Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, October 20, 2011

Miaka 50 ya Uhuru
Nakumbuka kuna haditho moja alinisimulia babu, na hiyo ilikuwa inaaminika kuwa hivyo, kuwa unapoona kuku wamesimama mlangoni, hata kama sio mlangoni, lakini maeneoya nyumbani na kuku hawo ni wa kwako, ujue atakuja mgeni, sasa katika hadithii hiyo, babu alisema kuwa hawo kuku wanajadiliana kuhusu huyo mgeni kuwa atakuja na neema gani, lakini mmoja wa huyo kuku anamwambie mwenzake kuwa huenda akija siwe ni neema, bali inaweza ikawa ni kilio…

Katika hali halisi anapokuja mgeni mwenyeji anajaribu kuleta mabadiliko, hasa ya usafi na maandalizi ya kumfanya huyo mgeni ajisikie kuwa anathaminiwa. Lakini inaweza ikawa sio mgeni kama mtu, inaweza ikawa tukio muhimu katika jamii, na ili kuleta tofauti watu wanakuwa na maandalizi rasimi, ikiwemo usafi, matayarisho na hata malazi na vyakula, ilimrtadi kuwe na utofauti fulani,…wanasema waswahili kuwa mgeni njoo mwenyeji apone, au sio.

Utotoni mgeni akija tulikuwa tunafurahia kuwa kutakuwa na maankuli ya tofauti na hasa kule kwetu lazima pilau ipikwe na kuku kuchinjwa kama sio mbuzi, …basi mnakuwa hamchezi mbali, maana mgeni anakuja wenyeji tutafurahia, hata kama hatuju ugeni huo ni wa namna gani, huenda ukawa ugeni wa kumuadhibu mmoja wetu kwa utukutu wake, lakini vyovyote iwavyo siku hiyo kutakuwa na furaha.
Mwaka 1961, ndipo tulipata uhuru wetu, na maandalizi ya mwaka huu naona ni tofauti kidogo, kwani mashirika mengi hasa ya kiserikali yamekuwa yakijiandaa kwa mapana zaidi, kwa vile tumeona ikitangazwa , na sio ya mashirika ya kiserikali tu , na hata ya watu binafsi wale walio na uzalendo wa ncho hii wamekuwa wakitumia mwanya huo katiika kutangaza biashara zao.

Kwakweli miaka 50 ni mingi sana, kwa nchi kama hii yetu ni jambo la kujivunia, kwani mengi yamepita, ya heri na ya shari na kila mmoja wetu anastahili kujivunia, na hata kupongezana, na kupongezana kwenyewe ni huko kufanyika kwa sherehe ya kumbukumbu ya uhuru, ambayo hufanyika kila mwaka, na mwaka huu maandalizi yameanza mapema kivitendo, na kila mmoja anakuwa anajua nini kinachokuja mbele yetu, na wengi tunachekelea tukisema mgeni aje mwenyeji apone.

Wenye umri kama wangu ambao hawakubahatika kushuhudi hilo tukio muhimu la kupata uhuru, tunasimuliwa au kusoma na hata kuona kwenye runinga, jinsi tukio hilo lilivyokuwa,na siku ya kilele, tarehe 9 December, macho yetu yanageukia uwanja wa taifa, na hapo ndipo nawaza kwa mbali na kuiuliza hivi mbona kunapokua na sherehe kama hizi tunaishia kuangalia tu, …..hakuna jinsi nyingine ya kufanya hasa katika siku-kuu kama ili kila mtu, ajihisi kuwa naye ameshiriki, maana mgeni aje mwenyeji afurahi, sasa sisi tubakia majumbani tukiwa tumefunga mkanda….

Sio mbaya, kunakuwa na mapumziko ya kutokwenda kazi, …lakini je kweli unaisherehekea hiyo siku? Kwa maoni yangu ni kuwa, ingelifaa, wote kwenye makampuni, wawe na namna ya kuwafanya wafanyakazi wao wahusike, wajisikie, kama tunavyofanya sherehe za kumaliza mwaka na x-mas, mofisini, na hata wafanyabisahara wawe na namna yao…hata kwa kupmba bendera, ingelisaidia tu, kuonyesha kuwa ni siku pekee nay a muhimu.

Nimeona mwisho wa mwaka, kuna kuwa na vijizawadi kwa wale mabosi wanaojali wafanyakazi wao lakini siku-kuu muhimu kama hii, mmmh,, tujaribu kufanya hivyo kwasababu siku hii inamgusa kila mtu bila kujali dini yake, imani yake kabila lake …ni siku-kuu ya kila mtu… au ndio sherehe ya kiserikali tu, tuwaangalie uwanjani wanavyofanya gwaride …tukiwa majumbani kwetu na tuombee mungu kuwepo na umeme, maana umeme ndiye mtawala wa kina-mna yake, vinginevyo tutaishia kusoma magezeti ya kesho yake..kuwa ilikuwaje, tuweni na uzalendo.?


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Umenikumbusha mbali sana mkuu, ujumbe mnzuri, lakini nani atakusikia, wabunge walitakiwa waweke hata sheria kuwa siku kubwa kama hii iheshimiwana kila mtu anayeishi humu nchini,...toeni hata vialawance...ili watu wapinge wali wale na watoto wao....mwisho wa mwakamnatoa zawadi, lakini je hii iliyofanya hata wewetajiri uwekeze kwanini usiiheshimu...mafisadi sijui wananisikia

Anonymous said...

Umenikumbusha mbali sana mkuu, ujumbe mnzuri, lakini nani atakusikia, wabunge walitakiwa waweke hata sheria kuwa siku kubwa kama hii iheshimiwana kila mtu anayeishi humu nchini,...toeni hata vialawance...ili watu wapinge wali wale na watoto wao....mwisho wa mwakamnatoa zawadi, lakini je hii iliyofanya hata wewetajiri uwekeze kwanini usiiheshimu...mafisadi sijui wananisikia