Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, December 1, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-56




Maua alitaka kugeuka kuangalia ni kwanini aliyeingia hajasema kitu tangu muda wote huo, mwanzoni alijua kuwa huyo ni shangazi yake, ambaye alikuwa akiiingia mara kwa mara, ingawaje kuna muda alikaa muda mrefu bila kuingia na hapo ndipo ,Maua akaanza kupatwa na hayo mashaka,mashaka yaliyomtia hasira.

Au atakuwa mpambe wake, ambaye aliondoka muda, na kumuacha mwenza wake kwa muda mrefu Hapo Maua akaona azionyeshe hasira zake kinamna, ajifanye kudeka, kwa kukaa kimya, huku akiwa kalala kifudifudi na kufumba macho, akisubiri wao waanze kuongea, na hapo atajua nini cha kuwaambia…,ikawa kimiya hawasemi kitu na ulalaji ule ulikuwa ukimtesa, na hata kuwaza kama kuna kiumbe tumboni na ulalaji ule, unaweza ukaleta athari, kwahiyo akajigeuza kidogo na kulala kugeukia ukutani.

Maua alijua shangazi yake anavyompenda ataanza kwa kumbembeleza, lakini alijua kuwa akizidisha sana, anaweza akala viboko, …kwahiyo aliifanya ile kwa malengo maalumu na kwa muda fulani tu baada ya hapo atajua nini la kufanya, akasubiri muda aliouweka, lakini kulikuwa kimiya, hakusikia sauti ya shangazi wala mpambe wake. Mwili ukaanza kumsisimuka, akahisi kuna kitu kisicho cha kawaida, …

Alipoona kimiya kimezidi na muda wake alioweka umepita,akahisi kuna kitu kischo cha kawaida, akainua kichwa taratibu na kuangalia muelekea wa mlangoni,…hakuona vyema, …akainua zaidi na kuwa kama anajibinua, huku anaangalia mlangoni,...

Mara Moyo ukashituka,…mwili ukaanza kumsisimuka, akahisi uwoga fulani, ina maana Yule mtu ndiye kaingia,….hapana,...kaingiaje mle ndani asiweze kukutana na shsngazi yake, haiwezekani, ... akaanza kusikia mwili ukimuisha nguvu, lakini safari hii akasema hakubali, kama ni mwanga, basi yeye atakuwa giza nene lisilopitisha mwanga....nitapambana naye, nitapambane naye kama alivyofanya shangazi, na kuitwa mwanamke wa shoka. Mara akajiinua harakaharaka, na cha ajabu safari hii hakuiona ile dalili ya viungo kuisha nguvu, akasema kimoyomoyo , huyu sasa haniwezi.

Hata wakati ule anajitutumua kuinuka, akiwa anamuwaza yule Tajiri, kuwa ndiye aliyeingia, bado aliogopa kumwangalia huyo mtu, hakuwa anaangali mlangoni moja kwa moja, alikuwa kaangalia chini kwenye sofa, na huku akijaribu kuangalia kwa jicho moja huko mlangoni akaona miguu,…

Oh,kweli sio shangazi au mpambe, viatu, sio vya kike..akafuatilia kwa jicho hilo moja, kuelekea juu ooh, mbona kweli kvaa suruali, lakini hata mpambe wake hupendeela kuvaa suruali, na viatu vyake vilikuwa kama vya kiume, alipokuja mara ya kwanza, atakuwa mpambe nini….inawezekana mpambe wake, akasema kwa kujipa moyo, akasema huenda,mpambe wake, aliamua kuvaa suruali kwa ajili ya shughuli zake na baadaye atabadili na kuvaa nguo za kiharusi , akajipa moyo na kutulia kidogo, huku akijaribu kugeuza kichwa taratibu, ….alipoona kimiya kinazidi, akainuka mzima mzima na kuanza kusema;

‘Hivi ndio nini mnanifanyia hivi, kuniacha peke yangu muda wote huu, mnafikirii mimi nina hisia za mnyama au…hamuoni jinamizi la Yule nduli, Yule….jamani, kwanini mnanifanya hivyo….?’ Akaanza kusema kwa hasira, huku kafumba macho, ili asione aibu akiongea na wakubwa zake.

‘Mhhh, Maua…naona ulikuwa mbali sana, umesharizika nah ii hali, kuwa bibi harusi, au sio…?’sauti hiyo, ikamshitua na kumfanya afyumbue macho haraka, ili sisje ikawa ni ndoto,….akayafumbua macho yake haraka, lakini cha ajabu hakutaka kuangalia moja kwa moja, hata hivyo akili yake haikutaka kukubali haraka, haikuwezekana hakusikia vyema nini, mwili ukaanza kumuishia nguvu, safari hii sio kama vile mwanzoni alivyoishiwa nguvu na kushindwa kuinua hata mkono, safari hii ilikuwa kiajabu kabisa, akafunua macho na kuangalia pale sauti ilipotokea, kwa taratibu, na akamuona, …

‘Mzuka, shetani, ….’akajikuta akisema kimoyomoyo. `sio kweli wewe I mzuka au shetani, potea mbali….ushindwe na upotee….mung nilinde na kuniepushia na mashetani hawa wabaya….’akasema Maua kimoyomoyo. Halafu kwa sauti ya amshaka akasema;

‘Wewe ni nani, …tafadhali potea ,nakuomba mungu unilinde na …’akajikuta akianza kumuomba mungu kimoyomoyo , akijua hilo ni shetani limekuja kwa sura hiyo, huyo ni mzuka, kasimama pale mlangoni, na akijikuta macho yakizidi kumtoka zaidi zaidi na zaidi , yalimtoka kwa woga, yalimtoka kwa kutoamini, yalimtoka, akitamani na mdomo utoe sauti, lakini haikuwezekana, akawa katulia na kukodoa macho akiangalia kile kilichopo mlangoni, …

‘Maua tafadhali nakuomba unielewe, kwani muda uliopo hapa n mfupi sana, na nisingependa kuharibu kile kilichokusudia, nakuomba unilewe na utilize akili yako vyema….’akasema huyo mtu, au hicho kitu kilichopo mlangoni.

‘Nakuuliza wewe ni nani…unataak kufanya nini , kwanini hubaki huko kuzimuni,…kwanini unanitesa…..’akajikuta Maua akisema na sasa machozi yakaanza kumtoka, kwa wingi.

‘Maua najua hutaamini , hata kama ingelikuwa mimi labda ningelifanya kama ulivyofanya wewe, lakini yote ni mapenzi ya mungu, inabidi tuyakubali, lakini lazima tuwe na subira asa mitihani kama hii inapotekea, na kabla sijakuelezea kisa cha yaliyonisibu ningpenda nikuulize swali moja, ambalo unatakiwa ulijibu kwa makini, ….’yule mtu akasema huku akiwa bado kasimama pale mlangoni.

‘Maua akajiuliza huyu mtu, kama sio ni mzuka aliingiaje humo ndani, maana ili uingie mle ndani ni lazima upitie hapo walipo akina shangazi na watu wengine, aliwapitaje bila kuwaona, ndipo akaamini kuwa huyo ni mzuka, shangazi asingelikubali mtu kuingia mle hasa huyo, kwani sio binadamu, shangazi yake ni mkali wa vitu kama hivyo, kiimanii kaiva, haiwezekani, huyu ni mzuka katokea hewani, na huenda sio mzuka wa huyo anyemzania ni mzuka wa huyo tajiri, kaamua kujigeuza hivyo ili kumzuga na aingiwe na huruma.

‘Wewe najua ni tajiri Papa unataka kuvuuga kichwa changu, kwasababau ya uchawi wako najigeuza vile upendavyo, tokomoea huko ulipotoka,….tokomoea mbali, tokomoa mbali….’akajikuta Maua akisema, lakini cha ajabu sauti ilikuwa haimtoki vyema, hata pale alipojaribu kuongea kwa sauti ili shangazi yake asikie huko nje….

‘Maua mimi ndiye Yule Yule, na wala sio mzuka kama unavyozania, na swali langu ni muhimu sana kwako, ili dunia na nafsi yako iwe hury, `je una uhakika na unalotaka kulifanya, je unampenda huyo unayetaka kuoana naye, kauli yako ni muhimu sana, kwangu, ili name niwe hutu kwako, najua nitaumia, najua nitateseka, lakini kama moyo wake umesharizika, sina budi kukubaliana na hilo, na naomba ulitamke hilo ukiwa huru kabisa, je una mpenda huyo unayetaka kuoana naye, …?’akauliza Yule mtu.

Maua akabakia kimiya na kuanza kulia, sauti, ni ile ile, mwili ni ule ule….mbona nachanagnyikiwa, kwanini imetokea hivyo, kwanini itokee kwangu, kwanini….mungu wangu sasa nitafanyaje kama ni kweli, …haiwezekani iwe kweli, huu ni mmoja wa mtihani ,….haiwezekani, na hata kama ni kweli nitafanyaje,…’akainamisha kichwa na kuangliana tumboni, na mkono wake ukashika tumboni…

‘Maua kimiya bila kauli ni utata, lakini wahenga walisema ukikaa kimiya ina maana unasiki ahaya kujibu ulicho nacho na mara nyingi ni ishara ya kukubali, nshukuru sana, na huend andoto nilizoziota wakati nipo huko naeseka kwa mengi, zilikuwa kweli, kuwa wewe umeamua kunisaliti, na kulisaliti lile pendo letu tuliloahdiana, …kwa namna nyingine siwezi kukulaumu, maana hutokea hivyo, subira ni ngumu sana,na kuishinda inataka imani…ninachokuomba, usije ukamwambi huyo rafiki tyangu lolote…kabla sijasikia kauli yako, ngoja nikuhadithie kisa changu, nini kilinitokea, …

‘Mimi sijakusaliti…hujui ni mateso gani niliyoyapata hadi kufikia hatua hii,huenda ungelikuta kaburi, kama sio huyo…..anayetaka kunioa…sijakusaliti…oooh. Wewe umekaa niaka zaidi ya miwili, hata kupiga simu kutuarifu kuwa upo hai…siamini kwanza kuwa wewe ndio kweli….siamini, kwasababu ingelikuwa ni kweli, na ukatujali, …hata kama mimi uliamua kutonithamini tena, lakini wazazi wako, jamaa zako, ambao walifikia hata kusoma hitima mara mbili….ulishindwaje kupiga simu,…ooh , hapana sio kweli, wewe ni mzimu, .. kwanini itokee kwangu mimi, sina jinsi , nitafanyaje, maji yameshamwagika, nitafanyaje mimi….mungu wangu nisaidie…’Maua akaanza kulia.

‘Kisa changu kinaanzia mbali sana, nakuomba unisikiliza kwa makini, ili uone jinsi ilivyotokea, kukuonyesha kuwa sikufanya makusudi, ilitokea kwasababu sikuwa mimi , akili , na fahamu zote zilipotea, sikujijua kabisa, ninachoweza kusema ni kuwa akili zote na fahamu zilipotea na mara ziliporejea tu sikupoteza muda, haraka nikaja huku kukuona nikijua unanisubiri, unaitunza ahadi yetu ya ndoa,….sikujua kabisa kuwa nitakutana na mambo haya, …

'Maua nimeongea na shangazi akanielezea kwa ufupi, na nimeahidi kutimiza alichoniomba,ila kwa masharti ya kauli yako…kama bado una mapenzi na mimi, au ndio mapenzi yameshavunjika, sijaelezwa sababu nyingine ya muhimu . Au ipo sababu nyingine ya muhimu, uniambie, nataka kuisikia kauli yako, lakini kabla ya yote ningelipenda usikie kisa changu.

‘Kwasasa sizani kama kauli yangu itakuwa na maana yoyote, kwani mambo yameshaharibika…mambo kwasababu..mambo yameha…har….’Maua nguvu zikamwishia, akataka kudondoka, lakini, taratibu akajilaza kwenye lile sofa, akajikuta akilia, akiwa haamini anachokiona, aliomba iwe I moja ya zile ndoto, za kila siku, lakini hiyo haikuwa ndoto hata hivyo akili yake ilikuwa haijaamini.

‘Sikuelewi ukisema mambo yameharibika, kwasababu, bado mimi ni mume wako halali, …mambo gani hayo yaliyoharibika, ….Maua, miaka miwili ndio imekusinda…kuna nini cha zaidi umepewa mpaka kuivunja ahadi yetu…lakini sitaki kukulazimisha kwa hilo, maana, mpende akupendaye bwana, hata hivyo siwezi kujua rafiki yangu kwa kakupa nini, kakufaa nini wakati wa shida , wakati ukiteseka, ….Je upo tayari kusikiliza kisa changu, au huna haja nacho, nakuahidi kuwa kauli yakoo nitaiheshimu sana, kama kweli umebadilika na kutoamua kutonipenda mimi na kumpenda rafiki yangu, basi , nitafanyaje….labda …’akasema huyo jamaa.

‘Nakuomba sana usiseme hivyo, kwani name yaliyonikuta sio kama unavyozania, sawa anitasikiliza hicho kisa chako, lakini…..’akasema Maua huku akihisi tumbo likimuuma, akalishika, huku akiwazia mbali, je amwambi ukweli kuhusiana na hilo, haamui hivyo kwasabaabu kuwa hampendi, anaamua hivyo kwasababu ya kiumbe kisicho na hatia,….akamwangalia jamaa, ambaye hadi muda huo hakutaka hata kumuita jina lake maana akili yake ilikuwa haijaamini kuwa kweli ni yeye, haiwezekani, …

‘Sikiliza Maua ninachoomba ni wewe usikilize kisa changu ili uone jinsi gani ilivyokuwa, sikumbuki baada ya kuzama meli ilikuwaje, nakumbuka pale ilipozama, na hapo kumbukumbu ziliponijia kwahiyo nitakuhadithia nini kilitokea kwenye meli, hadi nilipozama kwenye dimbwi la kupotewa na fahamu, maana hapo sijui ilikuwaje,nina hamu sana ya kujua kilitokea nini wakati sina fahamu zangu, ……..natamani sana kujua ilikuwaje, lakini sijapata mtu wa kunisimulia, kwani nilipopata fahamu tu, nikaamua kuja huku.

Na hapo mhusika mkuu akaanza kutuhadithia jinsi ilivyokuwa kwenye tukio hilo la kuzama kwa MV Bukoba



Ni mimi: emu-three

2 comments :

samira said...

mimi nilijuwa tu mhuja atatokea haya sasa sijuwi kama kuna ndoa wala cha mimba nasubiri nione
m3 vipi my dear mungu yu pamoja nawe popote ulipo

Unknown said...

Nasubiri hiyo story ya MV Bukoba