Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, November 22, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-53Maneno alikuwa keshavaa na alikuwa akimsubiri msaidizi wake ambaye alitoka kidogo, na kumuacha peke yake ndani, akiwa peke yake alijikuta akiwaza mengi, alishangaa toka jana akili yake ilikuwa haitulii vyema, hakuwa akiamini kuwa kweli sasa anakwenda kukabidhiwa yule mtu aliyekuwa akimpenda kwa moyo wake wote, hakuamini kuwa baada ay muda ataitwa mume wa mtu, …lakini upande mwingine wa akili yake alijikuta akiwaza ndoto aliyoiota jana, …
***
Ilikuwa ni sehemu ya tambarare sana, na macho yake yaliweza kuona mbali sana, na ilionekana alikuwa akisubiri kitu ambacho kwa muda ule hakuweza kukigundua ni kitu gani, na muda ulikuwa ukienda na hicho kitu hakikutokea, mara ghafla akasikia sauti kama upepo ukivuma, na likaja vumbi ambalo lilizoa matakataka na kuingiwa machoni, akajipangusa haraka, kwani wakati anainua mikono kujipangusa aliona taswira ya kitu mbele yake, …na wakati huo huo vumbi lilikuwa limeshaingia machoni, kwahiyo hisia za haraka ni kuondoa hilo vumbi machoni.

Alipikicha machonja cha mkono wake, na kujaribu kuangalia mbele yake, akashangaa macho yake yakiwa yana ukungu, ukungu ambao ulimfanya asione vyema, akapikicha tena , lakini kila alivyozidi kupikicha, ndivyo alivyozidi kupunguza nguvu ya uoni wa macho yake, na cha ajabu mbele yake alihisi kuwa kuna mtu anakuja, lakini kwa vile macho yalikuwa hayaoni vyema, hakuweza kumgundua ni nani, ila ilionekana huyo mtu anamfahamu sana. Je ni nani huyu mtu…?

Tatizo likawa ni jinsi gani ataweza kuona, maana akipikicha macho kwa mkono anazidi kuharibu nuru ya kuona, na akiacha vumbi linamkereketa machoni, na vile vile alikuwa na hamasa ya kutaka kumuona huyo mtu anayemjia, kwani alihisi anakuja kumzuru, …na kama ni hivyo kwanini alisimama pale kumsubiri kwa muda mwingi hivyo…alihisi kuwa alikuwepo hapo kusubiri kitu, na kitu hicho kumbe ni mtu , na mtu huyo inaonekana ni mtu anayemfahamu, lakini amekuja kwa nia mbaya, kwa vipi , ilikuwa ni hisia ilivyomtuma…

Akainua mikono kujipikicha teana kwani vumbi lilikuwa linamkereketa sana machoni, na sasa akajipikicha kwa nguvu sana, ili kuondoa ule utando uliojivika machoni na kumfanya asione vyema, alifanya hivyo mara kadha, huku anaomba , tatizo hilo limtoke, maana limeshaanza kumpa wasiwasi, isije ikawa ndio mwanzo wa kumpa upofu. Alikumbuka kisa cha jamaa yake eliyepoteza macho yake hivyo hivyo ,…alimuhadithia kuwa tatizo lake lilienza kwa kuingiwa vumbi machoni, ilikuwa vumbi kidogo tu ,akajipikicha na kila akifanya hivyo ndivyo ilivyoharibu macho yake na sasa ni kipofu.

Alipokumbuka hicho kisa cha jamaa yake akaanza kuogopa , na aliogopa hata kuondoa vile viganja vya mikono machoni, licha ya kuwa alishamaliza kazi ya kuondoa vumbi lililokuwa likimuathiri, na nia yake sasa ni kumuona huyo jamaa aalyekuwa akimjia, na kama ni adui ajiandae kupambana naye. Na kipindi anapikicha macho, mawazo ya hiyo taswira ya mtu haikuwa na umuhimu sana zaidi ya macho yake kuona. Aliogopa kupoteza macho, kwani macho ni kipenzi cha mtu, ambaye alijaliwa kuwa nayo.

Sasa akaanza kuyafunua macho yake, alifnya hivyo kwa wasiwasi na kwa hiyo aliyafunua kwa utaratibu sana , na kila hatua ilikuwa ni kiwewe kwake, kwani badala ya kuona mbele, baadala ya kuona mwanga, badala ya kuona ule upeo aliokuwa akiuona toka mbali, na badala ya kuiona ile taswira, aliona giza, giza nene, ….hakuamini akili yake, hakuamini kuwa sasa haoni tena, ina maana kawa kipofu,hapana …hapana, haiwezekani….

‘Ina maana nimekuwa kipofu..haiwezekani, oooh, mungu wangu nimekosa nini,…mungu wangu nisaidie nisamahe makosa yangu, kama kuna kitu nimekosa naomba unisamehe, naomba unirudishie macho yangu tena, sitarudia tena…’Maneno lijikuta akilia kwa sauti, na mara akazindukana, kumbe ilikuwa ni ndoto.

Alipoamuka cha kwanza kabisa, ni kukimbilia kwenye kiyoo, kukagua macho yake kuhakikisha kuwa kweli yapo sawa, na alipoona yapo sawa, akarudi kitandani kutulia, akiwazia ile ndoto, huwa haamini mambo ya ndoto, au ushirikina,…ila ile ndoto ilimtisha, kwanini ilenge macho yake…hakuamini, akaeeleka bafuni na kunawa, akajaribu kupikicha macho yake kama alivyokuwa akifanya kwenye ile ndoto na alipoona hakuna athari yoyote akarudu kitandani kulala, na kabla hajashikwa na usingizi mlango ukagongwa.

‘Nani sahizi teana asubuhi hii…?’akauliza kwa sauti.

‘Mimi baba yako mkubwa, nimefika na ugeni mkubwa sana…’ilikuwa sauti ya baba yake mkubwa, baba ambaye ndiye alimlea, na taarifa zilizofika awali ni kuwa hataweza kuhudhuria hiyo harusi kutokana na muda uliopangwa, na alilalamiak kweli na hata kufikia kusema labda mwane hakutaka ahudhurie hiyo arusi yake kwasababu anajishirikisha na mambo ya matambiko. Lakini akaipa baraka kuwa ifanyike tu maana asingeliweza kuacha shughuli zake za shamba kuna mbegu alishazitayarisha mapaka azipande kwanza. Maneno akajiuliza sasa imtokeaje mpaka akaamua kuacha hizo mbegu na kuwahi kufika tena kwa muda muafaka…kwa kweli, ilikuwa ni mshangao kwa Maneno.

‘Mimi nashangaa bwana harusi mtarajiwa unalala mpaka sahizi, ulitakiwa muda huu unachukua mazoezi, unajiimarisha mwili maana unakwedna kuingia uwanjani, lazima uonyeshe kuwa kazi unaiweza, sio unaingia uwanjani, hata dakika kumi na tano hazijaisha umechoka…namna gani mwanangu, unataka uniangushe…’ilikuwa kauli ya baba yake ambaye kwa kuongea Maneno kasingiziwa, na pembeni yake alikuwa kaongozana na wazee wengine watatu , ambao Maneno anawafahamu kuwa na wazee wa huko kijijini.

‘Baba na wewe kwa utani wako …hujazeeka tu, …mzee mbona raha, sikutarajia kuwa mngelifika, maana taarifa ile ya kunikatisha tamaa ilinivunja nguvu kabisa, mama yeye mbona hajafika,au yupo njiani? Niasameheni sana kwa kushindwa kubadili tarehe ya harusi , sio kusudio langu, ….’Maneno akawa anaongea hili na lile huku akaipokea mizigi ya wale wazee.

‘Haya yote yamepangwa ili iwe hivyo, usijali sana, ni heri pia kwako, …..Ingelikuwa hivyo nije na mama yako, lakini kama nilivyosema kuna mbegu zilikuwa tayari, …kwahiyo tukajiapnda, nije mimi au yeye, nikaona hapana, lazima nije mwenyewe, niliwaza sana, nikasema hapana, ,mtoto nimelea mwenyewe, nikampeleka jando mwenyewe, nikamsomesha, …halafu anafikia kuoa, nikose, hapana, ..sitaeleweka vyema na mdogo wangu huko alipo, nikawakusanya wenzangu hawa tukasema lazima tuwahi , maana lazima tufanye vitu vyetu kabla hujaweka mwali ndani, lazima tuweke mazingira yawe safi, na kweli tukiwa njiani tukahisi jambo, kama tusingeliwahi, mwanangu sasa hivi ungelikwua ukilia upofu….’akasema yule mzee.

‘Ningelikuwa kipofu, baba mbona sielewi hilo, ina maana ile ilikuwa sio ndoto ni kweli…?’Maneno akauliza kwa mshangao.

‘Wewekijana bado mdogo sana, hii dunia ina mambo ya ajabu huwezi kuyaona, ila sisi wazee tulishayajua hayo mapema sana…kuna jinamizi linakuandama, na hili ni kwasababu ya hii ndoa, …hebu kwanza niletee maji kwenye beseni tuondoe huo utando ambao umekwisha wekwa machoni mwako, unajiona kuwa unaona, kumbe huoni, huo utando ukipenya machoni mwako, basi umeshakuwa kipofu, utakuwa uanona giza …..’akasema mzee mwingine waliyeandamana na baba yao na kumfanya Maneno abakie kuduwaa.

Maneno akaleta majisafi kwenye beseni na wale wazee wakalizinguka lile beseni wakiozungumza maneno ambayo Maneno hakuyaelewa vyema, na mara akasikia mlio, ilikuwa sauti ya upepo,kama ule ule upepo aliousikia kwenye ndoto, na mara nje kukawa kama kuna vumbi, linalotokana na huo upepo, alichofanya Maneno na kuficha macho yake kwa kuvaa miwani yake ya jua...

‘Haya njoo hapa unawe hayo macho yako, ondoa hiyo miwani, haisaidii kitu , kama ingelisaidia ungeliivaa wakati huo utando ulipokuingia mwanzoni. Mwenzako alishajiandaa kukuharibu macho yako, alijua akikuharibu hayo macho hutampata huyo binti. Amekuwa akikuwinda kila siku, ila imani yako ya dini imekusaidia sana…, lakini alishajua wapi pakukupatia, alijua kuwa wewe ukilala unajisahau sana na hilo ni kwa wengi, watu wakilala wanalala kama magogo, hawamkumbuki mungu, utalalaje masaa manne au sita, bila hata kujigeuza na kumshukuru, au kumuomba mungu wako…sasa wenzenu wanatumia mwanya huo…na, hapo alitupa bomu lake…bahati yako….tuliliona sisi wakati tupo njiani, tukalizuia….’akasema yule mzee aliyeongozana na baba mkubwa.

‘Haya mapya ,sasa huyo jamaa ni nani?’ akauliza Maneno.

‘Haina haja ya kumfahamu, maana tutakuingiza kwenye ushirikina, nia yetu ni kusawazisha haya majambo, ila ni kwamba kuna mtu alikuwa anataka kumuoa huyo binti kabla yako, na wewe ukamizidi kete, sasa yeye kaamua kwenda mbali zaidi, akasahau kuwa kuna mungu, na kila kilichpangwa na mungu hakipingiki, kama kweli mungu kakupangia wewe kuwa huyo binti ni wa kwako, hataweza, atajisumbua na mwsiho wa siku ataumbuka…yeye, kuna mengi zaidi ya hayo , ila kwa vile umeshaharibu, haisadii kitu, huyu atakuwa wakwako…mungu atakusaidia’akasema baba mkubwa.

‘Namshukuru mungu,na namuomba mungu afanye hivyo, ila ningeliepnda kujau angalau kidogo, ndio nimeharibu, lakini sio kwa hivyo, wote tunafanya haivyomsiszani kuwa nyie wazee walimuoa tu, hata ,,,lakini namuomba mungu anisaidie na ndoa yetu ifanikiwe, nawashukuru wazee wangu kwa kufika wakati muafaka..’akasema Maneno.

‘Mshukuru sana mungu wako na mshukuru sana dada yako anakupenda sana, alisisitiza sana na kuniomba nisikose, alifikia hata kulia, kunibembeleza nifike, ni juzi nikaoata ndoto kuwa kuna jinamizi linakuandama, na ndoto kwangu ni kiyoo, inanibashiria mengi, nikaoan niwaone hawa wazee, na wao wakakubali kuwa kuna jinamizi, nikasema aaah,lazima tufike huko na wazee wenzangu hawa, …najua kuwa mnazarau sana mambo ya asili, …na baya zaidi mnazarau mambo ya sili na kujifanya mnafuata mambo ya kisasa, …’akasema baba mkubwa.

‘Tatzi hawa wanajifanya wanafuta dini, lakini dini yenyewe hawaijui, hawaifuati itakiwavyo, huwezi ukasema wewe ni dakiatari wakati hata udakiatari huujui, dini inakuwa kama kiini macho tu, kudanganyana, isomeni vyema, na ifuateni vyema, sio nusu nusunu, mnachofuata ni mambo ya kuiga, na mwisho wa siku mnazurika bila kujua, …mungu hampo naye, mambo ya sili mumeyazarau, mnaishi usasa ambao hautibi bila kuacha majeraha, na majereha mengine hayatibiki pia….’akasema mzee mmojawapo.

‘Duuh, kweli , lakini ni bora kufanya hivyo kuliko kukimbilia mambo ya asili kwa ujumla, yapo mazuri, tutayafuata lakini mambo, yale yaaah,…’akasema Maneno.

‘Nakuelewa vyema kijana, sasa hebu fikiria huyo mwenzako angetaka kukufanya kitu kibaya ungeligfanayje maana jamaa huyo alitaka hata kukiharibu kiumbe kisicho na hatia, lakini hajafanikiwa, …binti yupo safi ,….hongera bwana mdogo, ingawaje umeharibu kabla…cha muhimu jaribuni kusoma mambo yote , ya wazungu nay a wazee wenu pia….’akasema baba mkubwa, lakini Maneno hakuelewa kabisa baba yake alikuwa na maana gani, `kuharibu’ mawazo yake yalikuwa jinsi gani wazee hawo walivyogundua hilo tatizo aliloliota …..

‘Mwambie huyu, na wenzake wanaojifanya wasomi, ndio someni, lakini someni pia na mambo yenu ya asili, yapo mengi yatawasaidia…hata wazungu sasa wanafanya utafiti wa dawa asili na kuzirutubisha, wamegundua kuwa kuna tiba safi kabisa…na pia sisi wazee wenu wapo waliobarikiwa kuwa na uoni wa mbali,..huo ni usomi wa hali juu, uoni huo wanao wazee wenu, lakinihatujakwenda shule, lakini tuanaweza kufanya mambo yetu tukaona hatari inayokuja tukajihami nayo, hebu jiulize, hilo bomu, lililotupwa na huyo mwenzako ulikuwa uanlijua, …mbona sisi tumelijua, tuakalizua kabla halijakuathiri wewe na mwenzako na mtarajiwa… huo ni usomi wa asili, ….sasa zarauni hayo, na sisi mababu zenu tunaondoka, mtabakia na usasa wenu….’akasema mzee mwingine na kumuacha Maneno hoi.

Maneno akaishia kutabasamu, maana wanavyomtaja mtarajiwa wake, wanazidi kumpa hamasa siku ifike, yeye hakuwa na mawazo zaidi lakini maneno haya ya mwisho yakamzindua na kuuliza…

‘Umesema mwenzangu na matarajiwa, inaonyesha kama mnataja watu wawili, yupi tena huyo mtarajiwa mwingine?’akauliza Maneno.

***********
Maua alijikuta kihema kwa wasiwasi, na kila alivyojaribu kukimbia alikuta hilo jitu linalimfuta lipo nyuma yake, lilikuwa jitu la ajabu limejifunika majani, na mara kwa mara aligeula ili kulitizama ni jituu gani, lakini hakuweza kuligundua sura yake, akazidi kukimbia, na akaanza kusukia maumivu, makali, maumivu hayo yalianza kama kichomi, na baadaye yakawa makali sehemu yote ya tumboni…

‘Ohhh, mtoto wangu….’akajikuta akisema

‘Na bado nitahakikisha kila kitu kinaondoka humo tumboni, na baadaye utakuja kunipigia magoti…’akasikia sauti kali ikisema, ni sauti ambayo alishawahi kuisikia, lakini hakuweza kuitambua mapema kuwa ni ya nani.

‘Huniwezi wewe, na ikuogopi….’akasema kwa kujipa moyo, huku anakimbia.

‘Tutaona mwisho wake…’ile sauti ikamjibu.

Aliendelea kukimbia , lakini sasa nguvu za kukimbia zilipungua sababu yay ale maumivu na lile jitu likwa limemkaribia na kumpita mbele yake likasimama na kusema `haya sasa hebu angalia akzi yangu, …’

‘Maua akajiuliza aangalie nini, ..!’

Kwasababu yay ale maumivu ya tumboni, Maua akaamua kuinama kutizama chini, mara akashituka na kurudisha macho kuliangalai lile jitu, na hakuona mtu tena, aliona mwanga mkali ukimmulika machoni, na alihsis kama alisikia kitu kama ukulele, lakini hakuweza kuwa na uhakika nao, mawazo yake yalikwua kuangalia kile kitu alichokiona mwanzaoni, na kuinama tena kujiangalia , lakini hakuweza kuinamisha kichwa, ilikuwa kama mtu aliyesimikwa hawezi kuinama.

Maua aliwaza akijiuliza kuwa hicho alichokiona mwanzaoni ni ndoto au ni kweli, na kama ni ndoto mbona sasa anashindwa kuinama na kujiangalia chini, na sasa hakusikia tena yale maumivu ya tumbo, bali alihisi njaa, akasema ngona niinuke nikatafute chakula, lakini mwili ulikuwa kama umekufa ganzi, akaanza kuwa na wasi wasi, ina maana mwili umekufa ganzi, ina maana kashikwa na kiharusi, haiwezekani, akajaribu tena na tena , lakini hakuweza…na mara ghafla aksikia kitu kama ukulele ambao ulimfanya ahisi vibaya masikioni, …akazindukana,kumbe ilikuwa ni ndoto.

‘Maua vipi , mbona nimesikia kama ulikuwa unapiga ukulele, na kuweweseka, ulikuwa ukimuota tena aliyekuwa mume wako nini, nakuomba sana ukubali kuwa huyo hayupo tena duniani, sasa mfikirie Maneno…?’ ilikuwa ni sauti ya shangazi yake, ambaye alikuwa kasimama mlangoni. Na Maua aliinuka pale kitandani na kukimbilia chooni,….baadaye akarudi!

‘Shangazi, siku zote namuota Mhuja, lakini leo nimeota ndoto nyingine ya ajabu kabisa…’Maua akasema na kuinama kujikagua tena na kufunua lile shuka ple kitandani kukagua kuwa hakuna kitu…, na hakuamini macho yake kuwa kile alichokiona ilikuwa ni ndoto, na alisimama tena na kujaribu kuinama na kuinuka, halafu akaangalia tena miguuni, halafu iakasema kwa sauti `kumbe ilikuwa ni ndoto.

‘Umeota ndoto gani mbaya mwanangu’akauliza shangazi ambaye alikuwa kaduwaa, alipoona hivyo vitendo vya binti yake.

‘Hata siamini, maana nilijiona nimesimama kweney dimbwi la damu…na hayo maumivu hayaelezeki…!’akasema Maua.

‘Dimbwi la damu, damu hiyo ilikuwa ikitokea wapi..?’ akauliza shangazi.

‘Huku. Chini…na sijui ilianza kutoka lini, ila nilisikia maumivu ya tumbo yaliyoaanza kama kichomi, na nilipoinama chini nikakuata hivyo, mwanzoni nilikuwa nikifukuzwa na jitu nisililolifahamu limejifunika majani, na karibu linikamate,lakini sijui lilipoteaje..’akasema Maua.

‘Nimeshakuambia ukilala hakikisha umemuomba mungu akulinde na mabaya ya usiku, ujue maadui na watu wabaya wapo wengii na wote wanataka kujionyesha kuwa wao wana uwezo zaidi ya mungu, lakini hawataweza kama utamtegeema mungu peke yake…sikiliza mwaangu usigope kabisa, na ukiota ndoto kama hizo usiwe na wasiwasi moyoni, jipe moyo na ikiwezekana liambie hilo jitu au kitu chochote cha kutisha kuwa halikuwezi, na omba kwa mungu atakusaidia..’akasema shangazi.

‘Na huyu mtu nitamwendea leo na tutapambana naye, nilihisi hivyo, na sikulala , ilibidi usiku niamuke na kukesha kwenye ibada, na hataweza, lakini lazima nikamuone ajue kuwa najua nini anachokifanya, yeye anajifanya anajua mambo ya kishirikiana sio, basi mimi simuogopi..’akasema Shangazi kwa hasira.

‘Kwani ni nani mbona inaoneka kuwa kuna mtu unamjau ambaye unahisi kama anataka kunizuru,..au sivyo shsngazi, usiniambie kuwa unaamini mambo hayo,shangazi unaamini mambo hayo ya uchawi…?’ akauliza Maua kwa wasiwasi.

‘Hayo yaache, usiwe na wasiwasi, hakuna kitu kitakachokuzuru, ilimradi umtegemee mungu wako, ngoja nitoke kidogo, lakini sasa unajisikaaje..?akauliza shangazi mtu.
‘Sasa najisikia mwepesi, sio akam ilivyoikuwa ndani ya ndoto, nilikuwa mzito wa ajabu , hata kukimbia ilikuwa nakimbia kama roboti.

‘Basi tulia kwani wapambaji watafika muda sio mrefu, mimi natoka kidogo, wakija muendelee,…’akasema shangazi akiwa kajawa na hasira moyoni, na nia yake ilikuwa kwenda kwa huyo mtu anayemuhisi moyoni kuwa anataka kuleta mambo ya kishirikina akatika familia yake…hakujali na huwa hajali mtu . Akaondoka akiwa na hasira zake, na hili aliliona Maua , na kujiuliza moyoni shangazi anakwenda wapi.

‘Lazima nimfuate maana huko anakokwenda kunaweza kukazuka balaa,sipendi shangazi aijingize kweney matatizo kwa ajili yangu..’Maua akasema huku akijiandaa kumfuata shangazi yake, na kabla hajaondoa mguu akasikia kama mtu anagonga mlango, akainuka kweda kufungua mlano, alipofungua, alishikwa na mshituko mkubwa sana, karibu adondoke chini,….

NB, hii sehemu kama kawaida imeandikwa katika uharaka usio wakawaida, tusameheane kwa makosa ya hapa na pale. Na swali kubwa hapa ni uchawi na nguvu za giza, unaziaminije, je iliwahi kutokea kwako, na je ndoa yako iliwahi kukumbwa na mambo kama haya, mvutano, nk, naombe tuchangiane mawazao

Ni mimi: emu-three

7 comments :

Anonymous said...

Uchawi upo ndio maana Mungu amesema tujilinde na wanaopulizia kwenye vifundo. Na uchawi hasa hutokana na hasada, mtu anapomfanyia uhasidi mtu huishia kumdhuru kwa uchawi au njia nyingine. Ila dua na sala ni kinga tosha sie waislamu tunafundishwa kila siku kabla ya kulala kusoma Quran sura zile 3 na Ayatul kursiy ili itulinde na ubaya wa usiku. Na tukiamka kusali na kusoma Quran itulinde na mabaya ya mchana. Nina mengi ya kusimulia kuhusu hasada lakini kujua kwangu kusoma Quran na dua mbali mbali kumenisaidia sana. Tena hii hadithi yako imenikumbusha jinsi nilivyopata tabu wakati wa ujauzito wa mwanangu mpaka nikamkuta mtu live anachoma madawa ya ushirikina, tena ukipenda sana kusoma Quran na kumuomba Mungu kwa dua na kufunga saumu vitu vingine unaviona wazi wazi na unakuwa jasiri huna hofu ya kuogopa uchawi wala ushirikina.

Story inazidi kunoga japo ndio inaelekea ukingoni.

samira said...

m3 asikwambie mtu uchawi upo amini usiamini mimi mwenyewe siamini kama nipo hai naona ndoto
muhimu kusali sali kuomba mungu hasa duwa na sadaka
m
kwani mungu hubainisha ngaja siku nikueleze mkasa wangu wa mama mkwe wangu hutaamini
lakini nashkuru mungu bado nipo hai na naendelea na maisha na mwanawe nipo nae
mungu mkubwa na tunamuamini sana

Swahili na Waswahili said...

Tena kunauchawi wa aina nyingi sana mpendwa, mwingine ni ugombanishi,uchochezi watu wanakosana mpaka wanaweza kuuana.

Duhh ndugu wa mimi Mungu amekubariki na kukupa hiki kipaji wangu, nafurahi sana kuona kazi ikiendelea, kila lililojema ndugu yangu PAMOJA SANA TUU!!!

SIMON KITURURU said...

Tuko Pamoja!

chib said...

Pamoja na kwamba nimetingwa na kazi, lakini tupo pamoja daima

Yasinta Ngonyani said...

Kila kitu ni imani ukiamaini kuna uchawi basi upo. Kaazi kwelikweli mpaka iwe hivyo jamani ......HIVI UCHAWI NI NINI KWANZA JAMANI?

emu-three said...

Nawashuru wapendwa kwa kushirikiana nami,kwani wkati naandika sehemu hizi nilizongwa na mawazo juu ya imani ya kishirikina na uchawi je ipo,nani aliye wahi kukumbana na mitihani hii