Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, September 14, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-26
‘Rose nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kukutetea, lakini imeshindikana, na kama ulivyoona kwenye kikao wote wameona kuwa nakudekeza , wamefiki hata kudai kuwa naingiza mapenzi kwenye kazi, …ni shutuma nzito kwa mtu kama mimi….ni sawa nimeyafanya haya kwasababu na kupenda, lakini kweli itawezekana kumpenda mtu asiyekupenda, kwa mtaji huo nikaona ni bora nilegeze kamba, ili nione ubavu wako, kuwa kweli na wewe unajali juhudi zangu…’ akasema Docta Adam, akiwa ameshika barua mkononi, ambayo ilikuwa amkabidhi Rose, lakini kila alaipotaka kunyosha mkono kumpa Rose, mikono yake ilikuwa inasita.

‘Kwahiyo ndio tuseme kikao kimeamua nini, maana mumeniita mbele ya kikao, nimejielezea, halafu mumeniambia nitoke nje, baadaye unaniita wewe, nasubiri kusikia kauli yenu, maana nyie ndio wenye mamlaka… lolote mnaweza kufanya…nyie ndio matajiri wa hii hospitali…’ akasema Rose akaonyesha mikono kuzuguka, kama vile anayaonyesha maengo ya hpo haopitalini.

‘Mimi ni kama wewe tu Rose, mamlaka yangu hayana uwezo mbele ya hawa wadhamini, ukumbuke wao ndio waliochanga mitaji yao hadi hospitali hii ikaanzishwa, hata kama chanzo cha hospitali hii ni wazazi wangu, lakini mtaji wa wazazi wangu ni mdogo ukilinganisha ni mitaji ya wafadhili hawa, na wana uwezo wa kunionoda mimi wakati wowote, kama kiongozi na kumuweka mtu mwingine wanayemuona anawafaa…na hili ndio linaloniweka mahala pabaya kuwa naonekana sifai kuongoza kwasababuya kukutetea wewe, …’ akasem Docta Adam

‘Kunitetea mimi…? Mbona nimeshajitetea mwenyewe, unanitetea mimi kwa vipi….?’ Akasema Rose na kusimama `Hivi nyinyi mna roho gani , ni utu gani huo mlio nao, wamekuja wagonjwa ambao hawana uwezo wa kutoa gharama za matibabu na wana hali mbaya, na wamefikia mikononi mwangu, nitawaacha kuwatibia wafe kwasababu hawana pesa, …..haiwezekani kujali pesa kuliko utu wa mtu, mimi hilo sitalkiweza kulifanya katu….ngoja nife masikini, lakini najua ipo siku wema wangu utalipwa tu….’ Akasema Roso.

‘Kwanza kama ningelifanya hivyo manavyotaka nyie, bado mngeligeuka na kunilaumu mimi..hilo nalijua kabisa kwa watu kama nyie…., au amnasema hivyo kwasababu imetokea tatizo hilo la kifedha ndio mnaanza kunilaumu, lakini mnashindwa kujua kuwa hata wagonjwa wengi wanakuja hapa kwasababau ya huduma zetu nzuri, kuwajali wagonjwa, na hawo wanawavuta wengine kuja au hilo hamulielewi….?’ Akasema Rose huku akiwa kasimama na kumtolea macho Docta Adam.

‘Ninakuelewa sana Rose, na ndio maana nikakutetea kwa hoja yako hiyo, lakini umewasikia wafadhili, walikuambia ungewaeleekeza hospitali ya serikali, ungeliwapa huduma ya kwanza halafu ukawaambia waende hospitli ya serikali….wao wamesema hivyo kwasababu hawapo kwenye uwanja wa vita, hawajui vita vilivyo…hawaju jinsi gani mgonjwa anfikishwa hapa akiwa mahututi na huwezi kumpa huduma ya wkanza tu, ukamwambia haya nenda hospitali ya serikali….hawa ni wanasiasa…. kama walivyo wanasiasa wengine, kazi yao kuagiza na kulaumu tu, lakini kama wangelikuwepo kwenye uwanja wa vita wakaona kazi ilivyo ngumu, wasingeagiza au kulaumu hivyo….’ Akasema Docta Adam.
‘Sasa kama ni hivyo, kama umenielewa, nini kinachofuata maana nina majukumu mengine, naomba nijue moja, nipo kazini au ….’ Akauliza Rose.

‘Kazi bado unayo Rose, mimi siwezi kukutupa, nakujali sana….nakupenda sana Rose, nitajitahidi kukutetea hadi nione mwisho wake,….ila wameagiza kuwa uendelee kuwepo lakini kwa masharti makali, kama ilivyoanishwa kwenye barua hii hapa…’ Docta Adam akampa Rose ile barua,na Rose alipoipokea hakutaka kuisoma, alichofanya ni kuiweka kwenye mkoba wake na kuanza kuondoka, na kumafanya docta Adam akashikwe na macho ya mshangao.

‘Sasa ndio nini Rose, ulitakiwa auisome hiyo barua tujue nini unatakiwa kufanya , ili nikufafanulie, na kama ni kusaidiana tusaidieane, wewe huoni hapo wamekutega na mwisho wa siku utakosa kazi kabisa, hebu subiri tuongee….’ Akasema Docta Adam, lakini Rose hakusimama akaondoka, na kumuacha Docta Adam akiwa kasimama mlangoni,na baadaye akasema `wewe binti unajifanya kichwa ngumu eeh, wewe mwenyewe utakuja kunipigia magoti…na nitahakikisha huyo anayekuharibu akili yako anapotelea huko alipotoka…wewe utakuwa mke wangu kwa udi na uvumba….
*********
Rose aliondoka kwa docta Adam akiwa kachanganyikiwa maana kile kikao kilimuweka njia panda, hakujua kwanini wamemlaumu kisi kile, badala ya kumsifia kwa juhudi zake za kujitolea za kuyaokoa maisha ya watu, hasa akina mama ambao ndio mara nyingi aliokuwa akiwasaidia…akina mama wanafika hapo wakiwa na hali mbaya, yeye hujitolea usiku na mchana kuwapa huduma, na wengine ni wajane hawana waume, hawana ndugu wa kuwasiadia anajitolea kuwapa huduma, na hata kujitolea pesa yake mwenyewe, lakini mwisho wa siku imekula kwake….sawa tenda wema uende zako….

Akiwa anawaza hayo mara akili yake ikamrudisha kwa huyu mgonjwa wake, akajiuliza kwanini ameamua kumsaidia huyu, ….naye atatoa sababu gani, ndio lazima amsaidie kwasababu hana ndugu , hana….na wala hajijui atokako, kwahiyo inahitaji huruma yake…alipowaza hayo akacheka na akajikuta akijiuliza mwenye `kweli ndivyo hivyo….’ Akacheka tena na kusema, `sijui kwanini nimeamua kumsaidia huyu mtu, na hata kuishi naye humu ndani, na hata kunihatarishia maisha ya ajira yangu.

Alipofika kwake akagonga mlango, akaona kupo kimiya, akajaribu kuufungua mlango , akakuta upo wazi, akaita `Sweetie, mbona mlango hujafunga kwa ndani, nilishakuambi…’ akajikuta akinyamaza na kuhis mwili ukimsisimuka na woga kumtanda….harufu…mmh, ile harufu ya wapiganaji ilikuwa imejaa ndani, na….ina maana wamekuja kumchukua Sweetie…hakuogopa kuingia ndani alaipofikiria hilo, na alipofika kati kati ya varanda akasimama kama mtu aliyeamrishwa kuwa `simama..’

‘Karibu Docta Adam , tulikuja kukutembelea nakama dakika kumi zilizopita, tukaamua tukusubiri kidogo, hatuna lengo baya kama tulivyokwisha kukuambia, lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunawapa moyo kwa kazi zenu za kujitolea hasa wewe mwenyewe…na, umeona sipo eke yangu leo, nimekuja na wapiganaji wenzangu….’ Rose alikuwa kama kamawagiwa maji ya baridi na kuganda, hakuweza kusema kitu.

‘Huyu hapa utamkumbuka sana, kwani wewe mwenyewe ulijitolea kumtibia , ingawaje alisema kuwa ulionekana ulikuwa unawachukia wanaume, kwani hata hiyo kauli uliwahi kuitoa na yeye akasikia, lakini hata hivyo ulimsaidia sana kumtibia, maana alikuwa hana kumbukumbu kwasababu ya mabomu na majeraha….na huyu hapa ndiye yule mtaalamu wa silaha, ambaye aliwahi kuwababaisha hata maaskari wa serikali na kumkamata mtu asiyehusika kabisa, wote awa wamekua kukua ahsanet zao, na tunaomaba kwa moyo wa dhati uzipokee zawadi zao…’ akasema yule askari wa msituni

Rose akawa na hamasa ya kumwangalia huyo mtaalamu wa vita, ili ajue kwanini walimfananisha na sweetie, na kweli alipomtizama , mwanzoni alitaka kusema ndiye Sweetie, akaamua kuvaa magwanda ya uaskari, lakini aligundua kuwa huyo jamaa ana midevu mingi, licha ya kuwa kajinyoa, lakini bado zilionekana zikiwa zinaanza kuota…

Wote walisimama wakainamisha vichwa kuonyesha shukurani na kimfuko kidogo cha ngozi kikatolewa, na yule jamaa ambaye ni kiongozi wao mwenye macho ya kutisha akamimina kwenye mikono yake na kutoa madini…

‘Hii ni zawadi ambayo watu wengi wanaitafuta kwa udi na uvumba, hii ni dhahabu …ukiiuza utapata hela za kukutosha kufungua hospitali yako mwenyewe….’ Akasema yule mkuu wao
`Na hutapata usumbufu tena, kwanza kauze kidogo, uwalipe hilo deni lao, halafu nyingine utaiuza uende Marekani ukasome, ukirudi unafungua hospitali yako, unakuwa huna matatizo, hii yote tunakupa kwasababau ya wema, wako, tenda wema popote pale bila kujali ni nani unayemtendea, ipo siku utalipwa fadhila zako na fadhila hizoo unaweza ukalipwa na hata yule usiyemtegemea, sisi mnatuona majangiri, mnatuogoapa kama simba, lakini tunajali watu…pokea hizii zawadi na wala usiogope kuwa labda tunakupa kwa masharti, hakuna masharti…vitu kama hivi tunavyoo vingi kutokana na kazi zetu za maporini…’ akasema yule wanayemuita mtaalamu wa silaha.
Rose hakuinua mikono yake alibakia mdomo wazi, hajawahi kuiona madini kama yale katika maisha yake anasikia tu dhahabu dhahabu leo anaziona kwa macho yake na aanaambiwa kuwa hiyo ni mali yake, na….hata kabala hajasema nini wale watu wakatoka na kupotea kama upepo, hata alipotoka nje kuangalia hakuona wapi walipoelekea…akazisogelea zile dhahabu na kuzitizama na kugundua kuwa ni dhahabu kamili…sio kuwa kadanganywa..

Akafungua kabati lake la nguo na kutoa kimfuko cha plastiki ambacho kilikuwa na mawe yeney rangi sawa na dhahabu, lakini zilikuwa sio dhahabu, akayatoa yale mawe na kuyaweka mezani . halafu akachukua zile dhahabu na kuziweka kwenye huo mfuko wa plastiki akazitafutia sehemu maalumu na kuziweka, na ule mfuko wa ngozi aliopewa na hizo dhahabu akachukua yale mawe mengine yanayofanana na dhahabu na kuyaweka humo, mawe yale aliwahi kupewa na watu waliotaka kumatapeli kuwa wanauza dhahabu a lipowashutukia wakakimbia, na hata alipozipeleka kwa wataalamu wakamwambia kuwa sio dhahabu.

Alipohakikisha kuwa kaweka kila kitu kwenye usalama, ndipo akakumbuka, …..ooh, Sweetie, yupo wapi jamani, kapotelea wapi….akatoka mle ndani na kuanza kutafuta huku na kule, hakuona daliliya mtu, na huku akiwaza kuwa huenda wale watu walimkuta wakamdhuru, au wamemteka nyara ili akajiunge nao….hapana mbona walisema hawakukuta mtu mle ndani, …jamani sweetie kaenda wapi ………….Rose akatoka kuelekea ufukweni akijifanya anachukua mazoezi lakini nia yake ni kumtafuta Sweetie…

NB, Kidogo kidogo kwa shida shida tutafika tu...TUPO PAMOJA


Ni mimi: emu-three

5 comments :

Pam said...

m3 kwa kweli hongera maana story inahamasisha kuchungulia blog yako hata mara kumi kumi natamani ungekuwa unabandika story mpya hata mara mbili kwa cku!!! back to story dr Rose pole kwa kulaumiwa ndo majukumu yalivyo utegemeavyo cvyo upatavyo, tenda wema wende zako!! hii ipo sana.

Yasinta Ngonyani said...

mmm umekatisha babaya au niseme penye mnogo..haya kweli kidogo kidogo tutafika tu...Hakika nakusifu mno kwa kazi unayoifanya ukizingatia na hii shida ya umeme. HONGERA.

Precious said...

Tuko pamoja M3 vp uko poa lakini? jamani Rose naona anakuwa milionea ghafla

Anonymous said...

Kweli tenda wema uende zako sababu swawabu yako iko kwa mungu au sehemu inakuja, ona sasa Rose wema uliyotenda umelipwa hapa hapa na imekuja muda mwafaka, unalipa deni unamwacha Doct Adam akishangaa jinsi ulivyolipa deni hilo. Tunza tu vizuri hiyo mali ili wasiiba. Kidogo kidogo kweli M3 laptop inakuja very soon na usumbufu wote wa kwenye internet utaisha. hongera kwa visa vizuri, nilimiss sana visa vyako maana nikipindi kirefu nilikuwa mbali na access ya computer

emu-three said...

Pam,Yasinta,Precios na Anyn. Nawashukuruni kwa kuwa pamoja nami. Hali yangu inaendelea vyema namshukuru munguruni kwa kuwa pamoja nami. Hali yangu inaendelea vyema namshukuru mungu