanya mamb yake bila kujulikana,..au mlitaka na mimi nikamatwe kwa kuambiwa nipo kundo moja na nyie,…nyie kweli watu wa ajabu, mnafikiri kila mtu ni gaidi, kwanini nisumbue watu, niue watu kwa tumbo langu, maslahi yangu, mimi najali watu na nchi yangu… mnajidanganya kweli, na kama ningeliwajua mapema ningelishawashitakia…lakini hata hivyo kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho…’akasema Rose kwa kujiamini.

‘Sawa, hamuwezi kujua nini tunakifanya kwasasa hivi, sisi tulikuwa ndani ya nchi, wengi walikuwa waajiriwa, wameona nini kinfanyika, watu walikuwa wakishibisha, wao wenyewe, ubinafsi na utawala mbovu, ndio uliotusukuma kuufnaya mambo kama haya, na mwishowe mtaona mabadiliko, lakini mabadiliko hayo yametokana na vuguvugu letu, hilo hamtaliuunga mkono, kwasababau ya propanda potofu, lakini tulichokianza kimefanya kazi yake, pindi hivi mtaona maabdiliko,…’akasema na kutulia kidogo, Rose akatulia kumskiliza.

Ila unacholaumiwa nacho ni hatua uliyoichukua,kwanini usingelimuomba mwenye pesa hizo ushauri kwanza,…dharau au sio, lakini yote hayo ujue kuwa huyo mtu anakujali na kukupenda lakini wewe hutaki kabisa kumfikiria vyema…kumbuka hizo pesa ulizotumia ni nyingi sana…na hata ukipewa muda wa kuzilipa hutaweza kumlipa,…cha muhimu ni wewe kmfikiria ombi lake, ..na utafaidi pesa hizo na nyingine zaidi bila masharti…’akasema yule mtu huku akishika kiuona kuonyesha kuwa anazo.

‘Hilo sahau, kama alifanya hilo, akitaraji malipo ya kupendwa, sizani kuwa ni sawa, mapenzi hayanunuliwi kama nguo, mapenzi ni utashi unaotoka moyoni, na kwangu kwa ajili yake hakuna kitu kama hicho. Ninakuomba umwambie kuwa mimi simtaki atafute mtu wa aina yake, sio mimi…kwanza anatafutwa na polisi,..na na…’Rose akawa anamwanglia yule mtu kwa makini, na huku akiendelea kuongea kwa mashaka, akijiuliza nini kitafuata baada ya hapo, aliombea simu ipigwe au mtu apige hodi, ili apate upenyo wa kufanya lolote.

‘Sikiliza Rose, usifikiri kuwa ulichofanya hakikuwa kinajulikana kuwa utachukua hatua hiyo..lakini…’akasema yule mtu kwa ukali na Rose naye akamkatiza kwa ukali

‘Mwambie huyo aliyekutuma, kama yupo huku, kaja kujificha huku, asijidanganye maana mkono wa sheria ni mrefu, atakamatwa tu, na asipende kuniingiza katika hali ya kufikiriwa kuwa hata mimi ni mshirika wake, watu wamekuwa wakihisi hivyo, kwa vile nilikuwa karibu naye, kuwa eti nashirikiana na yeye kwenye kazi zake za ujambazi, mimi sio gaidi, kama yeye ni gaidi asifikirie kila mtu ana uchu huo wa tamaa za kibinafsi…mwambie kabisa nikitoka hapa nawapigia simu polisi kuwaambia kuwa nimekuona …wewe…maana nahisi ndio wewe ..’akasema Rose. Huku akimwangalia kwa makini, na huku moyo wake ukimdunda kwa mashaka.

‘Hilo usisumbuke, na wala usipoteze muda wako kuwapigia hawo polisi, lakini kama unataka kufanya hivyo endeela chukua simu yako wapigie, hauzuiwi, ila nakuhakikishia kuwa hawawezi kumkamata mtu kama yule, yeye ni kama kinyonga, …Rose, pesa ulizotumiwa kwako hazikuwa na maana ya kutoa msaada, zilitumwa kwako kama njia, au sehemu ya kuzihifadhi kwa ajili ya mipnago mingine, wewe umevuruga,…umeharuibu kila kitu, sasa unafikiri hatua gani itachukuliwa juu yako, …swali ni je utazilipa kwa namna gani , vinginevyo itakuwa sehemu ya makubalioano,!’akasema huyo mtu akionyesha kuwa kakasirika.

‘Makubalino gani, jibu nimeshakupa mapema, kuwa sikuwahi kumuomba hizo pesa, kwahiyo mimi sijui na sikuwahi kuandikiana mkataba naye kwa mambo kama hayo….anajua au unajua mikataba ilivyo, wapi tuliandikishiana , kwa vipi…hapo asinilaumu bure, na mimi ningelikaa kimiya unafikiri nini kingefuata,kama sio na mimi kukamatwa…chukuenai hatua yoyote muitakayo, sijali….’ Akasema Rose akijitahidi kujiamini, lakini moyoni alikuwa na mshaka mashaka.

‘Ni rahisi sana kusema hivyo, lakini hujui nini ulichokifanya, kwani mwenzako alishahisi kuwa huenda ukafanya hivyo, na nini kitafuta baada ya hapo,…na unachotakiwa ni kujiandaa na hatua itakayochukuliwa, huenda isikuguse wewe moja kwa moja, lakini maumivu yake hutayasahau, na mwisho wa siku utakuja kumpigia huyo jamaa magoti, …hilo nakuahidi, utaona matokeo yake sio muda mrefu, …cha muhimu, ili kumuokoa huyo unayemuhangaikia ni kuolewa an mfadhili wako, basi, jamaa yako hatadhurika…’akasema yule mtu, na kumfanya Rose acheke kwa dharau.

‘Eti nini, nyie mnakimbilia kumuumiza mtu asiye husika, au sio, jaribuni muone, …mnafikiri hata mimi sijajiandaa kwa hili, sio mimi yule mliyekuwa mkimbabaisha kule nyumbani, kusoma kwangu nimejifunza mengi, na nipo tayari kufa kwa ajili yanchi yangu, ..nyie mnakimbilia watu wasio na hatia..huo ni unafiki, ni uwoga,…mwambie huyo jamaa asijidanganye, na asiwe moga, aje apambane na mimi mwenyewe,sio anakimbilia wagonjwa, watu wasio na hatia..hui ni uoga,…na kwanini mnakuja kufanya fujo kwenye nchi za watu…?’ akasema Rose

‘Hayo yote yameshafanyiwa kazi, ni kweli tupo kwenye nchi za watu, usiwe na wasiwasi , hili nikukuonyesha kuwa popote utakapokwenda au jamaa yako atakapopeelkwa kutibiwa au kuficha sisi tupo sote, tupo nyuma yenu, kila unapokwenda ujue nipo nyuma yako, ..hadi hapo utakapokubali ama kurudisha hizo pesa, au kukubali kuwa mtu mwenza wa jamaa yako, n ikwa nia njema, tu, sio kulazimisha,, ila nikukutakai maisha mema ya upendo na raha za utajiri…sasa sikiliza…’akasema yule mtu kwa ukali.

‘Sitaki zaidi nimekussikiliza vya kutosha, sasa amua fanay utakalo, mimi nataka kuondoka , unanipoteze amuda wangu…’akasema Rose kwa hasira.
‘Ooooh hilo ndilo tulikuwa taunataka, hatutaki kutumia nguvu kwa yule aiyetea nguvu itumike lakini ukitulazimisha utaona nini tunachokifanya, kama ndio huyo mgonjwa wako anayekutia kiburi, na humjui vyema, basi tutaona kiburi chako ukimkta maiti…kama maiti anaringiwa, haya endelea, cvha muhimu ni kukupa ujumbe, kuwa kama unajali uhai wake, basi msaidie kwa kumwambia aachane na wewe, mimi ndio ujumbe niliotumwa kwako….’akasema yule mtu na kutizama saa, na hapo hapo simu ya Rose ikaita. Rose akaipokea haraka na kusikiliza, na huku anamtizama huyo jamaa kwa makini.

‘Nakuja sasa hivi, kuna mtu ananichelewesha kidogo, lakini nipo njiani, kama nitachelewa nusu saa, naomba uwapigia polisi kuwa kuna jamaa katoroka huko Uganda na anatafutwa sana na polisi wa huko, kaja kujificha hapa, na ndiye …’kabla hajamaliza kusema yula jamaa akawa keshatoka mle ndani na kukimbilia nje, na ule mwendo ukamshitua Rose na kusema kimoyomoyo, huyu atakuwa ndiye yeye tu, anajifanya kusema katumwa na akasema kwa sauti….`nimeshakugundua wewe ni nani hata ukikimbia wapi…

‘Rose usipoteze muda wako kuwapigia simu hawo watu wako, na wala usipoteze muda wako kuwaambia chochote kuhusu mimi, nenda huko uendapo, lakini ujue nipo nyuma yako, na maisha ya jamaa yako yapo mikononi mwako….’

Rose hakujali alitoka mle hotelini kwa haraka na kulelekea hospitalini huku akijisikia vibaya vibaya,…na huku akiwaza hayo maneno `maisha ya jamaa yako yapo mikononi mwako…’ akaguna na kusema kwa sauti `wewe sio mungu, na wewe zako zinahesabika utakamatwa tu muda sio mrefu’. Lakini kwa upande mwingine moyoni mwake alikuwa akiona aibu kwa kutumia pesa za watu bila idhini ya mwenyewe, …je atawezaje kuzilipa, kwani sasa inabidi azilipe pesa za watu haraka iwezekanavyo, atazipata wapi pesa nyingi kama hizo…?

Rose akingia kwenye taksi, na alipoangalia nyuma akaona kuna gari linamfuatilia kwa karibu sana, mawazoni akajua ni huyo huyo mtu, na kwa muda huo hakujua afanye nini, angelikuwa nchini kwake angelimpigia simu Inspekta, ….akawaza hapa hajui nani ni nani ,achukua hatua gani, awafahamishe watu wa usalaam wa hii nchi, au anyamaze kimiya, na je ampigie simu Inspekta kuwa mtu wanayemtafuta yupo huku India au anyamaze kimiya..?

Kama akinyamaza kimiya akija kujulikana itaonekana alikuwa mshirika wake, na akiwaambia haraka haraka hivi inaweza ikampa shida, na huenda wakamdhuru mgonjwa. …akaona ni muhimu kwanza anyamaze kimiya asije akafanya jambo la kuharibu kila kitu, cha muhimu ni kujua kuwa mgonjwa anaendeleaje na kama ni kulipa hilo deni, itabidi awaangukie wazazi wake wamsaidie, lakini nipesa nyingi sana, zilizotumika, na wazazi wake hawatakubali kubeba mzigo wote huo , je sasa atafanyaje…?

Ni mimi: emu-three

12 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Hapa sasa naona kama mambo yanakuwa ya kulazimishana...ngoja nisubiri mwendelezo ila wee utamu kwelikweli...

emuthree said...

Dada Yasinta nashukuru kwa kua nami maana nilizania wapenzi wa blog híi wote wameenda kuhesabiwa makwao.
Jingine ni kua sehemu nitaiandika upya imehitimishwa haraka isome tena kesho tukijaliwa itakuwa tofauti kidogo na yenye mvuto!

samira said...

mhhhhh m3 natamani na mimi ningepata mtu akanilazimisha mapenzi akanipenda .... joke
nipo nawewe tunasonga mbele

Anonymous said...

mbona mi siwezi kuchangia yaani kila nizituma naona haziji sijui nakosea wapi

emuthree said...

Nawaombeni msome tena sehemu hii kwani imepata mabailiko baada ya kupata muda mzuri wa kuipitia na kuirekebisha, hivi ndivyo ilitakiwa iwe, mnasemaje?

Anonymous said...

Tuko pamoja,yaani natamani ungekuwa unatuwekea sehemu mpya kila siku,mungu akujaalie ili uzidi kutuletea mambo mazuri zaidi

emu-three said...

Kuna aliyeuliza jinsi ya kutuma maoni. Ukitaka kutoa maoni, unachotakiwa kufanya ni kwanza ni vyema ukawa na emil ya Google, halafu, unabofya sehemu iliyoandikwa comments, ipo chini kabisa unapomaliza kusoma story, na ukishabofya unafuta maelekezo , na mara nyingi utapata maandishi yaliyoandikwa kiajabu `word verification' yaangalie kwa makini na kuyaandika kwenye sehemu uliyoelekezwa

emu-three said...

samira said...

Mhhhhh m3 natamani na mimi ningepata mtu akanilazimisha mapenzi akanipenda .... joke
nipo nawewe tunasonga mbele.

Samira mimi nipo kwa ajili yako usikonde, nakupenda sana....

nb, wapendwa wa blog hii nawapenda sana, TUPO PAMOJA

emuthree said...

Anonymous said...

Tuko pamoja,yaani natamani ungekuwa unatuwekea sehemu mpya kila siku,mungu akujaalie ili uzidi kutuletea mambo mazuri zaidi.

NDUGU YANGU NATAMANI KUFANYA HIVYO HATA MM. LAKINI AMINI USIAMINI, HAPA NIPO INTERNET CAFE, NATUMIA ZAIDI YA ELIFU MOJA KILA UNAPOONA SEHEMU IPO HEWANI, KAMA NINGELIJALIWA KUWA NA SEHEMU YA KUJISHIKIZA NA KUPATA ANGALAU TANGAZO MOJA LIKANIIINGIZIA VIJISENTI, NINGELIWAFURAHISHA ZAIDI, LAKINI MUNGU YUPO, IPO SIKU, TUOMBEANE HERI

Anonymous said...

Je naweza kukuchangia hizo gharama ili nikupunguzie mzigo wa gharama japo ni kiasi kidogo lakini kitakusaidia.

emuthree said...

Nitashukuru kwa hilo 'kuchangiwa' ili kupunguza gharama lakini kabla ya kufanyika hilo kunahitajika utaratibu uliokubalika au sio,nimefurahi sana kwa moyo wako huo, ngoja kwanza niufanyie kazi!

samira said...

m3 dear unajitahidi sana nitakutafuta february nitakuwa tz niombee mungu
mungu akipenda tunaweza fanya mabadiliko kidogo usijali