Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, October 28, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-42



‘Natumai unanikumbuka Docta Adam,..’Sauti ya kikamavu iliyosikika ilimshitua Docta Adam , karibu adondoshe ule ufunguo aliokuwa kakamata mkononi, akainua kichwa haraka na kumtizama huyo mtu. Na huyo mtu alimkaribia na kuja kusimama karinbu yake huku akisema `Samahani kwa kukujia muda kama huu, ni tatizo la usafiri, nilikwama kidogo njiani ndio maana unaniona sijaja na gari langu…’Adamu hakuamini macho yake akasimama vyema na kumwangalia, ingawaje alikwu ana hasira za kusumbuliwa, lakini ile hasira iliyeyuka haraka na kubadilika kuwa woga na wasiwasi.

Adam alimtizama tena huyo jamaa, ili kuhakikisha macho yake, halafu akageuka kutizama mlango na kushika kitasa cha mlango na kukitikisa kitasa cha mlango kama vile anahakikisha kuwa kafunga mlango vizuri, kumbe ilikuwa hali ya kuvunga, ili huyo jamaa asimwangalie machoni, moyoni alishashikwa na wasiwasi, hakujua kwanini moyoni alikuwa akihis hivyo, hali ambayo hakuwahi kuihisi…akajipa moyo kama vile yupo vitani akageuka na kumwangalia yule jamaa, halafu akajifanya mnyenyakevu, akijua kuwa huyo aliyepo hapo ni mtu muhimu wa serikali, akatabasamu kiuongo-uongo na kusimama kama vile askari afanyavyo, akasema kwa sauti ya mkwaruzo.

‘Jambo afande, …mkuu, ..Inspecta, habari yako mkuu, sizani kuwa umenijia kwa jambo dogo hasa kwa muda kama huu, ndio nilikuwa nafunga funga, ofisi, na mimi nikapate muda wa kujipumzisha unajua tena hizi kazi zetu muda wowote unaweza kuitwa, hizi kazi zetu hazina tofauti na kazi zenu, …kwahiyo ukipata upenyo wa kujipumzisha unatakiwa uutumie ipasavyo, ndio mkuu nikusaidie nini…?’ akaongea kwa kujiamini, lakini moyoni alishatingwa an mashaka, kwanini huyu mtu amjie , toka mjini hadi huku anafuata nini..!

‘Ndio , sio jambo dogo, ukizingatia kuwa nina majukumu ya kiofisi, lakini …wakati mwingine unatakiwa kuwasaidia vijana, ….kwani mimi siwezi kuumwa docta, huenda nimekuja kutibiwa, ….au ukishafunga, hata akija mgonjwa taabani hihitajiki kutoa huduma….?’akauliza huyo jamaa.

‘Inategemea ugonjwa na mgonjwa, …na ujuavyo, kila ofisi ina utaratibu wake, kama ni mgonjwa wa dharura kaletwa baaada ya muda wa kazi, atakutana na dakitari wa zamu, lakini hawezi kuja kwangu moja kwa moja…labda iwe na mimi nipo zamu, maana hata mimi kuna kipindi nakuwa zamu, ikibidi…’akasema Adam.

‘Basi mimi ni mgonjwa maalumu, ndio maana nimekuja kwako moja kwa moja, …sawa, kwa ujumla nisingetakiwa mimi nikujie mwenyewe moja kwa moja, lakini wakati mwingine inabidi iwe hivyo,…na ili nisikupotezee muda wako, kwasababu sina usafiri, basi tutaongea tukiwa ndani ya gari lako, kama hutojali, au tukifika mahala patulivu tusimame kidogo tuongee, ni maswali machache ya kuhakikia, nina uhakika sitakupotezea muda wako mwingi…nahitaji saan ushirikianao wako…’akasema Inspecta.

Adamu aliposikia hivyo akaanza kujihami, kimoyoni alianza kumuwaza huyu mkuu, alishasikia sifa zake, na huwa anamuona tu juu kwa juu, hakuwahi kukutana naye na kuongea kwa karibu, leo ndio mara ya kwanza kuonana naye kwa karibu na sio karibu tu, ataka kuongea naye, sijui kuhusu maswala gani. Alianza kujipnga kichwani, vipi atamjibu, na kama ikiwa ni maswala magumu , dawa pekee iliyopo ni kusema asubiri ataongea wakili wake akiwepo…

Mkuu huyu wa polisi aliletwa hapa nchini ili kutoa mafunzo katika ile hali ya ujirani mwema, nchi hizi zimelkuwa zikibadilishana wanausalama wao, na hii imekuwa ikitoa changamoto, kwa kujenga ushindani fulani. Huyu mkuu alipoletwa alionekana mchapakazi , na hakuna mtu aliyeweza kumwingilia katika majukumu yake. Wapo waliojaribu kumbadilisha ili ashirikiane nao, lakini haikuwa rahisi, alikuwa mtu wa msimamo, na wahalifu wengi walikuwa wakigwaya pale wanapomuona.
Katika mafunzo yake , Adam, alikuwa kasomeshwa jinsigani ya kupambana na watu kama hawa, kwahiyo haikumtia shaka sana, ila kilichomtia shaka ni kutaka kujua nini kilichomleta, kinahusiana na jambo gani,…akageuka kumwangalia na kumwambia.

‘Sawa mkuu, lakini mimi nikiwa naendesha gari huwa sipendi kuongea, ….na hasa, ikitegemea aina ya mazungumzo,….ungenidokezea ni jambo gani unalotaka kuongea na mimi, ili kama…eeh, naweza kufungua mlango tuakongelea humu ndani, ni jambo gani mkuu?’ akauliza Adam.

‘Aaah, una wasiwasi na jambo lolote, sio jambo la kukutia wasiwasi, ni katika kuwekaan sawa, tu..usiwe na wasi wasi kabisa…wewe twende , na haina haja ya kufungua ofisi wakati ulishaifunga…’akasema Inspketa.

‘Nimekuuliza hivyo kwa lengo langu kubwa kama nilivyokuambia nikiendesha sipendi kuongea, pili ukiongea na polisi ni vyema kujua ni kwa kosa gani, …usije ukanitega kwa maswala yanayogusa sheria, ..' akanyamaza kidogo halafu aakendeela kusema;

'Vinginevyo kama sio maswali ya kisheria, hakuna taabu…naomba mkuu, yasije yakawa maongezi yakuniumiza kichwa…sawa haya twende, nipo tayari….’ Akasema Adamu, huku akiwa an shaka shaka, ya kutaka kujua ni nini kilichomleta huyu mtu toka mjini, …akajipa moyo na kusema kimoyomoyo,kuwa jambo jema ukikutana na tatizo ni kukabiliana na hilo tatizo ni sio kulikimbia, na ni vyema kuondoa shakashaka kwa kufanya utafiti, na utafiti wa shaka shaka kwa mwenzako ni kukubali kuingia katika mazungumzo. Kwahiyo akakubalina na Inspecta na wote wawili wakaingia ndani ya gari na kuondoka.
********
Maua hakuwa na amani, kila dakika iliyopita, aliona kama masaa, alitamani angelipaa na kurudi mjini haraka iwezekanavyo, ….pamoja na mengine kichwani alikuwa haacho kumkumbuka Sweetie, …alikuwa kamkwepa kuingia naye mazunguzo, mpaka wapate nafasi inayostahili, hasa baada ya kuona kuwa keshaanza kurudiwa na kumbukumbu zake. Pia alitaka kujipa nafasi, kujiandaa kwa lolote linalomhusu huyu mtu aliyekwisha iteka nafsi yake.

Moyoni alishajiuliza maswali mengi, kuwa kama huyu mtu kumbukumbu zimemrejea, na atasema anaye mke wake, atachuku ahatu again, wakati keshampenda, je atakubali kurahisrahis hivi hivi tu, …hapana, lazima ajitahidi kulinda penzi lake, lakinikwa njia gani kama itazihirika kuwa huyu ni mume wa mtu?

‘Lakini kama kumbukumbu zimemrejea vyema, mbona bado anasisistiza kuwa mimi ni mke wake, hii bado inanitia wasi wasi,…’akasema kwa sauti.

‘Hlafu anasema nimebadilika, kwa vipi, mke wake alikuwa vipi na mimi nipo vipi, …..ina maana kwenye kumbukumbu zake hajamkumbuka mkewe alikuwa na sura gani, ….hapa nahis ipo namna, labda sehemu ya kumbukumbu bado haijereeja vyema, na kwa sababu hii, bado huyu mtu anahitaji mapumziko ya kina, haihitaji nguvu, …lakini nitajitahidi sana kuhakikisha kuwa nalilinda pendo langu, ….nitafanya juhudi zote, ikibidi…..sijui , ikibidi, sijui…’akawa anaongea huku anajiangali kwenye kiyoo.

Alipofika kwenye nyumba ile waliyopanga, alikuta kupo kimiya, hakuon ajabu ,kwani rafiki yake hayupo, alishaambiwa kuwa kaenda likizo, kwahiyo hakukuwa na mtu wa kuongea naye, na hata hivyo..hakutaka kabisa kulala hapo kwake, alichofanya ni kufika chumbani kufanya usafi, na baadaye akaoga, na kuchukua madini yake yaliyokuuwa yamebakia na kuhakikisha kuwa kila kitu kipo sawa, halafu akatoka nje kidogo kuangali mazingira ya nje, kama kupo salama,

….alipohakikisha kuwa kupo salama, akasogelea mlengo wa rafiki yake kujaribu kuwa umefungwa…akakuta umefungwa….

Baadaye akaamua kurudi kwake, akasogelea mlango wake, …na akahisi nywele zikimsisimuka, akahisi hatari, na hali ambayo humpata mtu, hasa kiwa peke yake, na alikuwa akisi hatari, na kwa vile yupo peke yake, anaweza akzania kuna adui, au kuna kitu cha hatari kipo karibu yake…alihisi kama kuna mtu anamtizama kwa lengo kwa baya, akageuka kuangali barabarani, na huko hakuona kitu cha kutia wasiwasi, kila mtu aliyeonekana, alikuwa akitembea au akiwa katika hamsini zake…

Akafungua mlango wake…na mara pua yake ikahisi harufu ngeni….harufu hiyo alishaisikia kabla, harufu ambayo ilimtia wasi wasi, akatamani kurudishia mlango na kuondoka zake,…lakini viungo vya mwili havikukubali kufanya hivyo akasimama kama mtu aliyepigwa na ganzi, alikuwa kasimama katikakati ya mlango, ambao alishaufungua wote,….akapepesa macho huku na huko kuangali pale varandani kama atamuona mtu, …hakuona mtu, ila alihis harufu…..na mara akasikia sauti.

‘Usiogope Docta, tumekukosa sana, umeondoka kipindi ambacho tulikuwa tunakuhitaji sana, unajua Docta wewe ni mwenzetu ila hujui hilo, wewe ni mwenzetu kwaababu unajali sana maisha ya watu, unajali sana uhai wa watu, …na ndilo sisi tunalolipigania, ila watu hawatuelewi, wanafikiri kuwa sisi kazi yetu ni kuua,…lakini tunaua tu palle inapotulazimu,mfano ukikutana na adui ukamwambia nyosha mkono upo chini ya ulinzi akasalimu amri, hauwezi kumuua, unamkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya kisheria akahaukumuiwe…’ Rose aligundua hiyo sauti inatoka wapi, lakini hakuweza kumuona huyo mtu.

‘Sasa tatizo linakuja pale unapompa mtu huyo amri, akawa kaikaidi hiyo amri, na pili hata kama atakukublai hiyo amri yako, ukemuweka chini ya ulizi, aua hataka kama kakaidi, lakini umemdhibiti, unampeleka kwenye vyombo vya sheria, sheria haifanyi kazi yake barabara,….watu wanatakiwa kutekeelza majukumu ya kisheria, hawafanyi kazi yao ipasavyo, mtu huyo anarudi uraiani na kuendeela kufanya maasi kwa kiburi….hapo tunakuwa hatuna jinsi…’ Huyo mtu alikuwa akiongea huku akufunikwa na apzia kubwa lililopo dirishani, alikuwa kasimama kwenye dirisha, na lile dirisha linapazia kubwa, ambali lilikuwa limemfunika.

‘Wewe ni nani na umeingiaje humu ndani..?’Rose akaingiwa na ujasiri wa kuuliza.

‘Tayari umeshanisahau Docta, mimi ni yule yule anayekutembelea mara kwa mara, ila safari hii umetuweza kidogo, maana, umebadili mlango,….umebadili kitasa chako…najua ni kwanini…kazi nzuri docta, lakini nilijua utakuja leo ,…wakati nakusubiri nje hukuniona, , ulipotoka tu nami nikajikaribisha ndani sisi ni wepesi sana,…., usiwe na mashaka, kabisa….’akasema huyo mtu.
‘Haya niambie safari hii nini kimekuleta , maana nina haraka nataka kuondoka …’akasema Rose, na kabla hajamaliza yule mtu akamkatiza na kusema.

‘Najua unataka kuruudi mjini, kwa ajili ya ile kesi ya mauaji au sio, …hahaha..unajua dunia hii ni ya ajabu kabisa, hawo hawo unaowaona ni wa maana kwako ndio hawo hao wanaowazungukeni, unakula nao, unashinda nao na hata unafanya kazi nao, lakini ni maadui zako..pole sana, …ila kesi yenu imekaa vibaya sana , unatakiwa kuwa mwangalifu sana, kwasababu hawo hawo wanaotka kukutetea ndio hawo hawo maadui zako, jaribu sana kuwa mwangalifu,… ndio maana kwa nia njema niliomba sana nikukute na wewe , na bahati nzuri tumekutana nawe…’akasema yule mtu.

‘Silkuelewi nini unachokiongea na hata hivyo ninakimbizana na muda, …’akasema Rose.

‘Hili ninaliotaka kukuambia sasa hivi ni muhimu sana kuliko huko kuwahi kwako, na ni kwa ajili ya manufaa yako na yule jamaa yako wanayemuita tahira, sio tahira yule, ipo siku utagundua hilo, na sio mtu wenu yule, ole wenu auwawe, na wenyewe wajue…nashukuru kuwa umechukua hatua njema ya kumlinda, na ilitakiwa wakushukuru sana kwa hilo…’akasema huyo mtu,na Rose aliona kama anampotezea muda wake tu.

;Wanishukuru kwanini…?’ Rose akazidi kuhamanika kujua zaidi, alitamani hata ake amsikilize yule mtu, lakini akaona bora asimame hivyo hivyo.

‘Kwani uchunguzi wetu, jamaa aliyemuua yule mtu kule hotelini anafanana sawa sawa na huyo jamaa mnayeishi naye, ana ndvu kama za huyo jamaa, yako, tunachojiuliza ni kwa vipi alitoka humo hotelini na kwenda kufanya hayo mauaji na kurudi , wakati ulimuacha mle chumbani…tumejaribu kumtafuta mtu mwingine anayefanana naye hatujabahatika kumgundua….sasa kuna hatari jamaa yako kukamatwa, vinginevyo apatikane mtu mweney sifa kama hiyo…hata sisi hatukubalianai na hilo kuwa ndiyo yeye muuaji , hasa ukichukua ule muda uliotumika, haiwezekani ….’akasema yule mtu na kumuacha hoi Rose.

'Haiwezekani akawa yeye, hilo mumekosea, au ndio nyie mumeafanya hayo mauaji na manataka kumbambikia jamaa wa watu, haiwezekni kabisa….’akasema Rose.

‘Kwetu sisi hatuna shaka, hiyo ndiyo sifa yetu tuliyopewa kwa sisi ni wauaji, …wapiganaji wa msituni, lakini jiulize kwanini tumuue mtu kama huyo, ili iweje, …hatuna shida naye, ila nakuonya kuwa polsi wa kimgundua tu, …oooh, huyo atakamatwa na kufunguliwa mashitaka…wenzenu walicheza vyema,..ina maana kama sio yeye, walishamgundua na kumtafuta mtu anayefanana na yeye, au mtu alijiigiza tu, na kujiweka ndvu, za bandia maana siku hizi utaalamu huo upo….’akasema huyo mtu.

‘Hilo halitatokea, huyo jamaa yangu hawezi kufanya jambo kama hilo, na kwa hali hiyo naomba uondoke nataka kuwahi huko mjini….’akasema Rose

‘ Sawa utaondoka, usiwe na shaka, ila nakupa kama tahadhari usimwamini sana huyo bosi wako, hilo tulitaka tukuambie mapema, lakini hatukuwa na uhakika naye mwanzoni, ….alijivika ngozi ya kondoo…ni hatari sana, …hawa watu wa namana hiyo, watakuja kutuletea matatizo…lakini hata hivyo, lengo lao halipo mbali sana na sisi ina wao wanatumia utaalmu wao kudai haki inayodhulumiwa, kama sisi tunavyofanya kwa njia ya msituni…’akasema yule mtu na kumfanya Rose atulie kusikiliza

‘Mimi siwaelewi, kwanini muingize nchi kwenye vita mkidai kuwa mnadai haki…kwanini msikae kwenye meza moja na serikali mkajidili hilo….?’akauliza Rose

‘Swali zuri sana, kwasababu hawataki kufanya hivyo, wangelikubali hilo, mbona tungeshamalizana, na kwanini hawataki hilo, kwasababu wanajua hawatapata hicho wanachokitaka, kuhujumu mali ya uma, kuhakikisha wao wanashikilia madaraka…na sio kwmba hatukuwahi kuomba hilo, tuliomba tangu tupo makazini, lakini tulionekana mahaini, ndio maana tukajitosa maporini….’akasema yule mtu.

‘Haya sasa niambie umekuja kufanya nini, …na…nashukuru…’akataka kuongea zaidi, lakini yule mtu alitoka haraka pale alipokuwa, na kumpita Rose kama mshale, ilikuwa muda wa sekunde chache, alikuwa keshatoka nje na kuyeyuka, na Rose alibakia ameduwaa….

Rose alitulia kufikiria ni kwanini huyo mtu kaoandoka haraka hivyo, lakini hakuweza kupata jibu la haraka alichofanya ni kutoa chupa yake ya manukato na kupulizia humo ndani kwa haraka, ili angalau ile harufu ya majasho ya huyo mpiganaji wa msituni iondoke, na baadaye kwa haraka haraka akaanza kujiandaa kuondoka, huku akiwaza yale maneno, …

‘Usimwamini sana bosi wako…’akayarudia maneno hayo kwa sauti …halafu kashika shavu huku akiwaza, na kusema kwa sauti; `haijalishi kumwamini au kutokumwamini,…mimi sihitaji kazi kwake tena, …nitatafuta sehemu nyingine, lakini kwanza nijue kuhusu Sweetie…Sweetie wangu,….’ na mara akanyamaza kimiya, kwani alisikia kama mtu anagonga mlango,…kabla hajahakikisha hilo, mlango ukagongwa tena na safari hii kwa fujo….ooh, akajua ndiye huyo jamaa karudi tena nini…lakini…ooh

NB Tukutane sehemu ijayo, nawatakia ijumaa njema,


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Fadhy Mtanga said...

Kama nikiambiwa nitaje waandishi ama wasimulizi wa hadithi stadi kabisa wa kizazi hiki katika uandishi wa Kiswahili, basi jina lako nitaliweka namba moja katika orodha yangu. Hakika wewe ni msimulizi stadi kabisa wa kizazi kipya.

Ahsante sana.

emuthree said...

Nashukuruu sana mkuu , Fadhy Mtanga, na maoni kama haya yananipa moyo nakujipa matumaini kuwa , hata kama hawa jamaa wataniondoa hapa, naweza nikajiajiri katika utunzi wa vitabu(ndoto ya Alinacha), maana vitendea kazi na...lakini mungu yupo, shukurani mkuu