Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, November 7, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-46



Inspekta alivyotoka kwenye gari lake…hakuna hata mtu aliyeweza kugundua hilo. Alichofanya ni kutoka kwa haraka wakati gari likiwa katika mwendo, alifanya hivyo kwa tahadhari kubwa, akijua kuwa huenda kuna mtu alikuwa akiwachunguza. Alichofanya ni kupma ishara dereva wake kuwa anatoka ndani ya gari lakini asisimamishe, ila atampa taarifa baadaye amfuate hapo hotelini, na wakati huo huo alikuwa keshavaa kofia kubwa kichwani, kofia hizi walikuwa wamevaa watalii wengi waliokuwa wakiogopa jua kwahiyo isingelimtilia mashaka kwa wenye hoteli hiyo, ila kwa ukubwa wake,ilikuwa ikimafnya mtu asimgundue mapema.

Gari lilikuwa limeshaondoka kwa mwendo wa kasi,na yeye kwa mwendo wa haraka alielekea kule hotelini, kwa kupita sehemu ya maegesho ya magari, alipofika pale mlangoni mwa hoteli kwa haraka sana alipitisha macho eneo lote la nje ya hoteli, ambapo watu mbalimbali walikuwa wakiingia namgari yao na wengine kwa miguu. Kwa kawaida hoteli hii ina watu wengi sana wanaoingia na kutoka, ila walinzi wapo makini kuwakagua na kuwauliza wapi wanapotoka, na kuhakikihsa kuwa kila mmoja ana nyaraka zinazohitaika.

Yeye alipitia mlango wa dharura, na pale kuna mtu wao ambaye aliona ishara yake na kumruhusu apite kwa haraka, bila hata mtu kumjua, huku akipitisha macho eneo lote la nje kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayemshuku , na kwa kutumia uzoefu wake aligundua kuwa hakuna mtu yoyote pale nje aliyekuwa akimchunguza. Aliufikia mlango wa hotelini ambao hujifungua wenyewe kila unapoukaribia. Hakuwa na shaka na vyanzo vya usalama humo ndani ambayo alishagundua kuwa kila mtu anyeingia huonekana na kumbukumbu zake hihifadhiwa kwa usalama, kwani alishamuweka sawa mkuu wa ulinzi wa mle ndani, labda awe anahusika na hawo watu kwa kificho kitu ambacho Insepekta hakuamini kuwa huyo mkuu anaweza kuwa anajihusisha na hawo watu.

Akiwa na wasi wasi asije akamkosa Rose, na akiingia mikononi mwa hawo watu, kwani wakati wanatoka huko maeneo ya ziwani wakiwa na Rose alipigiwa simu na watu wake kuwa Rose yupo hatarini, yeye na mtu wake wanayeishi naye wanatakiwa kupatikana wakiwa hai au maiti, …aliposikia hivyo hakumwambia lolote Rose, aliwapigia watu wale anaowaamini kuwa watengeneze mtego, na Rose afanywe kama chambo, …alionge hilo bila hata Rose kugundua, ….

Taarifa hii kuwa Rose na mtu wake sasa wapo kwenye hatarini na ya kuwa wanaweza kutekwa au kuuwawa, ailimshitua sana Inspekta, na wazo la kumfanya Rose awe chambo, lilimfnya Inspekta kubeba dhamana kubwa sana, lakini hata hivyo angeliafnyaje, kwani watu hawo wakiamua kufnya hivyo, wanakuwa hawakamatiki, …wangeliweza kuwachukua na kuwahifadhi katika maeneo yao nab ado wakauliwa na watu waliopo kweney usalama ambao wamepandikizwa, kwahiyo yeye aliona jambo jema na kuingia kwenye mapambano na wao kwa kumtumia Rose kama chambo.

‘Ndugu naona wakati umefika,…nimevumilia mpaka nimeshindwa, inabidi sasa nianze kuchukua hatua, na hapo ndipo pa kuanzia, unasemaaje mpo tayari,…?’akamuuliza huyo aliyempigia simu, ni mmoja wa watu wanaowaamini sana, na inapofikia hatua ya utendaji huyo anamjua kuwa ni mtendaji mwema na mwaminifu, kwahiyo kwa wazo hilo lililomjia akilini, aliua hapo ndipo mahali pa kulifikisha na huyo angeliweza kutengeneza mtego ambao unaweza kufanya kazi kama alivyokusudia.

‘Mkuu usijali hilo litafanyika kwa uangalifu wa hali ya juu, na ni muda ni muda mrafu nilikuwa nasubiri amri kama hiyo, hawa watu wamezidi kutuchezea, a hata kuonekana hatufanyi kazi yetu vyema, …mkuu usitie shaka ……’akasema huyo jamaa aliyepiga simu.

‘Sawa…, lakini hakikisha watu wetu ndio wanaohusika …na nakuomba uwe mwangalifu kila hatua, na ni vyema pia ukapata kibali cha mwenye hoteli, ingawaje sio lazima, lakini kwa umakini fanya hivyo kwa vile inabidi watu wetu waingie na vifaa, na hatutaka kukaguliwa, fanya hivyo kwa mkuu wao …lakini kwa uangalifu..’akaongea huku anahakikisha kuwa Rose haelewi kitu, na baadaye akambonyeza dereva wao apunguze mwendo, ili wenzao huko wapate muda wa kusawazisha mambo yao, …dereva wake alishaelewa nini kinachoendelea akapunguza mwendo kinamna, na mwendo huo uliwafanya wazidi kuchelewa kufika hotelini.
‘Mbona naona kama umepunguza mwendo dereva, …unajua mnanichelewesha kufika huko mjini na kibali changu natakiwa nifike mapema kabla ya saa kumi na mbili na sasa ni saa kumi na mbili imeshatimia bado tupo huku mbali…’akalalamika Rose.

‘Waliokupa hicho kibali ndio hawo hawo wanaokufanya uchelewe kwa sababau maalumu, usijali, tupo pamoja…’akasema Inspekta, huku akiangalia saa, na kwa mtizamo wake kwa muda huo vijana wake watakuwa wameshafika hotelini na kuweka kila kitu sawa sawa.

‘Hata kama nyie ndio mumenipa hicho kibali, ..lakini nataka kumuwahi mgonjwa wangu , …hilo halihusu kibali chenu, huyo ni mgonjwa wangu namjua matatizo yake, …’akalalamika Rose.
‘Hata hilo usijali pia, tutahakikisha kuwa mgonjwa wako unamkuta katika mikono ya usalama, kwani hata kama ungeliwahi na ukamkuta katika mikono ya hawa watu hatari, unafikiri ungelifanya nini…tulia, usitie shaka..’akasema Inspeta kwa sauti ya uaskari, mpaka Rose akageuka kumwangalia kwa mashaka.

Inspekta alipotoa hilo agizo, la kutayarisha mtego wa kuwanasa hawo watu, na iwe sehemu ya mapambano yao, na ikibidi kikundi hicho hatari kikomeshwe, alijiona sasa keshaingia vitani na baya zaidi wanamuhusisha mtu ambaye usalama wake upo hatarini, na kwa namna hiyo alihitaji busara kubwa za kumfanya Rose amuelewe na alimuhitaji sana kuliko wakati mwingine wowote.Na kwa mtaji huo, inabidi baada ya tukio hilo ahakikishe kuwa Rose na mtu wake wanakuwa katika mikono yake, ili kuhakikisha usalama wao. Swali likabakia jinsi ya kumshawishi Rose, kwani alionekana mbishi kidogo, hasa kuhusiana na hawo watu…inavyoonekana yeye alikuwa hajakubalina na uhatari unaomkabili.

‘Kazi imeanza…’Inspekta alijikuta akisema maneno hayo kwa sauti, na Rose aliposikia hivyo akamuuliza Inspekta ni kazi gani hiyo imeanza.

‘Ni kazi ya kuhakikisha hawa watu wabaya wanasafishwa, …nakuomba sasa unielewe hivyo, sitaki kukutisha, ila ninachotaka kukuambia ni kuwa uhakikishe unafuata maagizo yangu, kama kweli unamjali mwenzako, …wewe wanaweza wakakusumba kidogo, lakini baadaye kama utakuwa mkaidi watakumaliza tu, ila mwenzako yupo hatarini zaidi,…hilo nitakufichulia baaadaye…..’akasema Inspekta huku akipokea simu toka kwa vyanzo vyake vya habari.

‘Rose nakuomba sana sasa , huu sio wakati wa mchezo tena , kwasababu umeshaachana na Adamu, ambaye ndiye alikuwa mtetezi wako, …na sijui kama atakuwa na moyo wa kukuwekea kinga tena, na ilivyo ni kuwa wameshachoka na kinga ya huyo bosi wako, …kwahiyo nakuomba sana uwe na mimi, ….’akamgeukia Rose ambaye alikuwa kaka kiti cha nyuma, na Inspekta alishangaa kumuona akitoa machozi, hakumuuliza kwanini, alijua kuwa kwa vyovyote hajililii yeye mwenyewe, bali alikuwa akimlilia rafiki yake.

Inspekta alijifunza jambo kati ya Rose na huyo jamaa yake, ilionekana kuna penzi kubwa limefungamana ndani yao, …alijua kabisa kuwa hawo sio mke na mume kama inavyojulikana, ….ila kuna fungamano la kimapenzi kati yao. Kwa muda mfupi wa maongezi yake na Rose, aligundua kitu kimoja kikubwa sana, kuwa Rose anampenda sana huyo jamaa anayeishi naye, na kama itatokea kitu kuwatenganisha basi Rose ataishi kwa mashaka makubwa sana…aliwaombea baraka kimoyomoyo kuwa kama itawezekana aweze kushiriki katika siku yao ya ndoa, kama itakuwa hivyo, kwani hakujua zaidi ya hayo katika mahusiana ya hawo watu wawili.

‘Inspekta kama ni hivyo mumegundua kuwa kun ahatari inayomkabili huyo mgonjwa wangu, nawaombeni muhakikishe anakuwa salama,…’akasema Rose huku akionyesha wazi huzuni hata katika sauti yake akiongea.

‘ndilo tunalolifanya, sio kwake tu, kwa kila raia, lakini hatuwezi kufanikiwa hili mpaka tupate ushirikiano wenu….’akasema Inspekta.

‘Lakini inspekta, kwanini wananiandama mimi hivi, …nina kitu gani cha zaidi , sipo madarakani, sina utajiri wowote, ….haya, labda wana lo kuhusu mimi, lakini kwanini wanamuandama hata huyu mtu ambaye hana hatia kabisa, mtu mwenyewe mpaka sasa hajulikani ni nani …mungu wangu akizurika huyu mtu akiwa mikonono mwangu, sijui kama nitaishai kwa amani…’akasema Rose.

‘Usijali, kuanzia leo mtakuwa katika ulinzi wangu, …ila nitakuarifu baadaye nini cha kufanya ili tuweze kufanikiwa katika hilo, usijali sana, utamkuta mtu wako yupo salama, unasema huyo mt wako , au mgonjwa wako, au mume wako ….jina lake ni nani vile….?’akauliza Insepkta.

‘Sweetie…’akasema Rose huku akiwa hayupo makini na anachokiongea.

‘Hilo sio jina lake, nauliza jina lake kamili anaitwa nani?...usiniletee lugha zenu za mapenzi , nipo kazini binti…’ akauliza Inspekt akwa sauti ya uaskari.

‘Jina lake kamili kwa kweli silijui, aheri ningelilijua jina lake huenda lingenirahisishia hata mimi, sijui anaitwa nani, na hata yeye mwenyewe hajijui anaitwa nani, labda ningelimjua vyema kama ningelijua jina lake, na huenda ingalisaidia kumjua wapi alipotokea, labda…ooh….mungu wangu mbona nitateseka kama atazurika, mnaweza kujua ni watu gani wanataka kufanya hivyo..…?’akasema Rose kwa masikitiko.

‘Kwanini unajitia katika hali kama hiyo ya kuwa mnyonge, kusononeka, nani kakumabia utamkosa huyo Sweetie wako...'akaongea kama mzaha, halafu akaongeza kwa kusema ` Rose, …ndio najua kuwa mpo kwenye hatari, lakini mengine mtajitakia wenyewe kama hamtatimiza nitakayo waambia mfuate, na nakuhakikishia kuwa kama mtakuwa nami bega kwa bega, nitawasiadia mpaka hatua ya mwisho na ikibidi tutaondoka wote mkaisho nchini mwangu, kwenye usalama…’akasema ainspekta.

‘Siwezi kuikimbia nchi yangu, mimi kama nikufa nitafia katika nchi yangu…siwaogopo kabisa hawo mafisadi,,,’akasema Rose kwa ushupavu na Insepkata akageuka kumwangalia nasasa alimkuta uso umeswajiga kuonyesha ujasii ambao ndio aliohitaika kwa wakati kama huo., Mnapokuwa vitani, uzalendo,ujasiri na kutokata tamaa ni kitu muhimu sana.
‘Hapo sasa Rose tupo pamoja, …nahitaji ujasiri wako, ili tuweze kushinda vita hivi, hakikisha unakuwa hivyo wakati wote…tutashinda …’akasema ainspekta na kupkea simu nyingine iliyokuwa ikiita.

Mkuu wa ulinzi wa hoteli alipokea simu ambayo mwanzoni hakujua inatokea wapi, na alipopewa maelekezo mwanzoni alibisha sana, na kuwaambi akuwa yeya hana haki ya moa kwa moja kuruhus jambo kama hilo, lakini akaambiwa kuwa hiyo ni amri, awe ana haki au hana, lakini inabidi hilo tendo lifanyike na hana amri tena kwani hivyo ni vita na vita havina mahali maalumu kwa mapambano.
Ikabidi akubali shingo upande huku akiwaza kwa makini, na akawa anajiuliza kwanini kila anaojaribu kutafuta maisha yake, mwisho wa siku anajikuta katika mitihani kama hiyo, …

Aliwaza huku akisema kimoyomoyo kuwa alichokikimbia ndio hicho kimemfuata hata sehemu isiyostahaili kwa mapambano, lakini ni kweli vita havina macho popote vinaweza kutokea, na yeye kama askari, yupo tayari kukabiliana navyo, na kustaafu kwakwe hakumpi mwanya wa kukwepa vita,

mejaakashindwa asemeje, kwani hiyo ilikuwa ni amri na hakuwa na uwezo wa kuikataa, lakini hata hivyo alihitajika kumuarifu mwenye hoteli ambaye alishamwambia anaweza kufika siku yoyote na huenda muda kaam huo yupo uwanja wa ndege. Huwa jamaa yake huyo hapendi kusema muda gani anakuja , huenda anafanya hivyo kwa ajili ya usalama wake, na hakumwamini yoyote hata yeye amabye humwamini kwa ulinzi.

Hakupenda kabisa hoteli yake igeuke uwanja wa mapambano, hakupenda kabisa kutokana na mahsrti waliowekeana na mwenye hoteli, lakini kama yeye angeliganyake, na hiyo ni amari ya serikali, akachukua simu kumpigia bosi wake mwenye hoteli na ikawa haipatikani,
Akamwangalia Sweetie akiwa katulia, na kujiuliza moyoni kuwa hawa watu wawili ndio wameitumbukiza hiyo hoeteli kwenye majanga yote hayo, je wanalijua hilo na je watamlipa kiaso gani kinachofanana na mashaka waliyompa, na sio mashaka tu, huenda wanaweza kuharibu ajira yake ,akaishia mitaani tena.

‘Nakuomba utulie humu ndani , usitoke au kufanya lolote, na hata ukigongewa mlango hakikisha unaulizia ni nani kakugongea, sasa hivi nitakuachia ufungua, maana kunaweza kukatokea kitu nikakumabia utoke humu ndani garaka iwezekakanvyo, na ninaweza nikabanwa na shughuli nishindwe kuja huku, ….hili inibid nikuamini hivyo, najua unaumwa, najua mpo katika ulizi wangu, lakini pia ninahitajika katika majukumu yangu….usijali tupo pamoja.nikitoka funga mlango kwa ndani….’akasema yule mlinzi na kuuchomkea ule ufunguo mlangoni, akatoka haraka na kusubiri hadi pale aliposiki amlango umefungwa kwa ndani.

Alikimbilia ofisini kwake na kuangalia mitambo yake , hakuamini yalitokea muda mfupi amba hakuwepo kwenye mitambo yake, akahamaki na kulaani, aliwapigia watu wake simu na kuwaulizia mambo kadhaa, hakuamini kuwa maaskari wamefnaya haraka kisai hicho na kila kona aliona watu wao wakiwa na silaha zilizofichwa kwenye makoti yao, Alichunguza kuwa anaweza kuwaona watu wengine ambao hawatambui na kuona kama wana silaha, lakini hakuweza kuwaona, hilo likampa aheani, akasimama na kuifuata silaha yake maalumu, akaitoa ile bastola ya mwanzoni na kuiewka hiyo silaha maalumu kwenye kwapa.

‘Sasa naingia vitani….hata kama nitapoteza ajira lakini sasa muda muafaka wa kuisadia serikali umefika,….nina imanai tutwashidna hawa watu…’akasema na kusogelea mitambo yake na kuchunguza huku akiwaza jinsi alivyojitahidi kiwa serikalini ili kufanya hilo jambo, lakini kila mara alipojaribu alijikuta akikabilina ana vikwazo, sasa limejileta lenyewe, na hapo mwili ukasisimkwa kwa munkari na kutamani aingie msitari wa mbele kuhakikisha hilo kundi linasambaratika,

‘Lakini kundi kili , hili Inspekta aanatakiwa kuwa makini, makundi kama hayo yapo mengi na kila moja lina maslahi yake….lakini hata hivyo, kidogo kidogo sio haba inaweza ikawa mwanzo mzuri wa mapambano, na mwisho wa siku tukamalaiza huu uhasama, …..tunahitaji amani , hataka kama iatakuwa sio amani ya kweli, maana najua bado mafisadi hawa ndio watakuwa madarakani, lakini tutakuwa tumepunguza shida kubwa ya kukosa amani.

Akakalia mitambi yakle na kuanza kuangalia kila kona, akijua sasa keshaingia kwenye mapambano, na hiyo ni sehemu moja muhimu sana, kumjua adui yako alipo …..na wakati aanangalia kwa makini akamuona Rose, ooooh, slihsmsahau Rose, akachukua simu na kumpigia mmoja wa watu wake ahakikishe kuwa anamchelewesha Rose kwa maongei mpaka ahakikishe ueslaam wake…

Akataka kumpifia Ispekta simu, alkini akaona si wakati muafaka, aliataka umwambia kuna kuwa hawo watu wabaya lengo lao na nia yao nikumchukua Rose na hata kumuua jamaa mmoja anayeshi na huyp Rose, kwahiyo hawow atu wawili wanahitaji ulizi mkali, …akaona aongee na mlinzi wake anayemuamini na kumwambi amfuatilie kwa nyuma Rose, ili kuhakikisha usalaam wake.

‘Kuna watu wawili nimewaona waanmfuatilia nyuma mmoja wa wateja wetu, wanafuatilia yule msichana anayeitwa Rose, hakikisha hawafanyi lolote..’akatoa amri.

‘Sawa mkuu, nimeshamuona huyo binti, nitahakikisha yupo salama…’akasema huyo jamaa yake, na kweli akamuona kwenye nitambo yake akiwa anawafuatilia hwo jamaa kwa karibu karibu.
Na kwa nje aliona watu wengine wakiongezeka, nah ii ilipma shida sana, jinsi ya kujua usalama wa leo, akatoa amri kwa watu wake kuhakikisha kuwa watu wanakaguliwa vyema, na wale waliopewa kibali lazima wakipita wapewe kitambulisho maalumu.

Akageukia upende ule waliopo Rose na akaona wale watu waili waliokuwa wakimfuatilia wameondoka na kupanda rosehni ya pili, akamwangalia Inspekta na kumuona akielekea huko huko, akachunguza na akagundua jambo, …yule jamaa wa mwanzo alikuwa kapanda juu kabisa na huko juu alimuona akiwayatarisha silaha ya kiona mbali…..akashituka, …akashituka na kusema;

‘Kazi imeanza…..’akasema na kuongeza kusema, `lazima nimuonyeshe Inspekta kuwa mimi ni rafiki wake wa kweli …akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli….’akajikuta akitamka hiyo methali kwa sauti na ujasiri, na kuinua simu yake….

NB Kazi imeanza, natumai mtanisamehe kwa makosa ya hapa na pale, ni kutokana na kukimbizana muda.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

samira said...

Hilo sio jina lake, nauliza jina lake kamili anaitwa nani?...usiniletee lugha zenu za mapenzi , nipo kazini binti…
M3 nilipofika hapo nilicheka sana yaani inspekta kanichekesha
big up m3 mungu akujaalie hapo kazini patulie