Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, November 2, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-44
Sweetie alikuwa kakaa kwenye kitanda akiwa na mawazo mengi, na kila sekunde iliyopita ilikuwa ikimweka katika maisha ya wasiwasi, …aliwaza mengi, kichwa kilikuwa kimejaa mawazo lukuki, na zaidi alikuwa akimuwaza mkewe. Alimiuwaza mkewe jinsi alivyomkaidi na kuamua kuondoka kwenda huko alipopaita kazini kwake, …siku hizi mkewe kapata kazi, na kazi yenyewe eti ya udakitari….maajabu haya, mkewe kausomea lini udakitari….hapo akawa hakubaliani na akili, na kusema kimoyomoyo, huenda kweli kumbukumbu zake hazijarejea vyema….

‘Kianachoniuma zaidi ni kuona jinsi mke wangu alivyobadilika, hakuwa na tabia hii kabla, nilikuwa nikimwambia kitu ananisikiliza, lakini siku hizi, …sijui kumetokea nini, ina maana mwaka mmoja unaweza ukambadili mtu kiasi hiki, haiwezekani, au ndio hiyo kazi aliyoipta ndio inampa kiburi…na pia naona kuna mabadiliko mengi nilyaonayo kwake, tofauti na zamani, labda ndio maendeleo, ….lakini, mbona nahisi kama sio yule mke wangu niliyemjua….’akawa anaongea mwenyewe kwa sauti.

Akainuka pale kitandani na kuelekea dirishani , aliangalia nje,lakini kulikuwa sio rahisi kuona nje vyema, kulikuwa na ukuta wa nyumba nyingine, uliozuia kabisa kuona huko nje, na mtu asingeliweza kupitia dirishani, kutoka nje, kwani upenyo wa majengo mawilihaukuwa mkubwa, sijui hawo wajengaji walifanayaje kujenga huo ukuta…akajaribu kuwaza hayo ilimradi kupoteza muda.
Hata pale alipobadili mawazo, hakuweza kukwepa kumuwaza Sweetie, wake, na safari hii alikuwa akwiaza kwanini mkewe hataki kumwambai ukweli wa matukio yanayotokea hapo, na imeonyesha wazi kuwa kila mara alikuwa akitafuta njia ya kukwepa kuongea nay eye. Akakumbuka jinsi alivyoambiwa na mkewe kuwa kumbukumbu zake zitakuwa hazijarejea vyema, kama kweli hajamtmbua mkewe yupoje….

‘Haiwezekani nimsahau mke wangu, hiyo haiwezekani, labda kama kapata mtu mwingine na sasa anatafuta njia za kunikimbia, hilo halitawezekana kamwe, ….’akaweka kidole shingoni kama mtu anayeapa. Halafu akarudi pale kitandani na kukaa, baadaye akajiegemeza kwenye mto ili kutafuta usingizi, lakini hilo halikuwezekana, kichwa kilikuwa kikimuwanga kwa kuwaza sana, na mambo mengi yalikuwa yakimsonga kichwani, na mara mlango ukagongwa, akautizama kwa wasiwasi, na aliombea aliyegonga awe Sweetie wake,…

Alisogelea ule mlango kwa bashasha, akijiandaa kumkumbatia Sweetie wake ,akazungusha ufunguo wa mlango, kwani aliambiwa ajifungie kwa ndani, na ahakikishe hatoki ila kwa kibali maalumu, …alikuwa kama mfungwa, na hali hii ilimtesa sana, alifikia hatua ya kugombana na huyo mlinzi wa hapo hotelini, kwani hakujua ana kosa gani mapaka afanywe mfungwa wa ndani…

‘Sikiliza, wewe upo hatarini, usifikiri mimi nafurahia kufanya hivi, naacha kazi zangu za maana nakulinda wewe, kama nikikuachia kuna mawili, utaenda kulala jela au utatekwa nyara na hawo wabaya wako, na hawo wabaya wako nia yako ni kukuua….nakupa kwa ufupi, na si vyema ukajua zaidi kwasababu kama nilivyoambiwa una matatizo ya ubongo, unahitai muda wa kupumzika…’akaambiwa na yule mlinzi.

‘Hiyo hatari sijaielewa, maana hata kama ni mfungwa alzima ajue kosa lake, sikumbuki kumfanyaia mtu ubaya, sikumbuki….ooh, mnanfanya hata kichwa kiume, na kwanini mke wangu aondoke peke yake, nilitakiwa tuongazane nay eye…?’ akauliza huku akiwa kachoka na hayoo anayotendewa.
‘’Yeye lazima arudi kule mara moja, na hili ameombewa kisheria, kuwa kwa vile yeye ni muajiriwa, anatakiwa afike kwa muajiri wake, amweelze hali halisi , halafu atarudi, na kpewa siku moja tu,, kwahiyo lazima atarudi…’akasema yule mlinzi.

‘Muajiriwa eeeh, haya sawa akirudi tutaongea vyema…’akasema kwa kukata tamaa.

Akaufungua ule mlengo akiwa na tabasamu tele mdomoni, na macho yake yakakutana na mtu tofauti na alivyotegemea, na kumfanya akunje uso kwa hasira,. Akasogea pembeni kumpisha yule mtu huku akiwa kakasirika, hakutaka hata kuongea kwa wakati ule, lakini ilibidi amtii huyu mtu, kwania kama kweli ndiye anayewalinda, basin i mtu muhimu sana kwao.

Akaingia mkuu wa ulinzi wa ile hoteli alipitisha macho kuzunguka kile chumba kuhakikisha kuwa kila kitu kipo salama , halafu akasogeela dirisha na kulifunga, akamgeukia Sweetie na kutabasamu, ….

‘Huatakiwi kulifungua hili dirisha na kuliacha wazi, wenzako wanaweza kutumia upenyo mdogo tu kukumaliza, ingawaje kwa hapa hakuna mtu anayeweza kufanya lolote kwasababu ya huo ukuta wa nyumba ya pili, …kuna mtu aliuliwa hapa kwa kupigwa risasi toka jengo la tatu toka hapa, wametumia bunduki yenye kiona mbali…sasa ni vyema tukachukua tahadhari zote kuhakikisha hakuna baya linaloweza kuwakuta, na hilo nawahakikishia hivyo.

Akasogea na kukaa kwenye sofa, na kusema kwa sauti ndogo, `Humu ndani kuna hewa ya kutosha,, kuna kiyoyozi kinachoweza kubadili hali ya hewa unayoitaka, kwahiyo huhitaji hewa ya nje…’akasema hku akiegeema lile sofa… alikuwa kashika kitabu, akionyesha kuwa yupo kazini, na hapo labda alikuja kusainisha bili ya siku mbili ambazo hakuweza kufika hapo na kumsainisha.

‘Nimekuja kukusainisha kumbukumbu zetu, maana siku ile tulipoachana sijaweza kufika maeeno ya hapa, lakin sio kwamba nimekutelekezeni, hapana, nipo nanyi, nawaona kwa muda wote, ulinzi ni mia kwa mia… natumai kila kitu kimekuwa kikienda shwari, sitegemei kutokea baya , kwasababu naviamini hivi vyumba vyangu maalumu..’akasema yule mkuu wa ulinzi akitoa kitabu na kumsainisha Sweetie.

‘Najua mkeo hajurudi …na hii inanipa shaka kidogo, nitampigiia simu kama muda ukienda sana, na sizani kuwa anaweza kufanya uzembe wa kuamua kulala huko, kwasababu wajamaa wanamfuatilia , kwa makini….lakini hadi saa hizi atakuja kwa usafiri gani, …labda kukodi gari, ….inantia wasiwasi wkasaabu mimi pia ni mmojawapo wa waliomzamini…kama atafanya uzembe, atanifanya nisiaminike tena…’akasema huyo mlinzi.

‘Mimi nina imani kuwa atakuja muda sio mfupi, huwa haahidi kitu bila kukitekeeleza, namfahamu sana mke wangu, labda ni sababu ya usafiri, au kapitia mahali….siju usafiri wa huko ukoje, …!’akasema Sweetie.

‘Hujui usafiri wa huko ukoje, mbona hapo unanishngaza kidogo, kwani wakati wa kuja mlipanda ndege , mpaka usikumbuke usafiri wa huko ulivyo, na barabara hazijabadilika kabisa, toka lini sijui, hakuna maendeelo kwasababu ya vita, watu kila kukicha tinasikia milio ya bunduki, …sasa hapa ni mjini tunasikia hivyo, je huko vijijini ambapo hawa wapiganaji wa msituni ndipo wanapojificha….wananchi wanapata shida…lakini yote haya yana mwisho…. ‘akasema yule mkuu.

‘Kwanini watu wapigane, ….inanipa shida kidogo, ndio maana akili yangu haikubali kuwa hapa ni kwetu, nina imani kuwa kumbukumbu ziangu zinaenda sawa, mimi sio mtu wa hapa….’ Akasema Sweetie, akijaraibu kutafakari. Halafu akasema kwa sauti ya chini…`’Inavyoonekana kwetu sio hapa, hata sijui nilifikaje huku, maana kama nchi hii sio Tanzania, basi hapa sio kwetu, nahisi niliokolewa…nahisi kama nlizama ndani ya maji, nahisi kama nilikuwa ndani ya meli, boti…nikazama, halafu nikaokolewa, lakini hilo la kuokolewa sina uhakika nalo, nakumbuka kitu kama hicho ….’ Sweetie akawa anaongea huku akitafakari.

Yule mlinzi alikuwa kamzarau, kwani alihsambiwa kuwa huyu mtu ana matatizo ya ubongo, kwahiyo inawezekana akaweweseka, au akaongea maneno ya ajabu ajabu…na hili anavyoliona alijua kuwa kweli huyu jamaa bado kachanganyikiwa. Akamtizama, halafu akawa anafungua kitabu chake cha kumbukumbu za wateja wake, ….

Sweetie naye alikuwa akainama chini akiwaza, na kutafakari, ….Kila siku kumbukumbu zilikuwa zikimrejea na mpaka akafikia hatua ya kukumbuka tuki o lililomtokea, lakini hakumbuki baada ya tukio lile ilikuwaje kuwaje hadi akafika nchi hii ngeni. Baadaye akainua kichwa na kumwangalia yule mlinzi, ambaye alikwua anaandika mambo yake kwenye kile kitabu, alipomaliza akainuka kichwa kumtizama Sweetie na macho yao yakakutana.

‘Uliwahi kusiki meli iliyozama, nchi ya jirani…?’akauliza Sweetie.

‘Meli iliyozama…?’ akauliza yule mlinzi kwa mshangao, halafu akainuka kutaka kuondoka, lakini akaona amibu ajuavyo yeye, ilikutomkatisha tamaa mteja wake…`Ndio, nakumbuka mwaka juzi, kama sikosei, ..mmh, ilikuwa mwaka juzi au mwaka jana, nafikiri kitu kama hicho…kulikuwa na meli moja ilizama katika ziwa Victoria, meli hiyo inamilikiwa nan chi ya jirani, kuna hata watuwetu walikuwemo humo…watu wengi walipoteza maisha, nakumbuka ilifiki hatua watu waligoma kununua samaki waliotoka kwenye ziwa Victoria….’akasema Yule mlinzi.

‘Mhh, basi kama ni hivyo, nahisi kumbukumbu zangu zinanijia vyema, nahisii hata mimi nilikuwa miongoni mwao, na sikumbuki niliponaponaje, nashindwa kujua niliokokaje…’akanyamaza na kumwangalia yule mlinzi ambaye alikuwa kitabasamu, kuonyesha kuwa anaambiwa porojo, ambazo sio za kweli.

‘Uliokokaje…?’ akauliza huku anacheka, akaanza kuondoka hatua ndogo ndogo na kusema `Usianze kutunga hadithi zako za kuchanganyikiwa hapa, ….haiwezekani mtu utoke mahali ilipozama hiyo meli hadi ufike huku nchini kwetu,…usijiafanye kwua wewe ni bingwa wa kuogolea, ….hahaha…ulikuwa uanwaza kuhusu meli au ulisoma mahali na sasa akili inakutuma hivyo?’ akageuka na kumwangalia kabla hajafungua mlango. ‘Nahisi akili yako inawaza mengi, umekunywa zile dawa zako , maana mkeo alianimabia niwe nakukumbusha, ingawaje kwakweli nilishaanza kuisahau kuhusu hizo dawa zako..?’akauliza yule mlinzi akiwa kasimama na kumwangalia Sweetie.

‘Najua wengi hawataamini hilo kwasababau mumeshaanza kuniona tahira, lakini huo ndio ukweli, kama kweli kulikuwa na meli ilizama, basi akili yangu imeshaanza kufanya kazi, ipo siku nitawaambia ilikuwaje, lakini kwasasa bado nashindwa kuunganisha hizi kumbukumbu vyema…na nashindwa kuelewa kwanini hata mke wangu haniamini …hata yeye, anafikia hata kusema kuwa nimeshindwa kumtambua vyema…lakini hata mimi nabakia kuduwaa, kwani namuona kabadilika kiasi kikubwa, …mmh, kweli kama hata mimi nawashangaa watu, namshngaa hata mke wangu, sembuese watu wengine…lakini nina uhakika sijamsahau mke wangu..tafadhali nakuomba umpigia simu uhakikishe kuwa yupo salaam, maana inatia wasi wasi…..’akasema Sweetie na kabla hajamaliza kuongea wakasikia sauti kama ya mtu anayegonga mlango, na yule mlinzi akageuka haraka kutizama mlngoni …na ghafla akatoa bastola yake..


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Pole Sweetie! kila asemacho wote wanamwona kama amechanganyikiwa..aahhh umekatisha utamu maaana hapa palikuwa kivyote patamu na pia pnaogopeshe kidogo...nasubiri kwa hamu kusoma ni nani aligonga mlango.....

Iryn said...

Duuuuuuuuh
m3 wewe ni noumer....!
2po pamoja sana

Anonymous said...

Yes! Finally something about psychic advisors.