Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, October 17, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-38
Rose alipoachiwa ka dhama alikimbilia hotelini kwake, na alipofika tu mapokezi akakutana na mkuu wa ulinzi mle hotelini, alikuwa akiongea na wenzake, na alipomuona Rose anaingia akakatiza mazungumzo na kua kumpkea pale mlangoni. Alimpa pole kwa yote yaliyotokea na kumhakikishai kuwa asiwe na wasi wasi, kwani muuaji atakamatwa tu, na polisi wanamshikilia yeye ki makosa,…

Rose yeye aliona huyo mkuu wa ulinzi anampotezea muda wake , yeye mawazo yake yalikuwa kwenda kukutana na Sweetie, ajue kuwa yupo salama na anaendeleaje, lakini kila alipotaka kutoa hatua yule jamaa mkuu wa ulinzi, alikuwa kama anamzua kwa kumganda na maswali mengi maswali na porojo nyingi mwishowe akaamua kumwambia ukweli;

‘Samhani mkuu, hapa nilip mawazo yangu yapo kwa mwenzangu, kwa ni nilivyomuacha jana lazima atakuwa na wasi wasi sana, ngoja nikamuona kwanza, kwasababu nilimuacaha akiwa anajisikia vibaya, na sijui hali yake ipoje..’akasema Rose.

‘Oooh, mwenzako, usiwe na wasiwasi naye kabisa …nilimuhamisha jana usiku, na kumpeleka sehemu ya usalama zaidi, na kule najua yupo salama, ingawaje sijamtizama tangu nimpeleke kule…lakini nina uhakika atakuwa hajambo na yupo salama….ila anaonekana kama mtu aliyechanganyikiwa kidogo, ana matatizo gani, ….?’ Akauliza yule jamaa, akiendelea kumpotezea muda Rose.

‘Ana matatizo …? ..kwani umemuonaje….?’ Akauliza Rose kwa wasi wasi,…`Ndio anaumwa , lakini sio kwa hali mbaya kiasi cha kuchnganyikiwa….ooh, unanitisha ngoja nikamuone haraka..’akasem Rose akianza kupoandisha ngazi za kwedna juu…...!’ akasema Rose.

‘Ngoja tuongozane maana chumba nilichomuhamishia huwezi kukiona na nilimfungia mlango kwa nje, baada ya kumuona kama kachanganyikiwa hivi , ili asije akatoroka…’akasema yule mlinzi na kumfanya Rose azidi kuwa na wasi wasi, na hatua alizipiga za haraka haraka kuelekea juu, huku yule mkuu wa ulizi akifuatia kwa nyuma, wakaongozana hadi kwenye hicho chumba alichowekwa Sweetie, …..Yule mkuu wa ulinzi akafungua mlango,…na mlango ulipofunguliwa tu macho yao wote wawili yalitua pale akafuni alipolala Sweetie…

‘Vipi Sweetie, …?’Rose akamkimbilia Sweetie pale sakafuni alipolala, na bahati nzuri wakati huo Sweetie ndio alikuwa anazindukana toka katika kupoteza fahamu, aliinua kichwa na kutizama huku na kule halafu akamwangalia Rose machoni, …akajaribu kutabasamu, lakini baadaye akakunja uso na kugeuka kumtizama yule mkuu wa ulinzi…akiwa kama anauliza kumetokea nini….!

‘Mke wako huyo kaachiwa , nilikuambia kuwa ataachiwa, ..na nimepewa amri kuwa msiondoke hapa mpaka upelelezi ukamilike, ….kwahiyo mna siku moja ya ziada, na mimi nitaendelea kuwalinda, lakini kwa masharti mawili, kwanza mfuate yale niliyowaagiza, kuwa msitoke toke nje bila kibali changu, kama ni lazima, itabidi tuongozane, pili nahitaji malipo ya mwanzo tuliyokubaliana, maana haya ya leo na sijuii ya kesho yatakuwa vipi hayo ni hayo ya kesho yatakuwa makubalianao mengine, sawa…?’a akasema Yulemkuu wa ulinzi.

‘Sawa, nitakupa hela yako, haina shida,….’akasema Rose.

‘Pesa umepatia wapi, Sweetie’akauliza Sweetie kwa haraka.

‘Usijali Sweetie, pesa zipo, tutamlipa tu, ninachotaka ni usalama wako,…’akasema Rose

‘Ila nakuomba ukiulizwa na polsi kuwa kwanini mlihama toka mlipokuwa awali na kuja huku, hakikisha mnasema kuwa mlitafuta vyumba vya bei ndogo, ili kubana matumizi, sijaongea na hao polisi kwa mapana, wamenihoji kidogo, lakini najua leo watauliza maswali mengi zaid na huenda hilo linaweza kuwepo, name nitawajibu hivyo hivyo, kuwa amliniomba niwatafutie chumba cha bei ya chini kuliko kile cha mwanzoni,…, ila kwa kujihami,…na kwa uaslama wenu, lazima tuwe pamoja kwa hili tukio la jana, aua sio…’akasema yule mlinzi kabla hajampa Sweetie nafasi ya kuongea kwani kwake yeye alishamuona kama mtu aliyechanganyikiwa….

‘Usalama wangu, kwani nimefanya kosa gani, mbona mnanichanganya, huyu mtu anayejiita mkuu wa hoteli anasema atatulinda, kwanini tulindwe, ..halafu …mnasema kwa usalama wangu, mara kwa uslama wetu, kuna nini kinaendelea hapa…?’kabla hajamaliza simu ya yule mkuu wa ulinzi ikalia, na kwafanya wote kuwa kimiya, …na yule mkuu wa uslama akaipokea… akasikiliza kwa makini , na baadaye akawageukia Rose na Sweetie, akasema .

Polisi wamekuja kwa uchunguzi, zaidi wanataka kuongea na wewe, lakini bahati nzuri wakili wako alifika mapema kawazuia kuongea na wewe bila yay eye kuwepo, lakini polisi hawataki , wanakutafuta, kwahiyo cha muhimu, nikutoe humu hadi kwenye chumba ambacho mtakutana na huyo wakili, ili hawo polisi wakikuona wakuone upon a huyo wakili….au unasemaje?’ akasema yule mlinzi, na kabla hajasema neno akaendeela kuongea.

‘Kwa ujumla hawajui kuwepo kwa huyu mumeo, sijui kwanini, na ni vyema mkaendelea kuwa hivyo, huyu mtu asionekane kwa muda huu, kuna kitu kinawasumbua polisi pia, kuhusiana na huyu mtu wako, kuwa ulipokuja hapa mara ya kwanza ulikuwa na mtu, akachukuliwa hapa kama mgonjwa, ….lakini uliporudi hukurudi naye…lakini hilo halina nguvu sana, …ila kwa polisi wanaweza wakahisi vinginevyo wakitaka kujua huyo mtu yupo wapi…na wanaweza pia wakasema huenda huyo muuajindiye huyo mtu mliyekuja naye,….kwasababu haonekani,…na najua polisi walivyo, watakuulizia tu ,huyo mtu yupo wapi. ….’akasema yule mkuu wa ulinzi.

Rose akashituka aliposikia hivyo, na akawa anawaza ataawaambIa vipi hawo polisi wakimuulizia maswali kama hayo…., ina maana kweli wanaweza wakaenda mbali kiasi hicho, cha kumuhisi Sweetie wake kuwa ndiye muuaji, ndio maana haonekani, na akisema ukweli, ina maana hawo watu wabaya watajua kuwa huyo mtu bado yupo hai…je atamlindaje Sweetie wake asiingizwe kabisa kwenye huo msukosuko…..na hawo watu wabaya wanaomtafuta Sweetie au yeye wana uhusiano gani na Adamu, ….kabla hajawaza zaidi ilibidi akubaliane na msimamo wa huyo mlinzi, kwani hakuwa na jinsi ila kukubali tu, akamgeukia Sweetie na kumwambia asiwe na wasiwasi, kwasababu hana hatia yoyote.

Sweetie akataka kusema kitu, lakini akatulia na kuwangalia wote wawili kwa zamu bila kusema kitu, hakujua hata aseme nini, maana kila kitu anachokiona kwa muda ule ni kigeni kwake, na kila akijaribu kuuliza majibu anayopewa hayaingii akilini, akajipa moyo kuwa muda bado upo,
….akamgeukia Rose, na kumwangalia kwa makini, akashindwa kuamini, ina maana mke wake ndio kabadilika kiasi hicho, …haiwezekani, ina maana akili zake hazijawa sawa au ni kweli….
‘Kabla hujaondoka naomba nikuulize kitu Sweetie…? ‘Sweetie akamnong’oneza Rose sikioni, wakasogea pembeni kidogo.

‘Hebu niambie ukweli, …wewe mbona umebadilika kiasi hicho, na nani ulikuja na wewe toka Dar, umekuja na rafiki yangu au ulikuja peke yako, na huyo aliyekufa ni nani..? ‘akajikuta anauliza maswali mengi kuliko alivyokusudia.

‘Toka Dar….?! ….Sikiliza Sweetie, huu sio muda wa kuyaongelea haya, najua una maswali mengi, ikizingatia kuwa kumbukumbu zako zimeanza kurejea, na hata mimi nina maswali mengi ya kukuuliza, na yote haya yanahitaji muda, na sasa sio muda muafaka, …nakuomba tafadhali tulia kwanza tulimalize hili, …au uansemaje Sweetie?’ akasema Rose huku akimfunga vifungo vya shati ambavyo vilikuwa havijafungwa vyema, na macho yao yakakutana….

Wakiangaliana machoni kwa muda mfupi na baadaye Sweetie aligeuka kumwangalia yule mlinzi aliyekuwa kasimama, kwa kuona aibu kwa kile anachofanyiwa na Rose, lakini yule mlinzi alikuwa kaangalia dirishani, kwani alijua hayo yanayoongewa ni maswala ya mke na mke hayamhusu, na kipindi hicho wakati, Sweetie anamtu jicho yule mlinzi ndio wakati huyo mlinzi keshachoka kuwasubiri, alikuwa amegeuka kuwahimiza wamalizie mazungumzo yao haraka…..

‘Usijali Sweetie nafanya hivi ili kumpa uhakika yule mlnzi kuwa sisi ni mke na mume, usiniangushe…’akasema Rose,

‘Kwani sisi sio mke na mume…?’ Akauliza Sweetie kwa mshangao

‘Usijali utalijua hilo karibuni, hasa akili yako ikiwa imerejea vyema, kwani kama hujanijua kuwa mimi ni nani ina maana bado kumbukumbu zako hazijawa sawa kidogo, lakini usijali ….’akasema Rose.
********
‘Rose polisi watakuja sasa hivi kukuohoji, ninachokuomba ni kutokusema lolote watakalo kuuliza, wewe waambie siwezi kuongea lolote bila idhini ya wakili wangu na utaongea tu pale watakapokubali kuwa mimi ni muwakilishi wako, unanielewa vyema, lakini kabla ya yote nilikuwa napenda kujua ukweli wa tukio zima, ilikuwaje hadi ukafika kwenye hicho chumba?’ akauliza yule wakili.

‘Mimi nilikwenda kuchukua vifaa vyangu kwenye kile chuba ukumbukle kuwa tulikuwa tunaishi mle kbla ahtujahama,lakini baadaye tuliamua kuhama kwenye chumba kingine cha bei ndogo kidogo, ili kubana matumiazi….’akasema Rose

‘Mliamua au mlishauriwa kufanya hivyo….?’akauliza yule wakili na hapo Rose akakaa kimiya.
‘Sasa nakuomba uongee hivyo hivyo bila kuongeza kitu ukiuliza na maaskari, kwani hata mlinzi wa humu amsema hivyi hivyo, na hapo ndipo polisi wanataka kuwatega…ingawaje kuna kitu kingine polis wamegundua na ndio maana wanataka kukuona, najua ndio hivyo….swali kwao muhimu ni kwanini ulikwenda kwenye hicho chumba, na usipojibu kwa uangalifu hapo watakuja kukuingiza kwnye kesi ya mauaji, kwani wamguendu kuwa, kuna mtu alionekana akipanda juu kwenye lile jengo, akiwa kashika kitu kama gitaa, wengi ndivyo walivyozania,…na jamaa jhuyo alipanda hadi juu kabisa ya hilo jengo…’akatulia yule wakili.

‘Utata unaokuja ni kuwa sio mara ya kwanza kwa mtu kama huyo kuoenekana akipanda kueleeka huko juu na kitu kama hicho,…je ni mpango wa siku nyingi, au imetokea tu kuwa hivyo…na kama ni mpango wa siku nyingi, basi utakuwa unaujua….,sasa kinachokunasa wewe kuingia kwenye haya mauaji, ni kwamba, huyo aliyeonekana akipanda kwenda huko juu, huwa anavaa koti refu, kofia na miwani ya kufunika uso, kama ulivyoonekana umevaa wewe jana walipokukamata…
‘Swali jingine, wakati mnatoka hospitalini mlionekana mkiwa na jamaa mwenye ndevu, huyo jamaa tangu uingie humu ndani hajaonekana tena, ni nani na yupo wapi?’ akauliza yule wakili.

'Jamaa mwenye ndevu..." akamaka Rose

NB: tutaonana sehemu nyingine tukijaliwa, wenyewe hawooooNi mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Duh, yaani kama naangalia movie ya kusisimua sana halafu umeme ukakatika ghafla! dah, i wish tungepata post hizi kila siku. nakuombea heri na mafanikio, utapata kilichoc hcema, usikate tamaa.